Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1595 | 1596 | (Page 1597) | 1598 | 1599 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ARKADIA Ltd. Dr. Ezio Copat walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwake mjini Dodoma .
  Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akimsikiliza Dr. Copat walipokutana kwa mazungumzo mjini Dodoma 
  Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akifafanua jambo wakati wa mazungumzo 
  Mazungumzo yakiendelea 

  0 0

  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ya kutaka asikamatwe hadi kesi yake ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda itakapomalizika.

  Maombi hayo yalitupwa kwa sababu kifungu cha sheria kilichotumika kuyafungua si sahihi na kwamba hutumika pale ambapo sheria ziko kimya.

  Uamuzi huo wa majaji umefikiwa kutokana na pingamizi la jamhuri lililowasilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu Gabriel Malata kuiomba kuyatupilia mbali maombi hayo kwani hayana msingi kisheria.

  Katika hatua nyingine, mwanahabari nguli nchini Jenerali Ulimwengu, ameungana na jopo la mawakili Tundu Lissu, Peter Kibatala na John Malya katika kumtetea Mbowe.

  Mbowe amefungua kesi hiyo ya kikatiba namba 1, ya mwaka 2017 dhidi ya wadaiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Kesi hiyo itasikilizwa tena Machi 8, mwaka huu.
  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akitafakari jambo ndani ya Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam akiwa na wakili wake Jenarali Ulimwengu (kati),na Meya wa Ubungo Boniface Jacob .


  0 0

  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

  Baada ya kutoka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu Tanzana Bara uliopigwa jana katika Uwanja wa Taifa hatimaye uongozi wa klabu hiyo umekata rufaa kwa kadi ya njano aliyopewa mshambuliaji wao Obrey Chirwa kwenye kamati ya masaa 72.

  Kadi hiyo aliyopewa Chirwa katika dakika ya 45 ilikuwa ni baada ya kufunga goli linaloleta utata mpaka muda huu ambapo mwamuzi Ahmada Simba alilikataa na kumlima kadi na baadae kidogo kufanya kosa la utovu wa nidhamu na kupatiwa kadi nyekundu.

  Uongozi wa Yanga umekataa rufaa hiyo kwenye kamati ya masaa 72 kuhusiana na kadi aliyopatiwa mshambuliaji wao wa kimataifa Chirwa aliyopatiwa katila dakika ya 45 baada ya mwamuzi kulikataa goli alilofunga.

  Baadhi ya viongozi wa Yanga waliokuwapo uwanjani walionesha kusikitishwa na tukio la kukataliwa kwa goli ma Chirwa kupewa kadi ya njano na kuamua kukataa rufaa haraka sana.

  Viongozi hao, walienda mpaka vyumba vya kubadilishia waamuzi na kumpatia kamisaa wa mchezo huo rufaa hiyo ili iweze kusikilizwa ndani ya masaa 72.

  Kwa sasa katika kikosi cha Yanga, Chirwa amekuwa tegemeo kubwa sana akiziba pengo la Mzimbabwe Donald Ngoma aliye majeruhi ya goti kwa takribani wiki tatu sasa.
  Mshambulaji wa Kimataifa kutoka Zambia Obrey Chirwa akitoka uwanjani baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting.

  0 0

   Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (kulia) akimkaribisha Naibu Kamishna Mkuu wa Shirika la Huduma za Forodha la Korea (Korea Customs Service-KCS) Dk. Jong-Yeul Kim alipotembelea TRA tarehe 1 Machi 2017 ili kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya taasisi hizo. Baadhi ya mambo waliyojadili ni pamoja na  utekelezaji wa mradi wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window Systems) kufuatia makubaliano ya ushirikiano  yaliyofanyika baina ya taasisi hizo mbili.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (kulia) akimuelezea jambo Naibu Kamishna Mkuu wa Shirika la Huduma za Forodha la Korea (Korea Customs Service - KCS) Dk. Jong-Yeul Kim alipotembelea TRA tarehe 1 Machi 2017 ili kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Taasisi hizo mbili.
    Naibu Kamishna Mkuu wa Shirika la Huduma za Forodha la Korea (Korea Customs Service-KCS) Dk. Jong-Yeul Kim  (aliyeshika picha kushoto) akifurahia moja ya zawadi aliyokabidhiwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (kulia) mara baada ya kumaliza mkutano wa pamoja  uliofanyika katika ofisi ya TRA Makao Makuu wakati wa ziara ya Dk. Kim nchini Tanzania.
  Timu ya  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) (kulia) ikiongozwa na Kamishna Mkuu Bw. Alphayo Kidata   pamoja na Timu ya Shirika la Huduma za Forodha la Korea (Korea Customs Service-KCS)  ikiongozwa na  Naibu Kamishna Mkuu Dk. Jong-Yeul Kim walipokutana katika ofisi ya TRA Makao Makuu ili kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili.
   Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (wa nne kulia)  pamoja na Naibu Kamishna Mkuu wa Shirika la Huduma za Forodha la Korea (Korea Customs Service-KCS) Dk. Jong-Yeul Kim (wa tano kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao cha pamoja kilichowakilisha taasisi hizo mbili. 

