Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1587 | 1588 | (Page 1589) | 1590 | 1591 | .... | 3283 | newer

  0 0

    Ramani ya kiwanda

    Wa kwanza kushoto mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, alhaj Magid Mwanga ,wa pili kushoto mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo na Jack Feng mkurugenzi wa kiwanda, wa tatu kushoto ni waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage na Ridhiwan Kikwete na Cliford Tandari wakiweka udongo kwenye jiwe la msingi.
  (picha zote na Mwamvua Mwinyi)

  Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze
  Waziri wa biashara, Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, amezitaka taasisi zinazohusika na uwekezaji kutokuwa na ukiritimba ili hali kufikia malengo ya serikali ya kukuza sekta ya viwanda.
  Aidha ameeleza kwamba, wizara hiyo, imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji ambayo yatawezesha kuvutia wawekezaji wa ndani na nje.
  Hayo aliyasema huko kitongoji cha Pingo Chalinze,Bagamoyo,wakati akiweka jiwe la msingi kwenye kiwanda cha Vigae cha Twyford Ceramics Ltd.
  Mwijage alisema, uwekezaji huo unaendana na dhana ya Rais Dk John Magufuli wa kuifanya nchi kuwa ya Viwanda .
  Alisema kwa kuanzishwa viwanda vingi vya aina hiyo kutasaidia kuongeza pato la nchi na kuzalisha ajira kwa wingi.
  “Zipo idara ambazo zinafanikisha uwekezaji ikiwemo brela, idara ya uhamiaji, kazi, mamlaka ya mapato TRA, wizara ya ardhi, shirika la viwango TBS, baraza la Mazingira NEMC ambazo zinapaswa kufanya kazi kwa wepesi ili kufanikisha uwekezaji,” alisema Mwijage.
  Alisema kati ya idara hizo baadhi zimekuwa zikifanya vizuri lakini nyingine zimekuwa zikiwapa usumbufu mkubwa wawekezaji.
  “Wizara yangu haina tatizo lakini kuna baadhi ya idara zimekuwa kero na ukiritimba usio na sababu .,naomba kama kuna idara zinakuwa kikwazo niambieni ili tuwachukulie hatua,” alisema Mwijage.
  Mwijage alisema nchi zilizofanikiwa kukuza uchumi wake kupitia viwanda zimeweza kutoa ajira nyingi kwa vijana kupitia sekta rasmi na isiyo rasmi.
  Mkurugenzi mkuu wa kiwanda hicho Jack Feng alieleza, kiwanda hicho asilimia 95 ya malighafi itakuwa inatoka nchini ambapo kigae kinatumia maliahafi zaidi ya 10.
  Alisema mara kiwanda hicho kitakapokamilika agosti mwaka huu kitaweza kupunguza asilimia 30 ya uagizaji wa vigae toka nje ya nchi.
  Feng alisema wanatarajia kuajiri wafanyakazi 2,000 moja kwa moja na 4,000 kazi za muda na gharama ya mradi huo ni dola mil. 56 sawa na bil. 120 .
  Alisema watauuza hadi nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Zambia, Uganda, Rwanda na Burundi.
  Nae mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji Cliford Tandari alisema kuwa uwekezaji wa kiwanda hicho ni wa mfano kwani utavutia makampuni mengi.
  Alisema kwasasa kituo hicho kimeweza kutoa wigo mkubwa katika kuandikisha miradi mbalimbali toka china na kufikia miradi 667 ambayo itazalisha ajira 83,141 kwa watanzania ,miradi 452 ni miradi inayohusiana na sekta ya uzalishaji viwandani.
  Mkuu wa mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo alisema ,mkoa huo una viwanda 264 huku vikubwa vikiwa ni viwili.
  Ndikilo alisema uwekezaji huo ni mkubwa na unatarajia kukuza ajira kwa vijana wa mkoa wa Pwani na Tanzania kwa ujumla.
  Alisema mkoa wa Pwani bado una maeneo makubwa ya uwekezaji na tayari kuna eneo lenye ukubwa wa hekari 5,000 linahitaji wawekezaji .
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete aliwapongeza wawekezaji hao kutoka nchi ya China .
  Alisema Chalinze imejipanga kuwa sehemu ya uwekezaji ambapo kuna ujenzi wa viwanda mbalimbali.
  Ridhiwani alisema kuwa changamoto kubwa inayokabiliwa wananchi na wawekezaji ni ukosefu wa maji,.
  Alibainisha wamekuwa wakijitahidi kuikabili lakini bado hawajafanikiwa kuidhibiti aliomba wawekezaji hao kutoa ajira bila ya kuwabagua wenyeji.

