Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1604 | 1605 | (Page 1606) | 1607 | 1608 | .... | 3272 | newer

  0 0
  0 0

  Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limemshikilia Mwanamziki Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya.

   Mwanasheria wake, Aman Tenga ametihibitisha kuwa mteja wake amejisalimisha mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi, kama ilivyoagizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akitaja majina ya wanaojihusisha biashara hiyo pamoja na watumiaji mapema mwezi uliopita.

   Mwanasheria Tenga pia ametihibitisha kuwa Vanessa alikuwa Afrika Kusini kikazi wakati jina lake likitajwa na Mkuu wa Mkoa. Pia aliongeza kuwa Polisi walikwenda Nyumbani kwa Vanessa kufanya upekuzi kabla ya kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi.

  Vanessa Mdee ni Mtanzania wa kwanza kuwa mtangazaji wa MTV VJ, Mdee, alizaliwa mwaka 1988 Arusha, alianza kufahamika zaidi mara baada ya kutangaza kwenye Redio na Luninga kwenye vipindi kama Epic Bongo Star Search na Dume Challenge na baadae kidogo wakati ananza kujikita kwenye muziki alikuwa chini ya Lebo B'hitts.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Marais wa Nchi nyengine wakipiga ngoma kama ishara ya ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (INDIAN ASSOCIATION-IORA) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt John Pombe Magufuli,mkutano huo ulifanyika jana katika ukumbi wa Balai Sindang Mjini Jakarta Indonesia.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kushoto)akiwa na ujumbe wake jana baada ya kumalizika kwa mkuutano wa kwanza wa Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (INDIAN ASSOCIATION-IORA) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt John Pombe Magufuli,mkutano huo ulifanyika jana katika ukumbi wa Balai Sindang Mjini Jakarta Indonesia,(kushoto) Rais wa Sychells Mhe,Danny Faure.(Picha na Ikulu, Zanzibar)

  0 0

  Na  Bashir  Yakub.
  Mara  nyingi  wazazi  wanapotengana  huwa  tunashuhudia  mabishano  ya  nani  anatakiwa  kukaa  na  mtoto. Ni  mama au  baba.  Kwa  suala  hilihili wapo  watu  wako  mahakamani  na  wengine  hawako  mahakamani  lakini  wako  katika  ugomvi  mkubwa  wa  nani  haswa  akae  na mtoto.

  Wapo  ambao  walikuwa  katika  ndoa  na  sasa  ndoa  imevunjika,  wapo  ambao  walikuwa wakiishi  kama  mke  na  mme  lakini  bila  ndoa  na sasa  mahusiano  yao  yamekwisha  na  wapo  ambao  hawakuwahi  kufunga  ndoa  wala  kuishi  kama  mke  na  mme ila  walizaa  tu  ila  kwasasa  wapo  katika  mgogoro  wa  nani  akae  na  mtoto.

  Makala  yataeleza namna  sheria  inavyozungumza  kuhusu  umri  wa  mama  kukaa  na  mtoto  lakini  kabla  ya hilo  ni  vema  pia  kutizama  ni  wapi  waweza  kupeleka malalamiko  ya  jambo  hili. Sheria  ya  Mtoto ,  namba 21 ya  mwaka  2009 ndiyo  inayohusika  katika  jambo  hili.

  1.WAPI  UKALALAMIKE  UKITAKA  KUKAA  NA  MTOTO.

  Zipo  sehemu  mbili  ambazo  waweza  kupeleka malakamiko  yako  ili  uweze  kupatiwa  haki  ya  kukaa  na  mtoto.  Kwanza  ni  ustawi  wa  jamiii  na  pili  ni  mahakamani. 

  Mahakama  yoyote  ya  mwanzo,  wilaya,  hakimu  mkazi  hata  mahakama kuu  unaweza  kupeleka  mombi  haya.  Ila  ni vema  ukaanza  mahakama  ya  mwanzo  au  wilaya. 

