Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1578 | 1579 | (Page 1580) | 1581 | 1582 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mchungaji Melgad Metili wa Kanisa la KKKT Usharika wa Msasani Dayosisi ya Mashariki na Pwani akiwaombea Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Ackson na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dr. Charles Kimei , Mkewe Rose Kimei pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na waumini wengine kwenye ibada ya shukurani kwa jinsi mungu aliyvowatendea katika kila jambo maishani mwao, Ibada hiyo imefanyika jana jumapili kwenye kanisa hilo lililopo Msasani jijini Dar es salaam.
  Naibu Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dr. Charles Kimei , Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB,Tully Mwambapa kushoto na Mama Rose Kimei wakiimba moja wa nyimbo katika ibada hiyo wakati ilipokuwa ikiendelea.
  Naibu Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dr. Charles Kimei , Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB,Tully Mwambapa kushoto na Mama Rose Kimei pamoja na waumini wengine wakiwa katika maombi.
  Baadhi ya wafanyakazi wa CRDB na waumini wengine wakiwa katika ibada hiyo.


  0 0

  Yanga na Simba zilianza kukutana kwa mara ya kwanza toka mwaka 1937 kwenye ligi ya daraja la pili, Dar es Salaam.

  Timu hizi zinakutana zikiwa na wafungaji wa kihistoria kwa pande zote mbili. Mfungaji bora wa muda wote ni  Omary Hussein  “KEEGAN” – Yanga akiwa ana magoli 6.

  Magoli aliyafunga katika michezo ifuatayo.
  Sept 18, 1982
  Yanga 3-0 Simba(alifunga magoli 2)
  April 16, 1983
  Yanga 3-1 Simba (alifunga goli 1)
  Machi 10, 1984
  Yanga 1-1 Simba
  Mei 19, 1985
  Yanga 1-1 Simba
  Agosti 23, 1986
  Simba 2-1 Yanga

  Mfungaji aliyefunga katika mechi tatu mfululiozo ni

  1. Kitwana Manara -YANGA
  Machi 30, 1968
  Yanga 1-0 Sunderland

  Juni 1, 1968
  Yanga 5-0 Sunderland (goli 4)

  Juni 4, 1972
  Yanga 1-1 Sunderland

  2. Madaraka Selemani – SIMBA
  Julai 2, 1994 – Ligi ya Bara
  Simba 4-1 Yanga (goli la tatu)

  Novemba 2, 1994 – Ligi ya Muungano
  Simba 1-0 Yanga

  Novemba 21, 1994 – Ligi ya Luungano
  Simba 2-0 Yanga (goli  la pili)

  3. Amisi Tambwe – YANGA
  Septemba 26, 2015
  Simba 0-2 Yanga (goli La Kwanza)

  Februari 20, 2016
  Yanga 2-0 Simba (goli la pili)

  Oktoba 1, 2016
  Yanga 1-1 Simba

  Kufunga bao pekee la ushindi mechi mbili mfululizo 

  1. Said Sued  SCUD – YANGA
  Mei 18, 1991
  Yanga 1-0 Simba

  Agosti 31, 1991
  Simba 0-1 Yanga

  2. Dua Said – SIMBA
  Julai 17, 1993
  Simba 1-0 Yanga

  Septemba 26, 1993
  Simba 1-0 Yanga (Ligi ya Muungano)

  Mfungaji wa bao la mapema
  Abdallah Msamba sek 56
  Aprili 26, 1997
  Yanga 1-1 Simba

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Baada ya ushindi wa  goli 2-0 dhidi ya Mwadui FC, timu ya Azam imeingia kambini kujiandaa na mchezo wa kombe la Shirikisho (ASFC) utakaopigwa siku ya Ijumaa katika uwanja wa Azam Complex.

  Azam wanatarajiwa kukutana na Mtibwa kwenye mchezo wa ASFC ijumaa ambapo awali mchezo huo ulipangwa kucheza saa moja usiku, na badala yake utapigwa saa kumi alasiri.

  Msemaji wa Azam, Jafari Iddy ametabanaisha kuwa baada ya mchezo wa jana dhidi ya Mwadui wameingia rasmi kambini kwa ajili ya kujiandaa na mechi dhidi ya Mtibwa ambao ni moja mechi ngumu kwani inahitaji matokeo chanya kwa kila upande ili kuweza kuendelea katika hatua ya nane bora kwenye michuano hiyo.

  Chini ya kocha Mromania Aristica Cioaba imejizatiti kutoka na ushindi kwenye mchezo huo kwani itakua ni njia mojawapo ya kuweza kushiriki michuano ya kimataifa na hilo ndiyop lengo kuu la klabu hiyo.

