Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

BARAZA LA DINI LAUNGA MKONO VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA


GWAJIMA AMSHUKIA MAKONDA

WEMA SEPETU NA TUNDU LISSU KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM

Shamrashamra za Burudani za Uzinduzi wa Tamasha la Sauti za Busara Viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani Zanzibar

$
0
0
Mwenyekiti wa Tamasha la Busara Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiwa na Mabalozi wa Norway na Uswisi kulia kwa Mhe Simai ni Balozi wa Uswisi Tanzania Balozi Florence Tinguely na Balozi wa Norway Tanzania Balozi Hanne Marie wakiangalia wakiangalia vikundi vya Utamaduni wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la Sauti za Busara katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani Kisongo leo wakiangalia burudani hizo.
Wasanii wa Kikundi cha Utamaduni kutoka Nchini Burundi wakitowa burudani kwa Wananchi wa Zanzibar katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani Zanzibar kabla ya kuaza kwa maandamano ya Uzinduzi huo yalioazia katika viwanja hivyo hadi katika viwanja vya bustani ya forodhani.
Wasanii kutoka burundi wakionesha umahiri wao wa kupiga ngoma za utamaduni wa Kwao. 
Wasanii wakitowa Burudani katika Viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani Kisonge.
Wanafunzi wa Skuli ya Maandalizi Jangombe wakicheza ngoma ya Bomo katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu kabla ya kuaza kwa maandamano ya Uzinduzi wa Tamasha la Busara Zanzibar.



BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 09/02/2017

HABARI KUTOKA TELEVISHENI LEO

WITO KWA WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA MGODI WA DHAHABU BULYANHULU WALIOPIMWA AFYA KATIKA HOSPITALI YA BUGANDO

$
0
0


Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) unawakaribisha walioorodheshwa hapo chini kufika katika ofisi za OSHA zilizopo katika jengo la Idara ya Kazi, Barabara ya Stesheni mkabala na Lake Hotel jijini Mwanzan kwa tarehe zilizotajwa katika makundi yao kuanzia saa 2.30 asubuhi ili waweze kupewa majibu yao. Tangazo hili linawahusu waliopimwa Bugando tu.

RC MTAKA AKABIDHI NG'OMBE KWA FAMILIA YA MD KAYOMBO KWA AJILI YA AROBAINI YA KIFO CHA MZEE KAYOMBO

$
0
0





Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kijiji cha MisasiMkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (katikati) na Mkewe wakifanya maombi katika kaburi la marehemu Mzee Kayombo, Kulia kwao ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Kayombo ambaye ni mjukuu wa Marehemu Mzee Kayombo
 Rc Mtaka akiwasalimu ndugu wa marehemu Mzee Kayombo mara baada ya kukabidhi Ng'ombe

Rc Mtaka (kulia) akisisitiza jambo, kulia MD Kayombo na katikati ni Mathias Canal Mhariri wa Tovuti ya (www.wazo-huru.blogspot.com) wakisikiliza kwa makini busara za mkuu huyo wa Mkoa wa Simiyu
MD Kayombo akiwa na ndugu na jamaa katika mazungumzo ya jioni.

WAJUMBE KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI, MBUNGE WA SIMANJIRO NA MKUU WA MKOA WA ARUSHA WATEMBELEA MNADA WA PILI WA KIMATAIFA WA MADINI YA TANZANITE

$
0
0
Teresia Mhagama na Zuena Msuya, Arusha

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na Mbunge wa Simanjiro, James Millya wametembelea Kituo cha Jimolojia Arusha, unapofanyika Mnada wa Pili wa Kimataifa kwa madini ya Tanzanite ili kujionea jinsi mnada husika unavyoendeshwa.

Mnada huo wa kimataifa unaofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 9 hadi 12, Februari, 2017 unahudhuriwa na wanunuzi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na wauzaji kutoka ndani ya nchi.

Akitoa maelezo kuhusu  mnada huo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji Madini katika Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo, alisema kuwa lengo la mnada huo ni kuhakikisha kuwa madini ya Tanzanite yanapata soko rasmi na Serikali kupata mapato yake stahiki.

 Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji Madini ya Almasi na Vito, katika Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo,(wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (wa Tatu kushoto) na Mbunge wa Simanjiro, James Millya (wa kwanza kulia) mara walipotembelea Kituo cha Jimolojia Arusha unapofanyika Mnada wa Pili wa Kimataifa kwa madini ya Tanzanite ili kujionea jinsi unavyoendeshwa.Wa kwanza kushoto ni mmoja wa wakurugenzi wa Mgodi wa Tanzanite One, Faisal Shahbhai. 
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Watumishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakiangalia jinsi wanafunzi katika Kituo cha Jimolojia jijini Arusha wanavyojifunza namna ya kukata madini ya vito na kuyaweka katika maumbo ya kuvutia. Kituo hicho cha Jimolojia kipo chini ya Wizara ya Nishati na Madini.

 Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji Madini ya Almasi na Vito, katika Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo,(wa kwanza kushoto) akitoa maelezo kwa Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Watumishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na Kituo cha Jimolojia jijini Arusha ambacho kipo chini ya Wizara ya Nishati na Madini.

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (katikati) akizungumza na mmoja wa wanunuzi wa madini ya Tanzanite katika Mnada wa Pili wa Kimataifa wa Madini hayo unaofanyika jijini Arusha. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji Madini ya Almasi na Vito, katika Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo na wa kwanza kulia ni mmoja wa wakurugenzi wa Mgodi wa Tanzanite One, Faisal Shahbhai.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji Madini ya Almasi na Vito, katika Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT) Archard Kalugendo, (katikati)  akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Simanjiro, James Millya (wa kwanza kulia) waliotembelea mnada wa Pili wa  Kimataifa wa Madini ya Tanzanite jijini Arusha. Wajumbe hao ni Mhe. John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini (CHADEMA), (wa kwanza kushoto), Mhe. Catherine Magige, Mbunge wa Viti Maalum (CCM),(wa pili kushoto),  ) na Mhe. Dunstan  Kitandula Mbunge wa Mkinga (CCM) (wa pili kulia). Wengine katika picha ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini, Adam Juma (wa Tatu kulia) na Kaimu Mratibu wa Kituo cha Jimolojia cha Arusha, Erick Mpesa (wan ne kulia). 

INTRODUCING NEW SONG "WIVU" BY ML

TEASER JOTO LA ASUBUHI IJUMAA FEBRUARY 10, 2017

TAFUTA TIKET RAHISI HAPA NI ONE WAY

TMF SPONSORED INTERNATIONAL AWARD WINNING FILM ON FIGHTING CORRUPTION IN TANZANIA

$
0
0

“We shot ‘Homecoming’ on a Red Epic Dragon and I wrote, directed and produced the film myself and it centers on examining corruption in Tanzania through the fresh eyes of a returnee. It starts off as a morality tale that develops into a thriller.” ~ Seko Shamte, director “Homecoming.”

Homecoming film that features corruption in Tanzania in an eye of the returnee, has been nominated for Best East African Film at the African Magic Viewers Choice Awards (AMVCA) that will be held in Lagos, Nigeria on 4th March, 2017.

The feature film received a grant from the Tanzania Media Foundation (TMF), has received a great honor on international stage. This testifies a productive relationship between TMF and its grantees such as Alkemist Media’s Seko Shamte, an independent producer who was initially supported to produce Mkwawa Documentary, an impactful documentary on the making of the nation.
Seko, a Tanzanian Film Producer and TV Presenter, is currently in the US on invitation to screen her Homecoming film at the Pan African Film Festival in Los Angeles, California this February.
According to the Africa Magic Viewers Choice Awards (AMVCA), the film viewership is over 50 countries around the world. This film about corruption in the country was launched towards the end of 2015 at Mlimani City by the Minister for Information, Nape Nnauye and was broadcast live by Azam TV. According to the Film Board, Tanzania is ranked the second after Nigeria in Film production in Africa.
Seko Shamte is a writer, producer, director and DJ. Shamte is the managing director of Alkemist Media based in Dar Es Salaam, Tanzania and has over 15 years of experience in the Tanzanian media industry.
She holds a BSc (Hons) in Finance and Media from Marymount Manhattan College (MMC) in New York City, USA. During her time as a student at MMC she won the business key, the top award given out by the school for the best student in the business department.
Tanzania Media Foundation (TMF), formerly Tanzania Media Fund, stands for an independent, quality, diverse and vibrant media in Tanzania. Their vision is of a strong and independent media sector that promotes accountability. For more CLICK HERE


RC IRINGA AAGIZA WANAFUNZI WASIORIPOTI SEKONDARI WASAKWE

$
0
0

Mkuu  wa Mkoa wa Iringa  Mhe. Amina  Masenza  akisalimiana na walimu  wa shule ya sekondari  Lundamatwe  Kilolo

Mkuu  wa mkoa wa Iringa  Amina  Masenza  akikagua  vyumba vya madarasa  katika  shule  ya sekondari  Lundamatwe  wilaya ya  Kilolo


Mkuu  wa mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza  akizungumza na wanafunzi wa  kidato cha  nne katika  shule  ya sekondari  Lundamatwe  wilaya ya  Kilolo.