  Tofauti  ya  ustawi  wa  jamii  na  mahakamani   ni kuwa mahakama  wana  amri  wakati   ustawi  wa jamii  hawana  amri( order) .  


  0 0


  0 0

  Mwana Ilala na  Dar-Es-Salaama mashuuri, maarufu Bi. SITU MWASA amefariki dunia siku ya jumanne Machi 7, 2017, marehemu Bi. Sita Mwasa Kipenzi na mtu wa watu aliyekuwa msatari wa mbele kila wakati katika shughuli za kijamii hapa jijini Dar-es-salaam atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika jamii hapa ILALA na jiji zima la Dar-Es-Salaam, ameshika nyadhifa mbali mbali katika jamii pia akiwa kada mashuuri wa chama tawala CCM. mara ya mwisho marehemu Bi. Situ Mwasa aliandika katika ukurasa wake wa Facebook (bofya hapa) kuwa anaumwa majeraha kutoka na ajali ya kupinduka na gari, lakini hatujui nini kilichosababisha kifo chake,
  Mwenyezi Mungu amlaze pema peponi.
  Innah Lillah wa Innah Lillah Rajiun

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akizungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Rogers Sianga, wakati Kamishna huyo alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya dawa za kulenya nchini.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akimuaga Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Rogers Sianga, mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO.

  Dunia ya sasa inapigania haki sawa kwa wanaume na wanawake ili waweze kushiriki kwa pamoja kwenye nyanja zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa ajili ya kuchangia kwenye ukuzaji wa pato la taifa na kupelekea kukua haraka kwa maendeleo ya nchi.

  Tumeshuhudia wanawake wengi nchini wakijikita katika kufanya biashara na ujasiriamali wa bidhaa na huduma mbalimbali ambazo zinawakomboa kiuchumi na kuwafanya waweze kujitegemea kama walivyo wananume. 

  Wanawake hao waliojiamini na kuamua kuanzisha biashara zao wameonekana kuwa na mafanikio makubwa ambayo yanasaidia kuinua uchumi wa mtu binafsi na wa nchi kwa ujumla.

  Kwa upande mwingine, baadhi ya wanawake wamekua bado hawana ujasiri wa kuanza kufanya ujasiriamali kwa kuhofia kuwa hawataweza kuendelea na wengine wakihofia waume zao kuwakataza.

  Dhima ya kujirudisha nyuma waliyonayo baadhi ya wanawake ndio inayorudisha nyuma hata maendeleo ya nchi hasa kwa wakati huu ambao Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kujikita katika kukuza uchumi wa viwanda.

  SOMA ZAIDI HAPA

  0 0


   Kikao cha siku tano cha wabobezi/wataalamu katika mambo ya miliki bunifu,kinaendelea kufanyika katika moja ya ukumbi wa mikutano katika Shirika la Utafiti na maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO),Msasani jijini Dar,ambapo kikao hicho kimejumuisha Wadau kutoka Serikalini sambamba na Sekta binafsi.

  Mchakato wa kikao hicho unafuatia wakati shirikisho la filamu Tanzania (TAFF) lilipoanza kufanya mchakato wa tatifi ya sera ya miliki bunifu  tangu miaka minne iliyopita kwa kufadhiliwa na  wahisani ‘Best Dialogue’ ,ambapo mwaka 2013 inaelezwa kuwa tafiti hiyo ndio ilipelekwa rasmi Wizarani  kwa ajili ya kuendelea na mchakato zaidi.

  Rais wa Shirikisho la Filamu hapa nchini (TAFF),Simon Mwakifwamba,alisema kuwa Mkutano huo wa kuhitimisha rasimu ya sera ya miliki bunifu,ni sera ambayo ilipatikana kwa kufuata taratibu zote, kwa maana ya ushirikishwaji kwa upande wa serikali na Sekta binafsi,Mwakifwamba alisema kwa upande wao kama wasanii hiyo ndio sehemu yenyewe muhimu ambayo wasanii wamekuwa wakiiliia kwa muda mrefu.

