Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110088 articles
Browse latest View live

TANZANIA YAWEKA HISTORIA KWA KURIDHIA MKATABA WA KUDHIBITI BIASHARA YA SILAHA

$
0
0
Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Ramadhan M. Mwinyi akitia sahihi  kwa niaba ya Serikali,Mkataba wa Kimataifa wa Kudhibiti Biashara ya Silaha ( ATT)  Tanzania  ilikuwa kati ya nchi 67 za kwanza ambazo zimetia sahihi katika siku ya kwanza ya uzinduzi wa tukio hilo la kihistoria. Baada ya  Mkataba  kutiwa  sahihi  nchi zaidi ya 50 kama sheria zinavyotaka  utaanza kufanya kazi rasmi baada ya siku 90. Mkataba  huu ambazo umechukua zaidi ya miaka sita hadi kupatikana unalenga katika pamoja na mambo mengine kusimamia na kuratibu biashara ya silaha zikiwamo mizinga ya kivita, magari ya deraya,  ndege za kivita, helkopta za mashambulizi, meli za kivita na silaha ndogo na nyepesi. vile vile mkataba unalenga kudhibiti silaha zisiangukie mikononi mwa   makundi ya kihalifu yakiwamo ya  kigaidi

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa miongozi mwa nchi za kwanza kutia sahihi Mkataba wa Kimataifa wa  Kudhibiti Biashara ya Silaha Duniani ( ATT)

Utiaji sahihi  wa tukio hilo la kihistoria  umeziduliwa jana jumatatu ( Juni 3) hapa Makao  Makuu ya Umoja wa Mataifa. Ukishuhudiwa na  viongozi  mbalimbali  akiwamo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon.

Katika  tukio hilo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliwakilishwa na  Balozi Ramadhan M. Mwinyi, Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

Utiaji  sahihi  wa mkataba huo  unafanyika ikiwa ni takribani miezi miwili kupita tangu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  lilipoupitisha kwa  kuupigia kura 154 za ndiyo na hivyo kuhitimisha majadiliano  ya uundwaji wa  mkataba yaliyodumu kwa takribani miaka sita.

Kutiwa sahihi kwa  Mkataba huo sasa kunafungua  fursa ya  kuanza kufanya kazi rasmi baada ya siku 90, kwa sababu  zilikuwa zikihitajika  sahihi    50 ili upate  baraka ya kuanza rasmi. Lakini idadi hiyo imepitiliza katika siku ya kwanza ya utiaji wa sahihi na kufikia nchi 67.

Dhumuni  kuu la  mkataba  pamoja na mambo mengine ni kusimamia na kuratibu biashara ya silaha za aina mbalimbali zikiwamo, mizinga ya kivita, magari ya deraya,  ndege za kivita, helkopta za mashambulizi, meli za kivita, makombora pamoja na silaha ndogo ndogo na nyepesi.

Aidha Mkataba pamoja  masuala mengineyo hautaingilia uhuru wa nchi  kununua silaha kwa matumizi yake  ya ndani na haki ya kujilinda na kulinda mipaka yake, vilevile mkataba hauzui nchi kufanya biashara ya kusafiri aina yoyote ya silaha ilimradi inazingatia sheria na taratibu zilizomo ndani ya  mkataba ikiwa ni pamoja na taratibu ambazo nchi yenyewe imejiwekea.

Matumaini ya Jumuiya ya Kimataifa ni kwamba utekelezaji wa  mkataba na kama utaekelezea ipasavyo utasaidia sana  kudhibiti silaha zisiangukie mikononi mwa makundi mbalimbali ya kihalifu yakiwamo ya kigaidi.

Akizungumza mara baada ya kutia sahihi,  Balozi Ramadhan Mwinyi aliungana na wasemaji wengine katika  kukaribisha hatua hiyo muhimu.  Huku akieleza kwamba  kwa Tanzania kutia sahihi ni uthibitisho wa utayari wake  wa kuutekeleza kwa  kuzingatia masharti na matakwa yanayoendeana na mkataba huo.

Akasema   Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi za mwanzo kutia sahihi mkataba huo  kwa kuwa  ilikuwa moja kati ya nchi zilizodhamini Azimio la Kuanzishwa kwa  Mkataba  na pia ilishiriki kikamilifu katika majadiliano yote yaliyozaa mkataba huo.

