Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live

BADO SIKU MOJA KUTHIBITISHA KWENDA KWENYE MKUTANO WA UWEKEZAJI ITALY

$
0
0
Chemba ya biashara, viwanda na kilimo( TCCIA) inatarajia kufanya ziara ya kibiashara nchini Italy na Uturuki ambapo Chemba inapenda kuwakaribisha wafanyabiashara walio wanachama na wasio wanachama kuungana nasi kwenye mkutano huu wa wawekezaji. Chemba inawakumbusha kwamba, imabaki siku moja kwa wafanyabiashara wa Italy kuthibitisha ushiriki wao ambapo mwisho ni tarehe 3 March 2017. Kwa 3wafanyabiashara wa Uturuki wana muda mrefu ambapo muda wa mwisho wa kuthibitisha ushiriki wao ni tarehe 30 March 2017. Ziara hii inatarajia kufanyika mwanzoni mwa mwezi May.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Ndugu Gotfrid Muganda alisema “Lengo kubwa la ziara hii ni kuwawezesha wafanyabiashara wa Tanzania kutanua wigo wa masoko na fursa za kibiashara na kubadilishana ujuzi”. 

Akizungumza juu ya ziara hiyo Mkurugenzi wa EAG Group ambao ni washauri wa biashara na masoko wa TCCIA Imani Kajula alisema “Ukuzaji wa masoko ya nje ni mkakati endelevu ambao sio tu utaongeza soko nje lakini pia kuleta urari mzuri wa biashara na hivyo kusaidia kuimarisha thamani ya shilingi”. 

 Aliwaambia wafanyabiashara ambao ni wanachama na wasio wanachama wanakaribishwa kijiandikisha ambapo mwisho kwa wanaoenda Italy ni tarehe 3 March 2017.Kwa taarifa zaid helen.mangare@eaggroup.co.tz au muganda@tccia.com.

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA KUJADILI UTEKELEZAJI WA PROGRAMU YA ISTANBUL KWA NCHI ZILIZO KWENYE KUNDI LA NCHI MASIKINI DUNIANI KWA UPANDE WA AFRIKA

$
0
0
Tanzania imeshiriki katika Mkutano ulioitishwa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya Nchi Masikini Duniani kushiriki katika Mkutano wa kujadili utekelezaji wa Programu ya Istanbul (Istanbul Programme of Action - IPOA) kwa nchi zilizo kwenye kundi la nchi masikini barani Afrika. Mkutano huo umefanyika kwenye Hoteli ya Radisson Blu, Dakar, Senegal kuanzia tarehe 28 Februari hadi 1 Machi 2017.

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo umeongozwa na Mhe. Bi. Maria Leticia Sasabo, Katibu Mkuu (Sekta ya Mawasiliano), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Wajumbe wengine waliohudhuria Mkutano huo ni Bw. Jestas A. Nyamanga, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa , Injinia Nikusubila Maiko ; Mtaalamu wa Masula ya Mkongo Mawasiliano na  Bw. Abilah Hassan Namwambe, Afisa Mambo ya Nchi za Nje, anayeshughulikia masuala ya Kundi la Nchi Masikini Duniani kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kauli mbiu ya Mkutano huo ni “Kufanikisha utekelezaji wa Programu ya Istanbul ndani ya mustakabali wa Ajenda 2030 ya Maendeleo Endelevu” (Accelerating the implementation of the Istanbul Programme of Action within the Context of the 2030 Agenda: A focus on broadband connectivity).

IPOA ilizinduliwa na Jumuiya ya Umoja wa Mataifa mwaka 2011 kwa lengo la kumaliza tatizo la umasikini kwa nchi zinazoendelea ifikapo mwaka 2020. Hadi sasa, Mpango huo unakaribia kuisha muda wake lakini tatizo la umasikini bado ni kubwa na pia idadi ya nchi zilizo kwenye kundi la nchi masikini duniani imeongezeka badala ya kupungua.
Katika Mkutano huo, Wajumbe kutoka nchi mbalimbali Duniani, wamejadili masuala ya matumizi ya Mkongo wa Mawasiliano ya Mtandao “BroadBand Connectivity”, kama nyenzo muhimu ya kuleta maendeleo.

