Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1586 | 1587 | (Page 1588) | 1589 | 1590 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini (CGP) Dkt. Juma Malewa (katikati) akizungumza katika hafla ya kusaini Mkataba wa Makubaliano (MOU) kwaajili ya Uendelezaji wa Mradi wa Kiwanda cha sukari na shamba la miwa Mbigiri Mkoani Morogoro, uliosainiwa kati ya Jeshi la Magereza na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF kwa pamoja na Mfuko wa PPF, yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam. kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara akizungumza katika hafla ya kusaini Mkataba wa Makubaliano (MOU) kwaajili ya Uendelezaji wa Mradi wa Kiwanda cha sukari na shamba la miwa Mbigiri Mkoani Morogoro, uliosainiwa kati ya Jeshi la Magereza na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF kwa pamoja na Mfuko wa PPF, yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini (CGP) Dkt. Juma Malewa akisainiana mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi wa Muda wa Kampuni ya Mkulazi Holdings Co. Ltd, Nicander Kileo huku wakishuhudiwa na Wakurugenzi wa NSSF (Prof. Godius Kahyarara) na PPF (William Erio), katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. 
  Picha ya pamoja na Watendaji wakuu wa Mifuko hiyo ya NSSF na PPF.
  Picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Magereza.

  0 0

  Wananchi wa Nakapanya, wilayani Tunduru mkoani Ruvuma  wameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Nakapanya-Tunduru yenye urefu wa KM 66.5 ambayo imekamilika  kwa asilimia  Tisini na tisa na sasa mkandarasi yuko kwenye hatua za kumaliza uwekaji wa alama za barabarani.

  Wakieleza furaha yao kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kukagua barabara  hiyo, wananchi hao wamesema kuwa uwepo wa barabara hiyo umechochea maendeleo makubwa katika mkoa huo na mikoa ya jirani.  "Tunaishukuru sana Serikali kwani  imesikia kilio chetu cha miaka mingi cha kuomba kujengewa barabara ya lami katika wilaya yetu, sasa tunafurahia matunda ya ujenzi huu", amesema Bw. Mohammed Ally.  Kwa upande wake, Waziri Prof. Mbarawa amewataka viongozi wa Wilaya hiyo na kamati za ulinzi na usalama kuhakikisha wanawasimamia wananchi katika kuitunza na kuilinda miundombinu ya barabara hiyo ili iweze kudumu na kuweza kutumika kwa vizazi vijavyo.  Ameongeza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kumeufungua mkoa wa Ruvuma na wilaya zake pamoja na mikoa jirani ya Mtwara na nchi ya Msumbiji, hivyo kuchochea fursa za kibiashara kwa kiasi kikubwa.  Kuhusu huduma za mawasiliano  mkoani humo, Waziri Mbarawa amesema kuwa Wizara yake itahakikisha inapeleka mawasiliano haraka iwezekanavyo katika maeneo yenye changamoto hususan vijijini.  Naye, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Juma Homera amemhakikishia Waziri huyo kuwa  atashirikiana kwa ukaribu na viongozi wenzake katika kutekeleza maagizo yote aliyowapa ikiwemo la ulinzi wa miundombinu ya barabara hiyo.  Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Ruvuma amemuhakikishia Waziri Prof. MBARAWA  kuwa Wakala utatatua changamoto zote zilizojitokeza wakati wa ujenzi wa barabara ikiwemo fidia kwa wananchi waliovunjiwa nyumba zao kupisha barabara hiyo.

