Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1602 | 1603 | (Page 1604) | 1605 | 1606 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto akizungumza na wakazi wa Kitunda Nyantira
    Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto akisalimiana na Mwenyekiti wa mtaa wa Nyantira
  Naibu Meya wa Manispaa wa Ilala, Omary Kumbilamoto akisaini kitabu cha wageni

  0 0

  Zulia Jekundu ni kipindi cha televisheni cha kila wiki kinachotayarishwa na kutangazwa na Mkamiti Kibayasi toka Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya America (VOA).

  Kipindi hiki hukuletea habari mbalimbali za burudani zinazotamba. Humu utapata kujua juu ya habari za mastaa zinazogonga vichwa vya habari, kujua baadhi ya wanaosherehekea siku zao za kuzaliwa wiki husika na hata filamu 5 zilizoongoza kwa mauzo katika wiki hiyo

  Juma hili, video mpya ya Ariana Grande, mzozo mkali kati ya Nicki Minaj na Remy Na unavyoendelea, matatizo ya iPhone 7plus, The Weekend alipokutana na Drake Ujerumani, Obamas ndani ya New York, kuelekea siku ya kimataifa ya wanawake duniani na kadhalika


  0 0


  Na Fredy Mgunda,Iringa.

  MASHINDANO ya kombe Mbuzi Cup yatafikia tamati tarehe 30 mwezi wa tatu kwa kuzikutanisha timu za Mkwawa Rangers na Waandishi wa habari mkoa wa Iringa na fainal hiyo itachezwa katika kijiji cha Kalenga kata ya Kalenga wilayani Iringa mkoani Iringa ikiwa lengo la kuinua vipaji wa wachezaji kata hiyo.

  Akishudia mchezo wa nusu fainal kati ya timu yaWaandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) na timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga katibu tawalawilaya ya Iringa Joseph Chitinka ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema ni wakati mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa,

  "Mashindano haya ni muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo hiyo" alisema Chitinka

  Aidha Chitinka aliongeza kwa kusema kuwa mpira wa miguu umekuwa na faida kwa wachezaji kwani wanaweza kujitengezea vyanzo vya ajira kama mbwana samatta na wachezaji wengine walipwa vizuri saizi hapa nchini hata nje ya nchi.
  Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwasalimia wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup. Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na  wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.
   Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na  wachezaji wa timu ya kijiji cha Mangalali kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.


  0 0


  Na Rhoda Ezekiel Kigoma

  KATIKA kuelekea siku ya Wanawake Duniani, Baafha ya Wanawake Mkoani Kigoma Wamewaomba Wanaume Mkoani humo kuacha tabia ya kuwanyanyasa wanawake kwa kuwaachia majukumu ya kuzihudumia familia zao, hali inayosababisha Watoto wengi kukosa elimu na wanawake kushindwa kufikia Malengo yao ya kujikomboa na umasikini.

  Akizungumza na Globu ya Jamii ofisini kwake jana, katibu wa umoja wa Wanawake Mkoani Kigoma , Salome Luhinguranya alisema kumekuwa na tabia ya Wanaume wengi kukimbia familia zao na kuwaachia mzigo wa malezi na kusomesha watoto wanawake wao hali inayo wapelekea wanawake wengi kishindwa kufanikiwa katika biashara zao kuyokana na Mzigo mkubwa unao Walemea.

  Luhinguranya alisema Watoto wengi wamekuwa wakikosa elimu Mkoani humo kutokana na matatizo ya Wanajme wengi kuwatelekeza wake zao na familia zao na kwenda kuoa wake wengine hali inayo wapelekea Wanawake kushindwa kuhudumia familia zao kutokana na ufinyo wa mitaji waliyo nayo.

