Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1568 | 1569 | (Page 1570) | 1571 | 1572 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

  Wiki chache baada ya Jeshi la Polisi mkoani hapa kukamata gunia 58 za bhangi ambazo ziliteketezwa kwa moto na kuharibu hekari 31 za mimea ya zao hilo katika maeneo ya Kismiri Juu na Engalaon wilayani Arumeru, Jeshi hilo limeendelea na misako dhidi ya wauzaji, watumiaji na wasafirishaji wa dawa za kulevya na kufanikiwa kuwakata watuhumiwa 80 katika misako iliyofanyika kwa muda wa siku 4 tu.

  Akitoa taarifa hiyo leo asubuhi ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema kwamba misako hiyo imefanikisha kukamata jumla ya kete 167 za madawa ya kulevya aina ya Heroin pia misokoto 3,845 ya Bhangi na mirungi kilogramu 33.

  “Katika misako hiyo ambayo ilifanyika wilaya zote sita za mkoa huu, watuhumiwa 54 walipatikana kwenye tuhuma za Bhangi, 14 ni tuhuma za Heroin na 12 ni wa tuhuma za mirungi.” Alisema Kamanda Mkumbo.

  “watuhumiwa 40 ni wauzaji wa madawa hayo huku 13 ni wale ambao walikuwa wanajihusisha kwa namna moja au nyingine na Bhangi na mmoja alikuwa anasafirisha, watuhumiwa 14 wa Heroin kosa lao kupatikana huku 12 makosa yao ni kupatikana na mirungi na hivyo kufanya idadi yao kuwa 80 ambao ni wanaume na wanawake”. Alifafanua Kamanda Mkumbo.

  Kamanda wa Polisi aliwashukuru wananchi wa mkoa huu kwa ushirikiano wa utoaji wa taarifa za uhalifu na kuwaomba waendelee kufanya hivyo na kutoa onyo kwa wale wachache wanaojihusisha na uhalifu wa namna hiyo waache mara moja vinginevyo watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo akionyesha baadhi ya kete za Heroin ambazo zilikamatwa hivi karibuni kutokana na misako inayoenndelea mkoani hapa. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha).
  …………

  0 0

  Na Greyson Mwase, Manyara

  Wananchi katika Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wamepongeza kampuni ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua ya Rafiki Power iliyopo chini ya kampuni tanzu ya E.ON ya Ujerumani, kwa kuwapatia huduma ya umeme iliyopelekea kukua kwa kasi ya maendeleo katika wilaya hiyo.

  Waliyasema hayo leo katika ziara ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini katika miradi ya umeme mkoani Manyara yenye lengo la kuangalia utekelezaji wa miradi ya umeme, changamoto zake na kutoa ushauri wa kitaalam.

  Akizungumza kwa niaba ya wenzake katika kijiji cha Komolo kilichopo wilayani Simanjiro mkoani Manyara, Thadeo Bura ambaye ni mmiliki wa duka la vifaa vidogo vya umeme jua na bidhaa nyingine, alisema kabla ya kampuni ya Rafiki Power kuwekeza katika kijiji hicho maisha yalikuwa ni magumu kwa kuwa hakukua na nishati ya kuwawezesha kuanzisha miradi midogo midogo.

  Alisema mara baada ya kupata umeme kupitia kampuni ya Rafiki Power, ameweza kuanzisha duka kwa ajili ya vifaa vidogo vya umeme jua, bidhaa nyingine na kutoa huduma nyingine kwa wanakijiji wenzake.

  Alisema huduma ya umeme imewekwa kwenye baadhi ya shule na hospitali hivyo kuboresha huduma za jamii.

  Naye Joseph Hango ambaye ni mmiliki wa saluni ya kunyoa nywele aliongeza kuwa uwepo wa nishati ya umeme kupitia kampuni ya Rafiki Power umepelekea kuongezeka kwa kipato kutokana na idadi ya wateja kuongezeka.

  Aliiomba kampuni hiyo kuendelea na juhudi za kusambaza umeme katika maeneo mengi ambayo hayajafikiwa na huduma ya umeme ili kukuza uchumi wa wilaya na mkoa kwa ujumla.

  Wakati huohuo, akizungumza katika ziara hiyo Meneja Mkuu wa Kampuni ya Rafiki Power, Joanis Holzigel alisema kuwa kampuni yake inatarajia kuongeza uzalishaji wa umeme ambapo kaya 20,000 nchi nzima zinatarajiwa kunufaika na huduma ya umeme ifikapo mwaka 2022.

  Alisema kwa kutambua umuhimu wa nishati ya umeme katika uchumi wa viwanda utakaopelekea nchi ya Tanzania kuwa kwenye orodha ya nchi za kipato cha kati ifikapo mwaka 2025, kampuni yake imeweka mipango ya muda mfupi na muda mrefu ambapo inatarajia kufikia wateja 20,000 ifikapo mwaka 2022.

