Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1601 | 1602 | (Page 1603) | 1604 | 1605 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Benki ya CRDB imedhamiria kuwainua wanawake kiuchumi kwa kuwawezesha kwa kufungua akaunti ya Malkia ambayo itakuwa ni yenye malengo yakinifu na manufaa kwa maendeleo kwa wanawake.

  Akizungumza na Globu hii, Muhamasishaji wa kampeni katika wiki ya wanawake kutoka benki ya CRDB Mary Gekura, amesema kuwa akaunti hii ya Malkia inakuwa na malengo makuu ya kumuwezesha mwanamke ili aweze kuwa na malengo yakinifu ya kujiendeleza kiuchumi.

  Mary amesema kuwa, kampeni hii imeanza machi mosi na itakuwa ni endelevu na taratibu zake za kufungua ni kwa kima cha chini cha shilingi cha elfu hamsini (50,000) na mteja atatakiwa kuweka hela kwa muda wa mwaka mmoja bila kuzitoa.

  Amefafanua kuwa, ndani ya mwaka mmoja mteja anaweza kupata faida ya kutosha na kuanzisha miradi mbalimbali.
   Mkurugenzi wa tawi la CRDB Water Front Donath Shirima (kulia) akiwa pamoja katika picha na wafanyakazi wa tawi hilo kuelekea maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani  Machi 08 mwaka huu.
   Wafanyakazi wa wa tawi la CRDB Water Front katika picha za pamoja kuelekea maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani Machi 08 mwaka huu.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  MWAMUZI wa mchezo baina ya Yanga na Ruvu Shooting Ahmada Simba anatarajiwa kuitwa kwenye kamati ya masaa 72 pindi pale atakapowasilisha barua yake ya utetezi kuhusiana kukataa goli na kumpatia kadi ya njano Obrey Chirwa.

  Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Yanga kutoka nchini Zambia alipatiwa kadi hiyo katika dakika ya 43 baada ya kufunga goli na mwamuzi kulikataa goli hilo ambalo baadae lilikuja kuonekana halina matatizo.

  Katika mchezo huo wa ligi kuu Vodacom, mwamuzi Ahmada Simba alimpatia kadi ya pili Chirwa na kupelekea kupata nyekundu lakini Yanga waliweza kutoka na ushindi wa goli 2-0 dhidi  ya Ruvu Shooting.

  Akizungumza na Globu hii, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Alfred Lucas amesema kuwa kamati hiyo itakaa pindi watakapopokea utetezi wa mwamuzi huyo na kisha kutoa maamuzi ya juu yake.

  Lucas amesema, kabla ya kamati ya masaa 72 kukaa kwa ajili ya kujadili mechi za Simba dhidi ya Yanga, Ruvu dhidi ya Yanga tayari uongozi wa Yanga ulishatuma barua juu ya malalamiko ya kadi ya njano ya kwanza aliyopatiwa Chirwa na kutaka kuangaliwa tena.

  Baada ya kadi ya kwanza ya njano kufutwa moja kwa moja inapelekea kufutika kwa kadi nyekundu ya mshambuliaji huyo kutoka nchini Zambia.


  Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Alfred Lucas.

  0 0

  Ujenzi wa jengo la kuongozea ndege la Kiwanja cha ndege cha Mwanza, ukiendelea, ambapo unatarajiwa kukamilika baadaye mwaka huu. Mnara huu umeelezwa utakuwa na kiwango cha juu cha mawasiliano kwa nchi za Afrika Mashariki.
  Jengo jipya la kuhifadhi mizigo la kiwanja cha ndege cha Mwanza, likiendelea na ujenzi wake, jengo hilo linaukubwa wa mita za mraba 1500.
  Mizigo ya mabaki ya samaki aina ya Sangara maarufu kama mabondo yakiwa kwenye Kiwanja cha ndege cha Mwanza yakisubiri kusafirishwa nchini China kupitia Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo hutumika kutengeneza nyuzi zinazotumika kushona wagonjwa kwenye hospitali.
  Mwanzo wa ujenzi wa daraja la kuunganisha barabara ya kiungio cha ndege za mizigo na barabara ya kutua na kuruka ndege, ambayo itawezesha ndege za mizigo kuelekea kwenye jengo jipya la mizigo.
  Afisa Usalama wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Juma Nyamhanga (kushoto) akimfafanulia mmoja wa abiria ujazo anaotakiwa kusafiri nao kwa chupa za mafuta na manukato mbalimbali, kama alivyoishika pichani. Ujazo unaotakiwa kwa abiria kusafiri nao katika begi la mkononi ni kuanzia ujazo wa 50-100, na ikizidi lazima uingie kwenye begi litakaloingia sehemu ya mizigo.

