Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1553 | 1554 | (Page 1555) | 1556 | 1557 | .... | 3285 | newer

  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akijibu hoja za wabunge mbalimbali waliochangia wakati wa kujadili Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Ukimwi Bungeni Dodoma Januari 6, 2017.


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akizungumza na baadhi ya wabunge mara baada ya kuhairishwa kwa Mkutano wa Bunge Mjini Dodoma Januari 6, 2017 katikati ni Mbunge wa Singida Mhe. Ashyrose Matembe.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Mhe.Hawa Ghasia nje ya viwanja vya bunge Dodoma Januari 6, 2017.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde (kulia) akizungumza na Mhe. Machano Othman nje ya ukumbi wa Bunge Dodoma mara baada ya kupitishwa kwa Taarifa ya Kamati ya Ukimwi na Dawa za Kulevya Januari 6, 2017.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba baada ya kupitishwa kwa Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Masuala ya UKIMWI kuwa makadirio ya Bunge wakati wa Mkutano wa Sita wa Bunge linaloendelea Mkoani Dodoma.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kuhairishwa kwa Mkutano wa Sita wa Bunge Januari 6, 2017 Dodoma.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba wakipongezana mara baada ya kupitishwa kwa Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Ukimwi na Dawa za Kulevya Januari 6, 2017. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA)

  0 0

  Bank M Tanzania Plc has yet again recorded a robust performance in the year 2016. In what has become customary for the Bank, it has posted a record growth in total assets crossing the one trillion mark as at 31st December 2016, which is only 10th year of its operation.

  The nine year old Corporate and Investment Bank registered a pre-tax profit of TZS 23.66 Bln during the year ended December 2016 which is 35% growth compared to TZS 17.49 Bln for the previous year. 

  According to the just released financial statements of the Bank, major part of the profit was earned from interest income amounting to TZS 94.63 Bln, an increase of 30.9% over last year. The bank has successfully contained Non Interest Expenses to TZS 34.15 Bln, which is a growth of mere 4.27% over the previous year.

  Total assets grew to TZS 1,051.89 Bln as at the 31st December 2016, registering a growth of over 22% over the previous year; whereas, deposits grew to TZS 805.94 Bln during the same period, recording a growth of over 6%.

  Commenting on the performance of the Bank for the whole year 2016, Ms. Jacqueline Woiso, the Acting CEO of the Bank said that the performance was exceptionally good despite of tough market conditions.  “We have again shown an excellent performance in 2016, and we believe that this year will be even better” she said.

  Ms. Woiso said that the Bank, which is just nine years old, has managed to attain this growth due to its client focus, professional expertise, trust and confidence reposed on it by its customers.

  In terms of product development during the previous year, Bank M rolled out Money. Moja Kwa Moja, which enables Bank M clients to upload their outward clearing cheques from the convenience of their offices rather than operating through the traditional ways where a client will be required to physically deposit the cheques at the bank prior to clearance. Additionally the bank is also in the final stages of upgrading its core banking system to Flexcube version 12, a product of Oracle Financial Services.

  “Bank M has continued to focus on family owned corporates and this single minded focus has helped the Bank to clearly understand the requirement of its target clients and develop all its products & services based on the needs and expectations of the clients. This recognition is due to the demands made on the Bank by its corporate clientele to whom the Bank is truly indebted. The bank was adjudged as the “Best Corporate Bank – Tanzania for 2016” during Banker Africa East Africa Awards for 2016 ceremony awards organised by the CPI Financials in Dubai”, she added.

  0 0


  Ujumbe wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL Limited) uliwasili Visiwani Komoro tarehe 5 February, 2017. Ujumbe huo ukiongozwa na Bw. Emmanuel Korosso ulipokelewa na Mhe. Chabaka Kilumanga, Balozi wa Tanzania, Visiwani Komoro. Aidha Mwenyekiti huyo aliongozana pia na Bw. Ladislaus E. Matindi Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL. 

  Madhumini ya ziara hiyo ilikuwa ni kuja kuangalia namna gani ATCL inaweza kutanua wigo wa safari zake Visiwani Komoro. Hii ikiwa ni sehemu ya mkakati wa shirika hilo kuweza kulidhibiti kikamilifu soko la anga la Visiwa vya Komoro ambapo kwa sasa Soko hilo limekuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa mashirika mengine ya Kimataifa kama vile  Ethiopian Airlines, Air Madagscar, Kenya Airways n.k.


  Katika ziara hiyo, wajumbe walipata fursa ya kuongozana na Mhe. Balozi kwenda Kisiwa cha Anjoun na kufanya mazungumzo na Gavana wa Kisiwa hicho Mhe. Abdou Salami Abdou. Ifahamike kwamba Shirika la ndege la ATCL hufanya safari zake mara tatu kwa wiki Visiwani Komoro ambapo ndege hiyo hutua katika uwanja wa Kimataifa wa Prince Said Ibrahim Jijini Moroni. 

