Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1582 | 1583 | (Page 1584) | 1585 | 1586 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wamezipongeza timu za Singida United na Njombe Mji kwa kufanikiwa kupanda ligi kuu msimu ujao.

  Rais wa TFF Jamal Malinzi amezipongeza kwa mpigo, timu za Singida United ya Singida na Njombe Mji ya Njombe kwa kupanda daraja. Juma lililopita, Rais Malinzi aliuandikia barua uongozi wa Lipuli ya Iringa kwa mafanikio ya kupanda daraja msimu huu kutoka Ligi Daraja la Kwanza hadi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2017/18 kama alivyofanya sasa kwa Singida United ya Singida na Njombe Mji ya Njombe.

  Katika salamu hizo kwa Lipuli ambayo imepanda daraja baada ya kusota miaka 17 iliposhuka daraja, Rais Malinzi alimwandikia barua Katibu Mkuu wa timu hiyo akisema: “Nitumie fursa hii kukupongeza wewe, uongozi wa klabu yako, benchi la ufundi na wadau wote wa timu ya Lipuli kufuatia kupanda daraja kwenda Ligi Kuu.

  Kama ilivyotokea kwa Lipuli, Rais Malinzi pia kwa moyo mkunjufu amewaandikia barua, viongozi wa Singida United ya Singida na Njombe Mji ya Njombe, akisema: “Pia nanyi nawapongeza kwa kupanda daraja. Bila shaka ni kazi kubwa imefanyika ikihusisha kujitolea kwa ari na mali kuhakikisha mnafika hapa mlipo.”

  Pamoja na salamu hizo za kuwapongeza, Rais Malinzi hakuacha kuziusia timu hizo akisema: “Rai yangu kwenu ni kuongeza juhudi na kuendesha klabu kwa weledi mkubwa zaidi ili muweze kuwa washindani wa kweli katika ligi (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara).”

  0 0

  Na  Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam imepitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 ya bilioni 20 kutoka bajeti ya shilingi bilioni saba ya mwaka wa fedha 2015/2016.

  Wajumbe wa baraza la jiji wamepitisha bajeti hiyo kwa kauli moja na kutaka kufikiria katika uwekezaji wa miradi mikubwa ili kufanana na majiji mengine duniani yenye ukubwa kama jiji la Dar es Salaam.

  Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es  Salaam, Chacha Mwita amesema kuwa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 imeweka kipaumbele katika kulifanya jiji la Dar es Salaam kuwa la mfano katika usafi.

  Amesema katika maeneo walioangalia ni kuongeza dampo katika manispaa za Kinondoni na Ubungo ili kuondoa usafirishaji wa taka hadi Pugu Kinyamwezi pamoja na ujenzi wa vyoo katika kila maeneo ambayo yana msongamano wa watu.

  Mwita amesema kuwa lazima wajumbe wa baraza kuumiza kichwa katika miradi yenye manufaa kwa jiji katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

  Aidha amesema kuwa mradi wa DDC utaingizia mapato jiji shilingi milioni 750 kutoka shilingi Milioni 50 kwa mwaka wa fedha uliopita kutokana mazingira yaliyokuwepo kwa wafanyabiashara kulipa milioni 36 kwa chumba kwa mtu mwingine ambaye jiji inakuja kupata milioni sita kwa mwaka.

  Akichangia katika baraza diwani  wa Mwananyamala, Songoro Mnyonge amesema kuwa vipaumbele vilivyowekwa vifanyiwe kazi katika kuleta mabadiliko katika jiji la Dar es Salaam.Amesema katika mradi wa kutafuta eneo la makaburi katika kuweza kuwahifadhi ndugu zetu pamoja na manispaa  ya zingine kufanya hivyo kutokana na maeneo yaliyopo kujaa.
  Wajumbe wa Baraza la Madiwa wa jiji la Dar es Salaam  wakiwa katika kikao cha bajeti leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amewataka wachimbaji mchanga na walimaji wa bustani katika bonde la mto msimbazi katika kata vingunguti iliyopo katika Manispaa ya Ilala, kuondoka mara moja na kuacha shughuli hizo.