  0 0

  Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jana tarehe 23Februari 2016 amekutana na kufanya mazungumzo  na Rais wa Ivory Coast, Mhe. Alassane Ouattara katika Ikulu yake jijini Abidjan.. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Makamu wa Rais, Waziri wa Fedha na Waziri wa Elimu.
  Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Ouattara wamezungumzia hali ya elimu bara la Afrika na Ivory Coast kwa ujumla na haja ya kufanya mageuzi makubwa katika elimu ili kuweza kuendana na kasi ya nchi zilizoendelea.
  Rais Mstaafu Kikwete amempongeza Rais Outtara kwa jitihada kubwa anayoifanya kuinua elimu nchini mwake. Kwa mujibu wa utafiti wa Kamisheni, Ivory Coast iko katika nafasi nzuri ya kufikia viwango vya juu vya ubora wa elimu vya nchi zilizoendelea iwapo itaongeza juhudi ya kufanya mageuzi kulingana na mapendekezo ya Kamisheni hiyo.
  Rais Outtara amemuhakikishia Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete azma ya nchi yake kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu nchini mwake. Ameelezea utayari wa nchi yake kujiunga na mpango huo wa kufanikisha mapinduzi ya sekta ya elimu ndani ya kizazi kimoja ifikapo mwaka 2040.
  Akiwa jijini Abidjan, Rais Mstaafu ametembelewa na viongozi wa Watanzania wanaofanya kazi Benki ya Maendeleo ya Afrika na Watoto  wa Watanzania hao ambao walitaka kujua kuhusu masuala ya uongozi na maisha baada ya kustaafu. 
   Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu  Dkt. Jakaya Kikwete akikaribishwa na Rais Alassane Ouatara wa Ivory Coast jijini Abidjan katika Ikulu ya nchi hiyo.
  Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akimkabidhi ripoti ya 'Kizazi cha Elimu' Rais Allasane Ouatarra wa Ivory Coast
   Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mazungumzo na Rais Alassane Ouattara. Kulia kwake ni Makamu wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Daniel Kablan Duncan
   Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiagana na Rais Alassane Ouattara baada ya mazungumzo yao   Ikulu ya Ivory Coast.

   Rais MStaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Uongozi wa Watanzania wanaofanya kazi Benki ya Maendeleo ya Afrika jijini Abidjan
   Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia mazungumzo na baadhi ya watoto wa Watanzania waishio Ivory Coast waliomtembelea hotelini kwake Abidjan
  Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiwasainia autograph  watoto waliomtembelea hotelini kwake  jijini Abidjan.

  0 0

  Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Anna Makinda amesema ukuaji wa uchumi hauwezi kufikiwa endapo hakutakuwa na uwekezaji wa kutosha katika mafunzo kwa rasilimali watu.

  Mama Makinda ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa kujadili ukuaji wa uchumi 'Business Transforming Africa Conference' ambao umeandaliwa na kampuni ya African Management Services (AMSCOukiwa na lengo la kujadili umuhimu wa mafunzo kwa rasilimali watu katika kukuza uchumi.

  Amesema hakuna usawa kati ya ujuzi unaotolewa mashuleni na mahitaji ya soko la ajira jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa ukosefu wa ajira kwa wahitimu wengi ambao hushindwa kukidhi mahitaji ya soko la ajira.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde alisema kuwa  pamoja na jitihada zinazofanywa na wadau wote wanaoshiriki katika kukuza uchumi ni muhimu kwa wadau hao kwenda sambamba na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ili kuweza kufikia malengo ya pamoja yaliyokusudiwa.

