Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1570 | 1571 | (Page 1572) | 1573 | 1574 | .... | 3283 | newer

  0 0
  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa michezo wa Kiteto akiwa katika ziara ya mkoa wa Manyara, Februari 15, 2017. 
  Wananchi wa Kiteto wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa michezo wa Kiteto Februari 15, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka Mzee Mbambire Oloi Kurukur, jani la mti ikiwa ni ishara ya amani ya kukomesha mapigano kati ya wakulima na wafugaji wilayani Kiteto kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa michezo wa Kiteto, Februari 15, 2017.. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Katibu wa Baraza la Amani la Kiteto, Salum Mambo, jembe la asili ikiwa ni ishara ya kukoma kwa mauaji kati ya wakulima na wafugaji wilayani Kiteto katika mkutano wa hadhara aliouhutubi kweye uwanja wa michezo wa Kiteto, Februari 15, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia mikono wananchi katika mkutano wa hadhara aliouhutubi kweye uwanja wa michezo wa Kiteto, Februari 15, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  0 0

  Baada ya serikali kusitisha agizo la Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) lililokataza TV za mitandaoni zisiendelee kutoa huduma, Michuzi TV imerudi hewani kwa kishindo huku ikiwaahidi wadau wote kwamba mambo sasa yatakuwa motomoto kuliko ilivyokuwa awali. 
  Serikali imesitisha agizo hilo la TCRA baada ya kuonekana halina mantiki kwa vile kanuni za namna ya kuendesha huduma hii hazipo tayari na kuzuia ni kutowatendea haki wananchi wanaofurahia huduma hii bila malipo. Michuzi TV itaendelea kupiga mzigo huku ikisubiri na hatimaye kutii kanuni zozote zitazowekwa.

  0 0  0 0

  Mgeni rasmi akiwa waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage wa tatu kushoto,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanga cha utengenezaji wa viungo,Vegata Podravka Ltd,kilichojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 16,Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Bagamoyo,Mh.Shukuru Kawambwa na kulia ni Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croati,Bi.Olivia Jakupec.
    Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croatia ,ambayo ni kampuni mama ya Vegeta Tanzania,Bi.Olivia Jakupec akimkabidhi Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage cheti cha heshima ya ushiriki wake mkubwa katika uzinduzi wa kiwanda hicho.Pichani kati ni  Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Vegeta Podravka Ltd-Tanzania,Davor Svar.
    waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijagea akipata maelekezo mbalimbali kuhusiana na baadhi ya bidhaa ambazo ziko tayari kutoka kwa Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croati,Bi.Olivia Jakupec.
    Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijagea  akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho wilayani Bagamoyo,Pwani.Waziri Mwijage alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano imeamua kujenga Uchumi wa Viwanda,ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya Watu.

  "Tanzania sasa tunajenga  viwanda na si Tanzania ya viwanda inawezekana,hiyo ilikuwa kauli mbiu ya zamani,kwa hiyo sasa tunajenga viwanda,mwenye macho haambiwi Tazama"alifafanua Waziri Mwijage.Waziri Mwijage amewashuruku wawekezaji hao kwa kuamua kuja kuwekeza nchini Tanzania,ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais wa awamu ya tano ,Dkt John Pombe Magufuli katika kuhakikisha Uchumi wa Viwanda unakwenda kwa kasi na kufanikiwa.
  Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croatia ,ambayo ni kampuni mama ya Vegeta Tanzania,Bi.Olivia Jakupec akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho cha utengenezaji wa viungo mbalimbali,mjini Bagamoyo mkoani mkoani Pwani.

  Olivia alisema kuwa wao kama wawekezaji wametembea nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Uganda,Kenya,Burundi,Zambia,Rwanda,Sudani Congo,Afrika Kusini na nyinginezo,lakini wakabaini Tanzania ndio mahali sahihi kwa uwekezaji."Hivyo tukafanya utafiti,tukabaini eneo la Bagamoyo linafaa kujengwa kiwanda cha aina hiyo,hivyo tukaamua kujenga kiwanda ndani ya mwaka mmoja na nusu,ambacho kimetumia kiasi cha shilingi bilioni 16 mpaka kukamilika.

