Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1565 | 1566 | (Page 1567) | 1568 | 1569 | .... | 3286 | newer

  0 0

   Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Barclays Tanzania, Simon Mponji (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la kisasa la benki hiyo katika jengo la Shirika la Nyumba (NHC), mjini Morogoro mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays Tanzania, Abdi Mohamed na kulia ni  Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Dk. Suleman Mohamed.
   Mkuu wa Mauzo wa Benki ya Barclays Tanzania, (kushoto), akieleza kuhusu huduma mbalimbali za kibenki zitolewazo katika tawi jipya Barclays la mjini Morogoro katika sherehe za uzinduzi wa tawi hilo juzi. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji, Abdi Mohamed, mjumbe wa bodi, Dk. Suleman Mohamed na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Barclays, Simon Mponji . 
   Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Barclays Tanzania, Simon Mponji (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi rasmi wa tawi jipya la benki hiyo mjini Morogoro. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays, Abdi Mohamed na  Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Dk. Suleman Mohamed.


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uzalishaji wa Umeme kwa kutumia Maji ya Darakuta, Raphael Bapsl (katikati) akionesha moja ya chanzo cha maji kinachotumika katika kuzalisha umeme.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uzalishaji wa Umeme kwa kutumia Maji ya Darakuta, Raphael Bapsl (kushoto) akielezea mitambo ya kuzalisha umeme inavyofanya kazi katika kituo hicho kwa Mtaalam wa Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Emillian Nyanda (kulia).

  Na Greyson Mwase, Manyara.

  Imeelezwa kuwa kampuni ya uzalishaji wa umeme kwa kutumia maji (Darakuta Hydro Power Project) iliyopo Babati mkoani Manyara inatarajia kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka Kilowati 370 hadi Megawati 1.3 zitakazoingizwa kwenye Gridi ya Taifa na kupunguza upungufu wa umeme nchini ifikapo mwaka 2021.

  Hayo yalielezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Raphael Bapsl wilayani Babati mkoani Manyara wakati wa ziara ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini katika wilaya hiyo, yenye lengo la kuangalia maendeleo ya miradi ya uzalishaji umeme na kubaini changamoto zake.

  Akielezea historia ya mradi huo, Bapsl alisema kampuni yake ilianza kuzalisha umeme wa Kilowati 50 mwaka 1995 na kuongeza kuwa Aprili mwaka 2016 kampuni ilianza kuliuzia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) umeme unaoingizwa kwenye Gridi ya Taifa.

  Alisema mbali na umeme huo kutumika kwa matumizi ya nyumbani ambao ni kidogo hususan katika shughuli za kilimo na ufugaji ili kujiongezea kipato, kampuni yake huuza umeme wa ziada kwa TANESCO ili kuongeza kiasi cha umeme katika wilaya ya Babati.

  Alisisitiza kuwa ili Tanzania kuingia katika uchumi wa kati kupitia uwekezaji kwenye viwanda, nishati ya umeme wa uhakika inahitajika na kuendelea kusema kuwa kwa kutambua hilo kampuni yake imeweka mikakati ya muda mfupi na muda mrefu ili kuhakikisha inachangia katika ongezeko la umeme katika Gridi ya Taifa.
  Mtaalam wa Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Emillian Nyanda (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uzalishaji wa Umeme kwa kutumia Maji ya Darakuta, Raphael Bapsl mara baada ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini kuwasili wilayani humo kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya umeme.


  0 0

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika wakati wa sikukuu ya Pasaka jijini Dar es salaam, Msama amesema maadalizi yanaendelea vizuri na wako kwenye mazungumo na waimbaji kutoka mataifa mbalimbali kama vile Rwanda, Nigeria, Afrika Kusini Zambia na kwingineko ili kuboresha Tamasha hilo ambalo pia litafanyika katika mikoa kumi ya Tanzania.

  Ameongeza kwamba Tamasha la mwaka huu pia lina kazi kubwa ya kumuombea Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk.John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta Maendeleo kwa watanzania lakini pia kupambana na vita mbaya ya Madawa ya Kulevya.
  2


  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Tamashahilo wakati alipozungumza na jijini Dar es salaam jana.