Mkutano huo uliowakutanisha viongozi wa Mataifa mbalimbali na wadau wa maendeleo wamejadili na kuweka mikakati mipya ya namna bora ya kufanikisha na kuharakisha utekelezaji wa malengo yaliyoazimiwa kwenye IPOA. Aidha, Mkutano huo umeainisha  matokeo ya utafiti uliofanywa kuhusu matumizi ya Mkongo wa Mawasiliano katika nchi za Rwanda na Senegal.

Vilevile, matokeo ya Mkutano huo yatazingatiwa kama maoni katika Jukwaa la Ngazi ya Juu la Kisiasa, High Level Political Forum litakaloitishwa na Baraza la Umoja wa Mataifa la Uchumi na Jamii (Economic and Social Council) litakapofanya mapitio ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ifikapo Julai, 2017.

Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi chache zilizopiga hatua kubwa sana katika kuwaletea wananchi wake Maendeleo hasa katika sekta ya Mawasiliano. Ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Huduma za kifedha, na za kibenki kwa kutumia mitandao na simu za mkononi na gharama ndogo za huduma za simu na kimtandao ni baadhi tu ya maeneo ambayo Tanzania inaongoza kwa kufanya vizuri.

Mhe. Mama Maria Leticia Sasabo, Katibu Mkuu (Sekta ya Mawasiliano), Wizara akifuatiwa na Bw. Jestas A. Nyamanga Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wajumbe kutoka nchi nyingine wakifuatilia mada mbalimbali katika Mkutano huo.
Bw. Abilah Hassan Namwambe, Afisa Mambo ya Nchi za Nje, anayeshughulikia masuala ya Kundi la Nchi Masikini Duniani kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akiwa katika maandalizi ya Mkutano huo.
Injinia Nikusubila Maiko Mtaalamu wa Masuala ya Mkongo wa Mawasiliano akiwasilisha mada katika Mkutano huo.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MACHI 3,2017

MICHUZI TV: Filamu ya Maisha ni Siasa yawekwa mtandaoni kuwapa uhuru watazamaji

$
0
0
Filamu ya Maisha ni Siasa ni sinema ya kitanzania inayoonyesha pilikapilika za wanasiasa katika chaguzi za Afrika. Imechezwa na Paul Mashauri, Loue Kifanya, Violet Mushi, Bahati Chando, Lilian Mwasha, Godwin Gondwe, Hudson Kamoga na wengine wengi. Imeandikwa na Paul Mashauri na Jacqueline Mgumia na kuandaliwa na Kileleni Productions kwa ushirikiano na Mashauri Studios na the 7th Elements. Waweza kuangalia filamu yote hapa chini.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA AKUTANA NA BALOZI WA SWEDEN NA COMORO NCHINI,LEO IKULU JIJINI DAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt,ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha kwa Hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais).
 
 Picha ya pamoja 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Comoro hapa nchini Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoui, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha kwa Hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais)
Picha ya pamoja

ZUIO LA USAFIRISHAJI WA MAKINIKIA (CONCENTRATES) NA MAWE YENYE MADINI (ORE) KWENDA NJE YA NCHI

DK. SHEIN AZUNGUMZA NA MABALOZI WALIOTEULIWA KUIWAKILISHA TANZANIA NCHI ZA NJE

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Dkt. Pindi Kichana anayeiwakilisha Tanzania Nchini Kenya akiwaongoza Mabalozi wengine walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,walipofika Ikulu Mjini Unguja leo kumuaga Rais.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mabalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioteuliwa kuiwakilisha Tanzania Nchi za Nje hivi karibuni wakiongozwa na Balozi Dkt. Pindi Kichana(wa pili kulia) anayeiwakilisha Tanzania Nchini Kenya walipofika Ikulu Mjini Unguja leo kumuaga Rais.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Mabalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioteuliwa kiwakilisha Tanzania Nchi za Nje hivi karibuni wakiongozwa na Balozi Dkt. Pindi Kichana(wa pili kulia) anayeiwakilisha Tanzania Nchini Kenya walipofika Ikulu Mjini Unguja leo kumuaga Rais. Picha na Ikulu, Zanzibar.

