Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

VODACOM YASHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KISHINDO NA AKINAMAMA WA MKOA WA DODOMA

0
0
 Mkuu wa maduka ya rejareja  wa Vodacom Tanzania,Brigita Stephen (kushoto) akimkabidhi zawadi ya simu mjasiliamali Neema Nzuki aliyejiajiri na  kuwaingiza  wateja wapya wa Vodacom Tanzania wa manispaa ya Dodoma,Wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa  ujasiliamali mkoani hum oleo yaliyoandaliwa na Vodacom Tanzania.
 Akina mama wajasiliamali wa Mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye picha ya pamoja baad ya kushiriki mafunzo ya siku moja yaliyotolewa na Vodacom Tanzania leo  katika maadhimisho ya siku ya wananawake Duniani.
 Mkuu wa maduka ya rejareja ya Vodacom Tanzania, Brigita Stephen akikata keki na Katibu wa Voice of Women Entrepreneurs Tanzania (VOWET) Anna Otieno ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Wananawake Duniani leo mjini Dodoma.
 Mkuu wa maduka ya rejareja ya mauzo ya simu Vodacom Tanzania,Brigita Stephen  akizungumza na akina mama wajasiliamali wa mkoa wa Dodoma leo,Wakati wa mafunzo ya ujasiliamali kwa akina mama hao katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani.
Mwezeshaji wa masomo ya ujasiliamali Ben Mwambela akitoa mada ya ujasiliamali kwa akinamama wa mkoa wa Dodoma  leo katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani,mafunzo hayo yalifadhiliwa na Vodacom Tanzania. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Skuli ya Kijini na Mbuyu Tendee Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja,Wafaidika na Mradi wa Ujenzi wa Kijiji cha Utalii Cha PennyRoyal kwa Kutoa Elimu ya Afya na Mazingira

0
0
Maafisa Afya na Mazingira kutoka (SUZA) Nahya Khamis Nassor Mwanafunzi wa mwaka wa Tatu wa Chuo cha SUZA anayetowa mafunzo ya Afya na mazingira kwa Wanafunzi wa Skuli ya Kijini Matemwe akizungumza na waandishi wa habari kufanikiwa kwa zoezi hilo la kutowa elimu kwa wanafunzi wa Skuli hiyo jinsi ya kuhifadhi mazingira na afya yao. Mradi huo unaosimamiwa na Kampuni ya Ujenzi wa Kijiji cha Kitalii Matemwe Pennyroyal kwa kutowa elimu hiyo.
Amesema umeleta mafanikio makubwa kwa watoto hao jinsi ya kujilinda na maradhi ya mripuko kwa kupata elimu hiyo.
Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu wa SUZA Nahya Khamis Nossor akitowa mafunzo ya Afya ya Mazingira kwa Wanafunzo wa Skuli hya Sekondari ya Kijini Matemwe jinsi ya kujikinga na maradhi ya mripuko kwa kutunza mazingira safi katika maeneo yao na skuli, Mradi huo wa Elimu hiyo unafadhiliwa na Kampuni ya Ujenzi wa Kijiji cha Utalii Matemwe  Pennyroyal.  
Wanafunzo wa Skuli ya Sekondari na Msingi Kijiji cha Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakifuatila mafunzo hayo wakiwa katika darasa wakifuatilia kwa utulivu  wakiangalia vipeperushi vinavyoelezea utungaji wa Afya na Mazingira katika jamii.

Afisa Afya na Mazingira Bi Zeldat Masoud Khamis akitowa mafunzo kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kijini Matemwe jinsi ya elimu ya afya ya mazingira kwa wanafunzi hao. 
Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kijini Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja wakifuatilia Mafunzo hayo yanayotolewa na Maafisa wa Afya na Mazingira wakitowa elimu hiyo.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

VIWANGO VYA MICHANGO KWA WANACHAMA WA NHIF

Experience Korea in Tanzania: “Building Connections and Strengthening Ties Through Education” May 25th – 27th, 2017. Dar es salaam, Tanzania