Balozi Mwinyi akaeleza pia kuwa kufanya kazi kwa  Mkataba  huo kutachangia katika amani ya Kimataifa, amani na  usalama wa Kikanda na pia utachangia sana katika kupunguza   madhara yatokanayo na biashara haramu na holela ya silaha lakini pia  utasaidia katika kukuza na kuimarisha uhusiano mzuri miongoni mwa  nchi wanachama.

Katika  hatua nyingine Muwakilishi huyo wa Tanzania amesisitiza haja na umuhimu wa  uwepo wa fursa sawa  kati ya  wasafirishaji wa silaha na waagizaji wa silaha  na kwamba Mkataba huo usidhibiti au kuzuia biashara ya silaha ambayo ni halali na kwamba mkataba haupashwi kuingilia au kwa namna yoyote  ile au   kuadhiri uhuru na haki ya nchi kujilinda na kulinda watu wake.

Tanzania pia imekaribisha misaada ya kiufundi katika maandalizi ya utekelezaji wa mkataba huo hasa  kwa nchi zinazoendelea.

Nchi  hizo 67 ambazo zimetia sahihi ni   , Albania, Antigua and Barbuda, Argentina, Australia, Austria,  Bahamas, Belgium, Belize, Benin, Brazil,  Burkina  Faso, Burundi, Chile, Costa Rica,  Cote D’ Ivoire, Croatia, Cyprus, Czech Republic , Denmark, Djibout,  na  Dominica Republic.

Nyingine ni  Estonia, Finland, France, Germany, Greece, Grenada, Guyana, Hungary, Iceland, Italy, Jamaica,  Japan, Latvia, Liechtenstein,  Lithuania, Luxembourg, Mali, Malta, Mauritania, Mexico na  Montenegro.


Mataifa mengine ni Mozambique, Netherlands, New Zealand, Norway, Palau, Panama,  Portugal,  Republic of Korea,  Romania, Saint Lucia,  Saint Vincent and the  Grenadines,  Senegal, Seychelles,  Slovenia, Spain, Suriname, Sweden, Switzerland, Togo,  Trinidad and Tobago, Tuvalu, United Kingdom of Great Britain and Northern  Ireland,  United Republic of Tanzania na Uruguay

.

MKATAA KWAO MTUMWA

MIONDOKO YA KUMEREMETA KWENYE MNUSO

msaada tutani

$
0
0
Habari yako ndugu Ankal. 

Mimi ni mwanamke, naandika kwenye blog yako natafuta mchumba, kijana ambaye yupo makini na anayetaka kuanzisha familia hivi karibuni. Awe na umri kuanzia miaka 35 mpaka 39. Naomba sana ambao hawako makini kwenye hili swala wasiniandikie.

Rafiki ninayemtafuta awe hajawahi kuoa, awe hana watoto, awe na elimu kuanzia chuo, awe tayari kupima ukimwi, awe mtu wa kumcha mungu (mkristo), mpole, anayejali na mwenye mapenzi ya dhati.
Napatikana kwenye email address:

Twanga kupepeta katika Miss Sinza 2013 ijumaa hii

$
0
0
BENDI yenye chati ya juu kabisa katika muziki wa dansi katika Afrika chini ya jangwa la Sahara, The African Stars Band ’ Wana Twanga Pepeta’ itaburudisha mashindano ya Redds Miss Sinza yaliyopangwa kufanyika Ijumaa (Juni 7) kwenye ukumbi wa Meeda Club wa Sinza jijini. 
Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa bendi hiyo itatumia fursa hiyo kutambulisha baadhi ya nyimbo zake mpya zilizomo katika albamu ya 12 ijulikanayo kwa jina la Nyumbani ni Nyumbani ambayo itazinduliwa rasmi Juni 30 kwenye viwanja vya Leaders Club jijini. Majuto alisema kuwa Twanga Pepeta itakuwa ikitumbuiza kwa mara ya kwanza tokea mwaka jana mwezi julai ambapo ilitumbuiza katika mashindani hayo hayo ya kumsaka mrembo wa Sinza. 
Alisema kuwa hii ni faraja kubwa kwa mashabiki wa muziki wa dansi na wa masuala ya urembo kwani Twanga Pepeta itakuwa ikimvua taji Redds Miss Tanzania, Brigitte Alfred ambaye atakuwa anavua taji lake la kwanza. “Ikumbukwe kuwa Twanga Pepeta haijatumbuiza Sinza kwa kipindi kirefu na hivyo kuandaa zawadi maalum kwa mashabiki wake katika mashindano hayo yaliyo dhaminiwa na Redds Original, Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Fredito Entertainment, CXC Africa, Clouds Media Group, Salut5.com na Sufiani Mafoto blog,” alisema Majuto. 
Alisema kuwa jumla ya warembo 12 wamejitokeza kuwania taji la mwaka huu la Sinza nan i matarajio ya waandaaji kuwa Miss Sinza wa mwaka huu atatwaa taji hilo na kufuata nyayo za Brigitte ambaye aliweza kutwaa taji la Miss Kinondoni na baadaye Miss Tanzania. 
“Tuna warembo bora ambayo wamedhamilia kufanya kweli katika mashindano ya urembo mwaka huu, wamepania kulinda hadhi ya mwaka jana, hivyo mashabiki waje kuona warembo bora waliopania kufanya kweli katika mashindano hayo,” alisema.
 Redds Miss Sinza ambaye pia ni Redds Miss Tanzania, Brigitte Alfred  alisisitiza jambo kwa warembo wa Redds Miss Sinza 2013  alipotembelea kambi ya mazoezi hiyo. Warembo hao watapanda jukwaani Ijumaa hii kuwania taji la mwaka huu

Maafisa wa Polisi kikosi cha usalama Barabarani wapewa somo juu ya matumizi ya kifaa cha kipimia ulevi madereva

$
0
0
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP. Mohammed R. Mpinga (kulia) na Mkurungezi wa Operesheni Upturn Group Co - Mr. Muhata Denis (kushoto) wakijadiliana jambo kuhusu kifaa cha kupimia ulevi (alcohol test) wakati wa semina ya Siku mbili ya kipima ulevi (alcohol test) yaliyohusisha maafisa na askari wawakilishi wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka baadhi ya mikoa Tanzania bara. Semina hiyo ilifanyika katika Chuo cha Polisi Dar es salaam- Kilwa road tarehe 29/05/2013 – 30/05/2013.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP. Mohammed R. Mpinga (katikati) akipewa taarifa fupi kuhusu semina ya siku mbili ya kifaa cha kisasa cha kupima ulevi madereva kutoka kwa Mkurungezi wa Operesheni wa kampuni ya (Upturn) - Mr. Muhata Denis (kushoto kwa Kamanda). Semina hiyo ilifanyika katika Chuo cha Polisi Dar es salaam - Kilwa road tarehe 29/05/2013 – 30/05/2013.
Picha inayoonyesha kifaa cha kipimia ulevi madereva (alchol tester) wakati wa semina ya siku mbili ya kujifunza kifaa hicho iliyofanyika katika Chuo cha Polisi Dar es salaa - Kilwa road tarehe 29/05/2013 – 30/05/2013.
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka baadhi ya mikoa Tanzania bara ambao ni washiriki wa semina ya siku mbili ya kifaa cha kupimia ulevi (alcohol tester) wakifanya mazoezi ya namna ya kutumia kifaa hicho. Semina hiyo ilifanyika katika Chuo cha Polisi Dar es salaam - Kilwa road tarehe 29/05/2013 – 30/05/2013.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP. Mohammed R. Mpinga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja iliyohusisha maafisa na askari wawakilishi wa semina wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka baadhi ya mikoa Tanzania bara. Semina hiyo ilifanyika katika Chuo cha Polisi Dar es salaam - Kilwa road tarehe 29/05/2013 – 30/05/2013.

