Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1573 | 1574 | (Page 1575) | 1576 | 1577 | .... | 3283 | newer

  0 0


  Na.

              Tukio

  Mhusika

  Muda

  1

  Kuw Washiriki kuwasili


  Kamati ya Maandalizi

  11.30 - 12.00 Asubuhi

  2

  Kuwasili Mgeni rasmi


  Kamati ya Maandalizi


  12.00 – 12.10 Asubuhi

  3

  Mazoezi ya mwanzo ( warm up)


  Kamati ya Maandalizi/ wakufunzi wa Mazoezi


  12.10 – 12.25 Asubuhi

  4.

  Matembezi ya Mazoezi


  Kamati ya Maandalizi/ wakufunzi wa Mazoezi


  12.25 – 1.25 Asubuhi

  5.

  Mazoezi ya kulainisha viungo baada ya Matembezi


  Kamati ya Maandalizi/ wakufunzi wa Mazoezi


  1.25 – 1.55 Asubuhi

  6


  Burdani


  1.55 – 2.10 Asubuhi

  7.

  Taarifa fupi kuhusu Madhumuni ya Bonanza

  Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO)

  2.10 – 2.15 Asubuhi

  8.

  Kumkaribisha Mgeni Rasmi

  Jukwaa la Wahariri (TEF)

  2.15-2.20 Asubuhi

  9.

  Hotuba ya Mgeni rasmi


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

  Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb)

  2.20 – 2.40  Asubuhi

  10.

  Neno la Shukran  Klabu ya Waandishi wa Habari wa Jiji la Dar es Salaam (DCPC)

  2.40 -2.45 Asuhihi

  11.

  Burdan


  2.45-3.00 Asubuhi

  12.

  Kutembelea mabanda ya upimaji Afya bila malipo na Mgeni rasmi kuondoka.


  Mgeni rasmi/Viongozi

  3.00 – 3.30 Asubuhi


  Burdani Kuendelea


  3.30 Asubuhi na Kuendelea

  13.


  Kuendelea na Bonanza, utoaji damu na upimaji Afya

  Wote

  3.30  Asubuhi na Kuendelea

  0 0

  Na Rhoda Ezekiel-Globu ya Jamii, Kigoma.

  JESHI la Polisi Mkoani Kigoma limekamata Wahamiaji haramu 226, Kete za bangi 191, Heroin kete tano , pombe ya moshi lita 300 na silaha aina ya gobore moja, katika msako wa kupambana na dawa za kulevya, wahamiaji haramu pamoja na uhalifu uliofanyika kwa kipindi cha Wiki moja ili kuhakikisha Mkoa upo salama.

  Akitoa taarifa ya Msako huo leo mbele ya Waandishi wa habari Mkoani humo , Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Kigoma, DCP Fredinand Mtui alisema kuanzia Februal 2 mwaka huu jeshi la polisi Mkoani humo lilianza Msako wa kuhakikisha wanakomesha vitendo vya uhalifu, matumizi ya Dawa za kulevya na uuzaji pamoja na wahamiaji haramu wanaoingia Nchini bila vibali, hali inayo sababisha uhalifu kuongezeka kutokana na vitendo hivyo.

  Mtui alisema kuwa mnamo februali 16 ulifanyika msako na kufanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 203 katika kijiji cha Mganza Wilayani Kasulu wakitokea nchini Burundi wakiwa katika mashamba ya Wakulima,alisema na kuongeza kuwa Kigoma mjini walikamatwa wahamiaji 7 , kibondo 9 na Buhigwe 7a na jumla yao ni wahamiaji 226 ambao waliingia nchini Kinyume na utaratibu huku wakipokelewa na Wenyeji na wanawahifadhi.

  Alisema Wengi wa wahamiaji hao wanatoroka Nchini mwao wakiwa wamefanya uhalifu na wanakuja Nchini na wanapokelewa na wenyeji na wanawatumia katika kilimo pia wengi wao ndio wanaotumika kifanya uhalifu mkoani humo ambapo Kamanda Mtui aliwaomba Wananchi kuacha kuwapokea Wahamiaji hao ambao wengi wao husababisha madhala makubwa katika maeneo yao.

  Aidha Mtui alisema kwa upande wa madwa ya kulevya jeshi la polisi lilikamata katika Wilaya ya Kigoma kete za bhangi 191 sawa na gram10 pamoja na Heroin kete tano, Kasulu walikamata robo eka na gram 500 , kibondo miche 10 na Kakonko miche 60 ,kilo moja ya Bhangi madawa hayo yalikuwa yakiuzwa kwa vijana ambao wengi wao hawafanyi kazi na wanaendelea kufanya vitendo vya uhalifu.

  " tumeweza kutoa kipaumbele katika uhalifu unao tusumbua kwa kiasi kikubwa Mkoani Kigoma ambao ni wahamiaji haramu , na matumizi ya Dawa za kulevya, kwa mujibu wa upelelezi tulio ufanya wengi wanaoingia bila vibali ni wale wahalifu wanao kimbia mikono ya sheria kutokana na uhalifu kama tunavyo fahamu muahalifu hawezi kuacha uhalifu kiurahisi ndio ambao wanakuja kiendelea kufanya uhalifu niwaombe Wananchi kuacha kupokea Wahamiaji halamu kwasababu kwa sasa tutakae mkamata anawahifadhi wahamiaji halamu watafikisha mahakamani", alisema Kamanda Mtui.

