Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 155 | 156 | (Page 157) | 158 | 159 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Salaam Ankal

  Kwa kweli wajumbe wa tume ya katiba wameyatendea  haki maoni ya watanzania  juu ya katiba  mpya. Ingawa  sijapata  muda  wa kusoma  kifungu hata kifungu kwa  utulivu, lakini kwa muonekano wa  awali  rasimu ni  nzuri  na itahitaji marekebisho machache  ya kimsingi.  


  Rasimu ya  katiba  imependekeza kuwepo kwa  serikali tatu, yaani ya  Muungano, ya Tanzania zanzibar(ambayo ipo kwa sasa) na ya Tanzania Bara( ambayo katika  katiba ya zamani imo ndani ya serikali ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania). Kwa  utaratibu wa tume rasimu ya katiba itajadiliwa katika mabaraza mbalimbali yalioundwa katika ngazi tofauti na baadae kwenye  bunge la katiba  na mwishowe itapigiwa kura ya maoni na itakuwa tayari mwaka 2014. Serikali , inataka   katiba hii ianze  kutumika katika uchaguzi wa mwaka 2015.
   
  Angalizo langu:
  Iwapo  katiba hii  itapita katika mchakato mzima na ikakubalika kwa wananchi kwamba  tuwe na serikali tatu. Serikali  ya Muungano itakuwa na katiba, Serikali ya Tanzania Zanzibar  wanayo katiba yao, Serikaliya  Tanzania bara itakuwa haina katiba yake, hivyo basi  tutabidi  tuanze  mchakato mpya  wa kupata  katiba ya serikali ya Tanzania bara mwaka 2014. Hili linaweza  kuchukua muda mrefu na pengine kuchelewesha au  kuhairisha  uchaguzi wa mwaka  2015.
   
  Sijui serikali na wanasiasa wanaliangaliaje  hili.
  Wadau wa blog je mna mawazo gani  kuhusu angalizo hili?

  0 0

  Katibu wa Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) Tawi la Tanzania Dkt Thomas Kashilillah akimpa muhtasari Mwenyekiti wa CPA Tawi la Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) wakati wa kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika kwenye Ofisi ya Bunge mjini Dodoma mapema leo.

  Afisa Dawati wa CPA Ndugu Saidi Yakubu akiwapitisha wajumbe kwenye dondoo za taarifa ya kikao kilichopita.
  Mwenyekiti wa CPA Tawi la Tanzania Mhe. Mussa Aaazn Zungu akiendesha kikao cha Kamati Tendaji.
  Mhe. John Shibuda (kulia), Mjumbe, akichangia kwenye kikao hicho ambacho kinafanya maandalizi ya kumchagua Mwenyekiti wa CPA tawi la Afrika.
  Makamu Mwenyekiti CPA Tawi la Tanzania Mhe. Beatrice Shelukindo akifafanua jambo la kimkakati.
  Mjumbe wa Kamati Mhe. Zainab Vulu akielezea uzoefu wake ndani ya CPA.Picha na Prosper Minja - Bunge.

  0 0


  0 0

  WAREMBO wanaotarajia kupanda jukwaani kesho Ijumaa kuwania taji la kitongoji cha Kigamboni mwaka huu "Redd's Miss Kigamboni 2013" katika shindano litakalofanyika kwenye ukumbi wa Navy Beach kuanzia saa 2:00 usiku hapa jijini Dar es Salaam wanaingia kambini leo katika hoteli ya Hope Country iliyoko Kigamboni.

  Akizungumza na gazeti hili jana, Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, alisema kuwa mkuurugenzi wa hoteli hiyo ameamua kuwapatia malazi warembo wa kitongoji hicho ili kuwafanya waweze kujiandaa vyema na shindano hilo wakiwa pamoja na wametulia.

  Alisema kwamba anaamini mshindi wa taji hilo mwaka huu atakiwakilisha vyema kitongoji hicho katika mashindano ya Redd's Miss Temeke na baadaye fainali za Taifa za Redd's Miss Tanzania zitakazofanyika mwezi Septemba mwaka huu.

  Somoe alisema kwamba Kamati ya Miss Kigamboni imejiandaa kufanya onyesho lililo na kiwango cha juu na wadau wa sanaa hiyo watarajie kuona mshindi anapatikana na kwenda kutetea taji la Redd's Miss Temeke kama iling'ara mwaka jana.

