Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Serikali ya Afrika Kusini yatakiwa kuitika wito wa Mahakama ya ICC hapo April 7

$
0
0
Mamlaka nchini Afrika Kusini wametakiwa kutokea mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC iliyoko mjini The Hague Uholanzi, Aprili 7 mwaka huu kuhusiana na kushindwa kwao kumkamata rais wa Sudan, Omar Hassan al-Bashir, wakati alipofanya ziara miaka miwili iliyopita.

Ayesha Johaar, mshauri masuala ya sheria wa Serikali, amesema kuwa utawala wa Pretoria umetakiwa kuhudhuria kikao cha mahakama hiyo kwa kushindwa kumkamata rais Bashir wakati walikuwa wanajua kabisa kuna hati ya kukamatwa ilikuwa imetolewa dhidi yake.

"Hati iliyotolewa na ICC inahusu kupewa maelezo ya kwanini Serikali ilishindwa kutumiza masharti ya mkataba wa Roma kama mwanachama kumkamata rais wa Sudan," alisema mshauri.

Serikali ya Afrika Kusini ilikuwa imetangaza nia yake ya kujiondoa kwenye mahakama ya ICC mwaka 2015, baada ya nchi hiyo kukosolewa kwa kushindwa kumkamata Bashir, ambaye anatuhumiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita aliyoyatekeleza kwenye jimbo la Darfur.

Mahakama kuu nchini Afrika Kusini, mwezi uliopita ilizuia mchakato wa Serikali kutaka kujiondoa kwenye mahakama hiyo.

Hata hivyo mwanasheria mkuu wa Serikali Michael Masutha amesisitiza kuwa Serikali itaendelea mbele na mchakato wake wa kujiondoa kwenye mahakama hiyo, kwakuwa uamuzi wa mahakama kuu ulijikita katika Serikali kufuata taratibu kujitoa.

Na kwa kutii uamuzi wa mahakama kuu, Serikali tayari imetangaza kuondoa hati yake kwenye umoja wa Mataifa kuhusu kujiondoa kwenye mahakama ya ICC. Chanzo: RFI Kiswahili.

Sudan Kusini yatangaza ada mpya za kupata kibali cha kazi kwa wafanyakazi wa kigeni

$
0
0
Licha ya kukabiliwa na vita pamoja na baa la njaa na kuhitaji msaada, Serikali ya Sudan Kusini imetangaza kuongeza ada ya kupata kibali cha kufanyia kazi nchini nchini humo, kutoka Fold 100 za Sudan hadi kufikia dola elfu 1 za Marekani.

Taifa hili changa zaidi duniani limekuwa likikabiliwa na vita toka mwaka 2013, wakati rais Salva Kiir alipomfuta kazi makamu wake Riek Machar, hali iliyosababisha kuzusha mapigano na mgawanyiko wa kikabila nchini humo.

Mwezi uliopita, umoja wa Mataifa ulitangaza baa la njaa kwenye baadhi ya maeneo nchi hiyo, ikiwa ni mara ya kwanza kwa hatua hii kuchukuliwa katika kipindi cha miaka sita.

Watu karibu nusu milioni, wanaelezwa kuwa watakosa huduma muhimu ikiwemo chakula.

Licha ya kukabiliwa na hali mbaya, utawala wa Juba sasa utatoza kiasi cha dola elfu 10 kwa wageni wanaofanya kazi rasmi, dola elfu 2 kwa wale wanaofanya kazi za kawaida na dola elfu 1 kwa kazi nyingine kuanzia Machi mosi mwaka huu.

Edmund Yakani, mkurugenzi mtendaji wa shirika moja la misaada nchini humo, amesema kuwa tangazo hili la Serikali linalenga kupunguza idadi ya wafanyakazi wa misaada.

"Ukweli ni kwamba gharama hizi za kupata kibali ni kubwa sana kwa wafanyakazi wa misaada, hasa ukizingatia kuwa asilimia 90 ya wafanyakazi wa kigeni wanaotaka kufanya kazi Sudan Kusini ni wafanyakazi wa mashirika ya kibinadamu," alisema mkurugenzi huyo.