  "Kwa mchakato huu sisi kama wadau tunasema kwamba hapa tulipofika tuko pazuri, na nina imani na wataalamu hawa kwamba tukiwa  na juhudi za pamoja tutaweza  kuhitmisha hii rasimu hii ya miliki bunifu na mwisho  wake tutatoka na sera nzuri ,na kama tutakuwa na msingi mzuri wa kuwa na sera nzuri itatupelekea na kuwa na sheria nzuri,tukiwa na sheria nzuri tutakuwa na  kanuni nzuri,tukiwa na vitu hivyo vitatu tunaamini serikali itakuwa imetengeneza mazingira mazuri kwa wabunifu wote katika nyanja   mbalimbali, kwamba hii sera itakuwa  yenye tija na mafanikio makubwa kwa nchi na hata kwetu  wasanii kwa ujumla".alisema Mwakifwamba.
   
  Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Biashara ya nje,Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Wilson Malosha akizungumza mbele ya wanahabari na Wadau   mbalimbali katika kikao cha siku tano cha kuhitimisha mchakato wa rasimu ya sera ya miliki bunifu,kilichofanyika jijini Dar na kuhudhuriwa na baadhi ya Wadau kutoka serikalini na Sekta binafsi,Kulia ni Rais Shirikisho la Filamu hapa nchini,Simon Mwakifwamba. 
   Wadau mbalimbali wakifutilia yaliyokuwa yakizungumzwa kutoka meza kuu,katika kikao cha siku tano cha kuhitimisha mchakato wa rasimu ya sera ya miliki bunifu,kilichofanyika jijini Dar na kuhudhuriwa na baadh ya Wadau kutoka serikalini na Sekta binafsi,
   Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijadiliwa katika kikao cha siku tano cha kuhitimisha mchakato wa rasimu ya sera ya miliki bunifu,kilichofanyika jijini Dar na kuhudhuriwa na baadhi ya Wadau kutoka serikalini na Sekta binafsi,


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 

  Na Hassan Silayo-MAELEZO

  Kuanzia 02 Machi, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alianza ziara ya kikazi ya siku 4 katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara iliyolenga kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.

  Ziara hiyo kwa kiasi kikubwa imeonesha dira na mwelekeo wa serikali ya awamu ya tano hasa katika utekelezaji wa miradi inayolenga kuwaletea wananchi maendeleo bila kujali Imani,kabila na itikadi za vyama vyao vya siasa.

  Siku ya kwanza ya ziara yake Rais Dkt. Magufuli aliweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd. kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani ambacho ni kikubwa Afrika Mashariki na Kati kilichogharimu Dola za Marekani Milioni 50 kwa awamu ya kwanza.
  Akiongea katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda chenye uwezo wa kuzalisha mita za mraba 80,000 za vigae kwa siku Rais Magufuli alifurahishwa na teknolojia ya kuyeyusha mchanga wa kutengenezea vigae inayotumiwa na kiwanda hicho na kuhoji kama kuna haja ya serikali kuendelea kusafirisha mchanga wa madini nje ya nchi.

  Rais Magufuli alisema kuwa “Nchi hii tumechezewa vya kutosha, sasa nyinyi hapa mnayeyusha mchanga kwa kuuchemsha hadi nyuzi joto 1,000 wakati wengine wanasafirisha mchanga nje ya nchi wakati uchemshaji wake hauhitaji kufika hata nyuzi joto 1,000, naiagiza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Wizara ya Nishati na Madini kuwa kuanzia sasa ni marufuku kusafirisha mchanga nje ya nchi".


  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa pili kushoto) akiwa pamoja na uongozi wa kituo cha redio 93.7 Efm wakati alipotembelea kituo hicho asubuhi hii ikiwa ni sehemu ya ziara yake aliyoianza ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini. kushoto kwake ni Mmiliki wa kituo cha Radio ya EFM, Francis Ciza (Dj Majay) na kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Redio EFM, Dennis Ssebo.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza jambo wakati akifanyiwa mahojiano katika moja ya vipindi vya redio hiyo.