  0 0

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage anataraji kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mafunzo ya wajasiliamli wasichana ya Taasisi ya Manjano, jijini Dar es Salaam.

  Shear Illusion  kupitia bidhaa yake ya manjano imeanzisha mpango maalum wa kusaidia kutoa ajira kwa wanawake ambao wamemaliza shule na kushindwa kupata kazi.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, afisa mtendaji mkuu wa Taasisi ya Manjano na Kampuni ya Shear Illusions Ltd, Shekha Nasser amesema ameamua kumualika Waziri Mwijage ili aweze kuona fursa zilizopo katika viwanda vidogo vidogo 

  Amesema kuwa mara baada ya kuona tatizo hilo wakaamua kuanzisha mradi wa uuzaji wa bidhaa za manjano kwa wanawake mbalimbali waliopo jijini Dar ese Salaam na mikoa mingine.

  “tasnia hii ya urembo ni moja ya vitu vinavyoweza kumsaidia mwanamke kuingiza zaidi ya shilingi milioni mbili kwa mwezi kama mtu atakuwa mwaminifu na biashara na kuifanya hii kuwa ni kazi yake ya muhimu katika kujikwamua kiuchumi” amesema. Shekha Nasser
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Manjano na Shear Illusion LTD, Shekha Nasser akizungumza na waandishi wa habari wakati kutangaza uzinduzi wa awamu ya pili ya mafunzo ya wajasiliamli wasichana ya Taasisi ya Manjano, Jijini Dar es salaam leo.

  Amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa wanatoa ajira kwa wasichana hao wameamua kutoa mafunzo ya wiki mbili kwa wasichana 30 ambao watapewa mtaji wa shilingi 300,000/-

  Amesema kuwa wasichana hao ambao wapo 30 wamepatikana kutokana na mchujo uliofanywa na watalaamu wa masuala ya urembo hadi kufikia hapo.
  Sehemu ya Washiriki waliofuzu kujiunga na mafunzo ya wajasiliamli wasichana ya Taasisi ya Manjano.

  0 0

  mako2
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akionesha majina mengine 97 ya wauza  Dawa za Kulevya awamu ya tatu kwa kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya,Bw. Rogers William Sianga   ili yaanze kushughulikiwa.RC Makonda amesema awamu hii itaitikisa nchi kwani wameanzia toka awamu ya tatu iliyoongozwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ya nne Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na hii ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli, Katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere JNCC
  mako3
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akikabidhi majina mengine 97 kwa kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa Bw. Rogers William Sianga, kuwa   ili yaanze kushughulikiwa.Rc Makond amesema awamu hii itaitikisa nchi kwani wameanzia toka awamu ya tatu iliyoongozwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ya nne Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na hii ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli.
  mako1
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza katika mkutano huo,ambapo amekabidhi majina mengine 97 ya awamu ya tatu   kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya,Bw. Rogers William sianga  ili yaanze kushughulikiwa. 

  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza jambo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Rogers William Sianga katika mkutano maalum wa kutoa tathmini ya kampeni ya kutokomeza biashara haramu ya madawa ya kulevya katika mkoa wa Dar es salaam na nchi nzima kwa ujumla.


  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Saimon Sirro akizungumza wakati akitoa taarifa ya kampeni hiyo leo.


  0 0


  0 0


  0 0

  The MNH Dir. Surgical Services Dr. Julieth Magandi who represented the Permanent secretary Min. of health, community Development, Gender, Elderly and Children cuts the ribbon marking the launch of the playground at the Muhimbili National Hospital last Saturday, the centre has been constructed by the Human Welfare Trust in partnership with Bank M. Others in the photo from left, front row are The MNH Director for Medical Services Dr. Hedwiga Swai and Human Welfare Trust Trustees Mr. Vikash Shah and Ms. Veena Jog.