   Muonekano wa barabara ya Nakapanya-Tunduru KM 66.5 iliyokamilika kwa kiwango cha lami, mkoani Ruvuma.
   Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Ruvuma Eng. Lazeck Alinanuswe (mwenye koti la kaki), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto kwa Meneja), ujenzi wa kingo za Daraja la Lumesule lililopo mpakani mwa mkoa wa Ruvuma na Mtwara wakati alipokagua daraja hilo.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisikiliza maoni kutoka kwa Bw. Mohammed Ally mkazi wa Nakapanya, Wilayani Tunduru, Mkoani Ruvuma kuhusu furaha yao juu ya kukamilika kwa ujenzi wa Barabara ya Nakapanya-Tunduru KM 66.5.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), picha ya barabara ya Nakapanya-Tunduru KM 66.5 iliyokamilika kwa kiwango cha lami wakati alipokuwa akikagua barabara hiyo, mkoani Ruvuma. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Juma Homera.
   Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu Mhe. Dua Nkurua (kushoto), akisisitiza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), mara baada ya kuzungumza na uongozi wa wilaya hiyo, mkoani Mtwara.
   Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Juma Homera (mwenye koti la kaki), akimuonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto kwa Mkuu wa Wilaya), moja ya ofisi katika jengo jipya la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya huyo, alipoikagua Wilayani humo.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiongea na uongozi wa Wilaya ya Tunduru, mara baada ya kukagua miradi iliyo chini ya Wizara hiyo.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akifurahi jambo na wafanyakazi wa kampuni ya Korosho, Wilayani Tunduru mara baada ya kutembelea na kuangalia uzalishaji wa korosho katika kiwanda hicho.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0


  Katoni ya Sukari feki ikiwa mezani ili kuonyeshwa kwa waandishi wa Habari na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya
  Operesheni ya aina yake iliyofanyika maeneo ya kibiashara ya Mwanjelwa na Kabwe Jijini Mveya ikisimamiwa na maofisa wa WMA (Wakala wa Vipimo) imeibua mengi na mazito hasa kukamatwa kwa zaidi ya Tani mbili za sukari iliyochakachuliwa kuanzia Uhalali wa kuuzwa na hata Vipimo vyake.
  Akiongea mbele ya Viongozi wa Mkoa na Wilaya kama Mkuu wa Mkoa Mhe.Amos Makalla na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Mhe.William Paul Ntinika
  Afisa Vipimo Bw.Deogratias M.Hussein Amesema mambo makuu waliyobaini kwenye Msako kuwa kuna Sukari wameona kwanza Kiwanda kitengenezacho hakitambuliki kisheria,hazina nembo ya ubora ya TBS na kuhusu ujazo ni tofauti.
  Amesema wafanyabiashara hao wameichakachua sukari iitwayo ILLOVE wao mifuko yao imeandikwa LILLOVE na ALLOAVE ambapo katoni ya kilogramu 10 ilipimwa na kukutwa ni kilogramu 7 hivyo walaji wanaibiwa.
  Jumla ya watu 14 walikamatwa na kulipishwa faini Jumla ya Shilingi Millioni 9.4.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Amos Makalla akionyeshwa sukari feki nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Mkapa na Afisa Vipimo kutoka Wakala wa Vipimo WMA.
  Huu ni moja ya Mfuko wa Sukari ambazo hazitambuliki na TBS na Ujazo wake ni mdogo.
  Afisa Vipimo Bw.Deogratias M.Hussein kulia akizungumzia Sakata la hiyo sukari mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Mhe.William Paul Ntinika wa kwanza kushoto pamoja na Katibu wa Umoja wa Vijana CCM Wilaya ya Mbeya Mjini Bw.Kiwairo.

  0 0

  Kampuni ya Resolution Insurance imekabidhi rasmi mchango wao kwa Kawe Jogging Club kuweza kushiriki mashindano ya Kili Marathon yatakayo fanyika Tarehe 26 Februari 2017. Mchango huu ulikua ni mwitiko kwa ombi la klabu hiyo kuweza kushiriki mashindano ya Kili Marathon. 

  Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Resolution Insurance, Bi. Maryanne Mugo alisema kuwa mchango huo upo ndani ya vipaumbele vya kampuni katika uwekezaji jamii hasa katika sekta ya afya. 

