Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

DC SHINYANGA ATOA MBINU KWA WANAWAKE KUJINASUA NA MFUMO DUME

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ametoa mbinu kwa wanawake kujinasua na mfumo dume kwa kuachana na tabia tegemezi, ambayo husababisha kukithiri kwa manyanyaso kwao kutoka kwa waume zao.
Amewataka wajikite kwenye vikundi vya ujasiriamali ambavyo vitawaondoa kwenye mfumo huo kwa kujikwamua kiuchumi. 
Matiro ameyasema leo mjini Shinyanga wakati wa hafla fupi ya ugawaji baiskeli 36 kwa wawezeshaji elimu ya ujasiriamali kutoka shirika lisilo la kiserikali (Rafiki-Sido ) mkoani Shinyanga linalojihusisha na mradi wa uwezeshaji wa vijana wa kike hususani wanaoishi katika mazingira magumu ili kuwainua kiuchumi. Habari kamili BOFYA HAPA

VIONGOZI WILAYANI HAI MKOANI KILIMANJARO WAKUNA VICHWA KULINUSURU ZIWA BOLOTI NA MAZINGIRA YAKE.

$
0
0
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Hai  Bw. Yohana Sintoo (wa kwanza kushoto),Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Gelasius Gasper Byakanwa (katikati) wakimsikiliza Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Mhe. Upendo Wela akitoa maelezo wakati wa makubaliano ya kila mtu kupanda miti ikiwa ni pamoja na viongozi wa Dini zote  kutokana na hali halisi ya uharibifu wa mazingira katika ziwa Boloti. Kwa habari zaidi za wilaya ya Hai tembelea blog yao: BOFYA HAPA

KAMPUNI YA KUFUGA SUNGURA YA "THE RABBIT BLISS" SASA YAHAMIA JIJINI DAR

$
0
0

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Rabbit Blill inayohusika na ufugaji wa kisasa wa Sungura pamoja na uuzaji wake, Payas Ruben akizngumza na Ripota maalum wa Globu ya Jamii alietembelea makao makuu mapya ya Kampuni hiyo, yaliyopo eneo la Majohe, jijini Dar es salaam. Kampuni hiyo hivi sasa ipo Dar es salaam ikitokea Jijini Arusha kulikokuwa na makazi yake ya awali baada ya mmiliki wa sasa kununua hisa zote zilizokuwa zikimilikiwa na mmiliki wa awali. Akizungumza katika eneo hilo, Bw. Ruben alisema kuwa ufugaji wa Sungura ni mzuri sana na unafaida kubwa kwa mfugaji, kwani unaweza kumuingia kipato kikubwa kama atazingitia taratibu zote za ufugani, hivyo ametoa wito kwa wale wote wanaotaka kufuga au kujifunza ufugaji wa Sungura wasisite kufika kwenye ofisi zao zilizopo Majohe, Jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Rabbit Blill inayohusika na ufugaji wa kisasa wa Sungura pamoja na uuzaji wake, Payas Ruben (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mwena wa Kampuni hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Rabbit Republic ya nchini Kenya, Moses Mutua wakati wakimuangalia mmoja wa Sungura anaefugwa kisasa katika Shamba ya Sungura, lililopo Majohe, jijini Dar es salaam.
 Sehemu ya Mabanda ya kisasa kabisa ya kufugia Sungura.
 Baadhi ya Sungura wanaofugwa na Kampuni ya The Rabbit Blill.
 Moses Mutua a.k.a Mr. Rabbit akiwa kabeba mabox maalum ya Sungura wanaokuwa katika hali kuzaa.

