Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

TAARIFA KWA UMMA AJALI YA WACHIMBAJI WADOGO WAPATAO 18 KUFUKIWA NA KIFUSI BAADA YA SHIMO KUPOROMOKA KATIKA ENEO LENYE LESENI YA UTAFUTAJI MADINI NA. PL 7132/2011 INAYOMILIKIWA NA STAMICO

$
0
0
Wizara ya Nishati na Madini inapenda kuufahamisha umma kuwa, Tarehe 13 Februari, 2017 kulitokea ajali ya wachimbaji wadogo wapatao 18 kufukiwa na kifusi wakati wakichimba dhahabu katika eneo la Buhemba Wilaya ya Butiama mkoani Mara lenye leseni ya utafutaji wa madini ya dhahabu, PL No. 7132/2011 inayomilikiwa na STAMICO. 
 Ajali hiyo ilitokana na kuporomoka kwa mwamba wakati wachimbaji hao walipovamia eneo hilo na kuanza kuchimba dhahabu kitendo ambacho kimekuwa kikifanyika hasa wakati wa usiku. Wachimbaji 13 waliokolewa tarehe hiyo hiyo 13 Februari, 2017 wakiwa hai na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Butiama kwa matibabu. 
 Zoezi la kutafuta wachimbaji wengine liliendelea ambapo tarehe 14 Februari, 2017 maiti mbili zilipatikana katika shimo hilo. 
Juhudi zaidi zinaendelea kutafuta wachimbaji wengine waliobaki ambapo Uongozi wa Wilaya ya Musoma kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Wizara ya Nishati na Madini kupitia Ofisi ya Madini Musoma kwa kushirikiana na Mgodi wa North Mara na Wachimbaji wadogo wanaendelea na zoezi la uokoaji. 
Juhudi za kufukua shimo lililoporomoka pia zinaendelea ili kuona kama kuna watu zaidi katika shimo hilo. Mgodi wa North Mara umetoa msaada wa mashine ya kuvuta maji na tope ili kuwezesha zoezi la ufukuaji kuendelea. 
 Wizara ya Nishati na Madini inachukua fursa hii kuwatangazia Wananchi wote kuwa shughuli za Utafutaji, Uchimbaji na biashara au shughuli yoyote ya madini zinatakiwa zifanyike kwa kuzingatia Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. 
Kwa maana hiyo, lazima shughuli hizo zifanywe na wamiliki wa leseni na vibali halali vinavyotolewa kwa mujibu wa sheria hiyo. Kwa kufanya hivyo, itawezesha wataalam wa Wizara ya Nishati na madini kufanya ukaguzi ili kuhakikisha kuwa shughuli hizo zinafanyika inavyotakiwa ikiwa ni pamoja na usalama katika shughuli za uchimbaji. 
Tunatoa wito kwa Wananchi wote ikiwa ni pamoja na wachimbaji wadogo kuacha tabia ya kuvamia maeneo na kuendesha uchimbaji katika eneo lolote bila kumiliki leseni kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. 

 Imetolewa na; 
KATIBU MKUU 
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

RC WA RUVUMA OLE SENDEKA AAGIZA TUME IUNDWE KUCHUNGUZA CHANZO CHA MOTO SEKONDARI YA ITAMBA

$
0
0
Na Edwin Moshi
Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy ameagizwa kuunda tume ya kuchunguza tukio la kuungua kwa bweni la wasichana liitwalo Serengeti la Itamba sekondari mkoani Ruvuma, pamoja na bweni lingine la wasichana lililoungua Jumamosi iliyopita.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka alipotembelea shule hiyo kujionea athari za moto huo ulioteketeza bweni moja lote

Amesema serikali haiwezi kukubali na ni lazima chanzo cha moto huo kijulikane na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wahusika endapo uchunguzi utabainisha kuwa kuna watu wamehusika.
Mhe. Olesendeka amesema serikali haiwezi kukubali vitendo vya moto kuendelea kuunguza shule mbali mbali hapa nchini.
Pia ameuagiza uongozi wa shule hiyo kuweka Mazingira mazuri kubaini ukweli wa hujuma kama hizi zinazoweza kujitokeza lakini pia kama kuna dosari mbali mbali miongoni mwa wanafunzi au shule nzima zijulikane ili ufumbuzi upatikane.
 Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka(wapili kushoto) akiangalia athari za moto wa bweni hilo

 Mabaki ya vitu vya wanafunzi vilivyoteketea kwa moto katika bweni hilo

Mkuu wa mkoa akizungumza na wanafunzi shuleni hapo

AMSHA KIPAJI CHAKO NA SINGA WA MBEYA

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 17,2017

Article 7

ZANTEL, BAKWATA WAZINDUA HUDUMA YA MPYA YA “ZANTEL MADRASA JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya kutoka Zantel iliyopewa jina la ‘Zantel Madrasa’ ambayo ni mahususi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Zantel watakaopenda kutumia huduma hii watatakiwa kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15586 na kufuata maelekezo. (katikati) ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin na Mkuu wa kitengo cha huduma na bidhaa Zantel Hamza Zuheri.

 Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza leo jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya kutoka Zantel iliyopewa jina la ‘Zantel Madrasa’ ambayo itawawezesha waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza kuhusu imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu zao za mkononi. (Katikati) ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry ambaye alikuwa mgeni rasmi na Mkuu wa Itifaki BAKWATA Mohammed Nassor.
 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin wakionyesha vipeperushi vya huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma hiyo uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Kongamano la Wanasayansi watafiti lamalizika Jijini Mwanza

$
0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Bonde la Ziwa Victoria ambaye pia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi cheti cha shukrani, Bi. Joyce Kasebela baada ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuwa mmoja wa wadhamini wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria lilimalizika jana jijini Mwanza.

Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dkt Leonard Chamuriho (kushoto) akifuatiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Prof. Faustine Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki wakishiriki Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria lililomalizika jana jijini Mwanza.
Mwakilishi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo wa Jijini Mwanza, Bi. Dorah Michael (kushoto) akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) katika maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria jana jijini Mwanza.
ASP Andrew Majaliwa (kulia) akiwa ameshika moja ya vipeperushi vya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), baada ya kupata maelezo kuhusu mazingira kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi kwenye maonesho ya washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria, lililomalizika jana jijini Mwanza.

UNDP WAKUTANA NA WANAFUNZI WA SHULE YA WASICHANA ,WERUWERU MKOANI KILIMANJARO KUJADILI MALENGO MAPYA YA MAENDELEO ENDELEVU

$
0
0
Mwakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Alavaro Rodriguez (katikati) akiwa ameongozana na Mkurugenzi anayesimamia Mashirika ya Umoja wa Mataifa ,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Balozi Celestine Mushi (kushoto) na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru ya mkoani Kilimanjaro,Rosalia Flavian wakiingia katika ukumbi wa shule hiyo kwa ajili  kongamano.
 Mwakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Alavaro Rodriguez akizunguza katika Kongamano hilo.
Baadhi ya wanafunzi katka shule ya Sekondari ya Wasichana  ,Weruweru wakiwa katika kongamano hilo.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania ,Hoyce Temu akizungumza katika kongmano hilo. 


WAZIRI MKUU ALIPOHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA WILAYANI SIMANJIRO

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA- MERERANI

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro wakati  aliposimama  akitoka  Orkesimet kwenda  Mererani Februari 16, 2017.
 Mwananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro  akiwasilisha kero yake kwa njia ya bango akidai mawasiliano ya simu za mkononi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  aliposimama na kuwasalimia wananchi wa kijiji hicho waliokusanyika  barabarani. Alikuwa akitoka  Orkesimet kwenda  Mererani Februari 16, 2017.
  Wananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati aliposimama na kuwasalimia akitoka  Orkesimet kwenda  Mererani Februari 16, 2017.
 Baadhi ya wananchi  Mererani mkoani Manyara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia  katika mkutano wa hadhara  kwenye uwanja wa mikutano wa Mererani ,  Februari 16, 2017.
 aziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema wingi wa mabango  katika mikutano ya hadhara  ya viongozi wakuu ni ishara ya wazi kuwa  watendaji wa  Halmashauri  hawawatembelei  wananchi na kutatua kero zao. Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa mikutano wa  Mererani mkoani Manyara Februari 16, 2017, Mheshimiwa Majaliwa alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro na watendaji wake kukusanya mabango  yaliyokuwa yakionyeshwa na wananchi kwani mengi ya matatizo yanapaswa kumalizwa na viongozi hao  na aliwaagiza  kurejea Mererani siku inayofuata ili waitishe mkutano na  kujibu bango moja baada ya jingine.
Pichani,  watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro wakikusanya mabango hayo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Ndugu Ali Juma baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara  kwenye uwanja mikutano  wa Mererani mkoani Manyara Februari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

PROFESA MBARAWA ATEMBELEA NA KUKAGUA KIVUKO CHA MV KILAMBO MKOANI MTWARA

$
0
0
Na Alfred Mgweno, TEMESA Mtwara.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa ametembelea na kukagua kivuko cha MV Kilambo kilichopo Mkoani Mtwara mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. Kivuko hicho kinavusha magari, abiria na mizigo kati ya Kilambo upande wa Tanzania na Namoto Msumbiji.