  Alisema katika msako huo zilipatikana idadi ya kesi katika msako huo ni kesi ya uhamiaji haramu ni nane , kupatikana pombe ya moshi kesi 11, kupatikana Bhangi kesi tisa , kupatikana na silaha kesi moja na kupatikana na heroini kesi moja, watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani ilikuweza kujibu tuhuma zinazo wakabili.
  Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Kigoma, DCP Fredinand Mtui akizungumza na baadhi ya wandishi wa habari mapema leo kuhusiana na operesheni walioifanya ya kupambana na dawa za kulevya, wahamiaji halamu pamoja na uhalifu iliofanyika kwa kipindi cha Wiki moja ili kuhakikisha Mkoa upo salama.
  Madumu ya pombe ya moshi (gongo),lita 300 zikiwa zimekamatwa
  Kete za bangi 191 zikiwa zimekamatwa 


  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  BAADA ya kupata kibali cha kufanya kazi nchini juzi, Kocha Mkuu wa Klabu ya Azam FC, Aristica Cioaba, amejinasibu ya kuwa yeye ni aina ya kocha anayependa falsafa ya soka la kushambulia na sio kujilinda.

  Cioaba aliyesaini mkataba wa kuinoa Azam FC mwezi mmoja na nusu uliopita, ameweka wazi hayo mara baada ya mchezo wao wa kirafiki na timu ya  Red Arrows ya Zambia na kuondoka na ushindi wa goli 1-0 ikiwa ni mechi yake ya kwanza kuiongoza kama Kocha Mkuu wa benchi la Ufundi.

  “Mimi ni kocha ninayependa soka la kushambulia, sio aina ya kocha ninayependa timu yangu icheze kwenye eneo la kujilinda, napenda kuwapa mabao mengi mashabiki wanaokuja uwanjani kushuhudia mechi na kuwafanya baada ya mechi wawe na furaha.

  Kocha huyo wa zamani wa Aduana Stars ya Ghana, alisema kuwa mchezo huo ulikuwa mzuri sana na anafuraha kubwa baada ya wachezaji wake kucheza vizuri na kwa nguvu muda wote pamoja na kupata matokeo mazuri ya ushindi.

  “Ninapenda sana mechi nyingi za kimataifa za kirafiki kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Afrika (Kombe la Shirikisho), hii ni mipango yetu ya baadaye na kila mtu ananielewa mimi, nimekuja hapa mwezi mmoja na nusu uliopita, kibali change cha kazi kimeshakamilika.

  Alisema kuwa katika mchezo huo, timu yake ilitengeneza nafasi tatu hadi nne za kufunga mabao kipindi cha kwanza lakini hazikuweza kutumiwa vema huku akisema kuwa mambo yatabadilika baadaye na timu hiyo kuweza kufunga nafasi wanazopata.

  “Inahitajika kufanya kazi kubwa, kuna baadhi ya matatizo kwenye ushambuliaji kwa baadhi ya washambuliaji, nitafanya kazi kila siku na ninawaamini wachezaji wangu watafika kiwango cha juu na hapo baadaye kuweza kufunga mabao na kila mmoja kufurahia,”alisema.

  Aidha alisema kuwa anaiamini timu yake na kama ikiendelea kucheza kwa namna hii na kila mmoja kufika mazoezini na kufanya kwa nguvu na kwa umakini na kushika kile anachowafundisha na kucheza kwa kiwango kikubwa zaidi ana uhakika watachukua pointi tatu kwenye mchezo huo.
   Kocha Mkuu wa Klabu ya Azam FC, Aristica Cioaba


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limewatahadharisha wanachama na wapenzi wa klabu ya Yanga, kutobeba mabango ya kukashifu Serikali wala kiongozi yeyote wa nchi kesho wakati wa mchezo wa marudiano na Ngaya Club de Mde ya Comoro.

  Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema jana kwamba wanawaonya mashabiki wa soka nchini waliopanga kuleta vurugu na kuonyesha viashiria vya kukashifu viongozi wa soka na Serikali katika mchezo wa wa kesho na wa Februari 25 dhidi ya Simba, wasithubutu kabisa kwani vyombo vya dola vinawajibika katika kushughulika nao.

  Lucas amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayethubutu kufanya kitu cha namna hiyo na kwamba kutakuwa na ulinzi mkali kesho Uwanja wa Taifa kwa ajili hiyo na kuwasihi mashabiki kuacha dhana hiyo kabisa na waje uwanjani kuja kushangilia mpira na kuipa sapoti timu yao

  Yanga watakuwa wenyeji wa Ngaya katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo mechi ya awali waliweza kutoka na ushindi wa goli 5-1 na hata hivyo tayari uongozi wa klabu ya Yanga ulishawasihi mashabiki wa timu hiyo kwenda kwa amani uwanjani na kutokufanya vurugu ya aina yoyote.