FARMERS MARKET DAY @ OYSTERBAY SHOPPING CENTRE

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN ANOGESHA SHEREHE SIKU YA NILE

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu akizungumza wakati wa sherehe za Siku ya Mto Nile leo Jijini Dar es Salaam. Sherehe hizo zimeshirikisha takribani nchi 1o zinazozunguka mto Nile zikiwa na kauli mbiu “Mto wetu wa pamoja Nile – Chanzo cha Nishati, Chakula na Maji kwa Wote”
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Tanzania Mhandisi Gerson Lwenge akizungumza wakati wa sherehe za Siku ya Mto Nile leo Jijini Dar es Salaam. Sherehe hizo zimeshirikisha takribani nchi 1o zinazozunguka mto Nile zikiwa na kauli mbiu “Mto wetu wa pamoja Nile – Chanzo cha Nishati, Chakula na Maji kwa Wote”
 Waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Nne Profesa Mark Mwandosya akielezea umuhimu wa Mto Nile wakati wa sherehe za Siku ya Mto Nile leo Jijini Dar es Salaam. Sherehe hizo zimeshirikisha takribani nchi 10 zinazozunguka mto Nile zikiwa na kauli mbiu “Mto wetu wa pamoja Nile – Chanzo cha Nishati, Chakula na Maji kwa Wote”

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu akipokea maandamano mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa sherehe za Siku ya Mto Nile leo Jijini Dar es Salaam. Sherehe hizo zimeshirikisha takribani nchi 10 zinazozunguka mto Nile ambazo ni pamoja na Kenya, Uganda, Burundi, Sudan, South Sudan, DR-Congo,Ethiopia, Rwanda, Misri na mwenyeji Tanzania. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula.
 Waandamanaji wakipita mbele ya Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu(hayupo pichani) huku wakipunga mkono walipokuwa wakiwasili katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere leo Jijini Dar es Salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA



MKUU WA MKOA WA KIGOMA BRIGEDIA JENERALI MAGANGA ATEMBELEA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Maganga (kati) akimsikiliza Afisa Suleiman Saleh (kulia) leo Jumatano Feb 22, 2017 Mhe. Mkuu wa mkoa wa Kigoma alipotinga Wiazani hapo kuwasabahi maswahiba wake waliowahi kutumikia pamoja miaka ya nyuma kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Kushoto ni mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika Wizara hiyo Bi. Mindi Kasiga.
Kutoka Kushoto ni mkuu wa kitengo cha mawasiliano Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Affrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga, Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Maganga na Afisa Suleman Saleh wakiwa katika picha ya pamoja.

VIFAA VYA OFISI VYA WATUMISHI WA MALIASILI WANAOHAMIA DODOMA AWAMU YA KWANZA VYASAFIRISHWA LEO

$
0
0
 Moja ya gari la jeshi lililokuwa limebeba vifaa vya ofisi vya watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii likiondoka rasmi makao makuu ya wizara hiyo leo kuelekea mjini Dodoma. (Picha na Hamza Temba - WMU)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiaga msafara wa magari yaliyobeba vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa wizara hiyo wanaohamia Makao Makuu ya Nchi Mjini Dodoma nje ya jengo kuu la Wizara hiyo (Mpingo House) Jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Hamza Temba - WMU)

DC MTATURU ATOA MWEZI MMOJA WAFANYABIASHARA WA ASALI KANDO YA BARABARA SINGIDA-DODOMA KUHAMIA JENGO JIPYA.

$
0
0

MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu ametoa mwezi mmoja kuanzia leo kwa wafanyabiashara wote wanaouza asali pembezoni mwa barabara kuu ya Singida-Dodoma kuhamia katika jengo lililojengwa na serikali ili kuongeza thamani na kurahisha upatikanaji wake.


Akizungumza katika uzinduzi wa vifungashio vya asali uliofadhiliwa na wakala wa misitu Tanzania(TFS)leo katika kijiji cha Issuna A wilayani humo Mtaturu amesema serikali iliwekeza kwa makusudi katika jengo hilo ili kuwainua wazalishaji wa asali lakini ni zaidi ya miaka mitatu sasa toka likamilike na halijaanza kutumika.

“Kauli mbiu yetu ni asali bora, maisha bora na hii inaenda sambamba na mikakati ya serikali katika kuboresha maisha ya wananchi na dira ya maendeleo ya Taifa 2025 lakini pia inaunga mkono Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 iliyoahidi kuendeleza program ya ufugaji nyuki ili kuwajengea uwezo wadau,”alisema Mtaturu.

Aliwapongeza TFS kwa juhudi zao katika uhifadhi wa misitu na kutoa mafunzo kwa kamati za mazingira karibu vijiji vyote wilayani humo lakini pia kwa hatua yao ya kuleta vifungashio na kwa wadau kuendelea na ushirikiano waliouonyesha.

