Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1574 | 1575 | (Page 1576) | 1577 | 1578 | .... | 3272 | newer

  0 0


  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Wahanga wa Ajali ya kufukiwa na kifusi katika Mgodi wa Dhahabu wa RZ uliopo katika Kijiji cha Mawemeru, Nyarugusu Mkoani Geita iliyotokea tarehe 26 Januari, 2017.

  Aidha, Prof. Muhongo amewataka Makamishna Wasaidizi wa Madini kote nchini kuchukua hatua za haraka kusimamia mazoezi ya uokoaji pindi zinapotokea ajali migodini pasipo kusubiri miongozo ya Waziri.

  Pia amewaagiza Makamishna hao kufanya ukaguzi katika migodi mikubwa na midogo katika maeneo nayo na kuongeza kuwa, zoezi hilo la ukaguzi linatakiwa kufanywa haraka.Pia amemtaka Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi, kufuta leseni zote za uchimbaji madini ambazo hazifanyi kazi.

  Akizungumzia kuhusu kuwaendeleza wachimbaji wadogo chini, Prof. Muhongo amesema kuwa, Sera na mipango ya Serikali ni kuwandeleza wachimbaji hao na kuhakikisha kuwa, wanatoka katika uchimbaji mdogo kwenda uchimbaji wa Kati.

  Katika hatua nyingine, Prof. Muhongo ameitaka Migodi Mikubwa yote nchini kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam na kueleza kuwa, migodi hiyo imepewa wiki 6 iwe imejiandikisha katika soko hilo.

  Pia Prof. Muhongo amemshukuru Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, Mkoa wa Geita, Viongozi wa Wizara, Wachimbaji na kampuni zote zilizoshiriki zoezi la uokoaji na kufanikiwa kuokolewa kwa wachimbaji 15 waliofukiwa na kifusi.
  Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akisalimiana na baadhi ya Wahanga wa ajali ya kufukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ, Mkoani Geita. Prof. Muhongo alifika mgodini hapo wakati wa ziara yake mkoani humo.
  Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga (katikati) akimuongoza Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na ujumbe wake kuelekea katika eneo la mgodi wa dhahabu wa RZ.
  Mkuu wa MKoa wa Geita Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga akimwongoza Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo katika eneo la mgodi ambapo wachimbaji wadogo 15 walifukiwa na kifusi.
  Mkuu wa MKoa wa Geita Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga akimwongoza Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo katika eneo la mgodi ambapo wachimbaji wadogo 15 walifukiwa na kifusi.
  Wachimbaji wadogo wakimwonesha Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na ujumbe wake namna walivyookolewa baada ya kufukiwa na kifusi katika mgodi wa dhahabu wa RZ, uliopo eneo la Nyarugusu mkoani Geita.
  Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi akiwaongoza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga na ujumbe wake kuelekea katika eneo la mgodi ambako wachimbaji 15 walifukiwa na kifusi na kuokolewa wote wakiwa hai.


  0 0

  Na Eliphace Marwa, Dar es salaam

  Chama cha Wakandarasi Tanzania kimeiomba Serikali kuwashirikisha katika zabuni za ujenzi wa miradi mbalimbali ya umma Wakandarasi wazawa.

  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Chama hicho, Mhandisi Lawrence Mwakyambiki wakati mkutano na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali katika sekta ya ujenzi hapa nchini.

  Alisema kuwa wanaiomba Serikali ya Awamu ya Tano kuwashirikisha wakandarasi wa kitanzania , wakimemo wakandarasi wa madaraja yote ili waweze kujijengea kitaalamu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo ujenzi wa majengo mbalimbali ya Serikali mkoani Dodoma.

  Mhandisi Mwakyambiki aliongeza kua hatua hiyo itasaidia kuongeza ajira kwa vijana na Kampuni za kitanzania katika shughuli za ujenzi hapa nchini.

  Aidha, Chama hiyo kimeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza mikakati na kusimamia sekta ya ujenzi hapa nchini.

  Aidha Mwakyambiki aliongeza kuwa kutokana na uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano kuhamia Dodoma ni vema wakandarasi wa ndani wakapewa fursa ya kushiriki katika kandarasi mbalimbali ambazo serikali inatarajia kuzifanya huko Dodoma.

  Kwa upande Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi John Bura alimshukuru Rais Magufuli na Serikali yake kwa kuitikia wito wa wakandarasi kwa kuwatengea miradi michache ambayo ilikwisha tangazwa.