  0 0

  Baadhi ya watumishi wa serikali wa wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wamekuwa wakishirikiana na wananchi katika kilimo halamu cha zao la bangi wilayani humu. Mpaka sasa wananchi watano wakiwemo watumishi wa serikali wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kujihusisha na kilimo cha bangi.

  0 0

  Mabalozi na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wa hapa nchini wametakiwa kuyahimiza makampuni ya nchi yao kutumia fursa za uwekezaji zinazotokana na zoezi la Serikali la kuhamia Dodoma. 

  Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb) katika kikao maalum cha kuwafahamisha wanadiplomasia hao uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano wa kuhamia Dodoma.

  “Uamuzi wa kuhamishia Makao Makuu ya Serikali mjini Dodoma umetengeneza fursa nyingi za uwekezaji katika maeneo mbalimbali kama vile utengenezaji wa vifaa vya ujenzi; ujenzi wa majengo ya ofisi, biashara na makazi; huduma za kijamii kama hospitali, shule, miundombinu ya maji safi na maji taka; TEHAMA; bustani za mapunziko; shughuli za kilimo na utalii. Hivyo, nachukua fursa hii kuwaomba muwahimize wawekezaji kutoka nchi zenu kuchangamkia fursa hizo”, Balozi Mahiga aliwambia wanadiplomasia wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza katika Mkutano na Mabalozi na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wa hapa nchini, kuhusu zoezi la Serikali la kuhamia Dodoma. mazungumzo hayo yalifanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam. Kushoto kwa Mhe. Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima.

  Balozi Mahiga alieleza kuwa uamuzi wa kuhamisha Makao Makuu ya Serikali kutoka Dar Es Salaam kwenda Dodoma ulifanywa mwaka 1973 lakini tokea kipindi hicho haukuweza kutekelezwa kutokana na sababu mbalimbali hadi Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ilipoingia madarakani.

  Mhe. Waziri alieleza kuwa zoezi la Serikali kuhamia Dodoma limepangwa kutekelezwa kwa awamu nne ambapo awamu ya kwanza tayari imeshakamilika. Katika awamu hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imehamisha watumishi 47 kati ya 152 waliopo Makao Makuu akiwemo yeye mwenyewe, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu. 
  Waziri Mahiga aliendelea kueleza kuwa kufuataia kuanza utekelezwaji wa uamuzi huo ambao ulitangazwa rasmi na Mhe. Magufuli alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM tarehe 23 Juali 2016, hakuna budi kwa Ofisi za Balozi na Mashirika ya Kimataifa nazo zianze kujiandaa kwa ajili ya kuhamia mji huo Mkuu wa Serikali.  

  Aliongeza kuwa, katika kipindi hiki cha mpito, baadhi ya Watumishi wa Wizara watakuwepo Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine watasaidia mawasiliano na ofisi hizo. Aidha, katika kipindi hicho, Wizara katika ofisi zake mpya zilizopo kwenye Jengo la LAPF mjini Dodoma itaimarisha mawasiliano kwa njia ya simu, mtandao wa internet na kufunga kifaa cha kufanyia mikutano kwa njia ya video ili kurahisisha mawasiliano na ofisi za Balozi.

  Mhe. Mahiga aliwafahamisha Mabalozi hao kuwa Serikali itatenga eneo maalum ambalo litakuwepo kwenye mji wa Serikali utakaojengwa Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za balozi na mashirika ya kimataifa.  Alisema pindi Serikali itakapokamilisha zoezi la kupitia upya Mpango Mkuu wa Mji wa Dodoma, itawasiliana na Balozi hizo ili ziweze kuwasilisha maombi ya mahitaji ya ardhi wanayohitaji.
  Balozi Mahiga alihitimisha kikao hicho kwa kuwashauri wanadiplomasia wanaomiliki majengo jijini Dar es Salaam kuingia makubaliano maalum na kampuni zinazohitaji ofisi hapa jijini ili kampuni hizo ziwajengee majengo ya ofisi mjini Dodoma. 

  Kwa ujumla wanadiplomasia walipokea uamuzi huo na kuiomba Wizara iwasilishe taarifa hiyo kwa maandishi ili nao waiwasilishe kwenye Serikali zao kwa ajili ya utekelezaji.

