Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

BEI YA MADAFU LEO


WAPI HAPA wadau?

0
0
 Katika pitapita zake kamera ya Globu ya Jamii ilifika mahali hapa katikati ya jiji la Dar es salaam na kukuta mambo mswano. Yaani barabara imetengenezwa na kugeuza kabisa sura ya sehemu hii kwa kusakafiwa concrete slabs (sijui kimatumbi inaitwaje - msaada tutani plizzz) badala ya lami kama ilivyozoeleka. Je, mdau ni mtaa gani huu??


TAIFA STARS yalala 2-1 kwa ETHIOPIA leo

0
0


Na mwandishi wetu, Addis Ababa
Tanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ethiopia uliochezwa leo (Januari 11, 2013) kwenye Uwanja wa Addis Ababa hapa jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Mechi hiyo iliyochezeshwa na Bamlak Tesema wa Ethiopia ilikuwa ya kusisimua, hasa kutokana na timu zote kucheza kwa kasi kwa muda wote. Wenyeji Ethiopia ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 13 lililofungwa na Fuad Ibrahim akiwa wastani wa hatua sita kutoka kwa mlinda mlango Juma Kaseja wa Taifa Stars.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kama kilivyokuwa cha kwanza, huku Ethiopia wakiwa wamefanya mabadiliko kwa wachezaji watano. Tanzania ilifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 50 likifungwa na Mbwana Samata baada ya kumzidi maarifa beki mmoja wa Ethiopia.

Bao la ushindi kwa Ethiopia lilifungwa kwa kichwa dakika ya 69 na mshambuliaji Shemelis Bekele aliyeingia kipindi cha pili akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na winga Yossuf Sallah kutoka upande wa kushoto.

Taifa Stars inarejea nyumbani kesho (Jumamosi, Januari 12 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7 kamili mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines.

Taifa Stars: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Thomas Ulimwengu/Khamis Mcha, mwinyi Kazimoto na Mbwana Samata.

swali la kizushi...

0
0

Salaam Ankal Michuzi na Wadau wote,
Nimeona mara kadhaa anapotangulia mtu yeyote mbele za haki alimradi ni mtu mashuhuri basi mwili wake hubebwa na GARI LA WAGONJWA. 

Sasa kinachonisumbua ni kwanini magari ya kubebea wagonjwa yana bebea maiti. 
Je kukitokea mgonjwa atasubiri mpaka hili gari limalize shughuli za msiba ndiyo likamhudumie mgonjwa? 
Sikuhizi kuna magari maalum ya kukubebea miili ya waliotutangulia kwenye haki kwanini yasitumiwe hayo. Sijajua hili wazo limetoka wapi ninauliza maana inawezekana kunasababu ya kufanya hivyo, kama kuna sababu naomba tuambiane ili na sisi wengine turekebisha akiba zetu kichwani.

Mdau wa Globu ya Jamii, Uswazi

Taarifa ya Mazishi

0
0
Kwa niaba ya Ndugu,jamaa na marafiki wa Marehemu Herman Minja wa jijini Arusha,Tunatangaza ratiba ya mazishi ya ndugu yetu Mpenda Marehemu HERMAN MINJA aliefariki ghafla nyumbani kwake jijini Arusha hivi karibuni,Tararibu ya kuuaga Mwili wa Marehemu itaanza saa moja asubuhi siku ya Jumamosi (leo) tarehe 12 Januari 2013 Nyumbani kwa Marehemu Arusha na baadae Mwili utasafirishwa kwenda nyumbani kwao Marangu Masia Mamba,Moshi kwa Mazishi. Ibada ya mazishi Marangu itaanza saa sita mchana . 

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe

Amen.

THE PUBLIC SEMINAR ON THE ROLE OF ENTREPRENEURSHIP, INNOVATION AND ICUBATION FOR DEVELOPMENT

0
0
The Commission for Science and Technology (COSTECH), is hosting a Public Seminar titled, “The role of entrepreneurship & innovation for development” to be held on the 11th January, 2013.

This seminar is organized by COSTECH and Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) and is presented by Mr. Aape Pohjavirta from Finland. Mr. Pohjavirta is an Entrepreneur, and Founder leader of the Human Learning Project/Inclusion in Finland.

He has been a CEO of several companies and is knowledgeable in entrepreneurship systems, innovation and in technologically business environments, including mobile learning environments.. The Seminar is about understanding the role of Incubation, Innovation and Entrepreneurship in a developing economy like Tanzania.

In the past few months, COSTECH and DTBi have received visitors from different organizations/entities understand the COSTECH/DTBi philosophy/model on entrepreneurship, innovation and incubation.