  Aliwataka wakandarasi kuunda umoja kwa ajili ya kuitekeleza kwa weledi ili kuongeza imani kwa Serikali. 
  Mwenyekiti wa Chama Cha Wakandarasi Tanzania, Mhandisi Lawrence Mwakyambiki akisistiza jambo kwa waandishi wahabari (hawapo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam kuhusu Serikali kuwapa kipaumbele wakandarasi wa ndani katika miradi ya ujenzi. 

  0 0


  MAMLAKA ya Uendelezaji Kanda Maalum za Kiuchumi (EPZA)na Kiwanda kilichopo ndani ya Mamlaka hiyo ya Tooku kinachojishughulisha na utengenezaji wa nguo zimetozwa faini ya kiasi cha sh.mill 30 kwa kosa la kutililisha maji machafu katika makazi ya watu. 

  Ambapo EPZA inapaswa kulipa faini ya Mill20 huku Kampuni ya TOOKU kulipa faini ya mill 10 na kuhakikisha zinarekebisha mifumo yake ya kupitisha maji taka ipasavyo na kuunganisha katika Mfumo maalum wa Dawasco . 

  Akizungumza Jijini Dar es Salaam ,Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano,Luhaga Mpina wakati wa ziara yake ya kukagua baadhi ya viwanda nchini,kuangalia hali ya mazingira ambapo aliambatana na Maofisa mbalimbali kutoka 

  Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC),alisema faini hizo zinapaswa kulipwa ndani ya siku 14.Mpina alisema anahasira zaidi na taasisi za serikali zisizofata sheria ya mazingira na kutililisha maji machafu katika makazi ya watu. 

  "Nina hasira na taasisi hizi za serikali kwani serikali yenyewe haiwezi kugeuka kupeleka sumu kwa wananchi wake, ambao muda wote inawazuia na kuwakinga wananchi hao hao wasipatwe na 
  madhara,"alisema 

  Alisema wanapokuta na taasisi ya serikali zinazokiuka miiko iliyoweka katika utunzwaji wa mazingira ni lazma wawapige faini kubwa zaidi kuliko taasisi binafsi ili kuweza kuwa mfano mkubwa kwa jamii.Mpina alisema Mamlaka hiyo ya Uendelezaji Kanda Maalum za Kiuchumi EAPZ ilisema kuwa mfumo wao wa kuyabeba maji taka na kuyapeleka katika mfumo rasmi wa maji taka wa Dawasco umeharibika lakini hawakuweza kuwaandikia NEMC barua ya taarifa juu ya matatizo hayo. 

  "Nawataka EPZA ndani ya siku saba mfumo wa kupitishia maji taka wa EPZA uwe umetengenezwa na kukamilika hivyo kuzuia maji taka yanayotoka kutotoka tena kwa sababu yatakuwa yanaingia rasmi katika mfumo wa Dawasco,"alisema.Aidha alisema kwa upande wa Kampuni ya TOOKU yenye inatakiwa kufanya marekebisho makubwa katika mitambo yake ya kutibu maji taka kwani inaonekana kuwa na kasoro. 
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiwa katika ziara ya ukaguzi wa Mazingira katika kituo cha uwekezaji cha EPZA, kilichopo Ubungo Jijini Dar es salaam. 
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiangalia shughuli za uzalishaji wa nguo katika kituo cha uwekezaji cha EPZA mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mazingira katika kituo hicho kilichopo Ubungo Jijini Dar es salaam. 
  . Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiangalia suruali aina ya Jinsi zinazozalishwa katika kituo cha uwekezaji cha EPZA wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa mazingira mapema hii leo Jijini Dar es salaam. 
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiangalia mfereji wa maji machafu yanayotiririshwa na kituo hicho ambayo yamekuwa ni kero kwa wananchi.


  0 0

  Na Zainul Mzige.

  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amesema kwamba wizara yake itashirikiana na wizara nyingine nchini kuhakikisha kwamba migogoro ya walimu inamalizwa ili kufanikisha utoaji wa elimu kuwa bora na jumuishi.  Kauli hiyo aliitoa wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika siku ya pili ya kuhitimisha kwa mkutano ulioshirikisha nchi 13 za Afrika Mashariki kujadili lengo la nne la elimu kati ya malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs).  Alisema kwamba migogoro ya walimu inayogusa mishahara, marupurupu pamoja na mazingira bora ya kazi linagusa pia Wizara za TAMISEMI na UTUMISHI na kusema kwamba wao kama wasimamizi wa elimu watakachoweza kufanya ni kuzungumza na wenzao kuhakikisha kwamba migogoro hiyo inafutwa ili utoaji wa elimu uendane na mipango ya kitaifa na kidunia ya lengo la maendeleo 2030.  Pamoja na kujibu swali hilo Prof Ndalichako alizungumzia  kwamba walimu walikuwa ni ajenda muhimu  na humo walikubaliana kwamba mwalimu ni kila kitu katika utoaji wa elimu na kuwa hawawezi kufanikiwa katika elimu bora na jumishi bila kuwa na walimu wenye umahiri, wanaowezeshwa kufanya hivyo.Kutokana na ukweli huo wamejipanga kuhakikisha kwamba walimu wanapata mafunzo bora na kuwakutanisha kubadilishana uzoefu.