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina, amemtaka kandarasi anaeshughulika na ujenzi wa ukuta wa mto Pangani kampuni ya ( DEZO CIVIL CONSTRUCTION L.TD ) kukamilisha ujenzi wa ufukwe wa huo kwa kipindi cha muda wa miezi kumi.

  Ujenzi huo wa sehemu ya ufukwe wa kaskazini ambao una urefu wa mita 950 ambazo kati yake mita 550 zipo katika ujenzi wa awali utagharimu kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 2.4, unafadhiliwa na Mfuko wanchi maskini zaidi duniani LDCF kupitia shirika la kimataifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira UNEP na serikali ya Tanzania, kwa usimamizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.

  Aidha, Katika ziara yake ya kutembelea utekelezaji wa miradi wa kuhimili athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi katika fukwe za mto pangani leo Mkoani Tanga, Naibu Waziri Mpina amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo hayo ya mto pangani kuhepuka uharibifu wa mazingira ya ufukwe huo kwa kupanda miche ya miti ya mikoko ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo wa kuhifadhi fukwe ya mto Pangani, na kuwaasa kuhepukana na shughuli za kibinadamu ambazo si rafiki kwa mazingira hayo ili kunusuru fukwe hiyo kuliwa.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi Zubeda Abdalah Amemuomba naibu Waziri Mpina Kuiangali kwa jicho ya pekee fukwe iliyoko katika maeneo ya Tanga DECO ambayo imeathirika kwa kiasi kikubwa na athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabia nchi na haipo kabisa katika bajeti na mchakato mzima wa kunusuru fukwe..”utafutiwe ufumbuzi kupitia serikali au taasisi za kimataifa ili kuweza kuinusuru.” Alisema Mkuu wa Wilaya.

  Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewasa wasimamizi wa mradi huo kutumia fedha husika kwa matumizi kusudiwa kama vile mafunzo ya upandaji, utunzaji na uendeleezaji wa mikoko kwa wana vikundi kwani imezoeleka huko nyuma kuwa fedha kama hizo zimekuwa zikitumika kwa matumizi yasiyo kusudiwa.

  Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Wilaya ya Pangani Bw. Sabas Chambas, amewataka wadau wa maeneo yote ya Pangani wasimamie na kutunza miti ya mikoko kuchukua taadhari kwa kuzingatia athari za kimazingira kupitia wataalam kutoka wakala wa Taifa wa misitu TFS, na Serikali ya Wilaya. Awali imeelezwa kuwa, serikali ipo katika mpango wa kutafuta fedha, kwa ajili ya ujenzi wa fukwe ya kusini mwa mto pangani.

  Mradi huo wa unaofadhiliwa na mfuko wan chi maskini zaidi duniani unahusisha, ujenzi wa kuta za fukwe ya mto pangani, Kisiwapanza Pemba na Kilimani Unguja.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela akizungumza na Naibu Waziri Mpina na Ujumbe wa Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Merdad Kalemani haupo Pichani, katika ziara za ma Naibu Waziri hao Mkoani Tanga., kulia ni Msaidizi wa katibu tawala wa mkoa wa Tanga, Bi. Monica Kinara.
  Afisa misitu wa Wilaya ya Pangani Bw. Twairu Mkongo akielezea jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri Mpina katika fukwe ya mto Pangani.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wsa Rais Mhe. Luhaga Mpina akiongea na wanahabari alipokuwa akihitimisha Ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa ukuta wa mto Pangani ulioathiriwa na athari za mabadiliko ya Tabia Nchi.
  Katika Picha ni sehemu ya Fukwe ya Mto wa Pangani iliyoliwa na Bahari. (Picha na Habari zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais).

  0 0

   Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Nape Nnauye akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,kuhusiana na ujio wa mmoja wa Wasanii mahiri katika tasnia ya Filamu nchini Nigeria,Mike  Ezuronye nchini Tanzania,ambaye amewasili nchini kwa mradi maalumu wa kutengeneza filamu.Waziri Nape amesema kuwa ujio wa msanii huyo ni hatua kubwa katika Tasnia ta filamu nchini,kwani ujio wake utaongeza chachu ya mabadiliko kwa namna moja ama nyingine kwa wasanii wenyewe na sanaa yenyewe kwa ujumla.