  AMSCO imekuwa ikiandaa mikutano ya namna hii kwa lengo la kukuza uchumi wa taasisi, mashirika nchi kwa ujumla.
  Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne S. Makinda akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha viongozi wa mashirika na taasisi ili kujadili ukuaji wa uchumi 'Business Transforming Africa Conference' ambao umeandaliwa na kampuni ya African Management Services (AMSCOukiwa na lengo la kujadili umuhimu wa mafunzo kwa rasilimali watu katika kukuza uchumi.(Picha na Geofrey Adroph)
  Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde akizungumza kuhusu upatikanaji wa ajira katika nyanja mbalimbali hasa pale ukuaji wa uchumi unapoimarika wakati wa kujadili ukuaji wa uchumi 'Business Transforming Africa Conference' ambao uliwakutanisha dawau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.
  Mwenyekiti wa Taasisi ya ATMS, Balozi Jan Berteling akizungumza jambo kwenye mkutano huo uliowakutanisha viongozi wa mashirika na taasisi kuhusu ukuaji wa uchumi 'Business Transforming Africa Conference' uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Recency jijini Dar.
  Meneja wa Heineken Afrika Mashariki na Kati, Kayode Adeuja akizungumzia jinsi kufanya biashara na kukuza mtani kama kampuni hiyo ilivyoimarika wakati wa kujadili ukuaji wa uchumi 'Business Transforming Africa Conference' uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Recency jijini Dar.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  0 0

  Serikali imesema itatuma wataalam wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), kuangalia Maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Viwanja vya ndege katika Wilaya ya Masasi na Tunduru ili kujiridhisha na kushauri Serikali namna ya kutekeleza miradi hiyo. 

  Akizungumza mara baada ya kuonyeshwa maeneo hayo Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema pamoja na maeneo hayo kutengwa na Wilaya hizo kuna ulazima wa kuwatuma wataalam wa Viwanja ili kuwa na Viwanja bora vinavyozingatia viwango vya kimataifa. 

  “Nawapongeza sana kwa kutenga maeneo kwa ajili ya kujengaViwanja vya ndege kwani ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi, hivyo ili kukidhi viwango vilivyowekwa kimataifa katika ujenzi wa viwanja vya ndege nitatuma wataalam kutoka TAA ili kukagua maeneo haya na watoe muelekeo kwa kuishauri Serikali kuhusu utekelezaji wa miradi hii muhimu”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa. 

  Kuhusu kiwanja cha Masasi Waziri Mbarawa ameiagiza TAA na Halmashauri ya Wilaya yaMasasi kukaa pamoja na kuainisha mipaka ya kiwanja hicho ili kuepuka uvamizi wa miundombinu ya kiwanja hicho. 

  Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amemuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo kuiandikia Wizara mahitaji ya eneo hilo na kuainisha sababu ya kuhamisha kiwanja cha ndege cha Tunduru kutoka mjini kwenda nje ya mji. 

  Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), mkoani Mtwara, Bi. Zitta Majinge, amemhakikishia Waziri huyo kuleta maombi ya mapendekezo ya viwanja hivyo makao makuu ili kuweza kutafutiwa ufumbuzi wa changamoto za viwanja hivyo. 

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Masasi, Bi.  Zita Majige (wa pili kushoto) Kuhusu kuweka mipaka kwenye eneo la kiwanja ili kunusuru uvamizi, mara baada ya kukagua kiwanja hicho, wilayani Masasi.

  Muonekano wa Kiwanja cha ndege cha Masasi, ambacho kina uwezo wa kuhudumia ndege za abiria saba mpaka kumi.


  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  amewataka wanasheria wa mkoa wa Dar es Salaam  kujitoa kwa kuwasaidia wanyonge na masikini kuweza kupata haki zao na sio kutumia taaluma katika  kuwatetea watu wanaofanya uhalifu.

  Makonda  ameyasema hayo wakati alipokuwa akipokea mrejesho kwa wanasheria waliojitolea kutoa msaada wa kisheria kwa jiji la Dar es Salaam, amesema kuwa kuna watu wanakosa haki kutokana na kukosa msaada wa kisheria.

  Amesema kuwa wanasheria wa mkoa wa Dar es Salaam wakijitoa watakuwa wamesaidia wananchi kupata haki pamoja na kupunguza migogoro iliyopo.
  Makonda amesema vijana waliotoa msaada  wa kisheria wameonyesha uzalendo na kuwataka kuendelea kuwatumikia wananchi.

  Mwakilishi wa Wanasheria waliojitolea  kutoa msaada wa Kisheria, Georgia  Kamina amesema kuwa wamesaidia makundi mengi ikiwa ni pamoja na kukutana na wananchi.

