Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

BOSI WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA AINADI NHC NCHINI SINGAPORE

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Bw. Nehemia Mchechu akilinadi shirika lake kwa wawekezaji wa Singapore katika hoteli ya Swissotel jijini Singapore

NBC donated books and other educational materials at Buguruni Primary School

0
0
NBC Chief Operating Officer, Maharage Chande addressing a section of the students (not in picture) during a brief handover ceremony held at Buguruni Primary School for Deaf Children. NBC donated books and other educational materials to the school recently.
NBC Chief Operating Officer, Maharage Chande hands over books to Buguruni Primary School for Deaf Children Head Teacher Ms. Winfrida Jeremiah who received them on behalf of the School. NBC COO’s department recently donated books and other educational materials to the school on behalf of the bank.

UJUMBE WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA VIETNAM WATUA DAR ASUBUHI HII

0
0
 Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Kimomunisti Cha Vietnam (CPV), Hoang Binh Quan, baada ya ujumbe wa CPV kuwasili asubuhi hii kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Quan na ujumbe wake wanatarajiwa kuwa na mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baadaye leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam, Ramadhani Madabiba.
 Balozi wa Vietnam Tanzania, NguyenThien akimtambulisha Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Kimomunisti Cha Vietnam (CPV), Hoang Binh Quan kwa katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Martin Shigela (kulia) baada ya kushuka katika ndege, kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Kimomunisti Cha Vietnam (CPV), Hoang Binh Quan, baada ya kumpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere asubuhi hii.
 Katibu wa NEC ya CCM, Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akiwatambulisha kwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Kimomunisti Cha Vietnam (CPV), Hoang Binh Quan, viongozi wa CCM aliofuatana nao katika mapokezi hayo, wakiwa chumba cha mapumziko Uwanja wa Ndege wa JN.
 Dk.Asha-Rose Migiro na mgeni wake, wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa mgeni huyo na viongozi wengine wa CCM, wakati wa mapokezi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JN, Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BASHIRI  NKOROMO

Waziri Mkuu Mizengo Pinda afungua Mkutano Mkuu wa kujadili Utekelezaji wa Miradi ya Maji Vijijini, Jijini Arusha leo

0
0
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akihutubia wajumbe (hawapo pichani) wakati wa ufungunzi wa Mkutano Mkuu wa kujadili Utekelezaji wa Miradi ya Maji Vijijini, Jijini Arusha unaojadili utekelezaji wa kuwapatia wananchi wa vijijini huduma ya maji kwa mwaka 2012/2013 na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji huo.
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe (Mb) akihutubia wajumbe (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa kujadili Utekelezaji wa Miradi ya Maji Vijijini, unaojadili utekelezaji wa kuwapatia.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Magesa Mlongo akiwakaribisha Wajumbe kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Kujadili Utekelezaji wa Miradi ya Maji Vijijini, jijini humo. wananchi wa vijijini huduma ya maji kwa mwaka 2012/2013 na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji huo.
Wajumbe wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa kujadili Utekelezaji wa Miradi ya Maji Vijijini, Jijini Arusha unaojadili utekelezaji wa kuwapatia wananchi wa vijijini huduma ya maji kwa mwaka 2012/2013 na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji huo.

mdau George na bi. Nembris Wameremeta

0
0
Hayawi hayawi yamekuwa , Bwana harusi George Madinda akimvisha pete ya ndoa mkewake Nembris Jackson wakati wa ibada ya ndoa yao ilioyofanyika katika kanisa la Angrican Mt. Batholomea lililopo Ubungo ,na kufuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika ukumbi wa Mbezi Garden jijini Dar es Salaam.
Bibi harusi Nembris Jackson akimvisha pete ya ndoa mme wake George Madinda wakati wa ibada ya ndoa yao ilioyofanyika katika kanisa la Angrican Mt. Batholomea lililopo Ubungo ,na kufuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika ukumbi wa Mbezi Garden jijini Dar es Salaam.
Bwana harusi George akiwa katika pozi la picha na mkewe Bi,Nembris baada ya kufunga ndoa yao Takatifu katika Kanisa la Anglican Mt. Batholomayo Ubungo jijini Dar es Salaam, na kufuatiwa na sherehe ya kuwapongeza iliyofanyika katika Ukumbi wa Mbezi Garden.