WENYE VISIMA VYA MAJI ILALA WAPEWA TAHADHALI

$
0
0
Meneja wa DAWASCO Mkoa wa Ilala, Ndugu Christian Kaoneka
akiongea na waandishi wa habari juu  Mpango mahususi Kwa
watumiaji wa huduma ya Maji ya visima kujiunga
rasmi na mfumo wa Majisafi kutoka DAWASCO. 
Wamiliki na watumiaji wa Maji ya visima hususani wakazi wa ilala jijini Dar es salaam wametakiwa kujitokeza ili kuunganishiwa huduma ya Majisafi yanayotolewa na shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) ili kuondokana na hujuma inayofanywa na wamiliki wachache wa visima binafsi vya Maji.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Dawasco Mkoa wa Ilala, Christian Kaoneka alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mpango wa kuunganishia wamiliki wa visima katika mfumo rasmi wa Dawasco.

Akielezea juu ya mpango huo, Bw.Kaoneka alisema kwa kipindi cha miaka ya nyuma kiasi cha maji kilichokuwa kinazalishwa hakikuweza kukidhi mahitaji ya wananchi wote hususani wakazi wa ilala, hivyo kupelekea wengi kuchimba visima vya maji binafsi.

“Tulikuwa na changamoto ya utoshelezaji wa Maji kwa maeneo mengi ya mji. Uzalishaji Maji haukuwa mkubwa hivyo kwa wananchi wengi iliwalazimu kuchimba visima vyao binafsi ili wapate huduma hiyo”alisema meneja huyo.

Alitolea mfano maeneo mengi kwa mkoa wa Ilala yenye huduma ya Visima kwa watu binafsi ni maeneo ya Kariakoo, Upanga na katikati ya Mji.

“Kwa sasa uzalishaji wa Maji umeongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka kiasi cha lita za ujazo milioni 182 hadi lita za ujazo milioni 270 kwa siku, hivyo kupelekea maeneo mengi ya jiji la Dar es salaam kuwa na utoshelezi mwingi wa Maji.

“Hivyo tutoe rai kwa wamiliki wote wa visima katikati ya mji kuja ofisi za Dawasco ili kujiunga rasmi na mtandao wa Majisafi. Tumekuja kugundua wengi wa wamiliki wa visima hufanya maunganisho ya Maji bila kufuata taratibu husika na mwisho hudai yale maji ni ya kisima wakati Dawasco tukishayapima tunagundua ni ya Dawasco” aliongeza Kaoneka.

Bw.Kaoneka alitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za wananchi wanaohujumu miundombinu hiyo kwa kupiga namba 0769 988 677 au 0743 451 879.

MRADI WA KUKWAWEZESHA WANAWAKE WAJASIRIAMALI UNAOFADHILIWA NA TAASISI YA MANJANO WAINGIA MBEYA

$
0
0
Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation utaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Mbeya kuanzia Jumatatu, tarehe 8 March 2017 kwenye ukumbi wa SIDO Mkoani Mbeya. Mafunzo hayo yatatolewa kwa jumla ya wanawake watakaochaguliwa 30 kutoka mkoani Mbeya. 

Baada ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha wanawake wa Mkoa wa Mbeya wanafikia malengo yao waliojiwekea katika kujikita kwenye kujiajiri. Wanawake wakazi wa Mkoa wa Mbeya waliotuma maombi kupitia tovuti ya Manjano Foundation na wanaopenda kunufaika na mradi huo wanaombwa kujitokeza kwa ajili ya usaili siku ya Jumatatu tarehe 6 Machi 2017 kuanzia saa tatu (9:00AM) asubuhi kwenye ukumbi wa wa SIDO Mkoani Mbeya.

Mafunzo yana lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. 