  Aliitaja bendi ya FM Academia maarufu Wazee wa Ngwasuma itatumbuiza katika shindano hilo ambalo kiingilio cha viti maalum ni Sh. 10,000 na viti vya kawaida ni Sh. 5,000.

  Mkurugenzi wa hoteli ya Hope Country, Geofrey Mugisha, alisema kuwa ameamua kudhamini shindano hilo kwa sababu yeye ni mkazi wa Kigamboni na anaamini kupitia shindano hilo washiriki watafanikiwa kutimiza ndoto zao.

  Aliongeza kuwa mpaka sasa jumla ya warembo 12 wanaendelea na mazoezi hapa jijini chini ya Blessing Ngowi. Aliwataja washiriki watakaopanda jukwaani kuwania taji hilo ni pamoja na Rogathe Michael, Irene Rajab, Magdalena Olotu, Latifa Mohammed, Axsaritha Vedastus, Angella Lutataza, Sara Makembo, Amina Mussa, Ellen Sulle, Zuhura Masoud, Joyce Kamtonosye na Margareth Gerald.

  Warembo watano watakaoshika nafasi za juu kwenye shindano hilo watapata nafasi ya kushiriki kinyang'anyiro cha Redd's Miss Temeke baadaye mwaka huu.

  Baadhi ya wadhamini ambao wamethibitisha kusaidia shindano hilo ni pamoja na kampuni ya bia Tanzania kupitia kinywaji cha Redd's Premium Original, Montage Limited, Clouds Media Group, Papa Z , Silver Boutique, Jambo Leo, Machapta Production na Logikit.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Idara ya uendeshaji- uhandisi wa Vodacom Tanzania,Bw.Andrew Lupembe,akifafanua jambo kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo cha kijeshi cha mawasiliano cha jijini Dar es Salaam,wakati walipofanya ziara ya kimafunzo makao makuu ya Ofisi za Vodacom Tanzania.
  Mkuu wa kitengo cha maendeleo rasilimaliwatu wa Vodacom Tanzania,Bw.Conrad Msoma,akielezea jambo kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo cha kijeshi cha mawasiliano cha jijini Dar es Salaam,wakati walipofanya ziara ya kimafunzo makao makuu ya Ofisi za Vodacom Tanzania.
  Mkuu wa kozi ya Mawasiliano wa jeshi la wananchi (JWT) katika Chuo cha Mgulani jijini Dar es Salaam, Luteni Moshi Masawani akiuliza swali njinsi Kampuni ya Vodacom inavyoendesha huduma ya mawasiliano, wakati walipofanya ziara ya kimafunzo makao makuu ya Ofisi za Vodacom Tanzania.
  Mkuu wa Idara ya uendeshaji- uhandisi wa Vodacom Tanzania Bw.Andrew Lupembe,akifafanua jambo kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo cha kijeshi cha mawasiliano cha jijini Dar es Salaam, baada ya kufika katika moja ya kituo cha kurushia mawasiliano cha Vodacom kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.Wakati walipofanya ziara ya kimafunzo makao makuu ya kampuni hiyo.
  Mkuu wa Idara ya uendeshaji-uhandisi wa mtandao wa Vodacom Tanzania,Bw.Andrew Lupembe,akiwaelezea jambo baadhi ya wanafunzi wa chuo cha kijeshi cha mawasiliano cha jijini Dar es Salaam, Wakati walipofanya ziara ya kimafunzo makao makuu ya kampuni hiyo.
  Mkuu wa kitengo cha uendeshaji wa mtandao wa Vodacom Tanzania,Bw.Andrew Lupembe,akiwaonyesha mitungi ya gesi ya kisasa ambayo inatumika kuzima moto wanafunzi wa chuo cha kijeshi cha mawasiliano cha jijini Dar es Salaam, Wakati walipofanya ziara ya kimafunzo katika moja ya kituo cha kurushia mawasiliano cha Vodacom kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Waombolezaji wa Msiba wa Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Marehemu Albert Mangwea waliokuwa wamejitokeza kwa wingi kwenye viwanja Leader s kwa ajili ya kuaga,wakielekea kwenye gari maalum la kubeba mwili Marehemu Mangwea tayari kwa Safari ya kwenda Mkoani Morogoro kwa Mazishi ambayo yatafanyika kesho Alhamisi.
   Mwili wa Marehemu Mangwea ukiingizwa kwenye gari.
   Msafara ukiondoka kwenye viwnja vya Leaders,Kinondoni Jijini Dar tayari kwa safari ya kuelekea Mkoani Morogoro kwa Mazishi.
  Taratibu za kuaga zikiendelea.

