Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1566 | 1567 | (Page 1568) | 1569 | 1570 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Na Raymond Mushumbusi WHUSM.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amevishauri vyombo vya habari nchini kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli katika vita dhidi ya madawa ya kulevya nchini.

  Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliofanyika katika Chuo Kikuu huria cha Tanzania na kusisitiza kuwa vyombo vya habari viwe sehemu ya kuwaunganisha watanzania katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.

  “Wanahabari tuliunganishe taifa letu tuwe kitu kimoja katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya” alisisitiza Mhe. Nnauye.

  Ameongeza kuwa sasa ni wakati wa watu wote kuungana kwa pamoja zikiwemo tasnia zilizopo katika Wizara yake za Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwani vita hii ni ya watanzania wote na sio mtu mmoja au Serikali pekee.

  Aidha Mhe. Nape amevitaka vyombo vya habari kutobaki nyuma katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya na kuhakikisha  haki inatendeka na vita dhodi ya madawa ya kulevya vinashinda.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau Redio na vyombo vya habari kwa ujumla katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es Salaam.  0 0

  Na.Vero Ignatus.

  Sherehe za kumuaga aliyekuwa Jaji mfawidhi wa mahakam kuu kanda ya Arusha Mhe,Fatuma Hamis Masengi ,zimefanyika leo katika mahakama kuu ya ndanda hiyo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo majaji,mahakimu,mawakili wasajili wa mahama watendaji pamoja na wageni waalikwa.

  Sherehe hizo zimeanza majira ya saa asubuhi katika mahakama ya wazi ambapo Jaji Fatuma alianza kufanya kazi mnamo mwaka 1974 katika mahakama ya mwanzo na kuendelea kuitumikia mahakama hadi alipoteuliwa kuwa jaji mfawidhi mahakama kuu.

  Amewataka majaji na mahakimu pamoja na wale wote wanaofanya kazi za kimahakama wafanye kazi kwa kumtegemea Mungu huku wakijua kazi yeyote ina changamoto zake hivyo ni vyema kufanya kazi kwa weledi zaidi na kwa kuzingatia sheria inavyosema,wakimtendea haki kila mtu kwa stahiki.

  Amewataka wanawake kutokukata tamaa huku akisema kuwa wanawake wanaweza kuliko wanaume japo kuwa wakati mwingine wanaume wanaona kama vile wanawake ni wanyonge lakini mwanamke anaweza pale ambapo anasimama kwa nafasi yake na kulitumikia kusudi kwa wakati na weledi.
  Mhe.Jaji Mstaafu wa mahakama kuu kanda ya Arusha Fatuma Hamis Masengi 
  Picha ya pamoja kati ya waheshimiwa majaji kanda ya Arusha na Kilimanjaro ,Wakwanza kulia ni mhe,Jaji Dkt.Modesta Opiyo,Wakwanza kushosto ni mhe,Jaji Salma Maghimbi,akifuatiwa na aliyeko kushoto kwake mhe,Jaji Sekela Mushi,akifuatiwa na mhe,Jaji mstaafu Fatuma Hamis Masengi wakiwa na majaji wengine pamoja na waheshimiwa mahakamu.Picha na Vero Ignatus Blog.
  Picha ya pamoja ya waheshimiwa majaji pamoja na mawakili wa serikali,na wale wa kujitegemea.Picha na Vero Ignatus Blog.


  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  JAJI Mkuu anatarajia  kupokea  orodha ya  majina ya mahakimu na majaji  ambao wanadaiwa kuvuruga kesi za watu wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

  Hayo ameyasema leo  Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Rogers Sianga wakati wa mkutano wa viongozi mbalimbali wa kitaifa na waandishi wa habari ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  kwa ajili  kupambana na dawa za kulevya.

   Sianga amesema kuwa kesi zimevurugwa na mahakimu na majaji. hivyo wale wote watakaobainika kuhusika watashitakiwa na hata wawe na mali ambazo wamezipata kwa biashara hiyo zitataifishwa.