MAHAKAMA YA TANZANIA YAENDELEA NA MABORESHO

$
0
0
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Prof. Ibrahim Juma(Mwenye shat ijeupe) akifuatilia Mada kuhusu Mpango Makakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Maboresho ya Mahakama iliyokuwa ikitolewa leo na Mratibu wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahahakama ya Tanzania (Judiciary Delivery Unit-JDU) jijini Dar es Salaam
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Ndg. Hussein Kattanga akifafanua jambo kuhusu Mada ya Maboresho ya Mahakama ya Tanzania iliyokuwa ikitolewa na Mratibu wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama ya Tanzania (Judiciary Delivery Unit) leo jijini Dar es Salaam
Wajumbe wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama ya Tanzania (Judiciary Delivery Unit) wakiwa na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Prof. Ibrahim Juma(mwenyeshatijeupe) kwa ajili ya kutoa taarifa za Maendeleo ya Maboresho ya Mahakama
Mratibu wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama ya Tanzania (Judiciary Delivery Unit) Mhe. Zahara Maruma (mwenyemiwani) akimuelezea Kaimu Jaji Mkuu waTanzania Mheshimiwa Prof. Ibrahim Juma(hayupo Pichani) Maendeleo ya Maboresho ya Mahakama leo jijini Dar es Salaam


PICHA NA LYDIA CHURI WA MAHAKAMA YA TANZANIA

CRDB YATOA MSAADA KATIKA HOSPITALI YA SARATANI YA OCEAN ROAD

$
0
0
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Taasisi ya Saratani Ocean road, Beatrice Erasto ,vifaa vya mgonjwa ikiwa ni moja ya vitu vilivyotolewa msaada vyenye thamani ya Milioni 10 kwa taasisi hiyo jana Dar es Salaam
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia)akimkabidhi Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Taasisi ya Saratani Ocean road, Beatrice Erasto kabati la kuhifadhia vifaa vya mgonjwa ikiwa ni moja ya vitu vilivyotolewa msaada vyenye thamani ya Milioni10 kwa taasisi hiyo jana Dar es Salaam.
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka  (kulia)akizungumza kabla ya kukabidhi msaada kwa taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
 Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road wakifatlia kitendo hicho cha utoaji wa Msaada kutoka benki ya CRDB
 Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Taasisi ya Saratani Ocean road, Beatrice Erasto akizungumza kabla ya kupokea msaada wa vifaa vya hospitali kutoka benki ya CRDB

RITA KUBORESHA MFUMO WA USAJILI WA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA KWA WATOTO KUPITIA MPANGO WA CRVS

$
0
0

Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) umeandaa maboresho ya ujumla ya mfumo mzima wa usajili chini ya Mkakati wa Kitaifa wa Kuboresha Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu (National Strategy on Civil Registration and Vital Statistics - kwa kifupi National CRVS Strategy), ili kuisaidia Serikali kupata takwimu sahihi za wananchi zinazoisaidia kupanga mipango ya maendeleo na huduma za jamii. Kwa mujibu wa Takwimu za Sensa ya mwaka 2012 ni asilimia 13.4 ya Wananchi ndiyo waliyosajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa.

Hayo yamesemwa na Kaimu Afisa Mtendaji wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Emmy Hudson, wakati wa Mkutano wake na baadhi ya wahariri na waandishi wa habari, uliofanyika kwenye makao makuu ya RITA, jijini Dar es salaam.

Alisema Mkakati huo wa CRVS una mipango mbalimbali ya utekelezaki ikiwa ya muda mfupi na mrefu kwa makundi yatokanayo na umri ili kufikia ufanisi unaotarajiwa.  Makundi hayo ni la Watoto wa Umri chini ya miaka mitano, kundi la watu miaka 5 - 17 na kundi la wananchi wa miaka 18 na kuendelea, ambapo Utekelezaji wa Usajili kwa kundi la kwanza umeshaanza kupitia Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri Chini ya Miaka Mitano ambapo kwa sasa unatekelezwa katika Mikoa mitano ya Tanzania Bara ambayo ni Mwanza, Mbeya, Songwe,Iringa na Njombe.
Kaimu Afisa Mtendaji wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Emmy Hudson akizungumza na baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waliofika katika Makao makuu yake Jijini Dar es salalaam leo, wakati akizungumzia Mkakati wa Kitaifa wa Kuboresha Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu hapa nchini.
Kaimu Afisa Mtendaji wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Emmy Hudson akiendelea kuzungumza na wanahabari hao.
Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Cuthbert Simalenga akifafanua jambo katika Mkutano huo.