Awamu ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada yanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation itawaunganisha na taasisi za fedha zinazotoa mikopo bila riba waweze kupata mtaji wa kununua bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.
Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 658 741711 au +255 712 378516.

TAWI LA MPIRA PESA KUANZA KUFANYA USAILI WA WANACHAMA JUMAPILI

$
0
0
Mwenyekiti wa Tawi la mpira pesa Ustadhi Masoud Hassan akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kufanya usaili wa wanachama wa tawi hilo kuanzia Machi 05.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Tawi la mpira pesa limetangaza kuanza kufanya usaili wa wanachama wa tawi hilo kuanzia Jumapili Machi 5 ili  kuhakiki wanachama na kuwapunguza hadi 250 kwa mujibu wa kanuni za klabu ya Simba.

Tawi la mpira pesa kwa sasa lina wanachama zaidi ya 750 ambao ni kinyume na kanuni za klabu hiyo ambayo inataka wanachama katika kila tawi kuwa 250.

Akizungumza na waadishi wa habari Mwenyekit wa tawi hilo Ustadhi Masoud Hassan  alisema  lengo la kufanya usaili huo ni kupunguza idadi ya wanachama ambao wengi wao walikuwa wakorofi na waliokosa nidhamu. 

"Tutataanza kufanya usaili wa kuhakiki wanachama keshokutwa Jumapili utakao endelea kwa siku sita ili kuendana na kanuni za klabu yetu ambayo inataka wanachama katika kila tawi kuwa 250" alisema Ustadh.

Masudi aliendelea kufafanua kwa kusema wanachama ambao hawatapata nafasi ya kusailiwa katika tawi hilo wataruhusiwa kwenda kufungua tawi jingine ambalo litakuwa na uongozi wake.

Wakati huo huo Ustadhi alisema hafikirii kugombea tena Uwenyekiti wa tawi hilo kwakua amelitumikia kwa muda mrefu huku akiwa na vyeo vingi.

"Sina uhakika kama nitagombea tena kwakua kwa sasa nina majukumu mengi ndani ya Simba" alisema Ustadhi.

Puma Energy yazindua kampeni ya Usalama barabarani.

$
0
0

KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania leo wamezindua kampeni maalumu ya Usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi, ikiwa ni mkakati wa kampuni hiyo kueneza elimu hiyo muhimu kuanzia ngazi ya chini.

Ikiwa ni muendelezo tu tangu ianzishwe rasmi mwaka 2013, hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga, maofisa wa serikali pamoja na walimu.

Utolewaji wa elimu kwa wanafunzi kuhusu usalama barabarani pamoja na matumizi ya sanaa hususani mashindano ya kuchora dhana tofauti zinazohusiana na mada kuu ya usalama barabarani vilitajwa kuwa ni ni miongoni mwa agenda muhimu katika kampeni hiyo.

“Lengo la kuhusisha wanafunzi katika kampeni hii ni kutokana na imani tuliyonayo kwamba elimu kuhusu usalama barabarani inatakiwa kujengwa miongoni mwetu tangu tukiwa katika umri mdogo kabisa. Kwa kufanya hivyo tutakua tukiwa na elimu ya kutosha kuhusu suala hili,’’ alibainisha Meneja Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw Philippe Corsaletti.

