Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

AFYA YA MOHAMED MATUMLA YAIMARIKA-MOI

$
0
0
UONGOZI wa taasisi ya Tiba ya mifupa Muhimbili [MOI] imesema kuwa mwanamasumbwi Mohamed Matumla (30) anaendelea vizuri baada ya jopo la madaktari kufanikiwa katika upasuaji na kwa sasa yupo kwenye uangalizi maalumu.

Matumla alipokelewa katika chumba cha wagonjwa wa dharura MOI jana alfajiri tarehe 06/02/2017 akiwa na maumivu makali ya kichwa na hali ya kupoteza kumbukumbu na fahamu  na baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina pamoja na kupata vipimo mbalimbali ikiwemo vya CT-SCAN ya ubongo ambapo kulibainika kuwa amepata jeraha kichwani na kwenye ubongo ambalo limepelekea damu kuvilia kwenye ubongo kitaalamu (Acute subdural hematoma) na kusababisha  mgandamizo kwenye ubongo upande wa kulia ambapo alihitaji upasuaji wa haraka na wa dharura.


Baada ya vipimo jana saa 3 asubuhi Matumla aliingizwa katika chumba cha upasuaji kwa ajili ya upasuaji mkubwa wa ubongo (craniotomy)na kuondoa damu iliyovilia kichwani na  upasuaji huo ulifanyika kwa mafanikio makubwa na ulifanywa na jopo la wataalamu wetu wazalendo 5 kwa muda wa masaa 3 na  tumejiridhisha kuwa ameondolewa kwenye hatari ya kupoteza maisha.

 Taasisi ya MOI inapenda kuwataarifu watanzania na wapenzi wa mchezo wa ndondi kwamba Matumla ataweza kurudi katika hali yake ya kawaida katika kipindi cha miezi 8 hadi 12 ambapo ataweza kucheza mchezo wa ngumi baada ya kupata kibali maalumu cha daktari.

IMETOLEWA NA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI MOI DR,OTHMAN KILOLOMA 7TH FEBRUARY 2017

WAZIRI WA FEDHA AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA KUJADILI MATUMIZI YA TAKWIMU ZA UMASKINI

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

MATUMIZI ya Takwimu rasmi katika kupanga maendeleo ya wananchi kwa nchi zinazoendelea yamekuwa hayaendi kwa kasi inayotakiwa kimataifa imefahamika.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Albina Chuwa Dar es Salaam leo wakati akisoma hutuba yake katika ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa kujadili matumizi ya takwimu za umaskini na namna bora ya kupima hali ya umaskini Afrika.

Alisema wakati dunia ikiendelea na utekelezaji wa malengo endelevu ya maendeleo ya dunia ya mwaka 2030 yapatayo 17, shabaha 169 na viashiria 231 ni dhahiri kuwa matumizi ya takwimu rasmi katika kufuatilia na kutathmini utekelezaji wake kila nchi haina budi kuyafanyia kazi ipasavyo.

“Kutokana na hali hiyo ndiyo maana Benki ya Dunia ikishirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango, Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeona umuhimu wa kuwa na mkutano huu wa kimataifa wa kukutanisha watakwimu, wachumi na fani nyingine za kitaalam kujadili kwa kina matumizi ya takwimu za hali ya umaskini na tafsiri yake kwa ujumla na nini kifanyike ili kuboresha zaidi tafsiri ya umaskini” alisema Dk. Chuwa.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akihutubia wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa kujadili matumizi ya takwimu za umaskini na namna bora ya kupima hali ya umaskini Afrika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Albina Chuwa akitoa hutuba yake.
Balozi wa Umoja wa Ulaya Kanda ya Afrika Mashariki, Roland Van De Geer, akitsoma hutuba yake.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird akizungumza kwenye mkutano huo.
Taswira katika mkutano huo.

WAZIRI LUKUVI AWATAKA VIONGOZI WA MIKOA YA TANGA NA MANYARA KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU

$
0
0
WAZIRI wa ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi William  Lukuvi amewataka viongozi kutoka Mkoa wa Manyara na Tanga kutekeleza agizo la Waziri Mkuu la kumaliza mgogoro wa mpaka katika ya Wilaya ya Kilindi na Kiteto kwa kuhakiki upya mpaka huo kupitia GN namba 65 ya mwaka 1961.

