Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MACHI 9,2017


CHAMA CHA WANAWAME TAWI LA GST DODOMA WAADHIMISHA KILELE CHA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI KWA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA KONGWA DODOMA

$
0
0
Wajumbe wa Chama cha Wanawake tawi la GST-Makao Makuu DODOMA wakiwa katika picha ya pamoja katika viwanja vya Hospital ya Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma baada ya kushirika katika kazi ya kufanya usafi ndani ya Hospital hiyo,siku ya Wanawake Duniani ambayo kilele chake kiliadhimishwa tarehe 08/03/2017, Mkoani Dodoma sherehe hizi kimkoa zilifanyika Wilaya ya Kongwa.

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUTEMBELEA KITUO CHA PEDDEREF SOBER HOUSE KIGAMBONI

$
0
0
Maafisa na Askari (Wanawake) wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Mkurugenzi wa People With Drugs Dependence Relief Foundation (Pedderef) bi. Nuru Salehe wa kwanza mbele (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wanawake waliopata kuathirika na madawa ya kulevya kituoni hapo, ambapo wanawake hao wameanza kurejea katika hali zao za kawaida mara baada ya kupewa elimu na malezi yanayostahili.

Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeungana na wanawake duniani kuadhimisha siku hiyo.

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi alisema katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano (5) kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya, kupitia Jeshi hilo Nzalayaimisi aliwaongoza Askari (wanawake) kutembelea kituo cha Pedderef Sober House na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali.

Ambapo aliiomba jamii isiwanyanyapae pamoja na elimu wanayoendelea kuipata kituoni hapo ameiasa jamii kujitokeza kuwasaidia na kuwawezesha kwa hali na mali ili waweze kujiajili wenyewe kwani wanapotoka kituoni hapo wanakuwa hawana uwezo wakujiajili na kujikuta wanarudia tena kwenye janga la madawa hayo.

Pia Nzalayaimisi aliendelea kusema kwa kutoa pongezi kwa serikali na wadau mbalimbali wote waliojitokeza na kuthubutu kufanya maamuzi ya kujitoa katika kupambana na janga hilo na pia alimpongeza mkuu wa mkoa wa dar es salaam paul makonda kwa kuongoza mapambano hayo. 

Mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe naye alisema napenda kutoa shukrani za kipekee kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa msaada wao wa hali na mali waliotupatia na kuomba taasisi nyingi na wadau mbalimbali kujitokeza katika kusaidia kituo hiki kwani wengi wamenufaika kutokana na elimu na malezi wanayoendelea kuyapata kituoni hapo.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi akitoa nasaa kwa wanawake na vijana walioathirika na janga la madawa ya kulevya kituoni hapo mapema leo asubuhi.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi (kushoto) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa kituo People With Drugs Dependence Relief Foundation (Pedderef), Nuru Salehe wakati wa sherehe ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani mapema leo asubuhi. Kulia ni Jacqueline Samson na Ashura Diwani.
Moja ya wanawake waathirika wa madawa ya kulevya bi. Jacqueline Samson aliyesimama (katikati) akitoa shukrani kwa viongozi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambao hawapo picha kwa kuwatembelea kituoni hapo pia kwa msaada waliowapatia.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jennifer Shirima ambaye aliambatana na msemaji wa Jeshi hilo katika ziara hiyo akiwasisistizia wanawake hao kutoajiingiza tena kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya na kuwakumbusha kuwa “Wanawake ni msingi wa mabadiliko kiuchumi” (kulia) ni Mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe na (kushoto) ni Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi ambaye pia ni msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Taasisi ya Ekama Development yaadhimisha siku ya wanawake wilayani Temeke

$
0
0
KATIKA kusherehekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, TAASISI ya Ekama Development , ilishirikisha wanawake wa wajasiriamali wadogo Wilayani Temeke, katika tamasha lililokuwa na nia ya kuchambua kauli mbiu ya Mwaka huu ya Tanzania ya viwanda, ambapo kulikuwa na mada mbalimbali kama, ajira na mazingira ya kazi na masoko kuelekea Tanzania ya viwanda.
 Sehemu ya wanawake wajasiriamali wadogo Wilayani Temeke, wakiwa na mabango yao katika kuashimisha siku ya Wanawake Duniani, ambayo huadhimisha kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka.
 Sehemu ya wanawake wajasiriamali wadogo Wilayani Temeke, wakiwa katika hafla hiyo.

TANESCO YATOA SIKU 14 KWA WADAIWA BILI ZA UMEME KULIPA, VINGINEVYO HUDUMA YA UMEME INASITISHWA

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limetoa siku 14 kwa Wateja wake wote linalowadai kulipa madeni yao, vinginevyo litasitisha utoaji wa huduma ya nishati kwa wahusika.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo Machi 9, 2017 ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (pichani juu), alisema, Shirika linadai jumla ya shilingi Bilioni 275.38.