Alisema vifungashio hivyo vitatumika kufungashia asali bora ya Ikungi na hivyo kuondokana na vifungashio ambavyo vimezoeleka ambavyo kiafya sio salama huku akiwaasa wazalishaji na wafanyabiashara kuwa pamoja ili kupata fursa mbalimbali na kuboresha uzalishaji wenye tija zaidi kiuchumi.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akionyesha moja ya kifungashio bora cha asali katika uzinduzi wa vifungashio hivyo.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akizungumza na wadau wa asali wakiwemo wazalishaji na wafanyabiashara katika uzinduzi wa vifungashio vya asali wilayani humo.
Mkurugenzi wa wilaya ya Ikungi Rustika Turuka akitoa salam kwenye uzinduzi wa vifungashio vya asali uliofanyika katika kijiji cha Issuna wilayani humo.


NHIF YAKUTANA NA WADAU NA KUAHIDI UBORESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA MKOANI GEITA

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi NHIF na Spika mstaafu wa Bunge mama Anna Makinda akisisitiza juu ya kuboreshwa huduma katika mfuko wa Bima ya afya wa Taifa. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akifungua mkutano wa wadau wa Mfuko wa Bima wa Taifa Mkoani Humo.
Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo wakisikiliza taarifa ya utekelezaji wa shughuli za NHIF.
Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Angela Mziray akifafanua namna ambavyo NHIF imekuwa ikisaidia wa gonjwa wenye magonjwa yasiyoambukiza.
Meneja wa NHIF Mkoani Geita Mathias Sweya akielezea namna ambavyo shughuli za kuandikisha wanachama wapya jinsi zikifanyika Mkoani Geita .
Wajumbe wakiendelea kufatilia mkutano.

KAIMU MKUU WA MKOA WA TANGA AIPONGEZA TAYODEA KWA KUSAIDIA KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa uzinduzi wa akibadhi vifaa vya vijana wa mradi wa WEKEZA (Wezesha Ustawi Endelevu kiwango cha Elimu Kuzuia Ajira kwa watoto) kulia ni Mkurugenzi wa Tayodea, David Chanyegea na kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga, Faidha Salim.
Mkurugenzi wa Tayodea, David Chanyege akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza kushoto akionyeshwa baadhi ya vifaa vya ushonaji waliokabidhiwa vijana kupitia mradi wa WEKEZA.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MBUNGE WA JIMBO LA ILEJE AMTEMBELEA NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI OFISINI KWAKE JIJINI DAR

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Ileje, mkoani Songwe Janeth Mbene, wakati Mbunge huyo alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya Jimbo lake la Ileje.
Mbunge wa Jimbo la Ileje mkoani Songwe, Janeth Mbene (kushoto) akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati Mbunge huyo alipomtembelea Naibu Waziri huyo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo lake la Ileje.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkaribisha Mbunge wa Jimbo la Ileje mkoani Songwe, Janeth Mbene, ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya Jimbo lake la Ileje. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MICHUZI TV: KAMPUNI YA KUFUGA SUNGURA YA THE RABBIT BLISS SASA YAHAMIA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Rabbit Blill inayohusika na ufugaji wa kisasa wa Sungura pamoja na uuzaji wake, Payas Ruben akizangumza na Ripota maalum wa Globu ya Jamii aliyetembelea makao makuu mapya ya Kampuni hiyo, yaliyopo eneo la Majohe, jijini Dar es salaam. 
Kampuni hiyo hivi sasa ipo Dar es salaam ikitokea Jijini Arusha kulikokuwa na makazi yake ya awali baada ya mmiliki wa sasa kununua hisa zote zilizokuwa zikimilikiwa na mmiliki wa awali. 
Akizungumza katika eneo hilo, Bw. Ruben alisema kuwa ufugaji wa Sungura ni mzuri sana na unafaida kubwa kwa mfugaji, kwani unaweza kumuingia kipato kikubwa kama atazingitia taratibu zote za ufugani, hivyo ametoa wito kwa wale wote wanaotaka kufuga au kujifunza ufugaji wa Sungura wasisite kufika kwenye ofisi zao zilizopo Majohe, Jijini Dar es salaam.