  "Kauli mbiu ya Mwaka huu katika maadhimisho ni Tanzania ya Viwanda wanawake ni msingi wa mabadiliko Kiuchumi,kuelekea. Mkoa wa kigoma wanawake wengi wanajishughulisha katika Shughuli mbali mbali na Wengine ni wafanya kazi ,
  UWT Mkoa imewahamasisha kuingia kwenye ujasiliamali huo na wanaume wengi wamekuwa Wakiwarudisha Nyuma kutokana na mizigo wanayo waachia , niwaombe wanaume kuepukana na fikra mgando ya kuwanyanyasa wanawake pindi wanapo jishughulisha kwa kuwaachia kulea familia ,
  Baba ni kichwa katika familia wanatakiwa kutafuta fedha na kuwasaidia wanawake kulea familia zao ilikuwasaidia watoto kupata elimu na malezi bora", alisema Katibu wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa kigoma.
  Baadhi ya akina mama wakijishughulisha na biashara zao mbalimbali za ujasiliamali mkoano Kigoma.


  0 0
  0 0

  Jovina Bujulu- MAELEZO.

  Kila mwaka ifikapo Machi 8 kila mwaka, wanawake duniani kote  huadhimisha siku yao ambapo hujitathmini kupitia shughuli mbalimbali za maendeleo walizofanya, changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya utatuzi wa changamoto hizo.

  Akiongea hivi karibuni katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi Sihaba Nkinga alisema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Tanzania ya Viwanda; Wanawake ni Msingi wa Mabadiliko”

  Kauli mbiu hii inasisitiza kuwajengea wanawake uwezo wa kitaaluma, kibiashara, upatikanaji wa mitaji, masoko na biashara ili waweze kushiriki kwa usawa, na kunufaika na fursa zilizopo badala ya kuwa wasindikizaji.

  “Ujumbe wa kauli mbiu hii umezingatia sera ya maendeleo ya wanawake na jinsia ya mwaka 2000 na ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu hususani lengo namba 5 kuhusu usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake kiuchumi” alisema Bi Nkinga.

  Kauli mbiu ya mwaka huu imetotolewa kutokana na kauli mbiu ya Umoja wa Mataifa (UN) isemayo “Uwezeshaji wa Wanawake Kiuchumi katika Dunia ya Mabadiliko ya Kazi”.


  0 0
 • 03/06/17--22:59: TANZIA
 • Inna lilahi wainna ilyhi raajiun, Napenda kuwapa taarifa za kifo cha Bi Nuru Bint Daudi (Mama yake na Yusuf Kikwete) kilichotokea usiku wa kuamkia leo hospitali ya Taifa Muhimbili. 

  Taarifa zaidi za mipango na mazishi yatafanyika wapi tutaarifiwa hapo baadae kadri muda unavyokwenda.
  HAKIKA SISI NI WA MWENYEZIMUNGU NA KWAKE TUTAREJEA.

  0 0

  Wadau wa zao la chai nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (mwenye hijabu ) aliyemwakilisha Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa wadau wa chai nchini, uliofanyika katika ukumbi wa TRIT Ngwazi Mufindi, kulia kwake ni Mwenyekiti wa bodi ya chai nchini Spika (mstaafu ), Anne Makinda, Mkurugenzi wa bodi ya wakurugenzi, Hamis Umande, Mathias Ndengi Mkurugenzi wa wakala wa chai , Nicholaus Mauya Mkurugenzi wa bodi ya chai kutoka kulia wa kwanza waliokaa ni Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa chai, Dkt. Emmanuel Simbua ,Twahili Nzalewaye Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao ya kilimo na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri Wiliam.


  WAZIRI wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amewaagiza wamiliki wa viwanda vya chai nchini kununua chai ya Wakulima wadogo kwa kuzingatia bei elekezi ya serikali na sio bei wanayojipangia wao ya kuwanyonya Wakulima wadogo wa zao hilo la chai nchini .

  Kuwa serikali imedhamilia kuwakomboa Wakulima wadogo wa zao la chai hapa nchini kama njia ya kukuza soko la bidhaa zitokanazo na chai hapa nchini ya duniani ,hivyo njia pekee ni kuona Wakulima wadogo wanaendelea  kuhamasika kuongeza kasi ya kilimo hicho cha chai ili kuviwezesha viwanda vya chai nchini kuzalisha chai kwa wingi na ubora zaidi. 