Lukuvi aliyazungumza hayo jana Mkoani hapa alipokutana na viongozi
  kutoka Mikoa ya Tanga na Manyara kuhusiana na mgogoro uliodumu kwa miaka mingi kati ya Wilaya hizo mbili ambapo aliwataka washirikiane kuhakikisha mgogoro huo unamalizika kama Waziri Mkuu alivyoagiza pindi alipofanya zira yake  mkoani hapa.

Aidha alisema kupitia Wizara ya ardhi imeteuwa wataalamu wa ardhi
  ambao hawatatoka kati ya Mikoa yenye mvutano wa mgogoro huo ili kujenga imani kwa wananchi na watakuwa na jukumu la kuhakiki upya mpaka huo kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

"Timu ya wataalamu kutoka wizara yangu imekwishaundwa kwa kufanya kazi
  hiyo mategemo ya utekelezaji wa majukumu hayo tunatarajia kuanza rasmi machi 1 mwaka huu na zoezi hili litadumu kwa mwezi mmoja tu na wala hakuna ubabaishaji"Alisema Lukuvi.

Alisema hakuna mpaka mpya utakaokwenda kupimwa kati ya Wilaya hizo
  mbili zaidi ya kuhakiki ule wa awali ambao unatokana na ramani ya mwaka 1961,zoezi hili la uhakiki lazima wananchi na viongozi watambue kuwa linafanyika kwa  mara ya tatu na litakuwa la mwisho.

Pia aliwataka viongozi wote kuanzia ngazi ya mkoa mpaka Kijiji

kushiriki vema katika zoezi hilo ili kuweza kujadiliana hasa pale
panapotokea mapungufu na waache kutatua mgogoro huo huku wakiwa na matakwa yao binafsi na kufanya hivyo hakutamaliza mgogoro huo zaidi ya kuuwongeza.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi akizungumza  kwenye kikao cha pamoja baina yake na viongozi wa mikoa ya Tanga na Manyara kuhusiana na mgogoro wa mipaka uliopo kati ya wilaya za kilindi na kiteto ili kuona namna ya kuumaliza
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza kwenye kikao hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Dokta Joel Bendera akizungumza kwenye mkutano huo kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Monica Kinala 
Baadhi ya wenyeviti wa halmasahuri zote mbili na wakuu wa wilaya za Kiteto na Kilindi wakifuatilia kikao hicho
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Sauda Mtondoo akifuatilia majadiliano hayo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Waziri Mahiga apokea hati za utambulisho za mabalozi wa Cuba, Zambia na Bundi

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi mteule wa Zambia nchini Tanzania Mhe.Benson Keith Chali alipowasili Wizarani Jijini Dar es Salaam kukabidhi nakala za hati za utambulisho
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea nakala za hati za utambulisho kutoka Balozi Mteule wa Cuba nchini Tanzania Mhe.Lucas Domingo Harnandez Pelledo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akipokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Burundi Mhe. Gervais Abayeho alipoziwasilisha Wizarani Jijini Dar es Salaam

MAJALIWA AKUTANA NA ASKOFU GAMANYWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Sylivester Gamanywa wa WAPO MISSION INTERNATIONAL kabla ya mazungumzo yao,Ofisini kwa Waziri Mkuu, Jijini Dar es salaam Februari 6, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Sylivester Gamanywa wa WAPO MISSION INTERNATIONAL, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 6, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MUHIMBILI YAADHIMISHA SIKU YA KIFAFA DUNIANI WILAYANI MKURANGA

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Leo imeadhimisha siku ya kifafa duniani kwa kutoa elimu ya ugonjwa huo kwa madaktari, wauguzi na wakazi wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Madaktari wa Muhimbili wameadhimisha siku hiyo ambayo hufanyika Februari 8 kila mwaka kwa kutoa elimu kwa jamii na wataalamu ili kupunguza vifo kwa watu wenye kifafa nchini.

Rais wa Chama Cha Wagonjwa wa Kifafa nchini (TEA), Profesa William Matuja amesema kwamba ugonjwa huo unatibika na amewataka wakazi hao kuacha imani za kishirikina na badala yake amewataka kuwapeleka wagonjwa hospitali mapema.

