Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live

TIMU YA NGAYA YA COMORO YAWASILI NCHINI KUMENYANA NA YANGA JUMAMOSI UWANJA WA TAIFA

0
0

Na Dotto Mwaibale


KIKOSI cha Timu ya Ngaya kutoka nchini Comoro kimewasili nchini kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Yanga katika dimba litakalofanyika kesho kutwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo imewasili leo saa saba na nusu mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC), huku ikiwa imeongozana na baadhi ya viongozi wake.

Mara baada ya kuwasili timu hiyo ilipokelewa na wananchi wa nchi hiyo wanaoishi hapa nchini hata hivyo viongozi wa timu hiyo hawakuwa tayari kuzungumza chochote na wanahabari badala yake walipiga picha ya pamoja na wachezaji na kisha kupanda kwenye magari na kuondoka.

Katika mchezo wa awali uliofanyika nchini humo Yanga iliibuka kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya timu hiyo.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na kuwa waamuzi wake wanatarajiwa kufika kesho.

Wachezaji wa Timu ya Ngaya ya nchini Comoro wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga utakaofanyika kesho kutwa Uwanja wa Taifa. Katika mchezo wa awali uliofanyika Comoro Yanga ilishinda bao 5-1.

Picha ya pamoja na viongozi wao baada ya kuwasili.

Mmoja wa viongozi wa timu hiyo (kushoto), akitoa maelekezo kabla ya kuondoka uwanjani hapo. (Picha na blog ya habari za jamii.com)

Wachezaji wa timu hiyo wakiingia kwenye gari kuelekea hotelini walikofikia.

WAKINA MAMA TABORA WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUTANGAZA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA

SOPHIA BIANAKO (MISS TANGA 2001) AJIKITA KATIKA KUSAIDIA JAMII

DC CHONGOLO ATAKA SERIKALI ISIPELEKE CHAKULA CHA NJAA

0
0
Na Wankyo Gati,,Arusha

Wananchi wa jamii ya kifugaji hususani vijijini wametakiwa kuacha kulalamika kuna njaa na badala yake watumie mifugo wanayofuga kuuza katika minada na kisha kununua chakula cha kutosha majumbani mwao na kuondoa tafsiri ya kupatiwa chakula na Serikali ili hali wanamifugo.

Pia ameitaka Serikali kutowaletea chakula cha njaa,ambapo jamii kubwa imejijengea tabia ya ya kutoacha chakula cha ziada kwa ajili ya Serikali badala yake kutegem,ea kuwa Serikali ittawaletea chakula cha msaada badala yake wabadili mtazamo na tabia zao za kuweza ziada na kuhifadhi chakula endepo kutakuwa na uhaba wa chakula kam hivi sasa kumekuwa na uhaba wa mvua hali ambayo mazao yamekuwa hayastawi kama awali.

Hata hivyo katika hoja hizo Mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Chongolo akatumia nafasi hii kuwataka viongozi wasiwajengee wananchi kuwa kuna njaa na badala yake wawajengee uwezo pindi wanapouza mifugo yao wasitumie fedha zao katika masuala mengine na badala yake wanu nue chakula na kwamba yeye katika wilaya yake haitaji msaada wa chakula kwani wananchi wake si masikini wa kununua chakula.

Mkoa wa Arusha umejaaliwa kuwa na wilaya Zaidi ya sita ambapo wananchi wengi wa vijijini ni wa jamii ya kifugaji ambapo katika kipindi cha hivi karibuni kulizuka mjadala kuwa maeneo ya wilaya za Mkoa huo kuna njaa ambapo serikali imekuwa ikipingana vikali na kauli hizo za wananchi na kuzua mjadala mkubwa kwa wananchi.

MSAMBAZAJI WA UJUMBE FEKI MITANDAONI ATIWA MBARONI

MFANYABIASHARA MAARUFU NA MWENYEKITI WA YANGA,YUSSUF MANJI AACHIWA KWA DHAMANA

0
0

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

Baada ya kusota rumande kwa takribani siku saba, hatimaeMwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusufu Manji amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya.