  Mbali na mechi hiyo, Azam pia wanakabiliwa na mechi ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mbabane Swallows utakaopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex Machi 12.


  Msemaji wa Azam, Jafari Iddy

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wawekezaji kutoka Uingereza, China na Afrika ya Kusini ambao wameonyesha nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Afya na Nishati,wengine waliopo kwenye picha hii ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Hamisi Kigwangalla. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imefanya upasuaji mkubwa kwa njia ya matundu madogo (Laparoscopy Surgery)  kwa watoto ambao haujawahi kufanyika hapa nchini.

  Upasuaji huu umefanywa na Madaktari Bingwa wa Muhimbili waliobebea katika upasuaji wa watoto kwa kushirikiana na mtaalam kutoka Hospitali ya King Faisal ya nchini Saudia Arabia.

  Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Upasuaji wa watoto wa Hospitali hiyo, Zaitun Bokhary  leo umefanyika upasuaji wa nyama iliyojitokeza sehemu ya haja kubwa kwa mtoto pamoja na upasuaji wa kuondoa kifuko cha ziada katika mfuko wa chakula.

  Upasuaji huu mkubwa ambao umefanyika leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili hufanyika nchi zilizoendelea hivyo Tanzania ni mara ya kwanza kufanyika na utaleta mageuzi makubwa nchini.

  Moja ya faida kubwa  ya upasuaji wa aina hii ni mgonjwa kupona haraka na gharama kidogo hutumika wakati  wa upasuaji tofauti na upasuaji wa kufungua tumbo.

  Upasuaji ambao umeanza leo unahusisha upasuaji wa nyama iliyojitokeza katika sehemu ya haja kubwa kwa watoto, upasuaji wa kushusha kokwa katika korodani, upasuaji wa kushusha utumbo mkubwa na kutengeneza njia ya haja kubwa kwa watoto ambao wamezaliwa bila kuwa na njia ya haja kubwa, upasuaji wa kuondoa mfuko wa ziada kwenye koo kwa watoto na upasuaji kwa watoto wadogo ambao hawana celi mbalimbali na hivyo kushindwa kusukuma choo kwenye utumbo mkubwa.
  Kutoka kushoto ni daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Zaitun Bokhary, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto, Profesa Zakaria Habib kutoka Falme za Kiarabu na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto wa Muhimbili, Dk Mbaga wakifanya upasuaji LEO wa njia ya matundu madogo ( Laparoscopy Surgery) wa kuondoa kifuko cha ziada katika mfuko wa chakula kwa mtoto mwenye umri wa miaka 10.
  Madaktari wakifanya upasuaji wa njia ya matundu madogo kwa mtoto huyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
  Dk Zaitun wa Muhimbili akizungumza na waandishi wa habari kuhusu upasuaji huo uliofanyika leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

  0 0

  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imefanya upasuaji mkubwa kwa njia ya matundu madogo ( Laparoscopy Surgery) kwa watoto ambao haujawahi kufanyika hapa nchini.

  Upasuaji huu umefanywa na Madaktari Bingwa wa Muhimbili waliobebea katika upasuaji wa watoto kwa kushirikiana na mtaalam kutoka Hospitali ya King Faisal ya nchini Saudia Arabia.

  Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Upasuaji wa watoto wa Hospitali hiyo, Zaitun Bokhary leo umefanyika upasuaji wa nyama iliyojitokeza sehemu ya haja kubwa kwa mtoto pamoja na upasuaji wa kuondoa kifuko cha ziada katika mfuko wa chakula.

  Upasuaji huu mkubwa ambao umefanyika leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili hufanyika nchi zilizoendelea hivyo Tanzania ni mara ya kwanza kufanyika na utaleta mageuzi makubwa nchini.Moja ya faida kubwa ya upasuaji wa aina hii ni mgonjwa kupona haraka na gharama kidogo hutumika wakati wa upasuaji tofauti na upasuaji wa kufungua tumbo.

  Upasuaji ambao umeanza leo unahusisha upasuaji wa nyama iliyojitokeza katika sehemu ya haja kubwa kwa watoto, upasuaji wa kushusha kokwa katika korodani, upasuaji wa kushusha utumbo mkubwa na kutengeneza njia ya haja kubwa kwa watoto ambao wamezaliwa bila kuwa na njia ya haja kubwa, upasuaji wa kuondoa mfuko wa ziada kwenye koo kwa watoto na upasuaji kwa watoto wadogo ambao hawana celi mbalimbali na hivyo kushindwa kusukuma choo kwenye utumbo mkubwa.
  Kutoka kushoto ni daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Zaitun Bokhary, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto, Profesa Zakaria Habib kutoka Falme za Kiarabu na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto wa Muhimbili, Dk Mbaga wakifanya upasuaji LEO wa njia ya matundu madogo ( Laparoscopy Surgery) wa kuondoa kifuko cha ziada katika mfuko wa chakula kwa mtoto mwenye umri wa miaka 10.
  Madaktari wakifanya upasuaji wa njia ya matundu madogo kwa mtoto huyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
  Dk Zaitun wa Muhimbili akizungumza na waandishi wa habari kuhusu upasuaji huo uliofanyika leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

