Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1588 | 1589 | (Page 1590) | 1591 | 1592 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu Ya Jamii

  Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga, Juma Mwambusi amekiri kuwa timu yake ilikuwa na tatizo katika eneo la ukabaji na kupelekea kuchapwa bao 2-1.

  Mwambusi amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo na kuelezaa ubovu wa timu yake.

  “tulianza mchezo huu vizuri lakini tatizo la ukabaji katika timu yetu ndio limetugharimu na kuwapa wapinzani wetu ushindi wa wazi ambao kila mtu ameuona” amesema Mwambusi.

  Mwambusi ametaja kuwa kulikuwa hakuna sababu ya timu yao kupoteza mchezo huo kwani tayari walikuwa washatangulia kwa bao moja hivyo walikuwa na nafasi nzuri ya kupata ushindi lakini uzembe wa wachezaji wachache umeigharimu timu.

  Ametaja kuwa tatizo lililowakumba wapinzani wao la kupewa kadi Nyekundu, lilikuwa zawadi tosha ya kuondoka na ushindi lakini bado wachezaji walishindwa kukaba.
  Kocha msaidizi wa yanga Juma Mwambusi akiwa na kocha mkuu wa timu hiyo George Rwandamina wakipanga jambo katika mchezo wao dhidi ya Simba.

  0 0


  Wachezaji wa Simba wakishangilia mara baada ya kuichapa Yanga bao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom.
   Kiungo wa kati wa Yanya Haruna Niyonzima akijaribu kumtoka beki wa SimbaJanvier Bukungu
   Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akiweka sawa mpira mbele ya beki wa kati wa Yanga Kelvin Yondan
   Golkipa wa Yanga Deogratius Munishi akiokoampira uliopigwa na mshambualiaji wa Simba Laudit Mavugo
   Kiungo wa Simba Said Ndemla akiwania mpira na kiuongo wa kati wa Yanga,Justin Zulu (Mkata umeme).


  0 0

  Kituo cha utalii mkoa wa Ruvuma kinatarajia kuandaa tamasha la miss utalii mkoa wa Ruvuma, kwa kuwatumia wazawa kutoka wilaya za SONGEA,MBINGA,NYASA , TUNDURU na NAMTUMBO kwa lengo la kumpata balozi mmoja atakaye wakilisha kutangaza utalii uliopo katika mkoa wa huo.Hii hapa video yake.


  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akiwaelezea Mawaziri kutoka Zanzibar jinsi Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kinavyorahisisha kutoa Huduma za Ardhi bila usumbufu kwa Wananchi. Kuanzia Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud, Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Hamad Rashid, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar Mhe. Salama Talib na Katibu Mkuu Wizara wa Ardhi Dkt. Yamungu Kayandabila.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud jinsi ya kutumia mashine ya kutolea huduma za Ardhi katika kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
  Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar Mhe. Salama Talib akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi jinsi Wizara yake ilivyofanikiwa kuyapatia ufumbuzi masuala mbalimbali ya Ardhi na kuwaondolea usumbufu Wananchi katika kupata huduma za Ardhi. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara wa Ardhi Dkt. Yamungu Kayandabila. 
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akiwa na ujumbe wa Mawaziri kutoka Zanzibar walipofika ofisini kwake.
  Wananchi wakipata Huduma za Ardhi katika Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

  0 0

  Mbunge wa Geita Mjini Constatine Kanyasu amesikitishwa kwa kitendo cha wananchi waliokuwa wamejenga kwenye hifadhi ya misitu kubomolewa huku wengine wakiachwa katika maeneo hayo na kuahidi kushughulikia ili haki itendeke sawa na wale ambao hawajabomolewa.

  Hayo aliyasema kwenye mkutano wa hadhara ambao umefanyika kwenye mtaa wa Mwatulole kata ya buhala hala wilaya na Mkoa wa Geita,wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika jimbo ambalo analiongoza.