Manji ambae pia ni Diwani wa Mbagala Kuu na mfanyabiashara maarufu ameshtakiwa chini ya kifungu cha sheria namba 17(1)(a) ya sheria ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya namba 5 ya mwaka 2015.

Amesomewa mashtaka yake leo na karani wa mahakama hiyo, Sarah Mulokozi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha.

Manji amekananusha kutumia dawa za kulevya na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kuweka dhamana ya milioni kumi na mdhamini mmoja ambaye nae ameweka kiasi hicho hicho cha dhamana

Manji alifika mahakamani hapo saa nane kasoro nne na alipandishwa mahakamani majira ya saa tisa. Katibu wa klabu hiyo, Charles Boniphace Mkwasa ndiye aliyemuwekea dhamana Manji na kumfanya awe huru.

Katika kesi hiyo Manji anatetewa na mawakili watatu waliokuwa wakiongozwa na wakili Alex Mgongolwa, Hudson Ndusyepo na Jeremiah Mtobesya huku upande wa Jamuhuri ukiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi wa mashtaka, Oswald Tibabyekomya aliyekuwa akisaidiana na wakili wa serikali Shadrack Kimaro.

Akisoma hati ya mashtaka, Mulokozi amesema kuwa, kati ya Februari 6 na 9 mwaka huu huko Upanga Sea View ndani ya Wilaya ya Ilala jijiini hapa, mshtakiwa alitumia dawa za kulevya aina ya Heroine (diacefyl Morphine)..

Mara baada ya kutimiza masharti ya dhamana Manji aliondoka katika viwanja vya mahakama hiyo akiwa katika gari aina ya Hummer lenye namba za usajili T 670 BBX huku akisindikizwa na umati wa mashabiki wa Yanga.

NAIBU BALOZI WA ISRAEL NCHINI MHE. MICHAEL BAROR ATEMBELEA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE(JKCI)

0
0
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimsikiliza Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye  makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Michael Baror alipotembelea Taasisi hiyo jana kwaajili ya  kuona huduma mbalimbali za matibabu ya Moyo wanazozitoa. Mhe. Naibu Balozi Baror aliahidi nchi yake kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo ili watanzania waendelee kupata huduma bora za matibabu ya Moyo. Mwanzoni mwa mwezi ujao jumla ya watoto tisa wanatarajia kwenda nchini Israel kwaajili ya matibabu ya moyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiagana na  Naibu Balozi wa Israel nchini ambaye makazi yake yapo Nairobi nchini Kenya Mhe. Michael Baror mara baada ya kumaliza kuitembelea  Taasisi hiyo jana kwa ajili ya  kuona huduma mbalimbali za matibabu ya Moyo wanazozitoa. Mhe. Naibu Balozi Baror aliahidi nchi yake kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo ili watanzania waendelee kupata huduma bora za matibabu ya Moyo. Mwanzoni mwa mwezi ujao jumla ya watoto tisa wanatarajia kwenda nchini Israel kwaajili ya matibabu ya moyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na  Naibu Balozi wa Israel nchini ambaye makazi yake yapo Nairobi nchini Kenya Mhe. Michael Baror alipoitembelea  Taasisi hiyo jana kwaajili ya  kuona huduma mbalimbali za matibabu ya Moyo wanazozitoa. Mwanzoni mwa mwezi ujao watoto tisa wanatarajia kwenda nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya moyo. Picha na Anna Nkinda - JKCI

ASKARI TISA WALIOSIMAMISHWA KAZI KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA, WAKABIDHIWA KWA KAMISHNA WA TUME YA DAWA ZA KULEVYA


NSSF YAKUTANA NA WAAJIRI WA MKOA WA DODOMA

0
0
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)  limeendesha semina maalum kwa waajiri wake wa mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu endelevu waliojipangia kukutana na waajiri wake ili kuendelea kuelezana umuhimu wa hifadhi ya jamii  kwa waajiriwa  wao  na pia kupata fursa ya kuambiana changamoto kutoka pande zote ili kushirikiana kuzitatua na kuboresha huduma kwa pande zote.