  Resolution Insurance inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalengo maeneo ya vipaumbele vya Elimu, Afya, Mazingira, Ujasiriamali na malengo yake hasa ni kujikita katika masuala ya ubinadamu.” Bi. Maryanne alisema na kubainisha kwamba hii ni mara ya pili wanaidhamini Kawe Jogging Club kushiriki mashindano hayo na inawahimiza wananchi kwa ujumala kujihusisha na mazoezi kwa ajili ya kuwa na afya njema. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Resolution Insurance Maryanne Mugo (kushoto), akikabidhi tishirt ya jersi kwa Katibu Mkuu wa Kawe Jogging Club Bw. Al Haj Seif Muhere, ikiwa ni moja ya vivaa vilivyotolewa na kampuni hyo kwa ajili ya kuwawezesha klabu hiyo kuweza kushiriki mashindano ya Kili Marathon. Pamoja nao kwenye picha ni Diwani wa Kawe Mheshimiwa Muta Rwakatare (wapili kushoto) na Mwenyekiti wa Kawe Jogging club Bw. Abdul Risasi 
  Katibu Mkuu wa Kawe Jogging Club, Al Haj Seif Muhere (wa kwanza kushoto) akitoa shukrani kwa Kampuni ya Resolution Insurance kwa niaba ya klabu yake. 
  Diwani wa Kawe, Mheshimiwa Muta Rwakatare akiongea na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa walivyodhamini Kampuni ya Resolution Insurance kwa Kawe Jogging Club. Mheshimiwa Diwani alitoa shukrani kwa kampuni hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Resolution Insurance, Maryanne Mugo (wa kwanza kushoto), Ofisa masoko wa kampuni ya Resolution Insurance, Laura Lyabandi (wanne kushoto), Meneja mauzo wa kampuni ya Resolution Insurance Nilufar Manalla (watano kushoto), Meneja wa wakala wa kampuni ya Resolution Insurance (njuma) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Diwani wa Kawe mheshimiwa Muta Rwakatare (wapili kushoto) na baadhi ya washiriki kutoka Kawe Jogging Club watakao shiriki kwenye mashindano ya Kili Marathon.
  0 0

  Above are the panelists during an open discussion from guests and panelists discussing the topic “Challenges and solutions of renewable Energy and energy efficiency sector in Tanzania”, the panel was moderated by Mr. David Sacotte at the center with other panelists that included: Emmanuel Baudarn (AFD Tanzania Representative), Mr. Kumar Krishan (Chairman CTI), Ms. Davikarani Williams (Head of Enterprise Banking BANK OF AFRICA – TANZANIA) Halfan Swai (Director Baobab school, Kemilembe Kafanabo (Principal Financial Analyst EWURA), Styedean Rwebangila (Moem Acting Assitant Commissioner (New and renewable Energy).
  Ms. Davikarani Williams (Head of Enterprise banking, BANK OF AFRICA – TANZANIA) at the center answering a question during the panel discussion at the luncheon event (SUNREF East Africa).
  Audience during the workshop at Serena Hotel on 24th February 2017 at Serena Hotel Dar es salaam, the main topic of discussion was the role of AFD/SUNREF in highlighting the challenges and solutions of renewable energy and energy efficiency in Tanzania.
  Mr Emmanuel Baudran (AFD Country Representative) giving a speech during the luncheon event.
  H.E. Mr. Roeland Van De Geer (Head of Delegation of the European Union) giving a speech during the opening of the renewable energy and Energy efficiency workshop at Serena Hotel.


  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze

  Waziri wa biashara, Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, amezitaka taasisi zinazohusika na uwekezaji kutokuwa na ukiritimba ili hali kufikia malengo ya serikali ya kukuza sekta ya viwanda.

