Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

WAZIRI MBARAWA AWATAKA TEMESA KUONGEZA UJUZI UTENGENEZAJI WA VIVUKO.

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameutaka uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) kushiriki kikamilifu shughuli za matengenezo ya vivuko ili kupata ujuzi wa ufungaji wa mifumo kutoka Kampuni zinazotengeneza vivuko vya Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha MV Kazi, Bandarini jijini Dar es Salaam, Waziri Prof. Mbarawa amesema kuwa kupitia mafunzo hayo Serikali itaweza kuokoa fedha nyingi ambazo kwa sasa inatumia kulipa kampuni binafsi zinazojenga na kukarabati vivuko

“Hakikisheni mnapata ujuzi kama walionao hawa, hatutaki kutumia fedha za Serikali kwa ajili ya kukarabati au kutengeneza vivuko wakati nyinyi TEMESA mpo”, amesema Waziri Prof. Mbarawa

Pamoja na ujenzi wa kivuko hicho Waziri Mbarawa amewataka Temesa kuhakikisha wanasimamia na kukitunza kivuko hicho ili kiweze kudumu kwa muda mrefu.

Aidha, Profesa Mbarawa ameuagiza Wakala huo kuhakikisha wanakamilisha mifumo ya ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki ili ili kudhibiti mianya ya rushwa.

Kuhusu huduma za kivuko mkoani Lindi Serikali imesema itahakikisha inapelekea huduma haraka iwezekanavyo ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wa mkoa huo.
Kivuko cha MV. Kazi kikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake.Kiuvko hicho kitakamilika na kuanza tarehe 15 mwezi huu na kina uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22 kwa wakati mmoja.
Meneja Mradi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport inayojenga Kiuvko cha MV. Kazi, Bw. Major Songoro, akitoa ufafanuzi wa mashine kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alipokagua Kivuko hicho jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia), akiangalia moja ya vifaa vilivyoko kwenye chumba cha kuendeshea kivuko katika kivuko cha MV. Kazi kinachojengwa jijini Dar es Salaam. Kivuko hicho kitakabidhiwa tarehe 15 Mwezi huu. Wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), Dkt. Musa Mgwatu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia),  akifafanua jambo kwa Uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha MV Kazi ambacho kinatengenezwa jijini Dar es salaam na Kampuni ya Songoro Marine Transport.


GAPCO yapongezwa kwa kuimarisha mbio za walemavu

$
0
0
Baadhi ya washiriki wa mbio za kilomita 10 kwa walemavu zinazodhaminiwa na GAPCO Tanzania, wameipongeza kampuni hiyo kwa kuwajali walemavu na kuhakikisha wanafanya vizuri katika riadha.

Pongezi hizi zinakuja siku chache baada ya kumalizika kwa mbio maarufu za Kilimanjaro Marathon ambapo GAPCO iliwadhamini washiriki zaidi ya 90. 

Mshindi wa mbio za baiskeli ya kunyonga kwa mikono kwa wanawake, Mpoki Ibrahim, alisema GAPCO wameweza kufanya jambo ambalo makampuni mengine yameshindwa. “Wametufanya tujisikie fahari kwani tunajua jinsi gani ni ngumu kuwasafirisha watu wote hawa wenye ulemavu lakini GAPCO wamefanya jambo la kipekee,” alisema.

 “Hii ni mara yangu ya pili kushiriki, mwaka jana nilikuwa mshindi wa tatu lakini nashukuru mwaka huu nimekuwa wa kwanza na nimejishindia Tsh milioni moja. Fedha hizi nitatumia kutunisha mtaji wa biashara yangu pale Machinga Complex Karume. Nitaongeza mtaji wangu wa maji na ninachoomba tu ni kuwa GAPCO waendelee kutudhamini mwakani,” alisema na kuyaomba makampuni mengine yaige mfano huo.
Katibu Mkuu katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akikabidhi Tsh milioni moja kwa Mpoki Ibrahim ambaye ni mshindi wa mbio za kilomita kumi kwa walemavu za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zinazodhaminiwa na GAPCO Tanzania zilizofanyika Moshi hivi karibuni. Kushoto kwa Katibu Mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa GAPCO Tanzania, Vijay Nair.
Washindi wa mbio za Kilimanjaro Premium lager Marathon za kilomita 10 kwa walemavu zinazodhaminiwa na GAPCO Tanzania wakiwa wameshikilia mfano wa hundi ya Tsh milioni moja walizoshinda kila mmoja. Kutoka kushoto ni Charles Mihambo aliyeshinda mbio za wanaume wanaoendesha baiskeli za kunyonga kwa mikono, Voster Peter-mbio za baiskeli za magurudumu mawili kwa wanaume, Sophia Mkenda-mbio za baiskeli za magurudumu mawili kwa wanawake na Mpoki Ibrahim-mbio za baiskeli za kunyonga kwa mikono kwa wanawake.