“Wengi wana imani potofu kwamba mtu mwenye kifafa, kimesababishwa na mashetani, lakini si kweli kwani karne ya 19 wanasayansi walibaini kuwa mshutuko wa ubongo ndio unasababisha kifafa kutokana na sababu mbalimbali,” amesema Profesa Matuja.

Naye Dk Njenje wa Hospitali ya Taifa Muhimbili amesema mtu anapata kifafa wakati anapozaliwa endapo ataumia sehemu ya kichwani, kukosa hewa au mtoto kuumizwa kichwani atapata degedege.

“Mtu mzima anaweza kupata degedege endapo sukari yake itakuwa imeshuka sana na ukitibu kisukari anapona,”amesema Dk Njenje.Dk Njenje amesema kwamba ili kubaini mtu ana kifafa, lazima degedege itokee zaidi ya saa 24, degedege itokee zaidi ya mara mbili au mara kwa mara na wakati mwingine inatokea bila mtu kuwa na homa.
Profesa William Matuja wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Sayansi na Tiba (MUHAS) na Rais wa Chama Cha Wagonjwa wa Kifafa nchini (TEA) akiwakumbusha madaktari na wauguzi mambo yanayosababisha kifafa na kuwataka waongeze bidii katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa hao.
Madaktari na wauguzi wakimsikiliza Profesa Matuja leo katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga ambako maadhimisho yamefanyika.
Wakazi wa Wilaya hiyo wakimsikiliza Profesa Matuja leo.
Dk Njenje akitoa elimu kwa wananchi wa Mkuranga kuhusu ugonjwa wa kifafa na jinsi ya kutibu mtu mwenye ugonjwa huo leo.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI HITIMISHO LA MKUTANO WA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI MJINI DUBAI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Profesa  Alicia Giron ambaye ni Profesa na Mtafiti wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Mexico (UNAM) wakati wa hitimisho la mkutano wa kuwawezesha wanawake kiuchumi mjini Dubai. 
SUZANA
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na mwezeshaji Susan Monahan wakati wa hitimisho la mkutano wa kuwawezesha wanawake kiuchumi mjini Dubai. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Hitimisho la  mkutano wa kuwawezesha wanawake kiuchumi mjini Dubai ukiendelea leo (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Wa pili kushoto ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan sambamba na washiriki wengine wakifutilia yaliyokuwa yakijiri kwenye  hitimisho la  mkutano wa kuwawezesha wanawake kiuchumi mjini Dubai mapema leo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

SERIKALI INAENDELEA KUDHIBITI MATUMIZI HOLELA YA FEDHA ZA KIGENI

$
0
0
Na Benny Mwaipaja-WFM,DODOMA

Serikali imesema kuwa katika kudhibiti matumizi holela ya fedha za kigeni, Benki Kuu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania imeongeza usimamizi katika maduka ya kubadilishia fedha za kigeni ambapo taarifa za kila muamala wa fedha za kigeni unaofanywa zinapaswa kuoneshwa.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni leo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Ashatu Kijaji, wakati akijibu maswali ya Mbunge wa Igunga Mhe. Dalaly Peter Kafumu aliyetaka kupewa ufafanuzi juu ya Kwanini Serikali isidhibiti matumizi holela ya dola nchini ili kupunguza utakasishaji wa fedha na kuimarisha ukuaji wa uchumi kama zinavyofanywa nchi nyingi duniani.

Aidha, Dkt Kijaji alifafanua hatua zimechukuliwa pia kuhakikisha kuwa miamala ya fedha za kigeni inayofanywa na mabenki ni ile inayohusu shughuli za kiuchumi tu ili kulinda thamani ya shilingi. 

Vilevile, tamko na mwongozo uliotolewa na Serikali mwaka 2007, ulieleza kuwa bidhaa na huduma zinazowalenga watalii au wateja wasio wakazi wa Tanzania, bei zake zinaweza kunukuliwa kwa sarafu mbili, yaani shilingi ya kitanzania na sarafu ya kigeni na malipo kufanyika kwa sarafu ambayo mlipaji atakuwa nayo. Pia, mkazi yeyote wa Tanzania asilazimishwe kulipia bidhaa au huduma yoyote hapa nchini kwa fedha za kigeni.

