Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live

MBUNGE TUNDU LISU ANYIMWA DHAMANA


MAGAZETI YA LEO JUMATANO FEBRUARI 8, 2017

Sitakubali Tanesco Kupandisha Bei ya Umeme - Prof. Muhongo.

0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO - Dodoma

Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amesema kuwa msimamo wake juu ya  Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) kutopandisha gharama za umeme kwa wateja wake upo palepale.

Prof. Muhongo ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu hoja zilizowasilishwa na wabunge  juu ya zuio la upandishaji bei ya umeme kwa shirika hilo wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya shughuli za Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini katika kipindi cha mwaka  2016/2017.

“Haiwezekani wakapandisha bei ya umeme wakati kuna watu ndani ya Shirika wanamiliki hadi hoteli nne, wakijaza lita 20 za mafuta  katika magari wanaandika lita 50 na kila mwisho wa mwaka wanagawana milioni 50 kama ‘bonus’,” alifafanua Prof. Muhongo.

Ameendelea kwa kusema kuwa Shirika hilo linadaiwa kiasi cha shilingi Bil. 820, katika deni hilo kiasi cha shilingi Bil.320 bado hazijachambuliwa. Hivyo shirika hilo haliwezi kujiamulia kupandisha gharama ya umeme wakati huo huo wakiwa bado hawajachambua baadhi ya madeni yao.

Aidha Prof. Muhongo amesema kuwa, Shirika hilo linahitaji kiasi cha Dola Bil. 12 kwa ajili ya uwekezaji ili ifikapo mwaka 2020 kiasi cha Mg 5000 za umeme ziweze kuzalishwa.

Hata hivyo, Prof. Muhongo amesema amekwisha anza kufanya mazungumzo na Benki ya Dunia ili kuona kama wataweza kufadhili kiasi hicho cha fedha ili kiweze kuwekezwa katika Shirika hilo.


Aliendelea kwa kusema kuwa Shirika hilo linahitaji mabadiliko ya hali ya juu ili kulifanya kuwa la kisasa na kuendana na dhima ya nchi ya  uchumi wa viwanda ambao kwa asilimia kubwa unahitaji nishati hiyo ya umeme.

WAZIRI MHAGAMA: VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA NI YETU SOTE

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa mapambano ya kukabiliana na tatizo la Dawa za Kulevya ni jukumu la kila mwananchi na wala sio suala la kuiachia Serikali peke yake.

Ameyasema hayo bungeni jana wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia juu ya Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya UKIMWI na Dawa za Kulevya iliyoibua maswali kwa Serikali kuendelea kupambana na wanaoshiriki katika biashara haramu ya dawa za kulevya nchini.

Waziri Mhagama alieleza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha jamii yote kwa ujumla inakuwa mstari wa mbele katika kutokomeza tatizo hili linalowaathiri vijana kwa kiasi kikubwa.

“Mapambano haya ni yetu sote, yasichague mtu na iwe agenda ya Kitaifa inayowahusu Watanzania wote na ikumbukwe kuwa tatizo la dawa za kulevya lina historia tangu mwaka 1990 na Serikali imekuwa ikipambana kwa jitihada nyingi hivyo niombe watanzania wote tuunge mkono vita hii ili kumaliza kabisa tatizo hili”. Alisema Waziri

Aliongezea kuwa, dhamira hii ya Serikali ilianza kuonekana tangu kuwepo kwa sheria namba 9 ya mwaka 1995 hadi ilipofanyiwa marekebisho mwaka 2014 na kubaini kuwa asilimia 56 ya nguvu kazi ya vijana ndiyo imeathiriwa na tatizo la dawa za kulevya.

Aidha pamoja na mapambano hayo, tayari sheria namba 5 ya mwaka 2015 na miundo ya mapambano inaelekeza namna ya kupambana na vita dhidi ya dawa za kulevya.

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe alieleza Bunge kuwa ziwepo jitihada za makusudi za kuunga mkono mapambano haya yawe ya Watanzania wote kwa kutoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano na kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda kwa namna alivyojidhatiti kupambana na wote wanaoshiriki katika biashara hizi za dawa ya kulevya.

