Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1597 | 1598 | (Page 1599) | 1600 | 1601 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Watu watatu wamefariki  na  28 wamejeruhiwa katika ajali ya basi la kampuni ya ILYANA yenye namba T  202 DGK , inayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Songea Mkoani  Ruvuma

  0 0


  0 0

  See this young Tanzanian kid being creative in a positive way...

  0 0
 • 03/03/17--12:30: IN LOVING MEMORY
 •  

  Rabbiel Daniel Swai (7/3/1941 – 3/3/1997)
  It's been 20 years today since you departed us. It broke our hearts to lose you, but you did not go alone.  A part of us went with you, the day God took you home. If tears could build a stairway, and heartaches make a lane, we would walk our way to heaven, and bring you back again. In life we loved you dearly, in death we love you still, in our hearts you hold a place no one could ever fill. You are missed by your lovely wife Elly Rabbiel Swai, your children Dorris, Nelson, Clemence, Frank and Edward. Your son and daughters in-law Albert, Aikael, Gloria and grandchildren Bradley, Dryden, Derine, Desmond, Donavan, Ellie and Nathan, your Sister Elly Ndossy, family members and friends. May God continue to keep you in comfort and peace till we meet again.


  Thanks giving will be held at 9:30 am Church Service at Azania Front on 5th March 2017.


  0 0
  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi ameagiza Kliniki tembezi ya huduma za kibingwa kwa mkoa wa Singida kuwa endelevu huku akizielekeza halmashauri kuandaa mpango wa utekelezaji wa zoezi hilo kwakuwa linagusa maisha ya wananchi wa hali ya chini.

  Dokta Nchimbi ametoa agizo hilo mara baada ya kufanya ziara katika Hospitali ya Iambi Wilayani Mkalama ambako zoezi la kliniki tembezi ya madaktari bingwa wa fani nane kwa Mkoa wa Singida lilikuwa linahitimishwa.

  Amesema mara baada ya kukamilika kwa halmshauri zote saba mpango wa kuanza kutoa huduma za kibingwa kwa awamu ya pili uanze mara moja kwakuwa wagonjwa wengi walionufaika ni wale webnye kipato duni na walikuwa wameshakata tama ya kupata matibabu.

  Dokta Nchimbi ametembelea wodi ya wanawake waliofanyiwa upasuaji na daktari bingwa wa wanawake, wodi ya akina baba waliofanyiwa upasuaji wa magonjwa ya tezi dume na matatizo ya njia ya mkopo pamoja, ametembelea chumba cha upasuaji wagonjwa wa macho na kumalizia wodi ya watoto waliofanyiwa upasuaji kutokana na matatizo ya mfumo wa upumuaji na midomo sungura.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akitoa mchango wa fedha kwa ajili ya upasuaji wa macho kwa mgonjwa aliyekosa fedha kiasi cha shilingi elfu thelathini kwa ajili ya huduma za kibingwa Wilayani Mkalama.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akizungumza na wananchi waliojitokeza kupata hududma za kibingwa katika hospitali ya Iambi ya Wilayani Mkalama.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akipanda Mkorosho katika shamba la Mkulima wa kijiji cha Gumanga wilayani Mkalama kama hamasa kwa wananchi wengine wapande zao hilo.
  Wananchi wa kijiji cha Nkungi na watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wakisaidiana kupanda viazi lishe katika shamba la Mkulima ili kuhamasisha kilimo hicho.  0 0

  Wito umetolewa kwa wananchi ambao wanafanya shughuli za uvuvi Mkoani Geita,kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali kwa kuwafichua wale ambao wamekuwa wakijihusisha na shughuli ya uvuvi haramu katika mialo iliyopo Mkoani Humo.

  Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga wakati wa zoezi la kuteketeza zana haramu za uvuvi kwenye Mwalo wa daladala uliopo kijiji cha Nyasalala kata ya Bukondo zilizokusanywa ndani ya miezi miwili kuanzia Januari hadi Februari mwaka huu.

  Aidha mh Kyunga amesema kuwa uhifadhi wa rasilimali zilizopo kwenye ziwa viktoria ni muhimu kwa kila mwananchi kwani endapo
  uvuvi haramu ukiachiwa madhara yake yanaweza kuwa ni makubwa kwa viumbe ambavyo vipo katika ziwa.

