Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

MAMA MAGUFULI, MAMA MAJALIWA WATEMBELEA GEREZA LA MAHABUSU MKOANI TABORA


TAKUKURU YAWABURUZA MAHAKAMANI WATUMISHI WA WIZARA YA ELIMU MANISPAA YA ILALA

$
0
0

Na Karama Kenyunko

Watumishi wanne wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi akiwemo Mkurugenzi na Mhasibu wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka saba ya kiwemo ya ubadhilifu na ufujaji wa fedha na kuisababishia wizara hasara ya zaidi ya bilioni 41.

Akisoma hati ya mashtaka, Mwendesha Mashtaka, wakili wa serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB), Emmanuel Jacob aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Mkurugenzi Bakari Issa, Mhasibu Emmanuel Mayuma, Mkurugenzi Msaidizi Hellen Lihawa na Mhasibu Msaidizi Mbarouk Dachi.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri ilidaiwa kuwa washtakiwa hao kwa makusudi na kwa nia ya kudanganya walitumia malipo ya tarehe 16 Julai 2014 kwa jina la Emanuel Mayuma ambayo ilikuwa na taarifa ya uongo kuonyesha kuwa zaidi ya sh. Milioni 18.4 zilikuwa ni malipo kwa ajili wanafunzi waliohudhuria mafunzo ya michezo yaliyokuwa yamedhaminiwa na British Council huku wakijua siyo kweli.

Aidha watumishi hao wanadaiwa kufanya ubadhirifu na ufujaji wa fedha kati ya Agosti 30 na Septemba 10 mwaka 2014 na kujipatia kiasi hicho cha milioni 18 ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya mpango wa walimu kwa mafunzo ya kadi za michezo zilizofadhiliwa na British Council.

Mhasibu Mayuma anadaiwa peke yake kuwa, kati ya Agosti 10 na Septemba 2014 wizarani hapo alitumia vibaya kiasi cha shilingi milioni 31.7 alizokuwa amekabidhiwa kwa ajili ya kugaramia mpango wa matumizi ya kadi za michezo.

Katika hatua nyingine watuhumiwa hao wote wanadaiwa kushindwa kutumia madaraka yao vibaya na kuisababisha wizara ya Elimu hasara zaidi ya shilingi milioni 18.4/- wakati Mhasibu Mayuma aliisababishia wizara hiyo hasara ya shilingi milioni 41.2.

Hata hivyo washtakiwa wamekana mashtaka na wako nje baada ya kuweka dhamana ya shilingi milioni 50 kila mmoja na kuleta wadhamini wawili wa uhakika. Aidha washtakiwa hao hawaruhusiwi kusafiri nje ya Dar es Salaam bila kupata kibali cha mahakama.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 1, upelelezi bado haujakamilika.



Watuhumiwa wa ubadhilifu wa fedha wakifikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi kisutu jijini Dar es Salaam
 

Serikali yapokea mrejesho wa mradi wa afya ya uzazi wa Thamini Uhai

$
0
0
Leo jijini Dar-es-Salaam, Thamini Uhai imetoa mrejesho wa shughuli zake tokea kuanzishwa kwake na kuwasilisha mipango yake kwa mwaka 2017 kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Thamini Uhai (iliyoitwa World Lung Foundation hapo awali), imefanya kazi kwa karibu na wahisani pamoja na serikali za mikoa, kujenga mfumo ambao umepelekea ugatuzi wa huduma za dharura za kuokoa maisha ya mama na watoto wachanga kutoka hospitali kwenda kwenye vituo vya afya. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto - Mh Ummy Mwalimu (katikati) na Dr Hussein Kidanto - kaimu mkurugenzi wa idara ya huduma za kinga Wizara ya Afya (kushoto) wakishauriana na Mkurugenzi mtendaji wa Thamini Uhai, Dr Nguke Mwakatundu (Kulia) wakati wa mkutano wa mrejesho wa shirika la Thamini Uhai, leo jijini Dar-es-Salaam.

Mfumo huu wa kipekee wa huduma ya afya umehusisha pia kuboresha vituo vya huduma za afya ili viweze kutoa huduma hizi za dharura, kuendeleza mafunzo ya jamii kupitia vyombo vya habari na waelimishaji jamii ili kuhamasisha jamii itumie vituo vya huduma za afya, kuboresha mifumo ya rufaa, kuhakikisha upatikanaji wa ushauri wa afya kila wakati. Pia shirika imetoa mafunzo, usimamizi na elimu endelevu kwa wahudumu wa afya, waganga wasaidizi (AMO) na manesi ambapo elimu hiyo inatolewa na madaktari bingwa ili kugatua huduma na ujuzi na hivyo kuongeza uwezo katika jamii zilizopo pemebezoni.