Akiwakaribisha waajiri hao katika semina hiyo, Meneja wa NSSF mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma aliwaambia waajiri hao kuwa huo ni urataribu endelevu waliojipangia wa kukutana nao na kuwataka watekeleze wajibu wao wa kuwaandikisha wanachama na kuleta michango kwa wakati ili kuwezesha Shirika kutoa mafao kwa wanachama wao kwa wakati na kwa usahihi na kuwakumbusha kuhusu sheria ya NSSF inayoruhusu kutoa adhabu kwa waajiri wanaposhindwa kuwasilisha michango kwa wakati.

Awali, Meneja Matekelezo wa Shirika hilo, James Oigo aliwaambia waajiri hao kuwa swala la hifadhi ya jamii ni muhimu kuliko ambavyo mtu anaweza kufikiri kwa kuwa kuna mfano wa wazee wengi ambao mnawajua wanaishi maisha duni  kutokana na kutokuwa katika mfumo wa hifadhi ya jamii.

NSSF imeendelea kuwa kinara katika mifuko ya hifadhi ya jamii katika wingi na ubora wa mafao na sasa imeelekeza nguvu zake katika uwekezaji wa viwanda kama fursa  ya kuendelea kuboresha mafao ya wanachama wake, kuongeza ajira na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.
Meneja Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), James Oigo akitoa Mada wakati wa Semina semina maalum kwa waajiri wake wa mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu endelevu waliojipangia wa kukutana na waajiri hao, iliyofanyika katika Ukumbi wa Veta, Mjini Dodoma.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma akizungumza wakati wa Semina semina maalum kwa waajiri wake wa mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu endelevu waliojipangia wa kukutana na waajiri hao, iliyofanyika katika Ukumbi wa Veta, Mjini Dodoma.
Kaimu Meneja Kiongozi wa Uhusiano na Masoko wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salum Kimaro akitoa maelezo kwa wanasemina hao, iliyofanyika katika Ukumbi wa Veta, Mjini Dodoma.
Washiriki wa semina wakiajiandikisha. 

Kesi dhidi ya anayedaiwa kuwa malkia wa Tembo yaendelea kuunguruma.

0
0
Na Karama Kenyunko, Blog ya Jamii 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa mshtakiwa Salvius Matembo anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kujihusisha na biashara ya Meno ya Tembo yenye thamani ya zaidi ya bilioni 13.9 alijaribu kuwatoroka polisi walipoenda kumkamata.

Askari wa Jeshi la Polisi Idara ya Upelelezi na Makosa ya Jinai, Koplo Emmanuel John alisema hayo leo wakati akitoa ushahidi wake mbele ya hakimu mkazi, Huruma shahidi kama shahidi wa pili.

Mshtakiwa matembo anashtakiwa pamoja na raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu, Yang Feng Glan (66) na Manase Philemon.

Akiongozwa na wakili wa Serikali, Paul Kadushi, Koplo Emmanuel alidai kuwa Mei 14,2014 akiwa ofisini kwake makao makuu ya polisi akiwa na askari wenzake waliitwa na msaidizi wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Mkosa ya Jinai na kupewa jukumu la kumtafuta Matembo.

Amedai kuwa baada ya siku saba, Mei 21, 2014 ndipo alipofanikiwa kumkamata Matembo baada ya kupata taarifa kutoka kwa msiri wao kuwa mtuhumiwa huyo alionekana katika baa ya Kilimanjaro iliyopo Sinza .