  Mh Kanyasu amesema kuwa amesikitishwa na hatua ya TFS kubomoa nyumba za watu wengine huku wale wenye uwezo wakiachwa na kuendelea kukaa kwenye maeneo hayo kutokana na hilo wameagiza watu wa TFS kuangalia kama wale waliobomolewa pale yalikuwa ni maeneo yao na ninani ambaye aliwauzia.

  “Naomba Nikiri na mimi iliniuma sana lakini kwa sababu ni serikali na sikuwepo na sijui kama walitumia sheria mimi naomba yeyote ambaye ni haki yake ya msingi alete na mimi nitashughulikia”Alisema Kanyasu

  Hata hivyo Bi,Chausiku Lusetula ambaye ni miongoni mwa wanananchi waliobomolewa makazi yao amemuomba Mbunge kuwasaidia ili wapate haki zao za msingi na kwamba kwa sasa hawana makazi ya kuishi baada ya makazi yao kubomolewa.

  “Mheshimiwa Mbunge sisi ni watu ambao tumekosa makazi kwa sasa hatujui ni wapi tutaishi na chakusikitisha kwanini sisi tubomolewe na wengine waendelee kukaa kwenye maeneo ambayo inasemekana ni hifadhi ya misitu kama ni hivyo ni vyema haki itendeke kwa wote”Alisema Chausiku

  Diwani wa kata ya Buhala hala ,Mussa Kabese amewaambia wananchi kuwa mbunge wa jimbo la Geita Mjini tayari amekwisha mwandikia Waziri mwenye dhamana barua ambayo imemwomba matumizi ya pori la buhala hala kubadilishwa na kuwekwa taasisi ambazo zitawasaidia wananchi ambao wapo kwenye mitaa ya shinde na magogo kupata mahitaji ya msingi ikiwemo swala la elimu na afya.

  Hatua hii imekuja ni baada ya takribani wiki mbili kumalizika ambapo wananchi ambao wamejenga kwenye hifadhi ya misitu inayosimamiwa na wakala wa misitu nchini TFS kubomolewa makazi yao.
  Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini ,Constatine Kanyasu,akizungumza na wananchi wa kata ya Buhala hala wakati aliipokwenda kusikiliza kero ambazo zimekuwa zikiwakabili kwenye maeneo ambayo wanaishi.
  Maeneo ambayo wananchi walibomolewa nyumba zao.
  Moja kati ya wananchi ambao wameuzulia Mkutano huo akielezea kero yake kwa Mbunge wa Geita mjini wakati wa Mkutano huo.
  Meza kuu ikiongozwa na Mbunge wa Geita,Mjini,Diwani wa kata ya Buhala hala pamoja na baadhi ya wajumbe wakifatilia maelezo kutoka kwa wananchi.
  Wananchi ambao walikuwa wamejitokeza kwenye mkutano huo wakisikiliza wakati Diwani wa kata ya Buhala hala alipokuwa akitoa maelezo na kujibu baadhi ya changamoto za wananchi.


  0 0

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni kwa pamoja wamekubaliana kutosaini mkataba wa mahusiano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Ulaya (EPA).

  Makubaliano hayo yamefanyika jana Ikulu, Jijini Dar es Salaam ambapo  Rais Yoweri Museveni yuko nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 25 – 26  Februari, 2017.

  Akiongea na waandishi wa habari Rais Magufuli amesema kuwa mkataba wa EPA hauna faida bali ni aina nyingine ya ukoloni ambao unataka kurejeshwa kwa nchi za Afrika.

  “Nimeongea na Rais Yoweri Museveni amekubali kutosaini mkataba wa EPA, nitawaagiza wataalamu waliosaidia kutupa maelezo juu ya madhara ya mkataba huo kwenda pia Uganda kuwapa maelezo ambao waliyatoa kwa Tanzania,” alifafanua Dkt. Magufuli.