  Playground at the Muhimbili National Hospital which has been constructed by Human Welfare Trust in partnership with Bank M. The playground was launched last Saturday.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Bodi ya Wadhamini ya Tanzania Motorcycles Movement Association (TAMOSA), Kizito Msangya pamoja na Mh. Devotha Minja (MB) wakimsikiliza kwa makini mtaalam kutoka Jeshi la Polisi (Usalama Barabarani) (hayupo pichani) wakati akielezea umuhimu wa Bodaboda kufuata sheria kuhakikisha usalama wao barabarani. Katibu Mkuu wa Tamosa alisema lengo kuu la semina hii ilikuwa kuwakutanisha wadau mbalimbali katika sekta ya usafirishaji ili kuibua fursa mbalimbali zinazoweza kupatikana, lakini pia kuhakikisha Bodaboda ni usafiri salama, wa haraka unaopendwa na kutumika kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla aliongeza pia kauli mbiu ya Tamosa ni "Bodaboda ni Huduma Ajira na Uchumi" Aidha alieleza wadau waliolikwa kwaajili ya kuwasilisha mada ni Jeshi la Polisi, TRA, SUMATRA, Mabeki ya Biashara pamoja na Mifuko ya Pensheni
  Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Tamosa Bw Aloyce Ntukamazina na Mh Joyce Mukya (MB) wakishiriki katika semina hii maalum kwa sekta ya usafirishaji ambayo imetoa ajira kwa vijana takriban 4,000,000 nchi nzima.
  Baadhi ya wadau mbalimbali waliolikwa katika semina hii maalum wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa na wahusika.

  0 0

  Baaadhi ya watu mbalimbali wakitembelea banda la Tanzania, nchini Saudi Arabia, katika maonyesho ya utalii ya '(Travel and Tourism Pioneers Forum - 2017).Maonyesho ya utalii nchini Saudi Arabia yaipaisha Tanzania

  Na Mwandishi Maalum, Saudi Arabia
  Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia mwishoni mwa juma hili ulishiriki katika maonyesho ya Safari na Utalii yajulikanayo kama '(Travel and Tourism Pioneers Forum - 2017).


  Maonyesho ya TPF 2017 ambayo hufanyika kila mwaka kwa uandalizi Al Awsat Expo chini ya uhisani wa Mwana Mfalme HRH Prince Dr. Seif al Islam bin Saud bin Abdulaziz, yamefanyika kwa mafanikio huku ubalozi wa Tanzania ukifanikiwa kwa kiasi kikubwa kutangaza utalii wa Tanzania.


  Akizungumza katika maonyesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, alisema kwamba maonesho hayo yalikuwa maalumu kwa wafanya maamuzi na viongozi wa asasi za utalii (decision makers and leaders and tourisma leaders) nchini Saudi Arabia.
  Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, mwenye suti nyeusi akizungumza jambo na wageni waliotembelea katika banda la Tanzania kwenye maonyesho hayo.

  Alisema kwamba kuwa banda la Tanzania lilifanikiwa kuonesha vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, hifadhi za taifa, maeneo ya kihistoria ya Zanzibar, kilwa na Bagamoyo.
  Mazungumzo yakiendelea yakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia
  Watu wakipata maneno juu ya utalii wa Tanzania nchini Saudi Arabia
  Karibuni Tanzania.
  “Tunashukuru kwa kiasi kikubwa kushiriki katika maonyesho haya sambamba na Tanzania kutangaza vivutio vya utalii wan chi yetu, tukiamini kuwa ni fursa adhimu kwa nchi yetu.


  “Tunaendelea na juhudi za kutangaza nchi yetu ya Tanzania sambamba na kuwaonyesha watu wa Saudi Arabia juu ya umuhimu wa kutembelea nchini kwetu ili kujionea fursa mbalimbali za kiuchumi na utalii,” Alisema.


  Kwa mujibu wa Balozi Mgaza, miadi na majadiliano kuhusu kukuza utalii (promotion of tourism) yalifanyika baina ya washiriki wa Tanzania na mawakala wa utalii (tour operators) na wa usafiri (travel agents). 