Kwa mujibu wa Bw Corsaletti tangu kuanzishwa kwa kampeni hiyo mwaka 2013, jumla ya shule 33 zenye jumla ya wanafunzi 39,000 wamefundishwa mafunzo hayo hapa nchini huku ripoti ya ukaguzi kuhusu elimu hiyo ikionyesha kupungua kwa ajali maeneo ya shule hizo.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga (Kulia) akikabidhi picha yenye mahudhui ya usalama barabarani iliyochorwa na mwanafunzi wa shule ya Msingi Bunge ya jijini Dar es Salaam, Veronica Innocent (wa kwanza kushoto) kwa mwalimu wake Bi Amina Kayeke wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kampeni maalumu ya Usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi inayoendeshwa na kampuni ya Puma Energy .Mwanafunzi huyo aliibuka mshindi wa kwanza kitaifa kwenye shindano la kuchora picha zenye maudhui ya usalama barabarani katika kampeni hiyo kwa mwaka jana. Wanaoshuhudia ni pamoja na Meneja Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw Philippe Corsaletti (wa pili kulia ) na Naibu Mkurugenzi wa taasisi inayoshughulikia masuala ya usalama barabarani ya Amend, Bw Tom Bishop.
Meneja Mkuu wa kampuni ya Puma Energy hapa nchini Bw Philippe Corsaletti (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na na mwanafunzi wa shule ya Msingi Bunge ya jijini Dar es Salaam, Veronica Innocent alieibuka mshindi wa kwanza kitaifa kwenye shindano la kuchora picha zenye maudhui ya usalama barabarani katika kampeni ya Usalama barabarani inayoendeshwa na kampuni hiyo.
Veronica Innocent alieibuka mshindi wa kwanza kitaifa kwenye shindano la kuchora picha zenye maudhui ya usalama barabarani katika kampeni ya Usalama barabarani inayoendeshwa na kampuni ya Puma Energy akizungumza mbele Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga, Uongozi wa Puma Energy, maofisa wa serikali pamoja na walimu kutoka shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam waliohudhuria warsha hiyo.

MAJALIWA AONGOZA KIKAO CHA KAZI CHA MAWAZIRI MJINI DODOMA

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kikao cha Kazi cha Mawaziri alichokiitisha kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Machi 3, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mkutano wa Tano wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar wahitimishwa

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itafungua tena kazi za uchimbaji  mchanga kuanzia Jumatatu ya Tarehe 6 Machi 2017 ikilazimika kuchukuwa uamuzi mgumu wa kusimamia moja kwa moja uchimbaji huo badala ya kuwaachia Wananchi.

Alisema maamuzi hayo ya Serikali yatakwenda sambamba na utolewaji wa bei elekezi ya mchanga ili kujaribu kuzuia uharibifu wa mazingira uliokwishaathiri maeneo mengi yaliyokwishachimbwa mchanga pamoja naulanguzi wa kupita kiasi kwa wauzaji wa rasilmali hiyo.

Akitoa Hoja ya kuahirisha Mkutano wa Tano wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar huko Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Wizara ya Kilimo itaandaa  zamu za kuchimba mchanga ili kupunguza msongamano wa gari zitakazokwenda katika maeneo ya Mchanga.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Akitoa Hoja ya kuahirisha Mkutano wa Tano wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar huko Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Alisema zamu hizo zitawapa fursa ya siku Tatu  kwa Wiki Wananchi wa kawaida kupata rasilmali hiyo ya Mchanga na Siku Mbili kwa Wiki zitazingatiwa kwa Makampuni na Taasisi  za Serikali  zilizopata vibali vya Ujenzi wakati Jumamosi na Jumapili zitakuwa siku za mapumziko.

Balozi Seif alisema utafiti unaendelea kufanywa na Kamati ya Wataalamu kwa kushirikiana na ile ya Mawaziri inayoshughulikia suala mchanga kujua kiwango cha mchanga kiliopo kwenye eneo la Kiwanda cha Sukari Pangatupu, Kichwele na maeneo mengi ili kubaini wingi wake  na endapo utafaa kwa matumizi ya ujenzi.
Alisema Zanzibar si nchi ya kwanza kuwa na upungufu wa mchanga ambapo ipo mifano ya uhaba wa rasilmali hiyo iliyokwishajitokeza katika baadhi ya nchi duniani kama vile Malaysia, Singapore, Phillipines na Tuvalu.

Balozi Seif alieleza kwamba upo ushahidi wa wazi uliothibitisha kuzama kwa Visiwa vodogo vidogo Vitano Nchini Phillipines kufuatia wimbi kubwa la uchimbaji wa mchanga kiholela pembezoni mwa fukwe zilizokuwa zimevizunguuka Visiwa hivyo.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA MWAKILISHI WA BENKI YA DUNIA NCHINI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba hii leo amekutana na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird. 