Akizungumzia mafanikio yao, Dr. Nguke Mwakatundu, Mkurugenzi Mtendaji wa Thamini Uhai, amesema:
Wadau kutoka shirika la Thamini Uhai, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Rais - Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa wakimsikiliza kwa makini Waziri Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa mrejesho wa shirika la Thamini Uhai, leo jijini Dar-es-Salaam.

“Moja ya mafanikio yetu muhimu ni jinsi shughuli zetu zimeweza kuleta mabadiliko katika maisha ya wagonjwa katika nyanja zinayotuhusu. Tumeona vifo vya uzazi na rufaa zikipungua kwa kiasi kikubwa na kwa njia endelevu katika maeneo haya, pamoja na kuona ongezeko la maana katika idadi ya wanawake wanaoamua kujifungua katika vituo vya huduma za afya.”

Akitilia mkazo baadhi ya changamoto, Dr. Mwakatundu ameeleza kuwa ili mafanikio haya yawe endelevu kuna haja ya kupanga rasilimali za kutosha kwa ajili ya wafanyakazi wa afya na kuboresha mfumo wa usamabazaji wa vifaa na madawa.

Waziri wa Afya, Mh, Ummy Mwalimu akitoa mchango wake kuhusu kazi za Thamini Uhai, amesema: “Ningependa kutambua mchango wenu katika kuhakikisha akina mama wanajifungua kwa usalama katika mikoa husika. Naelewa kuwa mmefanya kazi kubwa kuboresha mifumo ya huduma za dharura katika vituo vya afya na hospitali, mmeanzisha kampeni za mawasiliano na kuimarisha mifumo ya rufaa kutoka vituo vya afya kwenda hospitali.”

Thamini Uhai imekwisha kabidhi serikalini shughuli zake za mradi wa afya ya uzazi katika mikoa miwili – Morogoro na Pwani, na imepanga mwaka 2017 kuanza utaratibu wa kukabidhi shughuli zake katika mkoa wa Kigoma.
Wadau kutoka shirika la Thamini Uhai, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Rais - Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa wakishauriana wakati wa mkutano wa mrejesho wa shirika la Thamini Uhai, leo jijini Dar-es-Salaam.

KAMPUNI YA RED SEA YA KEKO JIJINI DAR ES SALAAM YAPEWA MWEZI MMOJA KUBOMOA UKUTA ULIOJENGWA JUU YA MTARO WA MAJI MACHAFU NA KUSABABISHA USUMBUFU KWA WANANCHI

$
0
0

NA Evelyn Mkokoi- Dar Es Salaam

Kampuni ijulikanayo kwa jina moja la Red Sea iliyopo katika Mtaa wa mafuta Keko Gerezaji jijini Dar Es Salaam, Imepewa mwezi mmoja wa kutakiwa kubomoa ukuta uliojengwa juu ya Mtaro wa maji machafu ambao pia ni eneo chepechepe, na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa maeneo hayo na hatari ya kupata magonjwa hasa katika kipindi cha mvua.

Akifuatila utekelezaji wa Maagizo ya ziara yake aliyoifanya tarehe 20 mwezi wa December mwaka jana, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amesema kuwa ujenzi huo holela, umekiuka sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake na kumtaka mmiliki wa kampuni hiyo kubomoa ukuta huo ndani ya siku thelathini na kinyume na hapo serikali kupitia halmashauri ya wilaya ya Temeke na NEMC itabomoa ukuta ukuta huo kwa gharama za mmiliki wa kampuni hiyo.

Aidha, Naibu Waziri Mpina Ameitaka NEMC pamoja na Manispaa ya Temeke kuwasilisha kwake ndani ya siku tatu vibali vilivyomruhusu mmiliki mwingine wa kampuni ya KOBIL kujenga juu ya mtaro huo, kinyume na hapo hatua nyingine zitachukuliwa.

Kwa Upande wake Mkaguzi wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Bw.Dismas Nyoni, ameeleza kuwa, TANROADS ina mpango wa muda mvupi wa kufanyia usafi mtaro huo ulioziba na kupita chini ya barabara katika eneo la kilwa road, na kuzibua mtaro huo ili kuwapunguzia wananchi usumbufu katika msimu wa mvua zinazokuja.