Kwa maelezo zaidi piga simu 
namba +255 713 448 899


MAGAZETI YA LEO ALHAMIS FEB 23,2017

WENGI WAJITOKEZA KUPIMA AFYA BURE KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA

$
0
0
Zoezi la upimaji wa Afya Bure kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani linalofanyika kuanzia jana, linaendelea katika viwanja vya Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela.

Mchungaji wa kanisa hilo, Dkt. Daniel Moses Kulola amebainisha kwamba jana zaidi ya wananchi 150 walijitokeza kupima afya zao ambapo zaidi ya 70 walihudumiwa na kurejea nyumba.

Alisema zoezi hilo limejikita kwenye uchunguzi wa afya ya uzazi, kisukari, presha pamoja na uzito likiongozwa na wataalamu wa afya kutoka Canada wanaosaidizana na wataalamu wazawa.
#BMGHabari
Umati wa akina mama waliojitokeza kwenye zoezi la upimaji afya bure katika viunga vya kanisa la EAGT Lumala Mpya
Zoezi la kuchukua taarifa likiendelea kwa umakini
Zoezi hilo la upimaji afya bure linafanyika kwa siku mbili kuanzia jana
Zoezi hilo la upimaji afya bure linafanyika kwa siku mbili kuanzia jana na linasimamiwa na wataalamu wa afya kutoka Canada

UTARATIBU WA KUPATA HATI UNAPONUNUA ARDHI YA KIJIJI KWA UWEKEZAJI

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.

Kawaida  hatimiliki( granted  right  of  occupancy)  hazitolewi  kwa  ardhi  za  vijijini. Ardhi  za  mijini  tu  ndizo  huwa  na hadhi  ya kupata  hatimiliki. Lakini  wapo  watu  ambao  wamechukua maeneo  ya  vijijni  kwa  ajili  ya  uwekezaji.  

Wapo  waliochukua ardhi  kama  wachimbaji  wadogo,  kilimo, madini, n.k. Hawa  pengine wangependa  wapate  hatimiliki  ili  kukuza  biashara  zao  sambamba  na  kupata  faida zinazotokana  na  kuwa  na  hati miliki. Moja  ya  faida  ya  kuwa  na  hatimiliki  ni  pamoja  na  kupata  mkopo. 

Swali  ni  je  inawezekana  kuipatia  ardhi  yako  ya  kijijni  hatimiliki  yenye hadhi  sawa na  ile  inayotolewa  kwa  ardhi  za  mijini?. 

1.ARDHI  YA  KIJIJI  NI  IPI.
Sheria  za ardhi  namba 4 na 5 kwa pamoja  zimeainisha  aina tatu  za  ardhi  kwa  hapa  Tanzania.  Kwanza  ardhi  ya  jumla,  ardhi  ya  hifadhi, na  ardhi  ya  kijiji. Ardhi  ya  jumla( general  land)  ni  hii  ardhi  ya  mijini  ambayo  huwa  na  hati  miliki( right  of  occupancy).  Hii  ni  asilimia  2  ya  ardhi  yote  ya  Tanzania.

Ardhi  ya  hifadhi( reserved  land)  ni  kama  mbuga,  kingo  za  mito na bahari, makaburi,  viwanja vya  wazi n.k. Hii  ni  asilimia 28 ya  ardhi  yote. Ardhi  hii  huwa  haimilikishwa  labda  isemwe  vinginevyo.

Ardhi  ya  vijiji( village  land). Hii ni  ardhi  ya  vijiji  kama  jina  lake  lilivyo. Sote  tunajua  vijijini  ni  wapi.  Inachukua  jumla  ya  asilimia 70 ya  ardhi  yote. 

2.  UMILIKI  WA   WA  AINA  TATU  WA  ARDHI  YA  KIJIJI.
Ardhi  ya  kijiji  iwe kwa uwekezaji, makazi  au  vinginevyo  inaweza  kumilikiwa  kwa  namna  tatu  tofauti. Kama  ifuatavyo.