“Msingi wa kuruhusu soko huru la fedha za kigeni hapa nchini ni hatua ya makusudi ambayo ilichukuliwa na Serikali ili kuiwezesha nchi kuondokana na hali ya kuadimika kwa fedha za kigeni ilikuwa dola za Kimarekani milioni 4,093.7 wakati amana za fedha za kigeni za wakazi wa Tanzania zilikuwa dola za Kimarekani milioni 2,933.1 na rasilimali za fedha za kigeni za mabenki zilikuwa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 1,021.1” alisema Dkt. Kijaji.

Dkt Kijaji ameeleza kuwa Tanzania ina urari wa biashara ya nje ambao umetokana na sera huru za kigeni, ambazo zimechangia kuimarisha uchumi kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita, wastani wa ukuaji wa uchumi wa Taifa letu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita ulikua ni asilimia 7, ikiwa ni wastani wa juu sana ikilinganishwa na nchi nyingine duniani. 

“Mfano, wastani wa ukuaji wa uchumi wa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara ni asilimia 5.4 katika kipindi hicho wakati ule wa nchi zinazoibukia kiuchumi ulikua ni asilimia 5.8” alisisitiza Dkt. Kijaji

Alisema kuwa njia zinazotumika kutakatisha fedha ni pamoja na kuziingiza haramu kwenye taasisi za fedha na kuziwekeza katika rasilimali halali kama ardhi na nyumba. Baadhi ya mambo yanayowapatia wahalifu fedha haramu ni pamoja na biashara ya dawa za kulevya, rushwa, ujangili, ujambazi, ukwepaji kodi n.k. Aidha fedha zinazotokatana na shughuli za kihalifu zinaweza kuwa shilingi za Kitanzania, dola za Kimarekani au fedha nyingine yoyote ile. 

Naibu Waziri huyo wa Fedha na Mipango amesema ziko kanuni ambazo zinafuatwa na vyombo vya fedha ili kuzuia utakatishaji wa fedha zote zilizopatikana kutoka vyanzo haramu na sio dola pekee huku akibainisha kuwa Benki Kuu ya Tanzania ina jukumu la usimamizi wa taasisi za fedha, hufuatilia mabenki ili kuhakikisha kuwa kanuni hizo zinafuatwa.



DAWA YA MSONGAMANO WA MBAGALA YAPATIKANA-WAZIRI MKUU

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Wilaya za Temeke na Mkuranga kuangalia namna ya kupunguza msongamano uliopo katika eneo la Mbagala.

Moja ya hatua alizowashauri kuchukua ni pamoja na kuhamisha kituo cha mabasi ya mikoa ya kusini ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kutoka Temeke hadi Mkuranga.Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 7, 2017) alipokutana na viongozi wa wilaya hizo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutafua njia za kuondoa msongamano huo.

Amesema kwa sasa hakuna namna ambayo wataweza kuondoa msongamano huo zaidi ya kuhamishia kituo cha mabasi ya mikoa ya kusini wilayani Mkuranga.Waziri Mkuu amesema eneo la Mbagala kwa sasa lina msongamano mkubwa ambao ni lazima Serikali ichukue hatua za haraka za kuuondoa.

“Ikiwezekana mabasi ya mikoa ya kusini yaishie Mkuranga, hivyo kirikianeni kutafuta eneo la kujenga kituo kikubwa cha kisasa cha mabasi,” amesema.Amesema kituo hicho watakachokijenga kiwe na uwezo wa kuhudumia mabasi yote yatokayo mikoa ya kusini na kituo cha Mbagala kiwe cha daladala za kawaida.

Pia Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa kituo hicho kutawezesha kuongeza mapato ya Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga.Aidha Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kwenda kujadiliana katika vikao vya mabaraza ya Madiwani juu ya mkakati huo na kisha kumpelekea taarifa ifikapo Februari 15 mwaka huu.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Bw. Filberto Sanga amesema wazo hilo ni zuri na wilaya yake ina maeneo ya kutosha kujenga miundombinu hiyo.

“Ni kweli wilaya ya Temeke imeelemewa kwa maana ya maeneo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maendeleo na haina pa kupumulia zaidi ya Mkuranga , hivyo tupo tayari kushirikiana nao,” amesema.Wakati huo huo, Bw. Sanga ameiomba Serikali itakapoanza awamu ya tatu ya ujenzi wa mradi wa mabasi ya mwendo kasi ufike hadi Mkuranga mjini badala ya kuishia Vikindu.