  Akitaja miradi inayotekelezwa na kampuni yake, Meneja Holzigel alisema katika mkoa wa Arusha kampuni yake ina miradi minne katika maeneo ya Digodigo, Soitsambu, Ololosokowani, na Malambo yaliyopo wilayani Ngorongoro na miradi mingine miwili iliyopo katika maeneo ya Itaswi na Kwamtoro wilayani Kondoa, mkoani Dodoma.

  Aliongeza kuwa, mradi mwingine mmoja unaotekelezwa na kampuni hiyo ni wa Komolo/Temeke, uliopo Simanjiro mkoani Manyara.
  Meneja Mkuu wa kampuni ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua ya Rafiki Power, Joanis Holzigel (kushoto) akibadilishana mawazo na Mtaalam wa Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Emillian Nyanda (kulia) katika ziara ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizarani katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya umeme.
  Mmiliki wa kioski kilichonufaika na huduma ya umeme jua kupitia kampuni ya Rafiki Power, Thadeo Bura (kushoto) akielezea manufaa ya mradi wake katika ziara ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya umeme.
  Moja ya kioski kilichonufaika na huduma ya umeme jua kupitia kampuni ya Rafiki Power kilichopo katika kijiji cha Komolo wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
  Mmiliki wa mghahawa wa chakula ambaye ni mmoja wa wanufaika wa huduma ya umeme jua kupitia kampuni ya Rafiki Power akionesha friji inayotumia nishati hiyo katika ziara ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya umeme.
  Mmiliki wa kioski kilichonufaika na huduma ya umeme jua kupitia kampuni ya Rafiki Power, Thadeo Bura akielezea matumizi ya compressor inayotumia nishati ya jua kwa matumizi mbalimbali, katika ziara ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya umeme.

  0 0

  Hussein Makame, NEC aliyekuwa Bukoba

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewatahadharisha watu wanaochukua kadi za kupigia kura za wenzao na kuzizuilia au kubaki nazo kuwa ni kinyume cha Sheria.

  Hayo yamesema na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe wakati akitoa elimu ya mpiga kura katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba na Shinyanga hivi karibuni.

  Alisema kifungu cha 88 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kinasema kuwa ni kosa la jinai kwa mtu kuchukua kadi ya mpiga kura mwingine na kuiziulia, kukataa kuirudisha au kubaki nayo kwa uzembe.

  Bw. Kawishe alifafanua kuwa kumekuwa na malalamiko kwamba inapofikia karibu na kipindi cha uchaguzi, baadhi ya watu wanachukua kadi za wapiga kura wengine na kuzizuia kinyume cha Sheria.

  Hata, hivyo alisema kutokana na kutoa elimu ya mpiga kura kupitia mikutano na kuhudhuria maonesho mbalimbali, baadhi ya wananchi wameelewa umuhimu wa kadi hizo na kuahidi kutoampa mtu kadi zao za kupigia kura.

  “Kwa hiyo katika jambo hilo tumekuwa na mrejesho ambo ni chanya lakini tunachowaomba ukiandikishwa tunza kadi yako ya mpigia kura” alisema Bw. Kawishe na kuongeza kuwa;
  Mkurugenzi waHuduma za Kisheria wa Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe, akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matirowakati alipomtembeleaofisinikwakemkoanihumo.
  Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe, akitoa Elimu ya Mpiga kura kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Old Shinyangailiyopomanispaaya Shinyanga.Pichana Hussein Makame, NEC.

  Mkurugenzi waHuduma za Kisheria wa Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe, akisamiliana na Mkurugenzi wa Halamashauri ya Manispaa ya ShinyangaBw. Geofrey Ramadhani Mwangulumbi baada ya kuwasili kwenye Halmashauri hiyo kutoa Elimu ya Mpiga kura.


  0 0


  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Wachimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia nchini, Wenyeviti wa Bodi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Wakuu wa Mashirika pamoja na Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake ili kujadili Kanuni za Local Content kikao hicho kilifanyika tarehe 11-12 mjini Dodoma.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akimsikiliza mmoja wa washiriki katika kikao cha kuandaa Kanuni za Local Content. Wengine katika picha ni wenyeviti wa Bodi za Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakuu wa Mashirika pamoja na Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake na wawakilishi wa kampuni za Wachimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Nchini.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akisikiliza mada kuhusu Local Content iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Mgamlagosi (hayupo pichani). Wengine ni washiriki walio hudhuria kikao hicho mjini Dodoma.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Ntalikwa (wa pili kulia) akiendesha kikao cha kujadili Kanuni za Local Content kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BG, Marc Hartog (wa kwanza Kulia) Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Profesa Sufiani Bukurura (wa tatu kulia), Kaimu Kamishna wa Nishati na masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga (wa nne kulia), Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Modestus Lumato (wa tano kulia) pamoja na Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini.