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Kikosi cha Simba kimeeendellea na mazoezi katika viwanja vya Chuo cha Polisi Kilwa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa l.igi kuu dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Jumamosi kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.

  Simba ambayo ipo kambini toka jana jioni, inajifua zaidi ili kuweza kutoka na ushindi kwenye mchezo huo ambapo wapo katika mbio za kuutafuta ubingwa wa ligi kuu Vodacom msimu wa 2016/2017.

  Wanamsimbazi hao ambapo katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Yanga waliweza kuvuna alama tatu na kufikisha alama 54 wakiwa wamejikwea kileleni wakifuatiwa na mahasimu wao wenye alama 52 baada ya ushindi walioupata kwenye mchezo wao wa kiporo dhidi ya Ruvu Shooting.

  Kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja ameweka wazi kuwa bado hawawezi kusema wameshakuwa mabingwa kwabni ligi ya msimu huu ni ngumu sana na haitabiriki kwani kila timu imejizatiti kutoka na ushindi.

  Mayanja amesema kuwa, kwa sasa kila kitu ni kuangalia namna gani wanashinda kwenye michezo iliyobaki ili kujihakikishia wanatoka na ubingwa msimu huu na zaidi kila mchezaji anajua nini wanakitaka ambapo ni ubingwa tu. 

  Kwa sasa viongozi wa Simba wanataka kuhakikisha wanachukua ubingwa ligi msimu huu baada ya kukaa miaka minne bila kuchukua kombe na kushindwa kushiriki michuano ya kimataifa.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wamenunua mtambo mpya wa kisasa unaojulikana kama ‘Energy Dispersive X-Ray Fluorescence Spectrometer’ (EDXRF) kwa ajili ya kurahisisha uchunguzi wa kimaabara.

  Mtambo huo uliogharimu kiasi cha shilingi 101,785,200 umesimikwa katika Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Nyanda za Juu Kusini mkoani Mbeya kuanzia Februari 21 hadi 23 mwaka huu.

  Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali. Prof. Samwel Manyele alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matumizi ya mtambo huo.

  Prof. Manyele amesema kuwa mtambo huo umesimikwa mkoani mbeya ikiwa ni moja ya hatua za kuboresha maabara za Kanda zilizopo Arusha, Dodoma, Mbeya, Mtwara na Mwanza, kusogeza shughuli za uchunguzi karibu na wananchi ili kupunguza gharama za kusafirisha sampuli kuja mkoani Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi.

  “Kuwepo kwa mtambo huo ni suluhisho kwa Serikali, Wizara, Viwanda, Mashirika, Wachimbaji wa madini, wajasiriamali na wananchi kwa ujumla ambao walikuwa wanahitaji kufahamu ubora na usalama wa bidhaa mbalimbali za viwandani na mashambani, kutambua uwepo wa madini ya thamani kwenye udongo na bidhaa za vito pamoja na sampuli zinazohusiana na usalama wa afya na mazingira,”alisema Prof. Manyele.
  Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu kuanza kazi kwa mtambo mpya wa kisasa wa Energy Dispersive X Ray Fluorescence (EDXRF) kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa kimaabara.Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma za Ubora wa Bidhaa, Bw. Daniel Ndiyo, Mkurugenzi Idara ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali Nchini, Bw. Sabanitho Mtega kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara Bw. George Kasinga pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba,Bw. David Elias.
  Baadhi ya watumishi wa Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kuhusu kuanza kazi kwa mtambo mpya wa kisasa wa Energy Dispersive X Ray Fluorescence (EDXRF) kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa kimaabara. Mtambo huo umefungwa kwenye Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mkoani Mbeya.
  Mtambo wa Energy Dispersive X – Ray Fluorescence (EDXRF) kushoto unaotumika kupima sampuli mbalimbali zenye asili ya yabisi na vimiminika kama vile vyakula, bidhaa za mafuta, maji, simenti, makaa ya mawe, bidhaa za chuma ili kutambua kiwango cha madini kilichomo ndani ya sampuli hizo. Mtambo huo umefungwa kwenye Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mkoani Mbeya.