“Nieleza wazi kuwa jitihada za Serikali pekee hazitoshi ni lazima jamii iunge mkono kwa kuwafichua wanaojihusisha na mtandao huu wa Dawa za Kulevya na Mhe.Paul Makonda nampongeza kwa kuthubutu kuingia kikamilifu katika vita hii”.Alisema Mwakyembe

Alimalizia kwa kueleza kuwa, kinachohitajika ni dhamira ya dhati na si fedha, hivyo Serikali imedhamiria kukomesha kabisa tatizo hili nchini.
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akijibu hoja za wabunge mbalimbali waliochangia wakati wa kujadili Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Ukimwi Bungeni Dodoma. 


   

KOMREDI KINANA KUONGOZA MAZISHI YA VIONGOZI WA CCM KILIMANJARO

0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ataongoza mazishi ya viongozi wa CCM, waliofariki juzi, kwa ajali ya gari wakati wakitoka kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya CCM, mkoani Kilimanjaro.

" Misiba hii ni mikubwa sana na yenye kuhuzunisha, kwa hiyo nitakiwakilisha Chama, katika mazishi yote ya viongozi wetu hawa kuonesha jinsi walivyokuwa muhimu kwa Chama", amesema Kinana wakati akisafiri kutoka Mjini Dodoma kwenda Arusha ambako atalala na kesho kwenda mkoani Kilimanjaro kuanza kuongoza mazishi hayo.

Kulingana na taratibu ilizopatiwa ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM kutoka CCM mkoa wa Kilimanjaro, mazishi ya viongozi hao yatafanyika kwa siku tatu tofauti kuanzia kesho ambapo Mjumbe wa NEC wilaya ya Same, marehem Ally Mbaga atazikwa Usangi, Mwanga kesho  Februari 8, 2017 kuanzia saa tisa alasiri.

Taarifa ya taratibu hizo imesema, aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (VCCM) Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Anold Swai, atazikwa Masama Mashariki katika kijiji cha Mboyera, Februari 10, 2017, kuanzia saa 8 mchana na aliyekuwa Katibu wa Hamasa wa Shirikisho la Vyuo Vikuu Mkoa wa Kilimanjaro, Edwin Msele atazikwa eneo la Ukaoni Moshi Vijijini Februari 11, 2017 kuanzia saa tisa alasiri.

Kulingana na taarifa hiyo ya taratibu za mazishi ya viongozi hao, mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT Tawi la Chuo Kikuu cha Ushirika (Moshi) Anastazia Mslamsha, utaagwa kesho Februari 9, 2017, kuanzia asubuhi kwenye Chuo hicho na baadaye kwenda kuzikwa Rombo siku hiyo hiyo alasiri.

Katika ajali hiyo, watu saba wakiwemo viongozi hao na wanachama wanne wa CCM, walikufa baada ya gari aina ya Toyota Hilux walilokuwemo kugongwa kwa nyuma na gari la mizigo la aina Fuso, lililokosa breki katika eneo la Mwika, Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoa wa Kilimanjaro, siku ya Jumapili ya Februari 5,  2017.

Viongozi na wanachama hao walikuwa wakitoka katika kutekeleza majukumu ya Chama ya Maadhimisho ya Miaka 40 ya Kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kimkoa Wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.

ONGEZEKO LA MADUKA YA KUCHEZA KAMARI HUONGEZA PATO LA TAIFA

0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali imetolea ufafanuzi juu ya swala la michezo ya kubahatisha kuwa  ni moja ya shughuli za kiuchumi, zinazoendeshwa kwa mujibu wa sheria kama shughuli zingine. Aidha michezo yote ya kubahatisha ikiwemo Kamari (slots machines) inaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Bodi ya Michezo ya Kubahatiba Namba 4 ya mwaka 2003, Sura 41 pamoja na Kanuni zake.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Ashatu Kijaji, wakati akijibu maswali ya Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Asha Abdullah Juma, aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kudhibiti mchezo wa kamari ambao amesema huwakosesha amani wazazi na jamii nzima, kwa kuchangia uvunjifu wa maadili na nguvu kazi ya vijana inayopotea kwa kucheza kamari badala ya kushiriki katika uzalishaji.

Aidha, Dkt Kijaji, amesema kuwa kwa mujibu wa sheria, hakuna mtu au taasisi inayoruhusiwa kuendelesha biashara ya Michezo ya Kubahatisha bila kuwa na leseni kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha pamoja na vibali vingine vinavyotolewa na mamlaka zingine za biasahra. Vilevile , sheria inakataza watoto wenye umri chini wa miaka 18 kushiriki, kuingia, kukaa au kuzururazurura karibu na maeneo ya michezo ya kubahatisha.