Amesema kwa sasa wilaya yake ina viwanda 67 ambavyo kati yake vipo vinavyofanya kazi na vingine vikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi, hivyo mabasi hayo yatarahisisha usafiri kwa wafanyakazi.Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaniva amesema amefurahishwa sana na mawazo hayo ya kuhamisha kituo cha mabasi cha Mbagala kwani katika vitu vilivyokuwa vinamnyima usingizi ni pamoja na msoingamano wa mabasi na wafanyabiashara wadogo wadogo katika eneo hilo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 7, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa wilaya za Mkuranga na Temeke, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 7, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanua jambo mbele ya viongozi wa wilaya za Mkuranga na Temeke, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 7, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WIZARA YA HABARI YAZINDUA PROGRAMU YA WADAU TUZUNGUMZE

Migogoro ya ardhi haiwezi kumalizwa kwa makatazo-Nyanduga

$
0
0
Na Mbaraka Kambona,

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mheshimiwa Bahame Tom Nyanduga amesema kuwa migogoro ya ardhi nchini haiwezi kumalizwa kwa makatazo bali majadiliano.

Nyanduga aliyasema hayo Februari 6, 2017 alipokuwa anazindua taarifa ya uchunguzi wa hadharani kuhusu mgogoro wa ardhi katika kijiji cha Nyamisati, kata ya Salale, Rufiji, Mkoani Pwani.

Wakati anazindua taarifa hiyo ya uchunguzi, Nyanduga alisema kuwa migogoro ya ardhi nchini inaweza kutatuliwa kwa majadiliano na mahusiano mazuri ikiwemo kila upande kutambua majukumu ya mwenzake kwa kuzingatia haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

Mwenyekiti huyo wakati akiongea alitaja azimio la Umoja wa Mataifa la Septemba 2015 lililohusisha nchi 194 ambalo linataja misingi 17 ya maendeleo endelevu, mojawapo ni ushirikishwaji wa wananchi hususan katika kupiga vita umasikini na njaa.

“Ukivamia na kukata mazao ya watu unasabisha njaa na hivyo itakuwa umekiuka haki za binadamu na ni kinyume na azimio la Umoja wa Mataifa, katika mivutano kama hii lazima ushirikishwaji uwepo tena unaotambua jinsia zote” alisema Nyanduga,

Kauli hiyo ya Mwenyekiti inafuatia taarifa ya uchunguzi huo uliofanywa na Tume mwaka 2013 baada na kubaini vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu na misingi ya utwala bora vilivyofanywa na mamlaka dhidi ya wananchi. 
Sehemu ya maliasili zinazotokana na miti ya mikoko zilizokamatwa na Idara ya Misita Wilayani Rufiji kwa madai ya kuvunwa bila kufuata utaratibu.
Sehemu ya msitu wa Mikoko katika eneo la Rufiji- Delta
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mheshimiwa Bahame Tom Nyanduga aliyeinua vijitabu juu ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa taarifa hiyo ya uchunguzi wa hadharani kuhusu mgogoro wa ardhi katika Kata ya Salale. Kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwanasheria, Ndugu Mohamed Magati na kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibiti, Ndugu Sanga, wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Tume, Ndugu Francis Nzuki ( aliyeshika kipaza sauti) na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyamisati, Ndugu Jumanne Kikumbi.
Baadhi ya Wazee wakiwa na vitabu wakati wa uzinduzi rasmi wa taarifa hiyo ya uchunguzi wa hadharani kuhusu mgogoro wa ardhi katika Kata ya Salale.

DKT SHEIN AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA YA WATOTO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa Mahkama ya Watoto iliyopo Mahonda Wilaya ya Kaskazini B Unguja leo (kulia)Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu (kulia) wakati alipotembelea jengo la Mahkama ya Watoto liliopo Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Unguja leo baada ya kulizindua rasmi
Mwakilishi wa UNICEF katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bibi,Maniza Zaman akitoa salama zake kwa Wananchi na Viongozi wakati wa Uzinduzi wa Jengo la Mahkama ya Watoto liliopo Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Unguja leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumushi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haroun Ali Suleiman alipokuwa akizungumza machache na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kutoa hutuba yake kwa Wananchi wakati wa Uzinduzi wa Jengo la Mahkama ya Watoto liliopo Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Unguja uliofanyika leo.
Wanafunzi wa Skuli ya Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Unguja ni miongoni mwa wananchi waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa Mahkama ya Watoto,ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwa mgeni rasm.