WAJUMBE WA BODI YA NHIF WAFANYA ZIARA MAKAO MAKUU

0
0
Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) jana walifanya ziara katika ofisi za Makao Makuu ya Mfuko huo kwa lengo la kutembelea ofisi hizo na kuangalia mazingira ya kazi. 

 Wajumbe walioteuliwa hivi karibuni wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Ali Mchumo, Mwanaidi Mtanda, Ezekiah Oluoch, Donan Mmbando, Mohamed Mohamed, Lydia Choma, Mohamed Hashim, Charles Kajege na Emanuel Humba ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo.
Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Raphael Mwamoto walipozuru Makao Makuu jana.
Mkurugenzi wa Uendeshaji, Eugen Mikongoti akitoa maelezo ya namna ya kuhifadhi kumbukumbu za wanachama katika kituo cha kisasa cha Mfuko huo.
Wajumbe hao wakipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa NHIF namna ya upatikanaji wa haraka wa kumbukumbu za wanachama zinazohifadhiwa katika kituo hicho.
Wajumbe wakiendelea kujifunza zaidi katika kituo cha kuhifadhia kumbukumbu.
Mkurugenzi Mkuu Emanuel Humba (wa nne kulia) akifafanua jambo wakati wa ziara hiyo.

Kero ya Mdau juu ya Matangazo yanayotumwa kwenye Email za Watu

0
0
Habari yako mkuu wa Libeneke.

Mimi naomba msaada wako maana kwa wiki kadhaa sasa nimekuwa nikipata unsolicited emails kutoka kwa watu wanajiita Dar-Insight ambao wanatuma matangazo ya ajabu ajabu ambayo mi hayanihusu, siyataki na yananijazia tu inbox yangu. Ubaya ni kwamba email zao hazina hata option ya ku-unsubscribe. Nimewaandikia mara kadhaa kuniondoa kwenye mailing list yao bila mafanikio kwani bado naendelea kupata email zao kadhaa kila siku.

Sasa naomba msaada kwa wadau kwanza kujua inakuwaje hawa watu wa push tu matangazo yao kwa watu ambao hawakujuandikisha wala kukubali kutumiwa matangazo yao. Sijui hata email yangu waliipata wapi.

Pili naomba kujua kwamba kwa sheria za Tanzania, ni hatua gani naweza kuchukua kuwashughulikia hawa jamaa maana email zao binafso zinanikera sana na nimejaribu njia ya kiungwana ya kuwaandikia email kuwaomba wasinitumie wamegoma kufanya hivyo. So hatua gani naweza kuchukua?

Asante sana, siku njema na sikukuu njema ya kupaa kwa Mtume.

Mdau anayekerwa na Dar-Insight.

DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA BALOZI WA OMAN NCHINI

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Maapinduzi DK Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Yahya Moosa Albakri,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar Leo asubuhi kwa mazungumzo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Maapinduzi DK Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Yahya Moosa Albakri,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar Leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Maapinduzi DK Ali Mohamed Shein,akifuatana na Balozi wa Oman Nchini Tanzania Yahya Moosa Albakri,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar Leo asubuhi,baada ya mazungumzo yao.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

Maonyesho ya Wurzburg Festival Ujerumani,Yavamiwa na mafuriko ya maji

0
0
Jumamosi ya tarehe 1 Juni 2013,katika viwanja vya maonesho ya Wurzburg Festival, Kulikuwa na majonzi na simanzi baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko yaliyosababisha hasara kubwa na kuvunjwa kwa tamasha hilo lililokuwa likisherekea miaka 25.

Habari za uhakika zimevuja kuwa vikosi vya zimamoto na wanausalama viliingiwa na mashaka baada ya wanii wa Ngoma Africa band aka FFU,kutoweka ghafla katika chumba cha kubadilishia nguo (back Stage) na kutojulikana waliko, wasi wasi ulitanda labda watakuwa wamezolewa na mafuriko !