DCB YATOLEA UFAFANUZI MAKUBALIANO YAO NA MANISPAA YA KINONDONI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

BENKI ya DCB imetolea ufafanuzi makubaliano yao na manispaa ya Kinondoni kuhusiana na mikopo ya vijana na wanawake iliyokuwa ikitolewa na benki hiyo ambapo kwa sasa imesitishwa kwa muda.

DCB wamesema kuwa katika gazeti la Uhuru la tarehe 2 machi lilimnukuu  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi kuwa mfumo wa benki hiyo unaotumika kuwakopesha vijana na wanawake kuwa kuna mazingira yasiyo rafiki na kusababisha vijana wengi kupata mikopo hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa amesema kuwa, taarifa hiyo haina ukweli wowote kwani wao waliingia makubaliano ya kimaandishi na Manispaa ya Kinondoni ya kuwapatia mikopo vijana na wanawake na wamekuwa wanafanya hivyo na wamekuwa wanatoa mikopo kwa bei nafuu ingawa Desemba 13, 2016 walipokea barua ya kusitisha kutoa mikopo hiyo kutokana na kuwa na mgawanyiko wa Wilaya ya Kinondoni.

Mkwawa amesema, taarifa zilizoandikwa na gazeti hilo si za kweli kwani wao walikuwa wanatoa mikopo kwa vijana na toka waingie makubaliano hayo wameshapokea fedha takribani bilioni mbili na wamefanikiwa kukopesha vijana na wanawake wa wilaya hiyo.

"Hata ukienda  DCB Commercial Bank ukiwaambia  wakupe mrejesho wa fedha walizozichukua za halamashauri kwa ajili ya kukopesha hawana na kwamba fedha hizo inafanyia biashara kinyume na lengo la Manispaa ya Kinondoni la kutoa mikopo hiyo bila riba"gazeti la uhuru lilimnukuu Mkuu wa Wilaya Kinondoni.

Mkwawa amesema kuwa kwa sasa wamemtumia barua Mkuu wa Wilaya Kinondoni barua ya kukanusha taarifa hiyo kwani benki ya DCB ilikuwa inatoa mkopo huo kwa wananchi bila masharti magumu pia barua kwa gazeti la Uhuru.

Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akizungumza na waandishi wa habari wakati akitolea ufafanuzi juu ya makubaliano baina yao na Manispaa ya Kinondoni. Kushoto ni Meneja uendeshaji wa Matawi DCB Haika Machaku.

Serikali Yaahidi kushirikiana na vyombo vya habari katika kujenga Tanzania ya Viwanda

$
0
0
Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Serikali imeahidi kuendelea kutengeneza mazingira rafiki kwa kushirikiana na vyombo vya habari ili kwa pamoja kuweza kuhamasisha, kuunda na kujenga nchi ya viwanda katika kuunga mkono azma ya Rais Mhe. John Pombe Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Mchezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokutana na wamiliki na watendaji waandamizi wa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Mhe. Nnauye amesema kuwa serikali na vyombo vya habari wakishirikiana na kuwa na lengo moja wataweza kuileta Tanzania pamoja na kuiweka katika mwelekeo ulio sahihi. 

“Tukiamua leo kila chombo cha habari kikawa na dawati maalumu linalozungumzia Tanzania ya viwanda kama ilivyo kwa madawati mengine ndani ya vyombo vyetu vya habari, na serikali ikaendelea kutoa hamasa za uanzilishwaji wa viwanda ambavyo vitasukumwa na dawati hilo maalumu la viwanda, tutaweza kutimiza ndoto yetu ya Tanzania ya Viwanda” amesema Mhe. Nnauye
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akiongea na wamiliki wa vyombo vya Habari (hawapo katika picha) wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze kuhusu namna vyombo vya habari vinavyoshiriki katika kufanikisha azma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda leo Jijini Dar es Salaam. katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni  Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jimy Yonazi.

 Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassani Abbas akitoa ufafanuzi kwa wamiliki wa vyombo vya habari namna uratibu wa matangazo utakavyokuwa ukiendeshwa  na Serikali wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze leo Jijini Dar es Salaam. 
 Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jimy Yonazi akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze uliowakutanisha wamiliki wa vyombo vya Habari  nchini kujadili nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga Tanzania ya viwanda. Wanaomsikiliza kulia ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel,Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye pamoja na . Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassani Abbas 
 Mkurugenzi wa Vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akichangia wakati wa mkutano uliowakutanisha wamiliki wa Vyombo vya Habari ikiwa ni muenedelezo wa vipindi vya Wadau Tuzungumze kinachoratibiwa  na Wizara wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo lengo likiwa ni kuimarisha ushirikaiano baina ya Wizara na wadau wa sekta zake.