  Ameyasema hayo alipokua katika ziara ya siku moja ya kutembelea kata ya Vingunguti na kujionea athari mbalimbali za kimazingira katika kata hiyo.
  Wakiongea mbele ya Waziri Makamba, Wananchi wamelalamika kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo bonde hilo kuzidi kumong'onyoka na kusogelea makazi ya watu pamoja na eneo la makaburi. 

  Hivyo basi kusababisha nyumba zao kuanguka na makaburi kumong'onyoka hali amabayo inahatrisha maisha yao na kuwafanya kuishi kwa hofu.
  Akijibu kero hiyo Waziri Makamba aliwaambia kuwa atayafanyia kazi maombi yao na atakaa na viongozi wa Manispaa na wa Ofisi yake ili kupata suluhu ya matatizo yao. 

  Pamoja na hayo alisema kuwa kwa hatua za awali anawataka  wachimbaji na wakulima wa bustani kuacha mara moja shughuli hizo wanazofanya katika maeneno ya bonde hilo. (Habari na picha toka Kitengo caha mawasiliano Serikalini OMR)
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiangalia bonde la mto Msimbazi katika kata ya Vingunguti lilivyoharibika kwa shughuli za kila siku za Wananchi ikiwemo kilimo cha mbogamboga na uchimbaji wa mchanga. Waziri Mkamba yupo katika ziara kutembelea kata ya Vingunguti kukagua athari za mazingira.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba pamoja na Mbunge wa jimbo la Segerea Mh. Bonnah Klauwa wakiskiliza kero mbalimbali zinazotolewa ana Wananchi wakati Mh. Waziri alipofanya ziara katika kata ya Vingunguti  kukagua athari mbalimbali za mazingira.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Wananchi waliojikusanya kumsikiliza wakati wa ziara yake katika kata ya Vingunguti katika wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akipata maelezo, toka kwa vijana wa kata ya Vingunguti  juu ya utenegenezaji wa majiko ya mkaa ambayo ni rafiki wa mazingira na ambayo hayatumii mkaa mwingi.

  0 0

  Asilimia 61 ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya juu katika vyuo mbalimbali nchini hawana ujuzi na sifa za kuajiriwa kwenye sekta binafsi ili kukuza uchumi na kufikia kiwango cha kati .

  Hayo yamebainishwa leo na Naibu waziri wa kazi,vijana na ajira Anthony Mavunde wakati akizungumza na wadau wa makampuni ya sekta binafsi jijin Dar es salaam na kusema kuwa baada ya kugundua changamoto hiyo serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi wameanzisha mpango wa miaka 5 wa kuwasaidia vijana kupata mafunzo kwa vitendo ili kuongeza sifa ya kuajiriwa na kujiajiri.

  ''Tumeamua kuanzisha programu hiyo ili kuhakikisha wanasaidia nguvu kazi ya nchi kupata ujuzi wa kuweza kujiajiri lakini pia kuajiriwa katika makampuni mbalimbali yenye uhitaji wa wafanyakazi walio bora katika utendaji kazi" alisema Mavunde.

  Mheshimiwa mavunde akaongeza kuwa programu hiyo ya miaka 5 iliyoanza mwaka 2016 na kutegewa kumalizika na kufikia mwaka 2021 unatarajiwa kuwafikia watu milioni 4 ili kuwasaidia kukuza ujuzi na kufikia uchumi wa kati kwa kuwepo nguvu kazi ya juu ya asilimia 34.
  Naibu wazir wa kazi,vijana na watu wenye ulemavu Mh,Anthony Mavunde akizungumza na wadau Mbalimbali sekta binafsi katika mkutano uliohusisha serikali na sekta Binafsi uliozungumzia Mafunzo ya miaka mitano ya kuwapatia ujuzi wa kuajiriwa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
  Mkurugenzi mtendaji Bw Godfrey Simbeye akitoa ufafanuzi katika Mkutano huo uliokutanisha Serikali na Sekta Binafsi
  Baadhi ya Wadau waliohudhuria Mkutano huo leo Jijini Dar es salaam.Picha na Yasir Adam Blogu ya Jamii.


  0 0


  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imehitimisha zoezi la upasuaji mkubwa kwa njia ya matundu madogo kwa watoto ambao ulianza jumatatu wiki hii .

  Upasuaji huo umefanywa na Madaktari Bingwa wa Muhimbili waliobebea katika upasuaji wa watoto kwa kushirikiana na mtaalam kutoka Hospitali ya King Faisal ya nchini Saudia Arabia Profesa Zakaria Habib .