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

WAZIRI MKUU MAJALIWA AHUDHURIA MAZISHI YA MAMA YAKE MDOGO MHE JAKAYA KIKWETE

0
0
Rais Mstaafu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohudhuria mazishi ya Bibi. Nuru Halfan Kikwete ambaye ni mama mdogo wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne mheshimiwa Dk. Jakaya Kikwete nyumbani kwa marehemu Bagamoyo mkoani Pwani leo Machi 8, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Bibi. Nuru Halfan Kikwete ambaye ni mama mdogo wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne mheshimiwa Dk. Jakaya Kikwete nyumbani kwa marehemu Bagamoyo mkoani Pwani leo Machi 8, 2017. Kulia ni Rais Mstaamu Dk. Kikwete (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Female pilots fly Emirates A380 for International Women's Day

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 08.03.2017


introducing newest & hottest joint in Dar es salaam - BAR 21 @ Mbezi Beach Interchick China town complex

MICHUZI TV: MWANAMITINDO KHADIJA MWANAMBOKA AADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUJUMUIKA NA MARAFIKI

0
0
Wakati Tanzania na Dunia nzima kwa ujumla zikiadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, leo Machi 8, 2017, Mwanamitindo nguli hapa nchini na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Vitu Vya Khadija, Bi Khadija Mwanamboka aliungana na wanawake wengine jijini Dar es salaam katika kuisherehekea siku hiyo muhimu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwanamboka alisema kuwa aliamua kuwaalika marafiki zake katika siku hiyo ili kuwataarifu mpango wake mpya alioupata kupitia Shirika lisilo la kiserikali la Sense International la nchini Uingereza lenye nia ya kuwasaidia watoto wenye ulemamu wa kusikia na kuona kwa pamoja waliopo hapa nchini, ambapo wataanzisha kitu kinaitwa Pendeza Kids Collection kwa kubuni mavazi mbalimbali ambayo yatauzwa katika Duka la Shirika hilo la Sense lililopo nchini Uingereza na zingine zitauwa hapa hapa nchini ili kuwasaidia watoto hao.

Hafla ya kuisherehekea siku hiyo adhimu kwa kina mama, ilifanyika katika Ukumbi wa Kamarambezi, Seacliff jijini Dar es salaam.
Khadija Mwanamboka (kati) akiwa na Marafiki zake waliofika kumuunga mkono katika mpango wake mpya wa kuwasaidia Watoto wenye ulemavu wa kusikia na kuona alioshirikiana na Kam
Sehemu ya Marafiki wa Khadija Mwanamboka waliohudhulia hafla hiyo.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

KAMATI ZA BUNGE KUANZA KUKUTANA MACHI 20 HADI TAREHE APRIL 2, 2017

0
0
Kamati za Kudumu za Bunge zitaanza kukutana Mjini Dodoma kutekeleza majukumu yake kuanzia Tarehe 20 Machi, 2017 hadi Tarehe 2 Aprili, 2017 kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Saba wa Bunge uliopangwa kuanza Tarehe 4 Aprili 2017. Kufuatia shughuli hizi za Kamati, Waheshimiwa Wabunge wanatarajiwa kufika Mjini Dodoma Jumapili tarehe 19 Machi, 2017.

Pamoja na Shughuli nyingine zitakazotekelezwa na Kamati katika Kipindi hiki, kuanzia Tarehe 20 hadi 27 Machi 2017, Kamati zitatembelea maeneo mbalimbali nchini kukagua miradi ya maendeleo iliyotengewa fedha kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 inayotekelezwa na Wizara/Idara zinazosimamiwa na Kamati husika.

Baada ya ziara hizo kukamilika, Kamati zitachambua Taarifa za utekelezaji wa Bajeti za Wizara inazozisimamia kwa Mwaka wa Fedha unaoisha kwa ajili ya kufanya ulinganisho kuhusu makadirio ya matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha unaofuata.

Aidha, kulingana na matakwa ya kikanuni, Tarehe 28 Machi, 2017 kutakuwa na Mkutano wa Wabunge wote kwa ajili ya kupokea Mapendekezo ya Serikali kuhusu Mpango na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Ratiba zote za Shughuli za Kamati za Bunge ikiwa ni pamoja na maeneo ambayo kamati hizo zitafanya ziara, vinapatikana katika Tovuti ya Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz.

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
DODOMA

MICHUZI TV: MUIGIZAJI LULU ASEMA HAYA KATIKA SIKU YA WANAWAKE

Serikali ya Kenya yawataka madaktari wote wanaogoma kurejea kazini haraka, wenyewe waendelea na msimamo wao

0
0
Madaktari nchini Kenya wamesema hawatarejea kazini licha ya agizo la Serikali kuwataka kurejea kazini haraka iwezekanavyo na kutangaza pia kuondoa nyongeza ya asilimia 50 waliyokubali kuilipa hapo awali.