  Alisema kila nchi itakuwa na mpango mkakati wake na kuonesha viashiria kwamba vinatekelezwa kwa namna gani. Mwisho wa siku mwaka 2030 mataifa yote yanapaswa kuhakikisha kwamba agenda namba 4 ya maendeleo endelevu ya elimu imetekelezwa.  Alisema katika mkutano huo wa siku mbili wa mawaziri wa elimu ulioandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na ILO, UNFPA, UNDP, UNICEF, UN Women, UNHCR pamoja na World Bank wamebainisha kwamba mikakati ya pamoja ni lazima ichukuliwe ili kufanikisha elimu jumuishi yenye usawa na ubora kwa watu wote huku ikitoa fursa ya elimu kwa wakati wote.

  Alisema kwamba mkutano ulitambua kwamba elimu haina mwisho, elimu inataka kuwa na mfumo wa kuwa na maendeleo ya kujifunza kwani mambo hayasimami kutokana na kubadilika kwa teknolojia, hivyo elimu inayotolewa haina budi kujazia nafasi hiyo kwa kuwapa uhuru watu kujisogeza zaidi.  Alisema nchi hizo 13 zimekubaliana kwa pamoja kufikia malengo endelevu 2030 kama yalivyosainiwa na kila nchi mwaka 2015 kwa kuweka mikakati ili mataifa hayo yaweze kufikia malengo yanayotakiwa.
  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akielezea jitihada zitakazofanywa na serikali ya Tanzania katika kuboresha sekta ya elimu kuelekea utekelezaji wa SDG4 kwenye mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar es Salaam.
    Mwenyekiti wa Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu ambaye pia ni Mkurugenzi wa UNESCO Kanda ya Mashariki mwa Afrika, Bi. Ann Therese Ndong-Jatta akiendesha mjadala wa kuhitimisha mkutano huo wa siku mbili wa wadau wa elimu kutoka nchi 13 uliofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Conventional Centre (JNICC) jijini Dar es Salaam. (Habari picha na Zainul Mzige)

  Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, iliyona makazi yake nchini Marekani akielezea kuhusu mradi wa XPRIZE unahusisha watoto ambao hawapo shuleni ukiwa na malengo ya kukuza teknolojia ya dunia kwa kutumia uwezo walionao ukilenga watoto wa miaka 5-12 wakati wa kuhitimisha mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Elimu, Rasilimali Watu na Tafiti za Kisayansi wa Mauritius, Leela Dookon Luchoomon (kushoto) akieleza mipango ya serikali yake katika kuboresha elimu wakati wa kuhitimisha Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na ILO, UNFPA, UNDP, UNICEF, UN Women, UNHCR pamoja na World Bank.
   Balozi wa Canada nchini Tanzania, Ian Myles akizungumza kwa niaba ya nchi wahisani wakati wa kuhitimisha Mkutano wa mawaziri wa Afrika Mashariki wa kujadili namna ya kufanikisha lengo la nne la elimu (SDG4) kati ya malengo 17 ya dunia ya maendeleo endelevu.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Fundi wa kuchoma vyuma kwa kutumia teknolojia ya gesi akiendelea na zoezi la kuchoma kufuli ya lango la ghala lililofichwa kwenye hoteli ya Butterfly iliyopo mtaa wa Muhonda eneo la Kariakoo. Ghala hilo limekutwa na shehena kubwa ya kazi haramu za muziki na filamu.
  Mmiliki wa ghala lilolokutwa chini ya hoteli ya Butterfly Phili Ulaya akijaribu kujitetea mbele za Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye mara baada ya zoezi la kuvunja kufuli ya lango la ghala hilo kukamilika. Waziri Nape kwa kushirikiana na viongozi wa taasisi zinazosimamia maslahi ya kazi za ubunifu wamefanya operesheni iliyofanikisha kukamtwa kwa shehema kubwa ya kazi haramu za filamu na muziki kwenye ghala la bwana Ulaya liliofichwa chini ya hoteli ya Butterfly.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akimfafanulia sheria mbalimbali ambazo mfanyabishara wa kazi za filamu na muziki anastahiki kuzifuata kabla ya kuanza kufanya biashara hiyo. Anaemsikiliaza Mheshimiwa Nape ni mmiliki wa ghala ambalo shehena kubwa ya kazi haramu za filamu na muziki zimekamatwa wakati wa operesheni iliyofanyika leo eneo la Kariakoo jijini Dar-es-Salaam.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akikagua rundo la filamu zilizokamatwa kwenye opersheni ya kutokomeza kazi haramu za filamu na muziki nchini. Kwenye operesheni hiyo shehena kubwa ya kazi za filamu na muziki imekamatwa kwenye ghala lililofichwa chini ya hoteli ya Butterfly iliyoko mtaa wa Muhonda, Kariakoo jijini Dar-es-salaam.