  Kwa upande wake, Rais Yoweri Museveni amesema kuwa ameongea na Rais Magufuli na wamekubaliana kutosaini mkataba huo na kuongeza kuwa suala la EPA ni lazima lijadiliwe na nchi zote za Afrika Mashariki ili kuwepo na msimamo wa pamoja kwa nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Aidha Rais Museni amempongeza Rais Magufuli kwa kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kununua ndege mpya Sita, hivyo amekaribisha shirika hilo kutoa huduma za usafiri wa anga nchini Uganda kutokana na nchi hiyo kuwa na uhitaji wa huduma hiyo.

  Vilevile amempongeza Rais Magufuli kwa ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway) kutoka Dar es Salaa mpaka Mwanza na Isaka mpaka Rwanda ambapo itapelekea ujenzi wa bandari kavu katika mkoa wa Mwanza hivyo wafanyabiashara wa Uganda kunufaika na bandari hiyo ambayo itakuwa karibu zaidi kuliko ilivyo kwa Dar es Salaam.

  Wakati huohuo Mawaziri wa Nje kutoka Tanzania na Uganda Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Oryem Henry Okello wamesaini makubaliano ya uhusiano katika mambo ya Diplomasia baina ya nchi hizo mbili.

  Museveni yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo atatembelea baadhi ya maeneo kadhaa ikiwemo kiwanda cha Juice cha mfanyabiashara Mtanzania Said Bakhressa ambaye pia amewekeza nchini Uganda.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni alipowasili Ikulu jijini Dar es salaam kuanza ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili leo Februari 25, 2017 .

  PICHA NA IKULU
   

  0 0  0 0

  Na Riziki Manfred Bonzuma, Mbinga 

  Wadau wa elimu na viongozi halmashauri ya Mbinga vijijini wamekutana kufanya tathimini ya elimu ikiwemo kushuka kwa ufaulu kwa wa elimu ya msingi miaka ya hivi karibuni. 

  Wakizungumza katika kikao hicho ,baadhi ya wadau wa elimu wamezitaja changamoto zinazopelekea kushuka kwa elimu kuwa ni pamoja kutoboreshwa kwa masirahi ya walimu, upungufu wa walimu, ushiriki hafifu wa wazazi hususani kufuatilia maendeleo ya watoto wao na kuchangia shughuli za elimu. 

  Pia wadau wameainisha changamoto zingine kuwa ni pamoja na kuto wahamisha walimu wakuu walio shushwa vyeo pamoja na kuongeza uwiano wa vitabu hasa vya kiada katika shule za halmashauri hiyo. 

  Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga vijijini Gombo Samandito Gombo amesema halmashauri hiyo imejipanga kuhakikisha inaongeza ufaulu kimkoa na kitatifa hasa elimu ya msingi ambayo imeonekana kulegalega huku akiwataka walimu kuto fanya uzembe katika kufundisha ikiwemo utotoni. 

  "sitakuwa na msamaha kwa walimu wanao acha kazi wanaenda kupiga boda boda ukiona nimekubaini nitakufukuza hata usiangaike kuniomba msamaha pia wapo walimu wanao kopa mpaka wanapiriliza muda wa kufundisha wanakimbia madeni waache mara moja" alisema Samandito . 

  Awali katika maada za utangulizi mkuu wa Polisi wilaya ya Mbinga OCD Maganga amekemea baadhi ya wazazi kuwahusisha wanafunzi katika biashara ya dawa za kulevya na kuwataka viongozi ngazi ya vijijini na kata kutoa taarifa za wahusika wa biashara hiyo pamoja na wale wanao wapa mimba wanafunzi. 

  Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ya Mbinga Consimas Nshenyi amendelea kukazia maagizo yaliyo tolewa wa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Binilith Mahenge wakati wa ziara yake wilaya Mbinga mapema mwaka huu juu ya uharibifu wa mazingira ikiwemo kufanya shughuli za kibinaadamu ndani ya mita sitini kutoka vyanzo vya maji pamoja na kuhakisha Benki tofauti zinatukamika katika kujenga majengo sio kukaa katika matanuru . 

  Matokeo ya darasa la saba mwaka 2016 yanaonyesha kushuka kwa elimu katika halmashauri hiyo ya wilaya ya Mbinga baada ya kushika nafasi ya 8 katika mkoa wa Ruvuma kati ya Halamashauri 8 za mkoa huo. 