  Alisema kuwa zao la chai ni moja kati ya mazao yanayopewa kipaumbele kama mazao ya biashara hapa nchini na kuwa zao la chai pekee huliingizia Taifa wastani wa dola za kimarekani milioni 50 na kutoa ajira kwa watu milioni 2 kwa mwaka hivyo ni zao lenye fursa kubwa ya kuongeza wigo wa kiuchumi nchini pamoja na kuendeleza kilimo cha zao hilo. 
   mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza aliyemwakilisha waziri wa wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba akifungua mkutano mkuu wa wadau wa chai nchini uliofanyika wilayani Mufindi.


  Waziri Dkt Tizeba aliyewakilishwa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa wadau wa chai nchini uliofanyika katika ukumbi wa taasisi ya utafiti wa chai (TRIT) Gwazi Mufindi, alisema kuwa uzalishaji wa chai nchini kwa upande wa majani makavu ni wastani wa tani 35 kwa mwaka wakati kwa wakulima wadogo wanazalisha wanazalisha kilo 1000 kwa hekta kwa mwaka na Wakulima wakubwa ni wastani wa kilo 2000 za majani makavu kwa hekta kwa mwaka ukilinganisha takwimu za nchi ya Kenya ambayo tija ni kwa mkulima mdogo ni wastani wa kilo 2500 kwa hekta takwimu ambazo zinaonyesha sekta ndogo ya chai nchini ipo nyuma ukilinganisha na Kenya. 

  Alisema kuwa serikali imedhamilia kushirikiana na wadau wa chai kwa kuongeza ardhi kwa maeneo yanayolima chai hadi kufikia hekta 27000 kuwa mwaka 2021/2022 kutoka hekta 22721 kwa sasa pia kuongeza uzalishwaji wa chai kavu kutoka wastani wa tani 32 kwa mwaka hadi kufikia zaidi ya tani 50,000 mwaka 2021/2022 na kuongeza uzalishaji wa tija kutoka kilo 1000 kwa mwaka hadi zaidi ya kilo 2000 za majani makavu. 

  Awali mwenyekiti wa mkutano huo, Spika Mstaafu wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Anne Makinda ambae ni mwenyekiti wa bodi ya chai nchini alisema kuwa kero kubwa ya Wakulima wadogo wa chai ni mbolea kwa ajili ya kukuzia zao hilo kwani zao hilo Wakulima hawana ruzuku ya serikali Kuwa mbolea inayotumika kwa zao la chai ni tofauti na ile ya mazao ya mahindi japo changamoto hiyo wanaendelea kuijadilia pamoja na serikali  huku akidai kuwa chai ya Tanzania inauzwa kwa bei ndogo sana kutokana na ubora wake kuwa duni ukilinganishwa na chai ya Wakulima wadogo wa Rwanda ambao walikuwa katika vita leo wamefikia chai kavu zaidi ta tani 20,000 lakini Tanzania ambayo ilipata uhuru miaka 50 iliyopita chai haina ubora.

  Makinda alisema migogoro midogo midogo inayoanzishwa na viongozi katika maeneo ya Wakulima wa chai ni changamoto ya kurudisha nyuma kasi ya uzalishaji wa zao la chai nchini hivyo zinahitajika jitihada za kuondoa migogoro hiyo ili kukuza zao la chai nchini. Imeandikwa na MatukiodaimaBlog ,Mufindi 

  0 0

  Kituo cha mafuta kilichopo eneo la Tegeta kikionekana kuteketea kwa moto asubuhi hii, huku chanzo kikidaiwa kuwa ni gari lililokuwa likishusha shehena ya mafuta kituoni hapo kushika moto. inaelezwa kuwa Gari hilo limeteketea lote huku sehemu ya kituo hicho pia imeteketea. Kikosi cha zimamoto kipo eneo la tukio kukabiliana na janga hilo.
  Sehemu ya Magari ya vikosi vya Zimamoto yakiwa tayari kukabiliana na tukio hilo.