BBC Africa debates “fake news” in Malawi

$
0
0
            
 BBC Africa will bring audiences across the world special programmes from Malawi.

Available to hear on Friday 17th Feb at 1500 GMT on the BBC World Service, BBC Africa Debate will look at how distrust of the news is affecting African press. Listeners from across the continent can also join in with the discussion by using the hashtag #BBCAfricaDebate on social media.

Presenters Akwasi Sarpong and Didi Akinyelure, will be joined by a local audience and a guest panel in Blantyre, Malawi. The recording will take place Weds 15th Feb and the debate will include a senior government official, media representatives from the public and private sector, media regulators, bloggers and news consumers.

The increased use of the internet and social media platforms has changed how journalists work and the way that citizens find and share information and entertainment. In Africa, rumours of such things as a country’s leader’s illness and allegations of ballot rigging can spread quickly. What problems does this present to the African press? And is it a journalist’s job to expose or respond to news that isn’t true?

As part of a week of special BBC events in Malawi, Focus on Africa radio will also be presented live from Blantyre on Thursday 16th and Friday 17thFebruary. The broadcasts will include features and reports from the city and beyond, plus live guests and musical acts.

BARAZA LA USHINDANI LAJIDHATITI KUWAHUDUMIA WANANCHI

$
0
0
Frank Mvungi-Maelezo

Baraza la ushindani Tanzania (FCT) lapokea na kushughulikia mashauri 139 kati 164 yaliyowasilishwa kutokana na maamuzi ya Tume ya Ushindani pamoja na Mamlaka za Udhibiti ili kuweka mazingira ya usawa katika soko nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mshauri wa Sheria wa Baraza hilo Bw. Kunda Mkenda wakati wa mkutano na waandishi habari Leo Jijini Dar es salaam.Akifafanua suala hilo Mkenda amesema kuwa dhamira ya Baraza hilo ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na ushindani wenye tija kwenye soko.

Akizungumzia majukumu ya Baraza hilo Mkenda alisema kuwa Baraza hilo linaweza kubadilisha uamuzi wa Tume ya ushindani au Mamlaka ya udhibiti ili kuweka mazingira ya usawa katika utoaji wa huduma katika soko.

“Jukumu kubwa ni kukuza na kulinda ushindani wa haki na kumlinda mlaji dhidi ya matokeo ya ukiritimba na tabia potofu katika soko ili kuepusha athari katika uchumi” Alisisitiza Mkenda.

Pia, aliongoza kuwa Baraza hilo linaweza kutoa adhabu, faini, amri, tamko au kuamuru kulipwa fidia kutokana na hasara anayokuwa amepata mlalamikaji au muwasilisihaji wa rufani katika Baraza.

Aidha, Mchumi Mwandamizi wa Baraza hilo Bw. Nonge Aly liongeza kuwa wananchi wanalo jukumu kubwa la kutumia huduma zinazotolewa na Baraza hilo.Baraza la Ushindani ni Chombo kilichoanzishwa na serikali chini ya kifungu cha 83 (1) cha Sheria ya ushindani namba 8 ya mwaka 2003.
Mshauri wa Sheria wa Baraza la Ushindani Tanzania (FCT) Bw. Ikunda Mkenda akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani)Leo Jijini Dar es salaam kuhusu mikakati ya Baraza hilo katika kushughulikia rufani za mashauri yanayowasilishwa kutokana na maamuzi ya Tume ya Ushindani(FCC) pamoja na Mamalaka za udhibiti kama EWURA,TCAA,SUMATRA na TCRA. kulia ni Mchumi Mwandamizi wa Baraza hilo Bw. Nonge Ally.
Mchumi Mwandamizi wa Baraza La Ushindani Tanzania (FCT) Bw. Nonge Ally akifafanua kwa waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu huduma zinazotolewa na Baraza hilo katika kuhakikisha kuwa kuna ushindani wenye tija katika soko. Mshauri wa Sheria wa Baraza la Ushindani Tanzania (FCT) Bw. Ikunda Mkenda
Mshauri wa Sheria wa Baraza la Ushindani Tanzania (FCT) Bw. Ikunda Mkenda akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) Leo Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Baraza la Ushindani Tanzania (FCT) Leo Jijini Dar es salaam.(Picha na Frank Mvungi-Maelezo)

MNADA WA PILI WA KIMATAIFA KWA MADINI YA TANZANITE KUFANYIKA JIJINI ARUSHA, TAREHE 9-12, FEBRUARI 2017.