Wakati huohuo Naibu Waziri Mpina, alitemebelea Gereza la Keko kujionea utekelezaji wa maagizo yake ambapo awali gereza hilo lilikuwa likiririsha maji taka katika maeneo ya makazi na kwa hivi sasa gereza la keko limekamilisha ujenzi wa miundombinu ya maji taka kwa asilimia 80, aliwapongeza na kuwapa muda wa wiki mbili kumalizia marekebisho yaliyobakia, nae Mkazi wa eneo la Keko Gerezani Bi ASha Hussein alisema gereza la keko likikamilisha ujenzi huo wa miundombinu ya maji taka wananchi wataepukana na magonjwa na watoto watacheza vizuri. 

Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina na Uongozi wa Gereza la keko wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Mpina ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa maagizo yake gerezani keko ya ujenzi wa miundombinu ya majitaka ambayo ni rafiki kwa mazingira.( Picha na Evelyn Mkokoi)
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, Akitoa Maelekezo kwa Uongozi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira (NEMC) Hamlashauri ya Wilaya Ya Temeke, na TANROADS kuhusu suluhisho la muda na la kudumu la Mfereji wa Mtaa wa Mafuta keko Gerezani Jijini dar Es Salaam, wenye kuleta kero ya kimazingira kwa wakazi wa eneo hilo hususan katika kipindi cha mvua.

NI SIMBA, AFRICAN LYON KESHO UWANJA WA TAIFA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Simba na African Lyon zitakutana tena kesho kwenye  mechi ya Raundi ya Sita ya kuwania Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) yaani Azam Sports Federation Cup.

Mchezo huo awali ulipangwa kufanyika Machi mosi, 2017 lakini ulirudishwa nyuma kwa sababu za kiufundi kutoka timu zote mbili.

Michuano ya raundi hiyo ya sita, itaendelea tena Februari 24, mwaka huu kwa michezo minne kuchezwa kwa siku hiyo kuanzia saa 10.00 jioni kasoro mchezo mmoja tu utakaochezwa saa 1.00 jioni.

Michezo ya siku hiyo kwa mujibu wa ratiba inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), itakuwa ni kati ya Madini FC ya Arusha na JKT Ruvu ya Pwani watakaocheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Kagera Sugar itacheza Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mechi nyingine itakuwa ni kati ya The Mighty Elephant ya Ruvuma na Ndanda FC ya Mtwara zitakazopambana kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea ilihali Azam na Mtibwa Sugar watacheza Chamanzi –Mbagala – mchezo utakaofanyika saa 1.00 usiku.

Jumapili Februari 26, mwaka huu timu ya Mbao FC itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City zote za Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Machi 7, mwaka huu Young Aricans SC itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

DIWANI WA KATA YA KIJICHI TAUSI MILANZI AAPISHWA LEO.

$
0
0
Diwani mpya wa kata ya kijichi Tausi Milanzi akiapishwa katika kikao cha madiwani kilichofanyika leo.

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imefanya kikao cha baraza la madiani ambapo katika kikao hicho mada na ajenda mbalimbali za kimaendeleo zinazohusu wananchi zilijadiliwa.

Sambamba na hilo diwani mpya wa kata ya kijichi Tausi Milanzi alipata kuapishwa katika kikao hicho na kumfanya diwani kutambulika rasmi katika baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
Madiwani wakiwa katika kikao wakijadili ajenda mbalimbali za kimaendeleo za Manispaa ya wilaya ya Temeke

WAAMUZI TOKA UGANDA KUCHEZESHA MCHEZO WA YANGA VS NGAYA JUMAMOSI

$
0
0
Kikosi cha Yanga

Na Zainab Nyamka, Globu 

Mchezo wa marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Young Africans ya Tanzania na Ngaya ya Comoro hatua ya awali utachezeshwa na Waamuzi kutoka Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), waamuzi hao ni Alex Muhabi Nsulumbi atakapuliza filimbi uwanjani.

Nsulumbi atasaidiwa na Ronald Kakenya na Lee Okello wakati Mwamuzi wa Akiba atakuwa Brian Nsubuga Miro huku Kamishna akitokea Afrika Kusini ambaye ni Monnyenyone Lucas Nhlapo.

Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kama ambavyo Young Africans walithibitisha CAF majuma mawili yaliyopita kabla ya terehe ya mchezo huo ambayo ni Februari 18, mwaka huu.