  Aidha ameeleza kwamba, wizara hiyo, imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji ambayo yatawezesha kuvutia wawekezaji wa ndani na nje.
  Hayo aliyasema huko kitongoji cha Pingo Chalinze,Bagamoyo,wakati akiweka jiwe la msingi kwenye kiwanda cha Vigae cha Twyford Ceramics Ltd.

  Mwijage alisema, uwekezaji huo unaendana na dhana ya Rais Dk John Magufuli wa kuifanya nchi kuwa ya Viwanda .Alisema kwa kuanzishwa viwanda vingi vya aina hiyo kutasaidia kuongeza pato la nchi na kuzalisha ajira kwa wingi.

  “Zipo idara ambazo zinafanikisha uwekezaji ikiwemo brela, idara ya uhamiaji, kazi, mamlaka ya mapato TRA, wizara ya ardhi, shirika la viwango TBS, baraza la Mazingira NEMC ambazo zinapaswa kufanya kazi kwa wepesi ili kufanikisha uwekezaji,” alisema Mwijage.
  Ramani ya kiwanda
  Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Magid Mwanga ,wa pili kushoto mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo na Jack Feng mkurugenzi wa kiwanda, wa tatu kushoto ni waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage na Ridhiwan Kikwete na Cliford Tandari wakiweka udongo kwenye jiwe la msingi.(picha zote na Mwamvua Mwinyi)


  0 0  0 0  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Mbunge wa Jimbo la Ileje, Janet Mbene amewatoa hofu wakazi wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kutokuwepo kwa ujenzi wa barabara na kusema kuwa muda wowote kuanzia sasa Barabara ya Isongole Mpemba itaanza kujengwa.

  Akizungumza na wakazi wa Ileje alipokuwa akijibu maswali kupitia mtandao wa kijamii wa Whats up, Mbene amesema kuwa Sasa hivi Evaluation ya tenda documents imemalizika.

  “Wamemaliza kupitia makabrasha ya 'Tender' wanaendelea na majadiliano na Mkandarasi juu ya gharama na vipengele mbalimbali, na watamtangaza Mkandarasi muda si mrefu kabla ya Mwezi wa Sita kama nilivyoelezwa na meneja wa Tanroads mkoa wa Mbeya” amesema Janet Mbene.

  Barabara hiyo ya Mpemba-Isongole ni moja ya barabara ambazo zipo katika ahadi ya Rais John Pombe magufuli hivyo muda si mrefu wakazi wa Wilaya ya Momba na Ileje wataunganishwa katika barabara hiyo.

  Ujenzi wa barabara hiyo utaweza kuinua fursa za kiuchumi katika Wilaya ya Ileje hasa kufungua biashara za mipakani kati ya nchi ya Tanzania na Malawi.

  0 0

  Wakili wa utetezi, katika kesi ya mauaji ya inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita, Peter Kibatala ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa haina mamlala ya kisikiliza kesi hiyo kwa kuwa washtakiwa walishaachiwa huru.Kibatala amedia kuwa kitendo cha Mahakama hiyo kusikiliza kesi ambayo Jana watuhumiwa waliachiwa huru ni sawa na kuichonganisha Mahakama na kufanya maamuzi ya Hakimu aliyewaachia huru kuonekana hapana maana. 

  Jana, Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa wa Mahakama hiyo aliwachia huru Mrita anayeshtakiwa pamoja na Revocatus Muyela baada ya upande wa mashtaka kushindwa kutekeleza amri ya mahakama iliyowataka kurekebisha hati ya mashtaka kwa kuwa inamapungufu.Hata hivyo, washtakiwa hao walikamatwa tena jana hiyo hiyo na jeshi la polisi na kisha Leo asubuhi wamepandishwa mahakamani hapo kusomewa upya tuhuma za mauaji ya Aneth.