 Mdau wa Habari Bw. Hamza Kasongo akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze uliowakutanisha wamiliki wa Vyombo 

Baadhi ya Wadau waliohudhuria mkutano wa Wadau Tuzungumze kuhusu namna vyombo vya habari vinavyoshiriki katika kufanikisha azma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda leo Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA MICHUZI JR.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Vodacom yawapiga msasa mawakala watakaokusanya fedha za hisa

$
0
0
Mawakala wa kuuza hisa za Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC, wamepatiwa mafunzo elekezi ya siku moja iliyokuwa na lengo la kuwaelimisha mawakala hao jinsi ya kukusanya fedha wakati wa zoezi la kuuza hisa za kampuni hiyo litakapoanza hivi karibuni kwani limekuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa na watanzania walio wengi.

Semina hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Mlimani City ambapo uongozi wa kampuni ya Vodacom Tanzania na mawakala walipata fursa ya kubadilishana mawazo kuhusiana na mchakato mzima wa zoezi hilo utakavyoendeshwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Ian Ferrao alisema “Tunawashukuru kwa ushirikiano wenu tangia tulipoanza mchakato wa maombi ya kuuza hisa kwa umma hadi kufkia sasa ambapo tayari tumepata kibali cha kutekeleza zoezi hili kutoka serikali kupitia Mamlaka ya Dhamana Masoko na mitaji (CMSA) na mkiwa wabia wetu katika mchakato huu tumewaita kwa ajili ya kubadilishana mawazo jinsi tutakavyofanikisha matarajio yetu tuliyokusudia na kuwa tayari kwa kazi iliyosubiliwa kwa muda mrefu”.

Ferrao alieleza kuwa Vodacom inatarajia  kuuza asilimia 25% ya hisa zake kwa umma  zenye thamani ya shilingi Bilioni 476/-na kila hisa itauzwa kwa shilingi 850/-

Vodacom Tanzania PLC,imekuwa ya kwanza kutekeleza  sheria ya Electroniki na Mawasiliano ya Posta (EPOCA) na sheria ya fedha ya mwaka 2016 inayoyataka makampuni kumilikisha asilimia 25% ya hisa zake kwa umma kupitia Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Ferrao, wananchi wataweza kununua hisa za zao katika matawi ya Benki ya NBC na mawakala wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) waliopo nchini kote.

Wakati zoezi la uuzaji hisa za Vodacom linatarajiwa kuanza rasmi hivi karibuni,wawekezaji na wananchi wamekuwa wakisubiri kwa shauku kubwa ambapo wamekuwa wakifuatilia kwa karibu jinsi zoezi hili linavyoendelea ili waweze kujipatia fursa ya kumiliki hisa katika kampuni kinara ya mawasiliano nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao akifafanua jambo kwa mawakala (hawapo pichani )wakati alipokuwa akitoa mafunzo elekezi ya siku moja jijini Dar es Salaam leo juu ya ukusanyaji wa fedha wakati wa zoezi la kuuza hisa za kampuni hiyo litakaloanza hivi karibuni.
Baadhi ya Mawakala watakaouza hisa za Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC, wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,Ian Ferrao(hayupo pichani) wakati alipokuwa akitoa mafunzo elekezi ya siku moja jijini Dar es Salaam leo juu ya ukusanyaji wa fedha wakati wa zoezi la kuuza hisa za kampuni hiyo litakaloanza hivi karibuni.

Jokate aanzisha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa kike

$
0
0
Mrembo mwenye vipaji lukuki nchini, Jokate Mwegelo ameanzisha mpango maalum wa kufundisha somo la ujasiriamali kwa wanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya sekondari ya Majani ya Chai iliyopo Vingunguti katika Manispaa ya Ilala.

Jokate ataanza mafunzo hayo maalum kwa wanafunzi wa kike kuanzia wiki ijayo na lengo la mafunzo hayo ni kuwapa ufahamu wanafunzi hao na kuanzisha biashara zao mara baada ya kumaliza elimu yao ya sekondari.