( a ) Kumiliki  kwa  haki  bila  nyaraka  yoyote  ya  umiliki( deemed  right of  occupancy). Kwa  mtu  anayewekeza  kijijini  huu  si  utaratibu mzuri  kwake. Hapa  mmiliki  atamiliki  ardhi  kijijini  bila  kuwa  na  nyaraka  yoyote  inayomtambulisha  kama  mmiliki   lakini  hilo  halitamwondolea  uhalali wake katika  kumiliki. Wamiliki  wengi  vijijni  humiliki  kwa   mtindo  huu.  Wengi  wana  ardhi  lakini  hawana  nyaraka  yoyote  kudhibitisha  kumiliki. 

( b ) Kumiliki  kwa  hati  ya  kimila(customary  certificate). Sura  ya  114 sheria  na  5  ya  1999  ya  ardhi  ya  vijiji  inatambua  uwepo  wa  hati  za  kimila. Hati  hizi  hutolewa  na  halmashauri  za  vijiji  kwa utaratibu  maalum.

( c ) Kumiliki  kwa  hatimiliki( granted  right  of  occupancy). Hatimiliki  hutolewa  kwa  maeneo ya  mijini  tu  lakini  hata  vijijini  zinaweza  kutolewa  ikiwa  ardhi  inachukuliwa  kwa  ajili  ya  uwekezaji au  shughuli  nyingine  za serikali. 


RC GAMBO AFANYA ZIARA YA SIKU TATU WILAYANI MONDULI, ARUSHA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo, Leo february 22,2017 ameendelea na ziara yake ya kikazi kwa siku ya tatu katika Wilaya ya Monduli ambapo yupo wilayani humo kwa ziara ya siku tano ambapo ijumaa ya wiki hii atakamilisha ziara hiyo. 


Akiwa kwenye ziara hiyo leo ametembelea Zahanati ya Mswakini Juu iliyopo Wilayani humo na kujionea utendaji kazi,na maendeleo ya zahanati hiyo pamoja na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi waishio jirani na kituo hicho cha Afya. 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, akiwasili kwenye Zahanati ya Mswakini Juu Wilayani Monduli. 
kutoka kushoto Mkuu wa mkoa akikagua maendeleo ya zahanati,Aliyeshika fimbo ni Mbunge wa Monduli Julius Kalanga,kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema ) akiwa ameambatana na wajumbe wake.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Akigagua baadhi ya mashine katika kwenye zahanati hiyo. 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WASANII WATAKIWA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KAZI ZAO

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa agizo kwa wasanii wa hapa nchini kutumia lugha fasaha ya Kiswahili katika kazi zao ili kuitangaza lugha hiyo inayotambulisha Taifa letu.

Agizo hilo limetolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akizindua program ya kuuza muziki na filamu kwa njia ya mtandao iliyoandaliwa na Kampuni ya Afroprimiere.

Prof. Gabriel alisema kuwa Tanzania inatambulika Duniani kwa lugha ya Kiswahili hivyo wasanii wana nafasi kubwa ya kuendelea kutumia lugha hiyo kwa ufasaha katika kazi zao wanazofanya ili kukuza lugha ya Kiswahili.

“Wasanii mnafanya kazi zenu kwa Kiswahili ni vyema mkatumia lugha hii kwa ufasaha zaidi lakini pia kuweni sehemu ya mafanikio ya mpango huu ili mfanikiwe zaidi.” Alisema Prof. Elisante.

Aidha amewahakikishia wasanii kuwa Serikali itaendelea kutunza haki za wasanii na kuwaunga mkono katika programu hii ili iwe na faida kwa Serikali katika kupata mapato na wasanii pia kupata faida ya kazi zao. “Kutunza Kazi za wasanii ni jukumu letu, nawahakikishia hakuna atakayekosa faida katika jambo hili kama tutakua pamoja na kushirikiana.” Aliongeza Prof Gabriel.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Afroprimiere ambao ndio waandaaji wa program hiyo Bw. Fredy Ngimba amesema kuwa program yao inalenga kuwasaidia wasanii namna wanavyoweza kufaidika na biashara ya kazi zao mtandaoni.