“Mtu yeyote atakaye ruhusu mtoto chini ya miaka 18 kushiriki, kuingia au kukaa karibu na eneo la Mchezo wa Kubahatisha, anahesabika kafanya kosa na anastahili kulipia faini ya shilingi 500,000/- au kifungo  kisichopungua miezi mitatu au vyote kwa pamoja” aliongeza Dkt. Kijaji

“endapo kosa hilo litafanywa na mwendesha mchezo wa kubahatisha, Bodi ina mamlaka kisheria kumfutia leseni. Hivyo basi, wajibu wa Serikali ni kuzuia watoto na vijana walio chini ya miaka 18 kucheza michezo ya kubahatisha. Natoa rai kwa wazazi na walezi kuwazuia wao kucheza michezo hiyo” alisisitiza Dkt. Kijaji

Amewataka wote wanaoendesha michezo ya kubahatisha wazingatie sheria na kanuni zilizowekwa, huku akiwaangaliza wazazi na walezi na jamii kwa ujumla ihakikishe kuwa vijana  wanazingatia mila na desturi zinazolinda maadili ya Kitanzania kwa kujishughulisha na shughuli halali za kiuchumi.

MFUMUKO WA BEI WA MWEZI JANUARI 2017 UMEONGEZEKA KWA ASILIMIA 0.8

0
0
Na Dotto Mwaibale


MFUMUKO wa Bei wa mwezi Januari 2017 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.8 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.7 ilivyokuwa mwezi Desemba 2016.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakati akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

"Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 105.92 mwezi Januari 2017 kutoka 1-05.04 mwezi Desemba 2016" alisema Kwesigabo.Alisema kuongeza kwa fahirisi za bei kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula.

Alitaja baadhi za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na mahindi kwa asilimia 6.3, ndizi za kupika kwa asilimia 5.8, magimbi kwa asilimia 5.3 na viazi vitamu kwa asilimia 6.5.

Alisema kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilichochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na mkaa kwa asilimia 3.2 na majokofu kwa asilimia 2.4.Kwesigabo alisema thamani ya shilingi ya Tanzania hupima badiliko la uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile za mlaji ambazo shilingi ya Tanzania ingeweza kununua katikavipindi tofauti.

"Ikiwa fahirisi za bei za Taifa zinaongezeka, uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma hupungua" alisema Kwesigabo.Alisema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 94 na senti 42 mwezi Januari, 2017 ikilinganisha na shilingi 95 na senti 20 ilivyokuewa mwezi Desemba 2016.
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei wa mwezi Januari 2017 jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth Minja.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakiwa kazini.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

UFAFANUZI JUU YA UVAAJI WA SARE ZA JWTZ NA SHUKRANI KWA VYOMBO VYA HABARI

0
0

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO


Simu ya Upepo  : “N G O M E”        Makao Makuu ya Jeshi,

Simu ya Mdomo: DSM 22150463    Sanduku la Posta 9203,

Telex                   : 41051                      DAR ES SALAAM, 07 Februari, 2017.

Tele Fax              : 2153426

Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk

Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz



Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu uvaaji wa sare za Jeshi kwa viongozi wanajeshi wanaoteuliwa na kupewa madaraka mbalimbali nje ya Jeshi. Hivi karibuni kumekuwa na mjadala juu ya uhalali wa uvaaji wa sare hizo.


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kuwataarifu wananchi kuwa kulingana na kanuni za Majeshi ya Ulinzi juzuu ya kwanza, viongozi hao wanaruhusiwa kisheria kuvaa sare za Jeshi wanapokuwa wakitekeleza majukumu maalum, hivyo wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa viongozi hao waliopo katika maeneo yao.



Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Uhusiano

Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.

Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085


WAZIRI WA ARDHI AKABIDHI HATI 1,361 MKOANI MOROGORO

0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekabidhi hati miliki za ardhi 1,361 kwa wakazi wa vijiji vya Hembeti na Dihombo wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Waziri Lukuvi amegawa hati hizo na kuwasisitiza wananchi wa wilaya ya Mvomero kuhakikisha wanapata hati za umiliki wa ardhi pamoja na kuwataka viongozi wa vijiji kote nchini kuhakikisha wanakuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji kuendelea katika maeneo yao.