Alisema kuwa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi ni muhimu kwani yanawawezesha kujiandaa vizuri kukabiliana na maisha mara baada ya kuhitimu masomo yao ya sekondari na kushindwa kuendelea na masomo ya ngazi ya juu.
Kwa mujibu wa Jokate, unaweza kusoma mpaka Chuo Kikuu ndani na nje ya nchi, lakini bado utakabiliana na ugumu wa kupata ajira ambazo kwa sasa ni haba.

“Kuna wengine wamesomea taaluma fulani  kwa ngazi ya Chuo Kikuu lakini mpaka sasa hawana ajira na kukata tama katika maisha, pia unaweza kufanya kazi tofauti na taaluma uliyosomea, lakini kwa ujasiriamali ni tofauti, utajifunzi jinsi ya kupata mtaji, kukopa na kurejesha, kufanya biashara gani na mbinu zake,”

“Mfano halisi mimi mwenyewe, nimesomea mambo tofauti na kazi ninazozifanya ni tofauti, ni mbunifu wa mitindo, mavazi, muigizaji wa filamu, mwanamuziki na pia ni mfanyabiashara, haya yote sikusomea, ila najivunia kwani ndiyo yanaendesha maisha yangu, wanafunzi wana vipawa tofauti, naamini katika programu hii nitapata wengi na kupata mafanikio,” alisema Jokate.

Alisema kuwa atakuwa anafundisha mafunzo hayo mara moja kwa wiki kuanzia wiki ijayo. “Nimeamua kuanza rasmi siku ya wanawake duniani, maandalizi yamekamilika na nawaomba wanafunzi wajiandae kwani mafunzo ni mazuri na yatawajengea moyo wa kujiamini kwani si kila anayesoma anatakiwa kuajiliwa,” alisema.
Jokate Mwegelo akicheza muziki na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Majani ya Chai ya Ilala wakati wa mahafari ya mwaka jana.
Jokate Mwegelo akikabidhi zawadi kwa mmoja wa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Majani ya Chai wakati wa maafali ya mwaka jana ya kidato cha nne.

Maandalizi Ya TANZANIA DAY 2017 Dallas Texas

$
0
0


Aprili 29, 2016, Mstahiki Meya wa jiji la Dallas, jimbo la Texas aliitangaza rasmi siku hiyo kuwa SIKU YA TANZANIA.

Na mwaka huu, Jumuiya ya waTanzania waishio jimboni humo kwa kushirikiana na Baraza la waTanzania waishio nchini Marekani (Diaspora Council of Tanzanians in America) wanaandaa maadhimisho makubwa ya siku hiyo yatakayofanyika katika jiji la Dallas.

Viongozi Ben Kazora wa Jumuiya ya Dallas na Charles Bishota wa DICOTA wamezungumza na Mubelwa Bandio kuhusu maandalizi ya siku hiyo
KARIBU USIKILIZE

WAZIRI MWIGULU AKUTANA NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI KUJADILI MASUALA YA USALAMA NA MAENDELEO KWA MASHIRIKA NA VIKUNDI VYA KIJAAMII

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akisalimia na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bi Virginia Blaser aliyefika ofisini kwa Waziri huyo kwa lengo la kujadiliana namna wanayoweza kusaidia Mashirika na vikundi vya kijamii katika masuala ya usalama wa raia na haki zao.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bi Virginia Blaser akisaini kitabu cha wageni alipofika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi alipomtembelea waziri wa wizara hiyo (anayesoma kadi) kwaajili ya kujadiliana namna wanayoweza kusaidia Mashirika na vikundi vya kijamii katika masuala ya usalama wa raia na haki zao. Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani nchini, Jamal Jafari.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akisisitiza jambo wakati alipokua akiongea na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bi Virginia Blaser aliyefika ofisini kwa Waziri huyo kwa lengo la kujadiliana namna wanayoweza kusaidia Mashirika na vikundi vya kijaa katika masuala ya usalama wa raia na haki zao. Kaimu Balozi huyo aliambatana na Jamal Jafari ambaye ni aliambatana na Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani nchini
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsikiliza Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bi Virginia Blaser aliyefika ofisini kwa Waziri huyo kwa lengo la kujadiliana namna wanayoweza kusaidia Mashirika na vikundi vya kijaa katika masuala ya usalama wa raia na haki zao. Kaimu Balozi huyo aliambatana na Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani nchini, Jamal Jafari.

NMB yamwahidi Rais Magufuli kuendelea kutumia mfumo wa kieletroniki

$
0
0
Benki ya NMB imemwakikishia Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kuwa itaendelea kutumia mifumo ya kiteknolojia ili kuwawezesha wateja wa benki hiyo kutumia Zaidi mifumo ya kietroniki kuliko unaotumika Zaidi kwa sasa wa malipo kwa kutumia pesa taslim.