  Akizungumzia kuhusu upasuaji huo Daktari Bingwa wa Upasuaji wa watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Zaitun Bokhary amesema upasuaji huo umekua na mafanikio makubwa na kwamba watoto wote waliofanyiwa upasuaji wanaendelea vizuri.

  ‘’ Tunamshukuru Mungu hadi leo tunapohitimisha zoezi hili watoto waliofanyiwa upasuaji huo wanaendelea vizuri na tayari wameanza kula pamoja na mazoezi ‘ ‘ amesema Dk. Bokhary.

  Tangu kuanza kwa upasuaji huo Februari 20 mwaka huu kwa njia ya matundu madogo ( Laparoscopy Surgery) jumla ya watoto sita wamefanyiwa upasuaji huo.

  Upasuaji huo umehusisha upasuaji wa nyama iliyojitokeza katika sehemu ya haja kubwa kwa watoto, upasuaji wa kushusha kokwa katika korodani, upasuaji wa kushusha utumbo mkubwa na kutengeneza njia ya haja kubwa kwa watoto ambao wamezaliwa bila kuwa na njia ya haja kubwa, upasuaji wa kuondoa mfuko wa ziada kwenye koo kwa watoto na upasuaji kwa watoto wadogo ambao hawana celi mbalimbali na hivyo kushindwa kusukuma choo kwenye utumbo mkubwa.
   Madaktari wakifanya upasuaji wa njia ya matundu madogo kwa mtoto huyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  leo

   Kushoto ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto, Profesa Zakaria Habib kutoka Falme za Kiarabu akiwa na timu ya  watalaam  wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimuandaa mtoto mwenye umri wa miaka minane kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa hatua ya pili ya kushushwa kokwa kwenye korodani 

  Madaktari bingwa wa upasuaji wa watoto  wakiendelea na zoezi hilo  ambalo umekua na mafanikio makubwa .

  0 0

   ASALAAM ALAIKUM WARAHMATULLAH WABARAKATU
  Taarifa ya shughuli ya Maulidi tarehe 11 /03/2017 Katika uwanja wa Madrasat RAHMAN Segerea Mwisho, Dar-es-salaam.
  Ndugu zetu katika Imani ,Uongozi na Jumuiya ya Madrasat Rahman

  Segerea inayo furaha kuwaalika katika shughuli ya maulidi yatakayo fanyika 11/03/2017 hapa segerea mwisho.
  Kuhudhuria kwenu ndio 

  mafanikio makubwa ya dini yetu tukufu. Pia michango yenu ya hali na mali  inakaribishwa. Tafadhali wasiliana nasi kwa simu hii 0622617961 au 0712407032 kimataifa piga +255 622617961


  0 0

  Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF ),Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini ya Kiislam, alipomtembelea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Zuberi ofisini kwake mapema leo.Waliokaa kuanzia kushoto sheikh wa mkoa wa Dar es salaam Alhd Mussa .Jenerali Venance Mabeyo .Sheikh Mkuu Muft Zuberi, waliosimama kuanzia kushoto Katibu Mstaafu Suleiman Lolila,Haidari Kambili,Sheikh Mussa Hemed, Katibu wa dini Mohammed Hamisi pamoja na Tabu kawambwa

  0 0

  Serikali imesema itaanza ujenzi wa barabara ya Mtwara-Masasi KM 210 sehemu ya Mtwara-Nnivata yenye urefu wa KM 50 kwa kiwango cha lami mwezi Aprili mwaka huu, ili kurahisisha usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo na kufungua fursa za kiuchumi katika mkoa huo na nchini jirani ya Msumbiji.

  Akizungumza na wananchi wa Nanyamba wilayani Tandahimba, mkoani Mtwara, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa mkandarasi Dott Services Ltd ataijenga barabara hiyo kwa viwango vya kisasa na kwa gharama za shilingi bilioni 89.5.

  "Mkandarasi atafika eneo la mradi mwezi wa nne mwaka huu na ujenzi utaanza mara moja, hivyo wananchi muwe na subira ili muweze kunufaika na barabara hiyo pindi itakapokamilika kwa kuwa itazidi kuchochea maendeleo yenu na Taifa kwa ujumla", amesema Waziri Mbarawa.