  Komoro ni Muungano wa Visiwa Vitatu ambavyo ni Anjoun, Ngazidja na Moheli.  Hata hivyo imeonekana kuwa abiria wengi wanaosafiri kuja Tanzania kwa ajili ya shughuli za biashara hutokea Katika Kisiwa cha Anjoun.  Imejidhihirisha kuwa  abiria kutoka Ksiwa cha Anjoun hupata usumbufu kwa vile hakuna safari za moja kwa moja kutoka Kisiwa hicho kwenda Dar es Salaam, hali ambayo imeonekana kuongeza ghara za usafiri kwa abiria hao.


  Aidha katika mazungumzo yao na Gavana wa Kisiwa cha Anjoun ujumbe huo uliwasilisha maombi ya ATCL kupewa kibali cha kutua Kisiwa cha Anjoun ambapo Gavana huyo aliridhia maombi hayo na kueleza kufurahishwa kwake na dhamira ya ATCL kufanya safari zake Kisiwani hapo. 
   Bw. Ladislaus Matindi akisamilimiana na Gavana wa Anjoun Mhe. Abdou Salam Abdou
    Mazungmzo yakiendelea katika ofisi ya Gavana
   Mhe Balozi akilakiwa na viongozi mbalimbali wa Kisiwa
   Mhe Balozi akiongoza kikao na wadau wa biashara kutoka Kisiwa cha Anjoun.


  0 0


  0 0
  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Kamati ya Bodi ya Ligi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa 72), imemfungia Kocha wa Stand United, Hemed Suleiman ‘Morocco’ kushiriki michezo mitatu uwanjani na faini ya Sh 500,000 (laki tano).

  Katika mechi Na. 160 ya Ligi Kuu ya Vodacom uliozikutanisha timu za JKT Ruvu na Stand United iliyochezwa Januari 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Morocco aliondolewa kwenye benchi (Ordered off) kwa kosa la kupiga maamuzi ya mwamuzi na kutoa lugha chafu.

  Kamati hiyo ya Saa 72 imechukua hatua hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 40 (11) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa Makocha. Morocco hata kama atakuwa amemaliza mechi tatu nje ya benchi, hataruhusiwa kukaa kwenye benchi hadi awe amelipa faini hiyo.

  Adhabu hiyo ya Morocco itaendelea kumhusu hata kama utakuwa umehamia kwenye timu nyingine na katika msimu mwingine wowote.

  0 0  0 0

   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Profesa Faustin Kamuzora akiongea wakati wa mkutano na ujumbe  kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha China waliomtembelea Ofisini kwake mapema hii leo. 

   Sehemu ya ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha China waliomtembelea Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Profesa Faustin Kamuzora

  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Profesa Faustin Kamuzora akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha China uliomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukuza mahusiano kati ya Tanzania na China katika masuala ya mazingira.


  0 0


  Na Kassim Nyaki-PSRS

  Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imefanya ziara katika Vyuo vya Zanzibar ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa utaratibu wake wa kuhamasisha na kuelimisha wanafunzi wa Vyuo mbalimbali nchini kuhusu utaratibu wa uendeshaji wa mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma.

  Ziara hiyo ambayo ilifanyika kwa ushirikiano kati ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Zanzibar ililenga kutoa hamasa na elimu kwa wanafunzi wa Vyuo kama sehemu ya wadau katika mchakato wa Ajira.

  Katika ziara hiyo mada mbalimbali zimeweza kutolewa kwa wanafunzi hao ikiwemo taratibu za uendeshaji wa Mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma na changamoto zake, Masharti ya msingi ya kuzingatiwa kabla na baada ya kuwasilisha maombi ya kazi, Matumizi ya TEHAMA hususani namna ya kujisajili katika mfumo wa maombi ya kazi.

  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira Bibi Riziki Abraham akiongea na wanafunzi wa Vyuo mbalimbali alibainisha kuwa mada hizo zimelenga kutoa uelewa kwa wanafunzi wa Vyuo ili waweze kujua majukumu ya Sekretarieti ya Ajira, taratibu za kufuata kabla ya kuomba ajira Serikalini, namna ya kujiandaa kabla na wakati wa usaili pamoja na utaratibu wa uwasilishaji wa maombi ya kazi kwa njia ya mtandao ujulikanao kama Recruitment portal.

  “Wanafunzi wa vyuo kama sehemu ya wadau wetu wakubwa katika masuala ya ajira ni mategemeo yetu kuwa mtakapohitimu masomo yenu mtaingia kwenye soko la ajira, hivyo ni vizuri mkafahamu taratibu za kuomba kazi, namna ya kuandaa wasifu binafsi (CV) namna ya kuandika barua za maombi ya kazi, jinsi ya kujiandaa kabla na wakati wa usaili na utaratibu mpya wa utumaji na upokeaji wa maombi ya kazi kwa njia ya Mtandao ujulikanao kama Recruitment portal” ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuweza kushindana katika soko la ajira nchini, alisisitiza Riziki.

  Vyuo Vikuu vilivyotembelewa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar-SUZA, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Tawi la Zanzibar, Chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar pamoja na Chuo Kikuu cha Sumait.

  Aidha, ziara hiyo pia ililenga kutoa uelewa kwa wanafunzi wa Vyuo kuzifahamu Wizara na Taasisi zinazotekeleza masuala ya Muungano ambapo katika mchakato wa Ajira kwa Wizara na Taasisi hizo waombaji kazi kutoka Tanzania Bara wanapata asilimia 79 na waombaji kazi kutoka Zanzibar asilimia 21 ya mgao wa Ajira kwenye Wizara na Taasisi hizo za Muungano.