  0 0

  Na Lydia Churi-Mahakama

  Mahakama ya Tanzania inatarajia kukamilisha miradi ya ukarabati na ujenzi wa majengo 70 ya Mahakama katika kipindi cha miaka miwili ili kusogeza karibu huduma ya utoaji haki kwa wananchi.

  Ili kusogeza huduma hiyo kwa wananchi, majengo ya Mahakama kuu katika mikoa tisa yanatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka miwili, Mahakama za Mikoa sita zitajengwa ndani ya miezi 6-12 wakati Mahakama za Wilaya 19 na za Mwanzo 36 zinatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 2017.

  Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika hivi karibuni, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma alisema Mahakama kwa kushirikiana na Wakala wa Majengo (TBA), Chuo Kikuu cha Ardhi, Baraza la Ujenzi la Taifa, Benki ya Dunia na wadau wengine wanaendeleza na kukamilisha miradi ya ujenzi wa Mahakama Kuu katika mikoa tisa nchini. 

  Aliitaja mikoa ambayo majengo ya Mahakama Kuu yatafanyiwa ukarabati na mengine kujengwa ndani ya kipindi cha miezi 24 kuwa ni Mbeya, Kigoma, Mara, Tanga na Dar es salaam. Mikoa mingine ni Arusha, Morogoro, Mwanza na Dodoma.

  Alisema nia ya Mahakama ni kuwa na Mahakama Kuu katika kila Mkoa ili kusogeza huduma za Mahakama kwa wananchi.

  “Tunapaswa kuwa na Mahakama Kuu 26 kwenye kila ngazi ya Mkoa, kwa sasa tunazo Mahakama Kuu kwenye kanda 14 tu”, alisema Kaimu Jaji Mkuu.

  Aidha, mikoa 12 isiyokuwa na Mahakama Kuu ni pamoja na Songwe, Katavi, Njombe, Lindi, Kigoma na Mara. Mikoa mingine ni Singida, Morogoro, Pwani, Simiyu, Geita na Manyara. 

  Kaimu Jaji Mkuu alisema kuwa wakati huo huo, Mahakama ya Tanzania inatarajia kukamilisha ujenzi wa Mahakama za Hakimu Mkazi katika mikoa sita ya Manyara, Geita, Simiyu, Njombe, Katavi na Lindi katika kipindi cha kati ya miezi 6 na mwaka mmoja.

  Kwa upande wa Mahakama za Wilaya na zile za Mwanzo, Kaimu Jaji Mkuu alisema wanakusudia kujenga Mahakama za Wilaya 19 na za Mwanzo 36 ambazo zitakamilika ifikapo Desemba 2017.

  Alisema hatua hii ya ujenzi wa Mahakama hizi si tu kwamba itasogeza karibu huduma za Mahakama kwa wananchi bali pia italeta mabadiliko makubwa ya miundombinu ya mahakama na kuweka historia ya upatikana wa miundombinu kwa wingi na kwa kifundi kifupi. 


  0 0

  Immaculate Makilika- MAELEZO

  Serikali imesema inatamani kuona watanzania wanakiweka kiswahili kwenye roho zao kwa kufikiri na kuzungumza lugha hiyo katika maeneo na shughuli mbalimbali za kitaifa na kimataifa ili kukienzi pamoja na kuipa heshima inayostahili.

  Akizungumza katika kipindi cha Je tutafika? kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Channel ten, Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alisema kuwa “Tunatamani ifike mahali kila mtanzania aone fahari kuongea lugha ya kiswahili, hii itasaidia kuipa hadhi lugha hiyo kitaifa na kimataifa na hatimaye kuifanya lugha ya kiswahili kuwa bidhaa ili iweze kuuzwa”. Alisema Prof. Ole Gabrieli.

  Ambapo aliongeza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Habari imeendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuikuza lugha hiyo ikiwemo Baraza kiswahili Tanzania kutoa kamusi mpya yenye maneno zaidi ya milioni moja na nusu, na zaidi ya istilahi 40.