  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Msanii wa Bongo Movie , Vicent Kigosi 'Ray' kesho anatarajia kuzindua filamu yake mpya,itakayojulikana kwa jina la Gate Keeper katika ukumbi wa Sinema wa Quality Centre.

  Ray ambaye hajatoa filamu kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja,amesema kuwa filamu hiyo ni moja ya akzi zenye ubora wa hali ya juu katika soko la filamu ambazo azijawahi kutokea tangu aanze kazi hiyo.

  ametaja kuwa watu ambao ameshirikiana nao katika filamu hiyo ni Kajala Masanja, Single Mtambalike na Nicole Franklin .

  Amesema kuwa filamu hiyo imeandaliwa na Rj Production na kusimamiwa na kampuni ya Steps Entertiment,aidha ametaja kuwa kingilio katika uzinduzi huo ni shilingi 10000 kwakila mtu atakaye fika katika ukumbi huo wa Suncrest Cineplex Cinema.


  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia) akipokea  Taarifa ya Kamati inayoshughulikia Mgogoro wa  Loliondo Kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati  amabye ni  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bwana Mrisho Gambo, Wanao shuhudia  Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi  Mkuu  Mamlaka ya Uhifadhi Tanzania  Martine  Loiboki, Mkuu wa Wilaya ya Loliondo Rashid Taka, Mkurugenzi Mkuu Tanapa Allan Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Wanyama Pori  Prof Alexander  Songorwa, Mkurugenzi Mkuu wa Thomson Safari s John Bearcroft , Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo Milian Ole Nasha (MB) ,Mwenyekiti wa CCM Arusha  Lekule Laiser  , Mkurugenzi wa Baraza la Wafugaji Wanawake Bibi Maanda Ngoitika , Kikao hicho cha Kukabidhi Tarifa kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma leo tarehe 2 Februari 2017.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akionyesha Kitabu cha Taarifa ya Kamati inayoshughulikia Mgogoro wa  Loliondo Kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati  amabye ni  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bwana Mrisho Gambo, Wanao shuhudia  Kutoka kushoto Kaimu Mkurugenzi  Mkuu  Mamlaka ya Uhifadhi Tanzania  Martine  Loiboki, Mkuu wa Wilaya ya Loliondo Rashid Taka, Mkurugenzi Mkuu Tanapa Allan Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Wanyama Pori  Prof Alexander  Songorwa, Mkurugenzi Mkuu wa Thomson Safari s John Bearcroft , Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo Milian Ole Nasha (MB), Mwenyekiti wa CCM Arusha  Lekule Laiser  , Mkurugenzi wa Baraza la Wafugaji Wanawake Bibi Maanda Ngoitika, Kikao hicho cha Kukabidhi Tarifa kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma leo tarehe 2 Februari 2017 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akisikiliza Tarifa ya Mgogoro  wa  Loliondo  kutoka kwa Mwenyekiti wa kamati na Mkuu wa Mkoa  wa Arusha , Bwana Mrisho Gambo.
   Waziri Mkuu Kassi Majaliwa akiwa katika kikao cha Wanakamati wanaoshugulikia Mgogoro wa Loliondo Kikao hicho kimefanyika katika  Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma
  (Picha na PMO)

  0 0

  Na Rhoda Ezekiel -Globu ya Jamii,Kigoma,

  VIONGOZI wa Mikoa na Wilaya wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano katika kuibua fursa za uwekezaji na kuibua miradi itakayo wawezesha Wananchi kunufaika na ukuaji Wa uchumi katika kuelekea kuwa Nchi ya viwanda ilikuwawezesha Wananchi kuepukana na umasikini .

  Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora , Agrey Mwanry ambae pia ni mwenyekiti wa Baraza la uwezeshaji kanda ya ziwa Mkoani kigoma katika  Semina ya mafunzo ya uwezeshaji kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya za Kigoma, Kagera , Tabora na Katavi ya kanda ya Mgharibi ambayo iliandaliwa na Baraza la uwezeshaji Taifa iliyo lenga kuwawezesha viongozi kuwajengea uwezo wananchi katika kukuza uchumi.