  0 0

  Mwili wa kiongozi wa upinzani nchini DR Congo, Etienne Tshisekedi hautarudishwa nyumbani wiki hii kama ilivyopangwa hapo awali.

  Familia ya Tshisekedi aliyefariki mwezi uliopita nchini Ubelgiji akiwa na umri wa miaka 84, ilikuwa imepanga kufanya mazishi ya ndugu yao nchini DR Congo Jumamosi inayokuja.

  Mdogo  wa Marehemu Tshisekedi, Gerard Mulumba aliuambia mtandao wa BBC kwamba familia haijakukubaliana na serikali kuhusiana na eneo atakalozikwa ndugu yao mjini Kinshasa.
  Familia ya Tshisekedi wanataka mwili uzikwe katika makao makuu ya chama cha UPDS alichokianzisha.

  Lakini serikali inataka kumzika katika maziko ya Gombe yaliyopo katikati ya mji, na mpaka sasa hakuna  jibu rasmi kuhusiana na tangazo hilo.

  Kifo cha Tshisekedi kimeliweka taifa hilo katika hali tete kwa kuwa kilijiri wakati ambapo kulikuwa na majadiliano kati ya serikali na upinzani kumaliza mgogoro wa kisiasa ambao umesababishwa na hatua ya rais Kabila kukataa kujizulu baada ya kukamilika kwa muhula wake wa kuongoza mnamo mwezi Disemba.

  Uchaguzi unakaribia kabla ya mwisho wa mwaka na mwana wa Tshisekedi Felix amechaguliwa kuongoza upinzani katika mazungumzo hayo.

  0 0

   Mechi za pili za raundi ya mtoano kwa timu 16 za Ligi ya Ulaya (Uefa Champions League) zinatarajiwa kuanza tena kupigwa usiku wa leo Jumanne Machi 7 kwa mechi mbili, ambapo huko katika dimba la Emirates Jijini London, Uingereza wenyeji Arsenal watawakaribisha Bayern Munich huku wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha 5-1 walichoshushiwa katika Mechi ya kwanza iliyochezwa huko Ujerumani.

  Ili kufuzu kuingia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, timu ya Arsenal inapaswa kufanya kitu ambacho hakijawahi kufanyika kwa urahisi kwa kushinda 4-0 au kwa idadi nyingine ya Mabao ilimradi tofauti ya Magoli iwe 4-0 dhidi ya wageni wao hao.

  Mechi ya pili ya leo itachezwa huko Naples, Italy wakati wenyeji Napoli itawakaribisha kwa mchezo wa marudiano Mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Real Madrid huku wakihitaji ushindi wa bao 2-0 kwa kuwa mchezo wa awali walichapwa 3-1 huko Santiago Bernabeu Jijini Madrid, Hispania kwenye Mechi ya Kwanza.

  Napoli pia wanaweza kufuzu ikiwa watashinda kwa idadi nyingine ya Mabao ilimradi tofauti ya Magoli iwe 2-0.

  Kesho, Jumatano Machi 8 zipo Mechi nyingine 2 ambapo Barcelona itakipiga na Paris Saint Germain, huku PSG wakiwa mbele kwa mabao 4-0 na mechi ya pili ni kati ya Borussia Dortmund na Benfica huku Benfica wakiongoza 1-0.

  Mechi za pili za raundi ya mtoano kwa timu 16 za Ligi ya Ulaya zitakamilika, Machi 14 na 15, kwa Mechi nyingine 4 ili kutoa Washindi watakaocheza robo fainali.

  0 0

  Rais wa Marekani Donald Trump amesaini amri mpya inayozuia watu kutoka mataifa 6 yenye Waislamu wengi kuingia nchini Marekani, ikiwa ni marekebisho ya amri ya kwanza ambayo ilikwamishwa na maamuzi ya mahakama.

  Amri hiyo mpya ya Rais iliyosainiwa na Donald Trump ambayo itaanza kutekelezwa tarehe 16 mwezi huu wa Machi, inashikilia marufuku ya siku 90 kwa wasafiri wanaotoka katika mataifa sita yenye waislamu wengi kuingia nchini Marekani. Nchi hizo ni Iran, Libya, Syria, Somalia, Sudan na Yemen. Inawahusu wale tu watakaotaka kupata visa kwa wakati huu, ikiwa na maana kuwa haiwaathiri watu 60,000 ambao tayari wamezipata visa, kama ilivyokuwa kwa amri ya awali.