  "Tunaishukuru Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Waziri wa Viwanda Mh.Charles Mwijage,Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na wengineo kwa ujumla, kwa kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji,kiasi kwamba hata nasi tukaiona furasa hiyo na tukachukua hatua ya kuwekeza kiwanda hiki hapa nchini",alisema Olivia. 
   Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Vegeta Podravka Ltd,Bw-Tanzania,.Davor Svar akizungumza kwa ufupi wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho cha viungo mbalimbali,jana mjini Bagamoyo,huku mgeni rasmi akiwa waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage.

  Davor alisema kuwa wameamua kuwekeza nchini Tanzania kwa sababu imeonekana ni kiungo muhimu katika mambo ya uwekezaji hasa kutokana na eneo lake, miundo mbinu yake,ukuaji wake wa kiuchumi na pia kuwa kiungo muhimu kwa kuwa mwanachama hai wa nchi za Afrika Mashariki na Kati,kufuatia vigezo hivyo,hurahisisha mambo ya kibiashara kufanyika kwa urahisi zaidi.

  Davor alisema kuwa kufuatia kuanzishwa kwa kiwanda hicho,kimefanikiwa kutoa ajira za kazi zaidi ya 200 katika Wilaya ya Bagamoyo ikiwemo kazi ya uuzaji na usambaji wa bidhaa za kiwanda hicho.
   Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa kiwanda cha Viungo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.PICHA NA MICHUZI JR.
  0 0

  13 Ministers from Eastern Africa, Unesco and the SDG4 co- conveners (ILO, UNFPA, UNDP, UNICEF, UN Women, UNHCR and World Bank) are in Dar es salaam to identify priorities and policy recommendations for a regional roadmap for the implementation of the SDG4- Education 2030 agenda and linkages with other SDGs;

  In two days meeting opened yesterday at Julius Nyerere International Convention Centre (JINCC) various people made different remarks on how to ensure inclusive and equitable quality education and promote lifelong learning opportunities for all.

  Opening the floor to welcome all participants including ministers from Comoros, Djibout, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Mauritius, Rwanda, Seychelles, Somalia, South Sudan, Tanzania and Uganda, Swedish Ambassador to Tanzania  H.E Katarina Rangnitt spoke about Young people being given proper education with relevant skills to make them competent.

  She talked about unlocking the potential of the people by keeping children in school and managing drop out with full knowledge that education is the tool to reach development goals.

  “With the growing frustrations among the youth on lack of employment, climate change and disasters she asked participants to come out with practical solutions making sure that nobody is being left behind with a keen attention to kids with disabilities.” She said.
  The Minister for Education, Science, Technology and Vocational Training Prof Joyce Ndalichako delivering key note address to officiate Ministerial SDG4 Regional Forum for Eastern African in Dar es Salaam.
  Chair of the Ministerial SDG4 Regional Forum for Eastern African in Dar es Salaam and Head Office and country Representative of UNESCO, Zulmira Rodrigues welcomes invited guests, dignitaries and key speakers during Ministerial SDG4 Regional Forum for Eastern African in Dar es Salaam.(All photos by Zainul Mzige
  Unesco Regional Office for Eastern Africa, Director Mrs Ann Therese Ndong-Jatta addressing Ministerial SDG4 Regional Forum for Eastern African in Dar es Salaam.
  Linda Madete from UNESCO Office Dar es Salaam gives out some of the education materials and brochures to invited guests during the Ministerial Sustainable Development Goals numbers 4 that focuses on ensuring inclusive and equitable quality education and promote lifelong learning opportunities for all at the Regional Forum for Eastern African in Dar es Salaam.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  Na  Bashir  Yakub.

  Sheria  inayoshughulikia   habari  nzima  ya  madawa  ya  kulevya  inaitwa “The  Drug  Control  And  Enforcement  Act”.  Ni  sheria  namba  5  ya  mwaka  2015.  Ni  sheria  mpya  kabisa. Msanii  Wema  Sepetu  ni  kati  ya  Watu  walioko  mahakamani  tayari  kuamuliwa  kwa  mujibu  wa  sheria  hii.