  Mkuu huyo alisema ilikuwawezesha Wananchi kunufaika na uchumi ni lazima Viongozi kushirikiana katika kuibua Fursa za uwekezaji na kuboresha  Miundombinu itakayo saidia Wananchi kunufaika na uchumi katika kufanya  shughuri zao katika mazingira mazuri na yanayo wavutia katika kuboresha uthamani wa bidhaa Wanazo zalisha.

  Mwanry alisema Viongozi kazi yao kubwa ni kuonyesha njia ya maendeleo kwa Wananchi juu ya ukuaji wa kiuchumi, fursa zinazotakiwa kuibuliwa ni pamoja na kila halmashauri kutenga bajeti ya maendeleo ya wananchi kwa Asilimia tano ilikuweza kuwawezesha Wananchi kuepukana na umasikini na kunufaika na Ukiaji wa uchumi.


  0 0


  Na Bakari Issa Madjeshi,Globu ya Jamii

  Shirika la Afya na Elimu ya Tiba-TAHMEF linatarajia kuendelea na Kampeni yake ya kuboresha Afya ya Wanawake na Watoto ili kuboresha Afya Bora na Ustawi.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Shirika hilo,Juliana Busasi amesema TAHMEF inatarajia kufanya shughuli maalum yakuchangia Mfumo wa Kuboresha Afya ya Mama na Mtoto siku ya Jumamosi Machi 04,2017.

  Amesema shughuli hiyo italenga mambo mawili ambayo ni Kuwekeza Bima za Afya ya Mama na Mtoto ikiwa kuchangia pesa,Kuwasaidia Bima ya Mwaka mmoja kukaa katika Mfumo na kuwekeza.

  Pia kuboresha Mazingira katika Hospitali na kuchangia vifaa katika hospitali za Serikali.

  Kwa upande wao Wanachama wa Shirika hilo,Kenneth Munanu na Consolata Msambichaka wamesema vijiji vingi hapa nchini vina uhitaji wa Bima ya Afya.

  Pia wamewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kuchangia shughuli hiyo ili kufanikisha Kampeni hiyo ya Nuru ya Afya.


  Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Shirika la Afya na Elimu ya Tiba (TAHMEF),Juliana Busasi (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Maandalizi ya Kampeni ya kuboresha Afya Wanawake na Watoto ijulikanayo kama Nuru ya Afya inayotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi Jijini Dar es Salaam. 

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting, Malale Hamsini ameweka wazi kuwa wachezaji walishindwa kuzitumia nafasi za wazi walizozipata katika mchezo wao dhidi ya Yanga na kuambulia kipigo cha 2-0.

  Malale ameweka wazi kuwa, hawezi kuwalaumu wachezaji wake kwa kushindwa kutoka na ushindi kwenrye mchezo huo ambapo dakika 45 za kipindi cha pili Yanga walicheza wakiwa pungufu baada ya mshambuliaji wao Obrey Chirwa kutolewa kwa kadi  nyekundu.

  Amesema , walipata nafasi za wazi ila safu ya ushambulaji haikuwa makini na hata hivyo umakini wa safu ya ushambuliaji wa Yanga uliweza kuharibu mipango yao ya kupata goli.

  “Washambuliaji wangu hawakuwa makini kuweza kupata goli kwani Yanga walicheza wakiwa pungufu kwa dakika 45 za kipindi cha pili na zaidi safu ya ulinzi ya Yanga ilikuwa makini kuharibu mipango ya  timu yangu,"amesema Malale.

  Uwezo wa wachezaji wa Yanga wa mmoja mmoja uliweza kuisaidia kupata ushindi ule ingawa walicheza wakiwa pungufu.

  Baada ya matokeo hayo Ruvu Shooting ipo nafasi ya tisa ikiwa na alama 29 ambapo Malale kwa sasa ameweka wazi mikakati yake ya kujiandaa na mechi zilizosalia za mzunguko wa pili.

  0 0

   Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria na Mbunge wa Kyela , ameshudia zoezi la kuingizwa majini kwa Meli mpya ya pili ya mizigo iitwayo MV Ruvuma kwenye bandari ya Itungi, Wilayani Kyela. 