  0 0  0 0
  0 0


  0 0

   Mbio za Kili marathon zimefanyika leo manispaa ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro katika viwanja vya chuo cha ushirika ambapo wakimbiaji zaidi ya 8000 wameshiriki mbio hizo.

  Mbio hizo zimefunguliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel majira ya saa kumi na mbili nusu asubuhi ambapo mbio za kilometa 42 zilianza, huku wale kilometa 21 wakianza mbio hizo majira ya saa moja kamili asubuh.

  Mbio hizo ziligawanyika katika makundi tofauti totauti kuanzia wale waliokimbia umbali wa kilometa 42, umbali wa km 21 huku kwa upande wa walemavu wao walishindana katika mbio za umbali wa km 10 pamoja na zile za kilometa 5 ambazo hazina ushindani. kila kundi walipatikana washindi wa mbio hizo.
  Washiriki wa Mbio za 21 Km wakiwa tayari kuanza kushindana katika Mbio za Kilimanjaro Marathon 2017, zilizofanyika katika viwanja vya Chuo cha Ushirika, Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro leo.
  Sehemu ya Washiriki wa Mbio za 21 KM wakichuana vikalia katika moja ya njia zao mapema leo asubuhi.
  Mshiriki wa kwanza kuwasili uwanjani kwa wale walioshiriki mbio za kilomita 42 kwa upande wa wanaume, Moses Mongick ambaye ni raia kutoka nchini Kenya akionyesha furaha yake.
  Mshiriki wa kwanza kuwasili uwanjani kwa wale walioshiriki mbio za kilomita 42 kwa upande wa wanawake, Shemith Nyamwira Muriuk kutoka Kenya akiwasili uwanjani huku akiwa ni mwenye furaha tele.
  Mshindi wa mbio za kilometa 21 ambaye ni raia  wa Tanzania Emmanuel Giniki akiwasili uwanjani.
  Mshiriki wa kwanza kuwasili uwanjani kwa wale walioshiriki mbio za kilomita 21 kwa upande wa wanawake, Grace Kimanzi kutoka Kenya akiwasili uwanjani.
  Mwanamitindo wa Kimataifa, Miriam Odemba alikuwa ni mmoja wa washirikiwa wa Mbio za kilometa 21.


  0 0

   

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Thobias Andengenye kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Pindi Chana kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Silima Kombo Haji kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sudani, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Abdallah Kilima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Matilda Masuka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akila kiapo cha Ahadi ya Uadilifu pamoja na Mabalozi Pindi Chana, Balozi Silima Kombo Haji, Abdallah Kilima pamoja na Balozi Matilda Masuka mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi (wapili kutoka kushoto), Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba(Wakwanza kulia) , Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Hamad Masauni (Wakwanza kushoto) pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye(Watatu kutoka kushoto waliosimama mstari wa nyuma) na Mabalozi Pindi Chana(Wakwanza kulia walisimama mstari wa nyuma ) , Balozi Matilda Masuka(Wapili kutoka kulia waliosimama mstari wa nyuma), Balozi Abdallah Kilima(Wapili kutoka kushoto mstari wa nyuma) na Balozi Silima Kombo Haji (Wakwanza kushoto waliosimama) mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.


  PICHA NA IKULU

  0 0

  Na. Immaculate Makilika na Lilian Lundo- MAELEZO.

  Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni ametoa wito wafanyabiashara wa Kitanzania kwenda kuwekeza nchini Uganda.

  Rais Museveni ametoa kauli hiyo leo wakati alipotembelea viwanda vya Kampuni ya Bakhresa vinavyozalisha Unga na Juisi vya Buguruni na Vingunguti jijini Dar es Salaam.

  “Nawakaribisha wafanyabiashara wa Kitanzania kuja nchini Uganda kuwekeza kwani kufanya hivyo kutasaidia kuzalisha bidhaa, upatikanaji wa soko pamoja na ajira” alisema Rais Museveni.