  Waziri Profesa Mbarawa amefafanua kuwa ujenzi huo utadumu kwa miaka miwili tangu kuanza kwa ujenzi wake hadi kukamilika, hivyo Prof. Mbarawa amewataka wananchi wa Mtwara kutoa ushirikiano kwa mkandarasi huyo ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati uliopangwa.

  Aidha, Waziri Mbarawa ameongeza kuwa kwa wale wananchi waliovunjiwa nyumba zao na kustahili kulipwa fidia kisheria ili kupisha ujenzi wa barabara hiyo watalipwa, na kazi ya kutathimini nyumba hizo itaanza mapema mwezi wa tatu mwaka huu.

  Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa Serikali itaongeza fedha za ujenzi wa barabara hiyo kwa awamu nyingine katika Mwaka wa fedha 2017/2018 ili kuweza kufungua barabara yote kwa kipindi kifupi.

  Kuhusu huduma za mtandao wa mawasiliano mkoani humo Prof. Mbarawa amewahakikishia wananchi kuleta huduma hiyo katika wilaya zote kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa wote ili kurahisisha mawasiliano ambapo kwa sasa hali ya huduma ya mawasiliano katika baadhi ya vijiji hairidhishi.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Evod Mmanda amesema kuwa barabara hiyo ikikamilika itarahisisha usafiri wa abiria na mizigo ikiwemo mazao yanayolimwa katika mkoa huo hususan zao la Korosho ambalo ni miongoni mwa mazao yanayoongeza pato kubwa kwa Taifa.

  Mradi wa ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba-Newala-Masasi yenye urefu wa KM 210 ambao unatarajiwa kuanza mwezi Aprili mwaka huu unatarajiwa kuunganisha wilaya tano za mkoa wa Mtwara na hivyo kufungua fursa za kiuchumi na kijamii katika Mkoa huo na nchi jirani ya Msumbiji.


  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Nnivata kilichopo mkoani Mtwara kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara ya Mtwara-Masasi yenye urefu wa KM 210 itakayojengwa kwa kiwango cha lami wakati alipokuwa akiikagua barabara hiyo.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wananchi wa Nanyamba katika mkutano wa hadhara kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara ya Mtwara-Masasi yenye urefu wa KM 210 itakayojengwa kwa kiwango cha lami wakati alipokuwa akiikagua barabara hiyo, mkoani Mtwara.
  Muonekano wa sehemu ya kwanza ya barabara ya Mtwara-Nnivata yenye urefu wa KM 50 itakayoanza kujengwa mwezi Aprili mwaka huu kwa kiwango cha lami. Mradi huo utagharimu kiasi cha Shilingi bilioni 89.5
  Muonekano wa Korongo lililoko kwenye moja ya barabara za Newala Mjini ambalo limetokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Mtwara.
  Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini Mhe. George Mkuchika (wa pili kulia), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), eneo lililoathiriwa na mvua (halipo pichani), zinazoendelea kunyesha katika moja ya barabara jimboni hapo mkoani Mtwara. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Newala Bi. Aziza Mangosongo.


  0 0

  Viongozi wa kata na mitaa wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam,wametakiwa kutoka nje ya ofisi zao ili kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

  Akizungumza na wananchi wa kata ya Kinondoni katika ziara yake ya siku kumi, mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi amesema viongozi wote wakitaifa akiwemo raisi, waziri mkuu na mawaziri wanafanya ziara za kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

  Hatahivyo mkuu huyo wa wilaya amewataka viongozi wa kata na mitaa kuwa wabunifu na kuwashirikisha wadau ili kuweza kutatua changamoto ndogondogo tofauti na kuzipeleka kwa ofisi ya mkuu wa wilaya.

  Aidha amesema serekali ya awamu ya tano imejipanga kikamilifu kutatua kero za wananchi nakutekeleza kikamalifu ilani ya chama cha mapinduzi kwa mwaka 2015/2020.