  PICHA NA VIDEO ZA MSIBA HUU ZITAWAJIA BAADAE.

  0 0

  Ewe mshabiki wa muziki wa dansi wa hapa nyumbani uliotamba katika miaka ya sabini hadi tisini, usikose kujivinjari katika ukumbi wa maraha wa nyumbani lounge kila siku ya jumatano kuanzia saaa tatu usiku, ambapo Isaac Muyenjwa Gamba akishirikiana na mchambuzi wa muziki wa dansi Rajabu Zomboko, watakuletea disco la muziki huo pamoja na miondoko ya bakulutu, katika BAKULUTU NITE ndani ya nyumbani lounge.

  Njoo wewe na yule upate zile za Dar International, maquiz du zaire, ochestra safari sound, sikinde ngoma ya ukae , msondo ngoma nk, bila kusahau za francoo luambo makiadi, tabuley, sam mangwana na bibie mbilia bell live ambazo hazijachakachuliwa. Pichani Isaac Muyenjwa Gamba akiwa mitamboni ndani ya club ya numbani lounge akiwapagawisha vijana wa zamani.

  0 0

  Mama Salma Kikwete akifuatilia maelezo ya historia ya watu wa Parekanas waishio nchini Singapore kama yanavyotolewa na Bibi Ghazala tarehe 5.6.2013.
  Mama Salma akiangalia kazi mbalimbali za mikono ziizokuwa zikifanywa na wanawake Waperakanas wa Singapore zilizohifadhiwa kwenye makumbusho hayo.
  Mama Salma akiangalia kazi mbalimbali za mikono ziizokuwa zikifanywa na wanawake Waperakanas wa Singapore zilizohifadhiwa kwenye makumbusho hayo.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Bibi Ghazala Aziz-Scott, (a museum docent) kutembelea makumbusho ya Perakanas yaliyoko huko Singapore tarehe 5.6.2013.Picha na John Lukuwi

  0 0

  Shirikisho  la Soka Tanzania (TFF) leo limejikuta likipata aibu ya mwaka baada ya Kampuni ya Flamingo Auction Mart, kuyapiga tanganyika jeki mabasi ya shirikisho hilo kutokana na deni la zaidi ya Sh.50 milioni wanalodaiwa na Kampuni ya Safina Holding ya jijini Dar es Saalam. 
  Magari binafsi ya maofisa wa TFF wa TFF yakwia getini
  Kampuni hiyo ya Flamingo  ilitia timu kwenye ofisi za shirikisho hilo kufuatia amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni ikitaka zoezi la ukamataji magari hayo hadi Juni 30 liwe limeshakamilika.
  Fedha hizo za Safina Holding zimetokana na hifadhi ya baadhi ya timu zilizoshiriki michuano ya Kombe la Kagame mwaka jana na Yanga kuibuka kidedea. Magari ambayo yameamriwa na mahakama hiyo kukamatwa ni basi aina ya Yutong lenye namba za usajili T 581 CGR amoja na Toyota Mini Bus lenye namba za usajili T 528 ASJ. 
  Lakini tofauti na amri hiyo ya Mahakama maofisa hao wa Flamingo walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuingia kwenye mzozo na maofisa wa TFF na kuzuka zogo kubwa huku maofisa hao wa TFF kuzuia magari hayo yasichukuliwe.
  Maofisa hao wa Flamingo wakiongozwa na Meneja Operation wao Noel Nyalila walitinga kwenye ofisi hizo na kulifunga gari lenye namba za usajili T 528 ASJ aina ya Coster na kulivuta kwenye gari lao lenye namba T 972 ABJ Jay Ambe, lakini walishindwa kuondoka nalo baada maofisa wa