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akisikiliza maelezo kutoka kwa kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Filamu wa Bodi ya Filamu Tanzania Wilhad Tairo wakati wa operesheni ya kutokomeza kazi haramu za filamu na muziki nchini. Operesheni hiyo imefanikisha kukamatwa kwa shehena kubwa iliyokuwa imehifadhiwa kwenye ghala lililofichwa chini ya hoteli ya butterfly iliyoko mtaa wa Muhonda, Kariakoo.

  Pichani ni jengo la hoteli ya butterfly iliyopo mtaa wa Muhonda, Kariakoo ambalo ghala lenye shehena kubwa ya kazi za haramu za filamu na muziki 

  0 0
  0 0

  Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu. Kufuatia mapambano yanayoendelea nchi nzima dhidi ya watu wanaojihusisha na uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya misako na Mafanikio yaliyopatikana katika Misako ni kama ifuatavyo:- 

  KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA [BHANGI].

  Mnamo tarehe 11.02.2017 hadi tarehe 16.02.2017 kwa nyakati tofauti, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya misako dhidi ya watu wanaojihusisha na uuzaji, usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya. Katika misako hiyo iliyofanyika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya, watuhumiwa wanne walikamatwa wakiwa na dawa za kulevya aina ya Bhangi misokoto mitatu yenye uzito wa kilogram 15 na gram 685

  Watuhumiwa waliokamatwa wakiwa na dawa za kulevya aina ya Bhangi ni:-


  1. GEOFREY ADAMSON [35] Mkazi wa Mabatini 

  2. ZUBER MWAMBENYA [24] na 3. GWAKISA ANYOSISYE [20] wote wakazi wa Mama John na  4. PHILIBERT MOSES [35] Mkazi wa Nonde 

  5. MPOKI IBRAHIM [37] Mkazi wa Kitongoji cha Igogwe Wilaya ya Rungwe 

  6. AGUST KIHAULILO @ KIDEVU [63] Mkazi wa Igawa Wilaya ya Mbarali 

  7. CALVINS MOHAMED [25] Mkazi wa Ilemi.

  8. NASSORO OMARI [17] Mkazi wa Mwambene

  9. OTHMANI SAIDI [24] Mkazi wa Mwambene

  10. KENEDY BROWN [21] Mkazi wa mwambene

  KUTEKETEZA SHAMBA KUBWA LA BHANGI

  Mnamo tarehe 16.02.2017 majira ya saa 16:20 jioni Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Kamati Kuu ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kipolisi Mbalizi lilifanya Oparesheni ya pamoja katika Kijiji cha Jojo kilichopo Kata ya Santilya, Tarafa ya Isangati, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kumkamata UPE NDUTA [30] Mkazi wa Jojo akiwa amelima shamba la bhangi lenye ukubwa wa ekari moja.

  Aidha katika Oparesheni hiyo zaidi ya miche 2,000 iliyokomaa ilikutwa shambani. Pia nyumbani kwake alikutwa na bhangi kilogram 2 na gram 145. Mtuhumiwa ni mkulima, muuzaji/msafirishaji na mtumiaji wa dawa za kulevya [Bhangi].

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0


  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Jumamosi Februari 18,2017 amewaongoza wakazi wa Shinyanga kufanya mazoezi katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga. 

  Mazoezi hayo yaliyoanza saa 12 asubuhi na kumalizika saa 2 asubuhi yamehudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Stephen Masele na Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro. 