Akifafanua zaidi alisema, Wizara na Taasisi za Serikali zinadaiwa zaidi ya Shilingi Bilioni 52.53, Shirika la Umeme Zanzibar, (ZECO), linadaiwa zaidi ya Shilingi Bilioni 127.87, na Makampuni binafsi na wateja wadogo wadogo deni ni zaidi ya Shilingi Bilioni 94.97.

“Zoezi hili litaambatana na utoaji taarifa (notice) kwa wadaiwa wote kulipa madeni yao ndani ya kipindi cha siku 14, baada ya hapo Shirika litachukua hatua ya kusitisha Huduma kwa Wateja watakaoshindwa kuanza kulipa madeni yao pamoja na hatua zingine za kisheria.” Alisema Dkt. Mwinuka.
Aidha, alisema kwa wale wateja wadogowadogo, Shirika halitawaandikia barua kwani ni wengi, isipokuwa kupitia ofisi ya Uhusiano ya Shirika, wataarifiwa kupitia vyombo vya habari.

Alisema Malimbikizo hayo ya madeni yamekuwa yakikwamisha jitihada za utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya msingi ndani ya Shirika kwa wakati, ikiwemo shighuli za Uendeshaji Shirika, Matengenezo ya Miundombinu pamoja na utekeelzaji wa miradi mbalimbali.

“Ni matarajio ya Shirika kuwa kuli[wa kwa malimbikizo haya ya madeni, kutasaidia TANESCO kujiendesha kiushindani na kwa ufanisi mkubwa zaidi na hivyo kuendelea kuchochea kasi ya ukuaji sekta mbalimbali zinazotegemea nishati ya umeme hapa nchini.” Alihitimisha Dkt. Mwinuka.

Taarifa hii ya TANESCO imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kuliagiza Shirika hilo, kuwakatia umeme wale wote wanaodaiwa ikiwemo taasisi nyeti za Serikali na hata Zanzibar.

Rais alitoa agizo hilo wakati akizindua ujenzi wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme wa Kilovolti 132 mkoani Mtwara ambacho kitaboresha upatikanaji wa umeme kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi.
 Baadhi ya viongozi wa TANESCO, kutoka kushoto, Dudu Fuime, (Kaimu Meneja Mwandamizi TEHAMA), Mhandisi Kahitwa Bishaija,(Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji umeme), Mhandisi Theodory Bayona,
(Meneja wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme)
  na Renata Ndege, (Afisa Mkuu wa Fedha) wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa mkutano huo
Baadhi ya viongoziwa juu wa TANESCO na waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo

PROFESA MUHONGO AITAKA KAMPUNI YA PR NG MINERALS KUANZA UZALISHAJI MADINI ADIMU

$
0
0
Na Veronica Simba - Dodoma

Serikali imeitaka Kampuni ya PR NG Minerals Limited ya Australia, inayofanya utafiti wa madini adimu (rare earth elements), eneo la Ngualla mkoani Songwe, kukamilisha utafiti huo haraka ili waanze uzalishaji mapema iwezekanavyo.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alimwambia Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Dave Hammond, aliyemtembelea ofisini kwake mjini Dodoma jana kuwa, Serikali imedhamiria kuachana na utamaduni au mazoea ya kujikita kwenye uzalishaji wa madini ya kawaida pekee badala yake inataka kuanza uzalishaji wa madini adimu pia ili kuendana na Soko la Dunia.

“Hivi sasa Dunia nzima inageukia kwenye uzalishaji wa madini adimu, hivyo nasi ni lazima tuanze uzalishaji wake mapema iwezekanavyo.” Aidha, Waziri Muhongo aliitaka Kampuni hiyo kuwasilisha Mpango Kazi wake ambao pamoja na mambo mengine utaonesha ni lini uzalishaji utaanza.

Akifafanua umuhimu wa kubainisha Mpango Kazi wa Kampuni hiyo, Profesa Muhongo alibainisha kuwa, baadhi ya wawekezaji katika sekta ya madini hapa nchini, wamekuwa wakishikilia leseni za madini kwa muda mrefu pasipo kuzifanyia kazi hivyo kuilazimu Serikali kuwanyang’anya kwa mujibu wa Sheria ya Madini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi huyo aliyeambatana na Meneja wa Masoko wa Kampuni husika, Ismail Diwani, alimhakikishia Waziri Muhongo kuwa watakamilisha utafiti wao na kuanza uzalishaji mapema iwezekanavyo.

Mkurugenzi Hammond aliongeza kuwa, kupitia Mradi huo wa madini adimu wa Ngualla, upo uwezekano wa Tanzania kuwa msambazaji mkubwa wa kimataifa wa madini hayo.