The objective of this seminar is to understand the crucial linkage between academia and industry in innovation and entrepreneurship through incubation. At the same time it is get an idea of how to create a critical mass of human resources who can be the “vehicles” for development of our national economy.

For more information about COSTECH and/or Dar Technology Business Incubator, please visit our websites: www.teknohama.or.tz or www.costech.or.tz. Our email are: info@teknohama.or.tz or info@costech.or.tz and Tel. No: 0766 368 387 or (022) 277 0745/6
Mr. Aape Pohjavirta, making his presentation
A portion of the participants listening to the Presenter
Ambassador Sinikka Antila making her Opening Remarks as Guest of Honour.
Sharing a light moment, Left to Right Prof. Bidanda, Vice Chancellor of the Open University H.E. Sinikka Antila, Resident Ambassador of Finland to Tanzania Eng. George Mulamula, CEO of Dar Teknohama Business Incubator
Group Photo, Left to Right Eng. George Mulamula, CEO of Dar Teknohama Business Incubator Mr. Aape Pohjavirta, Entreprenur & Founder Leader of Human Learning Project/Inclusion in Finland H.E. Sinikka Antila, Resident Ambassador of Finland to Tanzania Dr. Hassan Mshinda, Director General of the Commission for Science & Technology

GREATEST BONGO FLAVOUR ARTISTS FROM TANZANIA ON SPORAH SHOW

IGP MWEMA AKABIDHI PIKIPIKI 564 KWA MAKAMANDA WA POLISI NCHI NZIMA

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema akimkabidhi pikipiki Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova kama ishara ya kukabidhiwa Makamanda wote Tanzania bara na Visiwani ambapo jumla ya Pikipiki 564 zimekabidhiwa kwa ajili ya kuzuia uhalifu kwa lengo la matumizi ya Wakaguzi Tarafa wa Polisi Tanzania bara na Majimbo yote ya Zanzibar, program za Safiri Salama na Usalama wetu kwanza.Makabidhiano hayo yamefanyika katika makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Makamanda na maafisa mbalimbali wa jeshi hilo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova akijaribu kuwasha moja ya pikipiki zilizotolewa kwa maofisa mbalimbali wa jeshi hilo nchi nzima mara baada ya makabidhiano.anayeangalia katikati na Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema na kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Posta Bw. Sabasaba
Afande Inspekta Mkweru akijaribu moja ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa maafisa wa jeshi hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema kulia akiwa katika hafla ya makabidhiano hayo makao makuu ya jeshi la polisi jijini Dar es salaam leo asubuhi, katikati ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova
Maafisa mbalimbali wa jeshi la polisi wakiwa katika hafla hiyo leo asubuhi.
Maafisa mbalimbali wa jeshi la polisi wakiwa katika hafla hiyo.
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja akizungumza jambo na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania Advera Senso wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa maafisa hao wa polisi leo.

Mtoto wa Kike anaejishughulisha na Usafishaji wa Vioo vya Magari ya Watu Mabarabarani

0
0
Kamera ya Globu ya Jamii,imemnasa Binti huyu ambaye jina lake halikufahamika mara moja katika Maeneo ya Kamata Kariakoo akijitafutia riziki yake kwa kujishughulisha na usafishaji wa Vioo vya Magari ya watu yanayokuwa yamesimama kwenye Mataa ya Kuongozea Magari.Kwa kawaida imezoeleka kuonekana vijana wa kiume ndio wanaoonekana kujishughulisha na kazi hii sehemu kubwa ya jiji la Dar na si wa kike kama alivyoonekana huyu.

ngoma azipendazo ankal - kizazi kipya

0
0
Bibie Nyota Ndogo na ngoma ya 'Watu na Viatu' anaweza kumtoa nyoka pangoni

ngoma azipendazo ankal - enzi hizo

0
0
Ngoma ya Bee Gees ya Stayin' Alive iliturusha sana enzi hizo...

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA SHEREHE ZA MIAKA 49 YA MAPINDUZI ZANZIBAR LEO

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, akikagua Gwaride wakati wa Sherehe za Mapinduzi, zilizofanyika leo kwenye Uwanja wa Amani mjini Zanzibar. Picha na OMR.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Salmin Amour, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu,  Edward Lowassa, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ameir Pandu Kificho, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar
 Viongozi mbalimbali wa Kitaifa walihudhuria sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Amani mjini Zanzibar leo.

KILELE CHA SHEREHE za maadhimisho YA MIAKA 49 YA MAPINDUZI ya zanzibar yafana leo MJINI ZANZIBAR.