Pia amesema ili mwananchi aweze kujikimu kimaisha ahakikishe anazitumia hati miliki hizo za kimila kujiletea maendeleo na anaweza kuomba mkopo benki kwa kutumia hati hiyo ili kuendesha shughuli zake za kujipatia kipato kupitia eneo analomiliki kisheria.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe amewataka wananchi kuzitunza hati hizo walizokabidhiwa na kuyatumia mashamba yao waliyomilikishwa kwa kuyalima na sio kuyauza au kukodisha kwa watu wengine na wao kubaki masikini.

Waziri Lukuvi pia alimtaka Mkuu wa mkoa wa Morogoro ayaainishe mashamba mengine makubwa yasiyoendelezwa na kugeuka kuwa mashamba pori ili amshauri Rais kuyafutia umiliki wa mashamba hayo na kurudishwa kwao ili kuweza kuwapa kaya maskini ambazo zinaishi katika maeneo ya hayo.

Kazi hii ya upimaji wa maeneo na kutoa hati kwa wananchi ni katika mpango wa nchi wa matumizi bora ya ardhi,ambapo serikali imechangua Mkoa wa Morogoro kuwa wa Mfano katika upimaji wa ardhi na utahusisha nchi nzima kwa wapimaji wa ardhi kutumia vipimo vya kisasa zaidi ambavyo kwa kiasi kikubwa vipimo hivyo vitaweza kupima ardhi kwa kipindi kifupi na kila mtu kumiliki kipande cha eneo lake.

Lukuvi alisema kuwa wakati wa kampeni mwaka 2015,Rais Dkt. John Magufuli alihaidi wazi kuwa kipindi cha miaka 10 kutakuwa na upimaji katika maeneo yote ya nchi kwa utaratibu wa mpango mzuri na wa kisasa, na kwa miaka mitano takribani vijiji 7,500  vitapimwa kwa kupangwa kila halmashauri 25 ambapo na kila mwaka vitapimwa vijiji 1,500 na kutoa hati. Alisema kuwa zoezi la upimaji linaloendelea hivi sasa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)kwa wananchi katika kuondoa migogoro inayojitokeza.
Na Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Ardhi).

    Mzee Ali Juma mkazi wa kijiji cha Hembeti wilayani Mvomero mkoani Morogoro akimshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kumuwezesha kupata hati ya kumuliki ardhi yake ambayo amekuwa nayo kwa miaka mingi bila kupewa hati hiyo, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi (NLUPC), Dkt. Stephen Nindi anayemsaidia kwa kumshika mkono.
 Bi. Zaina Hussein mkazi wa kijiji cha Dihombo wilayani Mvomero mkoani Morogoro akipokea hati ya kumuliki ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe.
 Bibi. Magret Hamis mkazi wa kijiji cha Hembeti akipokea hati ya kumuliki ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe.
 Baadhi wa wakazi wa vijiji vya Hembeti na Dihombo wilayani Mvomero mkoani Morogoro wakiwa hati zao za kumuliki ardhi mbele Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe.

DK. PALLANGYO AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikia ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo akielezea sekta ya nishati katika kikao hicho.
Sehemu ya Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo (hayupo pichani).

CHAMA CHA WALIMU MKOA WA RUVUMA KIMEJIPANGA KUWA KOMBOA WALIMU

0
0

Katibu wa chama cha Walimu mkoa wa Ruvuma Shaibu Omary.

Chama cha walimu mkoa wa Ruvuma kimepanga malengo mbalimbali ya mwaka huu wa 2017 ikiweo kutatua matatizo ambayo yanawakuta walimu pamoja na kuwawezesha kupata mikopo bila masharti yeyote.

Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa chama hicho SHAIBU OMARY wakati akizungumza na Ruvuma tv ofisini kwake.

SIMU KUENDELEA KUMSOTESHA WEMA RUMANDE

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Matumizi ya simu ya mkononi huku akiwa ameshikiliwa na jeshi la Polisi ni moja ya mambo yalitajwa mtuhumiwa wa kesi ya Dawa za kulevya Wema Sepetu kuendelea kusota rumande.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Mkuu wa Mkoa RC Makonda amesema kuwa, moja ya makosa katika nchi hii ni mtu akiwa yupo chini ya ulinzi halafu kuendelea kutumia simu ya mkononi.