  Kauli hiyo ya Rais Museveni imetokana na mafanikio yanayotokana na Mwekezaji wa Kitanzania Said Salim Bakhresa aliyewekeza nchini Uganda ambapo anamiliki Kiwanda cha kusanga ngano nchini humo.

  Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni za Bakhresa Hussin Sufiani amesema kwamba Kampuni hiyo iko mbioni kuongeza uzalishaji wa unga wa ngano kutoka tani 1,100 hadi kufikia tani 2,000 kwa siku nchini Uganda.

  Aidha, amesema kutokana na uwekezaji wa Kampuni hiyo nchini Uganda jumla ya Waganda 650 wamenufaika na ajira mbalimbali ambazo zinasaidia kuwapatia kipato.

  Kwa upande wa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwaijage amesema kuwa Uganda na Tanzania zimeingia makubaliano ya ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya viwanda.

  Amesisitiza Watanzania wanaweza kwenda kuwekeza nchini Uganda kwa vile nchi hiyo wanalima tani milioni 4 za mahindi lakini wana uwezo wa kutumia tani milioni moja pekee, hivyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Kitanzania kwenda kuwekeza nchini humo.

  “Tunawahamasisha wafanyabiashara wa Uganda na Tanzania kuwekeza katika nchi zao ili kuzalisha , bidhaa na ajira za kutosha kwa wananchi” alisema Waziri Mwijage.

  Waziri Mwijage alitoa Wito kwa Watanzania kushiriki katika uchumi wa viwanda kwa kufanya uzalishaji wa bidhaa zinazotumika viwanda mfanio kwa kulima matunda au mbogamboga.

  Rais Yoweri Museveni aliwasili nchini jana kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili ambapo akiwa nchini alifanya mazungumzo na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kutembelea Viwanda vya Said Salim Bakhresa vya Tazara na Vingunguti.

  0 0

   
  NA EMERISIANA ATHANAS .


  DIWANI wa Kata ya Buguruni wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Adam Fugame ameagiza viongozi wa kata akiwemo Ofisa Afya, kuwakamata na kuwachukulia hatua watu wasiofanya usafi au kuchangia kwaajili yakuzolewa uchafu.

  Akizungumza jijini hapa jana, wakati wa zoezi la ufanyaji usafi ulioshirikisha viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Ilala akiwemo Mkurugenzi Msongela Palela, alisema ni vema viongozi wakafanya kazi kwa mujibu wa sheria ili kuwashughulikia watu hao. "Suala hili sio rai bali tufanye kama sheria ili kufanikisha zoezi la kuimarisha usafi katika maeneo yetu, kwani tusipofanya hivi hakuna litakalotekelezwa, watu hawafanyi usafi," alisema.

  Kutokana na umuhimu wa kufanya usafi alisema ni vema watakaokutwa hawachangii wala kujishughulisha na kufanya usafi wakachukuliwa hatua na kutozwa fedha. Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Palale alisema kuwa katika kata tisa zilizoko katika manispaa hiyo kata ya Buguruni ndiyo imekuwa na ugonjwa wa kipindu pindu ambacho husababishwa na hali ya uchafu.

  Alitumia nafasi hiyo kuwataka wakazi wa kata ya Buguruni kuhakikisha wanafanya usafi na kuwa walinzi katika kuhakikisha wanalinda mazingira na kuimarisha usafi kwenye maeneo yao.

  Diwani wa Kata ya Buguruni,Adamu Fugame (Cuf) akishirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Msongela Palela na Katibu Tawala wa wilaya hiyo,Edward Mpogolo (kulia) wakifanya usafi katika maeneo ya buguruni kwa malapa kutimiza kauli ya Rais Dk.John Magufuli ya kufanya usafi kila mwisho wa wiki ya mwezi jijini Dar es Salaam juzi. (PICHA NA ELISA SHUNDA) Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Msongela Palela akizungumza na wananchi wa eneo la Buguruni kwa Malapa na Darajani kuhusu kufanya usafi katika maeneo yanayowazunguka ili kujikinga na kujiepusha na magonjwa ya milipuko kama Kipindupindu baada ya kufanya usafi kutekeleza agizo la Rais Dk.John Magufuli ya kufanya usafi kila mwisho wa wiki ya mwezi jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Diwani wa Kata ya Buguruni,Adamu Fugame (Cuf) na Katibu tawala wa wilaya hiyo,Edward Mpogolo.