  Tukio hilo la kuiingiza Meli hiyo making limefanyika Machi Mosi . Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba mzigo zaidi ya tani 1000 inaungana na Meli nyingine mpya MV Njombe yenye uwezo wa kubeba zaidi ya tani 1000 ambayo iliingizwa majini siku tano zilizopita. Meli zote mbili zipo kwenye hatua ya mwisho ya utengenezaji na majaribio kabla hazijaanza rasmi kubeba mizigo kwenye ziwa Nyasa. 

  Tayari wateja mbalimbali wamejitokeza kutaka mizigo yao ianze kubebwa yakiwemo makampuni yanayojishughulisha na biashara ya makaa ya mawe.
     0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

  WATU watatu raia wa Nchi ya Burundi waliopewa hifadhi katika Kambi ya wakimbizi ya Mtendeli Mkoa wa Kigoma,wanashikiliwa na Jeshi la Polisi la hapo,kwa tuhuma za upangaji wa magogo katika barabara kuu ya Kigoma ,Kasulu na Kakonko kwa lengo la utekaji wa magari hasa mabasi ya abiria yaendayo mikoani.

  Pia, walipokaguliwa walikutwa na vitu vifuatavyo Bomu moja la kutupwa kwa mkono(Offensive hand Grenade),Bunduki moja ya bandia,panga mbili,rungu 3,viatu aina ya raba jozi moja,viatu vya kike jozi moja,simu aina ya nokia Nne,Tecno tatu,vipodozi vya kike,laptop ,power benki,saa,sanjari na nguo mbalimbali za kiume.

  Akizungumzia tukio hilo leo mbele ya wandishi wa habari ofisini kwake kigoma Ujiji,Kamanda wa Polisi Ferdinand Mtui alisema walibaini hilo baada ya askari polisi waliokuwa katika doria kwenye njia hiyo yenye mapori makubwa ndipo waliwakamata watuhumiwa hao ambao walikuwa
  kwenye mtego.

  Aliyataja majina ya watuhumiwa hao ni pamoja na Hakizimana David(21),Nepomseni Niogere(25) na Nduwamahoro Justine(20) wote ni wakimbizi wanaoishi katika kambi ya mtendeli iliyopo wilaya ya Kakonko
  na watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

  Alitoa mwito kwa raia wote wa kigeni waliopewa hifadhi katika kambi mbalimbali za wakimbizi mkoani humo watii sheria,kanuni na taratibu
  zote za nchi na waache kujihusisha na vitendo

  0 0


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd. kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani leo.Kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing,  Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd Fang Habibi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru(wapili kushoto).
    Jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd kama linavyooneka mara baada ya baada ya kuwekwa rasmi leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd mara baada ya kuweka jiwe la msingi leo Wilayani Mkuranga, Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 8000 za Vigae kwa siku.Kushoto kwake ni Balozi wa China nchini Tanznia Dkt.Lu Youqing na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mbunge wa Kilwa Kusini Suleiman Bungara(Bwege ) kutoka CUF katika eneo la Somanga wakati alipokuwa akielekea Nangulukulu katika ziara yake ya mikoa ya Kusini.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimian na mbunge wa Kilwa Kaskazini Vedasto Ngombale (CUF) mara baada ya kuhutubia wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpatia msaada wa Shilingi milioni moja kijana Abdulrahman Khalid ambaye ni mlemavu wa miguu katika eneo la Mchinga-1 mkoani Lindi, Katikati(Mwenye shati la maua) ni Mbunge wa Mchinga Hamidu Bobali kupitia chama cha (CUF) ambaye ameahidi kumpatia mlemavu huyo kiasi cha Shilingi Milioni moja pia.PICHA NA IKULU


  0 0

  Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Sam Kamanga kushoto akizungumza na ujumbe wa Mamlaka ya Bima nchini ukiongozwa na Kamishina wa Mamlaka hayo Dk. Baghayo Saqware (kulia), alipotembea Makao Makuu ya NIC jana Jijini Dar es Salaam 
  Kamishina wa Mamlaka Bima nchini Dk. Baghayo Saqware,akisisitiza jambo wakati alipotembelea Makao Makuu ya NIC jana. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Sam Kamanga kushoto akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mara baada ya ziara hiyo ya ujumbe wa Mamlaka ya Bima Nchini. 
  Picha ya pamoja: Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Sam Kamanga (wa tatu kushoto) na Kamishina wa Mamkala ya Bima Nchini Dk. Baghayo Sakware (wa Wa nne kushoto) wengine pichani ni maofisa wa taasisi hizo. 