 Katika mazungumzo yao Mwakilishi huyo wa Benki ya Dunia ameahidi kuisaidia Tanzania katika Sekta ya Mazingira ikiwa ni pamoja na uhifadhi wa mifumo ya ikolojia na bioanuai, pamoja na kulijengea uwezo Baraza laTaifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Kushoto) akiongea na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird. Mazungumzo hayo yamefanyika hii leo Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Kushoto) akiongea na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird. Mazungumzo hayo yamefanyika hii leo Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora.

U.S. GOVERNMENT SPONSORS ANTI-CORRUPTION TRAINING IN TANZANIA

$
0
0
Dar es Salaam, TANZANIA. From February 27 to March 3, U.S. trainers with expertise in rule of law conducted anti-corruption training for 15 Tanzanian investigators and prosecutors from the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) and 12 prosecutors from the Office of the Director of Public Prosecutions (DPP).

Entitled, “A Team Approach - The Investigation and Prosecution of Corruption Cases,” the U.S. Embassy’s Office of Overseas Prosecutorial Development, Assistance and Training (OPDAT) organized the training. Both the PCCB and the DPP contributed to the training design.

Through interactive lectures, demonstrations, and trainee participation, the event achieved two major goals. It fostered a closer working relationship between investigators and prosecutors, and it built the PCCB’s investigative and prosecutorial skills to ensure that prosecutions are conducted professionally, efficiently and fairly. To achieve these goals, the training focused on a case-study involving corruption in connection with government purchase orders.

A Tanzanian prosecutor who participated in the training told the trainers, "We have learned so much working with you as a team, especially all the interactive work. We are looking forward to using all of this in our jobs."

Specific topics addressed included understanding the complementary roles of the prosecutor and investigator in a corruption investigation; prosecutor/investigator relations; investigative techniques; evidence gathering; charging strategies; and basic trial advocacy skills.  The training culminated on March 3 with a mock trial based on a factual scenario, allowing the trainees to experience first-hand how to present gathered evidence effectively in court using the trial techniques learned in training. 

Speaking at the conclusion of the training, Chargé d’Affaires of the U.S. Embassy to Tanzania Virginia Blaser commended attendees’ dedication to Tanzania’s anti-corruption efforts, and their hard work throughout the training program. “I wish you the best as you put this training, and your newly-acquired skills, to good use as you fight corruption through strong, efficient and fair investigations and prosecutions,” she told them.
Participants of the training "A Team Approach - The Investigation and Prosecution of Corruption Cases," which was organized by the U.S. Embassy's Office of Overseas Prosecutorial Development, Assistance and Training (OPDAT) and took place February 27 to March 3 in Dar es Salaam.
Chargé d’Affaires of the U.S. Embassy to Tanzania Virginia Blaser (2nd left) presenting a certificate to participant Ms. Mbumi Kisiku (left) after she completed a one-week anti-corruption training organized by the U.S. Embassy’s Office of Overseas Prosecutorial Development, Assistance and Training (OPDAT).
Chargé d’Affaires of the U.S. Embassy to Tanzania Virginia Blaser (2nd left) presents a certificate to Mr Saleh Mbwana (left), one of the participants, after he completed a one-week anti-corruption training organized by the U.S. Embassy’s Office of Overseas Prosecutorial Development, Assistance and Training (OPDAT).

TRA na Bodi ya Mapato Zanzibar wasaini makubaliano ya mafunzo juu ya namna ya ukusanyaji wa mapato