Madini adimu yanajumuisha kundi la metali muhimu 17 ambazo ni pamoja na Neodymium, Praseodymium, Scandium na Thulium. Mojawapo ya matumizi yake ni katika magari yanayotumia umeme pamoja na kutengenezea vifaa vya kisasa vya kielektroniki.

Kwa Tanzania, madini adimu yanapatikana katika mikoa ya Songwe, Mbeya na Morogoro.
Mkurugenzi wa Kampuni ya PR NG Minerals Limited, Dave Hammond (wa pili kutoka kushoto), akifafanua jambo kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika jana ofisini kwake – Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma. Wengine kutoka kulia ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Rayson Nkya, Mjiolojia Mkuu kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Alphonce Bushi na Meneja wa Masoko wa Kampuni husika, Ismail Diwani.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akisisitiza jambo kwa Ujumbe kutoka Kampuni ya PR NG Minerals, waliomtembelea ofisini kwake jana – Makao Makuu ya Wizara, mjini Dodoma.

TAMASHA LA PASAKA KUFANYIKA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama akizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema leo mchana jijini Dar kuhusiana na maendeleo ya maandalizi ya tamasha la pasaka linatlotajia kuanza hivi karibuni.


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Tamasha kubwa la muziki wa injili linalofahamika kama "Tamasha la Pasaka" sasa kufanyika katika uwanja wa Uhuru april 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mratibu wa Tamasha hilo, Alex Msama amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na sasa uwanja wa uhuru ndio sehemu maalum ya kufanyia Tamasha hilo.

“Malengo ya tamasha la pasaka ni yaleyale ni kuliombea taifa na kumuombea Rais wa nchi Dkt John Pombe Magufuli  ili aendelee kutawala kwa amani katika taifa hili” amesema

Ametaja kuwa tamasha hilo kwa sasa litatembea katika mikoa kumi na kufanya uzinduzi wa albamu mbili

Airtel Money yaisaidia WFP kutuma Pesa kwa Wakimbizi katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu

$
0
0
Airtel Tanzania imeanzisha njia  mpya  na rahisi ya Near – Field Communication (NFC) ambayo ni mfumo wa malipo utakaoisaida Shirika la chakula Duniani  (WFP)  kuhamisha fedha kwa wakimbizi wapatao 10,000 kama sehemu ya mgao wao wa chakula kwa miezi mitatu ikiwa ni  mpango wa majaribio wa kuboresha huduma katika kambi ya wakimbizi ya  Nyarugusu.

Chini ya majaribio hayo, kwa sasa wakimbizi hao watapokea fedha kwa njia ya simu ya mkononi yenye dhamani ya  fedha za kimarekani $ 4.50 (shilingi 10,000) mara mbili kwa mwezi wakiwa katika kambi hiyo. Fedha hizo zitawekwa katika kadi zao za  Airtel Money Tap Tap kadi zilizounganishwa na teknolojia ya malipo ya NFC ambao umeunganishwa na akaunti zao za Airtel Money. Tap Tap kadi inatoa urahisi wa malipo na ni njia rahisi inayomfanya mteja kufanya malipo bila ya kuwa na simu yake ya mkononi  wakati wowote. Ni ufumbuzi  mzuri kwa wakimbizi  unaowawezesha kufanya shughuli za haraka na kwa urahisi kwa kugusisha tu kadi  kadi zilizounganishwa  na akaunti zao za Airtel Money na kufanya malipo ya kupokea au kununua bidhaa.
 "Tap Tap  kadi imeungwanishwa na huduma ya Airtel Money ili inatoa huduma ya kipekee na urahisi kwa wateja wetu  katika utumiaji wa  wa fedha kwa njia ya mtandao, inawawezesha  wateja kutumia teknolojia ya kisasa kabisa yakufanya malipo au kuwa na uwezo wa kumiliki akaunti zao za fedha kwa njia ya mtandao hata kama simu ikiwa imezima," alisema Mkuu wa kitengo cha huduma cha  Airtel Money, Isack Nchunda. "Tunafura kubwa kuona kadi hizi mpya zinawawezesha  kufanya manunuzi ya chakula na kusaidia maisha ya wakimbizi waishio Tanzania."

Baada ya kupokea fedha kutoka kwenye kadi ya Tap Tap, wakimbizi wanauwezo wa kununua  chakula katika soko la Nyarugusu ambalo lilifunguliwa mwaka 2016. soko, hilo lipo maeneo ya buffer zone kati ya kambi na wenyeji wa maeneo hayo, ambapo imewapa nafasi  wafanyabiashara wa maeneo hayo kuweza  kuuza mazao yao kwa wakimbizi.