  0 0

  Na Mroki Mroki, TSN Digital-Simiyu .
  Ni ile siku iliyosubiriwa ya kuumulika kibiashara mkoa wa Simiyu ulioanzishwa mwaka 2012, ambao umejipambanua kuwa ‘mkoa  darasa’, mintarafu suala zima la ujenzi wa viwanda nchini.  Mwezi uliopita, Rais John Magufuli alipotembelea mkoa huu, alipongeza juhudi zinazochukuliwa na mkoa huu chini ya mkuu wake, Anthony Mtaka, katika kujenga uchumi wa viwanda na hivyo kuelekea kuifanya ndoto yake ya Tanzania ya viwanda kutimia.  Kupitia Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayochapisha magazeti ya Daily News na HabariLeo pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii, imeshirikiana na Mkoa wa Simiyu kuandaa Jukwaa la Biashara Simiyu likiwa na lengo la kuibua fursa za uchumi za mkoa huu darasa ambazo zitadadavuliwa na kuchambuliwa hii leo, na hivyo kuwasaidia wawekezaji wa ndani na nje kujua ‘kunani’ Simiyu.
   Mkuu wa Mkao wa Simiyu, Anthony Mtaka (kulia) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel katika Jukwaa hilo la Biashara Simiyu.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Biashara Mkoa wa Simiyu ambapo alilisitiza kuwa Simiyu itajengwa na wana Simiyu wenyewe na si kutegemea watu kutoka nje.


  0 0

  Jengo la NSSF Water Front lililopo eneo la Stesheni jijini Dar es Salaam likionekana kufuka moshi mzito ikidaiwa limeshika moto mchana huu ambapo mpaka sasa hakujajulikana nini chanzo cha moto huo. Kwa taarifa zaidi zinakuijia hapo baadae.
  Baadhi ya wapitanjia wakitazama jengo hilo linadaiwa kuungua moto muda huu.

  0 0

  Na Theresia Mwami TEMESA

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa boti nne za kisasa unaofanywa na kampuni ya Songoro Marine Boatyard jijini Mwanza. Akiwa katika karakana ya kampuni ya Songoro, Dkt. Mgwatu amesema kuwa Serikali imepanga kutekeleza mradi huo ili kutoa huduma za usafiri wa majini kwa wananchi katika maeneo manne tofauti.

  Aliyataja maeneo hayo kuwa ni Pangani mkoani Tanga ambako wananchi walimuomba Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa alipokuwa akizindua Kivuko cha MV. Tanga kuwaletea boti ndogo itakayokuwa inatumika kuwasaidia wananchi wanapokuwa na dharura nyakati za usiku wakati ambapo kivuko cha MV. Tanga kinakuwa kimeegeshwa. Boti ya pili itapelekwa sehemu ya Msangamkuu mkoani Mtwara na vile vile itatumika kwa nyakati za dharura. Boti hizi mbili zitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 8 kila moja.

  Boti ya tatu itapelekwa eneo la Kilambo, Mtwara ambako kivuko cha MV. Kilambo kinatoa huduma ya kuvusha wananchi kati ya upande wa Tanzania na Msumbiji kupitia mto Ruvuma. Boti hii itatumika katika vipindi ambavyo maji ya mto ni machache kuweza kuendesha kivuko cha MV. Kilambo na itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 25.

  Boti ya nne ambayo inajengwa kwa kutumia chuma itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 40 na itapelekwa kwenye eneo la Utete mkoani Pwani ili kiweze kutoa huduma wakati wote hata pale maji ya mto yanapokuwa machache. Nae Mkandarasi kutoka kampuni ya Songoro Marine Boatyard, Bw. Major Songoro amesema kuwa kazi ya kujenga boti zote nne inatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi huu.

  Dkt. Mgwatu alikuwa katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza kukagua na kujionea maendeleo ya ujenzi wa boti hizo nne.
  Mtaalamu kutoka kampuni ya Songoro Marine Boatyard Ndugu Mohamed Salim (alie ndani ya boti) akimuelekeza jambo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (wa kwanza kulia), pembeni yake ni Major Songoro pamoja na Meneja wa TEMESA mkoani Mwanza Mhandisi Ferdinand Mishamo. Boti hiyo ni moja kati ya mbili zinazotarajiwa kupelekwa maeneo ya Pangani mkoani Tanga pamoja na Msangamkuu mkoani Mtwara kwa ajili ya kutumika nyakati za dharura.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (alieshika nguzo ya boti) akiangalia moja ya boti kati ya mbili yenye uwezo wa kubeba abiria nane zinazotarajiwa kupelekwa maeneo ya Pangani mkoani Tanga pamoja na Msangamkuu mkoani Mtwara kwa ajili ya kutumika nyakati za dharura.
  Sehemu ya chini ya boti inayojengwa kwa ajili ya kutoa huduma mto rufiji katika eneo la Utete/Mkongo, boti hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 40. Ujenzi wa boti hiyo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu. Picha zote na Theresia Mwami TEMESA