“Programu hii itawasaidia wasanii kujua idadi kamili ya wanunuzi wa kazi zao mtandaoni na namna ambavyo watagawanya mapato kwa wote wanaohusika kuanzia Serikali, Waandaji, Watengenezaji na wasambazaji wa kazi hizo.”Alisema Bw. Ngimba.

Mapato kwa wote wanaohusika katika kazi hiyo yanaonyesha kuwa Msanii ambaye ndio mwenye kazi yake atapata 50%, Muandaaji 25%, Kampuni ya Mawasiliano 20%, mtengenezaji 08% na Serikali 18%.imeandikwa na Shamimu Nyaki.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Pof.Elisante Ole Gabriel akizungumza na Wasanii (hawapo pichani ) katika uzinduzi wa programu ya kuuza muziki na filamu kupitia mtandao (online)iliyoandaliwa na Kampuni ya Afroprimiere jana Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi maendeleo ya Sanaa Hajjat Shani Kitogo na wa kwanza Kulia ni Bw.Fredy Ngimba Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo.
Baadhi ya Wasanii walioshiriki katika uzinduzi wa programu ya kuuza muziki na filamu kupitia mtandao (online) iliyoandaliwa na Kampuni ya Afroprimiere jana Jijini Dar es Salaam.

RC MRISHO GAMBO AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYANI MONDULI

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo, jana  february 22,2017 ameendelea na ziara yake ya kikazi kwa siku ya tatu katika Wilaya ya Monduli ambapo yupo wilayani humo kwa ziara ya siku tano ambapo ijumaa ya wiki hii atakamilisha ziara hiyo.

Akiwa kwenye ziara hiyo leo ametembelea Zahanati ya Mswakini Juu iliyopo Wilayani humo na kujionea utendaji kazi,na maendeleo ya zahanati hiyo pamoja na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi waishio jirani na kituo hicho cha Afya.
Pichani Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Akiwasili kwenye Zahanati ya Mswakini Juu Wilayani Monduli .
Picha na msumbanews blog
kutoka kushoto Mkuu wa mkoa akikagua maendeleo ya zahanati,Aliyeshika fimbo ni Mbunge wa Monduli Julius Kalanga,kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema ) akiwa ameambatana na wajumbe wake.Picha na msumbanews blog
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Akikagua baadhi ya mashine katika kwenye zahanati hiyo.

Mkuu wa Mkoa Akikagua baadhi ya nyumba za wauguzi wa Zahanati hiyo ya Mswakini juu. Picha na Msumbanews blog.

Ujenzi wa Ubungo interchange kuanza mara moja

$
0
0
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), jana umetiliana saini na kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) mkataba wa ujenzi wa barabara za Juu ‘Interchange’ katika makutano ya barabara ya Sam Najoma na Mandela Ubungo jijini Dar es salaam.

Mkataba huo unamtaka Mkandarasi kampuni ya CCECC kutoka China kuanza ujenzi huo mara moja na ujenzi huo unatarajiwa kutumia takriban miezi 30 hadi kukamilika kwake.Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale amesema zaidi ya shilingi Bilioni 177.4 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo utakaowekewa jiwe la msingi mwezi machi mwaka huu.

“Hakikisheni mnaanza ujenzi mara moja kwani Serikali imeshakamilisha taratibu zote na tayari kiasi cha shilingi bilioni 2.1 kimelipwa kwa ajili ya fidia kwa wananchi walioguswa na mradi huo”. Amesema Eng. Mfugale.Ujenzi wa Ubungo interchange unajengwa kwa fedha ya mkopo kutoka Benki ya Dunia ambapo Serikali kwa upande wake imeshalipa fidia ya zaidi ya shilingi bilioni 2.1

“Zaidi ya magari 65,000 yanapita kila siku katika katika makutano ya barabara za morogoro,Mandela na sam nujoma eneo la Ubungo hali inayosababisha msongamano katika barabara ya Morogoro ambayo ndio lango kuu la kuingia jijini Dar es salaam hivyo ufanisi wa mradi huo utahuisha hali ya usafirishaji katika jiji la Dar es salaam na kuchochea ukuaji wa uchumi” amesisitiza Eng. Mfugale.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CCECC Bw, Jiang Yigao amemhakikishia Eng. Mfugale kuwa wataanza maandalizi ya ujenzi huo mara moja na watafanya kazi hiyo kwa wakati.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao wakibadilisha hati za mikataba mara baada ya kusaini ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao wakisaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao (Katikati) wakisaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange).Kushoto ni Meneja Mradi wa ujenzi huo Li Haiquan.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akifafanua jambo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange) utakaotekelezwa na kampuni M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akitoa maelezo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange) utakaotekelezwa na kampuni M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC).
Baadhi ya wawakilishi wa Mkandarasi wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) wakifuatilia hafla ya utiaji saini ya ujenzi wa Ubungo interchange Jijin Dar es salaam.