Lakini baada ya masaa kadha watayarishaji waligundua kuwa mkuu wa bendi hiyo field-marshal Kamanda Ras Makunja alikiondoa kikosi chake baada ya makachero wa bendi hiyo maarufu kama "Anunnaki Empire" kumtonya boss wao kuwa eneo la festival sio salama mto ulio jirani wa eneo hilo unajaa maji kwa kasi,Kamanda bila kuaga kawatoa FFU wa Ngoma Africa band katika hali ya usiri na kuwanusuru vijana wake, na simu yake ikazimwa hadi baada ya masaa fulani ndipo ikawashwa na kuwajulisha waandalizi wa onyesho wasiwe na shaka kamanda na kikosi cha Ngoma Africa band wapo salama kambini,kitendo hicho kiliwaacha midomo wazi baadhi ya wadau ! wengine kudiriki kusema kuwa Simba ni Simba.

Wadaku watonya kuwa tamasha hilo lilianza mwishoni mwa mwezi mei siku ya ijumaa 31.Mai 2013 kukiwa na maelfu ya watu na wasanii mbali mbali walioalikwa wakiwamo mkongwe Manu Dibando,Alfa Blondy,Salifu Keita ndio walioanza kufungua dimba, Ijumaa hiyo hali ilikuwa shwari lakini ilipofika jumamosi hali ya hewa ilianza kubadilika kwa mvua na upepo,wasinii wengine wakiwa kwenye vyumba vya kujitayarishia miongoni mwao wakiwamo "Ngoma Africa band " a.k.a FFU Ughaibuni, baada ya hali ya hewa kuanza kubadilika kwa upepo na mvua ndio inasemekana kuwa mkuu wa F.F.U Kamanda Ras Makunja na kikosi chake Ngoma Africa band,Kuondoka katika eneo la festival (eneo la hatari) liliokumbwa na maji, katika mazingira ya ajabu. Watonyaji wa habari wamedai kuwa walitoroshwa kwa magari mawili meusi aina ya van yalikuwa na madilisha ya kiza.

Kamanda Ras Makunja kateleza kama nyoka na kikosi chake. Mafuliko hayo yamevamia pia baadhi ya miji nchini Ujerumani na ulaya ya mashariki ka kusababisha vifo vya watu 12.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa eneo la tukio
Watu wote walilazimika kuondoka eneo hilo.

Mpigie Kura Feza Kessy abaki kwenye Jumba la Big Brother

News Alert: Mume wa Khadija Kopa afariki Dunia leo

0
0
Taarifa zilizopatikana mapema leo asubuhi,zinaeleza kuwa Mume wa Mwanamuziki Mkongwe wa Miondoko ya Taarab,Malkia wa Mipasho,Bi. Khadija Kopa, aitwaye Jaffari Ally amefariki dunia usiku wa kuamkia leo majira ya saa 9 usiku.

Taarifa za kuthibitika juu ya msiba huo,zimetolewa na Katibu wa Bendi ya TOT,Gasper Tumaini.

Taarifa za awali zilieleza kwamba chanzo cha kifo chake ni ugonjwa wa Malaria, ambapo siku ya Jumatatu marehemu Ally alipelekwa Hospitali ya Lugalo kwa ajili ya kupata matibabu.

Taarifa zaidi zinasema kwamba marehemu alipata nafuu na kurudi nyumbani kwao Bagamoyo, hali ambayo ilimpelekea Khadija Kopa kusafiri kikazi, na inasemekana mpaka umauti unamkuta Jaffari, Mkewe Khadija Kopa alikuwa yupo kikazi mikoani kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki.

SHUKRANI – TANZIA

0
0
ADELAIDA JOHN KWALEWELE MIKONGOTI (BINTI KWALE)

Familia ya Marehemu Pius Hassan Ngavochya Mikongoti ya Dar Es Salaam inapenda kutoa shukrani za dhati kwa kutufariji katika msiba mkubwa tulioupata kwenye familia kwa kuondokewa na Mama Yetu kipenzi Adelaida John Kwarewele Mikongoti (Bint Kware) mnamo tarehe 27th May 2013 huko Mlimba Ifakara Morogoro na kuzikwa huko Kijijini Mlimba Ifakara Morogoro.