Akiwa katika ziara hiyo Profesa Mbarawa aliambatana na viongozi mbalimbali wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mkoani hapa. Profesa Mbarawa  alikaribishwa na Mkuu wa Kivuko hicho Jaston Mbawala, Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wa Mkoa wa Mtwara Mhandisi Saidi Mongomongo, Mhandisi  Msaidizi wa Kivuko Samwel Chibwana pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko Mhandisi Japhet Y. Maselle.



Akiwa kivukoni hapo, Profesa Mbarawa alipata wasaa wa kusikiliza baadhi ya  changamoto zinazokikumba kivuko hicho ambapo Mhandisi Saidi Mongomongo alitaja changamoto hizo kuwa ni upungufu wa maji nyakati za kiangazi, ubovu wa maegesho ambayo husababisha magari makubwa kunasa wakati yanatoka au kuingia ndani ya kivuko pamoja na kukosekana kwa boti ndogo za uokoaji ambazo zingesaidia wakati wa dharura.



Baadae Profesa Mbarawa alipata fursa ya kuongea na watumishi walio chini ya Wizara yake katika kikao kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa mkoa huku akiwataka watumishi  kuendelea kushirikiana na serikali, kufanya kazi kwa kasi na uadilifu kwa kuzingatia weledi. Pia aliwataka watumishi kujenga tabia ya kujitoa kwa ajili ya nchi yao.



Profesa Mbarawa alikuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja mkoani humo kwa nia ya kutembelea na kukagua utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya wizara yake.


 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasaliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Kivuko cha MV Kilambo kinachomilikiwa na TEMESA Jaston Mbawala wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya mkoani Mtwara. Kulia kwa Waziri ni Mhandisi Samwel Chibwana wa TEMESA Mtwara.
 Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mkoa wa Mtwara Mhandisi Saidi Mongomongo akimuelezea jambo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa alipotembelea kivuko cha MV Kilambo kilichopo mkoani Mtwara kinachotoa huduma mto Ruvuma mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa akikagua injini ya kivuko cha MV Kilambo kinachotoa huduma mto Ruvuma kati ya Kilambo, Tanzania na Namoto, Msumbiji. Picha na Alfred Mgweno, TEMESA

Rais wa Zanzibar Dk Shein Akutana na Mkurugenzi wa NMB Tanzania

$
0
0


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Tanzania Bi. Ineke Bussemaker, alipofika Ikulu Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimsindikiza mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Tanzania Bi Ineke Bussemaker, baada ya mazungumzo yao leo Ikulu Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Tanzania baada ya mazungumzo yao Ikulu leo 

PICHA NA IKULU

BURUDANI MURUA KABISA YA TWANGA PEPETA KILA JUMAPILI PALE MZALENDO PUB.

RED CROSS YAKABIDHI KADI ZA UANACHAMA IDARA YA MAAFA

$
0
0
 Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania Bw. Mwadini Jecha (katikati) akiweka saini kitabu cha wageni Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu walipotembelea Idara hiyo na kukabidhi Kadi za Uanachama kwa Idara  hiyo, tarehe 16 Februari, 2017.
 Mkurugenzi wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Tanzania Bw.Renatus Mkaruka (wa kwanza kulia) akizungumza jambo wakati wa zoezi la kukabidhi kadi za Uanachama wa chama hicho kwa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Februari 16, 2017 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jenerali Mbazi Msuya (kulia) akipokea kadi ya uanachama wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania kutoka kwa Rais wa Chama hicho Bw. Mwadini Jecha Februari 16, 2017 katika Ofisi za Idara hiyo Dar es Salaam.
Mratibu wa Maafa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Charles Msangi akipokea kadi ya uanachama wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania kutoka kwa Katibu wa chama hicho Bw. Julius Kejo Februari 16, 2017 katika Ofisi za Idara hiyo Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

TASAF KISHAPU YAWAPIGA MSASA WADAU

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Stephen Magoiga ameagiza watendaji wa vijiji kuhakikisha wananchi waliochukua fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Taifa (TASAF) bila kuwa na sifa wanarudisha mara moja.

Magoiga alitoa agizo hilo jana wakati akifungua mafunzo kwa wadau wa TASAF kwa vijiji vitatu katika Kata ya Mwakipoya ili kuwajengea uelewa katika kuwaudumia walengwa.