Amesema kuwa, kwa kuwa hakuwa akimfahamu mtuhumiwa alienda na msiri huyo hadi katika baa hiyo na kufanikiwa kumkamata baada ya kuonyeshwa alipokuwa amekaa na kujitambulisha kuwa wao ni polisi na kumueleza yupo chini ya ulinzi kwa kujihusisha na Meno ya Tembo .

Aliongeza kuwa Matembo alitaka kutoroka lakini kwa kuwa walijipanga aliweza kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi.

Alieleza kuwa baada ya hapo walimpeleka katika kituo cha polisi cha Kijitonyama lakini kabla ya kumfikisha, wakiwa njiani Matembo aliwashawishi kuwapa rushwa ili wamuachie lakini walikataa.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22,2014 walijihusisha na biashara ya nyara za serikali.

Katika kipindi hicho washtakiwa hao wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilogramu 1889 zenye thamani ya Sh 5.4 bilioni bila ya kuwa na leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyama Pori.

Wanadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22,2014 kwa makusudi raia wa China, China, Yang Feng Glan aliongoza na kufadhiri vitendo vya kijinai kwa kukusanya na kusafirisha vipande hivyo 706 vya Meno ya Tembo bila ya kuwa na kibali chochote kile kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama Pori.

Kwa upande wa washtakiwa Salvius na Manase wanadaiwa kuongoza makosa ya uhujumu uchumi kwa kusaidia biashara ya nyara za serikali kwa kukusanya, Kusafirisha na Kuuza Meno ya Tembo kwa nia ya kujipatia faida. 

Ilidaiwa kuwa Mei 21, 2014 katika eneo la Sinza Palestina wilaya ya Kinondoni mshtakiwa Manase alitoroka chini ya ulinzi halali wa askari wa Jeshi la Polisi D 7847 Koplo Beatus ambaye alikuwa akimshikilia kwa makosa ya kujihusisha na biashara za nyara za serikali.
Anayedaiwa kuwa Malkia wa Tembo,Yang Feng Clan anyedaiwa kujihusisha na biashara ya meno ya tembo ya zaidi ya bilioni 13 akirudishwa mahabusu.

PROF. MBARAWA: UWANJA WA NDEGE WA MTWARA UJENZI MWEZI JULAI

0
0
Serikali imesema  ina mpango wa kukarabati uwanja wa ndege wa  Mtwara  ifikapo mwezi Julai mwaka huu ili kuruhusu ndege kubwa kuweza kutua uwanjani hapo na hivyo kufungua fursa za kiuchumi mkoani humo.

Akizungumza mara baada ya kukagua uwanja huo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amesema kuwa ukarabati huo utahusisha njia ya kuruka na kutua ndege, maeneo ya maegesho pamoja na barabara yenye urefu wa km 1.5 inayoingia katika uwanja huo.



"Tunategemea mwisho wa mwezi huu kutangaza zabuni ya ukarabati wa uwanja huu, matumaini yetu tutampata mkandarasi mzuri kwa ajili ya kazi hii", amesema Waziri Mbarawa.Aidha, Profesa Mbarawa amefafanua kuwa Serikali itahakikisha kuwa  inajenga uzio katika uwanja huo ili kuhakikisha usalama wa uhakika uwanjani hapo.

Sambamba na hilo, Waziri Mbarawa ametanabaisha kuwa Serikali ina mpango wa ununuzi wa rada nne  mpya kubwa na za kisasa ili kubaini taarifa za ndege  nchini tangu zinapoanza kuruka hadi kutua.

“Tukiwa na rada kubwa na za kisasa zitatusaidia kubaini ndege zote hata ndogo zinazoingia katika maeneo ya viwanja vya madini kwa lengo la kuona ndege hizi zinaingia na zinatoka na nini?”, amesisitiza Waziri Mbarawa.