Amesema kuwa mrembo huyo ambaye alikuwa akituma Video na sauti mbalimbali kuhusu hali ya maisha akiwa mahabusu ya kituo cha kati huku akimkejeli mkuu wa mkoa huenda akaendelea kuwa katika wakati mgumu zaidi kutokana na kitendo hicho cha kutumia simu akiwa mahabusu.

Makonda amesema kuwa  amezungumza na wakuu wa Magereza yote yaliyopo Dar es Salaam na wakuu wa mikoa juu ya vitendo vya watu kuingia na simu katika vituo vya Polisi.

Pia amesema kuwa matumizi ya simu hizo watu wakiwa gerezani yamekuwa yakitumika kuendeleza biashara zao za dawa za kulevya kwa njia ya mawasiliano hata kama wakiwa ndani.

KIPINDI MAALUM CHA MHE. RAIS DKT MAGUFULI MKUTANO WA AU ETHIOPIA JAN.30 - 31 2017

BREAKING NEWZZZ: Makonda ataja watuhumiwa wengine 65 wa Dawa za Kulevya. Wamo Freeman Mbowe, Mchungaji Gwajima, Yusuf Manji, Idd Azzan.

0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam,Paul Makonda amewataja watuhumiwa 65 wa Dawa za Kulevya,katika majia hayo ametajwa Freeman Mbowe,Mchungaji Gwajima,Yusuf Manji,Idd Azzan.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake mapema leo jijini Dar,RC Makonda ameingia katika awamu ya pili ya kutaja majina hayo na kuyaweka hadharani,huku akieleza kuwa watuhumiwa hao watatakiwa kufika kituo cha polisi kati siku ya Ijumaa,saa tano asubuhi kwa mahojiano zaidi.

Katika hatua nyingine RC Makonda amekiri kukamatwa kwa Mmiliki wa kituo cha Radio ya EFM,ajulikanae kwa jina la Francis Ciza,almaarufu kwa jina la Dj Majay."tulipokuwa tukifanya opereseheni ya kuwakamata Wahusika weote wa Dawa za kulevya juzi usiku nae akakamatwa kw mahojiano zaidi;"alisema Makonda.

Makonda amejibu habari za kukamatwa kwa Dj Majay mara baada ya kuulizwa swali na mmoja wa waandishi wa habari,kufuatia tetesi nyingi zilizokuwa zikisambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Soma zaidi majina ya watuhumiwa wa sakala hilo la Dawa za kulevya.






RAIS MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI WA SAUDI ARABIA, MOROCCO, ZAMBIA, CUBA, IRAN NA BURUNDI LEO

0
0
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa Saudi Arabia nchini Mhe. Mohamed Ben Mansour Al Malek Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017.
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa Morocco Mhe Abdellah Benryane Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa Zambia Mhe. Benson Keith Chali  Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017. 
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa Cuba Mhe. Lucas Dominingo Hermandes Polledo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa Iran Mhe Mousa Farhang  Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017.
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa  Burundi  nchini Mhe. Gervais Abayeho Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017.PICHA NA IKULU

Wanawake wajasiriamali wa Kisiwa cha Zanzibar wapatiwa mafunzo ya ujasiliamali na Benki ya KCB Tanzania.

0
0

Ofisa Mawasiliano ya Umma wa Benki ya KCB Tanzania Aziza Mkwizu, (aliyekaa kulia), Ofisa biashara wa benki ya KCB Tawi la Stone Town Zanzibar Lutfy Said (aliyekaa wapili kulia), Ofisa biashara wa Tawi la Stone Town Zanzibar wa Benki ya KCB, Rashid Mshana (aliyekaa wapili kushoto) na Ofisa mawasiliano ya Umma wa Benki hiyo Margaret Makere (aliyekaa watatu kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali wa Zanzibar.
Ofisa Biashara wa Tawi la Stone Town Zanzibar wa Benki ya KCB Tanzania, Rashid Mshana akimkabidhi mmoja wa wanawake wajasiriamali Bi. Rayyan Khelef cheti cha kushiriki semina ya mafunzo hayo. Meneja wa Tawi la Stone Town Zanzibar wa Benki ya KCB Tanzania Iddy Mwacha, akizungumza na wanawake wajasiriamali waliohudhuria semina ya mafunzo ya siku tatu kwa ajiri ya wanawake wajasiriamali inayoitwa 2JIAJIRI iliyoandaliwa na benki hiyo Kisiwani Zanzibar.
Mwalimu wa ujasiriamali wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Seif Abdullah akizungumza na wanawake wajasiriamali wa Zanzibar.
Mkurugenzi msaidizi wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Daniel Mghwira akitoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wajasiriamali Kisiwani Zanzibar. 