  0 0


  Na: Genofeva Matemu – WHUSM

  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeanza kutekeleza malengo iliyojiwekea ya kuifanya Lugha ya Kiswahili kuwa bidhaa yenye thamani ili iweze kupata soko na kutumika duniani kote katika kurahisisha mawasiliano ya watumiaji wa lugha hiyo.

  Rai hiyo imetolewa na Waziri mwenye dhamana ya Sekta na Utamaduni Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akizungumza na wadau wa Sekta hiyo jana Jijini Dar es Salaam.

  “Tumejipanga kuangalia changamoto zinazotokana na Sera na Sheria tulizonazo, changamoto za kirasilimali na mambo ya kiutashi kwani kwa kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo Kiswahili kitaendelea kuwa bidhaa ambayo itavuka mipaka ya nchi na kuitangaza nchi yetu” amesema Mhe. Nnauye.

  Akizungumza wakati wa Mkutano huo Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Selemani Sewangi amewataka waandishi wa vitabu vya Kiswahili kuzingatia weledi wa matumizi fasaha ya lugha ya Kiswahili wakati wa uandishi wa vitabu ili kuweza kuisaidia jamii hasa mashuleni kujua misamiati fasaha ya lugha hiyo.

  Kwa upande wake mdau wa Utamaduni nchini Dkt. Musa Hans ameiomba serikali kuhamasisha wageni wote wanaoingia nchini kujifunza lugha ya Kiswahili na kuandaa mwongozo kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu utakaowataka watoto wote wanaoingia sekondari kuwa na kamusi za Kiswahili na kamusi za Kiswahili Kingereza zitakazowasaidia kujua misamihati ya lugha ya Kiswahili.

  Naye Mdau wa Utamaduni mama Mipango ameipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kutafuta njia mbalimbali za kueneza na kukuza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi.

  Katika kuendeleza ukuaji wa Lugha ya Kiswahili Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekua mstari wa mbele kutumia lugha ya Kiswahili katika shughuli mbalimbali za kiserikali kama vile Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) ambapo kwa kufanya hivyo lugha hii imeweza kusambaa kwa kasi zaidi.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau wa sekta ya Utamaduni walipokutana nao Jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kukifanya Kiswahili kuwa bidhaa yenye thamani na kukisambaza nje ya mipaka ya nchi.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura (katikati) akichangia wakati wa majadiliano jana  Jijini Dar es Salaam na wadau wa Sekta ya Utamaduni katika kukuza na kukifanya kiswahili kuwa bidhaa yenye thamani. Kushoto ni Waziri wa Habari Mhe. Nape Moses Nnauye na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na wadau wa Sekta ya Utamaduni (hawapo pichani) walipokutana jana Jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kukifanya Kiswahili kuwa bidhaa yenye thamani ndani na nje ya nchi.
  : Baadhi ya Wadau wa Sekta ya Utamaduni wakifuatilia kwa makini hoja zilizokua zikiendelea wakati wa majadiliano na viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kujadili namna ya kukifanya Kiswahili kuwa bidhaa yenye thamani ndani na nje ya nchi jana Jijini Dar es Salaam
  Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Selemani Sewangi akitoa taarifa ya namna Kiswahili kinavoendelea kukua wakati wa majadiliano na wadau wa sekta ya Utamaduni kujadili namna ya kukuza na kukifanya Kiswahili kuwa bidhaa yenye thamani ndani na nje ya nchi  jana Jijini Dar es Salaam.
  Mdau wa Utamaduni Mama Mipango akichangia mada wakati wa majadiliano na wadau wa sekta ya Utamaduni kujadili namna ya kukuza na kukifanya Kiswahili kuwa bidhaa yenye thamani ndani na nje ya nchi jana Jijini Dar es Salaam.
  : Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (waliokaa katikati) katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya Utamaduni walipokutana kujadili namna ya kukifanya Kiswahili kuwa bidhaa yenye thamani jana Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia waliokaa ni Naibu Waziri wa Habari Mhe. Annastazia Wambura, Wapili kushoto waliokaa ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Prof. Elisante Ole Gabriel, na wakwanza kushoto waliokaa ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Bibi. Nuru Millao.

  Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Mh. Tundu Lissu (kulia) akijadiliana jambo na mawakili wake, Peter Kibatala (wa kwanza kushoto) na Jeremiah Mtobdesya baada ya kesi yake inayomkabili ya uchochezi kuahirishwa. Katika kesi hiyo Lissu anashtakiwa pamoja na wanahabari, Simon Mkina, Idrisa Jabir na Ismail Mehboob.
  Mhariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na mwanahabari Idrisa Jabir wakiwa nje ya chumba cha mahakama baada ya kesi yao ya uchochezi kuahirishwa.