  Iraq ambayo ilikuwa kwenye orodha ya amri ya mwanzo imeondolewa, na kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Rex Tillerson, hatua hiyo imetokana na ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.

  ''Iraq ni mshirika muhimu katika vita dhidi ya kundi la IS. Mikakati ya uhakiki iliyofanywa mnamo mwezi mmoja uliopita, imeonyesha hatua mbali mbali za kiusalama, ambazo zitaziwezesha serikali ya Iraq na wizara ya mambo ya nje ya Marekani, kutimiza lengo la pamoja, la kuzuia watu wenye malengo ya kigaidi kufika nchini Marekani''. Amesema Tillerson.


  0 0


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 

  MAOMBI kwa ajili ya Taifa yamefanyika leo Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga pamoja na Mchungaji maarufu na mfanya biashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston, Bill Winston kutoka nchini Marekani.

  Mkutano huo uliokuwa na lengo la kuliombea taifa uliweza kuhudhuriwa na viongozi wa dini na serikali na Bishop kutoka nchini Zambia Bernard Nwaka aliendesha maombi hayo. 

  Aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Dr Oby Ezekwesili aliweza pia kuchangia mada juu ya kuliombea taifa na namna wananchi wanavyotakiwa kuishi ndani ya nchi yao.
  Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustino Mahiga akzungumza katika mkutano wa maombi ujulikanao kama Tanzania National Prayer uliofanyika leo Jijini Dar es salaam na kuendeshwa na Mchungaji maarufu na mfanya biashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston, Bill Winston. 
  Mchungaji maarufu na mfanya biashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston, Bill Winston akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa maombi kwa taifa ujulikanao kama Tanzania National Prayer uliofanyika leo Jijini.
  Aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Dr Oby Ezekwesili akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa maombi kwa taifa ujulikanao kama Tanzania Natipnal Prayer uliofanyika leo Jijini.
  Bishop Bernard Nwaka kutoka Zambia akiongoza maombi kwa ajili ya taifa yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustino Mahiga,Mchungaji maarufu na mfanya biashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston, Bill Winston na Aliyewahi kuwa makamu wa raisi wa benki ya Dunia kanda ya Afrika Dr Oby Ezekwesili.
  .Picha zote na Zainab Nyamka.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Muhamasishaji wa akaunti ya Malkia katika wiki ya wanwake Duniani kutoka benki ya CRDB tawi la Water Front, Mary Gekura amesema kuwa mpaka kufikia Machi 06 zaidi ya akaunti 100 za Malkia zimefunguliwa na zaidi wanawake wengi bado wanaendelea kujitokeza kwa wingi.

  Mary amesema kuwa kuelekea katika kilele cha Wanawake Duniani bado wanaendelea kuhamasisha wanawake wajitokeze kufungua akaunti hizo kwani zina manufaa kwao na zinawapatia faida baada ya mwaka mmoja.