Tangazo hili la kushangaza la Serikali limetolewa baada ya mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kugonga mwamba, madaktari hao wanataka nyongeza ya asilimia 150 hadi 180.

Kwenye makubaliano mapya yaliyofikiwa kwa msaada wa wapatanishi uliojumuisha ujumbe wa viongozi wa dini, madaktari hao walitakiwa kutia saini hati ya kukubali kurejea kazini na kuanza kazi mara moja, lakini hata hivyo viongozi wa madaktari wamegoma kutia saini.

Mgomo huu unaojumuisha zaidi ya madaktari elfu 5 nchini Kenya kutoka kwenye hospitali za uma, sasa umefikia miezi mitatu na kwa hali hii hakuna dalili ya kusitishwa kwa mgomo wenyewe.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta anasema kuwa madaktari hao wanailaghai na kuihujumu Serikali yake.

Mgomo huu ambao ulianza mwezi Desemba mwaka jana, umeibusha hasira miongoni mwa wa Kenya na kuongeza shinikizo kwa Serikali ya rais Kenyatta kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti mwaka huu.

Makubaliano ya awali na haya yaliyokuwa yanaratibiwa na viongozi wa dini, yalitaka pia kuboreshwa kwa mazingira ya kazi ya madaktari, kurekebishwa kwa mifumo ya kazi na vigezo vitakavyotumika kupandishwa vyeo.

Mgomo huu pia umesababisha hata baada ya viongozi wa madaktari nchini humo kutupwa jela baada ya kukutwa na hatia ya kukaidi amri ya mahakama kusitisha mgomo. Chanzo: RFI Kiswahili.

WAZIRI SIMBACHAWENE AFANYA UKAGUZI WA USAFI MAENEO MBALIMBALI MJINI DODOMA

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akiambatana na Afisa Masoko Manispaa ya Mji wa Dodoma, Stephen Maufi katika ziara fupi ya kutembelea na kukagua usafi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akifurahia ubunifu wa uhifadhi wa mbogamboga na matunda katika ziara fupi ya kutembelea na kukagua usafi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene na Naibu Katibu Mkuu Afya , Dkt. Zainabu Chaula wakiangalia mrefeji wa maji machafu uliopo katika Soko la Mwembeni katika ziara fupi ya kutembelea na kukagua usafi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akizungumza na mmoja wa wafanya biashara katika soko la Mwembeni Bw. Mjahidina Hassani katika ziara fupi ya kutembelea na kukagua usafi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma.

WANAWAKE WANAOFANYA KAZI MGODI WA BULYANHULU WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA BAISKELI KWA WANAFUNZI WA KIKE NA SHUKA VITUO VYA AFYA

0
0

Wanawake wanaofanya kazi katika Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu uliopo katika halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wameadhimisha siku ya wanawake duniani Machi 8,2017 kwa kutoa zawadi ya baiskeli kwa wanafunzi wa shule za sekondari pamoja na kuwatembelea na kuwapatia zawadi wagonjwa waliolazwa kwenye vituo vya afya.

Wanawake hao wametoa zawadi ya baiskeli 10 zikiwemo 8 kwa ajili ya wanafunzi waliofanya vyema katika masomo yao katika shule ya Sekondari Bulyanhulu na Bugarama na baiskeli mbili kwa ajili ya walimu wa kike walezi wa wanafunzi hao.

Mbali na kutoa zawadi kwa wanafunzi,pia wametembelea kituo cha afya cha Bugarama na Lunguya vilivyopo jirani na mgodi huo kisha kutoa zawadi ya shuka 70 kila kituo na kuwapa wauguzi na wagonjwa sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa za meno vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 12.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya wanawake,Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo alisema wameamua kusherehekea siku hiyo muhimu kwa kuwapongeza wanafunzi wanaofanya vizuri shuleni ili kuwapa ari ya kujifunza zaidi na kuwarahisishia usafiri kufika shuleni.

“Tuwatembelea wanafunzi wa shule ya sekondari Bulyanhulu na Bugarama,tumetoa msaada wa baiskeli 10 hivyo kila shule imepata tano ambapo nne kwa ajili ya wanafunzi kike na moja ni kwa ajili ya walimu wa kike kwa kila shule”,alieleza Senkondo.