 Kuhusu ujio wa ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Bombadier Q 400, Waziri huyo amemhakikishia Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda,  kuwa Serikali inatarajia kuanzisha safari zake kutoka Dar- Mtwara na Songea hivi karibuni.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), mkoa wa Mtwara, Bi. Zitta Majinge (wa pili kulia), kuhusu ukarabati wa uwanja huo mara baada ya kuwasili leo mkoani hapo. Kushoto kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Evod Mmanda.
 Muonekano wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara ambalo lina uwezo wa kubeba abiria 100 kwa wakati mmoja.
 Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), mkoa wa Mtwara, Bi. Zitta Majinge (katikati), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), mipaka ya Uwanja wa Ndege huo ambao unahitajika kuwekwa uzio ili kulinda usalama wa uwanja.
 Muonekano wa barabara ya kuruka na kutua ndege katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara yenye urefu wa mita 2258 na upana wa mita 30.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WATENDAJI WA MANISPAA YA WILAYA YA ILEMELA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameunga mkono jitihada za kupambana na dawa za kulevya nchini kama hatua ya kuliokoa na taifa janga hilo ambalo limesababisha madhara makubwa katika jamii.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.Makamu wa Rais amesisitiza kuwa mapambano dhidi ya dawa za kulevya yatakuwa ni endelevu lengo likiwa kukomesha kabisa uuzaji,usambazaji na utumiaji wa dawa hizo kama hatua ya kuokoa kizazi cha sasa na kijacho nchini.

Amesema kamwe serikali ya wamu ya Tano hatarudi nyuma katika vita dhidi ya dawa za kulenya na ameomba wananchi waendelee kutoa taarifa za siri kwa vyombo vya dola zitakazosaidia kuwabaini watu wanajihusisha na biashara hiyo ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Kuhusu tatizo la uvuvi haramu, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi wa mikoa ya kanda ya Ziwa wakiwemo viongozi wa Mwanza na mikoa mingine nchini kuanzisha mara moja oparesheni kali ya kupambana na wavuvi haramu katika Ziwa Victoria ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa samaki katika Ziwa hilo.

“Viwanda vya samaki kwa sasa havipati samaki wa kutosha hali ambayo imezorotesha shughuli za kuchakata samaki hivyo nawaagiza viongozi wote kupambana ipasavyo na wavuvi haramu na kamwe wasionewe huruma” amesisitiza Makamu wa Rais.

Makamu Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini ni muhimu yakaenda pamoja na oparesheni ya kukomesha uvuvi haramu katika Ziwa Victoria na maeneo mengine nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia Watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ilemela jijini Mwanza. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe. Angelina Mabula (kulia) wakati wa mkutano wa Makamu wa Rais na Watendaji  wa Halmashauri ya wilaya ya Ilemela jijini Mwanza. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akihutubia mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wa watendaji na Halmashauri ya wilaya ya Ilemela jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Picha ya pamoja.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUIMARISHA SEKTA YA UVUVI

0
0
Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuimarisha Sekta ya Uvuvi katika azma yake ya kujenga uchumi imara unaojitegemea utakaostawisha maisha ya Wananchi wake.

Alisema uimarishaji huo utaelekezwa zaidi katika ujenzi wa Viwanda Vidogo vidogovya usindikaji wa mazao ya Baharini utakaotoa fursa ya kukaribisha Makampuni na Taasisi za Kimataifa kuwekeza miradi yao Visiwani Zanzibar. 

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Ujumbe wa Viongozi wa Kampuni ya Uvuvi ya Hong Dong kutoka Nchini China ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wake Bwana Lan Ping Yong hapo Ofisini kwake Majengo ya Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. 

Alisema Sekta ya Uvuvi bado ina rasilmali ya kutosha inayoweza kusaidia uchumi wa Taifa unaokwenda sambamba na fursa za upatikanaji wa ajira zitakazosaidia kupunguza ukali wa maisha ya Wananchi walio wengi Nchini. 