  Akaunti ya Malkia inamuwezesha mwanamke kuweza kupata mtaji au faida ya kujiendeleza kiuchumi baada ya kuifungua na kuweka fedha kwa kipindi cha mwaka mzima bila kutoa.
  Muhamasishaji wa akaunti ya Malkia katika wiki ya wanwake Duniani kutoka benki ya CRDB tawi la Water Front Mary Gekura akimkabidhi fomu ya klufungulia akaunti moja ya kina mama waliojitokeza kufungua akaunti hiyo kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani Machi 08.
   Muhamasishaji wa akaunti ya Malkia katika wiki ya wanwake Duniani kutoka benki ya CRDB tawi la Water Front Mary Gekura akimuelekeza namna ya kujaza fomu  ya kufungua akaunti ya wanawake ijulikanayo kama Malkia.
  Wafanyakazi wa CRDB tawi la Water Front wakiwa katika picha za pamoja.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Indonesia Joko Widodo,ambae ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (INDIAN ASSOCIATION-IORA) kabla ya kuanza kwa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Balai Sindang Mjini Jakarta Indonesia,Rais Dk.Shein anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli
  Rais wa Indonesia Joko Widodo,ambae ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (INDIAN ASSOCIATION-IORA) akisalimiana na Rais wa Msumbiji Philipe Nyusi wakati wa mkutano IORA uliofanyika leo katika ukumbi wa Balai Sindang Mjini Jakarta Indonesia ambao ulihudhuriwa na Viongozi wakuu wa Nchi mbali mbali 
  Viongozi Wakuu wa Nchi mbali mbali wakiwa nkatika Picha ya pamoja wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (INDIAN ASSOCIATION-IORA) uliofanyika leo katika ukumbi wa Balai Sindang Mjini Jakarta Indonesia,ambapo Rais Dk.Shein (wa tatu kulia)anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli katika mkutano huo,[Picha na Ikulu.]

  0 0

  Na Karama Kenyunko Blogu ya jamii.

  WAFANYAKAZI 16 wa Kampuni ya Quality Group, inayomilikiwa na Yusuph Manji  wanaokabiliwa na tuhuma tano, ikiwemo ya kutaka kutoroka nchini sasa kusomewa maelezo ya awali Machi 24 mwaka huu.

  Maelezo hayo yatasomwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya upelelezi wa kesi zao kukamilika.

  Wakili wa Idara ya Uhamiaji, Method Kagoma amesema hayo  mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi,  Cyprian Mkeha wakati shauri lilipokuja leo kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo yao ya awali.

  Lakini kabla ya kuwasomea aliiomba Mahakama kubadilisha hati ya mashtaka kwa kuwaongeza washtakiwa wawili ambao walisomewa mashtaka peke yao.

  Kuunganishwa kwa washtakiwa hao ambao ni meneja Uwekezaji, Jose Kiran (40) na Prakash Bhatt (35) kumefanya idadi ya washtakiwa hao kufikia 16, pamoja na mashtaka mengine wanadaiwa Pia kuwa, wakiwa raia wa India na waajiriwa wa Kampuni ya Quality Group walimzuia Ofisa wa Idara ya Uhamiaji kutekeleza majukumu yake Februari 20, mwaka huu.

  Inadaiwa kuwa katika tarehe hiyo washtakiwa hao wakiwa jijini Dar es Salaam, walimzuia Ofisa huyo ambaye alitaka kutoa taarifa katika makao makuu ya Idara ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam kwamba watu hao wanataka kutoroka kupitia mpaka wa Horohoro,  
  Upelelezi wa kesi hiyo umkamilika na imeahirishwa hadi Machi 24,mwaka huu kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

  Mbali ya wawili hao washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni  Rajat Sarkar (35), Jagadish Mamidu (29), Niladri Maiti (41) Divakar Raja (37) ambao ni washauri wa kampuni hiyo, huku Mohammad Shaikh (44) mhasibu na Pintu Kumar (28) ambaye ni Meneja msaidizi wa kampuni.

  Wengine ni Bijenda Kumar (43), Prasson Mallik (46), Nipun Bhatt (32), Anuj Agarwal (46), Varun Boloor, Arun Kateel (46), Avinash Chandratiwari (33) na Vikram Sankhala (50) ambao wote ni washauri wa kampuni hiyo.

  Baadhi ya Wafanyakazi hao wa kampuni ya  Quality Group walipopandishwa mahakamani kwa mara ya kwanza,Mahakama ya Kisutu jijini Dar

  0 0

  Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wakiwa katika matembezi ya Maadhimisho ya Chama Cha Girl Guides Tanzania (TGGA) ya kumuenzi mwanzilishi wa chama hicho Duniami, Roden Barden Powell yaliyofanyika Manispaa ya Temeke Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa TGGA Tanzania, Profesa Martha Qorro na Kamishna Mkuu wa TGGA Tanzania, Symphorosa Hangi . PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
  Kamishna Mkuu wa TGGA Tanzania, Symphorosa Hangi akiwasalimia wanafunzi ambao ni wanachama a TGGA Temeke
  Wanafunzi wanachama wa TGGA Temeke wakiandamana wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Shule ya Tandika wilayani Temeke, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Viongozi wa TGGA wakipiga makofi wakati wa kuyapokea matembezi ya wanachama wa TGGA.


