Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

WAZIRI MWIJAGE AZINDUA AWAMU YA PILI YA MAFUNZO YA WAJASILIAMANI WASICHANA YA TAASISI YA MANJANO

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji ,Charles Mwijage amewataka watanzania kuwekeza katika mfumo unaoweza kutoa ajira za moja kwa moja kwa vijana kama ilivyo katika kampuni ya Manjano Foundation.

Mwijage amesema hayo mapema leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mafunzo ya wanafunzi 30 juu ya masuala ya urembo yanayoendeshwa ta tasisi ya Manjano Foundation ya hapa hapa nchini.

“huyu ni moja ya wawekezaji ambao wanapaswa kuungwa mkono na kila mmoja kwani ameamua kuwekeza kwa kutengeneza bidhaa ambazo zinatumia malighafi kutoka hapa hapa nchini na kuamua kuwawezesha wanawake wadogo kupata mafunzo hili waweze kuingiza pesa kupitia bidhaa hizo” amesema Waziri Mwijage.

Mwijage ameongeza kuwa mbali na Manjano foundation kutoa elimu ya ujasiliamali kwa wasichana hao pia ipo katika mpango kabambe wa kujenga kiwanda mjini kibaha ambapo tayari wameshapata ekeri tatu kwa ajili yakujenga Godown ambalo litasaidia kufanya uzalishaji.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Manjano Foundation Shekha Nasser amesema kuwa wasichana ambao wanapata mafunzo kutoka tasisi hiyo wanaweza kuingiza kiasi cha Milioni mbili mpaka tatu kwa mwezi.

Aidha ametaja kuwa program hiyo katika mwaka hu itaweza kuwafikia wanawake katika mikoa mitano nchini hili waweze kujikwamua kiuchumi.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akipata maelezo kutoka kwa Mwasisi wa Taasisi ya Manjano na Mmiliki wa Shear Illusions, Shekha Nasser  kuhusu darasa linalotumika katika ufundishaji wa wasichana hao leo katika ofisi ya Shear Illusion iliyopo jengo la Millenium Tower jijini Dar
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akizungumza na wanafunzi wa Manjano Academic mara baada ya kufika na kujionea mafunzo hayo leo katika ofisi ya Shear Illusion jijini Dar
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya kuwawezesha wanawake kiuchumi ijulikanayo kama "Manjano Dream Makers" kwa awamu ya pili iliyozinduliwa leo na waziri huyo katika ukumbi wa LAPF Millenium Towers jijini Dar es Salaam leo.
Mwasisi wa Taasisi ya Manjano na Mmiliki wa Shear Illusions, Shekha Nasser akizungumza kuhusu uzinduzi rasmi wa program ya ajira kupitia tasnia ndogo ya urembo pamoja na kufanya utambulisho kwa wageni waalikwa.
Baadhi ya washiriki walioudhuria katika uzinduzi huo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MKUU WA WILAYA AELEZA SABABU ZA KUWAAMURU WAFANYA BIASHARA KUFUNGA MADUKA YANAYOLIZUNGUKA SOKO KUU - SONGEA

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Songea Mkoani RUVUMA Pololiti Mgema , aelezea sababu kuu za kuwaamuru wafanya biashara kufunga maduka yao, ambayo yana lizunguka soko kuu la Songea

TAASISI YA CSI YAIKABIDHI DMF MSAADA WA MAVAZI YA WATOTO NJITI

$
0
0
Mkurugenzi wa Taasisi ya Childbith Survival International (CSI) Tanzania, Stella Masala Mpanda akikabidhi kwa Mkuu Msaidizi wa Kitengo cha Elimu wa Taasisi ya DMF, Rahma Amood, sehemu ya mavazi maalum ya Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti), makabidhiano yaliyofanyika katika Ofisi za DMF, Victoria jijini Dar es salaam leo. Mavazi hayo yametolewa ikiwa ni msaada kutoka Taasisi hiyo ya CSI inayosaidiana na Serikali katika kupungiza vifo vya wanawake na watoto, kuwafundisha wasichana namna ya kujikwamua kimaisha na mambo mengine mengi ya kijamii. Sehemu ya msaada huo ni pamoja na Kofia za watoto hao, soksi pamoja na pempas.