  “Ndugu wananchi kwa kweli uhifadhi rasilimali zilizomo katika ziwa letu hili ni muhimu ,ni muhimu kwa sasa na vile vile kwa baadae isipokuwa mimi nisisitize sisi wote hapa kwa ajili ya ustawi wetu na vizazi vijavyo tuone kwamba tuna wajibu wa kuhifadhi mazingira na matumizi bora ya ziwa letu hili,tukilivuruga kama hawa wenzetu wanavyolifuruga kwa kuendesha uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira hasara ambayo wanatuachini ni kubwa sana hawa watu kwa lugha nyingine naweza kusema ni wachawi”Alisema Kyunga
  Mkuu wa Mkoa wa GeitaMeja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga akiteketeza
  dhana haramu ambazo zimekamatwa katika oparation iliyofanyika kwenye
  mialo iliyopo Mkoani Geita lengo likiwa ni kutokomeza uvuvi haramu ambao
  umeendelea kwa kasi kwenye mialo ya Izumacheli na Mganza.
  Baadhi ya wananchi wakivuta kokolo wakipeleka eneo la kuchomea.
  Dhana haramu za uvuvi zikiwa zimekusanywa kwaajili ya kuchomwa kwenye mwalo wa dala dala uliopo kijiji cha Nyasalala kata ya Bukondo.
  Meza kuu ikongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita ,wakisiliza kwa makini
  taarifa ambayo ilikuwa ikisomwa na afisa uvuvi.


  0 0

  Kaimu Mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Amina Abdulkadir akizungumza na wanafunzi wauguzi wa Chuo Kikuu cha Wright Jimbo la Ohayo nchini Marekani walipotembelea Skuli hiyo Mbweni kubadilishana uzoefu.
  Mwanafunzi Muuguzi kutoka Chuo Kikuu cha Wright nchini Marekani Melissa Vanscoy akieleza lengo la ziara yao hapa Zanzibar wakati wanafunzi wa vyuo hivyo viwili walipokutana katika Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA Mbweni.
  Wanafunzi wauguzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA wakibadilishana mawazo na wanafunzi wenzao wa Chuo Kikuu cha Wright kutoka Jimbo la Uhayo Marekani walipowatembelea skulini kwao Mbweni.
  Wanafunzi wauguzi kutoka Chuo Kikuu cha Wright na SUZA wakiwa katika darasa la kufanyia mazoezi ya vitendo wakielekezana namna ya kumuhudumia mgonjwa alielezwa wodini.
  Picha ya pamoja ya wanafunzi wauguzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA wakiwa na baadhi ya walimu na wenzao wa Chuo Kikuu cha Wright, Jimbo la Uhayo nchini Marekani wakiwa katika kempasi ya Mbweni.

  Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Na Mathias Canal, Dar es salaam

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amewataka wenyeviti wa Mitaa iliyopo katika Manispaa hiyo kutumia vyema nafasi zao za uongozi kwa kuwatumikia wananchi kwa haki huku akiwasihi kuishauri serikali katika majukumu yake ili kuwa na maendeleo chanya katika maeneo yao sawia na kupunguza lawama za mambo yaliyopita ili kuwa na Manispaa imara yenye ukusanyaji mzuri wa mapato.

  MD Kayombo amewasihi wenyeviti hao kuwa na mahusiano mazuri baina yao na maafisa watendaji wa Mitaa kwani kufanya kazi kwa Ushirikiano na Upendo ndio silaha pekee ya kuimarisha utendaji na ufanisi wa ukusanyaji wa mapato katika Mitaa.

  MD Kayombo ameyasema hayo Wakati wa kikao cha kazi pamoja na wenyeviti wa Mitaa kilichokuwa na dhamira ya kushauriana namna bora ya kuimarisha mapato ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ili kuwa na uchumi imara, kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa hiyo Mtaa wa Kibamba CCM na kuhudhuriwa pia na Wakuu wa Idara na Vitengo.

  Mkurugenzi huyo amesema kuwa atazuru kata hadi Kata ili kubaini wapi kumwepwaya na kipi kipaombele katika maeneo husika ili kuanza nayo katika kuimarisha maendeleo ya wananchi.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo (Aliyesimama) Boniface Jacob akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo, Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo na kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo Ramadhan Kwangaya
  Wenyeviti wakisikiliza kwa makini maelekezo mbalimbali wakati wa kikao cha kazi kilichoendeshwa na Mwenyekiti wa kikao hicho Mhe Boniface Jacob ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo (Picha zote na Nassir Bakari).