  "Huyu ni mmoja wa wageni waliokuja na wengine wataendelea kuja,Sisi kama Serikali kazi yetu ni kunatengeneza mazingira mazuri waje zaidi katika nchi yetu,waje washirikiane na sisi,Wakija wataleta teknolojia,wataleta ujuzi na uzoefu wao lakini pia wakishirikiana na wasanii wetu kufanya kazi zao,kazi zetu zitaingia kwenye nchi yao na za kwao zitaingia kwenye nchi yetu na sote kwa pamoja tutafaidika kama nchi na wasanii kwa ujumla,
  .

  Amesema kuwa imefika wakati wasanii wa Tanzania waone haja ya kutumia sanaa zetu za Filamu na muziki kuliunganisha bara letu la Afrika,amesema kuwa hilo ni jambo kubwa sana  na anatamani Watanzania na wasanii wenyewe kwa ujumla waone wajibu walionao katika kuzitumia kazi zao kulifanya bara la Afrika kujivunia kazi za wasanii wake popote pale ulimwenguni. 
  Mkurugenzi wa kampuni ya  Entertaiment Project and Design (EPD) Halima Yahaya almaarufu kwa jina la kisanii Davina akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,kuhusiana na ujio wa Msanii Nguli wa Filamu kutoka nchini Nigeria,Mike  Ezuronye nchini Tanzania.

  Davina amesema kuwa ujio wa msanii huyo umefanyika kwa Msaada mkubwa wa Serikali kupitia Wizara ya Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo.Anasema wamefanikiwa kumleta msaniii huyo kupitia kampuni yake kwa ajili ya kufanya mradi (Project) ya Filamu hapa nchini,Davina amesema kuwa msanii huyo mahiri anatarajia kukaa nchini kwa wiki mbili mpaka pale mradi huo utakapokamilika.Pichani kulia ni Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Nape Nnauye.
    Msanii Nguli wa Filamu kutoka nchini Nigeria,Mike  Ezuronye akizungumzia ujio wake hapa nchini,kwa Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,Pichani kulia ni Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo,Nape Nnauye.
   Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Msanii huyo wa nyota wa Filamu kutoka nchini Nigeria,alipokuwa akizungumzia ujio wake hapa nchini.Picha na Michuzi Jr.


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe Kamati Maalum ya Kupitia Mpango Kabambe wa Mji Mkuu wa Dodoma, Ofisini kwake mjini Dodoma Machi 6, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri).


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


  Jukwaa la kiuchumi la kifalme lililokuwa na malengo ya kutoa elimu kwa wananchi namna ya kutafuta na kuhifadhi fedha kwa ajili ya kujiinua kiuchumi linatarajiwa kuanza kesho katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam.

  Mkutano huo utakaohudhuriwa na Mchungaji maarufu na mfanya biashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston kutoka Marekani utakuwa ni wa siku tatu na atakuwa akitoa mada ya namna ya wafanyabiashara pamoja na wananchi wengine kujua namna ya kutafuta mtaji na kujiendeleza kiuchumi pamoja na 
  makamu wa raisi wa benki ya Dunia kanda ya Afrika Dr Oby Ezekwesili 
  .


  Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu mkuu wa Katibu Mkuu wa taasisi ya Kingdom Leadeship Network Tanzania (KLNT), Dk. Charles Sokile amesema kuw amkutano huu utakuwa na faida kubwa sana kwa wafanyabiahsra na wananchi wengine kwani kutakuwa na faida kubwa kwani kutakuwa na wafanyabiashara mbalimbali kutoka nchi mbalimbali duniani.

  Mbali na hilo, kutakuwa na mafunzo ya namna ya kutafuta mtaji na kujiendeleza, uadilifu wa kumpendeza mungu, serikali na kulipa kodi kwa wakati.

  Sokile amesema kuwa, pia kutakuwa na maombi kwa ajili ya taifa yatakayoendeshwa na Bill Winston pamoja na aliyewahi kuwa makamu wa raisi wa benki ya Dunia kanda ya Afrika Dr Oby Ezekwesili pamoja na Bishop Bernard Nwaka kutoka Zambia.
  Mchungaji maarufu, mfanyabiashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston (wa pili kulia), kutoka Marekani akiwasili katika Hotel ya Hyatt KIlimanjaro Dar es Salaam leo ambapo atatoa mada katika Mkutano Mkubwa wa Kiuchumi wa siku tatu pamoja na Maombi ya Kitaifa 2017 unaotarajiwa kuanza jijini humo kesho. Mkutano huo unaandaliwa na taasisi ya Kingdom Leadeship Network Tanzania (KLNT). Pamoja naye kutoka kushoto ni, Mkurugenzi Mtendaji wa KLNT, Isaac Mpatwa, Mratibu wa Kamati ya Maandalizi, Carol Mbaga na Katibu Mkuu wa KLNT, Dk. Charles Sokile
  Katibu Mkuu wa taasisi ya Kingdom Leadeship Network Tanzania (KLNT), Dk. Charles Sokile akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkutano mkuu wa jukwaa la kiuchumi unaootarajiwa kuanza kesho. Kulia ni mwanasheria wa KLNT Fred Ringo.