MUHIMBILI KUFANYA UPASUAJI WA KWANZA KWA WATOTO KUPITIA MATUNDU MADOGO

.USAFI HAUHITAJI SIASA- RC MAKALLA.

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA KUSHIRIKIANA HOSPITALI YA BLK YA NCHINI INDIA WATOA HUDUMA YA MATIBABU YA MOYO BILA YA KUFUNGUA KIFUA KWA WAGONJWA 16

$
0
0
Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge (kushoto) na Subhash Chandra (kulia) kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India wakimwekea mgonjwa kifaa kitakachosaidia moyo kupata umeme kwa jina la kitaalam Pacemaker . JKCI kwa kushirikiana na BLK hospital kwa kutumia mtambo wa Cath Lab wamewafanyia wagonjwa 16 huduma mbalimbali za matibabu ya moyo ya bila kufungua kifua (Catheterization).
Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge (kushoto) na Subhash Chandra (kulia) kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India wakimwekea mgonjwa betri ambalo litatumiwa na kifaa kitakachosaidia moyo kupata umeme kwa jina la kitaalam Pacemaker . JKCI kwa kushirikiana na BLK hospital kwa kutumia mtambo wa Cath Lab wamewafanyia wagonjwa 16 huduma mbalimbali za matibabu ya moyo ya bila kufungua kifua (Catheterization).
Daktari bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akimuhudumia Monica Mahenge ambaye amelazwa katika Taasisi hiyo baada ya kufanyiwa matibabu ya moyo kupitia mishipa ya damu bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab . Monica ni mmoja kati ya wagonjwa 16 ambao JKCI kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India walitoa huduma za matibabu ya kuzibua milango ya moyo (Valve), balloon mitral valve procedure (Valvuloplasty), kuzibua mishipa ya damu ya moyo, kufunga kifaa kitakachosaidia moyo kupata umeme (Pacemaker) na kuangalia utendaji kazi wa Moyo.
Madaktari bingwa wa Moyo, Wauguzi, Technologists, wataalam wa dawa za usingizi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kumpatia mgonjwa huduma za matibabu ya kuzibua milango ya moyo (Valve) bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab .
Kazi ya kutoa huduma ya matibabu ya Moyo kwa mgonjwa kupitia mishipa ya damu bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab ikiendelea.


Picha na Anna Nkinda – JKCI

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APOKEA MADAWATI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) baada ya kupokea Sh. milioni 5.5 ukiwa ni mchango wa watumishi wa Ofisi hiyo kwa ajili ya madawati wilayani Ruangwa. Makabidhiano hayo yalifanyika, Ofisini kwa Waziri Mkuu mjini Dodoma Februari 14, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) baada ya kupokea mchango wa watumishi hao wa sh. milioni 5.5 kwa ajili ya madawati wilayani Ruangwa. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu mjini Dodoma Februari 14, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mchango wa sh. milioni 5.5 kutoka kwa Mhasibu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Rose Makange (katikati)ukiwa ni mchango wa watumishi wa TAMISEMI kwa ajili ya madawati wilayani Ruangwa. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu, mjini Dodoma Februari 14, 2017. Kulia ni Rose Nyoni. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na baadhi ya watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) baada ya kupokea mchango wa watumishi hao wa sh. milioni 5.5 kwa ajili ya madawati wilayani Ruangwa. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu mjini Dodoma Februari 14, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SUMA JKT KUJENGA BANDARI KAVU RUVU

$
0
0
Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imetiliana saini Mkataba wa ujenzi wa Bandari Kavu na Shirika la Uzalishaji mali la Jeshi la kujenga Taifa (Suma JKT), eneo la Kwala – Ruvu mkoani Pwani.

Mkataba huo wa zaidi ya shilingi bilioni 7.2 unaitaka Suma JKT kukamilisha bandari hiyo katika kipindi cha wiki Tisa kuanzia sasa ambapo tayari eneo la Hekta 500 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi huo.