  0 0


  0 0

  Baadhi ya wauguzi na Madaktari wa Idara ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla hiyo.

  Watumishi wa afya wamekumbushwa kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ya taaluma ya kazi ili kuendelea kutoa huduma bora .

  Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa alipokua akizungumza katika hafla fupi ya kumuaga Muhudumu wa afya Mama Eda Kapange aliyekua akihudumu katika Idara ya watoto Hospitalini hapo.

  Amesisitiza kuwa suala la kuzingatia maadili ya taaluma hiyo ni muhimu kwani mgonjwa anahitaji upendo na kupewa maneno yenye matumaini na kwamba hiyo pekee ni tiba .

  Pia Mkurugenzi Mtawa amemuelezea Mama Eda Kapange kuwa ni mtumishi hodari na mchapakazi hivyo amewataka watumishi wengine kuiga mfano wake kwa vitendo.
  Baadhi ya viongozi wakimtakia heri na afya njema mama Eda Kapange katika maisha yake baada ya kulitumikia taifa.
  Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Agnes Mtawa akitoa neno katika hafla fupi ya kumuaga Muhudumu wa afya Mama Eda Kapange iliyofanyika katika Hosppitali ya Taifa Muhimbili.
  Kushoto ni Mama Eda Kapange akikata keki katika hafla hiyo ya kumuaga, keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya kumuaga.
  Baadhi ya Wauguzi na Madaktari wa Idara ya watoto wakishangilia huku wakiinua maua juu kama ishara ya upendo.

  0 0  Vice Chancellor of the University of Dar es Salaam, Professor Rwekaza Mukandala, (L), and Deo Mwanyika , who is Acacia Vice President (Corporate Affairs), sing the renewed Memorandum of Understanding (MoU) under which Acacia Mining will support 52 students and staff in various areas hence to improve quality of engineering sector. The signing ceremony was held late on Tuesday at the University’s Mlimani Campus in Dar es Salaam.

  K-VIS BLOG/Khalfan Said

  THE University of Dar es Salaam (UDSM) has signed a renewed Memorandum of Understanding (MoU) with Acacia Mining that would support 52 students and staff in various areas hence improve quality of engineering sector .

  Speaking shortly before signing of the MoU on Tuesday in Dar es Salaam , Deo Mwanyika , who is Acacia Vice President (Corporate Affairs) , said there are a number of aspects that the company and University are partnering.

  He mentioned some of aspects as a two year practical work experience for 2nd and 3rd year students, funding for university laboratory equipment, sponsorship of postgraduate mining/mineral process engineering students and bursary for six students.

  He said the two year practical work experience for the mentioned students in the chemical and Mining engineering department in various fields of significance to Tanzania’s development agenda in relation to the mining sector.

  Mwanyika congratulated the first 52 students who will be part of the program and asked them to apply the knowledge and experience gained from practical training for the development of Tanzania.

  Further more, he said Acacia is committing more than 22m/- finances for purchase of laboratory equipment, student site visit and practical experience at its mine sites and helps supervise final year students on their project works.

  “This support , exposure and experience are critical to our students the future professional workforce of our country Acacia creates that solid foundation one needs for their career ahead”, he said.

  Under the two year signed Mou, he said the company has for the new study year allocated 6 scholarship for students at CoET.


  Vice Chancellor of the University of Dar es Salaam, Professor Rwekaza Mukandala, (2nd-L), and Deo Mwanyika, (2nd-R) , who is Acacia Vice President (Corporate Affairs), display documents after they had signed at the University’s Mlimani campus in Dar es Salaam late on Tuesday. The University of Dar es Salaam (UDSM) has signed a renewed Memorandum of Understanding (MoU) with Acacia Mining that would support 52 students and staff in various areas hence to improve quality of engineering sector. Right is Acacia's Chief Advisor, Learning and Training, Jannet Reuben Lekashingo, and UDSM's Acting Secretary to Council and Corporate Counsel who is also, the Intellectual Property Manager, Dr. Saudin Mwakaje. 