  0 0

  Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania, Egon Kochanke akipewa maelezo na Mchoraji wa picha, Bw. Douglas Kahabuka katika Maonyesho ya kitalii ya kazi za sanaa na uvumbuzi wa kitaalamu juu ya Watanganyika waliokuwa wakipambana na Utawala wa Wajerumani, Onyesho hilo limepewa jina la ‘Kuishi Ndani ya Simulizi’ linahusisha vitu, michoro, picha za kuchora, filamu, vifaa na utafiti yaliyofanyika jana mjini Songea katika Jumba la Makumbusho ya vita vya Majimaji mjini Songea. Wengine ni Chifu wa kabila la Wangoni, Emmanuel Zulu akiwa pamoja na viongozi wenzake wa kabila la wangoni.
  Mtaalamu wa Tafiti za Historia, Lili Reyels (kulia) akimueleza Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania, Egon Kochanke ( wa tatu kushoto) ,kuhusiana na Maonyesho ya kitalii ya kazi za sanaa na uvumbuzi wa kitaalamu juu ya Watanganyika waliokuwa wakipambana na Utawala wa Wajerumani, Onyesho hilo limepewa jina la ‘Kuishi Ndani ya Simulizi’ linahusisha vitu, michoro, picha za kuchora, filamu, vifaa na utafiti yaliyofanyika jana mjini Songea katika Jumba la Makumbusho ya vita vya Majimaji. Wengine ni Chifu wa kabila la Wangoni, Emmanuel Zulu ( wa pili kulia) akiwa pamoja na viongozi wa Mila ya wangoni. 
  Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania, Egon Kochanke (kushoto) akiwa na Chifu wa Kabila la Wangoni, Emannuel Zulu ( wa kwanza kulia) akizungumza mara baada ya kupata maelezo kwa Mchoraji wa picha, Bw.Douglas Kahabuka (katikati) katika Maonyesho ya kitalii ya kazi za sanaa na uvumbuzi wa kitaalamu juu ya Watanganyika waliokuwa wakipambana na Utawala wa Wajerumani, Onyesho hilo limepewa jina la ‘Kuishi Ndani ya Simulizi’ linahusisha vitu, michoro, picha za kuchora, filamu, vifaa na utafiti yaliyofanyika jana mjini Songea katika Jumba la Makumbusho ya vita vya Majimaji. Wengine ni Chifu wa kabila la Wangoni, Emmanuel Zulu akiwa pamoja na viongozi wenzake wa kabila la wangoni.  Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania, Egon Kochanke (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kabila la wangoni huku wakipeana mikono na Chifu wa Kabila la Wangoni, Emannuel Zulu (kushoto) mara baada ya kuzindua Maonyesho ya kitalii ya kazi za sanaa na uvumbuzi wa kitaalamu juu ya Watanganyika waliokuwa wakipambana na Utawala wa Wajerumani, Onyesho hilo limepewa jina la ‘Kuishi Ndani ya Simulizi’ linahusisha vitu, michoro, picha za kuchora, filamu, vifaa na utafiti yaliyofanyika jana mjini Songea katika Jumba la Makumbusho ya vita vya Majimaji. Wengine ni watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