Akizungumza jijini Dar es salaam leo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema ujenzi huo utapunguza msongamano bandarini na katika jiji la Dar es salaam kwa kuwa magari mengi ya mizigo yanayokuja bandarini kuchukua mizigo sasa yataishia katika bandari hiyo.

“Mizigo itasafirishwa kwa njia ya reli kutoka bandarini kwenda Ruvu, hivyo magari ya mizigo hayatafika Dar es salaam na hivyo kupunguza msongamano”, amesema Waziri Mbarawa.Aidha, Profesa Mbarawa ameitaka Suma JKT kufanya kazi kwa uadilifu na kwa muda mfupi ili kuiwezesha mipango na mikakati ya Mamlaka hiyo kufanikiwa kwa urahisi.

Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa amesema Mamlaka hiyo itaanza ujenzi wa gati lenye urefu wa mita 300 katika bandari za Dar es salaam na Mtwara ili kuwezesha meli kubwa kuweza kutia nanga na kuongeza ufanisi wa Bandari nchini.“Upanuzi wa Bandari za Dar es salaam na Mtwara utavutia wasafirishaji wengi kutumia bandari hizi, hivyo wafanyakazi wote wa Mamlaka hii wafanye kazi kwa bidii na weledi”, amesisistiza Waziri Mbarawa.

Kwa upande wake Mwanasheria mkuu wa JKT, Kanali John Mbungo, amemhakikishia Waziri huyo kuwa kazi ya ujenzi huo itafanyika kwa ubora na katika kipindi kilichopangwa.Ujenzi wa Bandari Kavu katika eneo la Ruvu ni mkakati wa Serikali wa kupunguza msongamano katika jiji la Dar es salaam.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko (Wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kulia) kabla ya kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa bandari kavu baina ya TPA na Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la kujenga Taifa –SUMA JKT jijini Dar es salaam.



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko (Wa pili kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Shirika la uzalishaji Mali Jeshi la kujenga Taifa –SUMA JKT Kanali John Mbungo, (Wa pili kulia), wakitiliana saini mkataba wa ujenzi wa bandari kavu katika eneo la Kwala-Ruvu mkoani Pwani. Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko (kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Shirika la uzalishaji Mali Jeshi la kujenga Taifa –SUMA JKT Kanali John Mbungo (Kulia) wakikabidhiana mikataba ya ujezi wa wa bandari kavu katika eneo la Kwala-Ruvu mkoani Pwani. Katikati ni Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akishuhudia makabidhiano hayo.
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa(Katikati), akisisitiza jambo kwa watendaji wa Mamlaka ya Bandari (TPA) mara baada ya kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa wa bandari kavu katika eneo la Kwala-Ruvu mkoani Pwani.

Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

PROF. MBARAWA AKAGUA UJENZI FLY OVER YA TAZARA

$
0
0


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi ya Sumitomo Mitsui anayejenga barabara ya juu (Fly over) ya Tazara kuongeza kasi ya ujenzi huo ili  kupunguza muda wa ujenzi wa mradi huo.

Akizungumza katika eneo la ujenzi huo leo jijini Dar es salaam, Profesa Mbarawa amepongeza hatua iliyofikiwa sasa lakini pia amesisitiza kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi huo ili wananchi waweze kunufaika.

“Hakikisheni badala ya kutumia miezi 35 kujenga mradi huu, mnatumia miezi pungufu zaidi ili kuwawezesha wananchi na wadau wengine kunufaika na fursa za mradi huu”, amesisitiza Waziri Mbarawa.

Aidha, Amewataka wafanyakazi wote katika mradi huo kufanya kazi kwa bidii na uaminifu mkubwa kwa kuwa Serikali ina mpango mwengine wa kujenga Fly over kama hiyo itakayowawezesha kupata tena fursa ya ajira. 

Hatua hiyo itapelekea kuwezesha wananchi kunufaika na mradi huo mapema, hivyo kupunguza gharama wanazozipata kutokana na msongamano wa magari uliopo sasa jijini Dar es salaam.