RAIS WA ZANZIBAR AREJEA NCHINI BAADA YA KUMALIZA ZIARA YAKE NCHINI CHINA

$
0
0
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akisalimiana na Viongozi mbalimbali waliofika kumpokea hapo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar mara baada ya kuwasili akitokea nchini China kwa Ziara ya Kiserikali.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akiangalia ngoma ya kibati iliokuwa ikichezw na wanakikundi wa Amani Mkoa waliofika Uwanja wa Ndege Kumpokea akitokea nchini China kwa Ziara ya kiserikali.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akizungumza na Waandishi wa Habari hapo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar mara baada ya kuwasili akitokea nchini china kwa ziara ya Kiserikali. PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

RASIMU YA KATIBA ILIYOZINDULIWA JANA JUNI 3 2013


Waziri wa Nishati na Madini akutana na Rais wa Kampuni ya Chiyoda Corporation ya Japan

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Mh.Profesa Sospeter M. Muhongo, akimfafanulia jambo Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Chiyoda Corporation ya Japan, Bw. Shogo Shibuya. Waziri Muhongo alikutana na Bw. Shogo kwa lengo la kufanya mazungumzo kuhusu uwekezaji nchini kwenye miradi ya uzalishaji wa umeme kwa kutumia jua pamoja na ujenzi wa miundombinu ya usindikaji wa gesi asilia na mitambo ya kuzalisha umeme. Mkutano huo ulifanyika mjini Yokohama, Japan wakati wa Mkutano wa tano wa Kimataifa wa Tokyo unaojadili Maendeleo ya Afrika (Tokyo International Conference on African Development (TICAD V) uliohudhuriwa na Wakuu wa nchi za Afrika na Japan pamoja na Mawaziri na Maofisa wa Serikali hizo. Mkutano ulifanyika tarehe 1 hadi 3 Juni, 2013.

Yale yaleeeee!

Usumbufu wa waosha vioo vya magari kwenye mataa

$
0
0
ANKAL

NAOMBA UUFIKISHE UJUMBE HUU KWA WAHUSIKA WAWEZE KUTUSAIDIA KUONDOA KERO HII. 

HUYU BWANA YUPO MATAA YA UBUNGO KAMA TULIVYO MNASA LEO ASUBUHI, ANAKAWAIDA YA KUJA KUSAFISHA KIOO CHA GARI NA MARA NYINGI HUPANDA KWENYE BONAT YA GARI KUKAA NA KUEGEMEA KIOO KAMA HUTO MPATIA SENTI KIDOGO YA HUDUMA ALIYOTOA BILA KUTUMWA.

 AMEKUWA NI KERO SANA KATIKA ENEO HILO. TUNAOMBA WAHUSIKAWATUSAIDIE KUONDOA KERO HII PAMOJA NA WENGINE WALIOZAGAA MAENEO YOTE YA MATAA HAPA MJINI.

 AHSANTE SANA
 MDAU.

Ndungulile mgeni rasmi Redd's Miss Kigamboni Ijumaa

$
0
0
MBUNGE wa Jimbo la Kigamboni, Faustine Ndungulile, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika onyesho la kumsaka malkia wa kitongoji cha  Kigamboni mwaka huu "Redd's Miss Kigamboni 2013" katika shindano litakalofanyika Ijumaa Juni 7 kwenye ukumbi wa Navy Beach kuanzia saa 2:00 usiku hapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu, alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yamekamilika na mbunge huyo amekubali kuja kubariki shindano hilo.  

Mratibu huyo alisema kwamba Kamati ya Miss Kigamboni imejiandaa kufanya onyesho lililo na kiwango cha juu na wadau wa sanaa hiyo watarajie kuona mshindi anapatikana na kwenda kutetea taji la Redd's Miss Temeke na baadaye kushinda taji la taifa.

Alisema kuwa bendi ya FM Academia maarufu Wazee wa Ngwasuma itatumbuiza shindano hilo ambalo kiingilio cha viti maalum ni Sh. 10,000 na viti vya kawaida ni Sh. 5,000. Aliongeza kuwa mpaka sasa jumla ya warembo 12 wanaendelea na mazoezi hapa jijini chini ya Blessing Ngowi.

"Shindano la Redd's Miss Kigamboni mwaka huu litakuwa bomba na wadau wasisite kujitokeza safari ya Miss Tanzania inaanzia katika kitongoji hichi Ijumaa hii," Somoe aliongeza. Aliwataja washiriki watakaopanda jukwaani kuwania taji hilo ni pamoja na Rogathe Michael, Irene Rajab, Magdalena Olotu, Latifa Mohammed, Axsaritha Vedastus, Angella Lutataza, Sara Makembo, Amina Mussa,  Ellen Sulle na Zuhura Masoud.