  0 0

  Na Magreth Magosso, Kigoma 

   Wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Msingi Munyika Kijiji cha Kajana tarafa ya Muyama wilayani Buhigwe mkoani kigoma wamekubwa na ugonjwa wa ajabu hali iliyowalazimu wazazi na walezi kufika shukeni hapo kwa ajili ya kuwapatia tiba mbadala na wengine 80 wapelekwa katika Zahanati ya Kijiji hicho baada ya kuzidiwa na maumivu ya kichwa, tumbo huku joto la miili yao ikiongezeka kila mara. 

   Akithibitisha hilo kwa njia ya simu, Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mnyika Japheti Lukanka alikiri kutokea kwa tukio hilo, ambalo limejitokeza machi 6, mwaka huu, saa 1:30 asubuhi , hali iliyowalazimu baadhi ya wazazi kuwaombea ruhusa watoto wao wanaosoma katika shule hiyo ili kuwapatia matibabu.

  Lukanka alisema kuwa wakiwa paredi katika zoezi la ukaguzi wa usafi , ghafla mwanafunzi mmoja alidondoka na kupewa huduma ya kwanza hatimaye alirudishwa nyumbani kwao kitendo kilichozidi kuwashtua ni pale wanafunzi wa darasa la sita walienda ofisini kwakwe na kuomba ruhusa kwa kuugua ugonjwa huo na kufika saa 6.00 mchana idadi ya wanafunzi waliokutwa na hilo walikuwa zaidi ya 80.

  Akithibitisha kuwapokea wagonjwa hao Ofisa Tabibu wa Zahanati ya Kijiji cha Kajana Festo Eliakimu akiri kupokea wanafunzi 70 wakiwa na hali mbaya na kuwapatia huduma ya kwanza lakini alikabiliwa na tatizo la ukosefu wa kipima joto (thermometer) , hali iliyomlazimu aombe kipimo hicho kwa ofisa afya wa Wilaya ya Buhingwe. 

  “chanzo cha ugonjwa hakijajulikana mapaka leo na wanafunzi 70 nimewapumzisha na kuwapatia huduma ya kwanza, hapa sina vipimo vya joto hivyo nimeomba msaada kwa afisa afya wa Wilaya na amekwisha fika hapa japo baadhi ya wazazi wamewachukua watoto wao na kuwapeleka Hospitali ya shunga ambayo ina vipimo zaidi , baada ya kuona hali zao zinazidi kuwa mbaya” alieleza Eliakimu.

   Kwa niaba ya wazazi wa watoto hao Violethi John alisema tukio hilo limewashangaza kwa kuwa ni mara ya kwanza kuona watoto wao wanaumwa wakiwa shule, na kuupongeza uongozi wa shule hiyo, zahanati na Wilaya hiyo kwa ushirikiano walioutoa katika kuokoa maisha ya wanafunzi hao.

  0 0

  Joint Message from UN Women Representative, Maria Karadenizli and UNESCO Head of Office and Representative for the United Republic of Tanzania, Ms Zulmira Rodrigues on International Women’s Day -Everybody has a stake in promoting equality between men and women, at all levels of society 
  “The story of women's struggle for equality belongs to no single feminist nor to any one organization but to the collective efforts of all who care about human rights.” These words by activist Gloria Steinem testify to the universal nature of the fight for women’s rights and once a year, on 8 March, we restate our commitment to gender equality as a force driving dignity for all.
   Inequality between men and women penalizes societies at all levels of development. The violence, injustice and stereotypes suffered by too many women in their personal or professional lives undermine society as a whole, and deprive of it considerable potential for creativity, strength and confidence in the future. 
  As the United Nations has adopted the ambitious 2030 Agenda for Sustainable Development, the full empowerment of girls and women is one of humanity’s most powerful levers for development. Rural women are directly responsible for the production of half the world’s food – and it is primarily women who manage and gather natural resources. Ninety per cent of rapes in the world take place precisely when women are on their way to collect water or firewood. 
  Two thirds of illiterate adults in the world are women. One in three women is subject to physical violence in the private sphere, and the wage gap between men and women, for equal work and with equal skills, is a fact across the world. For UNESCO, the main engine for change rests on education, training, and the possibility given to all girls and women of pursuing careers in research, politics and culture. Equality also lies in ridding the media and collective imagination of prejudice by highlighting the women scientists, artists and politicians who are moving humanity forward in all fields.
   On the occasion of this 2017 International Women’s Day, UNWOMEN and UNESCO call on all to make a commitment to women’s’ rights, and thereby enhance rights and dignity for all.