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma leo tarehe 9/03/2017. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. PICHA NA IKULU.
Rais Dkt Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan mapema leo mchana mara baada ya kumaliza kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma,kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kutoka kwenye kikao cha Baraza la Mawazili,kilichofanyika leo mjini Dodoma
Waziri wa habari,Utamaduni Sanaa na Michezo,Nape Nnauye akizungumza jambo na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma leo.PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS.

MICHUZI TV: ZIFAHAMU FAIDA ZA UFUGAJI WA SUNGURA PART 1

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 09.03.2017


MICHUZI TV: WAGOMBEA URAIS CHAMA CHA MAWAKILI TANGANYIKA (TLS)

JE BABA ANATAKIWA KUTOA SHILINGI NGAPI ZA MATUNZO YA MTOTO ?

$
0
0
Image result for MATUNZO YA MTOTO

Na Bashir Yakub
Wazazi  wanapokuwa  wametengana  matunzo  ya mtoto  ni  jambo  jingine  linaloleta    faraka  kubwa. Nani  anawajibu  wa  kutoa  matunzo  ya mtoto,  na  matunzo  yenyewe  ni  kiasi  gani  hubaki  kuwa  kiini  cha  ugomvi.


Wapo  wanaotoa  lakini  anayepewa  anasema  anapewa  kidogo.  Anayetoa  naye  anasema  natoa  kidogo  kwasababu  sina. Huyu  naye  anauliza  kama  huna  kwanini  ulizaa. Mambo  kama  hayo  na mengine  mengi  yanayofanana  na  hayo.


Basi  katika  kupitia  Sheria  namba  21, Sheria  ya  mtoto  ya  mwaka  2009   tutatizama   nani  anatakiwa  kutoa matunzo  ya  mtoto  halikadhalika  ni  kiasi  gani  kinatakiwa  kutolewa.  Kusoma zaidi BOFYA HAPA

TECC - Vijana watakiwa kuchangamkia fursa za mafunzo ya ujasiriamali

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC), Bw. Sosthenes Sambua (katikakati) akizungumzia awamu ya pili ya program ya VIA Jiandalie Ajira ambayo imetangaza fursa za mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 24 kwa manispaa ya Mtwara, Mikindani, Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam, Dodoma na Kibaha mkoani Pwani. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Rais na Kujitegemea (PTF), Bi.Haigath Kitala na kushoto ni Afisa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC), Bw. Sosthenes Sambua (wa pili kutoka kulia) akizungumzia awamu ya pili ya program ya VIA Jiandalie Ajira ambayo imetangaza fursa za mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 24 kwa manispaa za Mtwara, Mikindani, Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam, Dodoma na Kibaha mkoani Pwani. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Rais na Kujitegemea (PTF), Bi.Haigath Kitala, wa pili kutoka kushoto ni Afisa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam, na kushoto ni Bi. Zahra Mahmoud,Meneja Biashara wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA).

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI,MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA ENEO LENYE MGOGORO LA PORI TENGEFU LA LOLIONDO.

$
0
0
Mwenyekii wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi ,Maliasii na Utalii,Atashasta Ndetiye (katikati) akiongozana na wajumbe wengine wa kamati hiyo kutizama vyanzo vya maji vilivyoko katika Pori Tengefu la Loliondo.
Waziri wa Malisili na Utalii ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo,Prof Jumanne Maghembe akiongozana na wataalamu katika ziara ya kamati hiyo.
Mtafiti Mkuu wa Idara ya Ikolojia (TAWIRI) Dkt Edward Khoi akitoa maelezo ya kitaalamu kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Ardhi,Malisili na Utalii wakati wakitembela Pori tengefu la Loliondo.

NSSF YAHAMASISHA WAKULIMA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magesa, akizungumza na viongozi wa Vyama vya Ushirika wa Mazao (AMCOS), wakati wa uhamasishaji wakulima wilayani humo. Mpango huo umeanzishwa na NSSF kwa ushirikiano wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) na Benki ya Azania.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma, akizungumza na viongozi wa Vyama vya Ushirika wa Mazao  (AMCOS), wakati uhamasishaji wa wakulima wilayani humo. Mpango huo umeanzishwa na NSSF kwa ushirikiano wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) na Benki ya Azania. 
Meneja wa NSSF Mkoa wa Manyara, Alexander Josephat, akizungumza na viongozi wa Vyama vya Ushirika wa Mazao (AMCOS), wakati wa uhamasishaji wa wakulima wilaya ya Kiteto. Mpango huo umeanzishwa na NSSF kwa ushirikiano wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) na Benki ya Azania. 