  Mkurugenzi wa Mipango na Rasilimali watu kutoka Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Bw. Hamis Haji Juma wakati akizungumza na wanafunzi wa vyuo hivyo alibainisha kuwa ziara hiyo imesaidia kuwaelimisha wanafunzi kujua fursa za Ajira kwa upana wake ikiwa ni pamoja na waombaji kazi kutoka Zanzibar kuomba nafasi za kazi zinatotangazwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Ajira zinazotangazwa kupitia Wizara na Taasisi zenye masuala ya Muungano.

  Ziara hiyo pia imetumika kuwafahamisha wadau mbalimbali ikiwemo wanafunzi wa Vyuo hivyo juu ya uwepo wa Ofisi ya Sekretarieti ya Ajira katika eneo la Shangani Zanzibar ambayo itasaidia kuboresha utendaji kazi na kuratibu masuala mtambuka yanayohusiana na uendeshaji wa mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma hasa katika Wizara na Taasisi za Muungano.
   Naibu Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Zanzibar anayesimamia Utawala  Dkt. Zakia M. Abubakar (Kulia) akiongea na Ujumbe wa Sekretarieti ya Ajira uliotembelea Zanzibar kwa ajili ya kutoa elimu ya maswala mbalimbali ya Ajira kwa wanafunzi wa vyuo Vikuu vya Zanzibar.

  Sehemu ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Tawi la Zanzibar wakisilizilza mada kuhusu namna ya kujaza Taarifa zao kwenye portal ya Ajira ili  kurahisihsa utumaji wa maombi ya kazi kwa njia ya Mtandao  (e-Application) wakati ajira zinapotangazwa.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali kuhakikisha wanatumia uwakilishi wao kutafuta wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika sekta ya viwanda nchini.
  Amesema  mkakati wa Serikali ni kuimarisha uchumi  hadi wa kati kupitia sekta ya viwanda, hivyo jukumu la mabalozi hao ni kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 7, 2017) alipokutana na mabalozi wa wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi za Uturuki, Brazil, China, Italy, Ufaransa, Jamuhuri ya Kidemkrasi ya Congo (DRC) na Uswisi.

  Mabalozi hao ni Balozi Dk. Emmanuel Nchini (Brazil), Balozi Elizabeth Kiondo (Uturuki), Balozi George Madafa (Italy), Balozi James Msekela (Uswisi),Balozi Samuel Shelukindo (Ufaransa), Balozi Paul Mella (DRC), Balozi Mbelwa Kairuki (China).

  “Serikali inahitaji watu wa kuja kuwekeza katika viwanda ili kuongeza thamani ya mazao kabla ya kuyauza nje ya nchi, hivyo jukumu lenu ni kuhakikisha tunapata wawekezaji wenye sifa,” amesema.

  Pia Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao kutumia uwakilishi wao katika nchi hizo kwa kuhakikisha wanatangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuongeza idadi ya watalii wanaokuja Tanzania.
   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akizungumza na mabalozi ambao wanaiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wanatarajiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akizungumza na mabalozi ambao wanaiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wanatarajiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akizungumza na mabalozi ambao wanaiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wanatarajiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017 .
   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017. Kutoka kushoto ni Samwel Shelukindo (Ufaransa), Dkt. James Msekela (Uswisi), Mbelwa Kairuki (China), Paul Mella (DRC), Dkt. Emmanuel Nchimbi (Brazil) George Madafa (Italy) na Elizabeth Kiondo (Uturuki). (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


  0 0

  Na: Genofeva Matemu

  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imebuni na kutanganza Programu ya kushirikisha wadau inayoitwa wadau tuzungumze itakayosaidia wizara kupata vionjo, maoni, mawazo na fikra za wadau katika kuhakikisha kwamba Wizara inafanya kama wadau wake wanavyotegemea.

  Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokua akizungumza na waandishi wa habari kutangaza programu hiyo yenye kauli mbiu ya kuitoa wizara ofisini kuipeleka kwa wadau leo Jijini Dar es Salaam.

  Prof. Gabriel amesema kuwa Wizara imekua na kauli mbiu ya kuitoa Wizara Dar es Salaam kuipeleka mikoani na sasa inaendelea na mkakati wa kuitoa wizara ofisini na kuipeleka kwa wadau kwani Shabaa kubwa ya wizara ni kuhakikisha kwamba yale yanayofanywa na wizara jamii iyafahamu katika kutekeleza nia na hari ya hapa kazi tuu ya serikali ya awamu ya tano.

  “Mpango wa programu ya wadau tuzungumze utafanyika kisekta ambapo utakua ni mkutano utakaoshirikisha mmoja wa viongozi wa wizara kukutanana na wadau na utakua na utaratibu madhubuti kwa kila mwezi siku ya jumanne saa nne asubuhi ambapo viongozi hao watakutana na vyombo vya habari wakiwa na wadau kujadili mambo ya kisekta” amesema Prof. Gabriel.