  0 0

  Bila shaka kila mmoja wetu anakumbuka ahadi ya RC Makonda aliyoitoa mwaka jana ya kujenga viwanja vitatu (3) vya mpira kwa ajili ya maendeleo ya mashindano mbalimbali ya michezo ikiwemo Ndondo Cup kwani mashindano haya kwa ujumla wake yanalenga kuboresha mazingira ya michezo na kuzalisha vipaji vingi zaidi ambavyo vinabeba ajira nyingi za vijana ndani yake.

  Kimsingi RC Makonda hakuishia tu kuahidi bali alikwenda mbali zaidi na kumualika balozi wa China kushuhudia hali halisi ya viwanja vinavyotumika kwa sasa kama sehemu ushahidi wa kile alichokuwa amemueleza wakati akimshawishi.

  Ikiwa imepita miezi kadhaa tangu Balozi kukubaliana na ombi la Mkuu wa Mkoa, leo tarehe 3 Balozi huyo wa China akiwa na RC Makonda wameweka historia mpya baada ya kuweka jiwe la msingi la kuanza ujenzi wa viwanja hivyo, huku wakianza na kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000,

  Huku kikijengwa kwa viwango vya kimataifa na kampuni iliyojenga uwanja wetu wa taifa. Kuonyesha na kutambua utendaji na msukumo mkubwa wa RC Makonda katika kutimiza azma ya Rais John Pombe Magufuli ya kutatua changamoto za wanyonge, Balozi pia amemuahidi Mkuu wa Mkoa kutoa kipaumbele cha ajira vijana wote watakaoshiriki mashindano ya Ndondo Cup kwenye kampuni mbili ambao watakuwa vijana zaidi ya 20000.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa kushirikiana na Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing wakiweka jiwe la msingi kuanza ujenzi wa kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000,jana jijni Dar e Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiteta jambo na Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing jana jijini Dar es Salaam.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza katikahafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kuanza ujenzi wa kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000, jana jijni Dar e Salaam.
  Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing akizungumza katika hafla yauwekaji wa jiwe msingi kuanza ujenzi wa kiwanja cha Bandari ambacho kitagharimu Dola za Kimarekani 450,000, jana jijni Dar e Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.


  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo amewataka watumishi katika halmashauri zote nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wawe wabunifu katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

  Katika ziara yake mkoani Arusha katika halmashauri za Meru,Longido na Monduli alisema serikali imeshatoa fedha za Mfuko wa Pamoja wa Afya(Basket Fund)katika halmashauri hizo hivyo kukosekana kwa madawa na vifaa tiba sio jambo linaloweza kuvumilika.

  Alisema miradi yote ambayo fedha zimeshaletwa na serikali kuu kwenye halmashauri itekelezwe mara moja ili iweze kuwahudumia wananchi.
  Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo(kulia)akizungumza jambo alipotembelea eneo linapojengwa soko la kisasa la mifugo katika Kijiji cha Orendeke Kata ya Namanga mkoa wa Arusha,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Chongolo. 
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo akizungumza na wananchi wa Kata ya Makuyuni wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha baada ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya,serikali imetenga kiasi cha Sh 700 milioni kwaajili ya upanuzi wa Kituo cha Afya Mto wa Mbu. 
  Muuguzi katika Kituo cha Afya cha Usa River,Emiliana Sulle(kushoto) na Mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Meru mkoa wa Arusha,Bonifas Ukio(kulia)Mh.Suleiman Jaffo kumpima uzito mtoto ili kujua maendeleo yake. 
  Mkuu wa wilaya ya Longido mkoa wa Arusha,Godfrey Chongolo akizungumza wakati wa zira ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo(kulia)anayesikiliza kwa makini na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa halamshauri ya Longido,Juma Mhina.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),Mh.Suleiman Jaffo(kushoto)akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu mkoa wa Arusha,Lootha Laizer 


  0 0


  Na Woinde Shizza,Arusha

  Maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani yameanza rasmi mkoani Arusha ambapo wananchi wa mkoa wa Arusha pamoja na vitongoji vyake wamepata fursa ya kupata huduma ya kupima magonjwa mbalimbali bure

  zoezi hilo ambalo limeanza jana jijini hapa, katika uwanja wa sheikh Amri Abeid limeonekana kuwavuta wananchi wengi,kwani zaidi ya wananchi 100 wamejitokeza kupima afya zao bure katika viwanja hivyo

  Akiongea na waandishi wa habari muandaaji wa maadhimisho hayo ya wiki ya wananwake duniani kwa mkoa wa Arusha,Mkurugenzi wa Phide
  Entertaiment,Phidesia Mwakitalima alisema kuwa muamko ni mzuri na wananchi wameanza kujitokeza kwa wingi .