  0 0

  Mkurugenzi wa Benki ya CBA Tanzania, Gift Shoka ( kushoto) akisaidiwa kukata keki na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za wateja wa benk hiyo,Hyasinta Mwimanzu wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya wapendanao duniani ambapo benki hiyo iliadhimisha siku hiyo pamoja na wateja wao(hawapo pichani) katika . makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Ssalaam jana.
  Mkurugenzi wa Benki ya CBA Tanzania, Gift Shoka ( kushoto) akimlisha keki mmoja wa wateja wa benki hiyo ambaye ni Meneja Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni ya Britan Insurance ( T) Limited, Farai Dogo wakati wa kuadhimisha siku ya wapendanao duniani(Valentine’s Day) ambapo wafanyakazi wa benki hiyo walishirikiana na wateja wao kuadhimisha siku hiyo muhimu duniani kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam jana.
  Baadhi ya wateja wa benki ya CBA Tanzania pamoja na wafanyakazi wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Benki hiyo, Gift Shoka ( kulia) wakati wa hafla fupi ya kusherehekea siku ya wapendanao duniani pamoja na wateja wa benki hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.


  0 0

  WANANCHI katika mikoa ya Pwani, Morogoro na Dar es Salaam inayopatikana kanda ya mashariki wametakiwa kujikita katika kilimo na ufugaji ili kujiinua kiuchumi kwani ndizo shughuli zinazoleta maendeleo ya haraka hasa kutokana na rasilimali zilizopo nchini.

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe, mkoani Pwani jana wakati akifungua mafunzo ya siku nne ya viongozi na waratibu wa uwezeshaji kutoka mikoa hiyo mitatu yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

  Dkt. Kebwe alisema, ni ajabu kuona Tanzania inashindwa kupiga hatua kiuchumi huku ikiwa na eneo kubwa la kilimo na mifugo kuliko baadhi ya mataifa mengine duniani.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt.Kebwe Steven Kebwe akisisiiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne kwa Viongozi na Waratibu wa Uwezeshaji katika Kanda ya Mashariki mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro mafunzo hayo yanafanyika Kibaha mkoani Pwani na kuratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi NEEC, Dkt.John Jingu . wapili kushoto ni Katibu Mtendaji wa NEEC,Bi.Beng’i Issa. Kulia kwake ni Katibu Tawala- Pwani, Bw.Zuberi Semataba na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha,Bi.Asumpta Mshama.

  “Tanzania ina ng’ombe milioni 26 sawa na nchi ya Australia, kwa taarifa yenu Australia kwa mwaka wanaingiza Sh trilioni 28 kutokana na bidhaa za mifugo hiyo ni sawa na bajeti yetu ya serikali kuu. Tuna utajiri mkubwa hatuna sababu ya kulalamika, kwa sababu Morogoro tu ni sawa na nchi ya Malawi pamoja na maji yake na ardhi.

  “Kwa hiyo viongozi mliofika katika mafunzo haya muondoke mkiwa mmepikwa hasa kwa kuwa muongozo huu ndio dira ya kusimamia uwezeshaji wananchi kiuchumi, wananchi wakiendelea kiuchumi maana yake taifa limeendelea,” alisema Dkt. Kebwe.

  Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa wa Morogoro ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo aligusia suala la nchi kujitegemea kiuchumi ili kuondokana na aibu ya kutegemea wahisani.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC),Bi.Beng’i Issa akisisitiza jambo wakati ufunguzi wa mafunzo ya siku nne kwa Viongozi na Waratibu wa Uwezeshaji katika Kanda ya Mashariki mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro , mafunzo hayo yanafanyika Kibaha mkoani Pwani na yanaratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC). Kushoto kwake ni mwenyekiti wa bodi NEEC, Dkt.John Jingu na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt.Kebwe Steven Kebwe.

  “Ng’ombe kuanzia kwato hadi pembe ni mali tupu, tutumie viwanda vyetu kuwawezesha wafugaji kujinufaisha kiuchumi. Taifa kuwa tegemezi kwa wahisani ni aibu, utajiri tunao kikubwa ni kujipanga kwa sababu wapo watu wana ng’ombe zaidi ya 10,000 halafu bado wanaitwa wafugaji hapana hao ni wawekezaji wanaweza kuajiri watu na kulipa kodi,” alisema Dkt Kebwe.

  Akimkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa NEEC, Dkt. John Jingu alisema ili taifa liendelee lazima wananchi walio wengi wasaidiwe namna ya kujiletea maendeleo, ndio maana wakachagua kuwawezesha wakulima na wafugaji kwa kuwa ndilo kundi kubwa.

  “Wakulima ndio wanaotulisha lakini hawana mitaji, wafugaji nao ni wawekezaji lakini hawana mikakati mizuri ya malisho. Katika mikakati yetu tunatafuta namna ya kuondokana na vurugu za wakulima na wafugaji kugombania ardhi kwa kuunganisha wafugaji wadogo katika ranchi moja.
  Viongozi na Waratibu wa Uwezeshaji wa Kanda ya Mashariki wakifuatilia wakisikiliza mada wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani. Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo viongozi hao juu ya dhana ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia fursa zilizopo katika maeneo yao. Mafunzo hayo yameratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC).