  Aidha, Profesa Ole Gabriel, alimpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuzungumza lugha ya kiswahili katika mikutano mbalimbali ya kimataifa, kwani hatua hiyo inasaidia kuikuza lugha hiyo na kuwavutia watu wengi zaidi kuizungumza kwa vile ni lugha inayounganisha watanzania pamoja na wananchi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  ” Lugha ni nyenzo muhimu ya kuhifadhi utamaduni, kwasababu utamaduni ndio namna tunayoishi na tunavyofikiri, hivyo watanzania tunatakiwa kufikiri na kuzungumza lugha ya pamoja ambayo kila mmoja ataelewa”.Alisema Prof. Ole Gabrieli.

  Alitoa wito kwa watanzania kuwa na utamaduni wa kuongea lugha ya kiswahili ikiwa ni pamoja kuwafundisha watoto wao kuzungumza lugha hiyo kwa ufasaha.

  Katika hatua nyingine Prof. Ole Gabrieli aliviomba vyombo vya habari nchini kuandaa vipindi na vipindi mbalimbali vyenye lengo la kukuza lugha ya kiswahili kwa kuielekeza jamii juu ya matumizi sahihi ya lugha hiyo.

  0 0

  Serikali ya Tanzania na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) wameisaini makubaliano ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo imekuwa ikitumika kwa takribani miaka 19 hadi hivi sasa.

  Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi amesema mpango huo utagharimu kiasi cha shilingi milioni 280 ambazo zimetolewa na FAO kwa ajili ya kufanya utafiti wa kuongezea takwimu ambazo zitaboresha Sera ya Misitu ya Taifa ili iweze kufikia hadhi ya kimataifa.

  Amesema hatua hiyo imekuja Kutokana na Sera ya Misitu ya Taifa ya mwaka 1998 inayotumika hadi hivi sasa kupitwa na wakati yakiwemo mabadiliko ya Kiuchumi, Kuongezeka kwa idadi ya watu pamoja na Mabadiliko ya tabia ya nchi.

  Maj. Gen. Gaudence ameeleza kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la ufyekaji misitu na hivyo kumechangia kupunguza uoto wa asili kutoka hekta milioni 55.9 kwa mwaka 1990 hadi kufikia hekta milioni 46 kwa sasa lakini Sera ya Misitu ni ile ile.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( kushoto) akiwa na Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) , Fred Kafeero (kulia) wakisaini hati ya makubaliano ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo imekuwa ikitumika kwa takribani miaka 19 hadi hivi sasa. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili) 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( kushoto) akiwa na Mwakilishi Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Fred Kafeero (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya  kupitia upya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo imekuwa ikitumika kwa takribani miaka 19 hadi hivi sasa. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
  Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akionesha kitabu cha Sera ya Taifa ya Misitu ya Mwaka ya 1998 ambayo imepitwa na wakati kutokana na mabadailiko mengi kutokea nchini. Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( kushoto) akiwa na Mwakilishi Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Fred Kafeero (kulia).( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( kushoto) akizungumza kabla kutia saini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo imekuwa ikitumika kwa takribani miaka 19 hadi hivi sasa. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)


  0 0


  Na John Nditi, Morogoro

  JESHI la Polisi mkoani Morogoro limewatia mbaroni watu  66 kwa tuhuma za  makosa ya kupatikiana na dawa za kulevya aina za heroine, mirungi na bangi viroba 39.

  Watuhumiwa hao walikamatwa wakati  wa operesheni maalumu dhidi ya mapambano ya dawa za kulevya iliyofanyika kuanzia Februari 19, mwaka huu kutoka wilaya za mkoa wa  Morogoro.

  Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, alisema  hayo Feb 20, mwaka huu ofisini mwake wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafanikio ya  operesheni inayoendelea kufanyika kuhusu  mapambano dhidi ya dawa za kulevya  kwenye  wilaya  za mkoa huo.

  Matei alisema , watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na   watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili .
   Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, akionesha kifurushi kilichohifadhi dawa za kulevya aina ya heroine iliyokamatwa  wakati wa oparesheni ya mapambano  dhidi ya  dawa za kulevya iliyofanyika  kuanzia Februari 18, mwaka huu  sambamba na ukamataji wa viroba 39  vya bangi pamoja  na mirungi  kama alivyokuwa akiwaonesha waandishi wa habari Februari  20, mwaka huu  kwenye  uwanja wa Jengo la Polisi la mkoa huo.
   Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, akionesha kifurushi kilichohifadhi dawa za kulevya aina ya heroine iliyokamatwa  wakati wa oparesheni ya mapambano  dhidi ya  dawa za kulevya iliyofanyika  kuanzia Februari 18, mwaka huu  sambamba na ukamataji wa viroba 39  vya bangi pamoja  na mirungi  kama alivyokuwa akiwaonesha waandishi wa habari Februari  20, mwaka huu  kwenye  uwanja wa Jengo la Polisi la mkoa huo.
   Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, akitoa taarifa ya operesheni ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa waandishi wa habari , Februari 20, mwaka  huu ofisini kwake .