Naye, Balozi wa Japan nchini Bw. Masaharu Yoshida, amemhakikishia Waziri huyo kuwa ujenzi wa mradi huo utamalizika kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa, hivyo kuondoa changamoto ya msongamano katika barabara ya Nyerere na Mandela.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa miradi kutoka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Crspinius Ako, amesema kati ya nguzo 66 zinazohitajika kwenye awamu ya kwanza ya ujenzi huo, tayari nguzo 43 zimeshasimikwa ardhini, hali itayopelekea ujenzi huo kwenda kwa kasi.

Mpaka sasa mradi huo uliozinduliwa tarehe 1 Disemba 2015 umekamilika kwa asilimia 25.3 na zaidi ya shilingi bilioni 96.5 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa mradi huo ambao utakamilika mwezi Oktoba mwaka 2018.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkandarasi wa kampuni ya Sumitomo Mitsui Eng. K Tsuji, anayejenga barabara ya juu (TAZARA fly over) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi huo jijini Dar es salaam.
Mkandarasi wa kampuni ya Sumitomo Mitsui Eng. Mitsui Eng. K Tsuji, (Wa pili kulia) akifafanua jambo kuhusu ramani ya ujenzi wa barabara ya juu (TAZARA fly over) kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa tatu kulia) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi huo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akikagua maendeleo ya Ujenzi wa barabara ya juu (TAZARA fly over), jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisalimiana na baadhi ya mafundi wanaojenga barabara ya juu (TAZARA fly over), jijini Dar es salaam. Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MADAKTARI BINGWA WA MARADHI YA MOYO KUTOKA SHIRIKA LA SAVE A CHILD HEART KUTOKA ISRAEL WAPO ZANZIBAR KUWAFANYIA VIPIMO WATOTO WANAOSUMBULIWA NA MARADHI HAYO

$
0
0
Waziri wa Afya Mahmoud Thabi Kombo akipata maelezo kutoka kwa Dkt. Alona Roucher kuhusu matatizo ya moyo yanayomkabili Muslim Muhd Ali kutoka mtaa wa Jangombe ambae ni mmoja kati ya watoto watakaopelekwa Israel kwa matibabu.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na madaktari wa maradhi ya moyo kutoka Israel ambao wapo nchini kuwafunyia uchunguzi watoto wenye m.aradhi hayo ambao baadhi watapelekwa Israel kufanyiwa upasuaji.
Dkt. Yifat Brosh kutoka Shirika la Save a Child Heart la Israel akimfanyia vipimo mmoja ya watoto wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.
Baadhi ya wazazi wakiwa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja wakisubiri zamu za kuwapeleka watoto wao kufanyiwa uchunguzi na madaktari bingwa wa moyo kutoka nchini Israel.Picha zote na Makame Shenga-Maelezo.

Wakazi wa Mwanza wazifurahia Simu za Smart Bomba

$
0
0
Wakazi wa jiji la Mwanza wamezifurahia simu za kisasa za Smart Bomba ambazo zilizinduliwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania hivi karibuni,Simu hizo zinazidi kuchangamkiwa na wananchi wengi hususani wakazi wa maeneo ya jiji la Mwanza na wanaozunguka mkoa huo ambapo wameshukuru kwa hatua hiyo ambayo imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya mawasiliano nchini.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati wa promosheni ya mauzo ya simu hizo inayoendelea mkoani Mwanza,baadhi ya wananchi wamesema kuwa hatua ya kampuni hiyo kuingiza sokoni simu za kisasa za Smart Bomba zinazopatikana kwa gharama nafuu imedhihirisha dhamira ya kweli ya kampuni hiyo ya kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa kidijitali.

Bw.Focus Phabian mmoja wa wananchi ambaye amenunua simu hiyo akiongea kwa niaba ya wenzake alisema kuwa Smart Phone ni mkombozi wa mawasiliano ya kisasa kwa kuwa licha ya kuwa na unafuu wa bei pia imetengenezwa kwa kuendana sambamba na mazingira halisi ya watanzania.
Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa ,Ayubu Kalufya akiitambulisha simu ya Smart Bomba kwa wakazi wa jijini Mwanza jana, kulia ni Mkuu wa Maduka ya Rejareja wa kampuni hiyo,Brigite Steven. 
Baahi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kanda ya Ziwa wakiandamana kwenye barabara ya Kenyatta jiji Mwanza jana, wakati wa kuitambulisha wa simu aina ya Smart Bomba kwa wakazi wa jiji hilo jana. 
Mkazi wa Nyasaka mkoani Mwanza Michael Alfred, akipokea simu
aina ya Smart Bomba ikiwa ni zawadi kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya ziwa ,Ayubu Kalufya,baada ya kununua moja ya simu hizo wakati wa kuzitambulisha simu hizo jijini Mwanza.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