  “Kwa mfano ranchi ya Kongwa ina uwezo wa kuchukua ng’ombe 20,000 lakini hadi sasa ina ng’ombe 9,000 tu. Hilo eneo lililobaki tunaweza kuunganisha wafugaji wadogo wenye ng’ombe kuanzia 200 wakawekwa pamoja itasaidia kupata malisho ya uhakika na kuiepusha mifugo na maradhi ambayo hushusha thamani ya ngozi, nyama na maziwa,” alisema Dkt Jingu.
  Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa NEEC Bi. Beng’i Issa, alisema lengo la mafunzo hayo ni kujadiliana kwa pamoja na viongozi ili kupata njia muafaka za kuwakwamua wananchi na machungu ya umasikini.

  “Lengo la baraza hili ni kusimamia, kuonyesha njia, kufanya utafiti na kutafuta fedha kwa ajili ya kuwainua wananchi kiuchumi. Tunataka kila kiongozi kufanya kazi katika maeneo yao kwa sabbu wapo ambao hawajui mipaka na kulazimika kufanya kazi za wengine.

  “Matarajio yetu baada ya mafunzo haya kila aliyehudhuria atakuwa na taarifa sahihi pamoja na nia ya kusaidia wananchi, kwa sababu wananchi wanahitaji kuelekezwa na kusimamiwa katika kila shughuli za kiuchumi wanazofanya,” alisema Bi. Beng’i.

  Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa wilaya waliohudhuria mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Ally Hapi alisema “Sisi ndio tunaokaa na wananchi na kujua matatizo wanayokumbana nayo, kwa muda mrefu katika wilaya yangu tunakabiliwa na tatizo la ajira kwa hiyo tuanpiga kelele viajana wajiajiri.

  “Kama mnavyofahamu Kinondoni ni wilaya ya mjini hakuna wakulima wala wafugaji asilimia kubwa ni wafanyabiashara, lakini kuna aina mpya ya ufugaji kama kuku, samaki na kilimo cha Greenhouse, vilevile kuna vikundi vya usindikaji uyoga, maembe na matund amengine. Tulijipanga kuandaa programu ya mafunzo ya usindikaji kwa vijana 10,000 tayari vijana 3,000 wameshapata mafunzo, pia ufugaji wa samaki hauhitaji maeneo makubwa nio biashara yenye tija katika wilaya yangu,” alisema Hapi.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt.Kebwe Steven Kebwe(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Wilaya wa Kanda ya Mashariki mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro mara baada ya kufungua mafunzo ya siku nne kwa Viongozi na Waratibu wa Uwezeshaji wa Kanda hiyo yanayofanyika Kibaha mkoani Pwani. Mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo yanaratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC).


  0 0

  Mafundi kutoka Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco) wakiondoa laini ya Majisafi iliyounganishwa bila kufata utaratibu na vishoka katika eneo la Boko Magengeni, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya kupambana na wizi wa Maji katika jiji la Dar es salaam na Mkoa wa Pwani.


  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia), akipokea taarifa ya upembuzi yakinifu kuhusu uwekezaji katika miundombinu ya Madaraja kutoka kwa Bw. Lord Clire Hollich (Kushoto) wa Ubalozi wa Uingereza, katikati ni Balozi wa Uingereza hapa Nchini Sarah Cooke.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akijadiliana jambo na Balozi wa Uingereza hapa Nchini Sarah Cooke (Kushoto), walipokutana Jijini Dar es Salaam leo hii. Katikati ni Bw. Lord Clire Hollich.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akisisitiza jambo kwa Balozi wa Uingereza hapa Nchini Sarah Cooke (Kushoto), walipokutana Jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Bw. Lord Clire Hollich.

  0 0


   Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Zamaradi Kawawa akizungumza juu ya Bonanza hilo
   Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Theophil Makunga akizungumza na waandishi wa habari juu ya Tamasha hilo

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Waziri wa habari Sanaa, utamaduni na Michezo, Nape Nnauye anataraji kuongoza  Bonanza la mazoezi na upimaji afya February 18 mwaka huu ulionadaliwa na Chama cha maofisa mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na jukwaa la wahariri Tanzania na Dar es Salaam City Press Club.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Msemaji wa chama TAGCO, Abel Ngapemba ametaja kuwa lengo la Bonanza hilo ni kuhamasisha wananchi kujenga tabia ya kufanya mazoezi na kupima afya kama ilivyozoeleka kwa kuunga mkono kampeni iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

  “washiriki wa bonanza hili ni pamoja na maofisa mawasiliano wa Serikali na wasekta binafsi ,Wahariri , Wahandishi wa habari na Bloggers na wananchi kwa ujumla kwa kuongozwa na Waziri Nape Nnauye na kuhudhuliwa na viongozi wa Wizara ya afya na ustawi wa jamii, jinsia wazee na watoto” amesema  Abel.