  Amesema kuwa watazunguka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ili kuhakikisha mtandao huo unapatikana na kwenda hata Zanzibar na mbinu zote wanazijua katika kufanya biashara hiyo.

  Nae Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemkabidhi orodha ya majina 97 wanaojihusisha na dawa za kulevya na kuongeza kuwa moto umewashwa dhidi ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya.

  Amesema kuwa kuna nyumba 200 zinajihusisha kufanya biashara ya madawa ya kulevya hapa jijini ambapo wote hao watafikiwa katika operesheni,ambayo mojawapo wanatarajia kuifanya usiku wa leo.

  Nae Msanii wa muziki wa kizazi kipya Khalid Mohamed almaarufu kwa jina la kisanii TID , amesema kuwa sasa ni mnyama ambae yuko tayari kupambana na watu wanaouza pamoja na kutumia dawa za kulevya na amerudi kwa kufanya kazi na kuongeza kuwa kuimba hakuitaji dawa za kulevya.

  Katika mkutano huo watu wawili wametakiwa kufika katika Kituo cha Polisi kati ambao ni Chidi Mapenzi,  Ayuob Mfaume Kiboko.

  Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Rogers Sianga 

  0 0

  MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametoa rai kwa Wanzania kujenga tabia ya kusaidia watu wasiojiweza na wenye mahitaji maalumu.

  Wake hao wa viongozi pia wamewatahadharisha watumishi wanaofanya kazi katika vituo vya kulelea wazee wasiojiweza wahakikishe misaada inayotolewa na wadau mbalimbali inawafikia walengwa bila ya kuchakachuliwa.

  Wameyasema hayo leo (Jumatatu, Februari 13, 2017) wakati walipotembelea Makazi ya Wazee wasiojiweza na walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma ya Sukamahela wilayani Manyoni Mkoani Singida.

  Katika kituo hicho wamekabidhi tani 7.5 za vyakula mbalimbali ukiwemo mchele, unga wa sembe na maharage, ambapo Mama Janeth amewataka viongozi wa kituo kuhakikisha chakula hicho hakichakachuliwi.

  Akizungumza na wazee wa makaazi hayo, viongozi mbalimbali na wananchi wanaozunguka eneo hilo Mama Janeth amesema “Naomba chakula hiki kitunzwe vizuri na hakikisheni kinawafikia walengwa na kisichakachuliwe hii ni sadaka,”.

  Kwa upande wake Mama Mary amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuwasaidia wazee wanaoishi katika makaazi ya kulelea walemavu na wasiojiweza nchini kwa sababu wanakabiliwa na changamoto nyingi.
  “Watanzania wote popote mlipo tukumbuke kutembelea vituo vya kulelea wazee kikiwepo na hiki tulichokitembelea leo cha Sukamahela na kutoa misaada mbalimbali kkwa kadri tutakavyojaaliwa,” amesema.

  Awali Mkuu wa Makazi hayo Bw. Yeremia Ngoo alisema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1974 chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii kwa lengo la kuwasaidia watu wenye ukoma na wazee wasiojiweza mkoani Singida.

  Bw. Ngoo alisema kituo hicho chenye wakazi 62 kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa wapishi ambapo kwa sasa yupo mmoja huku mahitaji yakiwa ni wapishi wanne. Pia nyumba nyingi ni chakavu na zina nyufa.

  Naye Mwenyekiti wa Wazee waishio katika makaazi hayo, Mzee Andrea Yohana aliwashikuru wake hao wa viongozi na kuwaomba waendelee na moyo huo wa kusaidia watu wasiojiweza.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa na Bibi Agnes Kamota (75) walipomtembelea nyumbani kwake katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
    Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitembelea  Zahanati ya Sukamahela katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitoa msaada wa vyakula tani 7.5  katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipokea msaada wa vyakula na vinywaji kutoka kwa Meneja wa tawi la Benki ya NMB Singida Bw. Abius Mlengwa katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipokea msada wa vyakula na vinywaji kutoka kwa Meneja wa Tawi la CRDB Manyoni Bw. Richard Karatta katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017. PICHA NA IKULU.