  Georgia amesema walichojifunza katika kazi walioifanya  ni wananchi kushindwa kujua sheria na jinsi ya kupata haki.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari juu umuhimu wanasheria kujitoa kwa ajili ya kuwatetea wanyonge jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwakilishi wa Wanasheria waliojitolea  kutoa msaada wa Kisheria, Georgia  Kamina.Picha na Emmanuel Massaka,Globu yaj  jami.
   Mwakilishi wa Wanasheria waliojitolea  kutoa msaada wa Kisheria, Georgia  Kamina akizungumza na waandishi wa habari juu msaada wa sheria walitoa kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
   Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.


  0 0

  Wakazi wa Tunduru mkoni Ruvuma na watumiaji wa barabara ya Namtumbo – Tunduru, Tunduru Mangaka wametakiwa kuitunza barabara hiyo ili iweze kudumu na kuweza kutumika kwa vizazi vijavyo. Barabara hiyo ambayo imekamilika kwa asilimia Tisini na tisa na sasa mkandarasi yuko kwenye hatua za kumaliza uwekaji wa alama za barabarani. Wito huo umetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kukagua barabara hiyo.

  0 0

  Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imezikutanisha Asasi za Kiraia zilizopo katika manispaa hiyo kwenye semina ya siku moja iliyolenga kuzijengea uwezo ili ziweze kutekeleza vyema shughuli zao katika kuwaletea maendeleo wananchi.

  Mgeni rasmi katika semina hiyo ya siku moja iliyofanyika katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo katika manispaa ya Shinyanga alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro. 

  Akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo Matiro amezitaka asasi za kiraia (NGO’s,CBO’) kuepuka kuwa sehemu ya kushiriki uovu katika jamii wakitumia mwamvuli wa asasi na kuzitaka kuepuka kuilaumu serikali badala ya kuishauri pale inapokosea. 

  “Serikali inatambua kazi nzuri zinazofanywa na asasi za kiraia katika kuisaidia jamii,nyinyi ni sehemu ya serikali,mnafanya kazi pamoja na serikali kuisaidia serikali,serikali yetu haiwezi kufanya kila kitu,hivyo haipendezi kuilaumu serikali,ishaurini pale mnapoona mambo hayaendi sawa”,amesema Matiro. 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini.Kulia ni Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya
  Mwenyekiti wa semina hiyo Mchungaji Dkt. Meshack Kulwa kutoka TCCIA Shinyanga akimkaribisha mgeni,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ili afungua semina hiyo.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na viongozi wa asasi za kiraia katika manispaa ya Shinyanga.Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Ali Hapi amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha anapeleka Mameneja pamoja na mashine za kielektronic(EFD),kwenye masoko kwa lengo la kudhibiti upotevu wa mapato unaoendelea. 

  Ametoa agizo hilo jana  alipokuwa akisomewa taarifa ya mapato na matumizi ya Masoko na Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama Bi. Elizabeth Minga  ambapo ilionesha upotevu mkubwa wa fedha kwenye masoko hasa soko la wamachinga lililoko Mwenge. 

  Amesema fedha nyingi zinapotea kutokana na kutokuwepo utaratibu mzuri wa kukusanya mapato kwenye masoko. 

  Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya amepiga marufuku uanzishwaji wa vikundi vya kiholela vya kusimamia masoko ili kudhibiti upotevu wa mapato unaoendelea.

  Kijitonyama ni Kata ya nne kati ya Kata kumi za awamu ya pili zinazotembelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo pamoja na utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi.
   Mkuu wa wilaya ya Kinondoni akiongea na Wamachinga wa soko la Mwenge ,Jijini Dares salaam
   Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akiendelea na ukaguzi soko la Mwenge, Jijini Dares salaam  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Baraza la Sanaa nchini (BASATA) limeziomba taasisi za Serikali na mashirika mbalimbali,kununua kazi za Sanaa za uchoraji za wasanii Watanzania na kuacha kununua michoro kutoka nje ambayo haina ubora.

  Hayo yamesemwa na Afisa habari wa Basata, Agnes Kimwaga alipotembelea maonyesho ya wazi ya uchoraji wa michoro mbalimbali yaliyoandaliwa na kundi la 14 + la hapa nchini.