AMSHA KIPAJI CHAKO NA SINGA WA MBEYA

TANZIA

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

RC GAMBO ATEMBELEA KATA YA KISONGO KUJIONEA MAENDELEO YA MKOA WAKE

$
0
0


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo Akikagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Engorora,Akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkoa

Na Imma Msumba, Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo Amefanya ziara katika Kijiji cha Engorora leo februari 14 na kujionea maendeleo mbalimbali hususani katika sekta ya Afya kijiji cha Engorora kilichopo Kata ya Kisongo.

Mh: Gambo akiwa kwenye ziara hiyo amekagua Kituo cha Afya kilichojengwa kijini hapo kwa nguvu za Wananchi ambapo Mkuu wa Mkoa Alisema,

" Nipende kuwapongeza wananchi wa kijiji hiki kwa kuweza kujitolea kwa nguvu zenu zote kwenye maendeleo ya kijiji hiki na Taifa kwa ujumla, Sisi kama Serikali inayoongozwa na Rais Dr. John Joseph Pombe Magufuli tumeamua kuchukua jukumu hili la kumalizia ujenzi wa Kituo hiki cha Afya,nipende tu kuwaambia wananchi wa kijiji hiki nitahakikisha kabla ya mwisho wa mwezi wa tatu, nitawaagiza watu wa Tanesco wajekuweka umeme kwenye zanahati hii,sambamba pia na watu wa Idara ya maji na wao pia wataleta huduma ya maji hapa haraka iwezekanavyo."

Mkuu wa Mkoa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Vijijini kuhakikisha kabla ya mwisho mwezi huu anaonana Mwenyekiti wa Kijiji hicho na kuweza kuweka utaratibu wa kifedha juu ya swala la kumalizia ujenzi wa Kituo hicho kwa upande wa kuweka Tiles pamoja na kufunga milango ambayo ipo tayari mpaka sasa.

Pia mkuu wa Mkoa alimalizia kwa kuwapatia wananchi wa kijiji hicho saalamu za pongezi kutoka kwa Rais Magufuli
" Mh:Rais anawasalimia sana na pia anashukuru kwa kura zenu nyingi za ndio na kumuwezesha kuwa Rais wa awamu ya Tano."HAPA KAZI TU"

Wananchi wa Kijiji cha Engerora wakifuatilia Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa makini.

Baadhi ya Wawekezaji wa Kata ya Kisongo waliojitokeza kwenye kumsikiliza Mkuu wa Mkoa

KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA, AMEWATAKA WANANCHI KUWAFICHUA WATUMIAJI PAMOJA NA WAUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA.

$
0
0

Wakazi wa mkoa Ruvuma wametakiwa kuwa mstari mbele kupinga matumizi ya madawa ya kulevya na kuwafichua wanaotumia kwani yamekuwa yakipunguza nguvu kazi ya taifa.

MAMA MAGUFULI NA MAMA MAJALIWA WATEMBELEA GEREZA LA MAHABUSU LA TABORA, WATOA ZAWADI KWA WAFUNGWA

$
0
0
MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametembelea Gereza la Mahabusu Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu gerezani hapo. 

Wake wa viongozi wametembelea gereza hilo leo (Jumanne, Februari 14, 2017) wakiwa katika ziara mkoani Tabora, ambapo Mama Janeth amesema wameamua kuwatembelea wafungwa na mahabusu hao kwa nia ya kuwafariji kwa kuwa wao ni sehemu ya jamii. 

“Vitabu vitakatifu vinasema kwamba ukiwasaidia watu wenye mahitaji utakuwa umetoa sadaka kubwa kwa Mwenyezi Mungu, hivyo tumeamua kuja kutembelea wafungwa na mahabusi kwenye gereza hili na kuwapa zawadi kwa kuwa nanyi mnahitaji faraja,” amesema. 