  1.AINA  YA  DAWA  ZA  KULEVYA.

  Sheria  hii  inataja  aina  nyingi  mno  ya  vitu  ambavyo  imeviita  dawa  za  kulevya. Vipo  jamii  ya  kimiminika,  jamii  ya  unga,  jamii  ya  miti,  majani, mbegu  n.k.

  Kifungu  cha  2   cha  sheria  hiyo  kinachosomwa  sambamba  na Schedule  ya 1  ya  sheria  hiyohiyo  kimeorodhesha  zaidi   ya  sampuli  100  ya  vitu  ambavyo  vinahesabika  kuwa   ni  dawa  za  kulevya hapa  Tanzania. Humo  imo  pia  bangi,  mirungi, cocaine, heroine na  aina  nyingine  nyingi.  Katika  hizi  Msanii  Wema  anatuhumiwa  kukutwa  na  misokoto  ya  bangi.


  2.   JE  ILIKUWA  SAWA  WEMA  KUPEWA  DHAMANA  ?.

  Ndio  ilikuwa  sawa.  Wako  watu  wanasema  kuna  mtu  amemkingia  kifua  akapata  dhamana. Hili si  kweli .  Dhamana  katika   kesi  za  madawa  ya  kulevya  hunyimwa  kutokana  na  kiwango  ulichokutwa au  unachotuhumiwa  nacho.   Kifungu  cha  29  cha  Sheria  hiyo  ya  kupambana  na  dawa  za  kulevya  kimeeleza  hilo  kama  ifuatavyo;.


  ( a ) Kama  ni  cocaine, heroine, mandrax, morphine, cannabis  resin au  opium   kuanzia gramu  200  au  zaidi  hakuna  dhamana.  Ni  pote  polisi  na  mahakamani.

  ( b ) Kama  ni  dawa  aina  ya  majani  au  mimea  kama  bangi n.k  kuanzia  kilo  100  au  zaidi  hakuna  dhamana. Ni  pote  polisi na  mahakamani.

  ( c ) Kama  ni  dawa  zenye  mfumo  wa  kemikali  kuanzia  lita  30 au  zaidi au  kilo  100  ikiwa  zimewekwa  katika  mfumo  wa  unga au  vinginevyo  hakuna  dhamana.  Ni  pote  polisi na  mahakamani.

  Wema  Sepetu  alikutwa  na kiwango  kidogo kwa  taarifa  zilizotolewa,  ni  kama  msokoto  mmoja  hivi.  Ukiangalia  hapa  juu  hakuna  popote  ambapo kiwango  hicho  kimetajwa  kuwa hakidhaminiki.  Kwa  hiyo  kosa  lake  lilikuwa  la  kudhaminika  kabisa  kwa  mujibu  wa  kifungu  hiki.


  3.   JE   WEMA  ANAKABILIWA  NA  ADHABU  ZIPI ?.


  Kifungu  cha  17 ( 1 )  cha  Sheria  ya  Kuzuia  na  Kupambana  na  dawa  za  kulevya   kinaeleza  adhabu  ya  miaka  mitatu  jela, au  faini  isiyopungua  laki  tano   au  vyote  viwili.

  Kwahiyo  panapo  kupatikana  na  hatia   atatakiwa  kwenda  jela  miaka  mitatu,  au  asiende  jela  iamuliwe  alipe  faini  inayoanzia  laki  tano  za  Tanzania,  au   aende  jela  miaka  mitatu  na  hapohapo  alipe na  faini  inayoanzia  shilingi  laki  tano  kwenda  mbele.


  KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com.
  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kwenye Ikulu ndogo ya Orkesimet akiwa katika ziara ya Mkoa wa Manyara, Februari 16, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya wilaya ya Simanjiro kutoka kwa Mkuu wa wilaya hiyo, Mhandisi Zephania Chaula baada ya kusomewa taarifa hiyo kwenye Ikulu ndogo ya Orkesimet akiwa katika ziara ya Mkoa wa Manyara, Februari 16, 2017.
  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mhandisi Zephania Chaula akisoma taarifa ya wilaya hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye Ikulu ndogo ya Orkesimet Februari 16, 2017
  Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Ikulu ndogo ya Orkesimet akiwa katika ziara ya Mkoa wa Manyara , Febuari 16, 2017.