  Ametaja kuwa mbali ya mazoezi taasisi zitakazo shiriki kutoa huduma siku hiyo ni pamoja na Tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Saratani ya Ocean Road,Hospitali ya Sanitas,CCP Medicine Kinyerezi na Mfuko w Bima ya Afya (NHIF), Chama cha madaktari wa meno Tanzaniana tasisi ya wagonjwa wa mifupa MOI.

  Abel ametoa wito kwa wahariri wa vyombo vya habar, waandishi wa habari , Bloggersna maofisa mawasiliano Serikalini, mashirika binafsi na tasisi za kimataifa kujitokeza kwa wingi katika bonanza hilo.

  0 0
  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Eng. Tumaini Magesa na Mkurugenzi wa Halmsahuri ya wilaya hiyo, Bw. Tamim Kambona waende kata ya Engusero Jumamosi wiki hii wakafanye mkutano wa hadhara na kujibu kero za wananchi wa kata hiyo.

  Mkuu wa Wilaya hiyo na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo wametakiwa pia wafuatane na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Bw. Lairumbe Mollel wakatoe ufafanuzi bila kukosa.

  Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Februari 15, 2017) katika kijiji cha Engusero wilayani kiteto baada ya kusimamishwa na wananchi wakati akiwa njiani kuelekea mjini Kibaya yalipo makao makuu ya wilaya hiyo ili aanze ziara ya kikazi ya mkoa wa Manyara.

  Akijibu baadhi ya maswali aliyoulizwa na wananchi wa kijiji cha Engusero, Waziri Mkuu amesema analichukua ombi la wakazi hao la kupata kujengewa soko la kimataifa katika kata hiyo ili waweze kuuza mahindi hapo hapo.

  “Nitaawagiza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri waje hapa Jumamosi hii na kufanya mkutano ili wawaeleze wana mpango gani kuhusiana na ujenzi wa soko hilo,” amesema.

  Awali , Mkazi wa kata hiyo Bw. Ali Athumani alimuomba Waziri Mkuu awasiaidie ili wajengewe soko la kimataifa kwa sababu wao ni wazlishaji wakubwa wa mahindi lakini hawafaidiki nayo kwa sababu yote yanaenda kuuzwa katika soko la Kibaigwa.

  Naye Bw. Said Shabani alimuomba Waziri Mkuu awasaidie kufuatilia upatikanaji wa gari la wagonjwa na ujenzi wa wodi nyingine ya wagonjwa pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti kwenye zahanati yao.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali imeweka nia ya dhati ya kupambana na dawa za kulevya na amewataka watendaji wote kuanzia ngazi ya vijiji wadhibiti suala hilo.

  “Serikali haiwezi kuona vijana wanaangamia kwa dawa za kulevya. Tumeamua kudhibiti hali hiyo. Hii vita ni ya nchi nzima. Kuanzia sasa, viongozi wa Serikali za vijiji wakamateni wale wote wanaojihusisha na biashara hii.”

  “Tunataka vijiji vyetu, kata zetu, wilaya zetu na mikoa yetu iwe safi bila hata chembe ya dawa za kulevya. Tukikuona kijana unayumbayumba au kuweweseka, tunakupima na tukikuta umetumia ile kitu, tunakukamata ili utuambie ni nani amekupa,” amesema na kuongea:

  “Sisi tunataka vijana wafanye kazi za kujiletea maendeleo. Kijana hawezi kuwa na maendeleo wakati hufanyi kazi, huwezi kuwa na ndoto za maendeleo wakati umelewa bangi au dawa za kulevya. Kila mmoja afanye kazi kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu,” amesisitiza.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Engusero wilayani Kiteto waliofunga barabara wakitaka asimame kuwasalimia. Alikuwa kitoka Dodoma kwenda Kiteto kwa ziara ya kazi mkoani Manyara Februari 15, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akivalishwa skafu baada ya kuwasili mjini Kibaya kuanza ziara ya kazi wilayani Kiteto Februari 15, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara, Eliakim Maswi baada ya kuwasili mjini Kibaya kuanza ziara ya wilaya ya Kiteto Februari 15, 2017.


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuibua mbinu mpya zitakazosaidia kukabiliana na changamoto zinazolikabili bonde la Ziwa Victoria ikiwemo uchafu wa ziwa hilo unaotokana na shughuli za kibinadamu.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo 15-Feb-2017 wakati anafungua mkutano wa siku Mbili unaojuisha wadau wa mazingira, wasayansi na watafiti wa bonde la Ziwa Victoria Jijini Mwanza.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema anaimani kubwa kuwa mkutano huo utakuwa ni chachu katika kuibua mbinu mpya na bora za kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaoendelea katika Bonde la Ziwa Victoria.