  “Sanaa za uchoraji na uchongaji za hapa nchini zinatengenezwa katika ubora wa hali ya juu, ndio maana michoro mingi inayopelekwa nje kutoka hapa inapata sifa kubwa hivyo ni wakati wa tasisi zetu za umma na ofisi za serikali kuanza kupambwa na michoro hii” amesema Agnes.

  Kwa upande wake kiongozi wa kikundi cha 14 +, Lutengano Mwakisopile amewataka watanzania kuendelea kuwaonga mkono katika harakati zao hili waweze kujivunia sanaa hiyo kama ilivyo kwa nchi jirani.
  Kundi la wasanii wa uchoraji la 14+ ikiwa katika maonyesho ya uchoraji picha katika maeneo ya wazi.
  Msemaji wa kundi la 14 +, Aman Abeid akitoa maelezo kwa afisa habari wa Barza la Sanaa nchini (BASATA) Agnes Kimwaga wakati wa maonyesho hayo
  Mchoraji Nguli wa sanaa za uchoraji, Raza Muhamed akichora wakati wa maonyesho hayo ya uchoraji wa moja kwa moja katika eneo la wazi
  Mchoraji Lutengano Mwakisopile akionyesha ufundi wake wa kuchora katika eneo la busatani ya kaburi moja Posta jijini Dar es Salaam
  Mchoraji Chilonga Haji akionyesha umahiri wake wa kuchora katika maonyesho hayo


  0 0
  0 0

  Msanii wa Filamu na Muigizaji mahiri hapa nchini Steve Nyerere, akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar kuhusiana na mambo mbalimbali yaliyotokea hivi karikuni ,likiwemo suala la ujumbe wa sauti ambao umekuwa ukisambazwa katika mitandano ya kijamii ukimuhusisha yeye Steve pamoja na Mama Wema Sepetu.
  ''Kulikuwa na maongezi ya simu kati ya mimi na mama Sepetu, mimi ndio nilikuwa naogea na mama Sepetu,Maneno yasipindishwe",amesema Steve Nyerere na kuongeza kuwa yeye ana miaka 25 kwenye sanaa, inakuaje leo mtu anatoa ama anasambaza mambo binafsi waliokuwa wakiyazungumza kwa ajili ya kumsaia Mtoto wake.
  Msanii wa Filamu nchini Steve Nyerere, leo amekutana na Waandishi wa Habari, ambapo katika mkutano huo amekanusha kuwa Wasanii nchini hawakidai Chama Cha Mapinduzi fedha kwa ajili ya Mradi wa Mama Ongea na Mwanao, wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

  Katika Mkutano huo STEVE NYERERE amesisitiza kuwa kilichosemwa na WEMA SEPETU kuwa anaidai CCM fedha ni uongo, kwani walilipwa huku akisema Msanii aliyelipwa fedha nyingi katika kazi hiyo ni Wema Sepetu, hivyo anashangaa kusikia akidai kuwa hajalipwa.

  Mradi wa Mama Ongea na Mwanao uliratibiwa na Steven Nyerere huku akisaidiwa na Wema Sepetu na kazi yake ilikuwa ni kutoa elimu kwa wazazi kuwa karibu zaidi na vijana wao wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

  Hata Hivyo, Steve Nyerere, ametumia mkutano huo kukiri kuwa Sauti iliyotumwa kwenye Mitandao ya Kijamii inayohusisha mazungumzo yake na Mama yake Wema Sepetu ni ya kwake, hivyo amewaomba radhi viongozi wote aliowataja katika mazungumzo hayo.

  'Kulikuwa na maongezi ya simu kati ya mimi na mama Sepetu, mimi ndio nilikuwa naogea na mama Sepetu yasipindishwe,"Ile Sauti imekuja kuachiwa juzi wakati watu wanahama chama, kwanini nirekodiwe? naamini wamefanya hivyo makusudi" ,alisema Steve Nyerere