  Mkuu wa wilaya ya Kinondoni akitoka katika ofisi ya mtendaji wa Kata ya Kinondoni akielekekea kukagua miradi mbambali na Kinondoni leo hii katika Ziara yake
  Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ally hapi akiwashukuru wafanya biashara katika soko la mtambani lililo kinondo ni Jijini Dar es salaam leo hii.
  Mkuu wa wilaya ya Kinondoni wilaya ya Kinondoni Ally Hapi Akizungumza na viongozi wa Kata na mitaa wilaya ya Kinondoni Jijini dar es salaam leo hii katika Ziara yake ya kukagua miradi mbambali na kusikiliza kero za wakazi wa Kinondoni Pembeni Kushoto ni Diwani wa Kata ya Kinondoni Mustapha Muro 

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea ujumbe wa Mfalme wa Qatar, Mtukufu Sheikh Tamim Hamad Bin Khalifa Al-Thani kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Ujumbe huo uliwasilishwa leo katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam na Balozi wa Qatar nchini, Mhe. Abdullah Jassim Al Maadadi. 
  Waziri Mahiga akizungumza na Mhe. Jassim Al Maadadi ambapo pamoja na kuzungumzia masuala ya ushirikiano Waziri alimpongeza kwa hatua nzuri za maandalizi ya Kombe la Dunia linalotarajiwa kufanyika nchini Qatar mwaka 2022. Vilevile alimuarifu kuhusu hatua iliyofikiwa na Serikali ya Tanzania katika kukamilisha ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi mjini Doha, Qatar. 
  Mhe. Jassim Al Maadadi alitumia fursa hiyo kuwasisitiza Watanzania kuzichangamkia fursa za ajira zilizopo nchini Qatar wakati huu wa maandalizi ya Kombe la Dunia kwa kuwa nchi hizi zilikwisha saini mkataba wa ushirikiano kwenye kazi na ajira mwaka 2013. 
  Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga, Afisa Mambo ya Nje, Bw. Hangi Mgaka na Katibu wa Waziri, Bw. Gerald Mbwafu wakifuatilia mazungumzo. 
  Mazungumzo yakiendelea 
  Picha ya pamoja. 

  0 0

  Na Karama Kenyunko-Globu ya Jamii
  Raia wa 14 wa India ambao wanafanya kazi Quality Group leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu likiwemo la kufanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali. Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha.

  Hati ya mashtaka, iliyosomwa na mwendesha Mashtaka, wa uhamiaji Method Kagoma imewataja washtakiwa hao kuwa ni Rojat Surkar, Jagadish Mamidu, Niladri Maiti, Sivarar Raja Sekaran, Mohammed Taher Shaikh, Bijenda Kumar, Prasoon Kumar Mallik na Nipun Dinbandhu Bhatt.

  Wengine ni Pintu Kumar, Anuj Agurwa, Varun Boloor, Arun Kumar Kateel, Avinash Chandratiwari na Vikram Sankhala.

  Akisoma hati ya mashtaka, Kagoma amedai kuwa, Februari 13, mwaka huu, huko katika ofisi ya Quality Group Ltd iliyopo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao walikutwa wakiwa na viza zilozoghushiwa za kufanyia kazi.

  Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa siku na mahali hapo washtakiwa hao wakiwa raia wa India walikutwa wakiishi nchini Tanzania bila ya kuwa na kibali.
  Kagoma aliongeza kuwa, Februari 13 mwaka huu, katika jengo la Quality Group washtakiwa hao wakiwa raia wa India walikutwa wakijihusisha na kufanya kazi katika kampuni hiyo kama washauri bila ya kuwa na kibali cha kufanya kazi nchini.
  Hata hivyo, washtakiwa hao ambao wanatetewa na mawakili watatu, Alex Mgongolwa na Hudson Ndusyepo wamekanusha kujihusisha tuhuma hizo na wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dmahana.

  Mahakama iliwaamuru washtakiwa hao kuwa kuweka dhamana ya milioni tano kila mmoja na kuleta mdhamini mmoja kila mtu atakayeweka ya kiasi hich cha fedha. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 7, mwaka huu.

  Raia wa 14 wa India amabao ni wanafanyakazi Quality Group leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu likiwemo la kufanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali

  0 0  0 0

  Makamu wa Rais wa Tanzania Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa afisa mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja alipotembelea katika banda la Dawasco katika maadhimisho ya siku ya Mto Nile yaliyofanyika jijini Dar es salaam. 