  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0  Shule ya msingi Sinde iliyopo mtaa wa kagwina katika kata ya Sinde Jijini Mbeya imefungwa ghafla kutokana na Choo cha wanafunzi zaidi ya 1,600 kutitia na kubomoka hali iliyopelekea wanafunzi kukosa huduma ya choo shuleni hapo.  Mkuu wa Shule ya Msingi Sinde Mwl. Angomwile Mwanansyobe amesema kuwa Kutokana na janga hilo Jiji pamoja na Uongozi wa Shule uliamua kuifunga shule kwa kipindi cha majuma matatu ili kupisha Ujenzi wa vyoo hivyo na madarasa ya mitihani tu yaani Darasa la nne na darasa la saba ndio pekee wataendelea kusoma hapo shuleni kwa kutumia vyoo vya shule jirani ambazo zinapakana kwa ukaribu zaidi.

  Mwl Mwanansyobe amesema,....."Kama Uongozi wa shule tunajua ni kwa jinsi gani taaluma kwa wanafunzi waliopo majumbani hivyo sisi kama walimu tutaitumia likizo fupi ya mwezi machi kuendelea na vipindi. 
   Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sinde, Angomwile Mwansyobe akizungumzia kuhusu kufungwa kwa Shule na changamoto zilizowakumbuka
   Kina Mama ni jeshi kubwa, Hivi ndivyo inavyoonekana pichani huku wanafunzi kadhaa wakishuhudia wazazi wao wakichapa kazi kwa kujitolea
  PICHA NA MR.PENGO
  MAELEZO NA TOBIAS OMEGA

  0 0

  *Asisitiza amani kwanza, masuala mengine baadaye

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitakubali kuona watu wachache wanachochea vurugu na kusababisha watu wengine wapoteze maisha ilhali wao hawadhuriki.

  Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumatano, Februari 15, 2017) wakati akizungumza na maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa michezo wa mjini Kibaya, wilayani Kiteto, mkoani Manyara.

  Waziri Mkuu ambaye alikuwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku sita mkoani Manyara, alisema: “Hatutakubaliana na wachochezi. Hatutakubaliana na yeyote atakayesababisha kifo. Tukibaini kuna uchochezi, tutawasaka wahusika na kuwashughulikia,” alisema.

  “Hapa kulikuwa na majina ya ajabuajabu, hatutakubali Kiteto iitwe Soweto au Kossovo, hapa ni Tanzania. Hatuwezi kuishi kwa kubaguana, ni lazima tuheshimu maamuzi ya wazee wetu wa kimila ambao wamesimamia zoezi hili ili kurejesha amani ya Kiteto,” alisema.
  Alisema zamani Kiteto kulikuwa hakuna lugha ya amani lakini hali kwa sasa imebadilika na kuwa nzuri na akasisitiza kwamba hakuna kurudi nyuma.

  Alisema anamshukuru Waziri Mkuu mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda kuwa kufuatilia suala hilo na kuunda tume ya kutafuta amani wilayani Kiteto. “Nilipoingia madarakani, nami nilianza kufuatilia suala hilo ili nijue chanzo hasa ni nini. Nikabaini kuwa mgogoro mzima umechangiwa na chokochoko tu za watu wachache,” alisema.

  Mapema, viongozi wa kimila walimkabidhi Waziri Mkuu rungu, jembe dogo na jani la mti wa asili (Kimasai unaitwa elisibie) ikiwa ni ishara amani ya kukomesha mapigano baina ya wafugaji na wakulima. Pia alishiriki dua ya kuombea amani ambayo iliongozwa na viongozi wa dini.


  0 0

  Mwanasheria wa mmiliki wa Mtandao wa Jamii Forum, Jebra Kambore na mteja wake, Maxence Melo wakitoka mahakamani Mara baada ya kesi yake ya kuendesha mtandao ambao haujasajiliwa nchini "Domain" kuahirishwa hadi Machi 3, mwaka huu.