DC GONDWE ANG'ARISHA SIKU YA WANAWAKE HANDENI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya akikata utepe kuashiria ufunguzi wa maonesho ya bidhaa za kinamama.



Mkuu wa Wilaya akitazama moja ya bidhaa na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na akina mama katika kutengeneza Tanzania ya Viwanda.

Mh. Gondwe akihutubia wananchi siku ya wanawake ambapo alieleza Halmashauri kutoa kipaumbele cha mikopo kwa vikundi vya kinamama na kulinda watoto wa kike kuhakikisha wanamaliza masomo yao bila kukwamishwa. 
Mkuu wa Wilaya Mh. Gondwe akajumuika kucheza na kinamama kusherehekea sikukuu yao.
Moja ya kikundi cha kinamama wakipokea cheti cha utambulisho kutoka kwa Mkuu wa Wilaya.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akisoma moja ya bango la  wanawake wa kikundi cha Umoja ni nguvu linaloonesha taswira ya mama aliebeba mtoto mgongoni, kichwani kabeba kuni na jembe na mkononi akiwa  amebeba chakula huku mwanaume akiwa ameketi nyumbani kumngoja mama alietoka shamba aje kuandaa chakula.


Picha na Alda Sadango,Afisa Habari,wilaya ya Handeni

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 10,2017


Benki ya NMB, Mastercard yawaingiza wakulima kidijitali

$
0
0
 BENKI ya NMB imesaini makubaliano na Kampuni ya Mastercard kufanya kazi kiushirikiano ili kuhakikisha inaiinua sekta ya kilimo nchini Tanzania kwa kuanzishwa kilimo mtandao 'eKilimo' kinaomuwezesha mkulima kupata taarifa za masoko na bidhaa kuondoa urasimu waliokuwa wakiupata wakulima hapo awali. 

Huduma hiyo ya 'eKilimo’, ni jukwaa la kidigitali ambalo litamsaidia mkulima kupata uwazi na usalama wa bidhaa zake kimasoko na hata urahisi wa upatikanaji taarifa, huku ukiondoa urasimu uliokuwa ukifanywa na madalali sokoni, jambo ambalo wakulima wengi wamejikuta wakishindwa kunufaika kiufasaa kwa bidhaa zao. 
 
Ushirikiano huo umesainiwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker pamoja na Rais wa Kampuni ya MasterCard barani Afrika, Bw. Raghu Malhotra, ambapo kwa pamoja wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema huduma hiyo itawainua wakulima kwa kiasi kikubwa endapo itatumiwa na wakulima. 

Kwa upande wake, Rais wa Kampuni ya MasterCard barani Afrika, Bw. Malhotra, alisema kupitia huduma hiyo mkulima anaweza kufanya mauzo na kulipwa kwa kutumia simu iliyo na programu maalum huku benki ikipata taarifa, jambo ambalo litamrahisishia shughuli zake na kuokoa muda mwingi wa kuzunguka.
 
 Alisema takwimu zinaonesha kilimo kinachangia kiasi kikubwa cha fedha katika pato la taifa 'GDP', ambapo takribani shilingi bilioni 13.9 ikiwa ni takribani asilimia 30, hivyo kuna kila sababu ya kuinua sekta hiyo ili iendelee kufanya vizuri na pia kuwainua wakulima. "Kwa kutumia teknolojia ya kidigitali huduma hii italeta uwazi kwenye mchakato wa mauzo na ununuzi na kuongeza ufanisi katika eneo la ugavi, hivyo kuleta manufaa ya kiuchumi. 
 
Teknolojia inapaswa kusaidia wakulima kupata ufumbuzi kwa huduma za kifedha, hivyo kuwawezesha kuwa na maisha bora na familia zao hata baadae," alisema Rais wa Kampuni ya MasterCard barani Afrika, Bw. Malhotra. Akizungumzia huduma hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker alisema lengo kubwa ni kumuwezesha mkulima kunufaika zaidi na kilimo anachokifanya, huku benki ikiendelea kujenga mazingira ya mteja kupata huduma bora na kuaminika ili aendelee kupata mikopo kwa shughuli za kilimo.
 
Alisema mkulima anapokuwa na uhakika wa kupata taarifa sahihi za masoko na kuweza kufanya mchakato mzima pasipo na urasimu hunufaika zaidi na kuendelea kuaminika kwa taarifa zake benki jamboa ambalo ananufaika moja kwa moja kupata mikopo ya kilimo, ambayo humuongezea tija. "Nia yetu sisi ni kukua sekta ya kilimo Tanzania, na ndio maana tumeshirikiana na Mastercard na kuja na teknolojia ambayo inaweza kubadilisha maisha ya wakulima. 
 