Alisema lengo la mpango wa TASAF ni kusaidia kaya zisizo na uwezo hivyo ni wajibu wa wadau hasa wajumbe wa Serikali za vijiji kuhakikisha wanawatambua wananchi wa maeneo yao ili kubaini kaya maskini.



Mkurugenzi aliwataka wadau kusimamia vizuri walengwa akisisitiza kuwa Serikali kupitia TASAF ina jukumu la kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na maisha bora kwa kuwapa ruzuku ili kujiendeleza.



Magoiga aliongeza kwa kuwahimiza wadau hao kufuatilia maendeleo ya watoto wa walengwa wa mpango huo wanaopata ruzuku kwani elimu ndiyo inaweza kuondoa umaskini.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Stephen Magoiga akifungua rasmi mafunzo kwa wadau wa TASAF kwa vijiji vitatu katika Kata ya Mwakipoya ili kuwajengea uelewa katika kuwaudumia walengwa.
 Mratibu wa TASAF Wilaya ya Kishapu, Sospeter Nyamhanga akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga ambaye alikuwa mgeni rasmi kufungua rasmi mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (hayupo pichani).

 Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Stephen Magoiga.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


WAZIRI MAKAMBA AZUNGUMZA NA MABALOZI KUHUSU UHARIBIFU WA MAZINGIRA

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba (katikati) akiongea wakati wa mkutano na na Mabalozi ambao ni Washirika wa Maendeleo. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais liliko barabara ya Luthuli.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwasilisha mada na kuonyesha picha mbalimbali za uharibifu wa mazingira zilizopigwa wakati wa ziara yake ya mikoa 10 mwaka jana kwa Mabalozi ambao ni Washirika wa Maendeleo ya masuala ya mazingira.
 Sehemu ya Washiriki wa Mkutano huyo ambao ni Mabalozi  wakifuatilia kwa makini  wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwasilisha mada kwenye mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi (wa pili toka kulia)  akifanunua jambo wakati wa mkutano huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba wakiongea jambo Mwakilishi wa UN Nchini Tanzania Alvaro Rodriguez baada ya kumaliza mkutano huo.

WAZIRI NAPE AFANYA MSAKO KARIAKOO LEO KUKAMATA WANAODURUFU KAZI ZA WASANII

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Dkt. Hassan Abbas (kushoto) pamoja na maafisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), wakia katika oparesheni maalum ya kushtukiza la kukamata wafanyabiashara wanaodurufu kazi mbalimbali za sanaa nchini, katika eneo la Karikoo jijini Dar es salaam leo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto) akiongoza msafara huo wa kufanya oparesheni maalum ya kushtukiza la kukamata wafanyabiashara wanaodurufu kazi mbalimbali za sanaa nchini, katika eneo la Karikoo jijini Dar es salaam leo. Picha na Iman Nsamila.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiangalia baadhi ya DVD feki zilizokuwepo katika moja ya maduka ya Kariakoo, Jijini Dar es salaam leo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiingia katika moja ya stoo za Duka mojawapo linalouza na kudurufu kazi za wasanii mbalimbali nchini.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

$
0
0
Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu. 

Kufuatia mapambano yanayoendelea nchi nzima dhidi ya watu wanaojihusisha na uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya misako na Mafanikio yaliyopatikana katika Misako ni kama ifuatavyo:-

KUKAMATA WATUHUMIWA WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA UUZAJI/USAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA.

Mnamo tarehe 11.02.2017 majira ya saa 02:00 usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya misako katika maeneo ya Manga na Nsalaga – Uyole na kukamata watuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na wauzaji, wasambazaji na watumiaji [mateja]. Watuhumiwa waliokamatwa kutokana na kujihusisha ba usambazaji na uuzaji wa dawa za kulevya ambao ni 1.SHABAN RAMADHAN [40]Mkazi wa Uyole 2. RASHID YASIN [35]Mkazi wa Nonde 3. RODA MWAMBERA [60]Mkazi wa Mama John 4. MRISHO RAMADHAN[22] Mkazi wa Airport - Iyela na 5. MUSSA KIMBE [33] Mkazi wa Nonde.

Watuhumiwa wote wapo mahabusu na mahojiano zaidi yanaendelea ili kubaini mtandao mzima wa watu wanaojihusisha na dawa za kulevya.

KUKAMATA WAUZAJI/WASAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA.