  Mpango huu utahusisha Jumanne ya kwanza ya mwezi sekta ya habari na wadau wote wa habari, jumanne ya pili ya mwezi ni kwa ajili ya sekta ya Utamaduni na wadau wote wa utamaduni, jumanne ya tatu ya mwezi ni kwa ajili ya sekta ya sanaa na wadau wote wa sanaa na mwisho jumanne ya nne ya mwezi ni kwa ajili ya sekta ya maendeleo ya michezo na wadau wake.

  Pamoja na mambo mengine program hii itatoa fursa kubwa sana kwa wadau kuleta mawazo yao ili wizara iweze kuwaingiza kwenye mnyororo wa thamani wa shughuli zake kwani wizara inatamani ifanye kwa mlengo ambao wadau weke wanatamani ifanyike.

  Progamu hii itazinduliwa rasmi tarehe 14 Mwezi Februari mwaka 2017 hapa Jijini Dar es Salaam ambapo itahushisha sekta ya Utamaduni na hapo baadaye mikutano hii inaweza kufikiriwa na kufanywa kwa kanda. Mpango huu utahusisha pia Taasisi zilizo chini ya wizara.

  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na waandishi wa habari (hawapo Pichani) leo Februari 07, 2017 Jijini Dar es Salaam kuhusu mkakati wa Wizara kuanza kuzungumza na wadau katika sekta zinazosimamiwa na Wizara yake.

  Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) akizungumza leo Februari 07,2017 Jijini Dar es Salaa kuhusu mkakati wa Wizara kuanza kuzungumza na wadau wa sekta zinazosimamiwa na Wizara yake.Picha na Raymond Mushumbusi

  0 0

  Na Ismail Ngayonga,MAELEZO-Dar es Salaam


  KATIKA mwaka 2014/15 Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) ilifanya ukaguzi katika taasisi 70 za umma ili kuangalia iwapo taasisi hizo zilizingatia sheria na kanuni za manunuzi na matumizi ya nyaraka za miongozo iliyoandaliwa na PPRA.

  Taasisi zilizoguswa na ukaguzi huo uliofanyika kati ya mwezi Aprili hadi Septemba ni pamoja na taasisi 15 zilizo katika kundi la Wizara, Idara na Wakala za Serikali, Mamlaka za Serikali za Mitaa 25 na mashirika ya umma 30.

  Aidha jumla ya mikataba 21,313 ya manunuzi yenye thamani ya Tsh Trilioni 1.05 ilifanyiwa ukaguzi huo, ikiwemo mikataba 845 ya kazi za ujenzi, ambapo mikataba 130 yenye thamani ya Tsh 697 ikihusisha ukaguzi wa thamani halisi ya matumizi ya fedha.

  Matokeo ya ukaguzi huo iliyohusisha miradi ya mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya Tsh. Milioni 964, ilibainika kuwa miradi 10 ya sekta ya ujenzi ilipata alama isiyoridhisha kutokana na thamani halisi ya fedha iliyotumika kushindwa kulingana na kiwango cha utekelezaji wa miradi iliyoainishwa.

  Miradi iliyochaguliwa kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi wa kupima thamani ya fedha ilipatikana katika utekelezaji wa mikataba ya manununzi iliyothaminiwa kwa kutumia vigezo mbalimbali ikiwemo uandaaji, usanifu na uhifadhi wa nyaraka za zabuni, mchakato wa manunuzi pamoja na usimamizi wa kazi za ujenzi na mikataba.

  Sekta ya Ujenzi ni miongoni sekta za kiuchumi zinaoongoza katika upotevu wa fedha za Serikali, na hivyo kuiingizia hasara Serikali kutokana na miradi mingi kutekelezwa chini ya kiwango na kukosekana kwa uwazi katika mikataba ya mkandarasi na taasisi.

  Ili kukabiliana na changamoto hiyo, mwaka 2008 Serikali iliifanyia marekebisho sheria ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) ili kuhakikisha kuwa sharia hiyo inaenda sambamba mazingira yaliyopo katika sekta ya ujenzi nchini hususani katika usimamizi na uendeshaji wa miradi inayosimamiwa na mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo Mikoa na Wilaya.

  Hivi karibuni Baraza hilo lilitoa taarifa yake kwa umma kuhusu tathimini ya ukaguzi wa kiufundi katika miradi 163 ya ujenzi yenye thamani ya Tsh. Bilioni 2.8 ikihusisha barabara, majengo na viwanja vya ndege.

  Ukaguzi huo uliofanyika kati ya mwaka 2005-2009 ulilenga katika kufanya mapitio ya michakato ya manunuzi, utekelezaji wa miradi, ongezeko la gharama za miradi, ubora wa kazi zilizofanyika na gharama za malipo ya zabuni.


  0 0

  Karama Kinyuko-Globu ya Jamii.

  Mahakama imewataka mawakili wa utetezi katika kesi ya kukutwa na nyara za serikali zenye thamani ya sh. Milioni 785.6 inayomkabili Yusufu Yusufu maarufu kama Mpemba kuacha kuwaeleza washtakiwa lugha tamu tamu kana kwamba kesi yao imeiva.

  Hakimu Mkazi Thomasi Simba wa mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu aliwaambia mawikili hao kuwaeleza ukweli washtakiwa na siyo kuwapa lugha tamu wakati wakijua fika safari yao bado ni ndefu na mbele kuna shubiri.