  Katika kesi hiyo, mshtakiwa Mrita anadaiwa kumuua wifi yake Aneth Msuya akishirikiana na Revocatus Muyela.Inadaiwa kuwa mauaji hayo yalifanyika Mei 25, mwaka Jana huko Kibada Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

  Mata baada ya kusomewa tuhuma hizo za mauaji, washtakiwa hawakutakiwa kujibu kitu kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji ambazo zinasikilizwa Mahakama Kuu.
  Kabla upande wa jamuhuri haujasoma kesi hiyo Wakili Kibatala aliiomba mahakama kutoyasikiliza mashtaka hayo kwa kuwa Kisutu haina mamlaka.

  Lakini Hakimu Thomas Simba aliwaamuru upande wa mashtaka kuisoma kwanza kesi hiyo ndipo awasikilize hoja zao.Mara baada ya kusomewa tuhuma zao na kutotakiwa kujibu kitu, ndipo Kibatala alipoibuka na hoja hizo ambazo zilipingwa na upande wa Jamuhuri.Akijibu Hoja hizo, wakili wa serikali mkuu, Mutalemwa Kishenyi alidai kuwa uamuzi wa Hakimu Mwambapa kuwaachia huru washtakiwa hao uliishia hapo hapo.

   Mke wa aliyekuwa Bilionea Erasto Msuya na mwenzake Revocatus Muyela wakiwa mahakamani wakisubiri kusomewa mashtaka yao mapya ya mauaji baada ya Jana kuachiwa huru na kisha kukamatwa tena.   
  Mrita na mwenzake wanatuhumiwa kumuua kwa kukusudia Aneth Msuya ambaye ni Dada wa Marehemu wa Bilionea Msuya 
  Washtakiwa hao wakijadili jambo na wakili wao Peter Kibatala(wa pili kutoka kushoto).

  0 0  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akiongoza kikao cha ndani kilichoshirikisha Idara zilizopo ndani ya wizara.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam
  Kamishna wa Jeshi la Magereza Divisheni ya Utawala na Fedha,Gaston Sanga, akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, wakati wa kikao cha ndani kilichoshirikisha Idara zilizopo ndani ya wizara.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kamishna wa Fedha Jeshi la Polisi Albert Nyamuhanga.
  Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke na Afisa Tawala wa Idara hiyo,Jenita Ndone(Kulia), wakifuatilia kwa makini kikao cha ndani cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Regasira (hayupo pichani) .Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.
  Maafisa kutoka idara ya Uhamiaji wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(hayupo pichani) wakati wa kikao cha ndani kilichoshirikisha Idara zilizopo ndani ya wizara. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

   Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz Mikomangwa (kushoto) akila Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela leo jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz Mikomangwa akiweka saini katika Hati ya Kiapo cha Uadilifu leo jijini Dar es Salaam. Anayeshuduia kulia ni Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela leo jijini Dar es Salaam.
   Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela akimkabidhi Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa umma Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz Mikomangwa (kushoto).
   Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Ally Malewa(kushoto) akila Kiapo cha Uadilifu mbele ya Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela leo jijini Dar es Salaam.
   Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Ally Malewa(kushoto) akiweka saini katika Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa umma leo jijini Dar es Salaam. Anayeshuduia ni Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela leo jijini Dar es Salaam.
  Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela akimkabidhi Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa umma Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Ally Malewa.

  Picha zote na: Frank Shija - MAELEZO.

  0 0

  Mwakilishi wa Timu ya Wataalamu wa Afya kutoka China nchini Tanzania , Bwana Song Tao ametoa msaada wa Sh 100,000 kwa Neema Wambura (32) mkazi wa Kijiji cha Kyagata wilayani Tarime mkoani Mara ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbil. Neema amelazwa katika hospitali hiyo baada kumwagiwa uji wa moto na mume wake. Jana Rais John Pombe Magufuli alimpatia sh500,000 na kuahidi kumpatia hifadhi pamoja na watoto wake watatu.