   Gari aina ya Totota Noah yenye namba za usajili T. 799 BUG ikiwa imeshikiliwa na Polisi baada ya kukmatwa ikisafirish  bangi  viroba 21 kutoka katika kijiji cha Lubungo, Kata na Tarafa ya Mikese, wilaya ya Morogoro kwenda Jijini Dar es Salaam.( Picha na John Nditi). 


  0 0
  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wafanyakazi wanne wa Taasisi hiyo ambapo watatu kati yao wanahamia Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma na mmoja anahamia Hospitali ya kufundishia ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila kiliyopo Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wafanyakazi wanne wa Taasisi hiyo ambapo watatu kati yao wanahamia Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo Dodoma na mmoja anahamia Hospitali ya kufundishia ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila kiliyopo Dar es Salaam.
  Viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wanaohamia katika Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma na Hospitali ya kufundishia ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila kiliyopo Dar es Salaammara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwaaga wafanyakazi hao iliyofanyika jana.
  Baadhi ya Maafisa Wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na wenzao wawili wanaohamia katika Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo Dodoma na Hospitali ya kufundishia ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila kiliyopo Dar es Salaam.


  0 0

   Walimu na wanafunzi wa shule za Msimbazi na Mongo la ndege ambao ni wanachama wa chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), wakijitolea kufanya usafi katika viwanja vya Magomeni Kota, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra ya maadhimisho ya wiki ya utoaji huduma kwa wahitaji.

  Wanachama hao walioongozwa na Mwenyeikiti wa chama hicho, Profesa Martha Qorro pamoja na Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shaba walifanya usafi katika viwanja vya Magomeni Kota na Ufukwe wa Coco.

  Walimu na wanafunzi kutoka shule za Mugabe, Urafiki, Mongo la Ndege na Msimbazi ambao ni wanachama wa TGGA walishiriki ipasavyo kwenye usafi huo.

  Pia baadhi ya wanachama wa TGGA walikwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha Taifa cha Yatima cha Kurasini, Dar es Salaam.

   PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

   Wanafunzi wa Shule za Mugabe na Urafiki na walimu wao wakifanya usafi katika Ufukwe wa Coco Oysterbay, Dar es Salaam wakati wa kuadhimisha waiki hiyo ya utoaji huduma kwa wahitaji
   Wanachama wa TGGA wakifanya usafi katika viwanja vya Magomeni Kota
   Mwenyekiti wa TGGA, Profesa Martha Qorro (kushoto) na Juma Rashid wakiungana na wanachama wengine wa chama hicho kufanya usafi katika Ufukwe wa Coco, Oysterbay Dar es Salaam 

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Biseko Lisso Ibrahim WUUM (U)

  Kampuni ya Huduma ya Meli (MSCL) imesema meli yake ya MV Clarias itarejesha safari zake za kila siku kutoka Bandari ya Mwanza kwenda visiwa vya Ukerewe baada ya ukarabati mkubwa kukamilika mwishoni mwa wiki hii.

  Akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), mara baada ya kukagua meli hiyo Kaimu Mtendaji Mkuu wa MSCL, Bw. Eric Hamisi amesema meli hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 295 kwa safari moja ukarabati wake umefikia hatua za mwisho na umetumia fedha za ndani kiasi cha shilingi milioni 20.

  “Kwa muda mrefu meli zetu zimesimama kutoa huduma kwa sababu ya kukosa fedha za ukarabati, hivyo tumeweka mkakati wa muda mfupi ambapo tumeweza kukusanya fedha za madeni na tumekuja na mkakati wakudhibiti mapato ili tuweze kujiengea uwezo na kufanya ukarabati kwa meli ambazo zilikuwa zimaharibika na kukaa tu”, amesema Hamis.

  Ameongeza kuwa kwa sasa pamoja na mpango wa ukarabati wa meli hizo Kampuni iko kwenye hatua za mwisho kuboresha mifumo ya kukatisha tiketi za meli zake zote kutoka kwenye njia ya kawaida na kwenda njia ya ya kielektorniki ili kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.

  “Kwa sasa tunakamilisha utaratibu wa manunuzi ili kupata mzabuni atakayetupa huduma za ukatishaji wa tiketi kwa njia ya kielektoroniki ili kuweza kudhibiti mapato yanayopotea kwa kutumia njia za kawaida”, alisisitiza Bw. Hamis.