  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makala akitangaza kikosi cha watu nane kutoka nje ya halmashauri ya Jiji kinachojumuisha watalaam wa ardhi kutoka  ofisi ya Mkuu wa Mkoa, halmashauri Mbeya, Mkuu wa Wilaya, wanasheria na vyombo vya Dola. 
  amesema kikosi kazi kitaanza  kwa awamu ya  kwanza ambapo kitashughulikia migogoro ya ardhi Kata  ITEZI na MWAKIBETE.
  Amekipa kikosi kazi hicho muda wa siku 14 kushughulikia migogoro katika kata hizo mbili na watoe ushauri wa namna ya kuimaliza migogogoro  iliyopo. 
  Amebainisha kuwa migogoro mingi katika  jiji la Mbeya inakutokana na kutolipa fidia, umilikishaji watu zaidi ya mmoja katika  kiwanja kimoja na Baadhi ya wawekezaji kutoendeleza maeneo yao kwa muda mrefu
  Amefanikiwa kumaliza  mvutano wa umiliki wa soko kati ya CCM na serikali ya  mtaa na kata. Kwa mujibu wa hati za kiwanja CCM  ni wamiliki halali kwa kuwa na hati Bambi 81 BB
  Mkuu wa Mkoa  huyo amepokea  kero mbalimbali kutoka kwa wananchi kuhusiana na Mgogoro wa wananchi na wamiliki wa ardhi maeneo ya viwanda.
   Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makala  akitoa maagizo wakati alipotembelea sehemu mbalimbali zenye migogoro ya ardhi jijini humo
  Wananchi wakitoa kero zao za ardhi kwa Mkuu wa Mkoa  wa mbeya  kuhusiana na migogoro ya ardhi.
   Wananchi wakitoa kero zao za ardhi kwa Mkuu wa Mkoa  wa mbeya  kuhusiana na migogoro ya ardhi.
  Wananchi wakitoa kero zao za ardhi kwa Mkuu wa Mkoa  wa mbeya  kuhusiana na migogoro ya ardhi.

  0 0

  Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo, wakiongozwa na Askofu wa Good News  for All Ministry,  Dkt. Charles Gadi (katikati), wakiimba wimbo wa amani wakati wa kumuombea Rais Dk. Magufuli na Taifa.
  Askofu Filbert Mbepera (wa pili kuli) wa Kanisa la EAGT, akiombea amani nchi.
  Askofu Ernest Sumisumi (wa pili kushoto) wa Kanisa la Baptist akiiombea ramani ya Tanzania pamoja na picha ya Rais Dk. John Magufuli.
  Askofu wa Good News  for All Ministry,  Dkt. Charles Gadi na Askofu Filbert Mbepera (kuli), wakiyabariki mafuta ya kupaka picha ya Rais, Dk. Magufuli.
  Askofu Hezron Mwamsemba wa Kanisa la Baptist akiipaka mafuta picha ya Rais Dk. John Magufuli. Kwa habari kamili BOFYA HAPA

  0 0


  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya Uendeshaji wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (Law School) Bw.Gerson Mdemu na Katibu wa bodi hiyo Dkt. Zakayo Lukmay wamemtembelea Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe Ofisini kwake mjini Dodoma na kuzungumzia mambo mbali mbali juu ya Taasisi hiyo ya mafunzo ya vitendo kwa wanasheria nchini. Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Katibu MKuu Prof. Sifuni Mchome

  0 0

  Mikutano mikubwa mitatu atakayofanya Sheikh Shariff Majini kwa siku tatu mfululizo kuanzia Ijumaa tarehe 24-02-2017 mpaka siku ya Jumapili tarehe 26-02-2017 katika Viwanja vya Mbagala Zakheim jijini Dar es salaam kuanzia mida ya saa nane mchana mpaka kumi na mbili jioni. 
  Mikutano ni kwa ajili ya kuendesha kongamano la Khofu ya Mungu pamoja na kufanya DUA kwa wale wote wenye kila aina ya shida.

  0 0

  Mkurugezi wa Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu JOSEPH PERAMIHO, iliyopo halimashauri ya wilaya ya peramiho mkoani Ruvuma, BRUDA ASGARI STUFE ,amezindua miradi mitatu ya mabomba ya maji safi yenye thamani ya shilingi milioni 21 katika vijiji vya Mgazini,Peramiho B na Kiwulungi katika tarafa ya Ruvuma.


older | 1 | .... | 1582 | 1583 | (Page 1584) | 1585 | 1586 | .... | 3272 | newer