  0 0
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke aliyefika Ikulu kwa ajili ya Mazungumzo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika Mazungumzo na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Bhaswar Mukhopadhyay aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akizungumza na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Bhaswar Mukhopadhyay Ikulu jijini Dar es Salaam.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Wadau Bw. Nkaina na Bi Rehema wa Dallas, Texas wakiwa na nyusoza furaha sana baada ya meremeta huko  Miami, Florida USA, Jumapili 
   Bibi Harusi akiwa Na mwanae Jr Mazara
   Maharusi wakiwa Na wapambe wao
  Maharusi wakifurahia siku yao ya siku

  0 0


  0 0
  0 0


  0 0


  0 0

  SERIKALI imewataka wanahabari kusoma sheria, taratibu na kanuni zinaogusa tasnia yao ili iweze kuendelea na kuachana na kuamini kila kitu wanachoambiwa na mtu mmoja.

  Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye wakati  akizungumza katika siku ya radio duniani, hafla iliyofanyika Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam.

  "Watu someni sheria, taratibu na kanuni kwa kina ili kujua na kuzielewa, mkielewa kama kuna sheria inakwaza ukuaji wa sekta ya habari tuseme tukae chini.. " alisema Waziri Nape akijibu hoja kuhusu sheria za habari zilizopo ambazo zinadaiwa kukwaza uhuru wa ukusanyaji wa habari.

  Ilielezwa katika hafla hiyo kuwa sheria za sasa ya takwimu na habari  zinakwaza uhuru wa sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
  Katika hoja hiyo Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Redio za Jamii (COMNETA) Prosper Kwigize katika hotuba yake kwa Serikali, alisema kwamba redio hizo zinachangamoto nyingi katika utendaji wake ikiwamo sheria zilizopo,watoa habari wasioeleweka na wanazuia upatikanaji wa habari.

  Nape alisema kwamba sheria si msaafu na kwa kuwa asilimia 80 za habari zinazalishwa na serikali, waandishi wanahaki ya kupata habari hizo na kama kuna kikwazo ni lazima kitafutiwe suluhu.

  "Tukae tushindane kwa hoja tukubaliane na kuhakikisha kwamba tunarekebisha.. Bunge kazi yake ni kutunga na kufuta sheria" alisema Nape ambaye alisema kwamba sheria ya sasa imetoa nguvu kwa watoa habari na kwamba si kila habari iliyopo serikalini ni classified.
   
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye (wa pili kulia) akimpongeza Meneja wa Redio Jamii Orkonerei  FM, Baraka David Ole Maika baada ya kuwasilisha risala ya mafunzo ya ufundi kwa Redio za Jamii  wakati maadhimisho ya siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam jana. Kulia  Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fredrick Ntobi, Wa tatu kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishili wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues, Wanne kulia Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu na Menejementi ya Teknolojia  wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Dr. Edephonce Nfuka na Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari vya Jamii (COMNETA), Prosper Kwigize.
   Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
    Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akisheheresha kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya radio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam
   Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Zulmira Rodrigues akitoa neno la ukaribisho liliombatana na ujumbe maalum kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.


  0 0


  0 0

  Na Bartholomew John Wandi

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawawahakikishia Umma wa Watanzania kuwa hakuna kura yoyote inayoibiwa sikuwa ya kupiga kura, iwe Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani au Uchaguzi Mdogo wa Ubunge au Udiwani.

  Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchagzi, Kailima Ramadhan Kombwey wakati alipokutana na Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Pulisher waliotaka kujua Mchakato wa Uchaguzi hadi kuhesabu kura na kumtangaza Mshindi.
  Watu wengi vikiwamo vyama vya Siasa huwaminisha Wafuasi wao kuwa wakati wa kupiga kura huibiwa kura zao ndiyo maana huwashawishi wafuasi wao kulinda kura zao kitu ambacho hakipo

  Mkurugenzi alieleza kuwa Kabla ya siku ya Kupiga Kura, Vyama vyote vya Siasa vilivyosimamisha wagombea wao wa Urais,Ubunge na Udiwani huagizwa kuleta Mawakala wao wa Kulinda kura zao na maslahi ya Vyama vyao vya Siasa na kuwa makini na mchakato unavyoendelea Kituoni.

  Mara nyingi Mawakala wanatakiwa kutoka katika maeneo wanayoishi ili kubaini mtu ambaye hawamfahamu asiweze kupiga kura kwa kutumia kadi ya mtu mwingine.

  “Baada ya Mpiga Kura Kumpa Kadi ya Kupigia Kura, Msimamizi wa Msaidizi wa Kituo baada, hutafuta jila la Mpiga Kura huyo na anapoliona hulisoma kwa sauti kubwa ili Mawakala wa Vyama nao wasikie na kuhakikisha anayeitwa jina hilo ndye mwenyewe au siye?” alisema Mkurugenzi wa Uchaguzi.

  Kama anayeitwa jina ndiye Mpiga Kura Mwenyewe huruhusiwa kuendelea na Mchakato wa Upigaji kura lakini kama Mawakala wakiona siye mwenye jina hilo na wana ushahidi wa kutosha humzuia asipige kura.

  Mara nyingi pia baadhi ya mashabiki na wafuasi wa Vyama vya Siasa huvumisha kuwa watu waliokufa  majina yao wameonekana yametikiwa kuonyesha kuwa jina lake limetumiwa na mtu mwingine kupiga kura kuonyeha kuwa sio kweli kwa sababu Mawakala wa Vyama hivyo vya Siasa  wangembaini.

  Mkurugenzi alibainisha kuwa siyo jambo jema kwa Wakala wa Chama cha Siasa kukataa kusaini  Matokeo ya Uchaguzi ya awali yanapotangazwa kituo cha Kupigia Kura, Kwenye Kata baada ya Kujumlishwa na Kumtanga Mshindi wa Udiwani au Jimboni anapotangazwa Mshindi wa Ubunge au au Makao Makuu ya Tume anapotangazwa Mshindi wa Urais kwa sababu kwa sababu muda wote alishiriki hatua zote na hajaona mahali popote alipoona aliibiwa kura.

  Aidha, Murugenzi alisistiza kuwa kutosaini kwa Wakala wa Chama hakumzuii Mwenyekiti wa Uchaguzi kutomtangaza Mshindi wa Kiti cha Urais, Msimamizi wa Uchaguzi Ngazi ya Jimbo kutomtangaza Mshindi wa Kiti cha Ubunge au Msimamizi Msaidizi Ngazi ya Kata kutomtangaza Mshindi wa Udiwani.

  “Pamoja na hayo, hakuna hata siku moja Mawakala wa Vyama vya Siasa waliowahi kuleta ushahidi wao wa Matokeo ya awali vituoni Tume na kulalamika kuwa matokeo yaliyotangazwa ni tofauti na niliyo nayo”. Alisema Kombwey.  

  Mkurugenzi wa Uchaguzi alimalizia kwa kuwapa Wafanyakazi wa Global Publisher nafasi ya kufanya onyesho la Upigaji Kura Kituoni kwa kushiriki wenyewe nafasi zote kuanzia Mawakala, Msimamizi wa Kituo, Msimamizi Msaidizi wa Kituo na Wapiga Kura, Ujumlishaji wa Kura za Awali Kituoni za Ubunge Mpaka Jimboni na Kumtangaza Mshindi wa Kiti cha Ubunge.