  0 0

  NA HAMZA TEMBA - WMU

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imewahukumu kifungo cha miaka 20 jela Peter Kabi na Leonida Loi Kabi ambao ni wanandoa baada ya kukutwa na meno ya tembo 210 yenye uzito wa kilo 450.6 pamoja na mifupa mitano ya tembo.

  Meno hayo yanayodaiwa kuwa ni sawa na idadi ya tembo 93 waliouwawa yalikutwa nyumbani kwa washtakiwa hao tarehe 27 Oktoba, 2012 eneo la Kimara Stop Over Jijini Dar es Salaam.


  Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shahidi amesema ametoa hukumu hiyo leo baada ya mahakama kujiridhisha na ushahidi wa upande wa Jamhuri ukiongozwa na mawakili Paul Kadushi na Elia Athanas ambao kwa pamoja umewatia hatiani washtakiwa hao.


  Amesema katika kosa la kwanza kila mtuhumiwa atatumikia kifungo cha miaka 15 jela, kosa la pili na la tatu miaka 20 kila moja na kwamba hukumu hizo zitaenda kwa pamoja.
   Watuhumiwa wa Ujangili, Peter Kabi (wa pili kulia) na mke wake Leonida Loi Kabi (wa tatu kulia) wakielekea kusomewa mashtaka ya kukutwa na meno 210 na mifupa mitano ya tembo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam leo, wote wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela. 
   Mtuhumiwa wa Ujangili, Peter Kabi (wa pili kulia) akielekea kusomewa mashtaka ya kukutwa na meno 210 na mifupa mitano ya tembo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam leo, mtuhumiwa huyo na mke wake Leonida Loi Kabi (hayuko pichani) wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Gavana wa Lubumbashi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean Claude Kazembe kuhusu mipango endelevu ya matumizi mazuri ya Bandari ya Dar es Salaam ofisini kwake jijini Dar es salaam.
  Ujumbe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ukiwa katika mazungumzo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa, Makame Mbarawa na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eng, Deusdedit Kakoko leo, jijini Dar es salaam.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

   Na jacquiline Mrisho - MAELEZO.

  Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) wamejipanga kuendelea kuendesha mafunzo kwa wadau wa Kanda ya Mashariki wanaohusika na kemikali ili kuhakikisha kemikali zinatumika vema na kwa njia salama.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wasafirishaji na watumiaji wa kemikali nchini.

  Prof. Manyele amesema kuwa wakala hufanya usajili na ukaguzi kwa wadau wote wanaohusika na kemikali wakiwemo waagizaji, watengenezaji, wasafirishaji, watumiaji, wanaosafirisha nje ya nchi au yeyote yule anayehusika na kemikali kwa njia moja au nyingine. 

  Pia ukaguzi huo unahusisha mahali ambapo kemikali zinatumika, zinatunzwa au kuhifadhiwa.
  Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu mafunzo ya wasafirishaji na watumiaji wa Kemikali nchini, kutoka kulia ni Kaimu Meneja wa Maabara ya Kanda ya Mashariki, Everlight Matinga na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali nchini,Sabanitho Mtega, (kutoka kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, David Elias pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Biashara,George Kasinga.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamishna Mkuu wa Magereza, Dk. Juma Malewa asimamie zoezi la upimaji wa maeneo yanayomilikiwa na Magereza kote nchini na kuhakikisha yanawekewa mipaka. 

  Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumatatu, Februari 13, 2017) katika kikao baina ya Kamishna huyo mpya na Maafisa Magereza wa Mikoa yote na maafisa wanaoshughulikia kilimo na viwanda alichokiitisha ofisini kwake mjini Dodoma.