Amesema wameamua kwenda kuwaona wafungwa na mahabusu hao kwa lengo la kuwafariji na kuwatia moyo kwa sababu wanaimani kwamba wakitoka watakuwa raia wema na hayo wanayopitia ni sehemu ya kufanya marekebisho ya tabia. 

“Ni siku kubwa kwangu, nimejifunza mengi baada ya kufika hapa. Kitendo cha kwenda kuwaona wenye mahitaji wakiwemo wagonjwa, wafungwa ni jambo jema tunaamini hizi zawadi tulizozitoa zitawasaidia kwa sababu tunajua mnamahitaji mengi,” amesema. 

Katika gereza hilo wake hao wa viongozi wamekabidhi zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu, ambapo mwakilishi wa wafungwa hao Deo Kitave aliwashukuru kwa niaba ya wenzake. “Tunawashukuru kwa kutukumbuka, tunamuomba Mwenyezi Mungu muendelee kuwa na moyo huo,”. 
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea risala toka kwa Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tabora Mkuu wa gereza SSP Nahman Koko wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa mahabusu.

 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi zawadi  Naibu Mkuu wa gereza la Mahabusu Tabora Mrakibu wa Magereza Godliver Makwaruzi  wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14, 2017.
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa zawadi  Naibu Mkuu wa gereza la Mahabusu Tabora Mrakibu wa Magereza Godliver Makwaruzi  wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14, 2017
 Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitoka katika gereza la wanawake Tabora walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14, 2017
 Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri akiwashukuru sana kutembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14, 2017

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

JAFO-FEDHA ZA MIRADI YA AFYA ZITUMIKE KIKAMILIFU ILI KUJIBU CHANGAMOTO ZILIZOPO

$
0
0

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Selemani Jafo,amesema mkoa wa Pwani umepokea Bil.2.340 zitakazotumika kugawanywa kwenye vituo vya afya na zahanati 234 zilizopo mkoani hapo ili kuboresha na kutatua changamoto zilizopo.

Amesema fedha hizo zimetolewa kutoka katika mpango wa malipo kwa ufanisi unaotekelezwa kwa ushirikiano baina ya bank ya dunia na serikali ya Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.Aidha Jafo amewasihi wakurugenzi,wenyeviti wa halmashauri na mganga mkuu wa mkoa huo,kusimamia fedha hizo ili ziweze kuleta tija .

Katika hatua nyingine,ametoa wiki moja hadi kufikia februari 21 mwaka huu,kwa waganga wakuu wa mikoa (RMO)na makatibu tawala wa mikoa (RAS)kote nchini,kuhakikisha wanapeleka account za bank zinazotumiwa katika vituo na zahanati zote.Alhaj Jafo,aliyasema hayo wakati akizungumza na wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri pamoja na waganga wakuu wa wilaya mkoani Pwani.

Alisema kati fedha hizo kila zahanati na kituo cha afya kitapatiwa kiasi cha sh.mil 10 ili kuboresha na kutatua kero sugu zilizokuwa zikiwasumbua.“Kuna zahanati na vituo vya afya ambavyo havina magodoro,mapaa yamebomoka,,hakuna vyoo huku nyumba za mganga wa kituo nayo ikiwa haina choo”“Kuna maeneo mengine hayana hata vitanda vya kujifungulia,akinamama wanapata shida yaani unahofia wanaweza kuondoka hata na magonjwa mengine,hivyo kwa mazingira haya fedha hizi endapo zitatumika kikamilifu zitaondoa matatizo hayo”alisema Jafo.

Alisema katika miaka iliyopita fedha hizo zilikuwa hakuna hivyo kutokana na mpango huo kuanza,wahakikishe wanaleta matokeo chanya kwa kujibu changamoto zilizokuwa zikiwakabili.Jafo alisema hatofurahishwa akisikia mradi huo haujafanikiwa katika mkoa wa Pwani na mikoa mingine 8 ambayo ipo kwenye mradi huo kwa majaribio hapa nchini.
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Selemani Jafo,akizungumzia na wakurugenzi,wenyeviti wa halmashauri,waganga wakuu wa wilaya mkoani Pwani,jana.(Picha na Mwamvua Mwinyi) 


Bweni la Itamba Sekondari Makete Likiteketea Kwa Moto Leo

$
0
0
Bweni la Wasichana la shule ya sekondari Itamba iliyopo katika tarafa ya Matamba wilayani Makete mkoani Njombe leo limeteketea kwa moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika.