  Wafanyakazi hao wa Global Publisher walipata kufahamu kuwa Mchakato wote waliofanya Kituoni hakuna mwanya wowote ulioonekana kwa Chama Chochote cha Siasa kuiba Kura au kuibiwa kura au Mtu ambaye siyo wa Kituo hicho kuruhusiwa kupiga Kura.      


  0 0

  Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) inatekeleza mradi wenye thamani ya bilioni 18 unaolenga kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es salaam.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa ufundi na uendeshaji wa Mamlaka hiyo Bw. Romanus Mwangingo wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika eneo la Kimbiji ambako ndipo mradi huo unapotekelezwa .

  “Mkandarasi anaendelea na kazi na ameleta mabomba yote na amechimba visima 15 na vitazalisha maji yatakayotumika katika Jiji la Dar es salaam na mradi unatarajiwa kukamilika machi 2017” Alisisistiza Mwangingo. Aliongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 85 na utakapokamilika maeneo ya Kigamboni,Temeke,Ilala na Jiji la Dar es salaam kwa ujumla yatanufaika kwa kupata huduma ya maji.
  Maji yakitoka kwenye moja ya Kisima Kirefu kilichochimbwa katika eneo la Kimbiji unakotekelezwa mradi mkubwa wa unaolenga kutatua changamoto ya maji katika Jiji la Dar es salaam.

  Kwa upande wa miradi mingine kama ule wa ujenzi wa Bomba kutoka Ruvu juu hadi kimara Mwangingo amesema ulikamilika mwezi oktoba 2016 na uzalishaji wa majaribio unaendelea.

  Mradi huo wenye thamani ya dola za marekani milioni 59 ni moja ya mikakati ya Serikali katika kuhakikisha kuwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam wanapata huduma ya maji safi na salama. na kuondokana na changamoto hiyo. . Aidha mradi huo utawezesha kiwango cha maji kufikia lita milioni 196 kwa siku kutoka lita milioni 82 za awali.

  Kwa upande wake Bw.Salum Hamis mkazi wa mbagala amepongeza miradi ya maji inayotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi kwa kuwa imekuwa chachu ya maendeleo katika maeneo yao. Aliongeza kuwa miradi hiyo imechochea kupunguza tatizo la maji na imewawezesha wananchi kutumia muda mwingi katika shughuli za kiuchumi na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi.
  Meneja Uhusiano wa DAWASA Bi Neli Msuya akieleza kwa waandishi wa habari faida za miradi inayoibuliwa na Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na wananchi katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es salaam.

  Katika kukabilina na tatizo la miundombinu ya maji taka katika Jiji la Dar es salaam mamlaka hiyo iko katika mchakato wa kuanza ujenzi wa mtambo mkubwa wa kuchuja maji taka katika eneo la Jangwani na kuboresha mfumo wa maji taka katikati ya Jiji.

  Mradi mwingine ni ule wa upanuzi wa ruvu chini ambao umekamilika kwa asilimia mia moja na utawezesha upatikanaji wa maji kufikia lita milioni 270 kwa siku kutoka milioni 180 kabla ya mradi huo haujatekelezwa.

  Majukumu ya DAWASA ni kumiliki miundombinu ya maji safi na maji taka kwa niaba ya Serikali, kusimamia utoaji wa huduma ya maji safi na maji taka Dar es salaam, kugharimia,kupanga mipango na kusimamia upanuzi wa huduma na kuishauri Serikali kuhusu masuala ya huduma ya maji safi na maji taka Jijini Dar es salaam.
  Mtambo unaotumika kuchoronga Visima Virefu ukiwa katika eneo la Kimbiji unapotekelezwa mradi mkubwa wa uchimbaji visima virefu.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.

  0 0

  Hussein Makame, NEC aliyekuwa Bukoba

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewatahadharisha watu wanaochukua kadi za kupigia kura za wenzao na kuzizuilia au kubaki nazo kuwa ni kinyume cha Sheria.

  Hayo yamesema na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe wakati akitoa elimu ya mpiga kura katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba na Shinyanga hivi karibuni.