  Akizungumza wakati wa mazoezi hayo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amesema wakazi wa Shinyanga wataendelea kufanya mazoezi kila siku Jumamosi ili kumuunga mkono Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan .
  “Wiki iliyopita mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack alizindua mazoezi kimkoa,tumekubalina tuwe tunafanya mazoezi kila wiki siku ya Jumamosi ili kudhibiti Magonjwa yasiyo ya kuambukiza,nawakumbusha kuwa mazoezi ni afya hivyo wananchi naombeni muendelee kujitokeza kufanya mazoezi”,alisema Matiro. 

  Hivi karibuni Makamu wa rais Samia Suluhu aliagiza amewaagiza viongozi wa mikoa na wilaya zote kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi angalau kwa mwezi mara Moja.

  Alisema kila Jumamosi ya pili ya mwezi itakuwa siku ya mazoezi ambapo aliwaasa wananchi kufanya mazoezi na kuanzisha na kujiunga na vikundi vya mazoezi na serikali itatimiza wajibu wake wa kuweka mazingira mazuri ya kufanyia mazoezi kote nchini.

  Mwandishi wetu Kadama Malunde ametuletea picha 33 wakati wa mazoez hayo..Tazama hapa chini
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akitoa neno kwa washiriki wa mazoezi hayo ambapo alisema mazoezi ni afya na yanajenga upendo na kufahamiana kwa washiriki wa mazoezi
  Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Stephen Masele akizungumza na washiriki wa mazoezi hayo ambapo aliwahamasisha wananchi kuendelea kujitokeza kufanya mazoezi. 

  Mratibu wa Mazoezi hayo,Diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ili azungumze na washiriki wa mazoezi hayo katika viwanja vya Shycom Mjini Shinyanga.


  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, alipowasili katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Februari 18, 2017, kwa ajili ya mazungumzo baina yao .
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, alipowasili katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Februari 18, 2017, kwa ajili ya mazungumzo baina yao .
  Wakienda eneo la kufanyia mazungumzo 
  Wakiwasili eneo la mazungumzo Ofisini kwa Katibu Mkuu wa CCM. 
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akizungumza na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Feb 18, 2017. (Picha zote na Bashir Nkoromo) .  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alikuwa akipatiwa matibabu mpaka aliporuhusiwa kurejea nyumbani kwake mara baada ya kupata nafuu.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuombea Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumaliza mazungumzo yao nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumjulia hali nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam.

   Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya akimsindikiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alifika nyumbani kwake Upanga kwa ajili ya  kumjulia hali.  
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumjulia hali nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


  0 0

  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka saini katika hati ya Kamisheni muda mfupi kabla ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka saini katika hati ya Kamisheni muda mfupi kabla ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride wakati wa sherehe za Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
  Kikundi cha ngoma cha JWTZ kikitumbuiza kwa ngoma ya Chaso ya Pemba wakati Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipotunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Waziri wa ulinzi nja Jeshi la Kujenga taifa Dkt Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Juma Kijazi na viongozi wengine katika picha ya pamoja baada ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.PICHA NA IKULU

  0 0

  Kikosi cha timu ya Yanga kilichocheza na Ng'aya Fc uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jioni ya leo na Mchezo huo kumalizika kwa droo ya kufungana bao 1-1.
  Kikosi cha Timu ya Ng'aya Fc ya Comoro kikiwa katika picha ya pamoja katika mchezo wao dhidi ya Yanga, mchezo uliomalizika jioni hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
   Kipa wa Ng'aya Fc ya Comoro, Said Mmad akidaka mpira mbele ya mabeki wake na washambuliaji wa Yanga.
   Mshambuliaji wa Ng'aya Fc, Said Hachim akiwania mpira wa juu na beki wa Yanga, Kelvin Yondani katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika, uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, mchezo huo umemalizika kwa sare ya bao 1-1.
   Beki wa Yanga, Vicent Bossou akiokoa mpira mbele ya washambuliaji wa timu ya Ng'aya katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika, uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, mchezo huo umemalizika kwa sare ya bao 1-1.
   Beki wa Kulia wa Ng'aya Fc  akiokoa mpira mbele ya mshambuliaji wa Yanga , Deus Kaseke
   Beki wa kushoto wa timu ya Yanga , Mwinyi Haji akishangilia bao lake la kusawazisha dhidi ya Ng'aya Fc ya Comoro.