  Angetile Osiah akionesha barua yenye utata
  TFF  kuzuia kwenye geti. 
   Wafanyakazi hao wa TFF waliamua kuzuia kwa kuegesha magari yao binafsi getini. Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osia alisema waliamua kufanya hivyo baada ya barua ya  Mahakama alidai kuwa inaonyesha kwamba amri hiyo inapaswa kutekelezwa Juni 31 mwaka huu. 
   “ Tumelazimika kuzuia kwa sababu mwanasheria wetu amekwenda mahakamani ili kupata udhibitisho wa amri hii, kwa sababu tarehe ya kukamata magari haya ambayo ni Coster yenye namba T 528 ASJ na basi lenye namba T 581 CGR ni kweli tunadaiwa lakini tuna mpango wa kulipa,” alisema Osiah. 
  Kwa upande wake Meneja Noel alisisitiza kwamba amri hiyo ni halali na wamefika hapo ili kuitekeleza kwa kuwa hukumu ilitolewa April 23 mwaka huu, amri ikaandikwa Juni 3 mwaka huu, ambapo June 31 wanapaswa kurejea mahakamani. Hata hivyo waliomba msaada wa Polisi ili waweze kusimamia kuyachukua magari hayo, na kufanikiwa
  Basi la TFF likipigwa Tanganyika jeki


  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa Watanzania waishio Singapore na Balozi wa Tanzania nchini humo na India, Injinia John Kijazi alipokutana nao leo katika hoteli ya Swissotel jijini Singapore. Nchini humo kuna familia nne za Kitanzania ambao wote wanafanya kazi za kuajiriwa
   Rais Kikwete akiongea na Watanzania Waishio Singapore alipokutana nao leo
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya kumbukumbu na Watanzania waishio Singapore baada ya kuongea nao leo. Kulia ni balozi wa Tanzania nchini humo na India

  0 0

  Katibu wa asasi isiyo ya kiserikali ya Mategemeo Women Association,Viola Lindikikok akitoa mada katika mdahalo wa elimu ya uraia ulioandaliwa na asasi hiyo na kuwashirikisha zaidi ya vijana 100 kutoka katika kata za lemara na Daraja mbili za jijini Arusha,pembeni yake ni wahamasishaji katika mdahalo huo.
  Mkuu wa kitengo cha polisi jamii mkoani Arusha,Mary Lugola akitoa semina ya elimu ya uraia iliyoandaliwa na taasisi ya Mategemeo Women Association ya jijini Arusha.(picha na moses mashalla).

  0 0

  Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya simu nchini TTCL wakijumuika kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo wafanya kazi hawo walikuwa wakiungana na watu wote duniani kuadhimisha siku hiyo ambapo wamewaomba wananchi kuwa na moyo wa kufanya usafi katika maeneo yanayowazunguka na kuto tupa takataka ovyo TTCL ina azimisha siku hiyo kwa kaulimbiu yao ya 'TTCL  huleta watu karibu'
  Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya simu nchini TTCL wakijumuika kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya simu nchini TTCL wakijumuika kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo.

  BAAZI YA MAOFISA WA TTCL WAKIWA NA MAFAGIO KWA AJILI YA KUSAFISHA MAZINGIRA YA MAENEO YA HOSPITALI YA TAIFA.


  0 0

  Balozi wa Tanzania BENELUX na Jumuiya ya Ulaya  Dr. Diodorus Buberwa Kamala  (mwenye tai yenye rangi ya taifa) akiongoza Ujumbe wa Tanzania kushiriki kikao cha 97 cha Baraza la Mawaziri wa Nchi za Afrika, Caribbean  na Pacific (ACP) kinachofanyika Brussels. Kikao hicho kinajadili masuala ya ushirikiano ya Nchi za ACP na kuweka mikakati ya kuanzisha Benki ya Nchi za ACP, Ushirikiano mpya wa Nchi za ACP, kuimarisha uchumi wa Nchi za ACP na kuandaa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za ACP na Jumuiya ya Ulaya unaotarajiwa kufanyika Kesho Brussels.