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikagua gwaride la Vikosi vya ulinzi katika kilele cha sherehe za kutimiza Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wakati alipomaliza kukagua gwaride la  Vikosi vya ulinzi katika kilele cha sherehe za kutimiza Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, zilizofanyika leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Baadhi ya Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zabzibar.{Picha na Ramadhan Othman,IKULU.]
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho  Kikwete,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Amani Abeid Karume,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Salmin Amour Juma,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika leo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

U.S. Ambassador to the United Nations Food and Agriculture Agencies in Rome David J. Lane Press Conference in Dar es Salaam

0
0
U.S. Ambassador to the United Nations Food and Agriculture Agencies in Rome David J. Lane (second from left) elaborating a point during a press conference held in Dar es Salaam on January 12, 2013. Ambassador Lane reiterated United States' commitment to support Tanzania in its efforts to promote transformative agricultural development through the "Kilimo Kwanza" initiative. Ambassador Lane accompanied by a cadre of seven print and radio journalists from Italy, Ghana, Tanzania, Uganda, Malawi, France and Niger visited Tanzania from January 7 to 12 to observe how the United States government and the UN Food and Agriculture Agencies collaborate to support farmers, businesses, and Tanzanian government officials improve food security and promote agricultural development . Others in the picture are U.N Food and Agriculture Organization (FAO) Country Representative Diana Tempelman (right), World Food Program Country Representative Richard Ragan (second from right) and USAID Feed the Future Team Leader Tom Hobgood (left). (Photo courtesy of the American Embassy)

Just In: Ajali mbaya yatokea Posta Mpya jijini Dar jioni hiii,Mwanajeshi mmoja apasuka kichwa baada ya kujigonga mtini

0
0
 Baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakimshusha mwenzao baada ya kujigonga kwenye mti na kujeruhiwa vibaya sana kwa kupasuka kichwa wakati akiwa kwenye Lori lenye namba za usajili 5514 JW 07 aina ya IVECO kandokando ya barabara ya Samora jirani na Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam jioni hii. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Baadhi ya wasamalia wema wakimpeleka hospitali majeruhi huyo.
 Majeruhi akiingizwa katika Bajaji tayari kwa ajili ya kupelekwa hospitali.
 Lori aina ya IVECO ambalo majeruhi huyo alikuwa amepanda.
 Hii ndio Barabara ya Samora ilipotokea ajali hiyo. 
Hapa ndipo alipojigonga majeruhi na kupasuka kichwa.

TAARIFA YA MSIBA

0
0
FAMILY YA SAMEJI YA TANGA NA DAR-ES-SALAAM KWA MASIKITIKO MAKUBWA TUNATANGAZA KIFO CHA NDUGU YETU MPENDWA ALICE SAMEJI ALIYEFARIKI 11/01/2013 HUKO TANGA MUNGU AYIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMEN.

UTAKUMBUKWA SANA NA DADA, KAKA WAJOMBA, SHEMEJI ,WATOTO WAKO, MAJIRANI ,WAJUKUU NA WOTE WALIO GUSWA NA MSIBA HUU BILA KUSAHAU NDUGU ZAKO WALIOPO U.S.A SALOME ,BOBSO NA BRIAN.

UMETANGULIA NASI WOTE NI NJIA MOJA.
SALOME AND BOBSO
U.S.A

EMBE DODO ZIKIINGIA MJINI

MWALIKO WA KUSHIRIKI KATIKA TAMASHA LA SANAA NA UTAMADUNI LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI LITAKALOFANYIKA KIGALI, RWANDA TAREHE 9 – 16 FEBRUARI, 2013.

Article 7

0
0


Habari Waungwana
Natumaini u na afya njema hasa katika kusherekea Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar,Pamoja na hivyo bado tuna jukumu kubwa katika kuikomboa Jamii yetu ambayo ipo katika Mazingira Magumu hasa katika upatikanaji wa habari lakini pia kutoibua Changamoto zilizopo katika Jamii huska.

Kwa kutambua umuhimu wa Jamii yetu, JAMII INFORMATION NETWORK  (JIN) ni Asasi ambayo imeamua kusogelea Jamii  katika kuibua Changamoto mbalimbali na Kuipasha Jamii hska habari. Tunapenda  kuitumia blog hii kuitangaza Blog ya Asasi ya Jamii Information Network ambayo itakuwa ikielezea mambo mbalimbali yanayofanywa na Asasi hiyo
 
               Tembelea  blog hii kila Mara          www.jamiiinformation.blogspot.com

MHE JOHN POMBE MAGUFULI AONGEA WAKATI WA UZINDUZI WA UJENZI WA DARAJA LA MBUTU, IGUNGA

Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images