MKUU WA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI MEJA JENERALI YACOUB MOHAMED AZURU KENYA

$
0
0
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi kilichoko Kunduchi Dar es Salaam, Meja Jenerali Yacoub Mohamed, yuko nchini Kenya kwa ziara ya kikazi.
Kanali Mohamed amesema atatembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Kenya kuona miundombinu yake na kubadilishana uzoefu na wakuu wa chuo hicho kilichopo Karen katika viunga vya jiji la Nairobi.
Mkuu huyo wa Chuo ametembelea Ubalozi wa Tanzania Nairobi na kuonana na Kaimu Balozi, Bi. Talha Mohamed Waziri. Lengo kubwa la ziara yake ni kubadilishana uzoefu na Chuo cha Ulinzi cha Kenya kuhusu uendeshaji na uandaaji wa mitaala.
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Bi Talha Waziri (Kulia) akifurahia zaidi aliyokabidhiwa na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi,  Meja Jenerali Yacoub Mohamed (wa pili kushoto). Kushoto ni Mshauri wa Kijeshi wa Ubalozi wa Tanzania, Kanali Fabian Machemba.
Meja jenerali Yavoub Mohamed na Kaimu Balozi (Katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja. Wa pili kulia ni Mshauri wa Kijeshi Kanali Machema na kulia ni Kanali Maulid Surumbu kutoka Chuo cha Ulinzi. Kushoto ni Kanali Njoroge wa Jeshi la Ulinzi la Kenya.

MAMA MAGUFULI NA MAMA MAJALIWA WAWAOMBA WANANCHI WASAIDIE WATU WASIOJIWEZA

$
0
0

MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametoa wito kwa Watanzania kujengea utamaduni wa kutembelea vituo vya wazee na watu wenye mahitaji maalumu na kutoa misaada ili waweze kujikimu.
Wameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 15, 2017) wakati walipotembelea Makazi ya Wazee wasiojiweza na walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma ya Amani Ipuli yaliyoko kwenye Manispaa ya Tabora mkoni Tabora.
Katika makazi hayo wamekabidhi tani 7.5 za vyakula mbalimbali ukiwemo mchele, unga wa sembe na maharage pamoja na mafuta maalumu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaosoma katika shule mbalimbali mkoni Tabora.
Hata hivyo, Mama Janeth amewapongeza watumishi wote wanaofanyakazi kwenye makazi ya kulelea wazee na watu wenye mahitaji maalumu kwa sababu kazi hiyo ni ngumu na ina changamoto nyingi.“Ibada si kwenda katika nyumba za ibada pekee bali hata kuwatembelea wazee, watu wenye mahitaji maalumu na wasiojiweza utakuwa umetoa sadaka kubwa kwa Mwenyezi Mungu. Nawaomba tujitahidi kuwatembelea,” amesema.

Kwa upande wake Mama Mary amewaomba wananchi wote wawe na utaratibu wa kuwasaidia wazee wanaoishi katika makaazi ya kulele wazee, walemavu na wasiojiweza nchini na kuwafariji kwa sababu wanahitaji upendo na faraja kutoka kwao.
Pia Mama Mary ameipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na wadau mbalimbali kwa kujitoa kwa hali mali katika kuwahudumia wazee na watu wenye mahitaji maalumu.Naye Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amesema Serikali itahakikisha huduma zinaboreshwa katika makazi ya kulelea wazee na watu wenye mahitaji maalumu nchini kwa kuwa vingi viko katika hali mbaya.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwakabidhi mafuta maalumu wawakilishi wa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi walioalikwa kwenye hafla iliyofanyika katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakikabidhi sehemu ya msaada wao wa tani 7.5 ya vyakula katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiongea na mmoja ya wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiongea na mmoja ya wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakilakiwa kwa nderemo walipowasili katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akisalimia wananchi na wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akihutubia wananchi pamoja na wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017

ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA WILAYANI KITETO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimfariji, Aziza Ibrahim wakati alipotembelea wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya ya Kiteto akiwa katika ziara ya mkoa wa Manyara, Februari 15, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Jengo la Halmashauri ya wilaya ya Kiteto lililopo Kibaya, Februari 15, 2017. Yuko katika ziara ya mkoa wa Manyara. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda mti baada ya kuweka jiwe la Msingi la jengo la Halmashauri ya wilaya ya Kiteto akiwa katika ziara ya mkoa wa Manyara, Februari 15, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwanahamisi Abdllah akiwa na mtoto Yusra Juma (3.5) katika eneo la mapokezi la hospitali ya wilaya ya Kiteto wakati alipotembelea hospitali hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Manyara, Februari 15, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mwakyembe atembelewa na Uongozi wa TLS

$
0
0

Serikali imekiasa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) kibaki kuwa chombo cha kitaaluma cha kulinda weledi, viwango na maslahi mapana ya uanasheria na kisikubali kuyumbishwa na mihemko ya uanaharakati wa kisiasa isiyo na tija kitaaluma.