Hayo ya mesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Ineke Bussemaker wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Kibiashara cha Mtwara na kueleza kuwa nia ya benki ni kuendelea kukua Zaidi huku ikitoa suluhu ya vipau mbele vya serikali na kujikita katika ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa njia zakielektroniki.

“Kwa kutumia teknolijia mbalimbali, NMB tumewekeza Zaidi kwenye kutatua changamoto mbalimbali za wateja wetu na hivyo kutoa fursa za kutumia Zaidi njia za benki kuliko kutumia njia za malipo kwa kutumia pesa taslim,” alisema Ineke.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Prof. Joseph Semboja alisema kuwa NMB imefanya maboresho makubwa na hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa huduma za kifedha kwa kila kada ya watanzania na serikali kwa ujumla.

Prof. Semboja alisema kuwaSerikali kwa sasa inamiliki hisa asilimia 32 ndani ya benki ya NMB zenye thamani ya Zaidi ya Bilioni 430 hivyo kuiwezesha serikali kupata gawio la Zaidi ya bilioni 75 ndani ya miaka mitano.

“Kwa mwaka huu mheshimiwa raisi, kama mkutano mkuu wa wanahisa utakaokaa mwezi wa sita mwaka huu, utabariki Kiwango cha gawio, serikali itapata gawio la shilingi Bilioni 16.5 zinazotokana na faida iliyopatikana mwaka 2016,” alisema Prof. Semboja.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker mara baada kukifungua rasmi kituo cha Biashara cha NMB mjini Mtwara kijulikanac ho kama Mtwara Business Centre. Pamoja na mambo mengine, rais magufuli alimuagiza Waziri wa fedha Dr Philip Mpango kuhakikisha kuwa fedha zote za serikali zinapita NMB.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkurgenzi wa NMB – Ineke Bussemaker wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kituo cha kibiashara cha NMB – NMB Business Centre mjini Mtwara juzi. Kutoka kulia niAfisa Mkuu wa wateja wadogo na wa kati – Abdulmajid Nsekela, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi – Prof Joseph Semboja na kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara – Halima Dendegu na Waziri wa Fedha na Uchumi – Dr Philip Mpango.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

CUF ya Maalim Seif kuiburuza CUF ya Prof.Lipumba mahakamani

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

BODI ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF ), imefungua kesi ya madai dhidi wanachama wake nane akiwemo Naibu Katibu Mkuu, Magdalena Sakaya

Kesi hiyo imefunguliwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikitaka wanachama hao wasijihusishe na harakati  zozote za chama hicho.

Mbali ya Sakaya ambaye pia ni mbunge wa Kaliua mkoani Tabora, wadaiwa wengine ni Thomas Malima, mbunge wa Mtwara Mjini,Mafta Nachumu, Omar Mhina Masoud, Abdul Kambaya, Salama Masoud, Zainabu Mndolwa na Jafari Mneke.

Maombi hayo mbayo yametajwa mbele ya Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri yamewasilishwa na Wakili wa bodi, Hashim Mziray na yamepangwa kusikilizwa kesho.

Katika maombi hayo yaliyopewa namba 1 ya mwaka 2017, bodi inaiomba mahakama kutoa zuio kwa wadaiwa kutojihusisha katika masuala yeyote yanayohusiana na chama hicho.

Mbali ya maombi hayo, pia Wakili Mziray amewasilisha maombi madogo ya kuiomba mahakama kuwaamuru wadaiwa wasijihusishe na mikutano ya chama hicho.
Aidha, Mziray aliomba maombi yao madogo yasikilizwe kwa upande mmoja wa wadai tu kwa kuwa wamechelewa kuwapatia nyaraka za madai yao wadaiwa.

"Mheshimiwa tunaomba tusikilizwe upande mmoja ukizingatia maombi yameletwa chini ya hati ya dharula na kwa mujibu wa sheria mahakama hii... inayo mamlaka ya kufanya hivyo".

Hakimu Mashauri alisema anakubaliana na upande wa wadai na maombi hayo yatasikilizwa kesho mahakamani hapo.

Hatua ya Bodi ya CUF, kukimbilia mahakamani inakuja ikiwa ni siku moja baada ya l unaomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hammad kupinga uteuzi wa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.

Uteuzi wa Profesa Lipumba ambao unapingwa ni ule alioufanya Machi 6, mwaka huu baada kuwaondoa katika nafasi zao, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Omar Ali Shehe.

Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, Salim Abdull Bimani, Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi, Abdullah Bakar Hassan.