IRAN KUADHIMISHA WIKI YA UTAMADUNI KWA MAONYESHO KATIKA UKUMBI WA MAKUMBUSHO

0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bibi. Zamaradi Kawawa akizungumza wakati wa Mkutano baina ya waandishi wa habari, wawakilishi kutoka Kituo cha Utamduni cha Irani pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo jijini Dar es Salaam.Kituo cha utamaduni cha Iran kimeaandaa maonyesho ya utamaduni yatakayofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, kuanzia terehe 10 - 12 Februari kwa kuonyesha tamaduni kutoka Iran. Kutoka kulia Kutoka kushoto ni Msaidizi wa Kituo cha Utamaduni wa Iran nchini Tanzania Bibi. Fatma Ally, Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa Iran nchini Ali Bagheni na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hajjat Shani Kitogo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hajjat Shani Kitogo (wa pili kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonyesho ya Utamaduni wa Iran leo jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yanatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, kuanzia na terehe 10 - 12 Februari kwa kuonyesha tamaduni kutoka Iran. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bibi. Zamaradi Kawawa, Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa Iran nchini Ali Bagheni na Msaidizi wa Kituo cha Utamaduni wa Iran nchini Tanzania Bibi. Fatma Ally.
Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa Iran nchini Ali Bagheni akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya wiki ya utamaduni wa Iran inayotarajiwa kufanyika kuanazia tarehe 10 – 12 Februari leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Msaidizi wa Kituo cha Utamaduni wa Iran nchini Tanzania Bibi. Fatma Ally na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hajjat Shani Kitogo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bibi. Zamaradi Kawawa akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Kituo cha Utamduni cha Iran walioambatana na wasanii kutoka Irani pamoja na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. 


Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.

vodacom Tanzania bado inaendelea na zoezi la gawio la Tsh Bilioni 32 za M-Pesa kwa wateja wake

0
0
Vodacom Tanzania tunapenda kuwajulisha wateja wetu na wananchi wote kwa ujumla kuwa bado tunaendelea na zoezi letu la kuwapatia wateja wetu malipo ya faida ya kutumia M-Pesa ambayo tulianza mwezi Januari nakufanya yanaufanya mwanzo wa mwaka mpya kuwa mzuri zaidi kwa mamilioni ya wateja wetu na mawakala wa M-Pesa kwa ujumla.

Akiongea na mtandao huu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu alisema Mpaka sasa tumeweza kuwagawia wateja wetu kiasi cha shilingi Bilioni 6/- ikiwa hii ni awamu ya kwanza ya malipo ya faida ya utumiaji wa M-Pesa kutakuwa na awamu tatu za ugawaji wa fedha hizo ambapo awamu ya kwanza tayari imefanyika na awamu zingine zitaendelea mpaka mwezi wa tatu na kukamilisha zoezi zima la ugawaji wa billionii 32 kwa wateja wetu,Alisema Materu

“Napenda kuwahakikishia wateja wetu wote kwa ujumla ya kana kwamba Malipo haya yanafanyika kwa awamu kwa hiyo wasiwe na wasiwasi kwani yatawanufaisha wateja na mawakala wa M-Pesa waliopo kila kona ya Tanzania,Ugawaji huu wa faida ya kutumia M-Pesa kwa wateja na mawakala wetu ni muendelezo wa dhana kuu ya mtandao wetu tuliojiwekea”,Alisema Materu.

LISSU AWASILISHA MAOMBI YA DHAMANA MAHAKAMA KUU

0
0

Na Karama Kenyuko, Globu ya Jamii .

Mbunge wa Singida Mashariki ,Tundu Lissu amewasilisha maombi ya dhamana Mahakama kuu baada ya polisi kumnyima dhamana hiyo pamoja na kushindwa kumpeleka mahakamani licha ya kukaa kituoni hapo toka jana.

Maombi hayo yamewasilishwa na wakili wake, Peter Kibatala leo mchana katika Mahakama Kuu.