  0 0


  0 0

  Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya Integrated Communications kwa pamoja wametoa msaada wa taa zinazotumia mwanga wa jua (sola) kwa wakina Mama wajasiliamali wa eneo la Mwananyamala jijini Dar es salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.

  Taa hizo ambazo ni za kisasa zitawasaidia wakina mama hao katika shughuli zao wakati wa usiku, kwani mara nyingi walikuwa wakitumia taa aina ya vibarati ambayo hutumia mafuta na si salama kwa afya zao kutokana na moshi wake.

  Wakinamama 30 wamekabidhiwa taa hizo leo zenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni moja na laki tano.
  Diwani wa Kata ya Makumbusho, Ally Harubu akikabidhi taa ya kutumia mwanga wa jua (sola) kwa Bi. Mwajabu Mohamed mkazi wa Mwananyamala, zilizotolewa na Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya Integrated Communications, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani. Hafla hii imefanyika mchana wa leo katika Viwanja vya Mwinjuma, Kinondoni jijini Dar es salaam.
  Afisa Mahusiano wa Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania, Jamila Tindwa akizungumza jambo katika hafla ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, iliyofanyika mchana wa leo katika Viwanja vya Mwinjuma, Kinondoni jijini Dar es salaam.
  Afisa Mauzo wa Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania, Magreth Deodath akifafanua jambo wakati akitoa maelekezo ya namna ya kuzitumia taa hizo kwa kina mama wajasiliamali wa Mwananyamala, jijini Dar es salaam. Kulia ni Afisa Mahusiano wa Kampuni hiyo, Jamila Tindwa
  Mmoja wa wakina Mama hao akiwa na taa hizo baada ya kukabidhiwa.
  Picha ya pamoja.

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa umeme vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Tatu, kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini (Tanesco).Mradi huo umezinduliwa rasmi kitaifa katika kijiji cha Zingibari wilayani Mkinga mkoani Tanga.

  Na Zuena Msuya, Tanga

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani amezindua rasmi mradi wa usambazaji wa umeme vijijiji ,unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Tatu kitaifa kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini Tanesco,utakao sambaza umeme kwa vijiji vyote ambavyo havikupata huduma hiyo wakati wa REA Awamu ya Kwanza na ya Pili.

  Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji cha Zingibari wilayani Mkinga mkoani Tanga, Dkt . Kalemani alisema kuwa, REA Awamu ya Tatu itatekelzwa kwa miaka mitano kuanzia sasa hadi kufikia 2021.

  Dkt. Kalemani alifafanua kuwa,mara baada ya uzinduzi rasmi wa kitaifa wa mradi huo mkoani Tanga,Mikoa mingine itaendelea kuzindua mradi huo katika mikoa yao kulingana na makubaliano ya mikataba ya wakandarasi husika katika Mikoa hiyo.

  "REA awamu ya Tatu imezinduliwa rasmi hapa mkoani Tanga, mradi huu sasa utamaliza kazi ya kuunganisha huduma ya umeme katika vijijini vyote 7867 nchini vilivyoachwa katika Awamu ya Kwanza na ya Pili ya mradi huo, ili kifikia idadi ya vijiji vyote 12,262,Tanzania bara ifikapo mwaka 2021", alisema Kalemani.