  "Namuomba radhi Rais Magufuli na Chama changu cha CCM, yanaongelewa mengi ninayasikia, naomba radhi familia pia, niliteleza,Nimetaja viongozi katika ile sauti halafu mtu anakuja kuisambaza nimetaja viongozi wa Nchi, Mama alichofanya amenikosea sana,Lakini namuachia Mungu"alimaliza kusema.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agness Kijazi akizungumza leo kwenye warsha ya wanahabari kuhusu mwelekeo wa msimu wa mvua za masika kwa kipindi cha mwezi Machi hadi Mei 2017. Kushoto Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa.
  Mkurugenzi wa TMA, Dk. Agnes Kijazi akiongea pambeni ni sehemu ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa warsha kuhusu mwelekeo wa msimu wa mvua za masika kwa kipindi cha mwezi Machi hadi Mei 2017 iliyofanyika Kibaha, mkoani Pwani.
  Sehemu ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa warsha kuhusu mwelekeo wa msimu wa mvua za masika kwa kipindi cha mwezi Machi hadi Mei 2017 iliyofanyika Kibaha, mkoani Pwani.
  Mkurugenzi wa TMA, Agnes Kijazi (katikati) waliokaa kwenye viti akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari katika Warsha hiyo. Pembeni yake  Kushoto ni Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa na Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Samwel Mbuya (kulia).

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda,Yoweri Kaguta Museveni baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataija wa Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Uganda,Yoweri Kaguta Museveni akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar.

  Makamu wa Rais Mama Samia akimkaribisha Rais wa Uganda,Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege mapema leo kwa ziara ya siku mbili,anaeshuhudia pichani kati ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda,Yoweri Kaguta Museveni wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa.

  Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Masharika,Dkt Augustine Mahiga kwa pamoja wakiwa tayari kumpokea mgeni wao,Rais wa Uganda Yoweri Museveni
  Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika uwanja wa Ndege kumlaki Rais wa Uganda,Yoweri Museveni

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda,Yoweri Kaguta Museveni wakifurahia vikundi vya ngoma za asili vilivyokuwa vikiburudisha mara baada ya Rais huyo kuwasili. 

  0 0  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaomba viongozi wa Dini kuendelea kuamrisha mema na kukataza mabaya, kwani kufanya hivyo kunaipunguzia serikali mzigo.

  RC Makonda ameyasema hayo alipokuwa anafungua semina kwa Walimu wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) na kusisitiza kuwa viongozi wa dini wakiwafundisha mema waumini ambao ndiyo wananchi, Taifa halitakuwa na wahalifu au matukio ya wizi, ujambazi, utumiaji wa dawa za kulevya na ufanyaji wa biashara hiyo, jambo ambalo litaipunguzia gharama serikali ya kuwahudumia waathirika kwa kuwapa vidonge vya Methadone, na serikali haitatumia nguvu kubwa kujenga magereza kwa ajili ya wanaokiuka sheria na taratibu za nchi.

  Na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono viongozi wa dini kwani wanamchango mkubwa kwenye maendeleo ya Taifa hili.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa JUWAQUTA ambaye pia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema kuwa lengo la semina hiyo ni kuwaelimisha walimu hao juu ya kuunga mkono kauli mbiu ya HAPA KAZI TU ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwani kufanya kazi ni agizo kwa mujibu wa dini hiyo ya kiislamu ambapo waumini wake wameambiwa wafanya kazi za halali ili wapate ridhiki halali na siyo vinginevyo.

  Huku akifafanua kuwa hata manabii walikuwa wakifanya kazi hivyo ni vyema kama viongozi kufuata nyayo hizio na kuwaamrisha wengine kufuata utaratibu huo.
  .Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza katika unafunguzi semina ya Walimu wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) leo jijini Dar es Salaam.
  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum akizungumza katika unafunguzi semina ya Walimu wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiombewa dua na viongozi dini, leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Glob ya Jamii. 

  Picha ya Pamoja

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
  Ushindi wa bao 2-1 wa klabu ya Simba dhidi ya mahasimu wao Dar es Salaam Young Africa umeweza kuwaneemesha wafungaji wa Simba, Laudit Mavugo na Shiza kichuya.
  Wachezaji hao ambao waliweza kung’ara katika mchezo huo, walijipatia fedha za kutosha kutoka kwa mashabiki wa mchezo huo ,waliokuwa wakiwatuza fedha mara baada ya mchezo huo kuisha.
  Ushindi wa mchezo huo ameleta shnagwe na furaha kubwa kwa washabiki na kuamua kuwajaza manoti wachezaji hao.
  Mshambuliaji wa Simba , Shiza Kichuya 
  akiokota fedha ambazo amepewa na mashabiki