  Kiingilio cha chini katika mchezo wa kesho kitakuwa Sh. 3,000 Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, VIP A Sh 20,000, VIP B Sh 10,000 na VIP C Sh 10,000.

  Mechi hiyo itachezeshwa na marefa kutoka Uganda ambao ni Alex Muhabi Nsulumbi atayekapuliza filimbi uwanjani, akisaidiwa na washika vibendera Ronald Kakenya na Lee Okello.

  Refa wa Akiba atakuwa Brian Nsubuga Miro huku Kamishna akitokea Afrika Kusini ambaye ni Monnyenyone Lucas Nhlapo.  Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas

  0 0


  Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam

  Benki ya UBL imesema iko tayari kuwekeza Tanzania katika Sekta ya Kilimo ambayo itawezesha Tanzania kupata fursa ya kuweza kuuza mazao yake katika nchi za ughaibuni na pia kufanya kazi na Watanzania pamoja na Serikali yake. 

  Hayo yalisemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Tanzania, Bw. Faisal Jamall wakati akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

  Bw. Jamall alisema kuwa kwa sasa Tanzania inaenda vizuri hasa katika suala la ukuaji wa uchumi ingawa kuna baadhi ya wananchi wanalalamika kuwa fedha zimeadimika mitaani lakini ni wazi kwamba Taifa linarudi kwenye utaratibu. Hivyo wameonesha nia ya kuwekeza hasa katika Sekta ya Kilimo.

  Naye Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) amesema kuwa hali inabadilika na Jumuiya ya Mabenki inaanza kuwa na imani na Tanzania. Na kuongeza kuwa kitendo cha Benki ya UBL kuonesha nia ya kufanya kazi na Serikali katika Sekta ya Kilimo ni jambo jema katika maendeleo ya haraka ya Tanzania kwa kuwa Sekta hii mama bado inakabiliwa na changamoto nyingi.  

  Alisema dhamira kubwa ya Benki ya UBL ni kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji, uboreshaji wa mifugo pamoja na uvuvi. Na Serikali imeahidi kuitumia vizuri fursa hii ili nchi iweze kupiga hatua ya haraka zaidi hasa katika kipindi ambacho imedhamiria kuwa nchi ya Viwanda.

  Akitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya dola katika uchumi badala ya shilingi ya Tanzania, hasa kwenye mikopo, Waziri Mpango alisema kuwa suala hili Serikali imeshaanza kulifanyia kazi kwa kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja na kusimamia kwa karibu biashara ya maduka ya fedha za kigeni. 

  “Tumepiga hatua ya kufunga mashine za kielektroniki (EFDs) ili Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuona kinachofanyika ili wamiliki wa maduka hayo walipe kodi inayostahili. Aidha zoezi hili litaweizesha Benki Kuu ya Tanzania – BoT, kuona kiasi cha fedha za kigeni zilizopita katika maduka na itaimarisha matumizi ya shilingi ya Tanzania; japo tuna changamoto kubwa ya wananchi kutokudai risiti pindi wanapopata huduma ya kubadilisha fedha za kigeni,” Alisisitiza Dkt. Mpango.

  Katika kuhitimisha majadiliano hayo Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mpango alisema Serikali itaongeza ushirikiano na Benki ya UBL ili waweze kufanya biashara, ikizingatiwa kuwa Benki hiyo ni miongoni mwa Benki kubwa katika nchi za Uarabuni.

  Imetolewa na: 
  Kitengo na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Fedha na Mipango
  16 Februari, 2017
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akielezea namna matumizi ya vifaa vya Kielektroniki (EFDs) yalivyoongeza Makusanyo ya Mapato ya Serikali alipotembelewa na Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), Ofsini kwake jijini Dar es salaam.

  Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), akielezea nia ya Benki yake ya kutaka kuwekeza kartika Sekta ya Kilimo, alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani) ofisini kwake jijini Dar es salaam. 
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akichukua maelezo ya Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), baada ya ya Mtendaji huyo kumtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam na kueleza nia ya kuzitumia fursa zilizopo katika Sekta ya Kilimo.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akifafanua jambo kuhusu uwekezaji katika Sekta ya Kilimo unaotaka kufanywa na Benki ya UBL Nchini Tanzania baada ya kukutana na Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Faisal Aliza Jamall OfIsini kwake jijini Dr es salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

  0 0


   MBUNGE wa Simanjiro, Mheshimiwa James Ole Millya ametoa pongezi kwa viongozi wa serikali ya awamu ya tano kwa jinsi wanavyojali na kuwahudumia wananchi.

  Ametoa pongezi hizo jana (Alhamisi, Februari 16, 2017) kwenye mikutano miwili ya hadhara iliyofanyika Orkesumet na Mererani wilayani Simanjiro, Manyara, baada ya kupewa nafasi asalimie wananchi kabla Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hajazungumza na wakazi wa maeneo hayo.

  “Serikali hii ina viongozi wachapakazi akiwemo Waziri Mkuu. Kwa mara ya kwanza katika jimbo hili, wananchi watapata maji safi kupitia mradi wa maji kutoka mto Ruvu unaoendelea kujengwa hivi sasa,” alisema kwenye mkutano wa hadhara wa Orkesumet.