"Matumizi ya kadi hizo inawarahisishia wakimbizi kukidhi mahitaji yao ya chakula na wakati huo huo  kuinua uchumi wa nchi kwakuwa wanyeji hujipatia soko kwa bidhaa zao," alisema Mwakilishi wa WFP nchini Michael Dunford. "Pamoja na fursa kubwa ya kununua aina mbali mbali ya vyakula vinavyozalishwa ndani ya nchi na kuwasaidia kukidhi malazi, vilevile inasaidia kuboresha hali ya lishe ya kaya na kuhakikisha kwamba jamii na wenyeji pia wanafaidika kupitia shughuli nyingi za kiuchumi."

Katika kipindi hiki cha majaribio , wakimbizi wataendelea kupokea mafuta, uji na vitu vingine vidogo wakati mgawo wa wa nafaka, kunde na chumvi vitabadilishwa kwa fedha taslimu.alisisitiza Dunford.
Baadhi ya wakimbizi katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu wakipewa mafunzo toka kwa wafanyakazi wa Airtel huduma kwa wateja ya jinsi ya kutumia huduma ya Airtel Money tap tap card, kadi hiyo Inasaidia WFP kutuma Pesa kwa Wakimbizi katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu. Kadi ya Airtel Money Tap tap imeunganishwa na akaunti za Airtel Money ili kutoa usalama wa utumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya mtandao bila ya kuwa na simu ya mkononi.

NMB to digitize Tanzania’s agri sector with the Mastercard eKilimo mobile solution

$
0
0
National Microfinance Bank Pic (NMB) has signed a strategic partnership agreement with Mastercard to ensure the digitization of the agricultural sector in Tanzania with the rollout of eKilimo, amobile solution developed by the Mastercard Lab for Financial Inclusion.

eKilimo, which in Swahili means ‘eAgriculture’, is a digital platform that will help, introduce efficiency, security and transparency in the agriculture supply chain. The solution will make transacting faster, safer, and easier for all stakeholders including the farmer, the buyer and the agent.

Powered by the digital platformdeveloped by the Mastercard Lab, farmers are now able to conduct the entire transaction process of receiving payments and selling produce via a feature or smartphone, without having to walk hours to markets. This helps to ensure farmers benefit from the ability to capture a higher percentage of the wholesale value of their goods by providing price transparency and more direct access to buyers.
NMB Managing Director – Ineke Bussemaker signing a partnership agreement with Mastercard President for Middle East and Africa – Raghu Malhotra at a press signing ceremony held in Dar es Salaam today. The partnership will pave way for digitization of the agricultural sector in Tanzania with the rollout of eKilimo, a mobile solution developed by the Mastercard Lab for Financial Inclusion. Looking on the left is the NMB Acting Chief Retail Banking – Abdulmajid Nsekela and right is the Mastercard Division President Sub-Saharan Africa – Daniel Monehin.

“Contributing a significant USD 13.9bn to Tanzania’s GDP (nearly 30 percent), it is critical that solutions are found to support this vital sector, ensuring sustainability and growth.Technology is having a significant impact already, and the mobile device is giving small holder farmers the power and ability to move beyond cash,” said Raghu Malhotra, President, Middle East and Africa, Mastercard.

By providing digital payment to farmers, eKilimo will leverage the existing agency banking structure to facilitate account opening for farmers and joint ideation on new product features. This is in line with the Mastercard vision of a more digitally and financially included Africa.
NMB Managing Director – Ineke Bussemaker exchanging partnership contracts with Mastercard President for Middle East and Africa – Raghu Malhotra at a press signing ceremony held in Dar es Salaam today. The partnership will pave way for digitization of the agricultural sector in Tanzania with the rollout of eKilimo, a mobile solution developed by the MasterCard Lab for Financial Inclusion. Looking on the left is the NMB Acting Chief Retail Banking – Abdulmajid Nsekela and right is the Mastercard Division President Sub-Saharan Africa – Daniel Monehin.

READ MORE HERE

ROBO FAINALI ASFC SIMBA na MADINI SASA KUCHEZA MACHI 19, 2017

$
0
0

Mechi mbili za kwanza hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Azam (Azam Sports Federation Cup 2016/2017), zitachezwa Machi 18 na 19, mwaka huu kwenye viwanja viwili tofauti. 

Mechi hizo ni kati ya Kagera Sugar itakayocheza na Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani Kagera wakati siku inayofuata Machi 19 Simba itacheza na Madini kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Awali Simba ilikuwa icheze Machi 18, mwaka huu, lakini siku hiyo uwanja huo utakuwa na shughuli za kijamii hivyo sasa utachezwa siku ya Jumapili Machi 19, mwaka huu.

Mechi nyingine zitapangiwa tarehe za baadaye. Mechi hizo ni kati ya Azam FC na Ndanda FC kadhalika Tanzania Prisons ya Mbeya itakayocheza na mshindi kati ya Young Africans ya Dar es Salaam na Kiluvya United ya Pwani.