  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi akitangaza mkusanyiko huo kuwa mahafali ya 20 ya Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) kulia ni Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) Bw. Augustino Nongwe wakati wa mahafali ya 20 ya chuo leo Mjini Morogoro.
   Baadhi ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo
   Mhitimu katika Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) Elias Eliakim akisoma risala kwa Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi ambapo mbali na mambo mengine aliomba viongozi wa Serikali kuweka utaratibu wa kutembelea vyuo vya kati vya uandishi wa habari ili kujenga hamasa kwa wanafunzi.
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi akiongea na wahitimu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) ambapo alisisitiza umuhimu wa wanatasnia ya habari kuwa watendaji na sio waongeaji bila vitendo ikiwa ni moja ya mkakati wa kuikuza tasnia hii na kuendana na Sheria mpya ya Huduma za Habari wakati wa mahafali ya 20 ya chuo leo Mjini Morogoro.
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi akiwapa vyeti vya uhitimu wa Diploma na cheti katika uandishi wa habari waliokuwa wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) 
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja wahitimu,wafanyakazi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) wakati wa mahafali ya 20 ya chuo leo Mjini Morogoro.
  PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.


  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  CHUO Kikuu cha Bagamoyo (UB), kimefanikiwa kutoa falsafa ya kwanza ya Udaktari (PHD), licha ya changamoto ya utoaji elimu katika majengo ya kupanga kwa gharama kubwa.

  Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk. Costa Mahalu kwenye mahafali ya nne yaliyofanyika leo katika viwanja vya chuo hicho, Kawe jijini Dar es Salaam.

  Alisema katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 499 wamefanikiwa kumaliza masomo yao kwenye fani mbalimbali, wanafunzi 45 ngazi ya cheti na Stashahada 47.

  Wengine waliohitimu shahada 334,Shahada ya udhamiri 71 na shahada ya udamivu ni mmoja licha ya uongozi wa chuo hicho kukutana changamoto nyingi ndani ya miaka mitano lakini wanamshukuru mungu kwa hatua hiyo.

  “Namshukuru mungu kwa kutupatia kibali cha kufikia hatua hii ya kufanya mahafali, lakini bado tumekuwa na changamoto ya majengo kwa bado tupo kwenye majengo ya kupanga,” alisema.
  Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, akimtunuku Mtihimu wa kwanza wa Falsafa ya Udaktari (PhD), Fadhil Innocent baada ya kuhitimu katika mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo hicho, Kawe jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk. Costa Mahalu. Kificho alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.
  Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho (katikati), akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk. Costa Mahalu (kushoto) na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho.
  Mgeni rasmi Mheshimiwa Kificho (katikati), akiwa meza kuu na viongozi wengine. Kutoka kulia ni Mkuu wa Chuo cha Sayansi, Dk.Abdillah Chande, Dean Chuo cha Elimu, Dk.Mary Mosha, Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Dk. Costa Mahalu, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dk.William Kudoja na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Jaji mstaafu, Steven Bwana.
  Wahitimu wa shahada ya kwanza katika ngazi mbalimbali wakiwa kwenye mahafali hayo.  0 0  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered (Tanzania), Bw. Sanjay Rughani pamoja na Mwenyekiti wa Uamuzi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Salum Chamawachezaji wakiwa katika picha ya pamoja na timu mbalimbali kabla ya Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Standard Chartered kwa Mwaka 2017 yaliyoanza leo 25/02/2017 katika Viwanja vya JK Youth Park (Kidongo Chekundu) Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered (Tanzania), Bw. Sanjay Rughani pamoja na Mwenyekiti wa Uamuzi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Salum Chamawachezaji wakifanya mazoezi ya pamoja na wachezaji wa timu kabla ya Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Standard Chartered kwa Mwaka 2017 yaliyoanza leo 25/02/2017 katika Viwanja vya JK Youth Park (Kidongo Chekundu) Jijini Dar es Salaam. 


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akipiga mpira kuashiria ufunguzi rasmi wa Mashindano ya Kombe la Standard Chartered kwa Mwaka 2017 yaliyoanza leo 25/02/2017 katika Viwanja vya JK Youth Park (Kidongo Chekundu) Jijini Dar es Salaam. 


older | 1 | .... | 1587 | 1588 | (Page 1589) | 1590 | 1591 | .... | 3283 | newer