  Hatua hiyo ilikuja wakati kesi hiyo asubuhi ilipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa na Wakili wa serikali Elia Athanas kuieleza Mahakama kuwa jalada la kesi liko kwa RCO.

  "Mheshimwa kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa lakini jalada bado liko kwa RCO kwenye utaratibu wa kuandaliwa vijarada mbali mbali kwa ajili ya kupeleka mahakama ya mafisadi.

  Lakini kabla kesi haijaahirishwa mawakili wa utetezi wakiongozwa na Nehemia Nkoko waliwataka Jamuhuri kumpa presha RCO ili amalize kuandaa hayo majarada na kesi iende mahakama ya mafisadi.

  " kutokana na kauli za jamuhuri inaonekana kuwa upelelezi haujakamilika tu naomba wawe na kauli moja kuwa upelelezi bado", walisema.

  Baada ya hoja hizo hakimu Simba aliwataka mawakili wawe wawazi kwa washtakiwa, waache kuwafanya wajue kwamba jalada likitoka kwa RCO linarudi moja kwa moja mahakamani wakati wanajua fika kuwa ni lazima liende kwa DPP kisha Kisutu kwa Committal tayari kwa kwenda mahakama ya mafisadi.

  "Safari bado ni ndefu sana kwa washtakiwa, acheni kuwaeleza lugha tamu tamu wakati unajua mlolongo mzima" alisema hakimu Simba.Awali, upande wa Jamhuri uliiambia Mahakama hiyo kuwa jalada hilo liko kwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro analifanyia kazi ili liende ngazi zingine kwa hatua zaidi.

  Mkuu huyo akishamaliza kulifanyia kazi atalipeleka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga kwa hatua zaidi za kulitolea uamuzi atakaoona unafaa katika kesi hiyo.Mbali na Mpemba ambaye ni mkazi wa Tegeta, washitakiwa wengine ni Charles Mrutu (37) wa Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa (40) wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima (30) wa Mbezi, Ahmed Nyagongo (33) dereva na Pius Kulagwa (46).

  Washitakiwa hao wanadaiwa kujihusisha na mtandao wa ujangili na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 785.6.

  Ilidaiwa kuwa katika tarehe zisizofahamika kati ya Januari 2014 na Oktoba, mwaka jana wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walikusanya na kuuza vipande 50 vya meno ya tembo vyenye thamani ya dola 180,000 sawa na Sh milioni 392.8 mali ya Serikali bila kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

  Aliendelea kudai kuwa katika mashitaka ya pili, Oktoba 26 mwaka jana washitakiwa wakiwa Mbagala Zakhem, Temeke walikutwa na vipande 10 vyenye uzito wa kilo 13.85 na thamani ya dola 30,000 sawa na Sh milioni 65.4.

  Ilidaiwa kuwa katika mashitaka ya tatu, Oktoba 27 mwaka jana washitakiwa wakiwa Tabata Kisukuru, walikutwa na vipande vinne vyenye uzito wa kilo 11.1 na thamani ya dola 15,000 sawa na Sh milioni 32.7.


  Pia Oktoba 29 mwaka jana walikutwa na vipande 36 vya thamani ya Sh milioni 294.6.

  Kesi imeahirishwa hadi Februari 21 mwaka huu.

  0 0

  Tamasha la Sauti za Busara 2017 liko tayari kutikisa tasnia ya muziki wa Afrika kwa mfufulizo wa vikao vyenye lengo la kukuza mafunzo ya sanaa. Wataalamu kutoka Dar es Salaam na Dakar watakutanishwa na Movers & Shakers na kutoa nafasi kwa viongozi wa tasnia ya muziki kukutana na kubadilisha mawazo ya kitaalama.

  Ijumaa kutakua na mada inayohusu fursa za mitandaoni, changamoto na vitisho vinavuyoigusa tasnia ya muziki. Kutoka kwenye jopo la wageni Jude Clark, mwanzilishi wa Joose Digital na Eddie Hatitye, Mkurugenzi wa Music in Africa wataongelea ujuzi wao kwenye maeneo ya hatimiliki, utandawazi, digitali, soko la muziki duniani na maswala ya teknolojia ya mitandao. 

  Kwa kutambua uwezo wa kidigitali ni muhimu kwenye taaluma, wahudhuriaji watashuhudia nguvu ya mitandao ya kijamii ilivyo na nguvu ya kuunganisha mashabiki na wawekezaji, na kuongeza masoko kwa kutumia mitandao ya kijamii.

  Wanamuziki hujikuta mstari wa mbele kwenye harakati maarufu kwa kutumia sauti zao kwa niaba ya wasiosikika. Wakati mwingine wasanii hujikuta hatarini baada ya ujumbe wa muziki wao kuwatuhumu wasikilizaji na wenye mamlaka. Msanii anawezaje kutumia uhuru wa kuongea na kufungiwa kitaaluma? 