  0 0


  KUONA PICHA ZAIDI

  AU 

  0 0

  Big Brother The Chase, the 91-day reality series, produced for M-Net’s AfricaMagic, is being screened live 24/7 on DStv channels 197 and 198. For more information log onto www.bigbrotherafrica.com. Pictured here: Feza
  Big Brother The Chase, the 91-day reality series, produced for M-Net’s AfricaMagic, is being screened live 24/7 on DStv channels 197 and 198. For more information log onto www.bigbrotherafrica.com Pictured here: Nando

  0 0

  Ikiwa ni sehemu ya udhamini wake, bia ya Kilimanjaro Premium Lager imewapa vifaa vya michezo Simba na Yanga kwa ajili ya michuano wa Kombe la Kagame iliyopangwa kufanyika kuanzia tarehe 18 Juni mwezi huu.

  Akikabidhi vifaa hivyo Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema, ‘‘ Bila ubishi Simba na Yanga ndio klabu kubwa za mpira Tanzania na zote zimefika katika fainali za mchuano wa Kombe la Kagame kwa mara ya 19 sasa, haya ni mafanikio makubwa kwa hizi timu, kama wadhamini wakuu wa timu hizi, Kilimanjaro Premium Lager inaziunga mkono Simba na Yanga katika harakati zao kucheza tena fainali za michuano hii ya kusisimua na ya kihistoria.

  Aliongeza kuwa Kombe la Kagame ni mashindano makubwa Africa mashariki na kati, na ni jukwaa bora kwa wachezaji wetu kuonyesha vipaji vyao dhidi ya wachezaji wa viwango vya juu katika kanda hii lakini pia ni jukwaa zuri kwa wale wanaounda timu za taifa kuchagua wachezaji.  “Ushirikiano huu baina ya Bia ya Kilimanjaro na klabu hizi ni mizizi inayotokana na maadili katika kazi, kufanya kazi kama timu na ile kiu ya mafanikio. Na mafanikio ya ushirikiano huu ni pamoja na kushuhudia mara kwa mara timu hizi mbili zikitoa wachezaji kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) ambao wamekuwa na matokeo mazuri chini ya udhamini wa Bia ya Kilimanjaro.

  Tutaendelea kusaidia timu hizi, na kuhakikisha tunapeleka mpira wa nchi hii kwenye kilele cha mafanikio.

  Meneja wa Bia ya Kilimanjaro pia aliwataka Simba na Yanga kuhakikisha wanaiwakilisha nchi yetu vizuri katika mchuano huu mkubwa wa vilabu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kuwasihi kuchukua ushindi na kurudi na kombe la 12 la Kagame kwa mashabiki wanaosubiria kwa hamu.

  0 0

  Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili ulio wakutanisha wadau wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/ AIDS, leo kwenye ukumbi Wa Nssf Waterfront Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia akielezea changamoto wakati wa mkutano wa siku mbili ulio wakutanisha wadau wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/ AIDS, leo kwenye ukumbi Wa Nssf Waterfront Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/ AIDS, Dr Ellen M konya Senkoro akielezea mafanikio ya Taasisi hiyo.
  Wadau mbalimbali wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/ AIDS wakiwa kwenye mkutano huo.
  Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda,Rais Mstaafu, Mh. Benjamin Mkapa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia akiwa kwenye picha yapamoja na wajumbe wa Bodi ya wadhamini ya (BMAF)mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo.
  Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda,Rais Mstaafu, Mh. Benjamin Mkapa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadhamini (BMAF)mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo.

  0 0


   Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja (kulia) akimvisha nishani ya utumishi ulio Tukuka Tanzania ACP Hawa M. Simon ambaye pia ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa.

   Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja akimvisha Nishani ya utumishi mrefu na tabia njema SGT Yusufu F. Nzunda kutoka chuo cha Magereza Kiwira 


   Kamishina Jenerali wa Magereza CGP John C. Minja Akimpongeza Askari mara baada ya kutunukiwa nishani ya utumishi mrefu na Tabia njema.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, Bi. Julieth Rugeiyamu Kairuki akiinadi Tanzania katika mkutano wa wafanyabiashara wa Tanzania na Singapore katika hoteli ya Swissotel jijini Singapore, ikiwa ni mara yake ya kwanza toka ashike wadhifa huo hivi karibuni.

older | 1 | .... | 155 | 156 | (Page 157) | 158 | 159 | .... | 3284 | newer