  0 0
 • 02/18/17--08:24: LEO MEMORIAL T-SHIRT

 • 0 0  0 0

  Na Ismail Ngayonga, MAELEZO, Mwanza 
  MAAFISA Habari na Mawasiliano katika sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya nchini  wametakiwa kujitokeza na kuwajibika kikamilifu ili kuwawezesha waaajiri wao kutambua wajibu na majukumu yao ya msingi katika kutangaza shughuli na mafanikio ya Serikali katika maeneo yao ya kazi. 
  Rai hiyo  imetolewa leo Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali,  Dkt. Hassan  Abbas wakati alipokuwa akizungumza na Maafisa Habari na TEHAMA katika mafunzo elekezi ya tovuti yanayofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) na kusimamiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Wakala ya Serikali Mtandao (EGA). 
  Kwa Mujibu wa Dkt. Abbas alisema katika ulimwengu wa sasa suala la teknolojia ni jambo lisiloupekika, hivyo ni wajibu wa Afisa Habari kutmia nyenzo za kisasa za mawasiliano ikiwemo tovuti ili kuhakikisha kuwa wananchi na wadau wa maendeleo wanapata taarifa sahihi na zilizozingatia wakati. 
  “Zipo taarifa za miradi mbalimbali ambayo Serikali imeifanya, pamoja na taarifa za bajeti za halmashauri ambazo wananchi watanapenda kuzifahamu, hivyo ni wajibu wenu Maafisa Habari kuweka taarifa hizi” alisema Dkt. Abbas. 
  Aidha aliongeza kuwa ni wajibu wa kila Afisa Habari aliyopo katika Mkoa na Halmashauri nchini aweze kujiwekea malengo ya utekelezaji ili aweze kujitafakari kwa kuwa kuwa kupitia malengo hayo ataweza kutatua changamoto mbalimbali zinazomkabili katika eneo lake la kazi. 
  Akifafanua zaidi Dkt Abbas alisema ili kufikia malengo hayo Maafisa HabariHabari hawana budi  kutengeneza mtandao wa mawasiliano baina yao ili kuwawezesha kutatua changamoto mbalimbali  zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi. 
  Dkt. Abbas alisema Serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili maafisa Habari katika maeneo yo ya kazi, ambapo baadhi ya changamoto hizo zimeanza kupatiwa ufumbuzi ikiwemo suala la miongozo ya majukumu ya Afisa Habari na Mawasiliano.
   
  Kwa Upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Rebbeca Kwandu alisema katika mafunzo hayo yaliyotolewa kwa Maafisa Habari na TEHAMA yatasaidia kwa kiasi kikubwa kujibu hoja na kero mbalimbali za wananchi ambazo zimekuwa zikiwasilishwa mara kwa mara katika halmashauri mbalimbali nchini.
   
  “Afisa Habari atakuwa ndiye mhusika wa karibu zaidi  atayekuwa akiweka maudhui ya tovti hizi lakini pia Afisa TEHAMA yeye atawajibika kwa kiasi kikubwa katika eneo la la ufundii” alisema Kwandu. 
  Naye Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, John Mlyambato alisema baadhi ya Mikoa nchini ikiwemo Mkoa wa Tabora kwa kipindi umekuwa hauna watumishi wa kada ya Maafisa Habari hatua inayosababisha taarifa mbalimbali za Serikali kutowafikia kuwafikia wananchi. 
  Mkurugenzi wa Habari na  Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas akizungumza na Maafisa Habari na Tehama wakati wa Mafunzo elekezi ya matumizi ya tovuti katika Mikoa na Halmashauri za Wilaya nchini yaliyofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekaani (USAID) na kusimamiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wakala ya Serikali Mtandao. Mafunzo hayo yalianza tarehe 9-20 Februari, 2017, kulia ni Mkuuwa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Rais TAMISEMI, Rebecca Kwandu. 


  0 0

  MSHINDI wa Mbio za nusu Marathoni za Kunming Plateu za nchini China, Mtanzania Emmanuel Giniki kutoka Manyara, jana amefanikiwa kushinda mbio za taifa za Nyika za kilometa 10 baada ya kushika nafasi ya kwanza akitumia muda wa dakika 28:25.
   Mbio hizo zilizofanyika katika viwanja vya Gofu vya Moshi Club mkoani Kilimanjaro na kushirikisha zaidi ya wanariadha 220 kutoka mikoa 11 ya Tanzania ,Giniki alifanikiwa kuwaacha wapinzani wake ,Basil John aliyeshika nafasi ya pili baada ya kuhitimisha mbio hizo kwa muda wa dakika 28:50 akifuatiwa na Gabriel Gerald aliyemaliza wa tatu kwa kutumia muda wa dakika 28:54.
   Washindi wengine katika mbio hizo ni ,Dickson Marwa aliyeshika nafasi ya nne akitumia muda wa dakika 29:54: ,nafasi ya tano imechukuliwa na Fabian Joseph aliyemaliza mbio akitumia muda wa dakika 29:23 huku nafasi ya sita ikichukuliwa na Wilbert Peter aliyetumia muda dakika 29;39. 