  Alitumia fursa hiyo kumuomba Waziri Mkuu afuatilie suala la ujenzi wa hospitali ya wilaya kwani sasa hivi wanategemeakituo cha afya na hali ikibadlika inabidi mgonjwa apeekewe Arusha mjini ambako ni umbali wa km. 150 kutoka Orkesumet yalipo makao makuu ya wilaya hiyo.

  Pia aliomba ijengwe barabara ya lami ya kuunganisha wilaya hiyo pamoja wilaya jirani za Hai na Kiteto.

  Akiwa Mererani, Bw. Ole Millya aliipongeza Serikali kwa kujenga barabra ya lami kutoka uwanaja wa ndege wa KIA hadi Mererani. Hata hivyo, aliiomba serikali iongeze juhudi ili barabara hiyo iweze Mererani na Orkesumet.

  Akihibu hoja hizo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimpongeza mbunge huyo kwa uungwana wake wa kutambua juhudi ambazo Serikali imezifanya kwa wananchi wa jimbo lake.

  Waziri Mkuu ambaye alikuwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Manyara, aliwaambia wakazi hao kwamba Serikali itaendelea kufanya nao kazi bila kumbagua mtu yeyote kwa sababu ya itikadi za kisiasa.

  “Mmempa yeye dhamana ya kuwawakilisha kama mbunge wenu lakini dhamana ya kuongoza nchi mmempa Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuwapigia kura. Kwa hiyo, kazi yetu ni kuwatumikia ili tutatue kero zinazowakabili wana-Simanjiro,” alisema.


  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango ameitaka nchi ya Uingereza kutazama uwezekano wa kufanya biashara na Tanzania kwa kununua bidhaa zilizoongezwa thamani badala ya hali ya sasa ambapo nchi hiyo imekuwa ikinunua bidhaa ghafi ilihali ikiingiza nchini bidhaa zake za viwandani.

  Dkt. Mpango ameyasema hayo alipokutana na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Biashara Bw. Lord Hollick ailipo tembelea Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es salaam. 

  Amesema Tanzania inataka kuona inauza bidhaa zake zenye thamani ambazo zitatokana na maendeleo makubwa ya viwanda hapa nchini ikiwa ni Sera ya nchi kuwa na uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025. 

  Nchi ya Uingereza imekuwa ikifanya biashara na Tanzania kwa kiasi kikubwa na takwimu zinaonesha nchi hiyo inaingiza bidhaa zenye thamani mara nane ya Tanzania jambo ambalo linatakiwa kurekebishwa ili biashara iwe na manufaa kwa pande zote mbili. 

  Miongoni mwa bidhaa ghafi ambazo zimekuwa zikisafirishwa kwenda uingereza ni pamoja na Chai, kahawa na madini ya vito huku Uingereza ikiingiza bidhaa za viwandani zenye thamani kubwa ikijumuisha mashine (mitambo),vifaa vya umeme, bidhaa za plastiki na madawa. 
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akieleza kuhusu juhudi za Serikali katika kutengeneza mazingira mazuri ya kibiashara wakati wa mkutano na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
  Wajumbe wa Mkutano walioongozana na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick, wakisikiliza kwa makini maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), kuhusu umuhimu wa kufanya biashara ya bidhaa zilizoongezwa thamani ili kukuza viwanda vya ndani, wakati wa mkutano huo jijini Dr es salaam.
  Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick (kushoto) akifafanua jambo wakati wa Mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani) kuhusu nia ya kuwekeza katika ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Msalato Dodoma, Kulia ni Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke, Mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es salaam.
  Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza anayeshughulikia Biashara Bw. Lord Hollick (kulia) akisisitiza kuhusu kuendelea kuimalisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Uingereza huku Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akimsikiliza kwa makini katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es salaam.


  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 17 Februari, 2017 amekutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeshughulikia masuala ya nishati Bw. Amadou Hott ambaye yupo hapa nchini kwa mazungumzo na wataalamu na viongozi yenye lengo la kuboresha sekta ya nishati hususan uzalishaji wa umeme.

  Bw. Amadou Hott amekuja nchini ikiwa ni utekelezaji wa mazungumzo yaliyofanywa kati ya Mhe. Rais Magufuli na Rais wa AfDB Bw. Akinwumi Adesina Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 31 Januari, 2017 ambapo viongozi hao walikubaliana kuongeza ushirikiano kati ya AfDB na Tanzania katika maendeleo huku mkazo ukielekezwa kupata majawabu ya kuongeza uzalishaji wa umeme na wa gharama nafuu.

  Bw. Amadou Hott ameelezea kuguswa na dhamira ya Mhe. Rais Magufuli juu ya kuongeza uzalishaji wa umeme na wenye gharama nafuu kwa ajili ya kufanikisha mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa viwanda, na ameahidi kuwa Benki hiyo itahakikisha dhamira hiyo inafanikiwa.

  Kwa Upande wake Mhe. Rais Magufuli amemhakikishia Bw. Amadou Hott kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano wakati wowote itakapohitajika ili kufanikisha dhamira hiyo.