  “Magereza yetu mengi yako kwenye maeneo ambayo hayajapimwa. Baadhi ya maeneo kuna migogoro kwa sababu wananchi wamejenga karibu kabisa na maeneo ya Magereza. Lazima tupime maeneo yote na kuyawekea alama mipakani ili kubainisha maeneo yetu,” amesisitiza.

  Mbali ya maeneo ya Magereza, Waziri Mkuu amesema, jeshi hilo lina mashamba makubwa ambayo pia hayajapimwa hali ambayo amesema imechangia baadhi ya wananchi kulima ndani ya maeneo ya jeshi hilo.

  “Natambua kuwa jeshi hili lina mashamba makubwa lakini nayo pia hayajapimwa. Kila RPO ni mjumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wake, tumieni wapima ardhi kutoka kwenye Halmashauri zenu na mhakikishe kuwa maeneo hayo yanapatiwa hati,” amesema. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiongoza kikao kati yake na Maofisa wa Magereza kutoka makao Makuu ya Magereza , pamoja na Makamanda wa Magereza wa Mikoa yote nchini, ofisini kwake mjini Dodoma Februari 13, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Watalaamu na Wasimamizi wa Mkiradi ya Jeshi la Mgereza, baada ya kikao chake na Maofisa wa Magereza kutoka Makao ya Magereza na Wakuu wa Magereza wa Mikoa kilichofanyika Ofisini kwake mjini Dodoma Februari 13,2017. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kamishina Jenerali wa Magereza, Dr Juma Malewa baada ya kikao chake na Maofisa wa Magereza kutoka Makao ya Magereza kilichofanyika Ofisini kwake mjini Dodoma Februari 13,2017. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani Meja Jenerali Projest Rwegasira.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Msanii wa Bongo fleva Khalid Mohamed (TID) amesema kuwa hawezi kufumbia macho wala kuwaonea aibu kwa kuwataja watu wote ambao wanafanya biashara ya dawa za kulevya.

  TID amesema hayo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa mkuu wa mkoa na waandishi wa habari juu ya mapmbano dhidi ya dawa za kulevya kwa mara ya tatu.

  “Mimi mnyama na mkuu wa mkoa kaonesha unyama katika kupambana na madawa ya kulevya, hivyo namshukuru sana kwa hatua ngumu aliyoamua kuichukua,basi wote kwa pamoja tuanze kupambana na kuhakikisha biasha hii inapungua kama sio kuisha kabisa,tushiriki kwa pamoja kukomesha biashara hii kwa kupinga janga hili ” amesema TID.

  TID ambaye amekiri hadharani kuwa amekuwa akitumia dawa za kulevya kwa muda mrefu lakini zimekuwa zikimtesa ,hivyo RC Makonda amekuwa msaada kwake,akasema na kuongeza kuwa hahitaji nguvu ya dola kuacha uvutaji wa dawa za kulevya,hivyo ameamua kuacha mwenyewe ili awe mfano wa kuigwa .

  Amesema yeye bado ni kijana hana kasoro yoyote wala ulemavu wowote,hivyo itakuwa ni aibu kwake kuonekana mtumiaji wa dawa za kulevya mbele ya mtoto wake, hivyo atakuwa hajengi familia bali atakuwa anaibomoa kwa kumfanya mtoto aendelee kuiga tabia mbovu za baba yake. 
  TID ambaye aliiongea kwa ujasiri mkubwa bila kuhofu lolote akiwaomba Watanzania wamuelewe na kumpokea tena,kama kijana aliye amua kuacha matumizi ya dawa za kulevya. 
  TID akikumbatiwa na Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Rogers Sianga mara baada ya kumaliza kuzungumza wazi na kukiri kuwa ni kweli alikuwa anatumia Dawa za Kulevya na sasa ameweka wazi kuwa ameacha na yuko tayari kutoa ushirikiano katika suala zima la kupamba na dawa za kulevya.