Akiongea na ujumbe wa TLS kwenye ofisi yake ndogo ya Dar es Salaam leo (15/2/17), Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema TLS ibakie njia kuu kama ilivyo kwa vyama vingine vya kitaaluma nchini, isighilibiwe na michepuko.

Amesema uanzishaji na uendeshaji wa TLS kwa sheria ya Bunge umesukumwa miaka yote na dhamira njema ya Serikali ya kutaka kuilinda na kuilea taaluma ya uanasheria ili ikue na ijenge weledi stahili na hivyo itoe mchango bora katika ujenzi na uendeshaji wa utawala wa sheria nchini.

"Ikiwa TLS sasa inajiona imekua kiasi cha kutosha na sasa inataka iingie kwenye majukumu ya ziada ya uanaharakati wa kisiasa, Serikali haitasita kuifuta sheria iliyoanzisha TLS ili chama hicho kijisajili chini ya Sheria ya Vyama kama NGOs zingine nchini au ikiwezekana chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa kama vyama vingine vya siasa nchini".

Ameongeza kusema harakati zinazoendelea ndani ya TLS zenye mwelekeo wa kisiasa, zimeifanya ofisi yangu isimame kidogo kukamilisha marekebisho kadhaa ya sheria ya TLS maana hatma ya TLS haieleweki, "it remains in the balance".

Awali, waziri huyo aliueleza ujumbe huo wa TLS ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa TLS, Wakili Lameck Calleb, kuwa Serikali imefarijika sana kwa ushirikiano mkubwa uliotolewa na chama hicho katika maandalizi ya muswada wa sheria ya huduma ya msaada wa kisheria ambayo imepitishwa na Bunge na sasa unasubiri saini ya Rais wa Nchi kuwa sheria.

Aliongeza kuwa Wizara inaitegemea sana ushirikiano wa TLS hata katika utungaji wa Kanuni za sheria hiyo mpya, mchakato wake ambao tayari umeanza.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO

What do you know about the Africa Union?

$
0
0
 The advent of the African Union (AU) can be described as an event of great magnitude in the institutional evolution of the continent. On 9.9.1999, the Heads of State and Government of the Organisation of African Unity issued a Declaration (the Sirte Declaration) calling for the establishment of an African Union, with a view, inter alia, to accelerating the process of integration in the continent to enable it play its rightful role in the global economy while addressing multifaceted social, economic and political problems compounded as they are by certain negative aspects of globalisation.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu yapokea msaada wa pikipiki 14

$
0
0
Benjamin Sawe- Maelezo

Ofisi ya Taifa ya Takwimu imepokea msaada wa pikipiki 14 zenye thamani ya shilingi milioni 66 kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya ukusanyaji takwimu sahihi kwenye baadhi ya mikoa

Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia Bi.Nadia Belhaji Hassine alisema lengo la kukabidhi msaada huo ni kuboresha kazi ya ukusanyaji takwimu mikoani hasa sehemu ambazo hazifikiwi kwa usafiri wa gari.

Bi. Hassine amesema kutokana na kazi inayofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kufanikisha ukusanyaji na usambazaji wa takwimu mbalimbali ambazo zimekuwa na matokeo chanya taasisi hiyo imeamua kutoa msaada huo ili kuimarisha utendaji wa taasisi hiyo uweze kuwa bora zaidi.

Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano hayo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema msaada huo utaboresha na kukuza tasnia ya takwimu ili kuweza kupata taarifa muhimu kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Dkt Chuwa alisema msaada huo utarahisiha usafiri wa kutoka eneo moja la utafiti hadi lingine na kuweza kusaidia katika upatikanaji wa taarifa muhimu za kitafiti.

Akipokea moja ya pikipiki hizo Bw.Lugome Kalisto kutoka Ofisi ya Takwimu Mkoa wa Pwani aliishukuru Benki ya Dunia kwa msaada wa pikipiki hizo kwani wamekuwa wakipata shida ya usafiri katika ukusanyaji wa takwimu hasa maeneo ambayo usafiri wa gari haufiki.