   Kwa upande wa wanawake mbio za Kilometa 10, Mwanariadha Magdalena Shauri amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza akitumia muda wa dakika 33:19 akiwaacha mbali wakongwe katika mbio hizo kama Fabiliola William aliyemaliza nafasi ya saba na Banuelia Brighton aliyemaliza nafasi ya tisa.Nafasi ya pili imechukuliwa na Mwanariadha Angelina Tsere aliyemaliza mbio hizo akiwa ametumia muda wa dakika 33:42 akifuatiwa na Failuna Abdi aliyemaliza katika nafasi ya tatu huku akitumia muda wa dakika 34:25. 
   Mbali na mbio za Kilometa 10 pia zimefanyika mbio za Kilometa nane kwa upande wa wasichana na wavulana zikishirikisha zaidi wanariadha wenye umri chini ya miaka 19 ambapo kwa wavulana ,Mwanariadha Francis Dambel wa Manyara amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza bada ya kutumia muda wa dakika 23:30. 
   Nafasi ya pili imechukuliwa na Yohana Elisante (23:50:01) na nafasi ya tatu ikichukuliwana Ramadhan Juma (24:09:31) huku kwa upande wa wanawake nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Cecilia Ginoka (20:24) nafasi ya pili ikichukuliwa na Asha Salum (20:58) na nafasi tatu ikichukuliwa na Noela Remmy. 
   Kwa upande wa zawadi wanawake na wanaume mbio za Kilometa 10, zawadi zilitolewa kwa mshindi wa kwanza hadi wa kumi ambapo mshindi wa kwanza alijinyakulia kitita cha shilingi 400,000,mshindi wa pili tsh 300,000, mshindi wa tatu 200,000 mshindi wa nne tsh 100,000, mshindi wa tano tsh 90,000.
   Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi ,Mgeni rasmi katika mashindano hayo Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida,Miraji Mtatiru amesema mchezo wa riadha ndio pekee unaweza kuitangaza Tanzania kitaifa na kimataifa kuliko mchezo wowote. 
  Amesema Taifa lina vipaji vingi kwenye  riadha licha ya kuwepo kwa changamoto ya maandalizi kwa timu za riadha kabla ya kwenda kweye mashindano huku akitoa rai kwa shirikisho la riadha Tanzania kuweka mipango yao mapema na kusihirikisha serikali iweze kutoa mchango wowote. 
   Ametoa ombi la kusajiliwa kwa mbio za Ikungi Marathon ambazo zimefanyika kwa kushirikisha zaidi ya wanariadha 100 wa ndani ya wilaya hiyo kwa kukimbia mbio za Kilometa 21.