  0 0


  Stori na Biseko Ibrahim.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewataka watumishi wa Wizara hiyo Sekta ya Uchukuzi kutumia vizuri fursa ya kuhamia Dodoma kwa kuwatumikia watanzania kwa uadilifu na weledi.


  Amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akiwaaga watumishi wa Sekta ya uchukuzi wa awamu ya kwanza ambao wameondoka leo kuelekea mjini Dodoma.


  “Nawapongeza kwa kupata fursa ya kuwa katika awamu ya kwanza katika Wizara hii kuhamia Dodoma fahamuni hii ni fursa na si changamoto kwani hatua hii inasogeza huduma karibu na wananchi hivyo watumikieni kwa moyo”, amesema Prof. Mbarawa.


  Prof. Mbarawa amesema kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha watumishi wake wanahamia Dodoma na kuendelea na utekelezaji wa majukumu yake kwa wananchi.


  Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho amesema awamu ya kwanza ya watumishi zaidi ya 45 inahamia Dodoma mwezi huu na Awamu ya pili itaanza mwezi wa Machi na watumishi wote wa sekta ya uchukuzi watakuwa Dodoma ifikapo Agosti mwaka huu.


  “Watumishi wa Sekta ya Uchukuzi wanaohamia Dodoma katika awamu ya kwanza ni pamoja na Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi, Wakurugenzi na Wakurugenzi wasaidizi, wakuu wa vitengo na maafisa waandamizi”, amesisitiza Dkt. Chamuriho.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Uchukuzi), Dkt. Leornard Chamuriho kabla ya kuwaaga watumishi wa Wizara hiyo  wanaohamia Dodoma leo, jijini Dar es salaam. Picha na Biseko Ibrahim.

  0 0

  SERIKALI imewataka Maafisa Habari na Maafisa Tehama katika sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya nchini kuweka taarifa sahihi zenye kuzingatia muda na wakati ili kuongeza ufanisi wa kutangaza shughuli za Serikali kwa umma.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Mwanza na Katibu Tawala wa Mkoa huo, C.P Clodwig Mtweve, katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala Msaidizi, Johnsen Bukwali wakati wa mafunzo elekezi ya uwekaji wa taarifa katika tovuti yaliyoandaliwa na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Umma (PS3) kwa Maafisa Habari na Tehama wa Halmashauri na Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera na Simiyu.

  Kwa Mujibu wa C.P Mtweve alisema uwekaji taarifa katika tovuti hizo zitasaidia kuimarisha shughuli za utawala na kuifanya Serikali kufahamika zaidi kwa wadau wake na hivyo kupunguza malalamiko ya mara kwa mara yanayotolewa na wananchi kuhusu huduma zake kwa umma.

  “Ninyi ndio mmekuwa wachakataji wa taarifa za Serikali na kuhakikisha zinaufikia umma wa Watanzania zikiwa katika hali ya ubora kwa kutumia njia mbali mbali za mawasiliano kama vile mbao za matangazo na hata kwa njia ya mitandao” alisema C.P Mtweve.

  Kwa mujibu wa C.P Mtweve alisema kuwa lengo la Serikali ni kuongeza uwazi na wigo wa upatikanaji wa taarifa sahihi na zenye uhakika katika tovuti zake ili kuiepusha Serikali na habari za kuzusha na zisizo na maslahi kwa taifa.
   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Rebecca Kwandu akizungumza na wajumbe wa kikao cha mafunzo ya Maafisa Habari na TEHAMA kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera na Simiyu wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo Jijini Mwanza.  Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa huo, Johnsen Bukwali.
   Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Mawasiliano ya Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya Umma, Desderi Wengaa akizungumza na wajumbe wa kikao cha mafunzo ya Maafisa Habari na TEHAMA kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera na Simiyu wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo Jijini Mwanza.  Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa huo, Johnsen Bukwali
  Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mwanza, Johnsen Bukwali katikati (walipokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina ya mafunzo elekezi kwa Maafisa Habari na TEHAMA kutoka katika Hallmashauri na Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Kagera na Mara mara baada ya kufungua mafunzo hay oleo Jijini Mwanza.


older | 1 | .... | 1565 | 1566 | (Page 1567) | 1568 | 1569 | .... | 3286 | newer