”Tumekuwa tukipata shida katika ukusanyaji wa takwimu hasa maeneo ambayo hayafikiki kirahisi kwa gari hali ambayo imekuwa ikifanya utendaji wetu kuwa duni.Alisema Bw. Kalisto.

MUSEUM ART EXPLOSION @ MUSEUM AND HOUSE OF CULTURE FEBRUARY 24, 2017


BONANZA LA MICHEZO LA MAAFISA WA HABARI SERIKALINI KUFANYIKA JUMAMOSI HII VIWANJA VYA MNAZI MMOJA DAR ES SALAAM

INSTINCS RECORDS LABEL YANDAA MPANGO WA MAPINDUZI YA WASANII WA BONGO FLEVA

TRAFIKI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM YAZINDUA OPERESHENI OKOA MAISHA, YAANZIA CHAMAZI

NAMAINGO YATOA ELIMU KWA WANANCHI WA KATA YA MAANGA MTAA WA MAENDELEO JIJINI MBEYA

$
0
0
Kampuni isiyo ya  kiserikali  ya Namaingo Business Agency ukanda wa Mbeya katika Kata ya Manga ,mtaa wa Maendeleo imefanya mkutano wa mafunzo kwa wananchi wa Kata hiyo na maeneo ya jirani wakiwa na malengo makuu ya Kuifundisha jamii mbinu mpya na bora katika kuyaendea mafanikio binafsi na kupunguza utegemezi.
Akiongea kwa umaridadi mkubwa Bw.Gaudence Rwabyoma juu Pichani ambaye ni Mkufunzi wa masuala ya Uchumi ndani ya Namaingo ameutanabaisha Umma kwa kutumia mifano mtambuka kuwaeleza makumi ya wananchi waliokuwepo mkutanoni hapo mbinu mpya ya kufikia maendeleo hasa kwa kutumia mfano wa jinsi gani Serikali, mkulima, mnunuzi, taasisi za kifedha, mtaalamu na mwanasheria wanavyoweza kutegemeana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuzalisha zaidi.
Mkufunzi huyo ameutanabaisha Umma kuwa wao kama Namaingo wanafanya kazi kwa kushirikiana zaidi na serikali hivyo ni nafasi ya wananchi kukipatia maeneo mengi ya ardhi ya kuanzisha Vijiji mradi kwa kupata ekari nyingi za uwekezaji, pia Namaingo kuhakikisha wananchi wanapata mitaji kwa riba nafuu na masoko pia.
Wazee wa Mtaa wa Maendeleo kata ya Maanga wakifuatilia Semina elekezi iliyokuwa ikitolewa na Wakufunzi wa Namaingo Jijini Mbeya
Viongozi waandamizi wa Mtaa wa Kata ya Manga Jijini Mbeya wakiwa na Mratibu wa Namaingo Mkoa wa Mbeya (wa kwanza kulia) Bw.Jottam Willson
Elimu kwa vitendo Baadhi ya wakazi wa Kata ya Manga wakionyesha jinsi Namaingo inavyofanya kazi kwa kuwaunganisha serikali,Wakukima/wafanyabiashara, wanunuzi, taasisi za kifedha,wataalamu na wanasheria.
PICHA NA MR.PENGO.
MAELEZO  NA THOBIAS OMEGA

MBUNGE WA SHINYANGA MJINI STEPHEN MASELE AFANYA ZIARA JIMBONI, ATEMBELEA MRADI MKUBWA WA DARAJA LA GALAMBA

$
0
0

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Jumatano Februari 15, 2017 ameanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kuangalia miundombinu iliyopo katika jimbo hilo.  
Mhandisi wa Barabara wa Manispaa ya Shinyanga Injinia Stephen Manyangu akiendelea kutoa maelezo ingawa hata hivyo mbunge Masele aliahidi kutengenezwa/kujengwa kwa barabara hiyo kwa kiwango kwa fedha za mfuko wa jimbo la Shinyanga mjini wakati wanafanya utarabu wa kujenga barabara hiyo katika kiwango cha lami.
Hapa ni katika Mto Simba ambapo mradi wa Ujenzi wa Daraja lililopo katika kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga unaendelea.Pichani ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele (CCM) akiangalia upande wa pili wa daraja linalojengwa na Mkandarasi M/S Pasons Co.Ltd tangu mwezi Juni mwaka 2016 na unatarajia kukamilika mwezi Machi mwaka 2017.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa ndani ya darasa la saba katika shule ya msingi Bugweto.






Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images