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI


MNADA WA PILI WA KIMATAIFA KWA MADINI YA TANZANITE KUFANYIKA JIJINI ARUSHA, TAREHE 9-12, FEBRUARI 2017.


Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, inatoa Taarifa kwa Umma kuwa, itaendesha Mnada wa Pili wa Kimataifa kwa Madini ya Tanzanite ghafi na yaliyokatwa kuanzia tarehe 9 hadi 12, Februari 2017. Mnada huu utaendeshwa katika Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) kilichopo Jijini Arusha. Kampuni mbalimbali za ndani ya nchi zitaleta madini kwa ajili ya kuuzwa kwa wanunuzi kutoka mataifa mbalimbali Duniani.


Mnada huu ni muendelezo wa mnada wa kwanza wa madini ya Tanzanite uliofanyika mwezi Agosti, 2016 ambapo jumla ya gramu318,033.17 na Karati 3,274.70 za Tanzaniteziliuzwa na jumla ya Kampuni 43 kutoka mataifa mbalimbali Duniani zilihudhuria.


Lengo la mnada huu ni kuboresha ukusanyaji wa mapato ya Serikali katika Sekta ya Madini kwa kuhakikisha soko la uhakika kwa wauzaji wa madini hayo.


Imetolewa na:


KATIBU MKUU

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

7 FEBRUARI, 2017




TAARIFA YA SERIKALI TOKA BUNGENI LEO JIONI 07/02/2017

Mahakama imewataka mawakili wa utetezi katika kesi ya kina Mpemba kuwaeleza washtakiwa ukweli badala ya lugha tamu tamu

$
0
0

Mahakama imewataka mawakili wa utetezi katika kesi ya kukutwa na nyara za serikali zenye thamani ya sh. Milioni 785.6 inayomkabili Yusufu Yusufu maarufu kama Mpemba kuacha kuwaeleza washtakiwa lugha tamu tamu kana kwamba kesi yao imeiva.
Hakimu Mkazi Thomasi Simba wa mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu aliwaambia mawikili hao kuwaeleza ukweli washtakiwa na siyo kuwapa lugha tamu wakati wakijua fika safari yao bado ni ndefu na mbele kuna shubiri.
Hatua hiyo ilikuja wakati kesi hiyo asubuhi ilipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa na Wakili wa serikali Elia Athanas kuieleza Mahakama kuwa jalada la kesi liko kwa RCO.
"Mheshimwa kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa lakini jalada bado liko kwa RCO kwenye utaratibu wa kuandaliwa vijarada mbali mbali kwa ajili ya kupeleka mahakama ya mafisadi.
Lakini kabla kesi haijaahirishwa mawakili wa utetezi wakiongozwa na Nehemia Nkoko waliwataka Jamhuri  kumpa presha RCO ili amalize kuandaa hayo majarada na kesi iende mahakama ya mafisadi.

" kutokana na kauli za jamuhuri inaonekana kuwa upelelezi haujakamilika tu naomba wawe na kauli moja kuwa upelelezi bado", walisema.

Baada ya hoja hizo hakimu Simba aliwataka mawakili wawe wawazi kwa washtakiwa, waache kuwafanya wajue  kwamba jalada likitoka kwa RCO linarudi moja kwa moja mahakamani wakati wanajua fika kuwa ni lazima liende kwa DPP kisha Kisutu kwa Committal tayari kwa kwenda mahakama ya mafisadi.
"Safari bado ni ndefu sana kwa washtakiwa. Acheni kuwaeleza lugha tamu tamu wakati unajua mlolongo mzima" alisema hakimu Simba.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA

MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIBI ATEMBELEA MAANDALIZI YA TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA 2017 MJINI ZANZIBAR