Angalia video ya tukio hilo hapo chini:-

WATAALAMU WA CHANJO WANAKUTANA ZANZIBAR KUANDAA MIKAKATI YA KUHAKIKISHA MARADHI YA POLIO HAYAREJEI TENA NCHINI.

$
0
0
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar 


Wadau wa chanjo wa Tanzania na nchi jirani wapo Zanzibar kwa ajili ya mkutano wa kutathmini maradhi ya polio na matayarisho ya kuandaa mpango wa kukabiliana na maradhi hayo iwapo yatajitokeza.

Akizungumza katika mkutano huo unaofanyika Zanzibar Beach Hotel Mbweni, Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohd Suleiman amesema maradhi ya polio sio tatizao Tanzania kwa sasa, lakini bado hatupo salama kutokana na nchi jirani kuendelea kusumbuliwa na maradhi hayo.

Amesema Tanzania mara ya mwisho kuwa na mgonjwa wa polio ni mwaka 1997 lakini nchi ya Somalia, Jamhuri ya Watu wa Kongo na Nigeria bado wanakabiliwa na maradhi hayo na watu wake wanakuja kwa shughuli mbali mbali za maisha hivyo matayarisho ya kujiandaa ni jambo muhimu.

Amewashauri wazazi kuendelea na utaratibu wa kuwapeleka watoto wao katika vituo vya afya mara baada ya kuzaliwa kupatiwa chanjo zote ili kuhakikisha maradhi hayo na mengine yanayowasumbua hayarejei tena.Meneja wa Kitengo cha chanjo Zanzibar Dkt. Yussuf Haji Makame amesema hali ya chanjo iko vizuri baada ya asilimia 95 ya watoto wanaostahiki kupatiwa chanjo kupatiwa chanjo hizo.

Amesema kitengo hivi sasa kinaendelea kufuatialia kwa karibu watoto wenye umri kuanzia miaka 15 wanapopata ulemavu wa ghafla ili kujua chanzo chake na amewataka wazee wanapobaini kijana wao kupata tatizo hilo kumpeleka hospitali mapema.

Mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Andemichael Ghirmay ameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa juhudi kubwa za kupambana na polio na kufanikiwa kupewa cheti maalumu mwaka 2015.Amesema Shirika hilo litaendelea kuunga mkono juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na serikali na ametaka juhudi za pamoja za wadau na jumuiya za kimataifa kuhakikisha polio na maradhi mengine yanayozuilika kwa chanjo sio tatizo tena Zanzibar.

Akifungua mkutano huo Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Abdalla amewataka wadau wa chanjo kutoridhika na hatua iliyofikiwa ya kutokomeza Polio bali waendelee kuweka mikakati bora zaidi itakayo hakikisha maradhi hayo hayarejei.

Mkutano huo wa siku tatu unaowashirikisha wataalamu wa chanjo kutoka Shirika la Afya ulimwengu (WHO) na Shirika la kuhudumia watoto (UNICEF) utaundaa Kamati ya Maafa ya polio ya kujiweka tayari wakati wote kukabiliana nayo yatakapo tokea.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Abdalla akifungua Mkutano wa siku tatu wa matayarisho ya Mpango wa kupambana na maradhi ya Polio Tanzania katika Ukumbi wa Zanzibar Beach Resourt Mbweni.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa matayarisho ya Mpango wa kupambana na Polio wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kutoka Afrika Kusini Dkt. Mercy Kamupira akiwasilisha mada katika mkutano unaozungumzia maradhi ya Polio unaofanyika Zanzibar Beach Resourt Mbweni.
Washiriki wa mkutano unaojadili ugonjwa wa Polio wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Abdalla.Picha na Makame Mshenga-Maelezo.


…………..

Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images