  0 0

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna Charles Mkumbo


  Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

  Jeshi la Polisi mkoani hapa limewataka wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari zote katika kipindi hiki cha Masika. Akizungumza na waandishi wa habari mchana wa leo ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna Charles Omari Mkumbo alisema katika kipindi hiki cha mvua wananchi hawatakiwi kuvuka mito na mabonde yenye maji kwa hisia badala yake wanatakiwa wawe na subira.

  “Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha katika kipindi hiki cha masika hamtakiwi kujipa ujasiri na kuyakadiria maji ya mvua hivyo zinahitajika tahadhari za kutosha dhidi ya watoto, au vyombo vyovyote vya usafiri kwani maji hayo huwa yanakwenda kwa kasi, yasubirini yapite acheni hisia ili kuhakikisha maisha yenu hayahatarishwi na mvua”. Alisisitiza Kamanda Mkumbo.

  Kamanda Mkumbo alitoa wito huo baada ya jana usiku kunyesha mvua kubwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu na kusababisha vifo vya watu saba. Alisema katika tukio la kwanza jana Usiku wa saa 4:00 katika kijiji cha Kimbolo kata ya Enaboishu wilayani Arumeru, watu watano wote wakazi wa kijiji cha Kyoga walifariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Premio lenye namba za usajili T 579 BSG kusombwa na maji.  0 0

  KATIKA moja ya mambo ambayo serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa rais dokta John Magufuli inasisitiza kuyafanya ni kwa viongozi kushuka kwa wananchi kwa kuwatembelea ,kusikiliza kero zao na kuzitatua.

  Ili kulitekeleza hilo mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu ameitenga siku ya alhamisi ya kila wiki kuhamishia ofisi yake kwenye tarafa maalum kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi kutoka kwa wahusika.

  Alhamisi hii akiwa ameweka kambi tarafa ya Ihanja wilayani humo Mtaturu amemuagiza kaimu mkurugenzi wa wilaya hiyo Haika Massawe kumuelekeza mwanasheria wa halmashauri kutoa msaada wa kisheria kwa Fatma Mohammed ambaye anasumbuliwa kupata haki yake ya ardhi.

  Mama huyo anafuatilia shamba la baba yake mzazi ambaye ni mzee na anaumwa lililovamiwa na mtu bila ya mafanikio pamoja na kwamba alishinda kesi katika baraza la kata na wilaya lakini alikatiwa rufaa mahakama ya rufaa ya Dodoma.

  “Mkurugenzi fuatilia kwa mwanasheria ilia toe msaada wa kisheria,kesi hii imeelekezwa na jaji wa mahakama ya rufaa ya Dodoma kuwa kuna makosa yamefanyika kwenye baraza la kata huku,”alisema Mtaturu.
  Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akimkabidhi mashuka Dk. Frank kwa ajili ya kituo cha afya cha Ihanja wakati akiwa katika ziara ya kukagua huduma zinazotolewa kituoni humo na kusikiliza kero za wananchi.
  Dk. Frank wa kituo cha afya cha Ihanja akitoa maelezo mbele ya mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu na diwani wa kata ya Kituntu Said Tumbwi wakati walipofika kituoni hapo.
  Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akikagua shamba la mtama la mwananchi wa kijiji cha Puma ikiwa ni muendelezo wa ziara yake aliyoifanya katika tarafa ya Ihanja.