  0 0

  Na Greyson Mwase, Arusha

  Imeelezwa kuwa vyanzo vya nishati jadidifu kama vile upepo, jua, jotoardhi vitachangia upatikanaji wa nishati ya uhakika ya umeme kwa kila  kijiji ifikapo mwaka 2030 kama mpango wa nishati kwa wote unavyofafanua.  Hayo yameelezwa na Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila katika mafunzo  kwa  wadau wa nishati jadidifu kuhusu matumizi ya mfumo mpya  wa uhifadhi data  na utoaji taarifa kwa ajili ya  nishati jadidifu ujulikanao kama Tanzania Renewable  Energy  Management Information System (TREMIS) yaliyofanyika jijini Arusha leo.  Mhandisi Rwebangila alisema kuwa ili nchi ya Tanzania kuingia kwenye orodha ya nchi za kipato cha kati ifikapo mwaka 2025, nishati ya uhakika ya umeme inahitajika hususan katika kuchochea uwekezaji katika viwanda na kukuza uchumi wa nchi.  Alisema mbali na gesi iliyogunduliwa katika mkoa wa Mtwara na maeneo mengine, nishati ya umeme kutokana na vyanzo vingine kama vile upepo, jua, joto ardhi vinahitajika ili kuongeza kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa.  “ Kuna maeneo ambayo hayajafikiwa na miradi mikubwa ya  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme  Tanzania (TANESCO) kama visiwani, ambapo Wizara ya Nishati na Madini imeweka utaratibu wa kutumia vyanzo vya nishati mbadala kama jua, upepo na jotoardhi kulingana na maeneo husika ili kila mwananchi afikiwe na huduma ya umme,” alifafanua Mhandisi Rwebangila.  Aliendelea kusema kuwa ili kuvutia fursa za uwekezaji, Wizara imeanzisha mfumo mpya wa uhifadhi data  na utoaji taarifa kwa ajili ya  nishati jadidifu ujulikanao kama Tanzania Renewable  Energy  Management Information System (TREMIS) utakaowezesha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kupata taarifa kuhusu fursa za uwekezaji katika nishati jadidifu, sera na taratibu.  Alisema kuwa taarifa za kampuni zote zinazojihusisha na nishati jadidifu, fursa za uwekezaji, sera, sheria na taratibu zitawekwa katika mfumo huo utakaounganishwa na tovuti ya Wizara ili wadau kupata uelewa kabla ya kuwekeza.  Aliendelea kusema kuwa  hatua iliyofikiwa kwa sasa katika maandalizi ya mfumo huo, ni utoaji wa mafunzo na ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa nishati mbadala nchini ambapo mpaka sasa wamekwishafanya zoezi hilo katika Kanda ya Ziwa.

  Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi, Styden Rwebangila (kulia) akibadilishana mawazo na Mtaalam kutoka Kitengo cha Teknolojia ya  Habari na Mawasiliano (TEHAMA)- Wizara ya Nishati na Madini, Danford Phiri (kushoto) katika mafunzo yaliyokutanisha wadau wa nishati jadidifu jijini Arusha Februari 16, 2017
  Wadau wa nishati jadidifu  wakiendelea na majadiliano katika mafunzo hayo

  0 0

  Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula  Dunini (WFP) limepokea mchango wa Euro (€) milioni 9.5 kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kwa lengo la kuunga mkono Mradi wenye thamani ya Euro milioni 24.5 (takribani Shilingi za Tanzania bilioni 50) wa kusaidia kukuza Usalama wa Chakula na Lishe katika mikoa ya kati nchini Tanzania.

  Mradi umeandaliwa ili kuimarisha usalama wa chakula na lishe kwa watu wapatao 40,000  na wakati huohuo ukichangia katika kupunguza utapiamlo katika wilaya zinazolengwa za Bahi na Chamwino mkoani Dodoma na Ikungi na Singida Vijijini katika mkoa wa Singida. 