  Wakati huo huo,Mhe. Rais Magufuli amekutana na Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bharti Enterprises inayomiliki kampuni ya simu ya Airtel Duniani Bw. Sunil Bharti Mittal ambapo viongozi hao wamezungumzia utendaji kazi wa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania ambayo Serikali ya Tanzania inamiliki asilimia 40 ya hisa za kampuni hiyo.

  Baada ya mazungumzo hayo, Bw. Sunil Bharti Mittal ameelezea utayari wake wa kuingiza kampuni ya Airtel Tanzania katika soko la hisa la Dar es Salaam ili Watanzania wapate fursa ya kumiliki kampuni hiyo kwa kununua hisa.

  Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini Mhe. Jean Pierre Tshampanga Mutamba Ikulu Jijini Dar es Salaam.


  Gerson Msigwa

  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais , IKULU

  Dar es Salaam

  17 Februari, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amadou Hott aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amadou Hott Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amadou Hott mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) nchini Jean Pierre Tshampanga  Mutamba Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) nchini Jean Pierre Tshampanga  Mutamba mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bharti Enterrprise, Sunil Bharti Mittal aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bharti Enterrprise, Sunil Bharti Mittal mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bharti Enterrprise, Sunil Bharti Mittal Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  0 0


  0 0
 • 02/18/17--12:30: Article 0


 • 0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  KAMA Mwanamke ukiamua kujitoa na kupigania nini unafanya lazima utafanikiwa, nami naweza kusema kufika kwangu ni pale nilipoamua kujituma, kujiamini na kutambua nini malengo yangu.

  Hayo ni baadhi ya maneno aliyotoa mwanamke mjasiriamali Sophia Khalid Byanaku, ambaye ni Mkurugenzi wa Kliniki ya Doctor's Plaza, alikuwa akizungumza na Globu hii. 

  Sophia Khalid Byanaku  ni mke wa Profesa Mohamed Janabi (Mtaalamu wa magonjwa ya Moyo), ana Elimu ya Shahada ya sosholojia (Degree in Sociology), Shahada ya uzamili Sera za afya Mipango na Usimamizi (Master in Health Policy Planning and Management.

  Ulianzia wapi,


  Byanaku : Mwaka 2001 nilishiriki mashindano ya urembo kwa mkoa wa Tanga na kufanikiwa kuchukua taji la Miss Tanga 2001 na kupata nafasi ya kuwa katika kumi bora ya Miss Tanzania ambapo taji lilichukuliwa na mrembo Millen Hapiness Magese. 

  Unajivunia nn kupitia Miss Tanzania,
  Byanaku: Najivunia mambo mengi kupitia ushiriki wa Miss Tanzania mwaka ule kwani umeweza kunipa ujasiri wa kuweza kupambana kwa namna nyingine na hata miaka yetu tuliweza kupata nafasi nyingi za kushiriki kijamii zaidi.

  Baada ya kumalizika kwa Miss Tanzania ulijikita wapi zaidi:
  Byanaku:  Kabla ya kufungua Kliniki ya Doctor's Plaza, nilikuwa mfanyakazi wa benki Stanbic Bank Tanzania kwa takribani miaka 6, baadae nikafanya kazi benki ya NMB kwa muda wa mwaka mmoja na African Life Assurance (Sanlam).

  Doctors Klinik ilianza lini?

  Byanaku: Rasmi mwaka 2012 kwa kituo kimoja wakiwa wamejikita katika kutibu magonjwa ya moyo tu lakini sasa wanatoa matibabu ya ya magonjwa mbalimbali ya binaadamu na tayari wana vituo  vitatu ambavyo vyote vipo jijini Dar es Saalam.

  Madhumuni ya kufungua Doctors Kliniki ni nini?
  Byanaku: Lengo kuu la kufungua vituo hivyo ni kwa sababu napenda sana kujishughulisha na jamii, hivyo kuwa na vituo hivyo amejua mambo mengi kuhusu jamii inayomzunguka. 

  Matarajio ya Byanaku ya baadae:
  Byanaku:  Matarajio yangu ya  baadae ni kuwa na Hospitali kubwa ya kisasa Tanzania ambayo itaweza kutoa huduma karibia zote kwa wahitaji,na pia nataka kuwa Mtaalam wa Health care Management kwa Tanzania,yani nataka kukiwa na uhitaji wa ushauri kuhusu masuala ya uongozi wa Afya Tanzania mimi niwe mtu wa kwanza kufikiria kusaidia.

  Changamoto anazozipata katika vituo  Doctor's Plaza
  Byanaku: Kuna changamoto mbalimbali zinazotukabili kwenye vituo vyetu vya Doctor's Plaza ila kikubwa zaidi  ni madaktari kwani ni wachache ambapo mpaka sasa tuna madaktari 32 kutoka Muhimbili ila tunaendelea kufanya jitihada kuhakikisha  watu wanapata huduma wanazohitaji za matibabu.   Anachojivunia kama mwanamke mjasiriamali:

  Byanaku: Naweza kusema katika kufanikisha jambo uliloamua kulifanya, kwenye hili hakuna mwanaume wala mwanamke ili kuweza kufikia mafanikio yoyote,lazima kufanya kazi kwa bidii na kujituma,na sio kwa bidii tu lakini pia kwa akili,kusimamia malengo yako na pia kutokukubali kukatishwa tamaa na mtu yoyote yule,ilhali huvunji heshima ya mtu.
  Wanawake tusiogope wala kuona aibu fursa zinapotokea tuzikimbilie bila aibu wala woga na tuonyeshe uwezo wetu, kwa kusema haya haya Mimi mwenyewe bado sijafikia malengo yangu lakini nashukuru nimeweza kufikia kidogo safari bado ni ndefu tunajifunza kila siku na nina amini nitafika.
  Unapaswa kujiwekea malengo na kuyafanyia kazi ili kuyafikia, kila unachoona kinaweza kufanyika na kufanikiwa kwa asilimia kubwa. 