Uzoefu wetu katika sekta ya kifedha unatufanya kutafuta wadau kama Mastercard ambapo tumeona wamefanya vizuri nchini Kenya kuwasaidia wakulima kupitia programu ya '2KUZE'. Ndio maana nasi tumeungana kuhakikisha wakulima wadogo, wanunuzi na mawakala wananufaika kiuchumi," alisema Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Bussemaker. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (wa pili kushoto) pamoja na Rais wa MasterCard Ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika, Bw. Raghu Malhotra wakisaini makubaliano ya kiushirikiano jijini Dar es Salaam kuhakikisha sekta ya kilimo nchini Tanzania inakuwa na kilimo mtandao 'eKilimo' kinaomuwezesha mkulima kupata taarifa za masoko na bidhaa kuondoa urasimu aliokuwa akiupata mkulima hapo awali. Wa kwanza kushoto akishuhudia ni Kaimu Ofisa Mkuu Kitengo cha Wateja wadogo, Abdulmajid Nsekela na Rais wa MasterCard wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, Daniel Monehin. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (wa pili kushoto) wakibadilishana nyaraka za makubaliano na Rais wa MasterCard Ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika, Bw. Raghu Malhotra (wa pili kulia) mara baada ya kusaini makubaliano ya kiushirikiano jijini Dar es Salaam kuhakikisha sekta ya kilimo nchini Tanzania inakuwa na kilimo mtandao 'eKilimo' kinaomuwezesha mkulima kupata taarifa za masoko na bidhaa kuondoa urasimu aliokuwa akiupata mkulima hapo awali. Wa kwanza kushoto akishuhudia ni Kaimu Ofisa Mkuu Kitengo cha Wateja wadogo, Abdulmajid Nsekela na Rais wa MasterCard wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, Daniel Monehin. 

BALOZI KAMALA AHUDHURIA KAMATI TENDAJI YA KIBUNGE KUHUSU SHIRIKISHO LA BIASHARA DUNIANI (WTO)- BRUSSELS

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Mhe. Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kulia) akishiriki kikao cha 38 Kamati Tendaji Kuhusu Shirikisho la Biashara Duniani. Kikao hicho kimefanyika  Brussels - Ubeligiji kufanya tathimini ya mwenendo wa biashara na uwekezaji Duniani. Bunge la Tanzania limeteuliwa hivi majuzi kuungana na nchi  21 zinazounda Kamati Tendaji ya Kibunge Kuhusu Shirikisho la Biashara Duniani.

WAKURUGENZI WA SHIRIKA MISAADA YA KIMAENDELEO LA UINGEREZA WAWATEMBELEA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF WILAYANI KISARAWE,MKOANI PWANI.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji waShirika la Misaada ya Maendeleo la Uingereza DFID katika Benki ya Dunia Bw.David Kinder amepongeza hatua iliyofikiwa na serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- katika kuteleza Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini,PSSN.

Bw. Kinder ametoa pongezi hizo baada ya kukutana na walengwa wa Mpango huo katika vijiji vya Mzenga A na Vilabwa katika wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ambako amejionea mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta za uboreshwaji wa makazi,elimu,lishe na afya kwa walengwa hao.

Amesema hatua iliyofikiwa na walengwa hao inapaswa kuungwa mkono zaidi ili hatimaye waweze kuondokana na madhira ya umasikini unaowakabili.

Kwa upande wao, baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika vijiji hivyo wamesema tangu kuanza utekelezaji wa Mpango huo wameanza kuona fursa za maendeleo ikiwemo kuezeka mabati nyumba zao, kufuga kuku, na hata kuongeza shughuli za kilimo.