Warembo watano watakaoshika nafasi za juu kwenye shindano hilo watapata nafasi ya kushiriki kinyang'anyiro cha Redd's Miss Temeke baadaye mwaka huu. 
Wadhamini ambao wamethibitisha kusaidia shindano hilo ni pamoja na kampuni ya bia Tanzania kupitia kinywaji cha Redd's Premium Original, Montage Limited, Clouds Media Group, Papa Z , Silver Boutique, Jambo Leo, Machapta Production na Logikit.

Mwili wa Msanii Albert Mangwea wawasili nchini Mchana huu

$
0
0
Gari iliyobeba mwili wa Marehemu Albert Mangwea ikisukumwa na Mashabiki wake kutoka kwenye Sehemu ya maalum iliyokuwa imehifadhiwa maiti hiyo.Mwili wa Marehemu Mangwea umepelekwa kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili,ambapo taratibu za kuuga mwili huo zitafanyika kesho kwenye Viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar kuanzia asubuhi.
Msafara ukielekea Muhimbili.
Gari maalum la Kubeba Mwili Msanii wa Muziki wa Kizaki Kipya,Marehemu Albert Mangwea likiwa tayari tayari kwa kubeba mwili.
Wadau mbali mbali wakiwa wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa Ndege Julius Nyerere kwa ajili ya kuupokea Mwili wa Marehemu Albert Mangwea uliowasili mchana huu kutokea nchini Afrika ya Kusini.
Wadau kibao wapo uwanja hapa hivi sasa tayari kwa kuupokea Mwili wa Marehemu Mangwea.
Rafiki kipenzi wa Marehemu Albert Mangwea,Jay Mo akihojiwa na vyombo vya hapari uwanjani hapa.
Prof. Jay nae alipata wasaha wa kuongea na vyombo vya habari juu ya Msanii mwenzao Albert Mangwea alietangulia Mbele ya haki.

KUONA PICHA ZAIDI

AU 

Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai amtembelea Balozi Kamala

$
0
0
Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) Herman Von Hebel akiweka sahihi kenye kitabu cha wageni katika Ubalozi wa Tanzania mjini Brussels kabla ya kuanza mazungumzo na Dr. Diodorus Buberwa Kamala, Balozi wa Tanzania BENELUX na Jumuiya ya Ulaya. Mazungumzo yamefanyika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania, Brussels.

AFISA HABARI wa Wizara ya Viwanda na Biashara AVAMIWA NA MAJAMBAZI

$
0
0
Afisa Habari Daraja II wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Edward Denis Nkomola amevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo, nyumbani kwake Changanyikeni Dar es Salaam na kujeruhiwa vibaya mwilini.

Edward Nkomola ni bwana harusi mtarajiwa na maandalizi ya harusi yake yapo katika hatua za mwisho ambao ndoa yake ilitarajiwa kufungwa Juni 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyo tolewa na Afisa Habari mwenzake wa Wizara hiyo Ndugu Nicodemus Thom Mushi, tukio hilo lilimkuta Nkomola majira ya aa saba usiku, ambapo majambazi wanane wakiwa na silaha mbalimbali, walivamia nyumbani kwake na wakitaka wapewe fedha alizokusanya kwa ajili ya harusi yake.

Taarifa hiyo inasema kuwa kabla ya majambazi hao kufanikisha adhma yao hiyo walivunja mlango wa chuma (grill) na mlango wa kawaida na kuanza kumshambulia kwa mapanga na kumjeruhi mara kadhaa kichwani, kumvunja mkono, kumjeruhi kwa panga pajani na kumwibia samani za ndani, fedha, simu na vifaa mbali mbali vya harusi.

Wiki iliyopita alitoka Wilayani Same kwenye Send Off ya mke wake mtarajiwa Elizabeth.

Nkomola amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kitengo cha Mifupa MOI akipatiwa matibabu na hali yake inaendelea kusimamiwa na madaktari kwa ukaribu zaidi.

Kilele cha Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 kufanyika Mlimani City,Juni 8

Waweza tambua ni wapi hapa??

$
0
0
Hii ni moja ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam,je waweza tambua ni mahala gani hapa??

Ngoma azipendazo ankal

mwili wa marehemu albert mangweha ulivyopokelewa jijini Dar jana.