  Mada ya Jumamosi itaeleza mtazamo huru wa ubunifu Afrika, ripoti imeandikwa na waandishi 25 kutoka Nchi 14 na kuchapishwa kwa ushirikiano wa Artwatch Afrika kama sehemu ya mtandao wa Arterial, wenye lengo la kulinda uhuru wa kujieleza. Jopo litajumuisha Nelson Mandela wa kundi la Sarabi Kenya, Mamou Daffe – Mkurugenzi,Tamasha la sur le Niger, Mali na Dr. Omar Abdalla Adam –Mkurugenzi, Bodi ya Udhibiti Zanzibar.

  Jumapili wasanii wa tamasha wanakaribishwa kwa maswali na majibu ya kina. Washiriki wanatarajiwa kuwa Pat Thomas and Kyekyeku kutoka Ghana, Roland Tchakounte kutoka Cameroun, Bi Mariam Hamdani kutoka Zanzibar and Sahra Halgan kutoka Somaliland. Hii ni sehemu ya kipekee kwa wasanii kutoka bara la Afrika na sehemu mbalimbali kukutana na kubadilishana mawazo. Mada hii itaongozwa na Journey Ramadhan, meneja wa Tamasha.

  Movers & Shakers imeandaliwa kutengeneza nafasi za kipekee kwa wasanii na kuwajengea uwezo ili tasnia ya muziki Afrika Mashariki isonge mbele. Mada zitatolewa kila siku kuanzia saa 8:00 mchana mpaka saa 9:30 jioni . Hotel ya Monsoon. Kuingia ni kwa mwaliko tu. Hovyo wasanii na mameneja wa ndani wanahamasishwa kuwasiliana na waandaaji wa tamasha la Sauti za Sauti za Busara kama watapenda kushiriki.

  0 0
  Na Zainab Nyamka  Globu ya Jamii

  Kampuni ya simu ya Airtel sambamba na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Jamal Malinzi wamewataka wadau kujitokeza kuisapoti timu ya vijana ya chini ya miaka 17 Serengeti Boys ambao wamefanikiwa kwenda kombe la Mataifa Afrika kwa vijana (AFCON) nchini Gabon mwezi Mei mwaka huu.

  Malinzi alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kupata nafasi ya ushiriki kwa vijana hao baada ya timu ya Congo Brazaville kushindwa kumpelekea mchezaji wao Langa ambae alisadikiwa kuwa na umri mkubwa zaidi na kuchezeshwa kwenye mashindano ya vijana.

  Malinzi amewataka wadau kwa pamoja kusaidiana nao katika kuaindaa timu ya vijana kwani hakika mashindano haya yanahitaji kiasi kikubwa cha fedha takribani dola laki tano (500,000) ili timu iweze kuweka kambi nje ya nchi na hata kupata vifaa vya kutosha na vya kisasa.

  Meneja wa Mawasiliano  Airtel, Jackson Mmbando amesema kuwa wanawapongeza TFF kwa hatua kubwa waliyofikia ya kuifikisha hapa Serengeti Boys ila bado vijana hawa wanahitaji kupata sapoti kutoka kwa wadau na seriakali kwa ujumla.

  Mmbando amesema kuwa,  vijana hawa wanahitaji kuangaliwa kwa umakini zaidi na kujengwa kisaikolojia ili waweze kufanya vizuri kwani waliona walishaondolewa  kwenye michuano hiyo.

  "Vijana hawa wanahitaji sapoti kutoka kwa wadau ili waweze kufanikisha safari yao ya Gabon mwezi wa tano na sisi kama airtel tutasaidia katika kuitangaza timu hiyo,"amesema Mmbando

  Airtel wamekuwa wadau wakubwa sana wa kukuza soka la vijana kwa kuanzisha mashindano ya Airtel Rising Star ambapo hivi karibuni waliweza kufanya usaili wa vijana na wengine wakiwa tayari kwenye kikosi cha vijana wa Serengeti Boys.
   Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kufuzu kwa Serengeti kwenda Mataifa Afrika kwa vijana nchini Gabon, Kulia ni Meneja Mahusiano wa Airtel Jackson Mmbando.
  Meneja wa Mahusiano Airtel Jackson Mmbando akizungumza na waandishi na kuwataka wadau kujitokeza kuisapoti Serengeti Boys ili waweze kufanya vizuri kwa mashindano ya Mataifa Afrika kwa Vijana nchini Gabon

  0 0

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

  Wafanyabiashara wa Pombe za Kienyeji wanatakiwa kuwa na leseni ya kufanya biashara hiyo ambayo hutolewa na Halmashauri.

  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo ameyasema hayo, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Najma Giga juu ya Serikali imejipangaje kukabiliana na tatizo la ulevi wa kupita kiasi kwa pombe za kienyeji pamoja na sheria ya vileo ya mwaka 1969 kuwa ya zamani hivyo kutokidhi mabadiliko ya hali halisi ya vileo.

  “Pombe za kienyeji zimeanishwa katika kifungu cha 2 cha tafsiri katika Sheria ya Vileo, Sura ya 77 ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, wafanyabiashara wote wanatakiwa kuwa na leseni ambayo inatolewa na Halmashauri,” alifafanua Jafo.

  Aliendelea kwa kusema kuwa, biashara hiyo hairuhusiwi kufanyika katika muda wa kazi. Muda unaoruhusiwa kisheria ni kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 5:00 usiku kwa siku za Jumattu hadi Ijumaa na kuanzia saa 05:00 asubuhi hadi saa 06:00 usiku kwa siku za Jumamosi, Jumapili na Sikukuu.