  Mwenuyekiti wa bodi ya wadhamini wa Kingdom Leadeship Network Tanzania (KLNT) Bishop Bernard Nwaka (katikati) akijadiliana jambo na mwanasheria wa KLNT Fred Ringo (kulia) na Katibu Mkuu wa KLNT, Dk. Charles Sokile.

  0 0

  RAIS Dk. John  Magufuli ametengua  uteuzi wa   Mtendaji  Mkuu wa Shirika  Elimu Kibaha  Dkt. Crspin  Mpemba  ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali za kiutendaji zinazomkabili.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Simbachawene amesema kufuatia tuhuma mbalimbali za uendeshaji, zinazolikabili Shirika hilo ambazo zimekuwa zikiandikwa kwenye vyombo vya habari kwa muda mrefu sasa.

  Simbachawene amesema Mnamo Machi, 4 mwaka huu Rais Magufuli ametengua  rasmi nafasi ya Mtendaji huyo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo.

  Amefafanua kuwa kumekuwepo  malalamiko dhidi ya Mtendaji  Mkuu wa  wa shirika la Elimu Kibaha ambapo Ofisi ya Rais TAMISEMI  iliunda kikosi kazi  ili kufanya uchunguzi dhidi ya malalamiko hayo na kugundua  kuwepo kwa changamoto katika uendeshaji wa Shirika hilo.

   “Ni kweli tuhuma juu ya uendeshaji wa Shirika la Elimu Kibaha likiwemo suala la Mikataba iliyoingiwa na Shirika hilo zimekuwepo kwa muda mrefu sasa. Sisi kama Wizara hatukutaka kukurupuka kufanya maamuzi na tukaamua kuunda kikosi kazi ili kufanya uchunguzi na matokeo ya uchunguzi huo yanapelekea kuwepo kwa hoja  zinazohitaji uchunguzi zaidi,” ameeleza Waziri Simbachawene.

  Ameongeza kuwa ili uchunguzi huo uweze kufanyika kwa uhuru Mhe. Rais ameamua kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha ili kupisha uchunguzi wa kina dhidi yake.

  Waziri amesema uamuzi wa kumsimamisha umechukuliwa kwa kuwa tuhuma  na malalamiko mengi ya awali yaliyojitokeza  dhidi yake yanajenga hoja ya kuhitajika kufanyika kwa uchunguzi zaidi ambapo kwa sasa nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha inakaimiwa hadi hapo  uchunguzi utakapokamilika.  0 0

  Na Zainab Nyammka, Globu ya Jamii

  Msafara wa mabingwa wa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara  Yanga SC , umewasili salama jijini Dar es salaam ukitokea Morogoro walipokwenda kucheza na Mtibwa Sugar kwa matokeo ya sare ya 0- 0.

  Msafara huo umeelekea moja kwa moja kambini kwa maandalizi ya michezo miwili muhimu itakayofanyika kesho machi 7, 2017 dhidi ya Kiluvya United uwanja wa Taifa na machi 11, klabu bingwa Afrika dhidi ya Zanaco FC.

  Timu imeendelea na mazoezi jioni ya leo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kesho robo fainali kombe la FA dhidi Kiluvya ya kutoka mkoani Pwani . 

  Kocha mkuu wa Yanga George Lwandamiana amesema kuwa  licha ya ratiba ngumu kuikabili timu yake lakini amesema yupo tayari kupambana na vijana wake ili kuhakikisha klabu inapata matokeo mazuri katika michezo yote miwili. 

  Wapenzi , wanachama , mashabiki na wadau wa soka mnaombwa kujitokeza kwa wingi katika michezo yote miwili ili kuipa sapoti timu hiyo . 