  Alisema kuwa pamoja ni siku ya kwanza tu lakini zaidi ya wananchi 100 wamejitokeza kupima afya zao hivyo ni jambo zuri mno

  Alisema kumekuwepo na tabia ya wananchi wengi kutokuwa na tabia ya kupima afya zao hadi pale wanapoumwa, kitu ambacho sio kizuri na amewataka wananchi kujijengea tabia ya kupima afya zao mara kwa mara

  Zoezi hili la kupima afya limeanza jana na linatarajiwa kumalizika Machi 8,mwaka huu  na huduma za kupima magonjwa mbalimbali na ushauri wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu kuchangia damu unatolew bure hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kutumia fursa hiii ili kujua afya yake .  Baadhi ya wananchi wakichukuliwa vipimo vya afya na madaktari kutoka KCMC  pamoja na Mounti meru Hospital, ikiwa ni huduma inayotolewa bure katika viwanja vya kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid katika wiki ya wanawake duniani ambayo kwa mkoa wa Arusha imeandaliwa na Phide Entertaiment
  Baadhi ya wananchi wakiwa katika mstari wakisubiri kuchukuliwa vipimo vya magonjwa mbalimbali bure yakiwemo ,Kisukari ,Presha,Kansa ,Ukimwi na mengineyo 
  Mmoja wa madaktari akiendelea kupima mara baada ya kuchukuwa vipimo vya wagonjwa ndani viwanja vya Sheikh Amri Abeid

  0 0


  0 0

  Shalom!
  Ni jumapili hii ya March 5,2017
  Bwana ametupa kumfanyia Ibada ya kumwabudu kwa Wimbo Mmoja!
  Tafadhali unakaribishwa sana!
  Kwa niaba ya waandaaji, Ninakuomba UTUOMBEE, Utusaidie kuwakaribisha wengine kupitia mitandao ya kijamii na wale unaofahamiana nao!
  Lakini pia Usisite kuwasiliana nasi kama unalo jambo lolote kupitia 0713883797!
  Ibada itaanza Saa tisa na Hakuna Kiingilio!
  KARIBU SANA

  0 0
 • 03/04/17--00:23: UJUMBE TOKA IKULU


 • 0 0


  Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Omary Mziya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mpango wa Uwezeshaji Masoko, Mtaji na Hifadhi ya Jamii katika Hafla ya ufunguzi iliyofanyika mkoani Manyara.

  Meneja wa NSSF Mkoa wa Manyara, Alexander Joseph akizungumza wakati wa Semina ya Uwezaeshaji Masomo, Mtaji na Hifadhi ya Jamii mkoani Manyara Wilaya ya Mbulu. Kushoto ni Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma na kulia ni Meneja wa Kanda wa Bodi ya Nataka na Mazao Mchanganyiko (CPB).

  Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma, akizungumza katika Semina ya Uwezaeshaji Masomo, Mtaji na Hifadhi ya Jamii iliyofanyika Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.

  Semina ikiendelea.

  Picha ya pamoja mkoani Manyara Wilaya ya Babati.

  0 0  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kamishna mstaafu Zelote Stephen amelipongeza jeshi la polisi Mkoani Rukwa kwa kufanikiwa kukamata kilo mbili za madawa ya kulevya yadhaniwayo kuwa ni heroin na lori la scania lililosheheni pombe za viroba lililokuwa likitokea Mbeya na kuingia Rukwa kwa njia za panya.

  Jeshi la polisi Mkoani Rukwa limemtia nguvuni Mtuhumiwa wa madawa ya kulevya Linus Tenda Kamwezi (50) mfanyabiashara mkazi wa kizwite katika manispaa ya sumbawanga aliyebainika kuyaficha madawa hayo katika maua yaliyokuwa yamezunguka nyumba yake.  

  “Pamoja na kwamba mna-resource ndogo lakini kazi mnayoifanya ni kubwa sana, nawapongeza kwa kitendo hiki na mwendelee kushika kamba hiyo hiyo dhidi ya vita hii ya madawa ya kulevya ambayo si ya jeshi la polisi peke yao bali ni la wananchi wote wa nchi ya Tanzania,” Zelote Stephen alieleza.


  Sambamba na hilo Kamanda wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando alifafanua kuwa watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kukutwa na lori aina ya Scania lililosheheni pombe zenye vifungashio vya nailon maarufu pombe za viroba wakitokea Mkoani Mbeya kuelekea Rukwa.

  kusoma zaidi bofya hapa
  0 0

  Hapa ni ndani ya ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga ambapo usiku wa Ijumaa Machi 3,2017 Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanya sherehe ya kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017 pamoja na kuwaaga wastaafu wa jeshi la polisi. 