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) wamesaini makubaliano ya mafunzo yatakayowaongezea uwezo na namna bora ya ukusanyaji  mapato (kodi) ili kuweza kufikia malengo.
Akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutiliana saini makubaliano hayo, Kamishna wa TRA Tanzania,  Alphayo Kidata amesema kuwa mafunzo hayo yatakayokuwa na kozi 64 yataendeshwa na chuo cha Kodi Tanzania  (ITA) kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa katika kozi hizo, ambazo zinatarajiwa kuchukua miezi mitatu (Machi hadi Juni), mwaka huu, watumishi wote wa ZRB wanatarajiwa kupewa mafunzo hayo ambapo mpaka sasa kozi ya kwanza imeishaanza kufundishwa chuoni hapo.
“Tangu serikali ya awamu ya tano imeingia madarakani imekuwa ikiweka mikakakti ya kukusanya kodi  kwa wingi ili kuinua uchumi na kuifanya miundombinu ya nchi kuwa mizuri kwa hiyo tunaimani mafunzo hayo yatatuwezesha kufikia malengo” alisema Kidata.
Naye Kamishna wa Mapato Zanzibar, alisema wanatarajia mafunzo hayo yataiwezesha Zanzibar kupata matokeo mazuri katika ukusanyaji wa kodi Zanzibar na pia kuwajengea uwezo mzuri watendaji wake yatakayoleta mabadiliko katika kukuza uchumi.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa wakati wa kutiliana saini ya makubaliano ya pamoja ya mafunzo juu ya namna ya kuongeza uwezo wa ukusanyaji wa  kodi  baina ya TRA na ZRB jijini Dar es Salaam leo.  
Kamishna wa bodi ya mapato Zanzibar Bw.  Amour Bakari akizungumzia mafanikio wanayotarajiwa kuyapata baada ya kusaini makubaliano ya mafunzo juu ya namna ya kuongeza uwezo wa ukusanyaji kodi kwa watumishi wote wa Zanzibar katikati ni Kamishna Mkuu wa TRA Tanzania na kushoto ni mkuu wa chuo cha Kodi (ITA), Prof. Isaya Jairo leo kwenye ukumbi wa Makao makuu ya TRA jijini Dar.

MWANA FA AWEKA WAZI DUME SURUALI ILIVYOMSUMBUA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Msanii wa muziki wa bongo fleva anayefanya vizuri katika soko la muziki na wimbo wake wa Dume Suruali Dume kaptula Khamis Mwijuma ‘Mwana FA’ amesema ilimchukua muda sana kupata jina la wimbo huo.

Mwana FA amesema hayo alipokuwa akizungumza na globu ya jamii juu ya namna alivyoweza kurekodi wimbo huo katika mazingira magumu ya kurudia rudia.

“hii nyimbo niliifanya mara ya kwanza lakini nikaiona haipo sawa ndipo nikaamua kumshirikisha mwanadada Vanessa Mdee kutokana na staili yake ya uimbaji” amesema FA.

Amesema ni mara nyingi sana amekuwa akirudi studio kwa ajili ya kurekebisha mstari mmoja wa shairi kuhakikisha kuwa   anapata wimbo wenye ubora.

FA amemaliza kwa kusema kuwa ni vyema msanii ukatambua mashabiki wako nini wanataka kuliko kwenda kwenda studio kila siku kuleta mziki wa bigijii

MICHUZI TV: IGP MANGU AKEMEA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WANANCHI WA LINDI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi (Wakwanza kushoto), Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa pamoja na Mbunge mteule Mama Salma Kikwete.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi kuhusu masula mbalimbali ya mkoa huo pamoja na Taifa kwa ujumla.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuwaaga wananchi wa Lindi waliofika katika uwanja wa Ilulu kumsikiliza mara baada ya kumaliza kuwahutubia uwanjani hapo. 

PICHA NA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI ATOA MIEZI MINNE MRADI WA MAJI WA NG’APA MKOANI LINDI UKAMILIKE PIA AKUTANA NA BODI YA WAKURUGENZI WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB) KATIKA IKULU NDOGO YA LINDI

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge kuhakikisha kuwa Mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo mkoani Lindi unakamilika ndani ya miezi mine na si vinginevyo.




 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge kuhakikisha kuwa Mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo mkoani Lindi unakamilika ndani ya miezi mine na si vinginevyo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasalimia wananchi waliokusanyika karibu na mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo Mkoani Lindi. Pia Mama Salma Kikwete amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumteua kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sehemu ya Mradi wa Maji wa Ng’apa mkoani Lindi ambao Rais Dkt. Magufuli ametoa miezi minne kwa mkandarasi anayejenga mradi huo ili uweze kukamilika haraka.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live




Latest Images