“Pia tumetoa shuka 140 kwa ajili ya vituo vya afya viwili,Bugarama na Lunguya kisha kugawa sabuni,mafuta na dawa za meno kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa waliopo katika vituo hivyo”,aliongeza Senkondo.

Senkondo alisema wameamua kushiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa kukutana na watoto wa kike na wanawake ili kuwahamisha wanawake katika jamii kushiriki katika shughuli za migodi kwani wanaweza.

Mwandishi wetu Kadama Malunde,alikuwepo wakati wa maadhimisho hayo,ametuletea picha za matukio yaliyojiri mwanzo hadi mwisho…Tazama hapa chini .

Wafanyakazi wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiwa wamebeba mtoto aliyezaliwa na Salome Raphael baada ya kumpatia zawadi ya vipande 10 vya sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa ya meno 


Hapa ni katika Kituo cha afya Bugarama kilichopo katikakata ya Bugarama halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama.Kituo hiki cha afya kimepewa shuka 70 kwa ajili ya wagonjwa.Kulia ni Muuguzi katika kituo hicho Mwalushani Mabula akizungumza wakati wa kupokea shuka 70,sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa za meno kwa ajili ya wagonjwa waliokutwa katika kituo hicho siku ya siku ya wanawake duniani Machi 8,2017

Mwalimu Bumi Mwasalujonja akiwa amebeba juu baiskeli wakati akikabidhiwa na wanawake kutoka mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu

Wanafunzi wa shule ya sekondari Bulyanhulu wakiwa katika shule hiyo iliyopo katika kata ya Kakola halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakisubiri kupata zawadi kutoka kwa wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia dhahabu wa Bulyanhulu uliopo jirani na shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 920 wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani


RC Maganga apiga marufuku vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake mkoani Kigoma,awataka waachwe wachangamkie fursa za kimaendeleo.

0
0
Na Rhoda Ezekieli Kigoma

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga amepiga marufuku vitendo vya baadhi ya wanaume Mkoani humo kuwadhurumu na kuwatishia kuwafukuza wake zao pindi wanapothubutu kutetea haki zao,badala yake amewataka washirikiane nao kutambua na kuchangamkia fursa za maendeleo zilizopo nchini.

Mkuu huyo wa Mkoa aliitoa kauli hiyo wakati akifunga maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mkoani humo ambayo kimkoa yalifanyika katika kijiji cha kinyinya kata ya nyamutukuza wilayani kakonko Mkoani humo .
 
RC Maganga alisema kuwa pamoja na mambo mengine, wakati umefika kwa wanawake kuamka na kusimamia haki zao ikiwa ni pamoja na kutokukubali kubaki nyuma kwa kuchangamkia fursa hizo zinapozitokeza.

Alisema kumekuwa na tabia ya Wanaume wengi,Wake wanapo kuwa wakijishughulisha kutafuta fedha ili kuzitunza familia zao, wanawanyang'anya na kwenda kuzitumia kwenye  starehe zao, suala ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya Wanawake wengi.
 
Katika kuhakikisha suala la kuwa Nchi ya viwanda, ni lazima wanawake kushirikiana na wanaume katika kufanya kazi ili kuongeza kipato katika familia na taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akitoa zawadi kwa mmoja wa akina mama aliyejifungua katika kituo cha afya cha Nyanzige,Wilayani Kakonko mkoani Kigoma.
RC Maganga akiwasikiliza akina mama mbalimbali waliofika katika kituo cha afya cha Nyanzige,Wilayani Kakonko mkoani Kigoma kujipatia matibabu mbalimbali,kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko,Kanali Hosea Ndagala
Akina Mama wakisherehekea siku ya Wanawake hapo jana
RC Maganga akiwa ameongozana na DC wa Kakonko,Kanali Hosea Ndagala wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa wajasiliamali,kufuatia bidhaa zao walizozitengeneza.