  Vile vile amesema kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi ni tabia ya mtu ambayo inawezekana kabisa haitokani na mapungufu ya Sheria.

  Hata hivyo Wakuu wa Mikoa na Wilaya wameagizwa kusimamia taratibu za uendeshaji wa biashara za vileo na kuchukua hatua kwa watumiaji na wafanyabiashara wanaobainika kukiuka Sheria hiyo.

  Aidha amesema kuwa, endapo ipo haja ya kuifanyia marekebisho Sheria ya vileo, Serikali itakuwa tayari kupokea mapendekezo kwa eneo ambalo litaonekana kuwa na mapungufu ili kufanyiwa marekebisho kupitia Bunge.

  Jafo ametoa wito kwa Watanzania wote kutumia muda wao kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo kwa ustawi wa Taifa zima. Aidha Serikali haitasita kuchukua hatua kwa wanywaji pombe wasiozingatia utaratibu pamoja na wazururaji wakati wa kazi.

  0 0  0 0

   

  Mkuu wa wilaya wa Manyara amesema ofisi yake imejiridhisha kuwa wilaya yake inachakula cha kutosha mpaka msimu ujao: https://youtu.be/EqsYD_2byKY

  Bodi  ya maji ya bonde la maji la ziwa victoria imewataka watu wanaondesha shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji kusitisha: https://youtu.be/oSkmCFjqpQc

  Kamati ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii imeiyomba serikali kutoa fedha za maendeleo kwa wakati katika sekta mbalimbali: https://youtu.be/6OWy95qvTY4

  Chama cha wafanyakazi wa sekta ya migodi ngazi ya taifa wamewasimamisha kazi viongozi wa chama hicho kutoka tawi la GGM: https://youtu.be/9NvkVkEYEUQ

  Waziri wa ardhi amewaagiza wakuu wa mikoa ya Tanga na Manyara kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili kurahisisha migogoro ya mipaka: https://youtu.be/vQ2aC0MTrf4

  Serikali imeipongeza timu ya taifa ya vijana kwa kupata nafasi ya kushiriki michuano ya vijana wenye chini ya umri wa miaka 17 nchini Gabon: https://youtu.be/hTn33MTLHuU

  kamati ya saa 72 imemfungia kocha wa Stand United kutoshiriki michezo mitatu na faini ya laki tano kutokana na utovu wa nidhamu: https://youtu.be/HCtLloGmbyY


  0 0

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.

  Ada za uhakiki wa filamu hapa nchini zipo kwa mujibu wa sheria na kanuni, ambapo gharama hizo hulipwa kwa nakala mama na baada ya hapo mtayarishaji huzalisha nakala kwa idadi anayohitaji.

  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Anastazia Wambura ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi juu ya Serikali ina mpango gani wa kuwapunguzia wasanii gharama za ukaguzi ambapo kwa hivi sasa gharama hizo ni shilingi elfu moja kwa dakika.

  “Nchi yetu hutoza ada ambazo ni rafiki ukilinganisha na nchi nyingine, kwa mfano, Nigeria ambayo ni nchi iliyopiga hatua kubwa kwa upande wa filamu, hutoza filamu yenye urefu wa dakika 60 (filamu ya lugha asili) Naira 30,000 sawa na zaidi ya dola 150 ambayo ni sawa na Sh. 337,950 za Kitanzania na Kenya, ni sawa na Sh. 190,000,” alifafanua Anastazia Wambura.

  Aliendelea kwa kusema kuwa Tanzania hutoza filamu za Kitanzania zenye urefu wa dakika 60 kwa Sh. 60,000 (sawa na Sh. 1,000 kwa dakika) ambapo gharama hizo ni sawa na asilimia 18 ya gharama za Nigeria na asilimia 32 ya Kenya.

  Hivyo basi Tanzania imekuwa ikitoza ada hiyo ya uhakiki wa filamu kwa gharama nafuu na rafiki ukilinganisha na nchi nyingine Afrika.Akijibu swali la namna gani Bodi hiyo imejipanga kuhakikisha huduma zao zinatambulika nchi nzima tofauti na sasa ambapo wasanii wachache ndiyo wanafahamu wajibu na majukumu ya Bodi hiyo, Wambura amesema kwamba Bodi hiyo imeendelea kujitangaza kwa wadau kupitia shughuli mbalimbali za kitaifa na Kimataifa kama vile kushiriki katika maonesho ya Sabasaba.

  Vile vile bodi hiyo imekuwa ikishiriki katika wiki ya Vijana na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru pamoja na Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni Festivals (JAMAFEST). Pia hutumia vyombo mbalimbali vya habari kama vile TBC1, E-FM, Clouds media pamoja na magazeti mbalimbali kueleza watanzania kazi zinazofanywa na Bodi hiyo.

  Aidha Bodi hiyo imekuwa ikifanya warsha za kuwajengea wadau wake weledi katika masuala ya filamu sehemu mbalimbali ikiwemo mikoani na wilayani ikiwa ni moja ya maeneo ya kujitangaza.