  Bw. Hamis ametanabaisha kuwa hatua za kumpata mzabuni wa kujenga meli mpya moja katika Ziwa Viktoria ipo katika hatua za mwisho ambapo meli hiyo ikikamilika itarahisisha usafiri katika maeneo ya Kanda ya Ziwa.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho amesema kuwa Serikali kwa sasa inashughulikia suala la mishahara ili kuimairisha utendaji wa kampuni hiyo.Aidha, amewataka kuhakikisha wanadhibiti mianya yote ya mapato ili kuhakikisha Kampuni inatumia fedha zake za ndani katika ukarabati wa meli zake.

  Kampuni ya MSCL iko kwenye mpango mkakati wa muda mfupi ambao unaishia mwezi Aprili mwaka huu ambapo pamoja na kuboresha mifumo mbalimbali imejipanga kukarabati Meli nne ambazo ni MV clarias, MV Serengeti, MT. Sangara na ML Wimbi.

  0 0


  Na Salum Vuai, MAELEZO

  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Asha Ali Abdallah, leo amefungua mkutano wa pili wa kamati za kusimamia chanjo na matumizi ya dawa barani Afrika na kutahadharisha changamoto zinazotokana na kuibuka kwa dawa zilizo chini ya kiwango.

  Katika mkutano huo wa siku tano unaofanyika kwenye hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani mjini Unguja, Katibu Mkuu huyo alisema nchi za Afrika zinakabiliwa na changamoto kadhaa katika kusimamia na kusajili dawa. Alisema baadhi ya changamoto hizo zinahitaji kuelezwa na kuchukuliwa kama suala la dharura.

  Asha alieleza kuwa, dawa bandia na chanjo, uendeshaji wa kliniki zilizo chini ya kiwango na usimamizi mdogo wa sheria na miongozo juu ya matumizi ya dawa, yanahitaji kuwekewa mikakati maalumu ili kuweza kutoa huduma bora za chanjo katika nchi za Afrika.

  “Ikiwa mamlaka ya usimamizi, AVAREF ina kazi kubwa kuhakikisha usalama wa chanjo, kuepuka urasimu na ucheleweshaji ambao unaweza kuwakosesha huduma wananchi wengi,” alisisitiza.

  Alisema katika kuhakikisha ubora na usalama wa chanjo na dawa mbalimbali katika soko, Zanzibar iliamua kuanzisha Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi (ZFDB) mwaka 2007.

  Alizitaja kazi za bodi hiyo kuwa ni kuratibu, kusajili na kufuatilia usalama wa dawa, bidhaa za chakula na vipodozi kwa mujibu wa sheria namba 2 ya mwaka 2006 inayohusu bidhaa hizo.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Ali Abdalla akifungua mkutano wa siku tano wa kamati za usimamizi wa chanjo barani Afrika unaofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View.
  Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Zanzibar Dkt. Andemichael Ghirmay akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo na kuelezea juu ya majukumu ya kamati hizo.
  Mwakilishi wa (WHO-AFRO) Dicky Akanmoni akiwasilisha mada juu ya usimamizi wa matumizi sahihi ya dawa katika mkutano wa kamati za usimamizi wa chanjo barani Afrika ulioanza leo Februari 20, 2017 mjini Zanzibar.
  Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa kamati za usimamizi wa chanjo barani Afrika wakifuatilia mada zilizowasilishwa katika siku ya kwanza ya mkutano huo.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Asha Ali Abdalla (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa kamati za usimamizi wa chanjo barani Afrika unaofanyika Zanzibar.
  Mkurungezi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed Abdalla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa chanjo na matumizi ya dawa kando ya mkutano wa kamati za usimamizi wa chanjo barani Afrika ulioanza leo Februari 20, 2017 katika hoteli ya Zanzibar Ocean View.Picha na Makame Mshenga-Maelezo.


  0 0

   Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akielezwa jambo na Meneja wa Kituo cha Kufua umeme kwa kutumia mafuta mazito (HFO) cha Megawati 60 cha Nyakato Jijini Mwanza, Mhandisi Mathew Mwangomba (kushoto). Kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi John Mageni. 
   Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kulia) akikagua Kituo cha Kufua umeme kwa kutumia mafuta mazito (HFO) cha Megawati 60 cha Nyakato Jijini Mwanza. Kushoto ni  Meneja wa kituo hicho, Mhandisi Mathew Mwangomba. 
   Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akielekeza jambo wakati wa ziara ya kukagua mitambo ya kuzalisha umeme ya Nyakato Jijini Mwanza. Kulia ni Meneja wa Mitambo, Mhandisi Mathew Mwangomba.
   Moja ya mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta mazito (HFO) kwenye Kituo cha kufua umeme cha Nyakato jijini Mwanza. Kituo hicho kina jumla ya mitambo 10 yenye uwezo wa kuzalisha kiasi cha Megawati 60 huku kila mtambo ukiwa na uwezo wa kuzalisha kiasi cha Megawati sita.