  0 0

  Viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe za Uzinduzi wa Uwekaji wa jiwe la msingi wakiweka udongo kwenye jiwe la msingi kuashiria uzinduzi huo. Sherehe za Uzinduzi huo zilifanyika eneo la mradi huko Chalinze.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akihutubia wageni waliohudhuria Uwekaji wa Jiwe la Msingi wa Kiwanda cha Twyford Ceramic Tiles. Mh. Mwijage alisema Viwanda Vikubwa ambavyo vitatoa ajira na kuongeza pato la taifa vitajengwa na Watanzania watarajie mengi zaidi katika utekelezaji wa Agenda ya viwanda ii kuleta maendeleo kwa Taifa.
  Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Evarist Ndikilo akitoa machache wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa kiwanda cha Twyford Ceramics Tyles na kusisitiza anayependa kushuhudia ujenzi wa viwanda atembelee Mkoa wa Pwani kwani hapo ndiyo mahala ujenzi wa viwanda vingi unapofanyika.
  Picha ikionyesha wananchi wa Chalinze waliofika kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Vigae cha Twyford Ceramic Tiles. Wananchi hao waliongozwa na Mbunge wao wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete.
  Picha ya pamoja ikimuonyesha Ndugu Clifford Tandari Kaimu Mkurugezni wa Kituo cha Uwekezaji, Ndugu Majjid Mwanga, Mkuu wa Wilaya ya Chalinze, Mh. Evarist Ndikilo Mkuu wa Mkoa wa Pwani, MhCharles Mwijage, Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, Ndugu Jacq Feng Mkurugenzi wa Kiwanda cha Twyford Ceramic Tiles, Mh Ridwani Kikwete Mbunge wa Chalinze kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi. Nyuma ni taswira ya jinsi ambavyo kiwanda kitakavyokuwa mara baada ya ujenzi kukamilika.

  0 0

   Mhe. Dkt. James Alex Msekela, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa Geneva na Vienna akiwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nguvu za Nyuklia Duniani (International Atomic Energy Agency –IAEA) Bw. Yukiya Amano huko mjini Vienna leo 24 Februari, 2017
   Mhe. Dkt. James Alex Msekela, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za Umoja  wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa Geneva na Vienna  akiwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mkurugenzi Mkuu Ofisi za Umoja wa Mataifa Vienna  Bw. Yury Fedotov leo 24 Februari, 2017
   Mhe. Dkt. James Alex Msekela, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa Geneva na Vienna akiwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Katibu Mkuu Shirika la Kuzuia Majaribio ya Silaha za Nyuklia Duniani (Comprehensive Nuclear Test Ban Treaty Organization-CTBTO) Bw. Lassina Zerbo leo  23 Februari, 2017
  Mhe. Dkt. James Alex Msekela, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ofisi za Umoja  wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa Geneva na Vienna  akiwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mkurugenzi Mkuu Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda Duniani (United Nation Industrial Development Organization - UNIDO) Bw. LI Yong leo  23 Februari, 2017.

  0 0


  0 0


  0 0

  Kiwanja cha ndege cha Dodoma, sasa kinauwezo wa kupokea ndege zenye uwezo wa kubeba abiria 90, baada ya kurefushwa kwa barabara ya kutua na kuruka kwa ndege kwa kilometa 2.5.

  Ndege ya Shirika la ndege la Tanzania (ATCL), leo ikitua kwenye kiwanja cha ndege cha Dodoma ikitokea mkoani Kigoma.
  Mizigo ya abiria wa ndege ya shirika la ndege Tanzania (ATCL), ikiwa ndani ya gari la kampuni inayotoa huduma ya mizigo ya National Aviation Services (NAS), kwenye Kiwanja cha ndege cha Dodoma.
  Mkuu wa Dodoma (kushoto) Mhe. Jordan Rugimbana akielekea kupanda ya ATCL akiwa ni mmoja wa abiria akitokea kwenye Kiwanja cha ndege cha Dodoma na kuelekea Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). Kulia ni Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mlungwana.
  Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mhe. Jordan Rugimbana (kulia) akiagana na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma, Bw. Julius Mlungwana kabla ya kupanda ndege ATCL, akielekea Jijini Dar es Salaam, leo.
  Wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Uwela ya kitongoji cha Kikuyu mkoani Dodoma wakiwa katika ziara ya mafunzo kwenye Kiwanja cha ndege cha Dodoma, leo.

older | 1 | .... | 1586 | 1587 | (Page 1588) | 1589 | 1590 | .... | 3286 | newer