Bingwa wa michuano hiyo kwa mujibu wa kanuni, atazawadiwa Tsh. 50 milioni na

 ndiye atakayeiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ya Total wakati Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ndiye ataiwakilisha nchi kwenye michuano ya Total Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kikosi cha Simba

MWAMUZI AHMADA SIMBA AONDOLEWA KWENYE ORODHA LIGI KUU YA VODACOM

$
0
0
Mwamuzi Ahmada Simba akimuonesha kadi nyekundu mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa kwenye mechi ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting.

Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi za Tanzania (Kamati ya Saa 72), imemwondoa Mwamuzi wa kati, Ahmada Simba katika orodha wa waamuzi watakaochezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu wa 2016/2017.


Hatua hii imefikiwa baada ya utetezi wa Mwamuzi Simba kudai kwamba hakuona tukio la Mchezaji wa Young African, Obrey Chirwa ambaye alifunga bao ambalo hata hivyo, mwamuzi alilikataa na kumwonya mchezaji kwa kadi njano.

Tukio hilo lilitokea katika mchezo ambao Young Africans walikuwa wageni wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Machi mosi, mwaka huu.

Katika hiyo ya njano ilikuwa ni ya kwanza kwa Chirwa ambayo hata hivyo kamati ya Saa 72 imeifuta kadi hiyo kwa mujibu wa kanuni ya 9 (8) baada ya Kamati ya Saa 72 haikupaswa kutolewa kwa Chirwa kwa sababu hakukuwa na kosa wala mazingira ya kuonywa.

Kadi hiyo ilikuwa ni msingi wa kadi nyekundu baada ya Chirwa kufanya faulo ambayo aliadhibiwa tena kwa kadi ya njano hivyo kutolewa nje kwa mujibu wa taratibu.

Kufutwa kwa kadi ya njano ya kwanza, kunapelekea kufutwa kwa kadi nyekundu ambayo msingi wa kadi hiyo ulisababisha kadi nyekundu hivyo mchezaji angempaswa kukosa mchezo mmoja. Hata hivyo, kadi ya pili ya njano inahesabiwa.

Kadhalika uamuzi mwingine ulikuwa ni kuipiga faini Young Africans iliyocheza na Simba Februari 25, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya Wanajwani hao kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.

Kitendo hicho ni kwenda kinyume cha kanuni ya 14 (14) ya Ligi Kuu inayoelekeza kuwa timu zitaingia uwanjani kwa kutumia milango rasmi. Hivyo kwa kuzingatia Kanuni ya 14 (48) ya Ligi Kuu, Kamati imeipiga Young Africans fainali ya Sh 500,000 (lakini tano).

UMOJA WA AZAKI ZA VIJANA WAKUTANA KUJADILI VIPAUMBELE VYAO KATIKA BAJETI YA 2017/2018

$
0
0
  Mbunge wa viti maalum wa Pwani, Hawa Mchafu Chakoma (CCM) akizungumza kwenye kongamano la vijana kuhusu mchakato wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha na Geofrey Adroph
 Mbunge wa Kasulu Vijijini, Vuma Augustine (CCM) akizungumza na vijana kwenye kongamano lililoandaliwa na Asasi ya Dira ya Vijana (TYVA) kwa kushirikiana na asasi za mbalimbali za vijana katika kujadili vipaumbele vya vijana katika bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kuhusu namna ambavyo wabunge wanajaribu kupigania maslahi ya vijana kwenye bajeti. 

Mbunge wa viti maalum wa Katavi, Rhoda Edward Kunchela(CHADEMA) akizungumza na vijana kuhusu mchakato wa bajeti unavyofanyika kutoka ngazi ya chini mpaka ya juu kwenye kongamano la vijana lililofanyika leo kwenye ukumbi wa Wanyama jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

NGOMA, TAMBWE WAREJEA MAZOEZINI TAYARI KUWAVAA ZANACO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KOCHA Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema kuwa timu inaendelea na mazoezi na wachezaji wote wapo katika hali nzuri na wale waliokuwa majeruhi wamejiunga na wenzao katika mazoezi kuanzia jana tayari kwa kuwavaa Zanaco toka nchini Zambia siku ya Jumamosi..

Mwambusi amesema kuwa Donald Ngoma, Thaban Kamosoku na Amisi Tambwe wameanza mazoezi jana na wenzao ila mpaka sasa bado haijajulikana kama maamuzi ya benchi la ufundi kuwatumia katika mchezo wa Jumamosi wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Zanaco.

"tunaendelea na mazoezi yetu na tunamshukuru Mwenyenzi Mungu baadhi ya wachezaji wetu waliokuwa majeruhi ambao ni Ngoma Kamusoko na Tambwe tayari wamerejea na kuanza mazoezi na kikosi,kiujumla wachezaji wote wana umuhimu kwenye kikosi cha Yanga hivyo kwa yeyote ambae atatumika kwa upande wetu ni sawa na hakuna tatizo,"amesema  Mwambusi.