  0 0

  Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefanya ziara nchini Tunisia na kukutana na Rais wa Tunisia Mhe. Beji Caid Essebsi tarehe 17 Februari, 2017. Ziara hiyo ambayo ni muendelezo wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu ya kuwafikia viongozi wa nchi 14 za Afrika za kipaumbele katika kutekeleza mapendekezo ya Ripoti ya Kizazi cha Elimu (The Learning Generation).

  Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha kwa Rais Essebsi mapemdekezo ya ripoti ya Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu  na kuiomba Tunisia kujiunga katika mpango wa nchi za mstari wa mbele (pioneer countries) katika kufanikisha Kizazi cha Elimu ifikapo mwaka 2040. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Waziri wa Elimu wa Tunisia Mhe. Neji Jalloul.

  Kwa upande wake, Rais Essebsi wa Tunisia amemuhakikishia Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete uthabiti wa azma ya nchi yake kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu. Ameelezea utayari wa nchi yake kujiunga na mpango huo wa kufanikisha mapinduzi ya sekta ya elimu ndani ya kizazi kimoja ifikapo mwaka 2040.

  Mbali na mkutano wake na Rais wa Tunisia, awali, Rais Mstaafu alikutana na kuwa na Mkutano na Waziri wa Elimu wa Tunisia na kutembelea Kituo cha Uendelezaji Teknolojia katika Elimu kilichoko Tunis na baadae kuzungumza na wanahabari kuhusu kazi za Kamisheni na Ripoti yake.

  Kwa taarifa zaidi: 

   Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika mazungumzo na Rais wa Tunisia Mhe. Beji Essebsi
   Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokelewa na Rais Beji Essebsi katika Ikulu ya Tunisia
  Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Rais Essebsi wa Tunisia mara baada ya kumkabidhi Ripoti ya Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu

  0 0

  Taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalim inaeleza kuwa Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, limemuachia Mwenyekiti wa Chama hicho na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe usiku wa kuamkia leo baada ya kumshikilia kwa takribani masaa 10 kwa mahojiano juu ya tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevywa. 

  Mbowe alikuwa ni mmoja katika orodha ya majina 65 ya wanaodaiwa kuwa vinara wa biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya hapa nchini iliyotolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

  0 0

  Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella, akitoa hotuba ya kufunga Mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) ya nchini Marekani. Mafunzo hayo yaliratibiwa na Wizara hiyo ambapo yalitolewa kwa Maafisa Wapelelezi wa Jeshi la Polisi, Mahakimu na Waendesha Mashtaka (hawapo pichani) kwa kupewa uelewa na mbinu ya Kupeleleza, Kuendesha na Kusikiliza kesi dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu. Mafunzo hayo ya siku tano yalifanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Land Mark, jijini Dar es Salaam.
  Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella (kushoto), akipokea kitabu kinachoelezea Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu, kutoka kwa Jaji wa Mahakama Kuu nchini Marekani, Virginia Kendall. Taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) ya nchini Marekani, waliandaa mafunzo kwa Maafisa Wapelelezi wa Jeshi la Polisi, Mahakimu na Waendesha Mashtaka kwa lengo la kutoa uelewa na mbinu ya Kupeleleza, Kuendesha na Kusikiliza kesi dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu. Mafunzo hayo ya siku tano yalifanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Land Mark, jijini Dar es Salaam.
  Jaji wa Mahakama Kuu nchini Marekani, Virginia Kendall, akizungumza na Maafisa Wapelelezi wa Jeshi la Polisi, Mahakimu na Waendesha Mashtaka (hawapo pichani) kabla ya kufungwa mafunzo ya kutoa uelewa na mbinu ya Kupeleleza, Kuendesha na Kusikiliza kesi dhidi ya Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu kwa Maafisa hao. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) ya nchini Marekani na kuratibiwa na Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Mafunzo hayo ya siku tano yalifanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Land Mark, jijini Dar es Salaam.
  Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella (kulia), Afisa wa Sekretarieti hiyo, Happyness Laizer (wapili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wa Taasisi ya Wanasheria Wasio na Mipaka (Lawyers Without Borders) ya nchini Marekani, mara baada ya Mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo yaliyotolewa kwa Maafisa Wapelelezi wa Jeshi la Polisi, Mahakimu na Waendesha Mashtaka kufungwa. Mafunzo hayo yaliratibiwa na Secretarieti hiyo na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Land Mark, jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Waziri wa Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo amezindua Mafunzo ya  namna ya Kutengeneneza Taa na Chaja zinazotumia mwanga wa jua kwa vijana 20  katika Kata ya Nyegina Mkoa wa Mara.