  Alisema kifungu cha 88 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kinasema kuwa ni kosa la jinai kwa mtu kuchukua kadi ya mpiga kura mwingine na kuiziulia, kukataa kuirudisha au kubaki nayo kwa uzembe.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kulia) akisalimiana na mwenyeji wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Jaji Richard Kibela baada ya mwenyeji wake kumpokea wakati akiwasili mkoani Shinyanya kutoa Elimu ya Mpiga Kura mkoani humo.Kushoto ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Shinyanga Sekela Mwaiseje.

  Bw. Kawishe alifafanua kuwa kumekuwa na malalamiko kwamba inapofikia karibu na kipindi cha uchaguzi, baadhi ya watu wanachukua kadi za wapiga kura wengine na kuzizuia kinyume cha Sheria.

  Hata, hivyo alisema kutokana na kutoa elimu ya mpiga kura kupitia mikutano na kuhudhuria maonesho mbalimbali, baadhi ya wananchi wameelewa umuhimu wa kadi hizo na kuahidi kutoampa mtu kadi zao za kupigia kura.

  “Kwa hiyo katika jambo hilo tumekuwa na mrejesho ambo ni chanya lakini tunachowaomba ukiandikishwa tunza kadi yako ya mpigia kura” alisema Bw. Kawishe na kuongeza kuwa; “Jambo la pili mwananchi usikubali mtu achukue kadi yako ya mpigia kura na wala usitumie kadi yako ya mpiga kura kwenye kuchukulia dhamana sehemu yoyote”
  Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe, akisamiliana na Mkurugenzi wa Halamashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bw. Geofrey Ramadhani Mwangulumbi baada ya kuwasili kwenye Halmashauri hiyo kutoa Elimu ya Mpiga kura.

  “Kwa sababu itakwenda kuchukulia dhamana alafu utashindwa kwenda kupiga kura unapofika wakati wa kupiga kura, mwananchi ajue kwamba kupiga kura ni haki yake” Alisema mtu aliyejiandikisha asipokwenda kupiga kura anakosa haki ya kuchagua kiongozi anayemtaka na badala yake anawaacha wenzako wakuchagulie kiongozi.

  “Unaacha kupiga kura alafu baadaye anakuja kulalamika unasema huyu kiongozi simtaki kumbe kura moja inatosha kubadilisha matokeo ya eneo zima” alisema.

  Hivyo aliwasihi wananchi waendelee kuzingatia amani katika uchaguzi na kuwashukuru kwa jinsi uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na uchaguzi mdogo uliofanyika Januari 22 mwaka huu kwa jinsi ulivyokuwa na amani na utulivu.

  ”Kwa kweli Watanzania tutambue kuwa amani ni yetu sisi sote na sisi ndio tutakaoilinda hiyo amani tuiweke Tanzania yetu kwanza alafu sisi baadaye” aliwakumbusha Watanzania.

  Akijibu swali la mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Bukoba aliyehoji anayepoteza kadi ya mpiga kura anachukuliwa hatua gani kumuwajibisha, Bw. Kawishe alisema hakuna hatua yoyote inayochukuliwa dhidi yake.

  Alifafanua kuwa wale wote wanaopoteza kadi ya mpiga kura wanatakiwa wafike kwenye kituo cha uboreshaji wa daftari la wapiga kura na kujieleza na watapatiwa kadi nyingine.
  Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe, akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakati alipomtembelea ofisini kwake mkoani humo.
  Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe akitoa Elimu ya Mpiga kura kupitia Kituo cha redio Faraja Fm cha mkoani Shinyanga mwishoni mwa wiki hii.Kulia kwake ni mtangazaji wa redio hiyo Faustin Kasala.
  Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe, akitoa Elimu ya Mpiga kura kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Old Shinyanga iliyopo manispaa ya Shinyanga. Picha na Hussein Makame, NEC

  0 0

  Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

  Wiki chache baada ya Jeshi la Polisi mkoani hapa kukamata gunia 58 za bhangi ambazo ziliteketezwa kwa moto  na kuharibu hekari 31 za mimea ya zao hilo katika maeneo ya Kismiri Juu na Engalaon wilayani Arumeru, Jeshi hilo limeendelea na misako dhidi ya wauzaji, watumiaji na wasafirishaji  wa dawa za kulevya na kufanikiwa kuwakata watuhumiwa 80 katika misako iliyofanyika kwa muda  wa siku 4 tu.