  Byanaku nje ya kazi ni nani?

  Byanaku: Sophia Khalid Byanaku ni Mama wa watoto wawili, Nayla (6) na Akim(4), na nimeolewa na Profesa Mohamed Janabi (Mtaalamu wa magonjwa ya Moyo), muda wangu mwingi napokuwa nyumbani napenda kukaa na familia yangu.
  Kama Mwanamke mara nyingi nakuwa na suluhisho na nafanikiwa kujigawa kwa usawa katika majukumu yangu ya nyumbani, napenda sana kuwa na familia pale ninapoukuwa nyumbani  bila kuchanganya yote haya nayafanya na naweza ndiyo maana natarajia kuongeza zaidi hapa nilipoanza, kikubwa mwanamke unaweza kufanikiwa kama kweli umeamua kulifanya lako katika kuleta maendeleo katika jamii hasa iliyokuzunguka

  Anasema hata hivyo bado anajitahidi kuwa nkujifunza kwa kusoma vitabu na hata kuuliza watu walionitangulia waliwezaje na kufanikiwa, lakini pia kuweza kufanikiwa haya ni lazima pia upate ushirikiano kutoka kwa familia,ambayo nashukuru ninapata ushirikiano.

  Unapendelea nini? 

  Byanaku: Ni mpenzi wa kusoma vitabu Sana kwa sasa nasoma vitabu viwili; My Personal MBA By Josh Kaufman na The E Myth Revisited By Michael Gerber na kitabu ninachotarajia kusoma ni The Miracle Morning by Hall Elroy. Napenda Kusafiri,Mziki,na kusoma.

  0 0

  Wachezaji wa Simba wakiingia eneo la bandari kwenda kupanda boti ikiwa ni safari ya Zanzibar kwa ajili ya kambi ya wiki moja kuelekea mechi yao na watani wao wa Jadi Yanga utakaopigwa Februari 25.
   Mshambuliaji wa Kimataifa wa Burundi Laudit Mavugo akiwa anaongoza kuelekea eneo la kusubiria boti wakati wa safari ya Zanzibar kwa ajili ya kambi ya wiki moja kuelekea mechi yao na watani wao wa Jadi Yanga utakaopigwa Februari 25.

   Wachezaji wa Simba wakiwa wanasubiri kukaguliwa tiketi getini wakati wa safari ya Zanzibar kwa ajili ya kambi ya wiki moja kuelekea mechi yao na watani wao wa Jadi Yanga utakaopigwa Februari 25.
   Kocha wa Simba Joseph Omog akiongea na shabiki wa timu hiyo leo Jijini Dar es salaam wakati wa safari ya Zanzibar kwa ajili ya kambi ya wiki moja kuelekea mechi yao na watani wao wa Jadi Yanga utakaopigwa Februari 25.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege nchini ATCL mhandisi Ladslaus Matindi akikagua eneo la kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa Songea,kulia meneja wa mamlaka ya usalama na usafiri wa Anga mkoani Ruvuma Janeth Lwiva.
  Meneja wa shirika la ndege ATCL mkoa wa Mtwara na Ruvuma Esther Mahiga kushoto akimuongoza mkurgenzi mkuu wa shirika hilo mhandisi Ladslaus Matindi kukagua uwanja wa ndege wa Songea kabla ya ndege za shirika hilo kuanza safari zake mkoani Ruvuma, wa pili kulia meneja wa mamlaka ya usalama na usafiri wa Anga mkoa wa Ruvuma Janeth Lwiva na kulia meneja wa uwanja wa ndege wa Songea Fasha Valentin.
  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge kushoto akimweleza jambo mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege Tanzania ATCL Mhandisi Ladslaus Matindi ofisini kwake mjini Songea leo, ATCL kupitia ndege zake za Bombadier zitaanza safari zake kati ya D,slaam na Songea mkoani Ruvuma baada ya wiki sita.


  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya uchukuzi), Eng. Dkt. Leonard Chamuriho ameipongeza kampuni ya huduma za meli nchini (MSCL), kwa kukarabati meli zake kwa kutumia fedha za ndani na hivyo kuhuisha utendaji kazi wa kampuni hiyo.

  Akizungumza jijini Mwanza mara baada ya kukagua huduma zinazotolewa na kampuni hiyo Eng. Dkt. Chamuriho amesema Serikali itawekeza kikamilifu kwenye kampuni hiyo baada ya kuridhika na utendaji uliopo sasa.

  “Fanyeni kazi kwa bidii na fikra mpya Serikali inashughulikia kwa karibu suala la mishahara yenu na stahili nyingine” amesema Eng. Dkt. Chamuriho.

  Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa alimteua Kaimu Meneja Mkuu mpya wa kampuni hiyo Bw. Eric Hamisi ambaye kwa kushirikiana vema na menejimenti na wafanyakazi wamewezesha kuongeza mapato kwa kwa asilimia 100.

  Kampuni ya huduma za Meli MSCL ni moja ya kampuni ya Meli yanayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 na kusimamiwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Uchukuzi na inatoa huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo katika maziwa makuu yaliyopo nchini Victoria,Nyasa na Tanganyika
  Meli ya MV. Clarias inayomilikiwa na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), inayofanyiwa ukarabati katika bandari ya Mwanza ambao ukarabati wake utakamilika mwanzoni mwa wiki ijayo na kuanza kutoa huduma mwishoni mwa mwezi huu.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Sekta ya Uchukuzi, Eng.Dkt, Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Eric Hamisi (mwenye shati jeupe), wakati alipokagua ukarabati wa Meli ya MV. Clarias.
  Fundi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), akiendelea na ukarabati wa meli ya MV Clarias ambayo ukarabati wake utakamilika mwishoni mwa wiki na kuanza kazi ya kutoa huduma katika Ziwa Victoria.
  Nahodha wa Meli ya Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Swedi Ruganza akitoa maelezo ya namna nahodha anavyoendesha meli kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Sekta ya Uchukuzi, Eng. Dkt. Leonard Chamuriho (katikati), alipofanya ukaguzi wa ukarabati wa meli hiyo jijini Mwanza.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Sekta ya Uchukuzi, Eng.Dkt. Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Huduma za Meli (MSCL), Bw. Eric Hamisi (wa pili kutoka kushoto), mara baada ya kuangalia kina cha maji katika bandari ya Mwanza. PICHA NA Biseko Lisso Ibrahim, WUUM (U)

  0 0

  Kikosi cha Simba kikiongozwa na Nico na Renatus Njohole Dallas, Texas.
  Kikosi cha Yanga
  Kikosi cha Simba kikiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Wilson Masingingi na mkewe siku walipotwaa ubingwa Dallas, Texas wakati wa kongamano la DICOTA
  Kulia ni mkuu wa Wilaya Mhe. Kasesela akiwa Hoston katika picha ya pamoja na wachezaji wa Pazi enzi hizo Vitalis Gunda na Atiki Matata aliyekuja toka Uingereza kuiwakilisha Pazi.
  Timu ya Tanzania iliyoundwa na wachezaji waliotamba enzi hizo katika timu za Pazi, Vijana, Don Bosco na kwengineko wakinyanyua juu kikombe walicho kipata baada ya kuifunga timu ya Gabon

  0 0


  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji, itakuwa mwenyeji wa Maadhimisho ya 11 ya ‘Siku ya Nile’ yatakayofanyika Dar es Salaam, tarehe 22 Februari, 2017.

  Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kushirikiana na Sekretariati ya Nile Basin Initiative (NBI) itaandaa Maadhimisho ya 11 ya Siku ya Nile (Nile Day) yatakayofanyika tarehe 22 Februari, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

  Lengo la Siku ya Nile ni kukuza uelewa kwa watu wote kuhusu umuhimu wa ushirikiano baina ya nchi zote wanachama, masuala yanayotekelezwa na faida inayopatikana kutokana na matumizi bora ya rasilimali za Bonde la Mto huo. 
  Kauli Mbiu ya Maadhimisho hayo ni ‘Our Shared Nile: Source of Energy, Food and Water for All’. Kauli mbiu hii inalenga kuonesha umma umuhimu wa Mto Nile katika kuhakikisha usalama wa upatikanaji wa chakula, maji, na nishati ya umeme kwa jamii nzima na vilevile, kuonesha muingiliano uliopo katika sekta husika kwa lengo la kuondoa umasikini, kuboresha maisha ya jamii na kuleta maendeleo endelevu. 
  Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo atakuwa ni Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Washiriki takribani 600 watashiriki maadhimisho hayo zikiwemo sekta mbalimbali, taasisi za kiserikali, taasisi zisizo za kiserikali, wadau wa

  maendeleo na watu mashuhuri. 

  Maadhimisho yanatarajiwa kuanza saa 02:30 asubuhi, siku ya tarehe 22 Februari, 2017 kwa maandamano yatakayo ongozwa na Bendi ya Polisi kuanzia viwanja vya Mnazi Mmoja hadi Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, ambapo maonesho na ufunguzi rasmi wa maadhimisho hayo yatafanyika.


  KARIBUNI SANA!


  Inj. Emmanuel Kalobelo

  KAIMU KATIBU MKUU

  Wizara ya Maji na Umwagiliaji


  20 Februari, 2017


  0 0
  0 0

  Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amemaliza kufanya ziara yake ya siku tatu katika jimbo la Shinyanga.

  Katika ziara hiyo ya kikazi iliyoanza Februari 15,2017 kumalizika Februari 17,2017 ,Mheshimiwa Masele amekagua miradi ya maendeleo na kufanya vikao na wananchi wa kata 14 kisha kujadili na kuzitafutia ufumbuzi kero za wananchi. 