" Zanaco ni timu nzuri na kwa sasa inajengwa upya lakini kwenye soka katika mechi yoyote ile lazima ufanye vitu viwili kwa usahihi ; maandalizi mazuri na mipango sahihi ya ushindi kimbinu na kiufundi. Kushindwa katika hayo ni kufeli,"

Mchezo huo utakaochezeshwa na waamuzi kutoka nchini Djibout ni  Djamal Aden Abdi ambaye atapuliza kipenga wakati wasaidizi wake ni Hassan Yacin na Farhan Salime ilihali mwamuzi wa akiba atakuwa Souleiman Djamal.Kamisha katika mchezo huo Na. 61 atakuwa Luleseged Asfaw kutoka Ethiopia.

Kiingilio katika mchezo huo kwa mujibu wa Mratibu wa Mechi za Kimataifa wa Yanga Mike Mike ni Sh 20,000 kwa VIP ‘A’, Sh 10,000 kwa VIP ‘B’ na ‘C’ na Mzunguko (Viti vya Rangi ya chungwa, kijani na bluu) ni Sh 3,000.
Kikosi cha Yanga

LUGALO YAJIVUNIA MAFANIKIO YA MCHEZAJI WAKE UGANDA

$
0
0
Mshindi wa Divisheni A Nett Mashindano ya Enntebe Ladies Open 2017 kutoka Klabu ya Lugalo Vicky Elias akiwa katika harakati ya Mchezo huo katika Michuano iliyofanyika Uganda Hivi Karibuni.

Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Klabu ya Gofu ya jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo imejivunia kuanza vyema mwaka 2017 baada ya Mchezaji  wake Vicky Elias kuibuka na ushindi  wa Divisheni A Nett katika Mashindano ya Wanawake  Enntebe Ladies Open  yaliyomalizika hivi Karibuni nchini Uganda.

AKizungumza na Waandishi wa habari mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali  Mstaafu Michael Luwongo alisema Ushindi huo ni ishara tosha ya Mafamikio ya Kimchezo kwa mwaka 2017 kwani alikuwa mtanzania pekee kati ya Wachezaji 53  walioshiriki.

" Unajua tunajipanga kimataifa na tuliahidi kuweka nguvu katik mashindano kimataifa ,kwa mwaka 2017 na huu ndio mwanzo hivyo mashabiki wa Lugalo na Wanachama wajipange kufuarahia Timu yao kutokana na mafanikio yatakayopatikana kimataifa.

Aliongeza kuwa licha ya matokeo ya Kimataifa pia Michezo yeyote ambayo  Timu ya Gofu ya Lugalo itaalikwa basi watahakikisha wanafanya vyema ili adhama ya Timu ya Gofu ya Lugalo kuwa Timu Bora inatimia.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa ushindi wa Vicky ni Ushindi Mkubwa kutokana na Maandalizi pamoja na Washiriki waliojitokeza kushiriki michuano hiyo lakini ni sifa kwa Nchi kw sababu mbali na kutoka Klabu ya Lugalo lakini kubwa zaidi ni Mtanzania.

Kwa Upande wake Vicky Elias alisema mashindano yalikuwa magumu lakini alipambana kufa na kupona kurejesha heshima ya Klabu na Nchi kwa Ujumla na kufanikiwa kurejea na ushindi ambao haikuwa rahisi kwani siku ya kwanza alipiga mikwaju 83 na kutoa kiwango chake cha uchezaji ambacho ni Tisa.

Katika siku ya pili ya mashindano hayo Vicky aliibuka na Mikwaju ya Jumla 81 baada ya kutoa kiwango chake cha Uchezaji  cha Tisa na hivyo kuibuka na Ushindi wa Kwanza Divisheni  A na kuwashinda Wachezaji Wenzake kutoka Uganda na Kenya waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.

Wakati huo huo  kufuatia Maandalizi ya mashindano ya wachezaji wa Ridhaa nchini Tanzania Amature Stoke Play yanayotarajiwa kufanyika Moshi mkoani Kilimanjaro machi 12  Wachezaji wa Timu ya Lugalo wanaendelea na Mazoezi kujiwinda na Michuano hiyo.

Bingwa mtetezi wa mashindano ya   hayo kutoka Lugalo  Nicholous Chitanda amesema yuko katika maandalizi kujiandaa na michuano hiyo ili kutetea Ubingwa wake alionyakua mwaka jana ili kuhakikisha unabaki katika Klabu ya Lugalo.
Mshindi wa Divisheni A Nett Mashindano ya Enntebe Ladies Open 2017 kutoka Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Vicky Elias akiwa katika harakati ya Mchezo huo katika Michuano iliyofanyika Uganda Hivi Karibuni.
Bingwa Mashindano ya Wachezaji wa Ridhaa ya Moshi Mwaka 2016 Nicholous Chitanda akiwa katika harakati za mchezo huo.( Picha na Luteni Selemani Semunyu).