  0 0

  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akipokea vifaa vya kuzuia vumbi kwa askari wa usalama barabarani kutoka kwa msamaria mwema, Tahir Othman (kulia) ,aliyejitolea vifaa hivyo ili kusaidia askari kuepukana na vumbi kuingia kwenye njia ya hewa wawapo katika shughuli zao.Anayeshuhudia katikati ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni .Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akionyesha kwa waandishi wa habari jinsi ya kuvaa kifaa cha kuzuia vumbi kwa askari wa usalama barabarani alivyopokea kutoka kwa msamaria mwema,Tahir Othman(hayupo pichani) ,aliyejitolea vifaa hivyo ili kusaidia askari kuepukana na vumbi kuingia kwenye njia ya hewa wawapo katika shughuli zao.Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni. Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri, jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia jinsi ya kuvaa kifaa cha kuzuia vumbi kwa askari kutoka kwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, ambae pia ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo.Vifaa hivyo vilitolewa na msamaria mwema,Tahir Othman (hayupo pichani).Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (aliyesimama) katikati alipokuwa akitangaza mchango wake wa fedha Shilingi za Kitanzania Millioni Kumi zilizochangwa jana wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyotayarishwa na Wizara ya Afya katika ukumbi wa Park Hayatt Hoteli kwa ajili ya kusaidia Hospitali ya Makunduchi na Kivunge pamoja na maadhimisho ya miaka kumi ya Mradi wa kuendeleza huduma za Afya Zanzibar (HIPZ).
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akisalimiana na Mwenyekiti wa HIPZ RU Mac Donagh wakati alipowasili viwanja vya Park Hayatt Hoteli jana katika hafla ya chakula cha usiku iliyotayarishwa na Wizara ya Afya katika ukumbi wa kwa ajili ya kusaidia Hospitali ya Makunduchi na Kivunge pamoja na maadhimisho ya miaka kumi ya Mradi wa kuendeleza huduma za Afya Zanzibar (HIPZ).
  Baadhi ya Viongozi na Wageni mbali mbali wakiwa katika hafla ya chakula cha usiku iliyotayarishwa na Wizara ya Afya ya kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia Hospitali ya Makunduchi na Kivunge pamoja na maadhimisho ya miaka kumi ya Mradi wa kuendeleza huduma za Afya Zanzibar,(HIPZ) hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa Park Hayatt Hoteli Mji mkongwe wa Zanzibar.
  Mwenyekiti wa Mradi wa kuendeleza huduma za Afya Zanzibar,(HIPZ) RU Mac Donagh alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyotayarishwa jana na Wizara ya Afya kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia Hospitali ya Makunduchi na Kivunge pamoja na maadhimisho ya miaka kumi ya Mradi wa kuendeleza huduma za Afya Zanzibar,(HIPZ) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Park Hayatt Hoteli Mji mkongwe wa Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyotayarishwa jana na Wizara ya Afya kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia Hospitali ya Makunduchi na Kivunge pamoja na maadhimisho ya miaka kumi ya Mradi wa kuendeleza huduma za Afya Zanzibar,(HIPZ) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Park Hayatt Hoteli Mji mkongwe wa Zanzibar.[Picha na Ikulu.] 

  0 0
 • 02/26/17--09:58: KUWAIT NATIONAL DAY - LONDON

 • 0 0

   Jengo Jipya la Bodi ya Mfuko wa Barabara lililopo mjini Dodoma ambako Idara ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) imetoa ushauri wa kihandisi katika usimikaji wa mifumo ya TEHAMA, Umeme, Viyoyozi, lifti na Kangavuke.
   Jengo jipya la Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano lililopo mtaa wa Moshi mjini Dodoma, ambako Idara ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) imetoa ushauri wa kihandisi pamoja na kufanya usimikaji wa mifumo ya TEHAMA, Umeme na Viyoyozi.
   Mafundi kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakifanya kazi ya kusimika mifumo ya TEHAMA katika jengo jipya la Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano lililopo mtaa wa Moshi mjini Dodoma.
   Fundi kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) akifanya kazi ya kusimika mifumo ya umeme katika jengo jipya la Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano lililopo mtaa wa Moshi mjini Dodoma.
  Fundi kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) akifanya kazi ya kufunga taa katika jengo jipya la Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano lililopo mtaa wa Moshi mjini Dodoma. 
  Picha na Theresia Mwami – TEMESA

older | 1 | .... | 1588 | 1589 | (Page 1590) | 1591 | 1592 | .... | 3348 | newer