RAIS DKT SHEIN AREJEA NCHINI

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (katikati) wakiagana na Mhe, Airlangga Hartarto ambae ni miongoni mwa Viongozi wakuu Nchini Indonesia katika uwanja wa Ndege wa Soekarno Hatta Mjini Jakarta Nchini Indonesia baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi IORA Nchini humo Dk.Shein alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na kuagana na Mhe, Airlangga Hartarto ambae ni miongoni mwa Viongozi wakuu Nchini Indonesia katika uwanja wa Ndege wa Soekarno Hatta Mjini Jakarta Nchini Indonesia baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi IORA Nchini humo akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (kushoto) wakizungumza na kuagana na Mhe, Airlangga Hartarto ambae ni miongoni mwa Viongozi wakuu Nchini Indonesia katika uwanja wa Ndege wa Soekarno Hatta Mjini Jakarta Nchini Indonesia baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi IORA Nchini humo Dk.Shein alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, 

[Picha na Ikulu.] 09/3/2017.

SBL mdau muhimu wa maendeleo kiuchumi-Rc Mwanza

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella leo ameipongeza Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa kuzalisha bidhaa zenya ubora wa hali juu jambo ambo limiweizesha kampuni hiyo kushinda tuzo mbalimbali za ubora ndani na nje ya nchi.

Mongella alitoa kauli hiyo wakati alipokitembelea kiwanda cha Bia cha SBL cha Mwanza ambako pia aliipongeza kampuni kwa mchango wake katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi kupitia uzalishaji wa ajira, ulipaji kodi na hali kadhalika programu za kusaidia jamii.

“SBL ni mdau katika ajenda ya maendeleo ya nchi yetu. Kama serikali tutajaribu kuanzisha mazingira ambayo yanawezesha biashara kama hii ili istawi vizuri na kuvutia uwekezaji pia,” alisema Mongella.

SBL inazalisha chapa za bia ambazo ni Serengeti Premium Lager, Pilsner, Tusker Lager, TuskerLite, Kibo Gold, Guinness stout, Uhuru na Kick na hali kadhalika kusambaza pombe kali zinazofahamika duniani ambazo zinazalishwa na kampuni yake uwekezaji Diageo.

Mwezi uliopita Kiwanda cha SBL cha Mwanza kilianza uzalishaji wa bia chapa Allsopps ambayo inauzwa katika soko la Afrika mashariki.

“Hatua ya kuzalisha Allsopps katika kiwanda chetu cha Mwanza ni sehemu ya mbinu ya uendeshaji kikanda ya EABL. Hili limekuwa na matokeo ya kunufaisha kwa masoko yote na kwa biashara yetu,” alisema Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, John Wanyancha.

Kwa mujibu wa Wanyancha, SBL inaendesha miradi kadhaa ya kuisaidia jamii nchi nzima katika maeneo ya upatikanaji wa maji, utoaji wa elimu- ambapo wanafunzi walio na weledi mkubwa kutoka mazingira yenye uhitaji hupatiwa udhamini wa masomo kwa ajili ya kusomea kozi za shahada ya kwanza katika vyuo vikuu vya ndani na hali kadhalika kampeni ya Ukiwa Umekunywa Usiendesha gari ambayo inahamasisha unywaji wa kistaarabu.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela(katikati) akionyesha kwa waandishi wa habari bia mpya ya chapa Allsopps ambayo inauzwa katika soko la Afrika mashariki., kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha na Meneja kiwanda Dominic Mkemangwa. 
Waandishi wa habari wakishuhudia uzinduzi wa bia chapa
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akiongozana naviongozi wa SBL na waandishi wa habari maeneo ya kiwanda cha Bia cha SBL cha Mwanza mara baada ya uzinduzi wa wa bia chapa Allsopps ambayo inauzwa katika soko la Afrika mashariki. 

MPINA AIPONGEZA MIRADI YA MUUNGANO PEMBA

0
0
NA Evelyn E. Mkokoi – Pemba

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masula ya Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ameipongeza Miradi ya tasisi za Muungano Kisiwani Pemba, kwa kile alichodai, kutekelezeka kwa asilimia kubwa na kutatua kero za wananchi.

Naibu Waziri Mpina Aliyasema hayo Kisiwani Pemba katika ziara yake ya kutembelea na kukagua baadhi ya miradi inayotekelezwa chini ya taasisi za muungano na mashirika ya TASAF na MIVARF, ikiwa ni pamoja na miradi ya ujenzi wa soko, barabara, hospitali shule, ujenzi wa mabwa, matuta kama makingio ya maji ya chumvi yanayosaidia kuhimili madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na miradi mbali mbali ya maendeleo.