  Katika maeneo mengi aliyopita,Mheshimiwa Masele amekutana na kilio kikubwa cha tatizo la njaa linalowakabili wananchi ambao walidai wamekuwa wakiendesha maisha yao kwa kunywa uji hivyo kuiomba serikali iwaone kwa jicho la huruma na kuwapatia chakula. 

  Mheshimiwa Masele pia amekumbana na kilio cha bei kubwa ya maji inayotozwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga (SHUWASA),huku wananchi katika maeneo ambayo hayajafikiwa na mtandao wa maji kutoka ziwa Victoria wakiomba huduma hiyo ili kuondokana na kero ya maji. 
  Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiangalia eneo ambapo patajengwa choo kwa ajili ya shule ya msingi Twendepamoja yenye jumla ya wanafunzi 820 wanaotumia matundu 6 ya choo na walimu 8 pekee.Wa kwanza kushoto ni mwalimu Cephrine Philip anayefundisha katika shule hiyo. 
  Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa amebeba mtoto katika ofisi ya mtendaji wa kijiji cha Seseko inayotumika kama Zahanati ambapo kulikuwa kunatolewa huduma ya kliniki kwa watoto .
  Mheshimiwa Masele akiangalia choo kipya inachojengwa katika shule ya msingi Ushirika 
  Mheshimiwa akiwa katika eneo la choo cha shule ambacho kinatumiwa na walimu na wanafunzi,eneo hilo ndipo pia patajengwa choo kipya 
  Mheshimiwa Masele akiwasalimia wanafunzi wa shule ya msingi Kizumbi.


  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa atakayepokea rushwa kutoka kwa wauzaji, wasambazaji na watumiaji wa Madawa ya Kulevya.

  Ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kikao cha kwanza cha Baraza la Taifa la kudhibiti dawa za kulevya nchini.

  “Sheria ya udhibiti wa madawa ya kulevya itumike vizuri, Serikali na Baraza halitahitaji mtu yeyote mwenye mamlaka kupokea rushwa ikigundulika hatua kali zitachukuliwa” alifafanua Waziri Mkuu Majaliwa.

  Waziri Mkuu alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuendelea kuimarisha mapambano dhidi ya udhibiti wa Dawa za Kulevya nchini ambayo yamekuwa yakifanywa na Serikali za Awamu zilizotangulia.

  Aidha, Waziri Mkuu alisema kuwa mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya ni vita inayotakiwa kupigana kwa nguvu kubwa kwani madhara ya dawa hizo ni kubwa kwa jamii hususani vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa.

  “Tunahitaji ushirikiano wa karibu wa pande zote mbili za Muungano kwani tatizo hili limeathiri pande zote na ukanda wa bahari unatumika sana kama njia ya kuingiza dawa hizo” 

  “Wakuu wa Mikoa mna kazi kubwa katika vita hii, mkiwa wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na Usalama mpo kwenye nafasi nzuri ya kuendesha vita hii kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo” alisema Waziri Mkuu.

  Hata hivyo Waziri Mkuu alibainisha kuwa, wajibu wa Baraza ni kusimamia utekelezaji wa Sera ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya nchini, ambapo jukumu hilo ni kubwa na wajumbe wa Baraza hilo wanatakiwa kulitekeleza kwa uadilifu na umahiri mkubwa.

  Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya limeanzishwa chini ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Na. 5 ya mwaka 2015 ambapo Waziri Mkuu ndiye Mwenyekiti wa Baraza hilo pamoja na wajumbe wengine wakiwemo Waziri anayeshughulikia Mambo ya Sheria, Waziri anayeshughulikia Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Wengine ni Waziri anayeshughulikia Afya, waziri anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Waziri anayeshughulikia Mambo ya Nchi za Nje, Waziri anayeshughulikia Fedha, Waziri anayeshughulikia Maendeleo ya Vijana, Waziri anayeshughulikia Elimu, Waziri anayeshughulikia Kilimo, Waziri anayeshughulikia Uchukuzi na Waziri anayeshughulikia Ulinzi.

  0 0

   Kamishna Mkuu wamamlaka ya kupambana na kuzuia Dawa za KulevyaNchini Rogers William Sianga akijitambulisha mbele ya Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya wakati Waziri Mkuu alipokuwa akizindua Baraza Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya.

   Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza na  Mawaziri na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Udhibiti wa Dawa za Kulevya Nchini  wakati akifungua kikao cha Baraza hilo leo Jijini Dar es Salaam.

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza wakati wa uzinduzi wa kikao cha Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya.Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.
   
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga,Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Harrison Mwakyembe na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda wakizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa kikao cha Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya.

   Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo akizungumza jambo na Kamishna Mkuu wa mamlaka ya kupambana na kuzuia dawa Za Kulevya Nchini Rogers William Sianga wakati wa uzinduzi wa kikao cha Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya.

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga,Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Nape Nnauye, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Harrison Mwakyembe na Waziri wa Mambo ya NdaniMhe Mwigulu Nchemba wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu wakati wa uzinduzi wa kikao cha Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya.


older | 1 | .... | 1573 | 1574 | (Page 1575) | 1576 | 1577 | .... | 3283 | newer