Mkuu  wa mkoa  wa Iringa  Amina Masenza akikagua madaftari  ya wanafunzi  shule ya  sekondari  Lundamatwe  wilaya ya  kilolo  wakati wa ziara  yake 


Mkuu  wa mkoa  wa Iringa  Amina Masenza akitembelea sehemu mbalimbali za shule ya  sekondari  Lundamatwe  wilaya ya  Kilolo  wakati wa ziara  yake. Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

JOHN BARNES WA LIVERPOOL KUTUA NCHINI KUANGALIA KOMBE LA STANDARD CHARTERED

$
0
0


  Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah (kulia) ambaye pia ni mshabiki mkubwa wa Liverpool akitoa uchambuzi wa timu hiyo kwenye barabara ya kuelekea Anfield wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba akizungumzia tukio adhimu la Benki ya Standard Chartered, Tanzania Limited kutimiza miaka 100 tangu ilipofungua milango yake nchini Tanzania kabla ya kumkaribisha Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Sanjay Rughani kutoa risala katika sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
  Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahman Said (wa pili kushoto) akizungumzia katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu ujio wa mchezaji aliyewika wa timu ya Liverpool, John Barnes ambapo wateja wa Benki hiyo watapata fursa ya kukutana na mchezaji huyo.
 Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani (wa tano kulia) akimkabidhi zawadi Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah (wa tatu kushoto) ambaye pia ni mshabiki mkubwa wa Liverpool katika sherehe za uzinduzi huo. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba.





RAIS DKT. SHEIN AONGOZA SHEREHE ZA KILELE CHA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR

$
0
0

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (kushoto) mara alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  Mnazi mmoja Mjini Unguja leo katika sherehe za Siku ya Sheria Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizindua kitabu cha Sheria ya Mwaka 2015 katika sherehe za Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  Mnazi mmoja Mjini Unguja,(kushoto) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akinyanyua kitabu cha Sheria ya Mwaka 2015 baada ya kukizindua   rasmi leo katika sherehe za Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  Mnazi mmoja Mjini Unguja,(kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora (kushoto) makamo wa Pili wa Rais balozi Seif Ali Iddi akifuatiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa Majaji,Mahakimu na wafanyakazi wakati wa sherehe za Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  Mnazi mmoja Mjini Unguja,ambapo ujumbe wa mwaka huu unasema "SIMAMIA SHERIA NA MAADILI KATIKA UTENDAJI HAKI" (Picha na Ikulu).
  Baadhi ya Mahakimu na wafanyakazi wa idara ya Mahakama Zanzibar wakiwa katika sherehe ya kilele cha Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  Mnazi mmoja Mjini Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)

ONESHO LA LADY IN RED 2017 KUTIKISA JIJI LA DAR NDANI YA KING SOLOMON HALL KESHO JUMAMOSI

$
0
0
Ni siku moja tu imesalia kabla ya kutimia siku pendwa ya Wanamitindo wa hapa Tanzania ambao wanatarajia kukutanishwa kwenye Big Fashion Show ambayo hufanyika kila mwaka yaani  “Lady in Red”. 
Mwandaaji wa show hiyo Mama wa mitindo maarufu kama Asya Idarous Khamsin amesema kuwa show hiyo ni ya kipekee pia ina faida kubwa sana kwa wanamitindo chipukizi kwani Lady in red huwa inatoa kipaumbele kwa upcoming Designers kuonesha kazi zao jukwaani, hivyo mwaka huu  mambo yatakuwa mazuri sana ndani ya King Solomoni Hall”.
 Hivyo kwa wadau wote wapenzi wa mitindo mnakaribishwa  kuhudhuria usiku huo ili sanaa ya mitindo iweze kukua zaidi.
 Mama wa Mitindo Asya Idarous-Khamsin akiwa na wanamitindo wakiwa kwenye mkutano na wanahabari  akiongelea onesho la Lady In Red 2017 lililopangwa kufanyika kesho Jumamosi ndani ya ukumbi wa King Solomon Hall Namanga, Dar es salaam. 
 Mama wa Mitindo Asya Idarous-Khamsin akiwa na baadhi ya wanamitindo wakiwa kwenye mkutano na wanahabari  akiongelea onesho la Lady In Red 2017
Mama wa Mitindo Asya Idarous-Khamsin akiwa katika picha ya pamoja na badhi ya mamodo na wanamitindo wakiwa kwenye mkutano na wanahabari  akiongelea onesho la Lady In Red 2017

Zuriel Talking European Migration Crisis with Malta President

MAGAZETI YA LEO IUJUMAA FEBRUARY 10, 2017

VALENTINE'S DAY AT SHEKINAH GARDEN, MBEZI BEACH

Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images