Sio rahisi kumshukuru kila mmoja lakini kwa namna ya pekee tunapenda kutoa Shukrani zetu za dhati kwa Kaimu Baba Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Mahenge Father Mcharange kwa kushiriki nasi kwenye misa mpaka maziko ya Mpendwa mama yetu, Pia twamshukuru kwa namna ya pekee Paroko wa Parokia ya Mlimba kwa kuwa nasi karibu siku zote tangu kuumwa mpaka siku ya mazishi ya kipenzi mama yetu, Twamshukuru pia Mchungaji Mwasongwe wa Kanisa la Moraviana Mabibo Dar es salaam na Mchungaji na waumini wa wa Moravian Kanisa la Mlimba na Uongozi wa Msikiti Mkuu wa Mlimba – Ifakara.
 
Vile vile familia kwa namna ya pekee inapenda kuwashukuru Madaktari na Wafanyakazi wa Tumaini Hospital, Regency na Aghakhan na Hospitali ya Mlimba ambako marehemu alikuwa akitibiwa kwa matatizo yake ya kisukari, Pia Familia inatoa shukrani za dhati kwa Uongozi wa wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Uongozi na Wafanyakazi wa Rufiji River Basin Iringa, Uongozi na wafanyakazi wa Tanesco Kigamboni-DSM na Mlimba Kihansi, Uongozi na Wafanyakazi wa GS1 Tanzania, Idara ya Uhamiaji Makao Makuu – Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Uongozi wa Nakiete Pharmacy, Brons Investments,  Pia kwa namna ya kipee tunawashukuru Mr. Tamim Lukuta kwa niaba ya Friends of Mlimba, Zebby Kipussy na wengineo ambao walikwenda nasi mpaka Mlimba kuanzia siku ya kwanza mpaka siku ya mwisho, Bila kuwasahau Marafiki wa Mrs Baldwina Msomba na waumini wa Kanisa la Moravian Mabibo, Marafiki, Majirani wa Dar Es Salaam, Mlimba, na kwingineko ambao waliguswa na matatizo yetu na kwa namna ya kipekee kutufariji na kuwa nasi mpaka kijijini Mlimba.

Marafiki, jamaa na watakia heri wote waliokuwa wakitufariji kwa simu, kwa meseji kiukweli familia imefarijika sana na sisi kama familia hatuna cha kuwalipa ila tunawaweka kwenye sala zetu kwani mmetuachia deni.

Misa ya arobaini ya Kumuombea Marehemu itafanyika Kijijini Mlimba tarehe 12 kuamkia 13 Julai 2013.

Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe.

Raha ya Milele Umpe Eeeh Bwana …. Na Mwanga wa Milele Umuangazie. Apumzike kwa Amani – Amina.

Mapitio ya magazeti leo

Hotuba Ya Bajeti Ya Wizara Ya Fedha 2013-14

Hali ilivyokuwa baada ya Khadija Kopa kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe

0
0
Mkuu wa mkoa Rukwa Eng. Stalla Manyanya (kushoto) akimfariji msanii na taarab na malkia wa mipasho Tanzania,Khadija omar Kopa alipokua kwenye chumba maalum cha kupumzikia wageni kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leoa alfajiri kutokana na ugonjwa, Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani kitaifa yaliyoaadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana.
Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kuapanda ndege msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania Khadija Omar kopa kwenye uwanja wa ndege wa mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leo alfajiri kutokana na ugonjwa, Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye Maadhimnisho ya siku ya Mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana.
 (Picha na ofisi ya Makamu wa Rais)

News Alert: mabadiliko ya makamanda na wakuu wa upelelezi katika baadhi ya mikoa hapa nchini.

0
0
Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Said Mwema, leo amefanya mabadiliko ya makamanda na wakuu wa upelelezi katika baadhi ya mikoa hapa nchini.