  Mbali na hilo, droo ya kombe la Shirikisho hatua ya saba au robo fainali inatarajiwa kufanyika kesho baada ya kupatikana kwa mshindi  wa mechi kati ya Yanga na Kiluvya na kuungana na timu za Simba na Azam FC za Dar es Salaam, Mbao FC ya Mwanza, Tanzania Prisons ya Mbeya, Madini ya Arusha, Kagera Sugar ya Bukoba na Ndanda FC ya Mtwara.

  0 0

   Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche akionesha kwa waandishi wa habari moja ya pombe kali aina ya Nguvu zilizokamatwa wakati wa operesheni inayoendelea mapema leo hii jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya nne ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.
   Msimamizi wa ghala la Love kira  Enterprises lililopo Wazo Bi. Sia Mboya (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche (katikati) wakati wa operesheni ya kuondoa pombe hiyo katika soko, kulia ni Afisa Afya toka Manispaa ya Kinondoni Bw. John Kijumbe.

    Gari lililokutwa limebeba pombe kali aina ya kiroba original likiwa limeegeshwa nje ya duka kuuza vinywaji la Love Kira lililopo Wazo jijini Dar es Salaam mapema hii leo.

  BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI

  0 0

  Na.Vero Ignatus ,Arusha.

  Mtu moja ambaye jina lake hajijafahamika ameuawa na wananchi wenye hasira kali huko maeneo ya kwa Mrombo Jijini Arusha, akidhaniwa kuwa ni mwizi wa pikipiki baada ya mtu huyo kupita na kufananishwa na waendesha pikipiki hao.

  Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa majira ya saa saba mchana wananchi hao walimuona mtu huyo wakadhania kuwa ndiye aliyewahi kumnyanyanya mwenzao pikipiki hivyo wakaanza kumshambulia na kumburuza ambapo hadi jeshi la polisi kufika eneo la tukio mtu huyo alikuwa tayari ameshachoka na hali yake ilikuwa mbaya wakiwa njiani kumpeleka hospitali alifariki.

  Kamanda Charles Mkumbo amewataka wananchi kutochukua sheria mkononi kwani wanaweza kumdhuru mtu ambaye hausiki na tukio amesema kuwa wanapomuhisi mtu kuwa ni muhalifu watoe taarifa kwa jeshi la polisi ili sheria ichukue mkondo wake. 

  Hadi sasa jeshi la polisi mkoani hapa linawashikilia watu watano ambao ni waendesha pikipiki kwa kuhusika katika tukio hilo,mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya maountmeru ukisubiria ndugu na jamaa kwenda kumtambua.

  0 0

  Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli na Balozi wa China nchini Dkt wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi ya Uwanja wa kisasa wa ndegevita wa Ngerengere mkoani Morogoro leo Machi 6, 2017

   Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa  uzinduzi  rasmi ya Uwanja wa kisasa wa ndegevita wa  Ngerengere mkoani Morogoro leo Machi 6, 2017.
  Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli akijiandaa kufyatua risasi ya bastola kuashiria matumizi rasmi ya Uwanja wa kisasa wa ndegevita wa Ngerengere mkoani Morogoro leo Machi 6, 2017
   Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli na Balozi wa China nchini Dkt katika picha ya pamoja na viiongozi mbalimbali baada ya uzinduzi  rasmi ya Uwanja wa kisasa wa ndegevita wa  Ngerengere mkoani Morogoro leo Machi 6, 2017.

  PICHA NA IKULU

  0 0


  Akizungumza katika ukaguzi huo, Jafo alisema utekelezaji wake umesuasua hali inayosababisha wananchi wa eneo hilo waendelee kupata adha ya maji na kuiagiza Halmashauri ya Chamwino kuzuia fedha ya mkandarasi huyo zilizosalia kwa kipindi cha miezi mitatu mpaka ubora wa mradi huo utakapoonekana.

  Hata hivyo alisema mkandarasi aitwaye M/S Kijima fedha aliyopewa hadi sasa haiendani na kazi iliyofanyika huku akitilia mashaka mabomba yaliyowekwa kwamba yapo chini ya kiwango.

  “Mkandarasi umepewa Sh. Milioni 305.7, gharama ya mradi kwa ujumla ni Sh.Milioni 347.9, umebakisha fedha kidogo ambayo ni Sh.milioni 42.1 tukiangalia kazi iliyofanyika hata haiendani na fedha ulizopewa, unachokifanya hapa ni kama maigizo huu mradi haujafikia asilimia 90 na haya mabomba yanaonekana yapo chini ya kiwango maana yameanza kupasuka,”alisema Jafo

  Aidha alisema Halmashauri hiyo imekuwa na uzembe katika usimamizi wa miradi ya maji hali inayosababisha wananchi kukosa huduma ya maji kwa wakati.Jafo alimtaka Mkandarasi huyo kukamilisha mradi huo na kwamba ifikapo Aprili 3, mwaka huu atarudi kukagua na kuiagiza serikali ya wilaya hiyo kuwakamata watu watakaoharibu miundombinu ya maji.