  Akizungumzia mradi huo kwa Mkoa wa Tanga, Dkt. Kalemani alisema kuwa REA Awamu ya Tatu itasambaza huduma ya umeme katika vijiji 166, ambapo vijiji 20 kati ya hivyo ni vile ambavyo vilipitiwa na Mradi wa REA Awamu ya Kwanza na ya Pili lakini havikuunganishwa na huduma ya umeme , na vijiji 146 ambavyo havikupitiwa kabisa wala kuunganishwa na Mradi wa usambazaji wa umeme vijijini iliyopita.

  Aidha , Dkt. Kalemani alitoa wito kwa wakandarasi watakaotekeleza Mradi wa REA Awamu ya Tatu, kutekeleza majukumu yao kwa wakati kwa kuzingatia uhitaji wa huduma ya umeme nchini ili kutimiza azma ya Serikali ya kuwa nchi ya viwanda.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela aliwataka wakazi wa Mkoa huo waliokosa huduma hiyo katika miradi iliyotangulia, kutandaza nyaya za umeme katika nyumba zao ili kuweza kuunganishwa na huduma ya umeme ambayo hupatikana kwa bei nafuu ya shilingi elfu 27 .

  Aidha aliwataka wananchi hao kulinda na kuitunza miundombinu ya mradi huo kwa maslahi ya taifa na wananchi kwa ujumla kwa kuwa miundombinu hiyo ni ya gharama kubwa.
  Wakazi wa kijiji cha Zingibari Wilayani Mkinga mkoani Tanga wakisikiliza hotuba ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani ( hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa umeme vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Tatu, kwa kushirikiana na Tanesco.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani,(katikati), Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela( kushoto) na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhaga Mpina(kulia) wakiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tanga, Mawaziri hao walikuwa mkoani humo kwa ziara ya kikazi.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani, akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Zingibari wilayani Mkinga mkoani Tanga alipofika kijijini hapo kuzindua rasmi mradi wa usambazaji wa umeme vijijini kitaifa unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Tatu, kwa kushirikiana na Tanesco.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Gabriel Makalla amemkabidhi shilingi milioni moja Bi Fidea Lucas kwa ajili ya kumsaidia matibabu baada ya kumwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana miaka miwili iliyopita.
  Msaada huo ni utekelezaji wa ahadi yake Mkuu wa  Mkoa huyo aliyoitoa wiki kadhaa zilizopita kwenye kikao cha kusikiliza kero za wananchi, ambapo baada ya kuguswa aliahidi kumsaidia mama huyo hela ya matibabu
  Aidha, Mhe.Makalla ameahidi kufuatilia madai yake yote ikiwemo kumsaidia kupata haki zake kwa mwajiri wake na msaada wa kisheria.


  0 0
 • 03/08/17--10:43: Article 23


 • 0 0

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imewafaidisha zaidi ya wakazi elfu kumi na nne waishio katika vijiji vya Lushoto na Bumbuli kwa kuwapatia mawasiliano ya uhakika kupitia ushirika wao na mfuko wa Maendeleo wa mawasiliano kwa wote UCSAF yaani Universal Communication Services Fund.Uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa Airtel katika kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga, umekuja ikiwa ni wiki moja toka Mfuko wa maendeleo wa Mawasiliano kwa wote na Airtel walipozindua minara mingine mitatu mkoani Dodoma.
   Meneja Mauzo wa Airtel Tanga  John Nada alisema  "Airtel tumejipanga kuendelea kutoa mawasiliano ya uhakika hasa kwa kipindi hiki ambacho TCRA wamezindua huduma ya kuwawezesha wateja kuhama mtandano akiwa na namba ileile ikiwa hawapati huduma nzuri na za uhakika, hivyo basi kwa wakazi wa Balangai, Hebangwe, Kilimandege, Mahanga, Maluda, Mhezi, Mkinga, Mlai, Mlola, Mpalalu, Ndeme, Nkombola, Ponde, Sakare na Sakarre  Airtel ndio mtandao wenu wa ukahika kwa sasa”