“ Hii ni njia bora na mwafaka ya upatikanaji wa ajira hasa kwa Vijana ”. Alisema Balozi Seif Ali Iddi. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uvuvi kutoka Nchini China Bwana Lan Ping Yong kushoto akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi azma ya Kampuni hiyo kutaka kuwekeza mradi wa Uuvi Visiwani Zanzibar. Viongozi hao walikutana katika Ofisi ya Balozi Seif iliyomo ndani ya jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. 
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia akizungumza na Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bwana J.C Barupal kwenye Ofisi yake iliyomo ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni. 


Shule ya Msingi ya Wavulana ya Almuntazir yawatuza wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao

0
0
 Mwanafunzi Ali Askher Walji akifurahia zawadi kutoka kwa Mgeni Rasmi, Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile baada ya kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa ya Daraja la 7 ya mwaka 2016.
 Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile, akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Wavulana ya Almuntazir waliofanya katika Mitihani ya Taifa ya Daraja la 7 ya mwaka 2016.
Dokta Faraji Lydenge kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Wavulana ya Almuntazir waliofanya katika mitihani ya Taifa ya daraja la 4 ya mwaka 2016.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Shule ya Msingi ya Wavulana ya Almuntazir Bw. Mahmood Ladak akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Wavulana ya Almuntazir waliofanya katika Mitihani ya Taifa ya Daraja la 3 ya mwaka 2016.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MPINA AKITOZA FAINI YA SHILINGI MILIONI 25 KIWANDA CHA CHEMICOTEX CHA MBEZI JOGOO JIJINI DAR ES SALAAM KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA

0
0
NA EVELYN MKOKOI – DAR ES SALAAM


Kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amekitoza faini ya shilingi Milioni 25, kiwanda kinachotengeneza biadhaa mbali mbali za matumizi ya manyumbani kama vile mafuta ya kujipaka mwili na dawa za meno cha chemicotex, mkilichopo Mbeji Jogoo jijini Dar es Salaam Kwa uchafuzi wa mazingira.

Faini hiyo inayotakiwa kulipwa baada ya wiki mbili inatokana na ukiukwaji mkubwa wa sheria ya mazingira unaofanywa na kiwanda hicho kilichopo katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi, ya kutiririsha maji taka na maji machafu katika mfereji wa maji ya mvua.

Naibu Waziri Mpina ameshangazwa na uthubutu wa uchafuzi wa mazingira unaofanywa na kiwanda hicho, pamoja na jitihada za serikali kupitia Ofisi yake na NEMC za kuthibiti uharibifu wa mazingira kwa kutoa adhabu mbali mbali kwa waharibifu.

“Ujio wangu katika kiwanda hiki unatokana na malalamiko ya wananchi ya kututiririshiwa maji machafu katika makazi yao na maeneo ya biashara, hakuna atakaesalimika kwa kosa la kutokutunza mazingira na afya za watu, alisistiza Mpina”.

“Mpo Barabarani mnachafua mazingira Hadharani bila haibu, mmedharau jitihada za serikali hii ya awamu ya tano na kuona kama ni nguvu za soda, adhabu hii ilipwe kama ilivyo elekezwa hatuta kuwa na uvumilivu kwa muwekezaji yeyote atakaechafua mazingira. Alisema”.

Kwa Upande wake Mwanasheria kutoka NEMC Bw. Heche Mananche aliongeza kwa kusema kuwa Mmiliki wa kiwanda endapo hatakuwa tayari kulipa faini hiyo anaweza kupelekwa mahakamani.

Wakati Huo Huo, Naibu Waziri Mpina Amezindua Mfereji wa kutirirsha maji katika kiwanda cha Cement cha wazo, baada ya kujiridhirisha na utekelezaji wa maagizo yake kiwandani hapo katika moja ya ziara zake mwaka jana, ambapo ilibainika kuwa kiwanda hicho kimekuwa ni kero kwa wananchi majirani kwa kutiririsha maji na kusababisha mafuriko hasa katika kipindi cha mvua.