Aidha kufuatia misako iliyofanyika kuanzia tarehe 19.01.2017 hadi tarehe 09.02.2017 katika maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya, Watuhumiwa wawili walikamatwa katika matukio mawili tofauti wakiwa na dawa za kulevya.

Katika msako wa kwanza uliofanyika maeneo ya Ilemi Jijini Mbeya, HENRY MWAMFUPE [19] Mkodishaji Baiskeli na Mkazi wa Ilemi alikamatwa akiwa na kete 03 za dawa za kulevya aina ya Heroine.


NEWZ ALERT:WATUMISHI WAWILI WA TRA WANASHIKILIWA NA VYOMBO VYA DOLA KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Watumishi Wawili wa Mamlaka ya Mapato (TRA) wanashikiliwa na vyombo vya dola wakituhumiwa kujihusisha na upitishaji Wa kemikali ambazo hutumika kutengenezea dawa za kulevya aina ya Heroin.

Kukamatwa kwa watumishi hao wa umma kumetangazwa  leo na Kamishina Wa Operasheni ya Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya Mihayo Msekela.
Kamishina wa Oparesheni wa Mamlaka ya Kuzuia na kupambana na dawa za kulevya,Mihayo Msikhela akifafanua japo alipokuwa akizungumza na baadhi ya Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali mapema leo,katika ofisi za Mamlaka hizo zilizopo Upanga,jijini Dar Es salaam kuhusiana na Operesheni za kuwakamata watuhumiwa waliojihusisha na biashara haramu ya usafirisha wa dawa za kulevya hapa nchini,ambapo katika Oparesheni hizo zinazoendelea nchini,ilionesha mafanikio kwa baadhi ya mikoa kama taarifa inavyoonesha hapo chini.PICHA NA MICHUZI JR.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishina wa Operesheni wa Mamlaka ya Kuzuia na kupambana na dawa za kulevya,Mihayo Msikhela alipokuwa akizungumza na baadhi ya Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali mapema leo,katika ofisi za Mamlaka hizo zilizopo Upanga,jijini Dar Es salaam kuhusiana na Operesheni za kuwakamata watuhumiwa waliojihusisha na biashara haramu ya usafirisha wa dawa za kulevya hapa nchini
Kamishina wa Operesheni wa Mamlaka ya Kuzuia na kupambana na dawa za kulevya,Mihayo Msikhela akifafanua japo alipokuwa akizungumza na baadhi ya Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali mapema leo,katika ofisi za Mamlaka hizo zilizopo Upanga,jijini Dar Es salaam kuhusiana na Operesheni za kuwakamata watuhumiwa waliojihusisha na biashara haramu ya usafirisha wa dawa za kulevya hapa nchini,ambapo katika Operesheni hizo zinazoendelea nchini,ilionesha mafanikio kwa baadhi ya mikoa kama taarifa inavyoonesha hapa chini.

WAZIRI MKUU: SERIKALI KUPIGA MARUFUKU POMBE ZA VIROBA

$
0
0

​​WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia Machi mosi, 2017 Serikali itapiga marufuku matumizi ya pakiti za plastiki kufungashiwa pombe kali maarufu kwa jina la ‘viroba’.

“Tumekaa na wenye viwanda na kukubaliana kuwa wanaotengeneza Pombe waziweke katika ukubwa unaokubalika. “Sasa hivi viroba vimeenea kila kona hata watoto wa shule za msingi wanatumia kwa sababu ni rahisi kuweka mfukoni na kutembea navyo. Kuanzia tarehe moja Machi, tutakayemkamata ameshika pombe ya viroba, sisi na yeye.”

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Februari 16, 2017) wakati akizumgumza na maelfu ya wakazi wa mji mdogo wa Mererani, wilayani Simanjiro akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Manyara.

Amesema agizo hilo linaenda sambamba na vita dhidi ya dawa za kulevya kwani mji wa Mererani unaongoza kwa matumizi ya dawa hizo haramu.

“Tutawakamata wanaosambaza, wanaouza na wanaokula. Hapa Mererani kuna bangi, kuna mirungi, cocaine na heroine. Mkuu wa Mkoa hapa panahitaji operesheni kupambana na dawa za kulevya. Piteni kwenye vijiwe na kukagua wale waliolegealegea, kisha tuwapime,” alisisitiza.

Akifafanua suala la uwekezaji kwenye eneo la Shambalai kutokana na ujumbe ulioandikwa kwenye mabango, Waziri Mkuu alisema katika eneo hilo zimetengwa ekari 500 kwa ajili ya EPZA ili kujenga miundombinu mbalimbali.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images