  Amehimiza kuwa kutokana na muhimu wa bonde hilo ni vyema wadau wote katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kujumuika pamoja katika kulinda na kuendeleza uhifadhi wa bonde hilo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa jumuiya hiyo.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema bonde la Ziwa Victoria bado linakabiliwa na changamoto nyingi hasa kuibuka tena kwa magugumaji ambayo yameathiri shughuli za uvuvi, usafiri na kuchafua maji katika Ziwa hilo hivyo ni muhimu kwa makundi yote wakiwemo wanasayansi na watafiti kuweka mikakati mipya ya kukabiliana na changamoto hizo ambazo ni tishio kwa uhai wa Ziwa Victoria.

  “Kufanya Maamuzi kwa kuzingatia ushauri wa kisayansi ni jambo zuri na la msingi katika kutunga sera ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kulinda na kuhifadhi Bonde la Ziwa Victoria kwa ajili ya manufaa ya wananchi wote”amesisitiza Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza anaimani kubwa kuwa majadiliano yatakayofanyika katika mkutano huo yatakuja na mbinu mpya ambazo zitatumika katika kuhifadhi na kuendelea Bonde la Ziwa Victoria.

  Katika Mkutano huo wa siku Mbili unaofanyika Jijini Mwanza jumla ya mada 44 zitawasilishwa na kujadiliwa kwa kina na wadau wa mazingira, wanasayansi na watafiti.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan pia alitembelea mabanda mbalimbali ya maonyesho katika viwanja vya hoteli ya Malaika uliyopo Jijini Mwanza.

  Imetolewa na
  Ofisi ya Makamu wa Rais
  Mwanza
  15-Feb-2017

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  . Sehemu ya watu waliohudhuria wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akitafakari jambo kabla ya kuanza kwa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Augustine Mahiza akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiwa na (kushoto) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Augustine Mahiga pamoja na (kulia),Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Injinia wakiwa wamesoma kwa pamoja kabla ya kuanza kwa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0


  0 0  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akipeana mkono na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), anayeshughulikia masuala ya Nishati na Mabadiliko ya Tabianchi, Bw. Amadou Hott, (kushoto) baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao kuhusu ahadi zilizotolewa na Benki hiyo katika kuchangia maendeleo ya Tanzania kwa njia ya ruzuku na mikopo yenye masharti nafuu, katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), (Katikati) akiwa katika mkutano na ujumbe wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ukiongozwa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo anaye husika na masuala ya Nishati na Mabadiliko ya Tabia Nchi, Bw. Amadou Hott, na Ujumbe kutoka Tanzania, ambapo masuala kadhaa kuhusu uchumi, Nishati, Kilimo, Teknolojia jadidifu, yamezungumzwa ili kukuza uchumi wa nchi, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam

  Wajumbe wa mkutano wa kujadili ahadi zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kutoka Benki hiyo na Tanzania wakifuatilia maelezo kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (hayupo pichani) kuhusu umuhimu wa AfDB, katika utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kulia), Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara hiyo Bw. John Rubuga (katikati) na Afisa Mwandamizi wa Wizara Bw. John Mavura wakifuatilia mjadala kuhusu ahadi zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), katika kufanikisha maendeleo ya Tanzania, katika ukumbi wa Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam..

  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), anayeshughulikia masuala ya Nishati na Mabadiliko ya Tabia nchi, Bw. Amadou Hott, wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wengine baada ya kumalizika kwa mkutano kuhusu ahadi zilizotolewa na Benki hiyo juu ya maendeleo ya Tanzania katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam. 

  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM) .


  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (aliyesimama mbele) akiongea na Wageni waalikwa pamoja na Waandishi wa habari wakati wa hafla ya utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa kiwanja cha Baseball nchini kati ya Serikali ya Tanzania na Japan leo 15 Februari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (aliyesimama mbele kulia) akiongea na Wageni waalikwa pamoja na Waandishi wa habari wakati wa hafla ya utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa kiwanja cha Baseball nchini kati ya Serikali ya Tanzania na Japan leo 15 Februari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji wa mchezo wa Baseball mara baada ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa kiwanja cha Baseball nchini kati ya Serikali ya Tanzania na Japan leo 15 Februari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Chama cha Baseball Tanzania (TaBSA), Dkt. Ahmed Makata (aliyekaa kushoto mbele) akisaini Mkataba wa Ujenzi wa Uwanja wa Baseball, kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida.Wanaoshuhudia nyuma ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye pamoja na Mjumbe toka Japan.

older | 1 | .... | 1568 | 1569 | (Page 1570) | 1571 | 1572 | .... | 3285 | newer