Kwa upande wake mkazi wa eneo la wazo bwana David kahaga aliupengeza uongozi wa kiwanda hicho kwa ujenzi wa mtaro huo na kusema kuwa umetatua changamoto katika shule ya msingi jirani na kiwanda hicho ambayo ilikuwa ikikumbwa na mafuriko mara kwa mara hasa katika kipindi cha mvua, lakini bado wakazi hao wana hofu na usalama wao baada ya ujenzi wa mtaro huo na kuwa bado wanakabiliana na changamoto kubwa ya vumbi itokanayo na uchimbaji wa malighafi za uzalishaji katika kiwanda hicho.
Naibu Waziri Mpina akitolea Msisitizo adhabu ya uchafuzi wa mazingira aliyoitoa katika kiwanda cha Chemicotex Jijini Dar esSalaam alipofanya ziara ya kushtukiza leo.
Kulia Bwana Navneft Meneja katika Kiwanda cha Chemicotex, akieleza jambo kwa wajumbe wa msafara wa Naibu Waziri Mpina katika ziara ya kushtukiza kiwandani hapo leo.
Pichani Sehemu ya Uchafuzi wa mazingira unaofanywa na kiwanda cha Chemicotex cha jijini Dar es Salaam, kilichopo katika barabara ya Alai Hassan Mwinyi jijini.
Sehemu ya Mtaro Ulijengwa na kiwanda cha Wazo ikiwa ni katika kutekeleza agizo la Naibu waziri mpina katika iara yake aliyoifanya awali maka jana kiwandani hapo kupitia malamimiko ya wananchi.


SOPHIA MJEMA AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA KUGAGUA VIPIMO NA MIZANI FEKI ILALA LEO

0
0

Mkuu wa wilaya ya Ilala, kwa kushirikiana na Wakala wa vipimo Tanzania (WMA), mkoa wa Ilala, amefanya ziara ya kustukiza katika maeneo mbalimbali, katika kampeni yake ya kudhibiti vipimo na mizani 'feki'. Pichani, Mjema akikagua mzani kwenye bucha moja eneo la Kariakoo, Dar es Salaam, akiwa katika ziara hiyo, Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo na kulia ni mfanyakazi katika bucha hiyo, Omar Khalfan.

Kaimu Meneja wa WMA mkoa wa Ilala, Alban Kihulla, akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kulia), jinsi ya kutofauisha mizani 'feki' na ile iliyo bora, kabla ya kuendelea na ziara nje ya ofisi hiyo
Mjema akionyeshwamizani malimbali feki na iliyo bora, katika karakana ya WMA mkoa wa Ilala

Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza na wapokea mizigo hasa ya viazi mviringo, katika mitaa ya Kariakoo, Dar es Salaam, kuhusu umuhimu wa akuepuka kupokea magunia yaliyojazwa kwa mtindo wa Lumbesa, kwa kuwa utaratibu huo unakiuka vipimo halisi na hivyo kutia serikali hasara kwa kuwa siyo kipimo halali

WAZIRI UMMY MWALIMU ATOA TAMKO KUHUSU KADI YA MANJANO

Waziri Ummy afuta Vituo vya kutolea huduma za vvu Drop in centre

KATIBU MKUU RWEGASIRA: UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA MSUMBIJI BADO UPO IMARA, AWATAKA WATANZANA KUFUATA SHERIA ZA UHAMIAJI NCHI WANAZOISHI

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Watanzania wanaorudishwa nchini kutoka Msumbiji. Rwegasira amesema Uhusiano kati ya Tanzania na Msumbiji unaendelea kuimarika kila siku, hivyo aliwataka Watanzania wafuate Sheria za Uhamiaji za nchi hiyo kwani zoezi linalofanyika nchini humo halijawalenga Watanzania pekee bali raia wote wanaoishi na kufanya kazi bila kufuata taratibu za kisheria nchini humo. Aidha, amewataka wananchi kutolikuza tukio hilo bila sababu za msingi. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMIS 16.02.2017

Viewing all 109587 articles
Browse latest View live




Latest Images