  Hata hivyo alisema katika miradi mingi ya maji aliyotembelea amekutana na changamoto ya wakandarasi kuweka mabomba ambayo yapo chini ya kiwango na kusababisha wananchi wanapokabidhiwa mradi kushindwa kuiendesha.

  Naye, Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho ambaye pia ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Camp A, Waziri Sengoli, alisema wananchi wa kijiji hicho wamekuwa wakipata adha ya maji ka takriban miaka saba huku akiwaumbua viongozi wa Halmashauri hiyo kwamba wamekuwa hawatembelei kukagua mradi huo.

  Kwa upande wake, Mkandarasi huyo Enock Masanja, alijitetea kuwa ameshindwa kukamilisha mradi kwa wakati kutokana na kutopata fedha kwa wakati.
  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo akitoa maelekezo baada ya kukagua mradi wa maji wa Wilunze Wilaya ya Chamwino.
  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo akimsikiliza Mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa maji Wilunze Enock Masanja.
  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo akikagua mradi wa maji Wilunze wilaya ya Chamwino.


  NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo amefanya ziara ya kutembelea mradi wa maji katika kijiji cha Wilunze wilaya ya Chamwino na kutoa mwezi mmoja kwa Mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo kukamilisha kutokana na utekelezaji wake kuwa wa muda mrefu.


  0 0

  Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Umma kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Justus Mulokozi akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WILDAF) Naomi Kaihura (kushoto kwake), Mkurugenzi wa shirika hilo, Dk Judith Odunga (kulia kwake) na wajumbe wa shirika hilo wakati wa kongamano la Siku ya Wanawake Duniani lililoandaliwa na Shirika hilo na kufanyika Dar es Salaam leo.
  Washiriki wa kongamano la Siku ya Wanawake duniani lililoandaliwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF) wakifuatilia matukio ya kongamano hilo Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF), Dk Judith Odunga akizungumza na washiriki wa kongamano la Siku ya Wanawake Duniani lililofanyika Dar es Salaam leo (Machi 6). Kusoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Umma kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Justus Mulokozi, Mwenyekiti wa shirika hilo, Naomi Kaihula (wa pili kulia) na wajumbe wengine wa shirika hilo.
  Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Umma kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Justus Mulokozi akizungumza na washiriki wa kongamano la Siku ya Wanawake Duniani lililoandaliwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF) na kufanyika Dar es Salaam leo (Machi 6).


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Mhe. Dkt Harrisson Mwakyembe amesema Serikali haiwezi kuona Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kinajiingiza katika siasa na kama TLS wanataka hivyo, basi Serikali haitasita kuifuta Sheria ya TLS Sura ya 307 iliyoanzisha chama hicho cha Wanasheria.

  Amesema kuwaingiza wanachama ambao wana nasaba za siasa au viongozi wa vyama vya siasa ndani ya TLS ni kuruhusu mgongano wa maslahi na yeye kama mwanasheria hawezi kulikubali jambo hilo. DKt Mwakyembe alikuwa akizungumza hayo na ugeni wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) uliokuja kumtembelea Ofisini kwake mjini Dodoma ukiongozwa na Rais wao Bw. John Seka

  “Kama Wizara hatujui mwelekeo wa TLS kwa sasa, hatuwezi kuiacha TLS ikijiingiza katika siasa halafu tukawaangalia tu. Hatuna nia ya kuitawala TLS, ila tunawajibika kuwasimamia kwa kuwa Sheria yenu iko chini yetu, mkiharibu kwa lolote Wizara ndio yenye wajibu wa kuwatolea maelezo, katika hilo mnalotaka kulifanya sasa kuna mgongano wa maslahi, je nyinyi kama wanasheria hamkuliona au hamlioni?, alisema Mhe Mwakyembe.

  Alisema Serikali haina shida na wanachama wa TLS kuwa wanachama wa vyama vya siasa ila ni lazima wafahamu kwamba viongozi wanaowachagua ambao ndio watakaobeba sura ya TLS na mwelekeo mzima wa chama kama wanataaluma hawapaswi kuwa na nasaba za kisiasa ili kuepusha mgongano wa maslahi unapoweza kujitokeza.