NEWS ALERT: MKE WA BILIONEA MSUYA AACHIWA HURU NA KUKAMATWA TENA

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mwenzake Revocatus Muyela wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya Aneth Msuya.

Hata hivyo washtakiwa hao walikamatwa tena na jeshi la polisi.

Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa leo amewaachia huru washtakiwa hao baada ya upande wa mashtaka kushindwa kutimiza amri yake iliyowataka kufanyia marekebisho ya hati ya mashtaka

Washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya kukusudia.

Uamuzi wa mahakama kuifuta kesi hiyo umefikiwa leo baada ya jalada la kesi hiyo lililokuwa limeitwa Mahakama Kuu kurejeshwa mahakamani hapo.
Februari 20, mwaka huu, Hakimu Mwambapa aliupatia upande wa mashtaka muda wa siku tatu kurekebisha hati ya mashtaka.

Lakini mpaka siku hizo tatu zinaisha hawakuwa wamefanyia bali  Wakili wa Serikali, Hellen Moshi aliiambia mahakama kuwa baada ya ofisi yao kutafakari kwa kina wameamua kuwa hawana cha kubadilisha kwa hati hiyo ya mashtaka

Wakili wa utetezi,  Peter Kibatala alidai kuwa upande wa mashtaka licha ya kupewa muda wa kutosha kufanyia marekebisho hati hiyo lakini wamekaidi amri hiyo.

Kibatala aliiomba mahakama kuwaachia washtakiwa huru kwa kuwa amri ya mwisho ya mahakama ilisema kama wasipofanya marekebisho itachukua hatua  na pia hakuna rufaa yoyote iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kupinga uamuzi huo.

Hakimu Mwambapa amesema,kweli mahakama imeamuru upande wa mashtaka kufanyia marekebisho hati ya mashtaka pindi ilipoona inamapungufu lakini hawakufanya hivyo, akawaongezea muda hawakufanya hivyo, Ila leo wamekuja na maelezo ya kuwa hati ya mashtaka ni sahihi.

"Hati ipi ambayo ipo sahihi wakati mahakama ilisema haipo sahihi, nawaachia huru washtakiwa", amesema Mwambapa.

Awali ndugu wa marehemu waliwasilisha barua mahakamani hapo na Kwa mujibu wa barua hiyo walikuwa wanataka Hakimu huyo ajitoe kwa sababu hawana imani naye.

Hakimu Mwambapa alikuwa atoe uamuzi juu ya hoja zilizowasilishwa na upande wa utetezi pamoja na upande wa mashtaka ambapo Wakili John Malya aliomba washtakiwa hao waachiwe huru kwa sababu   hakuna hati ya mashtaka inayowashikilia washtakiwa hao mahakamani hapo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa yeye aliiomba mahakama iwape muda ili waweze kutekeleza amri ya mahakama iliyotolewa Januari 9, mwaka huu

Washtakiwa Miriam na Revocutus ambao wanadaiwa kumuua kwa makusudi Aneth Msuya, kwa kumchinja, nyumbani kwake Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Miriam  ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo alikuwa mke wa aliyekuwa kaka wa Aneth, marehemu Erasto Msuya, maarufu kama bilionea Msuya.

Erasto Msuya, ambaye alikuwa mfanyabiashara bilionea wa madini ya Tanzanite, pia aliuawa kwa kupigwa risasi, Agosti, 2015 eneo la Mijohoroni,  kando ya barabara ya Arusha – Moshi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Hata hivyo washtakiwa hao walikamatwa tena na kuondoka na gari la polisi.
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live


Latest Images