$
0
0
Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar  Simai Mohammed Said akitowa maelezo ya kukamilika kwa maandalizi ya Tamasha hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud alipotembelea Ngome Kongwe kujionea maendeleo ya matayarisho ya Tamasha hilo litakalohudhuriwa na Wasanii wapatao 400 kutoka Zanzibar, Tanzania Bara na Nje ya Tanzania kwa kutowa burudani ya Sanaa yenye ubunifu kwa kutumia Tamaduni za Kiafrika. Hapo ni  Jukwaa la amphitheatre.
Mwenyekiti wa Tamasha la Busara Zanzibar Simai Mohammed Said akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, wakati alipofanya ziara kutembelea na kujionea maandalizi ya Tamaasha hiyo wakiwa katika Jukwaa kubwa litakalotumika kwa Wasanii kutowa burudani wakati wa maonesho mbalimbali ya Tamasha kwa Wasanii.
Fundi Mkuu wa Tamasha la Busara Zanzibar Hamza Omar Abbas akimuonyesha vyombo vya muziki vitakavyowawezesha Wasanii wakati wakiwa jukwaani wakiimba kujisikia wenyewe sauti zao wakati wa show zikiendelea. 
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mohamoud akizungumza na wafanyakazi wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar alipofika kutembelea kujionea maandalizi ya Tamasha hilo na kuwataka kuitangaza Zanzibar kwa wageni wanaotembelea kujionea maonesho ya Tamasha hilo la Tamaduni za Kiafrika kuwakutanisha wasanii mbalimbali kutoka katika Nchi za Afrika.
Wafanyakazi wa Tamasha la Sauti za Busara wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammrd Mahmoud akitowa nasaha zake kwa wafanyakazi hao wakati alipofika kutembelea maandalizi ya Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika keshokutwa Zanzibar tarehe 9-2-2017 
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 07/02/2017

BODI YA STAMICO YAJIPANGA KUFUFUA MGODI WA MAKAA YA MAWE KIWIRA COAL MINE

$
0
0
Na Mr. Pengo, MMG
BODI ya Shirika la Madini Tanzania (STAMICO) limesema limejipanga kuhakikisha linafufua shughuli za uchimbaji wa makaa ya mawe katika mgodi wa Kiwira coal mine uliosimama kwa zaidi ya miaka nane.
Hayo yalibanishwa katika Ziara ya Wajumbe wa Bodi ya STAMICO katika migodi ya Kabulo na Kiwira iliyoko Wilaya ya Ileje mkoani Songwe iliyofanyika juzi kwa lengo la kujionea hali ilivyo.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Bodi, Balozi Alexander Muganda alisema bodi iliundwa Julai mwaka jana na imefanya zioara ya kutembelea miradi yote iliyochini ya Stamico ili kuona namna ya kuiendesha kwa manufaa.
Alisema kuhusu Mgodi wa Kiwira na Kabulo, Bodi imeona jinsi itakavyoweza kuishauri Menejimenti ili iweze kuanza kuchimba makaa yam awe kwa ajili ya kuuza na mpango wa baadaye uwe kuzalisha umeme.
Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Stamico, Mhandisi Said Mkwawa alisema bodi imeona mradi ulivyo na jinsi ya kufanya uwekezaji ili shirika liweze kujiendesha kwa tija.
Alisema bodi imegundua kuwa makaa ya mawe katika mgodi wa Kiwira na Kabulo unapatikana juu juu hivyo shirika haliwezi kutumia gharama kubwa ya kuanza uchimbaji na kwamba hadi sasa kuna hazina ya tani milioni 40 hadi 50.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Luten Mstaafu Chiku Galawa akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Madini Tanzania (STAMICO) Balozi Alexandekwake kabla ya kufanya ziara katika migodi ya makaa ya mawe ya Kiwira na Kabulo.

Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO, Balozi Alexander Muganda akitoa taarifa kwa Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya kuhusu Ziara ya Bodi kutembelea migodi ya Kabulo na Kiwira coal mine

Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Kiwira, Mhandisi Aswile Mapamba akitoa maelezo kwa wajumbe wa bodi ya Stamico kuhusu mgodi wa Kabulo uliopo Ileje mkoani Songwe. 
Taarifa kamili BOFYA HAPA
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images