  Mchango wa EU umetangazwa leo wakati wa hafla ya kutiliana saini makubaliano katika Jengo la Umoja jijini Dar es Salaam uliofanywa na Dr. Mpoki Ulisubisya, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Michael Dunford, Mwakilishi wa WFP nchini Tanzania na Roeland Van De Geer, Mkuu wa Ubalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania.

  “Licha ya kuimarika kwa viashiria vingi vya afya katika muongo uliopita, bado hakuna hatua kubwa katika kuimarisha hali ya lishe ya watoto na wanawake nchini Tanzania,” Roeland Van De Geer, Mkuu wa Ubalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, alisema wakati wa hafla hiyo".

  “Viwango vya juu vya kudumaa, kukosa uzito wa kuridhisha na upungufu wa viinilishe nchini kunaashiria dharura ya kimyakimya. Utayari wa kisiasa katika safu ya viongozi wa juu katika kukabili lishe duni nchini Tanzania kwa mtazamo wa sekta nyingi kwa hakika ni mageuzi makubwa. Kupitia mradi huu, EU pamoja na WFP ziko katika nafasi nzuri ya kubaini na kuunga mkono uhusiano kati ya kilimo, afya, usalama wa chakula na lishe, ambao hapo kabla haukuwa umeelezwa kwa kina au kufuatiliwa kikamilifu.”

  Mradi huu unatumia uwepo wa muda mrefu wa WFP katika mikoa ya kati nchini Tanzania na uzoefu wake katika kutoa chakula chenye lishe na mawasiliano yenye lengo la kubadilisha tabia ya kijamii kupitia vituo vya afya. Shughuli hizi zitakamilishwa na jitihada katika sekta nyingine ili kutoa mtazamo ulio kamili zaidi wa kupunguza kudumaa nchini. Viwango vya Taifa vya kudumaa viko katika asilimia 34 ambapo kwa Dodoma ni asilimia 36.5 na Singida ni asilimia 29.2

  “Tunashukuru kwa mchango huu kutoka Umoja wa Ulaya kwani umeiwezesha WFP kuendelea na programu hii bunifu inayolenga kukidhi mahitaji ya watu walio hatarini zaidi, hasa watoto katika kile kipindi muhimu sana cha ukuaji wao, yaani siku 1,000 za mwanzo tangu kubebwa mimba hadi kutimiza miaka miwili,” Mwakilishi wa WFP Michael Dunford alisema katika hafla hiyo. “Programu hii itatoa ushahidi ambao utatoa mwongozo kwa jitihada za baadaye, na kwa hiyo ina uwezekano wa kuleta mabadiliko ya kudumu nchini Tanzania.”

  Nchini Tanzania, viwango vya utapiamlo sugu miongoni mwa watoto unatokana na umaskini, ukosefu wa usalama wa chakula na ukosefu wa chakula cha kutosha kwa watoto wachanga na unyonyeshaji watoto. Mradi utalenga kukuza maarifa kuhusu lishe, mtawanyiko wa lishe na taratibu za kutumia maji, usafi wa mazingira na usafi wa mwili (WASH). Shughuli hizi zitapewa nguvu kwa kuhamasisha ufugaji wa idadi inayofaa ya mifugo, kupanda mazao tofautitofauti na kuhamasisha vijiji kuanzisha vikundi vya kuweka akiba na kukopa, yote yakilenga kukuza uwezekano wa kupata mtaji.

  Shirika la Save the Children ni mshirika wa WFP katika kuimarisha ushirikiano na uwezo wa asasi zilizojikita katika jamii ili kuhamasisha uwezeshaji wa jinsia na uhusiano wa sekta mbalimbali katika suala la lishe, pamoja na kuratibu utekelezaji wa kipengele cha kilimo katika mradi.

  Kwa kuratibu shughuli hizi chini ya mwamvuli wa WFP, Umoja wa Ulaya na Shirika la Save the Children zitakuwa zikishughulikia changamoto nyingi zinazolenga kuimarisha usalama wa chakula na lishe nchini Tanzania.