Wengine ni Pavu Juma, Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadam na Sheria, Mahmoud Ali Mahindo na Katibu wa Jumuiya ya Vijana, Yusuph Salim.

MAHAKAMA YA KISUTU KUFANYA UTAFITI WA KINA KABLA YA KUTOA MAAMUZI DHIDI YA KESI MPYA YA MKE WA MAREHEMU ERASTO MSUYA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema inahitaji kufanya utafiti wa kina kabla ya kutoa maamuzi dhidi ya kesi mpya inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Mariam Mrita (41) na mfanyabiashara Revocatus Muyela (40).

Hakimu Mkazi Thomas Simba amesema hayo Leo asubuhi wakati kesi hiyo ya mauaji ilipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kutolewa amuzi wa ifutwe au la kutokana na mabishano ya upande wa serikali na ule wa utetezi.

Washtakiwa Mrita na mwenzake Muyela waliachiwa huru mapema mwezi uliopita na kisha wakakamatwa tena na kusomewa upya Mashtaka ya mauaji.

Katika kesi hiyo, Washtakiwa hao wanatuhumiwa kumuua kwa makusudi Aneth Msuya ambaye ni Dada wa bilionea Erasto Msuya. Mauaji hayo yanadaiwa kutendeka huko Kibada Kigamboni Jijini Dar es Salaam.,Mei 25, mwaka jana.

Akiahirisha kesi hiyo, Hakimu Simba amesema Kuwa bado anafanya utafiti juu ya kesi hiyo."Maombi yaliyoletwa na upande wa utetezi na mjibu ya Jamuhuri, yanahitaji kifanyiwa utafiti wa kina kaba sijatoa uamuzi" amesema Hakimu Simba.

Kutokana na hayo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 20 kwa ajili ya kutolewa Manji.

Awali mara baada washtakiwa kusomewa tuhuma zao za, mauaji, Wakili wa washtakiwa, Peter Kibatala aliiomba Mahakama kufuta kesi hiyo akidai kuwa kuwa imefunguliwa kinyume na sheria kwani ilishafutwa.

MANISPAA YA UBUNGO YABAINISHA MPANGO WA KUKUZA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASIKINI ILI KUFIKIA MAENDELEO ENDELEVU

$
0
0

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imebainisha namna ya kuboresha maisha ya wakazi wake kwa kuweka mpango mzuri wa muda wa kati wa mwaka 2017/2018 – 2019/2020 ambao unalenga kukuza uchumi, na kupunguza umaskini ili kufikia maendeleo endelevu ya kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa wananchi wake. 

Mpango huo umeandaliwa kwa kuzingatia sera na miongozo ya Kitaifa, kwa mujibu wa sheria ya bajeti Na. 11 ya mwaka 2015, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambapo Mpango mkakati ni kutekelezwa kwa matokeo makubwa sasa (BRN), Sera ya Taifa ya UKIMWI, Sera za kisekta, Mipango Shirikishi Jamii ya Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O&OD) ya Kata na Mitaa. 

Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuelezea juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya kawaida na ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2017/2018, Makadirio yalijadiliwa na Waheshimiwa Madiwani katika Kamati za Kudumu,na kuidhinishwa na baraza maalumu la madiwani jumamosi ya tarehe 04/03/2017 kwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. 

Mstahiki Meya alisema kuwa ili kutekeleza dhana nzima ya ung’atuaji wa madaraka, mpango huu umeshirikisha jamii katika mpango shirikishi ambao huanzia ngazi ya Mtaa ambapo Hali hiyo imezingatia vipaumbele na mahitaji halisi ya wananchi katika maeneo yao.

Alisema kuwa Mpango huo umejielekeza katika kutoa kipaumbele maeneo yanayoweza kutoa matokeo ya haraka (quick wins) ambayo yatasaidia ukuaji wa uchumi kwa haraka katika kipindi kifupi na kutoa huduma bora kwa wananchi wa Ubungo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake. (Picha zote na Nassir Bakari)
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuelezea Makadirio ya Mapato na Matumizi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2017/2018.

WAKULIMA WA VIAZI MVIRINGO MKOANI NJOMBE WAIOMBA SERIKALI KUWASIDIA KUPANDA SOKO

$
0
0
Mkoa wa njombe ni kati ya mikoa inayolima viazi mviringo kwa wingi hapa nchini Tanzania na ni mkoa unaosifika kwa kilimo cha viazi hivyo, Wakazi wa mkoa huo wanategemea zao hilo kwa kuwaongezea kipato.