Katika mabadiliko hayo aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Michael Kamhanda amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhani Mungi ambae alikuwa Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai.

Aidha, DCP Ally Mlege aliyekuwa Makao Makuu ya Polisi amehamishiwa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwenda kuwa Mkuu wa utawala na raslimali watu.

Vilevile, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi wa makosa ya jinai  na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Arusha ACP Camilius Wambura. Aidha, ACP Duwan Nyanda aliyekuwa Makao Makuu ya Upelelezi anaenda kuwa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Arusha.

Uhamisho huo ni wakawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.


Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (T).

Balozi Kamala ashiriki Mkutano wa Taasisi ya Uwekezaji nchini Ubelgiji

0
0
Balozi wa Tanzania BENELUX na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji Tanzania kwa Wanachama wa Taasisi ya Uwekezaji ya Ubelgiji (FIT). Mkutano umeandaliwa na FIT kwa kushirikiana na Balozi za Tanzania na Kenya Brussels.
Wanachama wa Taasisi ya Uwekezaji ya Ubelgiji (FIT) Wakimsikiliza Balozi. Dr. Diodorus Buberwa Kamala kuhusu fursa za Uwekezaji Tanzania.

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR AZUNGUMZA NA WALIMU WILAYA YA KATI UNGUJA

0
0
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna akisisitiza jambo wakati alipozungumza na Wazazi pamoja na Walimu wa Wilaya ya Kati Dunga alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea Maskuli mbalimbali ya Unguja na Pemba na kukutana na walimu pamoja na kamati za wazazi ilikutatua matatizo mbalimbali yanayokabili katika Maskuli hayo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Kiboje Haji Shaban Waziri akitoa mchango wake kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna hapo Dunga Wilaya ya Kati katika ziara ya kutembelea Maskuli mbalimbali ya Unguja na Pemba ilikutatua matatizo mbalimbali yanayokabili katika Maskuli hayo.
Baadhi ya Wazazi pamoja na walimu wa Wilaya ya Kati waliohudhuria katika Mkutano wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali Ali Juma Shamhuna huko Dunga wakati alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea Maskuli mbalimbali ya Unguja na Pemba na kukutana na walimu pamoja na kamati za wazazi ilikutatua matatizo mbalimbali yanayokabili katika Maskuli hayo.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

REDD'S MISS MARA 2013 YAPEWA MIL. 10 KUTOKA AFRICA BARIC GOLD

0
0
Ofisa kutoka kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano wa Barrick Gold Mining Fatuma Mssumi akimkabidhi Kaimu Ofisa Tawala wa Mkoa wa Mara mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 10, ikiwa ni sehemu ya udhamini wa kampuni hiyo kwenye mashindano la Redd's Miss Mara yatakayofanyika leo mjini Musoma.
Baadhi ya washiriki wa shindano la Redd's Miss Mara 2013 wakiwa katika picha ya pamoja jana ikiwa ni siku moja kabla ya warembo hao hawajapanda jukwaani kuwania taji hilo ambalo linashikiliwa na Miss Tanzania namba mbili 2012. Shindano hilo linataraji kufanyika leo.

TAARIFA YA MSIBA

0
0
FAMILIA YA MAREHEMU JUMANNE NYANGASA WA DAR ES SALAAM, WANASIKITIKA KUONDOKEWA NA MAMA YAO MPENZI BI MAAJABU KHATIBU ABDALLAH MGANGA (83) (MAMI FATUMA), ALIYEFARIKI TAREHE 6/6/2013 SAA SABA MCHANA NYUMBANI MANZESE, MWILI UMEHIFADHIWA MWANANYAMALA HOSPITAL. 

 SHUGHULI ZOTE ZITAFANYIKA MANZESE TUNATEGEMEA KUUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU TAREHE 7/06/2013 SAA 10 KUELEKEA KIJIJINI MASIMBANI MUHEZA TANGA KWA AJILI YA MAZISHI YATAKAYOFANYIKA JMOSI, 8/06/2013.

“INNALILAHI WAINA ILAIHII RA’JUUN”
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live


Latest Images