ELIMU KUHUSU MFUMO WA TREIMS YATOLEWA NJOMBE

$
0
0
Wizara ya Nishati na Madini kupitia Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) imeendesha mafunzo kuhusu mfumo mpya wa uhifadhi data na utoaji taarifa kwa ajili ya nishati jadidifu ujulikanao kama Tanzania Renewable Energy Information Management System (TREIMS) kwa wadau wa nishati jadidifu wenye lengo la kutangaza fursa za uwekezaji katika nishati jadidifu nchini, mjini Njombe
Msimamizi wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji (CADESE), Paul Kiwele akisoma hotuba ya ufunguzi kwa ajili ya mafunzo kuhusu TREIMS kwa wadau wa nishati jadidifu kwa niaba ya Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi, Styden Rwebangila
Sehemu ya wadau wa nishati jadidifu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika mafunzo hayo.
Msimamizi wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji (CADESE), Paul Kiwele (kushoto) akielimisha moja ya wadau katika mafunzo hayo

WLAC YATOA ELIMU JUU YA HAKI ZA MTOTO KWA WANAFUNZI WA HANANASIFU SEKONDARI

$
0
0
 Mwanasheria wa WLAC , Wigayi Kisandu akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kinondoni hananasifu juu ya umuhimu wa mtoto wa kike katika kukuza uchumi wa Tanzania na familia kwa kuweza kutambua haki zake na majukumu yake
 Kaimu Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Hananasifu Fatuma Niyopa akizungumza wakati wa mkutano huo ambao umewezesha wanafunzi wa kike kujitambua juu ya haki za mwanamke
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Hananasifu wakiwa katika kikao hicho na tasisi ya Msaada wa Kisheria kwa Wanawake WLAC

MARY MWANJELWA AONGOZA MAHADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE MKOANI MBEYA

$
0
0
  Mbunge wa Viti Maalum Mbeya, Mary Mwanjelwa akinyoosha mikono juu pamoja na wageni wengine wa meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake mjini Mbeya.
 Mbunge wa Viti Maalum Mbeya, Mary Mwanjelwa akipiga makofi wakati wa mahadhimisho ya Siku ya Wanawake mkoa wa Mbeya.
Mbunge wa Viti Maalum Mbeya mjini, Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa kajumuika na kina mama wenzake katika burudani, wahati wa hafla ya kuadhimisha siku ya wanawake mkoani mbeya

CHUO CHA MIPANGO- DODOMA CHAHIMIZA MATUMIZI YA TAFITI KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI

$
0
0

Na Benny Mwaipaja,WFM

Wadau wanaofanya tafiti mbalimbali za Maendeleo ya uchumi nchini hasa maeneo ya vijijini kuhusu Mabadiliko ya Tabia nchi wametakiwa kuwasilisha matokeo ya tafiti hizo Serikalini na katika Mashirika mengine ya Maendeleo ili matokeo yake yafanyiwe kazi na kusudio la tafiti hizo liweze kufikiwa.

Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini – Dodoma, Prof. Razack Lokina wakati wa Mkutano uliohusu mabadiliko ya tabia nchi na athari zake kiuchumi uliozihusisha Taasisi za Serikali na Binafsi pamoja na Washirika wa Maendeleo.

Amesema Chuo cha Mipango kimekuwa kikifanya kazi zake vijijini, zikiwemo za tafiti mbalimbali na matokeo hayo huwasilishwa katika ngazi husika ikiwemo Ofisi ya Makamu wa Rais inayoshughulikia mazingira pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii ili kutumia matokeo hayo kwa manufaa ya maendeleo ya jamii hasa vijijini. 

“Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia nchi ambao umejadili mbinu mbalimbali za kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na Mabadiliko hayo, umetokana na andiko la Wanafunzi wa Chuo hicho waliokwenda katika mafunzo kwa vitendo vijijini na kushuhudia namna mabadiliko ya tabia nchi yalivyoathiri maendeleo ya wananchi”. Alifafanua Prof. Lokina

Tayari Chuo kina mradi ujulikanao kama Chololo Ecovillage unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) Mkoani Dodoma, ambao huwafundisha wanakijiji njia bora za uzalishaji mali, hivyo kuwafanya baadhi ya Wananchi waliokuwa wanakosa chakula, kutokana na hali ya Ukame wa Mkoa huo kuanza kupata mazao ya kutosha na kuongeza pato lao.
Wajumbe wa mkutano wa Mabadiliko ya tabia ya nchi na athari zake kiuchumi hapa nchini uliokishirikisha Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini –Dodoma na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU), wakiingia kwenye ukumbi wa Mikutano mmoja Jijini Dar es salaam, siku ya kwanza ya mkutano huo wa Siku mbili.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini – Dodoma, Prof. Razack Lokina (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano uliohusu changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi wakati wa mkutano uliowashirikisha wadau wa maendeleo kutoka ndani nan je ya nchi na kuandaliwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini-Dodoma.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akichangia mada mbalimbali kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi yanavyoathiri uchumi wa wananchi vijijini nchini Tanzania, zilizowasilishwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini-Dodoma, na kufanyika Jijini Dar es salaam.