MASAUNI ATEMBELEA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA ABEID AMANI KARUME, AAGIZA VYOMBO VYA ULINZI KUDHIBITI UINGIAJI DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Maafisa wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, wakati wa ziara ya kukagua udhibiti wa uingiaji wa Dawa za Kulevya Visiwani humo, huku akiagiza vyombo vya ulinzi na usalama kushirikiana kudhibiti madawa hayo ambayo yanaharibu nguvu kazi ya Taifa.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame, akitoa taarifa za utekelezaji wa zoezi la kudhibiti Dawa za Kulevya Visiwani humo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), wakati wa ziara ya naibu waziri kufuatilia utekelezaji wa zoezi la kudhibiti uingiaji wa dawa za kulevya Visiwani humo.
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji anayesimamia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Fulgenze Mutarasha, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni (wakwanza kushoto), juu ya hatua zinazochukuliwa na Idara ya Uhamiaji na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama kukabiliana na udhibiti wa uingiaji wa Dawa za Kulevya kiwanjani hapo.Wapili kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada Salum na anayefuatia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisikiliza jinsi mifumo ya kudhibiti uingiaji haramu inavyofanya kazi kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Uhamiaji anayesimamia Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume, Fulgenze Mutarasha.Ziara ya Naibu Waziri huyo ilikua na lengo la kukagua mifumo inayotumika kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WIZARA YA ARDHI YABORESHA OFISI ZA KANDA

$
0
0
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeboresha ofisi zake za kanda za ardhi zilizopo nchini ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma za ardhi karibu zaidi na wananchi.

Wizara imegawa magari katika kanda zake zote ili kurahisisha utekelezaji wa kazi za ardhi na kuharakisha huduma za sekta nzima ya ardhi katika maeneo yote ya nchi badala ya wananchi kuja ofisi za Dar es Salaam ambazo kwa sasa zinahamia makao Makuu ya Nchi Dodoma. 

Hatahivyo, huduma nyingine za kisekta kama vile za malipo ya kodi ya pango la ardhi, kituo cha huduma kwa mteja na ofisi za kanda za Dar es Salaam zitaendelea kufanyika kama ilivyokuwa awali.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati akitangaza kuhamia rasmi kwa Wizara yake mkoani Dodoma amesema kuwa Wizara imepanga kuwaweka wataalam wa sekta nzima ya ardhi katika ofisi za kanda ili kuondoa usumbufu uliokuwepo wa kufuata huduma za hati, usajili, Uthamini upimaji na ramani na mipango miji na vijiji – Dar es Salaam na Dodoma.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi, Naibu wake Mhe. Dkt. Angeline Mabulla, Katibu Mkuu; Dkt Yamungu Kayandabila na Viongozi wengine wakuu wa wizara wakikagua magari ya kuhudumia ofisi za ardhi za kanda nchini.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akikabidhi funguo ya gari kwa Kamishna wa kanda ya Dar es Salaam; Matthew Nhone.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi, Naibu wake Mhe. Dkt. Angeline Mabulla, Katibu Mkuu; Dkt Yamungu Kayandabila na Viongozi wengine wakuu wa wizara wakikagua magari ya kuhudumia ofisi za ardhi za kanda nchini.


MKUTANO WA JUMUIYA YA NCHI ZINAZOPAKANA NA BAHARI YA HINDI (IORA) NCHINI INDONESIA WAFANYIKA

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitia saini makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa kwanza wa Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (INDIAN ASSOCIATION-IORA) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt John Pombe Magufuli,mkutano huo ulifanyika leo katika ukumbi wa Balai Sindang Mjini Jakarta Indonesia,(kushoto) Rais wa Sychells Mhe,Danny Faure.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Waziri wa Ncho Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi (katikati) wakiteta jambo wakati wa vikao mbali mbali katika mkutano wa kwanza wa Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (INDIAN ASSOCIATION-IORA) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt John Pombe Magufuli,mkutano huo ulifanyika leo katika ukumbi wa Balai Sindang Mjini Jakarta Indonesia,(kushoto) waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mhe,Susan A,Kolimba,[Picha Ikulu.]

YANGA YAIFUNDISHA SOKA KILUVYA UNITED, YAIPIGA 6-1

$
0
0
Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la 5.
 Saimon Msuva akiwania mpira na beki wa Kiluvya United, Aloyce Nkya. 
 Beki wa Kiluvya United, Aloyce Nkya (kushoto), akimtoka, Hassan Ramadhani.
 Beki wa Kiluvya United, Aloyce Nkya akimiliki huku akizongwa na mshmabuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa.
 Mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi akipata huduma ya kwanza baada ya kuumia katika mchezo wa Kombe la Shirikisho.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.