  “Tunawaomba wakazi wote mtumie fursa hii ya mawasiliano kwa kuwa wabunifu zaidi,  tumumieni  huduma ya Airtel Money kwa kuwa pia mko mbali na huduma za kibenki tumeni na kupokea pesa ili kuboreshe kilimo kwa kutumia mawasiliano haya ya uhakika toka Airtel” alisisitiza Bw, Nada

  Kauli ya wananchi  juu ya tatizo la mawasiliano zilithibitishwa na diwani wa kata hiyo ,Mh Edwin Mahunda kwamba wakazi wa  Kata hiyo walikuwa wakipanda juu ya miti na kwenye vilele vya milima wakitafuta mawasiliano ili kufanya mawasiliano ya kibiashara na mambo mengine ya kijamii.

  “Tunawashukuru sana Airtel na UCSAF kwa jitihada zao za kutuletea mawasiliano, mawasiliano haya yatasaidia wakazi wa hapa kijijini na pia yatawasaidia wanaishio mbali na hapa ili kuweza kufanya shughuli zao vyema, awali hali ilikuwa mbaya sana, ilikuwa huwezi kupiga simu mpaka ufike sehemu yenye muinuko” alieleza Mh Mahunda-Diwani. 
   Diwani wa kata ya  kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga Mh Edwin Mahunda pamoja na Meneja mauzo  wa Airtel Tanga John Nada wakikata autepe kuzindua mnara wa mawasiliano uliojengwa kwa ushikiano kati ya Airtel na mfuko wa maendeleo wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ili kutoa mawasiliano kwa zaidi ya vijji 16 mkoani Tanga vikiwemo Balangai, Hebangwe, Kilimandege, Mahanga, Maluda, Mhezi, Mkinga, Mlai, Mlola, Mpalalu, Ndeme, Nkombola, Ponde, Sakare na Sakarre . Airtel mwaka huu imeanzisha kampeni hiyo na UCSAF ili kupanua mawasiliano katika vijiji ambavyo havijafikiwa na mawasiliano.
   Vifijo baada ya uzinduzi wa mnara huo
    Diwani wa kata ya  kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga Mh Edwin Mahunda akiongea na wananchi waliojawa na furaha baada ya uzinduzi wa mnara huo.
   Mnara wa mawasiliano uliojengwa kwa ushikiano kati ya Airtel na mfuko wa maendeleo wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ili kutoa mawasiliano kwa zaidi ya vijji 16 mkoani Tanga vikiwemo Balangai, Hebangwe, Kilimandege, Mahanga, Maluda, Mhezi, Mkinga, Mlai, Mlola, Mpalalu, Ndeme, Nkombola, Ponde, Sakare na Sakarre . Airtel mwaka huu imeanzisha kampeni hiyo na UCSAF ili kupanua mawasiliano katika vijiji ambavyo havijafikiwa na mawasiliano.
  Diwani wa kata ya  kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga Mh Edwin Mahunda pamoja na Meneja mauzo  wa Airtel Tanga John Nada wakiwa katika picha ya pamoja na baasdhi ya wananchi baada ya kuzindua mnara wa mawasiliano uliojengwa kwa ushikiano kati ya Airtel na mfuko wa maendeleo wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ili kutoa mawasiliano kwa zaidi ya vijji 16 mkoani Tanga 

  0 0

   Hon. Lady Justice Ntyam Ondo Mengue plants a tree at the African Court premises in Arusha to mark the International Women’s Day today.
    Hon. Lady Justice Ntyam Ondo Mengue and President of the African Court Hon. Justice Sylvain Oré cut a cake to mark the International Women’s Day in Arusha today.
  African Court women staff members and women judges raise their flowers handed over by their male colleagues as part of the celebrations to mark the International Women’s Day today at the Court’s seat in Arusha.
  (Pictures by a Correspondent)

older | 1 | .... | 1604 | 1605 | (Page 1606) | 1607 | 1608 | .... | 3272 | newer