Utumiaji Holela dawa za maumivu waweza kusababisha magonjwa ya Figo

$
0
0

Watanzania wametakiwa kuepuka utumiaji holela wa dawa za maumivu ili kuepuka uwezekano wa kupata magonjwa ya Figo.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Figo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Jakline Shoo alipokua akiwasilisha mada katika maadhimisha siku ya figo Duniani, katika kongamano la kitaaluma lililofanyika leo katika ukumbi wa CPL uliopo ndani ya Hospitali hiyo.

Akifafanua Dk. Shoo amesema ni vema watu wakaepuka matumizi holela ya dawa za maumivu kwani ni chanzo cha magonjwa ya figo lakini pia kuepuka unene uliokithiri kwa kula mlo bora na kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa ya Kisukari na shinikizo la damu ambayo yanachangia mtu kupata ugonjwa sugu wa figo.

Akielezea kuhusu wagonjwa wanaohudumiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Shoo amesema katika Kiliniki yao kwa kila mwezi huwaona wagonjwa watu wazima kati ya 120 hadi 150 .

Pia takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 10 ya watu Duniani tayari wanaugua ugonjwa sugu wa figo na kwamba inakadiriwa ifikapo mwaka 2025 asilimia 70 ya wagonjwa watakua wanatokea katika nchi zilizopo Ukanda wa Jangwa la Sahara.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Figo Duniani mwaka huu ni ugonjwa wa figo na uzito uliozidi , mienendo bora ya maisha kwa ajili ya afya bora ya Figo.
Dk. Gudila Valentine akiwasilisha mada kuhusu ugonjwa wa Figo katika kongamano la kitaaluma ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Figo Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Machi 9.
Baadhi ya Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali kuhusu magonjwa ya Figo zilizowasilishwa katika kongamano hilo leo .
Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimuhudumia mgonjwa katika kitengo cha Figo, kushoto ni kiongozi wa kitengo hicho Sister Judith Mwaipopo na kulia ni Sister Lucy Kyombo.

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUTEMBELEA KITUO CHA PEDDEREF SOBER HOUSE KIGAMBONI

$
0
0
Maafisa na Askari (Wanawake) wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Mkurugenzi wa People With Drugs Dependence Relief Foundation (Pedderef)bi. Nuru Salehe wa kwanza mbele (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wanawake waliopata kuathirika na madawa ya kulevya kituoni hapo, ambapo wanawake hao wameanza kurejea katika hali zao za kawaida mara baada ya kupewa elimu na malezi yanayostahili.

Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeungana na wanawake duniani kuadhimisha siku hiyo

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi alisema katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano (5) kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya, kupitia Jeshi hilo Nzalayaimisi aliwaongoza Askari (wanawake) kutembelea kituo cha Pedderef Sober House na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali.

Ambapo aliiomba jamii isiwanyanyapae pamoja na elimu wanayoendelea kuipata kituoni hapo ameiasa jamii kujitokeza kuwasaidia na kuwawezesha kwa hali na mali ili waweze kujiajili wenyewe kwani wanapotoka kituoni hapo wanakuwa hawana uwezo wakujiajili na kujikuta wanarudia tena kwenye janga la madawa hayo.

Pia Nzalayaimisi aliendelea kusema kwa kutoa pongezi kwa serikali na wadau mbalimbali wote waliojitokeza na kuthubutu kufanya maamuzi ya kujitoa katika kupambana na janga hilo na pia alimpongeza mkuu wa mkoa wa dar es salaam paul makonda kwa kuongoza mapambano hayo.

Mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe naye alisema napenda kutoa shukrani za kipekee kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa msaada wao wa hali na mali waliotupatia na kuomba taasisi nyingi na wadau mbalimbali kujitokeza katika kusaidia kituo hiki kwani wengi wamenufaika kutokana na elimu na malezi wanayoendelea kuyapata kituoni hapo.


Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jennifer Shirima ambaye aliambatana na msemaji wa Jeshi hilo katika ziara hiyo akiwasisistizia wanawake hao kutoajiingiza tena kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya na kuwakumbusha kuwa “Wanawake ni msingi wa mabadiliko kiuchumi” (kulia) ni Mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe na (kushoto) ni Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi ambaye pia ni msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Moja ya wanawake waathirika wa madawa ya kulevya bi.Jacqueline Samson aliyesimama (katikati) akitoa shukrani kwa viongozi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambao hawapo picha kwa kuwatembelea kituoni hapo pia kwa msaada waliowapatia. 
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images