Amesema wamepeleka maombi Mahakama Kuu iingilie kati ikiwezekana impe dhamana yenyewe kwa sababu wanaamini mahakama kuu inauwezo kwenye mazingira kama hayo ambapo polisi wamekataa kumpa dhamana na masaa 48 yanaisha bila kumleta mahakamanii.

Kibatala amesema hayo leo jioni wakati akiwapa taarifa fupi waandishi wa habari walioshinda mahakamani hapo tokea asubuhi wakimsubiri Tundu Lisu kufikishwa kizimbani.

Mara baada ya muda wa mahakama kuisha jioni ya leo bila mteja wake kuletwa mahakamani, wakili kibatala alisema, mteja wao (Lisu) analalamikia mambo kadhaa ya kisheria likiwemo suala la kukamatwa bila ya waliomkamata kuwa na hati ya kumkamata (arrest warrant).Aliongeza kuwa, Lisu aliwaeleza pia alikamtwa akiwa katika shughuli za bunge, bila ya spika wa bunge kufahamu. 

Alisema Lisu aliwaeleza kuwa hata polisi waliomkamata alikuja kuwatambua kuwa ni polisi wa kweli njiani, pale alipokuwa akikamatwa alimtambua polisi mmoja tu ambaye ni RCO wa Dodoma kwani hata utambulisho wao haukuwa na imani nao.

Aliongeza kuwa mara baada ya kumkamata walimsafirisha usiku kwa usiku kana kwamba ni mhalifu mkubwa, wakati ni mtu anayefahamika, “ni wakili, mkongwe, mbunge na mnadhimu mkuu kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni lakini bado polisi wamemnyima dhamana”.

Aliongeza kuwa walitegeme leo angeletwa mahakamani lakini mpaka sasa hajaletwa, kwa hiyo tumepeleka maombi mahakama kuu iingilie kati ikiwezekana impe dhamana yenyewe kwa sababu tunaamini mahakama kuu inauwezo kwenye mazingira kama haya ambapopolisi wamekataa kumpa dhamana na masaa 48 yanaisha bila kumleta mahakamai.

Kama wao walikuwa na mwezi mzima wa kupepeleleza kwa nini hawaleti mahakama. Tunatemea mahakama kuu kesho watasikiliza maombi ya dhamana au wale wanaohusika waandae majalada wamlete mahakamani tuendeshe kesi.
 Wakili wa mbunge,Tundu Lissu,Peter Kibatala akizungumza na waandishi wa habari katika viunga vya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo jijin Dar es Salaam. 

MANJI ATII AMRI YA MAKONDA,KWENDA CENTRAL POLICE KESHO BADALA YA IJUMAA

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Diwani wa kata ya Mbagala Kuu Yusuf Manji amesema amepata taarifa ya kuitwa kupitia vyombo vya habari kuwa anaitwa katika kituo cha Kati kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na kushukiwa kuwa na matumizi au uuzaji wa dawa za Kulevya .
Manji ambaye pia ni Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, amesema kuwa kama Mkuu a Mkoa anataka msaada wa kutajiwa majina ya wahusika basi asingemuita kwa kutumia vyombo vya habari kwani anahatarisha maisha yake .

Kutokana na hilo, Manji amesema kuwa yeye hatasubiri Ijumaa kwenda kuhojiwa Zaidi kesho asubuhi ataenda ili kujua anaitiwa nini ,kwani yeye ana kazi zake na hawezi kubadili ratiba, isitoshe wameitwa watu 65 kufika siku ya Ijumaa saa 5 na kutaka kujua watahojiwa kwa muda na kama akiingia mapema watasema ametoa rushwa.

Mbali na hilo ameenda mbali Zaidi na kusema kuwa amechafua jina lake na kwa suala hili na nikishatoka polisi nitamshitaki kwa udhalilishaji huu ili nipate haki yangu kwani kunichafua mimi ni sawa na kuichafua klabu ya Yanga, na kama wanachama wa Yanga hawana imani na mimi waandike barua ya kutokuwa na imani na mimi na nitjivua uongozi. 

“katiba inasema kila mtu ana haki yake, ukinichafua mimi kama Mwenyekiti wa Yanga unachafua Yanga nzima, na kama wanachama wa Yanga hawana Imani na mimi waandike barua ya kutokuwa na imani na mimi,”amesema Manji.
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live




Latest Images