  Akitoa taarifa hiyo leo asubuhi ofisini kwake mbele ya  waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo  alisema kwamba misako hiyo imefanikisha kukamata jumla ya kete 167 za madawa ya kulevya aina ya Heroin pia misokoto 3,845 ya Bhangi na mirungi kilogramu 33.

  “Katika misako hiyo ambayo ilifanyika wilaya zote sita za mkoa huu, watuhumiwa 54 walipatikana kwenye tuhuma za Bhangi, 14 ni tuhuma za Heroin na 12 ni wa tuhuma za mirungi.” Alisema Kamanda Mkumbo.

  “watuhumiwa 40 ni wauzaji wa madawa hayo huku 13 ni wale ambao walikuwa wanajihusisha kwa namna moja au nyingine na Bhangi na mmoja alikuwa anasafirisha, watuhumiwa 14 wa Heroin kosa lao kupatikana huku 12 makosa yao ni kupatikana na mirungi na hivyo kufanya idadi yao kuwa 80 ambao ni wanaume na wanawake”. Alifafanua Kamanda Mkumbo.

  Kamanda wa Polisi aliwashukuru wananchi wa mkoa huu kwa ushirikiano wa utoaji wa taarifa za uhalifu na kuwaomba waendelee kufanya hivyo na kutoa onyo kwa wale wachache wanaojihusisha na uhalifu wa namna hiyo waache mara moja vinginevyo watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo akionyesha baadhi ya kete za Heroin ambazo zilikamatwa hivi karibuni kutokana na misako inayoenndelea mkoani hapa. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)

  0 0

  Gavana wa Jimbo Katanga Jean Claude Kazembe amesema kuwa ili urahishaji wa ujenzi wa daraja katika mto Lwapula uliopo katika mpaka wa Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) utasaidia kurahisha usafirishaji wa mizigo kutoka Bandari ya Dar es salaam kwenda Jimbo la Hault Katanga DRC.

  Gavana huyo ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya ziara yake katika Badari ya Dar es salaam.

  Alisema kuwa endapo nchi za Zambia na DRC zitakubaliana kujenga Daraja hilo, kutaimarisha  biashara pamoja na kukuza uchumi wa nchi za Tanzania, DRC  na Zambia kwa kuwa itachukua muda mfupi kwa Wasafirishaji wa Mizigo kutoka Dar es salaam kwenda DRC.

  “Kujengwa kwa daraja hilo kutarahisisha usafirishaji wa mizigo  kutoka nchini Tanzania kwenda nchini DRC, na hivyo kufanya gharama za usafirishaji wa mizigo kupungua” alisema Gavana Kazembe.

  Gavana Kazembe aliongeza kuwa daraja hilo litakalogharimu dola milioni 85 litakalikuwa na urefu wa mita 700  linatarajiwa kujengwa kwa ushiririkiano wa Serikali za  nchi za Tanzania, Kongo na Zambia kwa vile litanufaisha nchi hizo kiuchumi.

  Aidha, Gavana Kazembe alisema kuwa atajitahidi kushauri Serikali hizo zijenge daraja katika mto Lwapula ili kusaidia Bandari ya Dar es salaam kuendelea kutoa  huduma nzuri za usafirishaji wa mizigo kati ya Dar es Salaam na Kongo.