  Mgeni rasmi katika sherehe hizo ambazo zimehudhuriwa na maafisa wa polisi,wakaguzi,askari wa vyeo mbalimbali na wadau wa usalama alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack. 

  Akizungumza wakati wa sherehe hizo Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro alisema Machi 3 kila mwaka huwa ni siku ya Polisi ‘Police Family Day’ ambapo pamoja na kuadhimisha siku hiyo,jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limeamua kuwafanyia sherehe ya kuwaaga wastaafu 10 wa jeshi hilo sambamba na kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017. 

  “Tumeanza sherehe hizi kwa mkuu wa mkoa kukagua gwaride katika uwanja wa Shycom lakini pia kutoa tuzo kwa askari na wadau waliofanya kazi vyema mwaka 2016 katika ulinzi na usalama wa mkoa wa Shinyanga”,alisema kamanda Muliro. 

  Naye Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack alitumia fursa hiyo kulipongeza jeshi la polisi mkoani humo kwa kuendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama na sasa vitendo vya mauaji ya vikongwe na watu wenye ualbino yamepungua kwa kiasi kikubwa. 

  Mwandishi wetu,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa sherehe hizo ametusogezea picha 65 za matukio yaliyojiri ukumbini 
  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akiwa ameshikilia kisu kabla ya kukata keki.Wa pili kutoka kulia ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo Elias Mwita 
  Ijumaa Machi 3,2016 katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga-Aliyesimama ni Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza wakati wa kufungua sherehe ya kuwaaga wastaafu wa jeshi la polisi na kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017.Kulia ni mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.Kushoto ni mke wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Mama Muliro 
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwaomba wadau wote wa ulinzi na usalama kuungana na jeshi la polisi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kuimarisha amani ya mkoa wa Shinyanga 
  Wadau wakiwa ukumbini .


  0 0

  By Staff Reporter-MAELEZO

  African Development Bank (AfDB) Board of Directors has commended President Dr. John Pombe Magufuli for his efforts in bringing economic revolution in the country.

  The AfDB board of Directors led by Madam Lekhethe Mmakgoshi met President Magufuli at Lindi state house today where they discussed various issues of mutual interest.

  Madam Lekhethe assured President Magufuli of the bank’s continued support of his efforts to revamp the economy and pledged to see to it Tanzania remains among the bank’s leading partners.

  “We will work on your request to collaborate with your government in implementing big energy projects and construction of standard gauge central railway line” Madam Lekhethe told the president.

  During the discussion, President Magufuli expressed his government’s appreciation and that of the people of United Republic of Tanzania for the support rendered by the African Development Bank which has enabled the country to implement various development projects.

  “With AfDB support, we have managed to implement various development projects including major road networks such as Iringa- Dodoma which connects with Cape Town in South Africa up to Cairo Egypt and Namtumbo-Tunduru- Masasi road” He said and added that “AfDB is Tanzania’s key partner in development”

  Dr. Magufuli praised the bank for providing affordable/soft loans enabling the government to implement many development projects but requested the later to ease access to and expediting loans delivery so that many projects can be timely executed. 

  Meanwhile, contributing to the discussion, Dr. Namajeje Weggoro, member of AfDB Board of Directors and bank’s Executive Director for East Africa revealed that Tanzania was the leading recipient of AfDB loans and reassured the President that the bank would seriously consider his requests.

  0 0

   Wanenguaji na wanamuziki wa bendi ya Fm Academia wakitumbuiza katika onyesho lao lililofanyika katika Bar ya Hawa II kimara baruti jijini Dar es Salaam
   Safu ya uimbaji ya bendi ya Fma Academia ikiongozwa na Rais wa Bendi hiyo, Nyoshi El Sadat wakiimba katika shoo yao ndani ya Bar ya Hawa II Kimara Baruti jijini Dar es Salaam
   Malu Stonch na Partcho Mwamba wakiimba katika onesho lao lililofanyika katika ukumbi wa Hawa II Kimara jijini Dar es Salaam
   Mpiga Drum akionyesha umahiri wake wa kupiga vyombo hivyo mbele ya Mashabiki wa Kimara Baruti Dar es Salaam
  Wanamuziki wa Bendi ya Fm Academia wakionyesha umahiri wao wa kutawala jukwaa mbele ya Mashabiki

older | 1 | .... | 1597 | 1598 | (Page 1599) | 1600 | 1601 | .... | 3348 | newer