Bi.Asha Khalifan Kikombe mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotelezwa na TASAF katika kijiji cha Vilabwa ,Wilaya ya Kisarawe ,mkoani Pwani akiwaonyesha wageni kutoka Shirika la Misaada la Uingereza (hawako pichani) nyumba aliyoezeka kwa mabati alizozinunua kwa kutumia fedha za ruzuku kutoka TASAF
Ujumbe kutoka DFID wakiwa na baadhi ya watendaji kutoka TASAF na Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe wakipata maelezo ya mradi wa kutunza mazingira unaotekelezwa na walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini kwa utaratibu wa Ajira ya Muda unaotekelezwa wakati wa kipindi cha hari kwa lengo la kuwaongezea walengwa kipato.
Baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Msikini katika kijiji cha Mzenga A wilaya ya Kisarawe wakishiriki katika mkutano ulioitishwa kuzungumzia mafanikio ya utekelezaji wa shughuli za Mpango uliohudhuriwa pia na wageni kutoka Shirika la Misaada la Uingereza DFID.
Ujumbe kutoka Shirika la Misaada la Uingereza DFID ukipata maelezo kutoka kwa mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Vilabwa juu ya namna alivyonufaika na fedha zinazotolewa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jmii TASAF.
Ujumbe kutoka Shirika la Misaada la Uingereza DFID ukipata maelezo kutoka kwa mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Vilabwa juu ya namna alivyonufaika na fedha zinazotolewa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jmii TASAF.

DC Kanali Ndagala kuwachukulia hatua watakaoshindwa kumaliza miradi ya ujenzi wa shule kwa wakati wilayani Kakonko,mkoani Kigomamizi wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya shule

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
 
MKUU wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala ameahidi kuwachukulia hatua wasimamizi wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, endapo watashindwa kukamilisha miradi hiyo na kuhakikisha inakamilika kwa muda muafaka kutokana na changamoto iliyopo ya upungufu wa vyumba vya madarasa kutatuliwa.

Maagizo hayo aliyatoa jana wakati akikagua ujenzi wa madarasa manne na ofisi mbili katika Shule ya Msingi Kakonko Wilayani humo, ambapo alibaini kuwepo kwa tatizo la ucheleweshwaji wa vifaa vya ujenzi kwa mafundi hali inayo pelekea kusua sua kwa ujenzi huo.

Mkuu huyo alisema mradi huo ulitakiwa kuwa umekabidhiwa, lakini mpaka sasa bado haujakamilika kutokana na uzembe wa baadhi ya wasimamizi Wa mradi huo kushindwa kuwasimamia mafundi ipasavyo waweze kukamilisha ujenzi huo, na ifikapo mwezi wa tatu Mwishoni ujenzi huo uwe umekamilika na wanafunzi wapate madarasa yao waendelee kuyatumia.

" niwatake Wahandisi wa halmashauri kwa kushirikiana na Watendaji wa kijiji kuwasimamia mafundi kwa karibu ilikuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati endapo mtashindwa kusimamia ipasavyo tutawajibishana, Wananchi wamejitahidi kuchangia na Serikali imetoa fedha kwa wakati ni lazima muhakikishe mnakamilisha suala hili ilikuwatia moyo wananchi kuendelea kuchangia jitihada za Serikali",alisema Kanali Ndagala.
 Sehemu ya Madarasa hayo ambayo bado hayajakamilika
 MKUU wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala akizungumza na baadhi ya Wanafunzi wa shule ya msingi Kakonko,alipofana ziara ya kukagua madarasa manne na ofisi mbili zilizoko katika ujenzi katika shule hiyo.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala akikagua ujenzi wa madarasa manne na ofisi mbili katika Shule ya Msingi Kakonko Wilayani humo, ambapo alibaini kuwepo kwa tatizo la ucheleweshwaji wa vifaa vya ujenzi kwa mafundi hali iliyo pelekea kusua sua kukamilika kwa ujenzi huo.

JAJI WARIOBA AZINDUA KITABU CHA KIONGOZI MWANAMKE

$
0
0
 Waziri mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba akionesha kitabu juu mara baada ya kuzindua kitabu cha Mwanamke kiongozi katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
 Jaji Joseph Sinde Warioba akizungumza na Wanawake waliofika katika kongamano la Wanawake na Wasichana  juu ya uongozi ndani ya Tanzania na kuzindua kitabu kinachohusu Mwanamke
 Dkt Mwele Malecela akizungumza juu ya mambo aliyojifunza wakati anagombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi na kuwataka wazazi kuwa ndio waangalizi na kuwatoa hofu wasichana pindi wanapohitaji kujaribu jambo lolote lenye manufaa kwa Jamii
 Waziri mkuu Mstaafu Jaji  Joseph Sinde Warioba akiwa na Mama Anna Abdalah wakiwasalimia wanafunzi wasichana wa chuo kiku cha Dar es Salaam ambao walifika katika kongamano hilo
Baadhi ya washiriki waliokaa Safu ya mbele katika kongamno hilo.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images