  Aidha, alisema kuwa katika mazungumzo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alifurahishwa na hatua hiyo kwa kuwa  itasaidia kukuza urafiki uliopo baina ya Tanzania na Kongo pamoja na kurahisisha usafirishaji wa mizigo na kwa gharama nafuu.

  0 0  0 0

  Katika kuhakikisha kuwa biashara haramu ya dawa za kulevya inakomeshwa hapa nchini na kwa kuzingatia dhamira ya serikali ya awamu ya tano ya kupambana na tatizo la dawa za kulevya, Jeshi la Polisi nchini limetoa maelekezo kwa  Makamanda wa Polisi katika mikoa yote kuongeza nguvu za Oparesheni katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya kwa kuwakamata wanaotumia, wanaouza na wanaosafirisha. 

  Aidha, Jeshi la Polisi nchini limewaagiza Makamanda wote pindi wanapoendesha oparesheni dhidi ya dawa za kulevya kutokuangalia sura ya mtu, cheo, wadhifa wala nafasi aliyonayo katika jamii.

  Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi nchini linakemea vikali tabia ya baadhi ya wananchi wanaokusanyika katika vituo vya Polisi pindi baadhi ya watuhumiwa wa makosa mbalimbali wanapotakiwa kufika kwenye vituo hivyo kwa ajili ya kuhojiwa kuhusiana na tuhuma wanazokabiliwa nazo. Ni marufuku kwa mtu ama kikundi chochote kukusanyika katika kituo cha Polisi bila ya kuwa na sababu ya msingi na watakaobainika watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

  Jeshi la Polisi nchini, linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu zikiwemo za watu wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya na taarifa hizo zitafanyiwa kazi kwa siri ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa katika hali ya usalama.

  Imetolewa na: 
  Advera John Bulimba-ACP,
  Msemaji wa Jeshi la Polisi,
  MAKAO MAKUU YA POLISI.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  KAMPUNI ya Star Times imesheherekea siku ya wapendanao na wateja wake kwa kutoa zawadi kadhaa katika promosheni yake ya "Ni Valentine na Startimes".

  Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Meneja Masoko wa kampuni hiyo Tanzania, Felix Awino amesema Star Times inasheherekea siku hii kwa kuwazawadia wapenzi kupata chakula cha jioni na malazi ya Hotel ya kisasa.

  “tunafurahi kusheherekea siku ya wapendanao na wateja kwa kuwa karibu nao kama sehemu ya upendo wetu kwao, kwa kuwapa promosheni na maudhui yanayoendana na wakati ,hivyo kwa wateja wetu wa Dar es Salaam watapata malazi SeaScape, Mwanza watalala katika hoteli ya Malaika , Meya wataenda Usungilo , Arusha Palece Hotel na kwa mkoa wa Dodoma watapata kupumzika katika Hotel ya Morena”amesema Awino.

  Kwa upande wake mmoja wa washindi wa promotion hiyo ya ni Valentine na Startimes, Nuezy Fredrick amesema kuwa ni furaha kubwa kwao kama wateja wa Star Times kupata nafasi hiyo ya kupelekwa sehemu ya kifahari kama hiyo hili waweze kufurahi na wapenzi wao kutokana na kutumia king’amuzi cha Star Times.

  Amesema kuwa star Times imemuheshimu na yeye ataendelea kutumia bidhaa za kampuni hiyo na kufurahia vipindi bomba vya kila siku.
  Meneja Masoko wa StarTimes Tanzania ,Felix Awino akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao
  Meneja uhusiano wa kampuni ya Sar Times Tanzania Juma Suluhu akikabidhi zawadi kwa Bwana na Bibi Nuezy Fredrick 
  Meneja uhusiano wa kampuni ya Sar Times Tanzania Juma Suluhu na Meneja Masoko wa StarTimes Tanzania ,Felix Awinowakikabidhi zawadi kwa washindi wa Ni Valentine's na Star Times.


older | 1 | .... | 1566 | 1567 | (Page 1568) | 1569 | 1570 | .... | 3270 | newer