LUNDENGA: MASHINDANO YA MISS TANZANIA HAKUNA RUSHWA YA NGONO

$
0
0
MKURUGENZI wa Kampuni ya Lino International Agency, waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, leo Jumanne jioni alitembelea kambi ya washiriki wanaojiandaa kushiriki katika shindano la Miss Sinza na kusisitiza hakuna rushwa ya ngono katika mashindano yao.

Lundenga aliongozana na ujumbe wake, ambao ni Bosko Majaliwa, Katibu wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye Mkuu wa Itifaki na Nidhamu wa kamati hiyo, Hidan Rico, Afisa wa Habari wa kamati hiyo, Yasson Mashaka, Mkuu wa Mipango wa Kamati hiyo na Lucas Luta, ambaye ni mjumbe.

Lundenga, alifika Meeda Pub, ambapo washiriki wa Miss Sinza wanafanya mazoezi, alifanya nao mazungumzo na washiriki hao kupata fursa ya kuuliza maswali yao yaliyokuwa yakiwakwaza kuhusu tasnia ya urembo.


Akizungumza na warembo hao, Lundenga aliwaonya washiriki hao kutojirahisi kutoa rushwa ya ngono ili kujihakikishia nafasi katika mashindano hayo.

''Msijirahisi kutoa rushwa ya ngono ili kupata nafasi, hata mimi nitakutafuna bure tu au mwandaaji yeyote atakudanganya tu na kukuacha kama ulivyo kwani mashindano haya yanafuata taratibu zake na kanuni za mashindsano yasiyoweza kutoa fursa kwa waandaaji kutoa upendeleo kwa yeyote'' alisema Lundenga

Ujumbe huo uliofika kuwatembelea katika shindano hilo, uliwataka kuwa makini kuepuka utapeli wa watu wanaowaomba ngono ili wapewe ushindi.

"Huwezi kupata ushindi kwa kutoa rushwa ya ngono, majaji wako wengi, je utawapa ngono wangapi ili uweze kufanikiwa kuwa mshindi. Hilo liko wazi kwamba huwezi kufanikiwa kwa kutoa ngono," alisema Lundenga.

Naye Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary alisema kuwa katika shindano hilo litakalofanyika Juni 7, litasindikizwa na bendi ya Twanga Pepeta, itakayotumia fursa ya kutambulisha baadhi ya nyimbo zake mpya zilizomo katika albamu ya 12 ijulikanayo kwa jina la Nyumbani ni Nyumbani ambayo itazinduliwa rasmi Juni 30 kwenye viwanja vya Leaders Club jijini.

Aidha Majuto, alisema kuwa Twanga Pepeta itakuwa ikitumbuiza kwa mara ya kwanza tokea mwaka jana mwezi  julai ambapo ilitumbuiza katika mashindano hayo hayo ya kumsaka mrembo wa Sinza. Alisema kuwa hii ni faraja kubwa kwa mashabiki wa muziki wa dansi na wa masuala ya urembo kwani Twanga Pepeta itakuwa ikimvua taji Redds Miss Tanzania, Brigitte Alfred ambaye atakuwa anavua taji lake la kwanza.
“Ikumbukwe kuwa twanga pepeta haijatumbuiza Sinza kwa kipindi kirefu na hivyo kuandaa zawadi maalum kwa mashabiki wake katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Redds Original, Mtandao wa Sufianimafoto.com, Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Fredito Entertainment, CXC Africa, Clouds Media Group na Salut5.com” alisema Majuto.

Alisema kuwa jumla ya warembo 12 wamejitokeza kuwania taji la mwaka huu la Sinza nan i matarajio ya waandaaji kuwa Miss Sinza wa mwaka huu atatwaa taji hilo na kufuata nyayo za Brigitte ambaye aliweza kutwaa taji la Miss Kinondoni na baadaye Miss Tanzania.

“Tuna warembo bora ambayo wamedhamilia kufanya kweli katika mashindano ya urembo mwaka huu,  wamepania kulinda hadhi ya mwaka jana, hivyo mashabiki waje kuona warembo bora waliopania kufanya kweli katika mashindano hayo,” alisema.
Viewing all 110088 articles
Browse latest View live




Latest Images