  “Serikali haina shida na wanachama wa TLS kuwa wanachama wa vyama vya siasa ila tatizo linakuja pale mnapotaka kuchagua viongozi ambao tayari wanazo kofia mbalimbali za uongozi ndani ya vyama vya siasa, hao ndio watakaobeba sura na mtazamo au mwelekeo wenu hapo hatuwezi kukubali kwa kuwa watatenganishaje uongozi wao katika chama husika na uongozi wao ndani ya TLS, huo sasa ndio mgongano wa maslahi alisema Dkt. Mwakyembe na kuongeza kuwa ndio maana mwanasheria yoyote akiingia katika utumishi wa umma uwakili wa kujitegemea anauweka pembeni ili kuepuka mgongano wa maslahi.”
  Alisema TLS sasa imekuwa na haihitaji muangalizi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma nchi ilipopata uhuru, kwani ina wasomi wengi na vijana wengi wamekuwa wanachama pia na kwa hiyo ni bora tuifute hii Sheria yenu na tuwape mwanya mkajisajili kama NGO ambako kiongozi yeyote wa chama cha siasa anaweza kuwa kiongozi wao.


  0 0

  Na: Frank Shija, MAELEZO.

  BODI ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) imeagizwa kuanza mara moja kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake umekuwa ukisuasua kwa muda mrefu huku kukiwa na fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji miradi hiyo.

  Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na wakati akizindua Bodi Mpya ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) leo Jijini Dar es Salaam.

  Profesa Ndalichako ameshangazwa na kitendo hicho cha ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi hiyo huku kukiwa na shilingi takribani bilioni 14.5 zilizotengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/207 kwa ajili ya kazi hizo.

  “Inasikitisha kuona kuwa tunakaribia robo ya mwisho ywa mwaka wa fedha 2016/2017, huku karibu miradi yote ya maendeleo haijaanza kutekelezwa,isipokuwa ile tu ya kujengea uwezo na siyo ya ujenzi wa VETA ambazo ndiyo hitaji kubwa kwa sasa.”Alisema Profesa Ndalichako.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Peter Maduki na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dkt. Bwire Ndazi.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board) Peter Maduki akizungumza mara baada ya Bodi ya uzinduzi wa rasmi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Kaimu Mkurugenzi wa VETA Dkt. Bwire Ndazi.
  Kaimu Mkurugenzi wa VETA Dkt. Bwire Ndazi akizungumza mara baada ya Bodi ya uzinduzi rasmi wa Bodi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board) Peter Maduki (kushoto).


  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli ametengua rasmi nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Shirika Elimu Kibaha Dkt. Crispin Mpemba ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali za kiutendaji zinazomkabili.

  Akijibu swali la Waandishi wa Habari waliotaka kupata ufafanuzi juu ya hatma ya tuhuma mbalimbali zinazolikabili Shirika la Elimu Kibaha ambazo zimekuwa zikiandikwa kwenye vyombo vya habari kwa muda mrefu sasa, Mhe. Simbachawene alisema kutokana na kuwepo kwa tuhuma mbalimbali za uendeshaji, Mhe. Rais Magufuli tarehe 4/3/2017 ametengua rasmi nafasi ya Mtendaji huyo ili kupisha uchunguzi.

  “ Ni kweli tuhuma juu ya uendeshaji wa Shirika la Elimu Kibaha likiwemo suala la Mikataba iliyoingiwa na Shirika hilo zimekuwepo kwa muda mrefu sasa. Sisi kama Wizara hatukutaka kukurupuka kufanya maamuzi na tukaamua kuunda kikosi kazi ili kufanya uchunguzi na matokeo ya uchunguzi huo yanapelekea kuwepo kwa hoja zinazohitaji uchunguzi zaidi. Hivyo, ili uchunguzi huo uweze kufanyika Mhe. Rais amemsimamisha kazi Mtendaji huyu Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha ili kupisha uchunguzi wa kina dhidi yake. Alisema Mhe. Simbachawene

  Alisema uamuzi wa kumsimamisha umechukuliwa kwakuwa tuhuma za awali zilizojitokeza dhidi yake zinajenga hoja ya kuhitajika kufanyika kwa uchunguzi zaidi.

  Kwasasa nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha inakaimiwa hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.

older | 1 | .... | 1601 | 1602 | (Page 1603) | 1604 | 1605 | .... | 3286 | newer