  0 0


  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  Ubalozi wa Kuwait nchini umekabidhi visima vinne katika shule za msingi Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

  Shule za Msingi  zilizopata visima hivyo ni Yombo, Umoja , Mwale pamoja na Bwawani. Akizungumza  wakati wa kukabidhi visima hivyo, Balozi wa Kuwait , Jasem Al-Najem  amesema kuwa wanatambua umuhimu wa maji ndiyo maana wameona umuhimu wa visima hivyo katika shule hizo.

  Amesema wataendelea kutoa misaada hiyo kutokana na mahitaji yaliyopo katika jamii kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Kuwait.

  Al-Najem amesema kuwa wameweza kuchimba visima 16 vyenye thamani ya  Dola za Kimarekani 63,000  na watu wengine waweze kujitokeza kusaidia jitihada mbalimbali.

  Ubalozi huo pia umekabidhi dawa za binadamu katika Hospitali ya Amana zenye thamani  sh.milioni tatu.
  Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akizundua kisima cha maji safi katika shule ya Msingi Yombo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Red Cresene , Anwari Abdallah Al-Hasawi.Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
  Afisa Elimu, Elimu ya Watu Wazima wa Manispaa ya Ilala , Hamisi Mlangala akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa visima ambapo alishukuru msaada huo.
  Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akikabidhi dawa kwa Mganga Mkuu Msaidizi wa Hospitali ya Amana, Amimu Kilomoni, jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Kuwait nchini , Jasem Al-Najem akitembelea Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Amana  jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Halmshauri ya Wilaya ya Mufindi  imesaini mikataba yenye zaidi ya Tsh. Bilioni moja  na wakandarasi wa Barabara kwa lengo la kuzifanyia matengenezo  baadhi ya barabara zilizo chini ya halmashauri hiyo, zikiwa na urefu wa takaribani km 151.

  Taarifa ya Afisa habari na mawasilino  wa halmshauri ya Wilaya ya Mufindi kwa vyombo vya habari Bw. Ndimmyake Mwakapiso, imetanabaisha kuwa, halmashauri imeingia mikataba na  makampuni  11 ikiwa na thamani ya  Tsh. Bilioni 01, milioni kumi, laki 05 na  elfu tatu miamoja na 24.

  Mwakapiso, amezitaja  baadhi ya barabara zitakazofanyiwa matengenezo kuwa ni pamoja na barabara ya Kilosa Mufindi matengenezo ya nara kwa mara  km12, mpangatazara- Mlimba km 21, Ihalimba- Igomtwa na usokami km 11 wakati ile ya Iramba – Ipilimo itatengenezwa kwa urefu wa km 13.

  Halmshauri ya Wilaya ya Mufindi inamajimbo mawili ya uchaguzi yenye mtandao mzuri wa barabara km 1,000.6 ambazo halmshauri imekuwa ikizifanyia  matengenezo ya mara kwa mara ili kuziwezesha zipitike misimu yote ya mwaka kwa kuzingatia kuwa uwepo wa shughuli za viwanda na mazao ya misitu hususani mbao na nguzo husababisha barabara hizo kutumika sana kwani mapema mwezi disemba mwaka jana ilisaini mikataba 10 yenye dhamani ya milioni 500.

  Aidha, halmashauri hiyo kupitia Mkurugenzi Mtendaji Profesa Riziki Shemdoe, ilianzisha utaratibu mpya wa kusaini kandarasi zote kwa uwazi kwa kuandaa hafla fupi ambayo huwakutanisha wakandarasi wote walioshinda tenda na kwa pamoja kutiliana saini kati ya pande zote mbili.
  Mwenyekiti wa halmashauri akikabidhi kandarasi zilizosainiwa kwa mmoja wa wakandarasi huku Mkurugenzi mtendaji Profesa Riziki Shemdoe akishuhudia.​
  sehemu ya wakandarasi 11 wakiwa ofisini kwa Mkurugenzi mtendaji, tayari kwa hafla fupi ya kusaini kandarasi zao, aliyeka mbele ni Profesa Shemdoe Mkurugenzi Mtendaji.

older | 1 | .... | 1595 | 1596 | (Page 1597) | 1598 | 1599 | .... | 3283 | newer