IN LOVING MEMORY: FIVE (5) YEARS TODAY - A REASON TO THANK GOD ALMIGHTY

$
0
0
JUDICA STEPHANO TERI
22.06.1946  to  08.03.2012
IT IS FIVE (5) YEARS  TODAY SINCE YOU WERE  PROMOTED TO GLORY

Your beloved wife, Janeth  and children Joan, Linda, Davis  and Hillary  together with their spouses Aliko, Leonard, Tina and Vicky and grandchildren Tumpe, Lusako, Evan-Tumaini, Elsa, Elvis and Abby continue to cherish your love and great wisdom.

Brothers Eliona & Tumainiel and sisters Monyiaichi & Elieng’sia always miss your great counsel. However, we are all comforted in knowing that: 
FOR AS  IN ADAM  WE  ALL  DIE,  EVEN  SO                                                                 IN CHRIST  ALL  SHALL  BE  MADE  ALIVE  (1 COR. 15: 22)

Kaya 1600 Njombe kupata umeme mwakani

$
0
0
Na Greyson Mwase, Njombe

Kaya 1600 katika vijiji kumi mkoani Njombe zinatarajiwa kupata umeme wa uhakika mara baada ya kukamilika kwa mradi wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia maporomoko ya maji wa Luponde Hydro Ltd unaotekelelezwa na kampuni ya Rift Valley Energy.

Hayo yalielezwa leo na Meneja Mradi wa Luponde Hydro, Mugombe Maxwell katika ziara ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini katika mkoa wa Njombe ili kujionea maendeleo ya miradi midogo ya umeme wa maporomoko ya maji na nishati jadidifu inayotekelezwa katika mkoa huo.

Maxwell alisema kuwa kampuni ya Rift Valley Energy ina miradi miwili ambayo ni Mwenga Hydro Grid wenye uwezo wa Megawati 4.1na Luponde Hydro Ltd utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 3 mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wake hivyo kuwezesha vijiji kumi katika mkoa huo kupata umeme wa uhakika ifikapo mwakani.

Akielezea mradi huo wa Luponde Hydro Ltd, Maxwell alisema kuwa mradi ulianza mwaka 2016 na kuongeza kuwa mradi huo upo katika maeneo mawili ambayo ni Luhololo na Igola yote yakiwa mkoani Njombe.

Akielezea ujenzi wa mradi huo, Maxwell alieleza kuwa mradi umegawanyika katika awamu mbili na kuendelea kusema kuwa awamu ya kwanza inahusisha usambazaji wa umeme wa uhakika katika vijiji saba vyenye kaya 1120, shule tisa na vituo vya afya vitano.
Mtaalam kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Stephan Kashushura (kulia) akibadilishana mawazo na Sister Richardis Chiwinga katika ziara ya wataalam wa nishati jadidifu katika mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Benedict Sisters of Saint Agnes Chipole, Mbinga mkoani Ruvuma.
Sister Richardis Chiwinga kutoka katika mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Benedict Sisters of Saint Agnes Chipole (katikati) akielezea hali ya maji katika bwawa la mradi huo kwa wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Sehemu ya bwala la maji katika mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Benedict Sisters of Saint Agnes Chipole, Mbinga mkoani Ruvuma.
Sister Richardis Chiwinga kutoka katika mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Benedict Sisters of Saint Agnes Chipole (kushoto) akiongoza watalam kutoka Idara ya Nishati Jadidifu, Wizara ya Nishati Jadidifu katika ziara kwenye eneo la mradi.

Operesheni ya Viroba Yaibua Wafanyabiashara Wasiokuwa na Vibali vya TFDA.

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO.

Operesheni ya kuondoa pombe kali zilizofungwa katika vifungashio vya plastiki (viroba) inayoendelea nchi nzima imeibua wafanyabiashara wanaofanya biashara ya pombe bila kuwa na vibali vya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).

Hayo yamebainishwa na Afisa Afya na Mratibu wa Masuala ya Chakula wa Manispaa ya Temeke Rehema Sadick, leo Jijini Dar es Salaam wakati wa operesheni hiyo inayoendelea nchini.

“Katika operesheni hii ya kuondoa pombe za viroba tumegundua wafanyabiashara wengi wanaojihusisha na uuzaji wa pombe kutokuwa na kibali cha TFDA ambacho hutolewa katika Halmashauri husika,” alifafanua Rehema Sadick.

Aidha amebainisha kuwa katika msako uliofanyika leo Kigamboni, ambapo wamekagua zaidi ya maduka matano yanayouza pombe kwa jumla, ni duka moja tu la Mangale Store lililoko Tuangoma ndilo lililokutwa na kibali cha TFDA.

Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images