Mpina aliwataka wakazi wa kaskazini na kusini Pemba kwa Pamoja kushirikiana na waithamini na kuitunza miradi hiyo inayotekelezwa kwa thamani ya shilingi za kitanzania Bilioni 14.297,na kusema kuwa ina manufaa kwa wakazi hao, na itaweza kudumu na kuwasidia kwa muda mrefu, akitolea mfano wa barabara yenye urefu wa kilometa 80 iliyojenjwa kusini Pemba.

Alipotembelea mradi wa umeme unaopita chini ya Bahari kutoka mkoani Tanga, Mpina alisema kuwa, awali kisiwani Pemba umeme ulikuwa unawafikia watu wachache, lakini kwa sasa umeme umekuwa ni wa Bei nafuu wa uhakika naunawafikia watu wengi.

Katika Ziara yake kisiwani Pemba, Naibu Waziri Mpina Pia alitembelea jengo la Makazi ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Kusema kuwa jengo hilo linatakiwa kutengewa fedha maalumu kwa ajili ya ukarabati, “viongozi wetu wakifanya kazi katika mazingira mazuri itaongeza ufanisi katika utendani wao.” Alisisitiza Mpina.

Naibu Waziri Mpina takuwepo kisiwani Unguja na Pemba kutembelea na kukagu miradi ya Muungano.
Naibu Waziri ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, akipongeza miradi ya muungano kisiwani Pemba, wakati wa Ziara yake ya kutembelea Miradi Hiyo, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya ChakeChake Bi Salama Mbarouk.
Mratibu wa Mradi wa TASAF kisiwani Pemba Bw. Mussa Said Kissenge akielezea utekelezaji wa majukumu ya Mradi huo kisiwani pemba Kwa Mhe. Luhaga Mpina na ujumbe wake (hawapo pichani) wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Huyo ya kutembelea Mirani ya Muungano kisiwani Pemba.
Katika Picha ni moja ya tuta lililojengwa na mradi wa TASAF kisiwani Pemba, kunusuru maji ya chumvi kuingia katika mashamba ya wakulima na kuharibu mazao kisiwani Pemba, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa miradi ya Muungano.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Mpina akichanganya Saruji na mchanga kuwasaidia mafundi wanaojenga bwawa la kuhifadhia maji ya mvua, litakalotumika kuhifadhi maji kwa matumizi ya kilimo na mifugo kisiwani Pemba, ikiwa ni moja ya utekelezaji wa miradi ya Muungano chini ya TASAF.
Katikati Injinia Said Kiure, wa Kiure Contraction ya Kisiwani Pemba, akimuelezea jambo Naibu Waziri Mpina, kuhusu ujenzi wa soko la wilaya ya Mwanakwerekwe linalojengwa chini ya mradi wa Muungano wa MIVARF.kushoto ni Mkurugenzi msaidizi Idra ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Lupi Mwaikambo.

MIKAKATI YA SERIKALI KATIKA KUMUINUA MWANAMKE KIUCHUMI

0
0
Jovina Bujulu – MAELEZO.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, ni hatua muhimu kwa wanawake kujipambanua na kufanya tathmini jinsi wanavyoshiriki katika ujenzi wa taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Serikali imeweka mikakati na mipango mbalimbali yenye lengo la kumkomboa na kumuinua mwanamke kiuchumi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, mama Sihaba Nkinga hivi karibuni alipokuwa akizungumzia mipango na mikakati mbalimbali iliyofanywa na Serikali katika kumkomboa na kumuinua mwanamke kiuchumi.

Pamoja na kuwa wanawake wengi wameamka na wanajishughulisha katika masuala mbalimbali ya kiuchumi, Serikali pia inahakikisha inawawezesha ili waweze kufikia malengo yao katika masuala ya kujiinua kiuchumi na kuondokana na dhana ya utegemezi.

“Serikali ina mipango mbalimbali katika kuhakikisha kuwa wanawake wamewezeshwa kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kuanzisha benki ya Wanawake ambayo moja ya majukumu yake ni kuhakikisha wanawake wanapata mikopo kwa kuzingatia viwango wanavyoweza kulipa” alisema mama Nkinga.

Aliitaja mikakati mingine kuwa ni pamoja na kuwa na mfuko wa maendeleo ya wanawake ambapo wanawake wanapewa mikopo yenye riba nafuu ambayo wanamudu kuilipa.

Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images