  0 0


  0 0

  Na Karama Kenyunko,Globu ya Jamii 

  Msanii Wema Abraham Sepetu (28), Ameendelea kusota Rumande huku wasanii wenzake 13 aliokuwa akishikiliwa nao kituoni hapo wameachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuwa chini ya uangalizi wa polisi na mahakama kwa kipindi cha miaka minne. 

  Miss Tanzania 2006 huyo anaendelea kushikiliwa kwa zaidi ya saa 72 kwa sasa kwa tuhuma za kukutwa msokoto mmoja wa bangi na kusubiri uchunguzi kukamilika . 

  Taarifa kutoka chanzo makini cha habari kinasema wema ad anashikiliwa kwa uchunguzi Zaidi na muda wowote wiki hii anaweza kufikishwa mahakamani. 

  Katika kesi hiyo iliyosikilizwa leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilisikilizwa na mahakimu wawili ambapo watuhumiwa nane wa mwanzo walipewa dhamana ya milioni kumi (10,000,000) kila mmoja na watakuwa chini ya uangalizi wa polisi kwa kipindi cha mwaka mmoja. 

  Watuhumiwa hao ni Hamidu Salum Chambuso (Dogo Hamidu), Rajabu Salum, Romeo George Bangura (Romy jons), Cedou Madigo, Khalid Salum Mohamed (TID), Johana Johanenes Mathysen (Director Joan), Rachael Josephat (Rachel) na Anna Patric Kimario (Tunda). 

  Mbele ya Hakimu Mkazi , Huruma Shahidi washtakiwa walitakiwa kujibu maombi ya waleta maombi ambao ni upande wa Jamhuri yaliyowasilishwa chini ya kiapo kilichoapwa na Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Dennis Mujumba wa kitengo cha dawa za kulevya. 

  Sehemu ya kiapo hicho inadai kuwa wajibu maombi hao wanajihusisha na madawa ya kulevya hivyo kutokana na tabia hizo kuwaachia huru katika jamii bila kuwadhibiti kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani katika jamii. 

  Katika maombi hayo,upande wa Jamhuri uliiomba mahakama iwaamuru wajibu maombi (wasanii hao), kuweka dhamana ya kuwa na tabia njema kwa kipindi cha miaka mitatu na kuwamuru kuripoti katika kituo cha polisi cha kati kwa mwezi mara mbili kwa ajili ya kuangalia mwenendo wa tabia zao. 

  Aidha Jamhuri waliiomba mahakama itoe amri yoyote nyingine itakayowafanya wajibu maombi hao kuwa na tabia njema na kuachana na kujihusisha na madawa ya kulevya. 

  Upande wa utetezi uliokuwa ukiongozwa na wakili Albert Msando ulidai kuwa kifungu cha sheria 73B ambacho wasanii hao wameshtakiwa nacho hakuna sehemu inayoonyesha makosa ya uvunjifu wa amani na kwamba mtu anayejihusisha na madawa ya kulevya hawezi kuvunja amani. 

  Akitoa amri, Hakimu Shahidi amewaamuru wasanii hao kuwa chini ya uangalizi wa mahakama kwa muda wa mwaka mmoja, wametakiwa kuwekewa dhamana ya kiasi cha milioni kumi (10,000,000) kila mmoja na pia wawe chini ya ulinzi wa polisi kwa ili waweze kujirekebisha na iwapo watakiuka watarudhishwa mahakamani. 

  Aidha hakukubaliana na maombi ya kuwataka wasanii hao walipoti polisi kila mwezi mara mbili akisema kuwa watakuwa wakijiandaa. 

  Wasanii Ahmed Hashim (Petitiman), Said Masoud Linnah (Said Alteza), Nassoro Mohamed Nassoro Bakar Mohamed Khelef and Lulu Abbas Chalangwe (Lulu diva) walifikishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi Cyprian Mkeha. 

  Katika amri zake, aliwataka wasanii hao kuweka dhamana ya kiasi cha shilingi milioni ishirini (20,000,000) kila mmoja na kutojihusisha na makosa ya dawa za kulevya kwa kipindi cha miaka mitatu na wanatakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Kati kwa mwezi mara mbili pamoja na kutakiwa wabadilike na kuacha kabisa matumizi ya dawa hizo. 

  Hadi Globu ya Jamii inaondoka katika viwanja vya mahakama hiyo, wasanii hao walikuwa wamekamilisha taratibu zote za mahakama na walikuwa wakisubiri kurudishwa polisi kumalizia taratibu kabla hawajaachiwa huru. 
  Watuhumiwa wa kesi ya dawa ya za kulevya wakishushwa ndani ya gari ya polisi katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu.
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya Khalid Mohamed akiingia katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu.
  Watuhumiwa wa kesi ya dawa ya za kulevya wakiingizwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es Salaam.
  Mama yake Diamond akiwa na familia yake wakifatilia kesi ya ndugu yao yao Peti Man wakuache.
  Petman wakuache akiwa na watuhumiwa wenzie akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu.
  Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wakiwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu.
  Msanii wa bongo fleva Rachel akiwa na wenzie katika mahakama ya Hakimu mkazi kisutu

older | 1 | .... | 1553 | 1554 | (Page 1555) | 1556 | 1557 | .... | 3285 | newer