  0 0

  Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika Machi 8 Mwaka huu, katika uwanja wa Mwembeyanga Temeke Jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam jana maadhimisho hayo yataongozwa na maandamano ya Wanawake na wadau mbalimbali, na yataanzia katika Shule ya Msingi Mabatini kuelekea viwanja vya Mwembeyanga.

  Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania ya viwanda, Wanawake ndio Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi”.

  Kauli mbiu hiyo inalenga kuikumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kujenga mazingira wezeshi kwa Wanawake hasa kutambua mchango wao katika kuleta Maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla.

  Taarifa hiyo pia imeikumbusha jamii kuhusu wajibu wake ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa Wanawake haki sawa katika nafasi za Elimu, Uchumi na uongozi ili wawe chachu ya mabadiliko yenye lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

  Maadhimisho hayo yataambatana na maonesho ya kazi za ujasiriamali yanayoendelea katika uwanja wa Mwembeyanga, ambapo Asasi za kiraia na vikundi mbalimbali vya wanawake vitaonesha bidhaa zao.

  Aidha, Wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam wanakumbushwa kushiriki kwa wingi katika maadhimisho hayo ikiwa ni pamoja na kuwa na mikakati ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinanazowakabili Wanawake kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa.

  0 0

  Na Masanja Mabula -Pemba ..

  MADAKTARI kisiwani Pemba wametakiwa kuwa tayari kutoa ushahidi mahakamani juu ya vitendo vya udhalilishaji vinavyoendelea siku hadi siku dhidi ya wanawake watoto, ili wasipoteze muelekeo wa kupata fursa za kiuchumi nchini.

  Hayo yalielezwa na Afisa Mdhamini Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Pemba Khadija Khamis Rajab katika hospitali ya Wete, ikiwa ni shamra shamra ya siku ya wanawake duniani.

  Alisema kuwa, iwapo wanawake na watoto watadhalilishwa ndoto zao hukatika na kutofikia malengo aliyoyakusudia yanayoweza kumpatia fursa za ajira katika kujiimarisha kiuchumi.

  Afisa huyo alisema kuwa, zipo kesi ambazo madaraktari wanahusika na udhalilishaji kwa wanawake na watoto na kuwataka kuwa mstari wa mbele katika kutoa ushahidi wa vipimo mahakamani pindi unapotokea udhalilishaj huo.Hata hivyo alipongeza juhudi zinazofanywa na baadhi ya madaktari akiwemo Sauda Kassim wa hospitali ya Chake Chake kutokana na kuwa mstari wa mbele kutetea na kutoa ushahidi wa kutosha mahakamani na kumuhudumia muathirika ipasavyo.

  Kwa upande wake daktari msaidizi katika hospitali hiyo, Kulthum Bakar Juma, ameeleza kuwa kutokana na udhalilishaji wanaofanyiwa mahakamani pamoja kuona watuhumiwa wanaachiwa huru bila kutiwa hatiani linawarudisha nyuma madaktari katika kutoa ushahidi mahakamani.

  Nae Daktari Asya Omar Abrahman kutoka kitengo cha Benki ya Damu katika hospitali hiyo amesema, wamekuwa wakipoteza muelekeo wanapotakiwa kutoa ushahidi mahakamani, kwani mwisho wa siku mtuhumiwa anaonekana mitaani na kurudia tena udhalilishaji bila ya kuogopa.

  Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8, ikiwa ujumbe wa mwaka huu unasema ‘imarisha fursa za ajira kumuwezesha mwanamke kiuchumi’.older | 1 | .... | 1602 | 1603 | (Page 1604) | 1605 | 1606 | .... | 3272 | newer