  0 0

  Benny Mwaipaja-WFM, Kyela​​​​​​​
  KATIBU Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, amesema kuwa Serikali inathamini mchango wa sekta ya biashara katika kukuza uchumi na maendeleo ya nchi hivyo itaendelea kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji biashara na uwekezaji.
  Prof. Mkenda amesema hayo wilayani Kyela Mkoani Mbeya, wakati ujumbe wa Serikali ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, ulipotembelea mpaka wa Tanzania na Malawi-Kasumulu, ili kujionea utendaji kazi wa Idara ya Forodha na Uhamiaji katika mpaka huo wa Kasumulu/Songwe.
  Amesema kuwa Serikali inapohimiza ulipaji na kusimamia ulipaji kodi haina maana kwamba inawachukia wafanyabiashara, bali inatambua umuhimu wa sekta hiyo katika uchumi wa Taifa na kutoa wito kwa idara za Serikali zilizoko Mipakani kuboresha mazingira ya utoaji huduma ili kurahisisha biashara.
  “Tunatakiwa kuondoa vikwazo vya ufanyaji biashara ikiwemo ucheleweshaji wa mizigo inayovushwa katika mipaka yetu kwa kuwa hatua hiyo itaongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam na kuzivutia nchi nyingi zaidi kutumia Bandari hiyo” Aliongeza Profesa Mkenda
  Amewaonya watendaji wa Serikali walioko katika mipaka yote ya nchi, kuacha kufanyakazi kwa mazoea na kusisitiza kuwa wale wote watakaoshindwa keendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano ni afadhali wapishe kwa hiari yao.
  Kwa Upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, amesema kuwa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifawa miaka Mitano, unahitaji zaidi ya Shilingi Trilioni 107 na kwamba upatikanaji wa fedha hizo utahitaji mazingira bora ya kukuza uchumi wa nchi ikiwemo mazingira mazuri ya ufanyaji biashara mipakani
  “Serikali itazifanyiakazi changamoto mlizozisema kama vile upungufu wa wafanyakazi, vitendeakazi na nyumba za watumishi, lakini wito wangu kwenu muendelee kufanyakazi kwa pamoja, mshirikiane kwa kuongeza nguvu ili kuongeza mapato ya Serikali” alisisitiza Bi. Amina Khmis Shaaban
  Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya, amelitaka jeshi la polisi hususan kikosi cha usalama barabarani kupunguza urasimu wakati wa kutekeleza majukumu yao wanapokutana na magari yaendayo masafa marefu nje ya mipaka ya Tanzania, wasiyacheleweshe njiani bila sababu za msingi.
  Kwa upande mwingine, Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Bw. Qandiyay Akonaay, ameeleza kuwa TRA imeanzisha mfumo wa kufuatilia mwenendo wa mizigo inayosafirishwa kutoka Bandari ya Dar es Salaam, kwenda nchi jirani, hatua ambayo imeboresha kwa kiasi kikubwa ucheleweshaji wa mizigo na kwamba hatua hiyo pia imeongeza mapato ya kodi ya Serikali
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (wa kwanza kushoto), Naibu Kamishna wa TRA, Bw. Qandiyay Akonaay (wa pili kushoto), na wajumbe wengine wakiwasili katika Ofisi za Idara ya Uhamiaji katika Mpaka wa Kasumulu/Songwe, (Tanzania na Malawi), ili kukagua shughuli za forodha katika mpaka huo, wilayani Kyela Mkoani Mbeya.
   Afisa Forodha  wa mpaka wa Tanzania na Malawi Mkoani Mbeya-Kasumulu, Bw. Lenny Mkolla (Wa nne kulia) akitoa maelezo kuhusu mpaka huo baada ya kutembelewa na  Ujumbe wa Serikali ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (wa tatu kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya (hayupo pichani), Wilayani Kyela Mkoani Mbeya.
   Baadhi ya maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji, na Mamlaka ya mapato Tanzania TRA, wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa wakati wa ziara ya ujumbe wa Serikali ukihusisha Makatibu wakuu wa Wizara hizo na Taasisi zake, walipotembelea na kukagua shughuli za forodha na uhamiaji zinazoendelea katika mpaka huo wa Tanzania na Malawi, eneo la Kasumulu.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya (wa kwanza kulia), akitoa ushauri kwa uongozi wa mpaka wa Kasumulu/Songwe (Tanzania na Malawi), upande wa Tanzania, Wilayni Kyela Mkoani Mbeya, namna ya kuboresha utendaji kazi mpakani hapo ili kuboresha biashara na kuongeza   mapato ya Serikali. Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (wa pili kulia), Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji-Kasumulu, Bw. John Gillagiza (wa kwanza kushoto), walipotembelea mpaka huo..
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (kushoto) akisisitiza kauli mbiu ya “siku moja! mzigo umetoka” kwa watumishi wa Idara ya Forodha katika mpaka wa Kasumulu/Songwe (Tanzania na Malawi), baada ya ujumbe wa Serikali ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (kulia) ulipotembelea na kukagua mpaka huo wilayani Kyela mkoani Mbeya. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

  0 0


  0 0

   Umati wa watu waliofurika katika uwanja wa Mwembe yanga katika Tamasha la mchiz wangu Concert liloandaliwa na EFM 93.7 Radio Station
   Msaga sumu akitumbuiza mbele yamashabiki wa Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam Katika Tamasha la Mchizi Wangu Concert
   Majid Migoma akitumbuiza katika Tamashalamchiz wangu Concert


   Msaga sumuakiendelea kuwapa raha wakazi wa Temeke
   Wacheza shoo muziki wasingelei wakifanya yao jukwaani
  Dula Makabila akitumbuiza mbele ya wakazi wa Temeke Mwembeyanga

  0 0

  Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege Tanzania ATCL LADISLAUS MATINDI, amerizishwa na matengenezo ya uwanja wa ndege ulipo songea mkoani Ruvuma, kwa ajili ya kuanza kutoa huduma za safari toka SONGEA hadi DAR ES SALAAM.


older | 1 | .... | 1574 | 1575 | (Page 1576) | 1577 | 1578 | .... | 3272 | newer