  Akifungua mafuzo hayo Profesa Muhongo amewataka vijana hao kuwa mabalozi wazuri wakati wanapohudhuria mafunzo na kueleza kuwa, yatakuwa chachu katika kupanua wigo wa  wa ajira ikiwemo wahitimu kujiari wenyewe.

  Profesa Muhongo amewataka vijana na wananchi mkoani humo kuweka nguvu kubwa katika elimu kutokana na umuhimu  na mchango wake kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

  Akizungumzia kuhusu Mradi wa Usambazaji Vijijini Awamu ya Tatu, Profesa Muhongo ameeleza kuwa, awamu hiyo itaanza kutekelezwa kuanzia mwezi Machi mwaka huu na kuongeza kuwa, mradi huo utafanywa kwa Awamu na kusisitisza kuwa, adhma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa, ndani ya kipindi cha miaka mitano vijiji vyote nchini viwe vimeunganishwa na nishati hiyo.

  " Vijiji vyote vitaunganishwa na nishati ya umeme. Tutasambaza  awamu kwa awamu na lengo letu ni kuhakikisha kuwa, vijiji vyote chini vinaunganishwa na umeme ndani ya kipindi cha miaka mitano. Wale ambao hawajafikiwa awamu ya kwanza na ya pili tutawafikia awamu ya tatu vivyo hivyo mpaka tufikie lengo letu," amesisitiza Prof. Muhongo.

  Kwa upande wake Balozi wa Korea Kusini nchini, Song Geumyoung ambaye nchi yake imefadhili mafunzo hayo, amesema kuwa,  uwepo wa taa hizo utasaidia upungufu wa umeme hususan maeneo ya vijijini na ambayo bado hayajaunganishwa na nishati hiyo.
  Aidha, amesema kuwa, mafunzo hayo ni fursa ya ajira kwa wahitimu watakaopata mafunzo hayo ikiwemo nafasi za kuajiriwa na hivyo kuwataka kutilia mkazo mafunzo hayo na kueleza kuwa, mafunzo hayo ni mwanga kwa vijana.

  Aidha, ameongeza kuwa,  kutokana na urafiki wa miaka mingi baina ya nchi za Tanzania nasini , hirikinchi hiyo itlea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na umeme wa uhakika.
  "Kama ilivyo kwa kaulimbi ya Awamu ya  Tano ya Rais Dkt. John Magufuli, Hapa Kazi Tu' na mimi napenda kusema tusiende polepole twende 'Haraka, Haraka", amesisitiza Balozi  Geumyoung.
  Kwa mujibu wa Professa Muhongo mafunzo hayo yanatarajiwa pia kutolewa katika  Kata za Mwirangi, Bukima na Mgango.

   Naye Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dkt.  Hong- Kyu Choi, amesema kuwa, baada ya kuzifikia Kata zote zilizoainishwa, watachaguliwa wanafunzi bora ambao watakuwa mabalozi wa mafunzo hayo na hivyo kuwataka washiriki wa mafunzo hayo kufuatilia mafunzo hayo na kuyachukulia kwa uzito mkubwa.

  Mbali na kufungua mafunzo hayo, Profesa Muhongo pia amekagua miradi ya umeme Awamu ya Pili inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Kome katika kijiji cha Kome, Kata ya Bwasi.
  Mafunzo hayo yamezinduliwa tarehe 20 Februari,2017
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akionesha mfano wa Taa zinazotumia mionzi ya jua ambazo vijana 20 katika Kata ya Nyegina watafundishwa namna ya kuzitengeneza baada ya kuzindua mafunzo hayo. Kulia ni Balozi wa Korea Kusini nchini, Song Geumyoung na kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo Dkt. Hong- Kyu Choi.
  Mkufunzi wa mafunzo ya kutengeneza Taa na Chaja zinazotumia mionzi ya jua, Dkt. Dkt. Hong- Kyu Choi, akiwaleza washiriki wa mafunzo namna mafunzo hayo yatakavyoendeshwa.
  Mkuu wa Wilaya ya Musoma Vijijini, Dkt. Vicent Naano, (wa tatu kushoto) akiongea jambo mara baada ya uzinduzi wa mafunzo ya Kutengeneza taa na chaja zinazotumia mionzi ya jua. Wengine ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muongo (katikati), Balozi wa Korea Kusini nchini,Song Geumyoung Mkufunzi wa mafunzo hayo Dkt. Hong- Kyu Choi (wa pili kulia) na baadhi ya wawakilishi wa vijana wanaoshiriki mafunzo.


older | 1 | .... | 1578 | 1579 | (Page 1580) | 1581 | 1582 | .... | 3272 | newer