  Mradi huu ni sehemu ya majukumu ya WFP katika kufanikisha Lengo la 2 katika Malengo ya Maendeleo Endelevu: Kufuta Njaa. Ili Kuondoa Njaa kabisa ifikapo mwaka 2030, WFP inashirikiana na washirika mbalimbali kama vile serikali, sekta binafsi na vyama vya kiraia.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  UONGOZI wa Klabu ya Yanga umetangaza viingilio vya mechi yao marudiano dhidi ya Ngaya unaotarajiwa kufanyika wikiendi hii.

  Akizungumnzia viingilio hivyo, Afisa Masoko wa klabu hiyo, Omar Kaaya amesema kiingilio cha chini kitakuwa ni shiilingi 3000 kwa majukwaa ya mzunguko na viti vya machungwa,  VIP A  ni Tsh  20,000, VIP  B  ni Tsh  10,000 na VIP  C itakuwa Tsh  10,000.

  Kaaya amewataka mashabiki wa Yanga kuja kwa wingi uwanjani ili kuishan gilia timu yao na zaidi amani inatakiwa itawale kwenye mchezo huo ambao ni muhimu sana kwao.

  Kwa upande wa Benchi la Ufundi wa Yanga, Kocha msaidizi wa Juma Mwambusi amesema kuwa katika mchezo huu hawatabweteka na ushindi walioupata mwazoni zaidi wanataka kuona wanapata ushindi mwingine.

  Mwambusi amesema, hawatabweteka na ushindi uliopita kwani ni hazina tosha ila kila kitu inakuja na mbinu yake kwahiyo lazima tucheze kwa umakini mkubwa sana na kuweza kutokuruhusu goli.

  "Tunajivunia ushindi mnono tulioupata ugenini kwani ni hazina tosha kwetu lakini tunatambua umuimu wa mchezo wetu wa marejeano ambao utafanyika siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Taifa,kikubwa nawaomba mashabiki wetu na wanamichezo wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao." amesema Mwambusi.

  Kuelekea mchezo huo wachezaji watakaokosekana kwa sababu ya kuwa majeruhi ni Donald Ngoma,Amisi Tambwe na Haruna Niyonzima.
                     
  Tayari Ngaya wamewasili asubuhi ya leo kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga ambao kwenye mechi iliyofanyika nchini Comoro Yanga walifanikiwa kutoka na ushindi wa goli 5-1.

   Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi (kushoto) akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wao wa marudiano na timu ya Ngaya utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, katika mechi ya kwanza Yanga walifanikiwa kutoka na ushindi wa goli 5-1 nchini Comoro.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Simanjiro, James Ole Milya kwenye Ikulu Ndogo ya Orkesimet wilayani Simanjiro Februari 16, 2017. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia kwaya ya Wamasai wa Simanjiro wakati alipowasili kwenye uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjairo mjini Orkesimet Februari 16, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa zana za asili za kabila la wamasai wakati aliposimikwa kuwa Mzee wa Simanjiro na kupewa jina la Ole Majaliwa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro mji Orkesimet Februari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro mjini Orkesimet Februari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

  Sehemu ya watumishi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika mazoezi ya kunyoosha viungo siku ya uzinduzi wa zoezi la ufanyaji mazoezi ya viungo yalizinduliwa mwishoni mwa juma katika ufukwe wa Bahari ya Hindi.
  Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga (wa pili kushoto) akiwa pamoja na watumishi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika uzinduzi wa mazoezi ya viungo katika ufukwe wa Bahari ya Hindi jijini Dar es salaam. 

  Baadhi ya watumishi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika mazoezi ya kunyoosha viungo siku ya uzinduzi wa zoezi la ufanyaji mazoezi ya viungo kwa Jeshi hilo. 

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Video Queen Agnes Masogange anayeshikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya Dawa za Kulevya.

  0 0

   Mfanyabiashara Maarufu na Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga SC, Yussuf Manji akifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mchana huu.

   Katibu mkuu wa Yangu, Boniface Mkwasa akiwa katika Mahakama ya Kisutu.
  Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yangu Clement Sanga akiteta jambo na mmoja wa Mawakili wanaomtetea Yussuf Manji, Alex Mgongolwa 

older | 1 | .... | 1570 | 1571 | (Page 1572) | 1573 | 1574 | .... | 3283 | newer