Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 153 | 154 | (Page 155) | 156 | 157 | .... | 3278 | newer

  0 0
 • 06/02/13--21:30: MKATAA KWAO MTUMWA

 • 0 0
 • 06/02/13--21:53: Air Tanzania yatua Tabora
 •  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora, Gulam Remtullah, (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mda mfupi baada ya kupokea abiria wa kwanza kutumia ndege ya Shirika la ndege la Taifa Air Tanzania, baada ya shirika hilo kurejesha huduma zake mkoani Tabora, iliyositishwa kwa kipindi ya zaidi ya mwaka mmoja  kupisha marekebisho ya uwanja huo. ATCL imekuwa ndege ya kwanza kubwa kuanza safari zake mkoani hapo. Kulia ni Afisa Mwongozaji wa ndege wa shirika la ndege la ATCL, Kabel Msumeno.
   Abiria wa kwanza kutumia ndege ya Shirika la ndege la Taifa ya Air Tanzania, wakishuka katika uwanja wa ndege wa Tabora, baada ya kufurahia safari yao kutoka Dar es Salaam. Ddege ya ATCL imekuwa ya kwanza kubwa kuruka mkoani hapo, baada ya huduma ya safari za ndege ya abiria kusitishwa kwa zaidi ya mwaka mmoja ili kupisha ujenzi wa uwanja huo.
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora, Gulam Remtullah, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika la ndege la Taifa ya Air Tanzania mda mfupi baada ya ndege ya shirika hilo kurejesha huduma zake mkoani Tabora, iliyositishwa kwa kipindi ya zaidi ya mwaka mmoja  kupisha marekebisho ya uwanja huo. ATCL imekuwa ndege ya kwanza kubwa kuanza safari zake mkoani hapo.

  0 0


  0 0
 • 06/03/13--00:46: Hoja ya Haja……….
 • Ankal Misupu mzee wa saundi. 

  Wasalaam aleuikum

  Ankal, mimi ni mdau blogu yetu ya jamii wa long taimu xana. Yaani wa siku nyingi kinoma. tangu globu ya jamii inazaliwa bado kichanga vile, nilikua naipakata. Na ki computer changu cha henzi hizo na dial-up, ilikuwa ni lazima niichungulie blog ya jamii mara tatu kwa siku, nitupe komenti mbili tatu za uongo na kweli nianze kucheka vituko vya Peter Nalitolela wa muzumbe univesiti. unaona
   
  Ankal mimi ndo watu wa mwanzoni wa kukomenti kwenye globu yetu. ila leo, nalazazimika kuchukua fursa hii kutoa dukuduku moja tu. Globu ya jamii imebadilika Kuna vitu ambavyo vimepotea na tunavimisi sana. Tumemisi ze- fulunazz ya Ankal, tumemisi konoz za ankal, tumemisi nondozz za mzee wa Oxford, mbishi ngangari us-Blogger, Debates na nondoz zilizoenda shule za economy of walsstreet, Prof.John  Mashaka na Dr. hidleband Shayo.  tumemiss Salamu za Mtu mzima Baraka wa Chibiriti wa inter milan, huko Cessnia , Mzee wa vitu vitamu vya uhakika, za italy, ma Spania, mzee wa menyu, Chef Issa,  na taswira za ankal akiwa vekesheni huko maju. unaona, yaani listi ndefu

    itakuwa vizuri sana, you know, kama vipi,  ukiwaita hawa waasisi waendeleze libeneke. Au ndio wamekuwa Zilipendwa ma classic? Ankal hawa jamaa walichangamsha sana genge. Globu ya jamii ilikuwa ni kijiwa cha kujiburudisha na kujielemisha. Tunaokaa ugenini bila marafiki, globu yetu ndiye rafiki mkubwa tuliyekuwa naye.  Hasa peter nalitolea, Ze fulanazz, US blogger na John Mashaka, Ze Konozz. Tunaomba warudi walikuwa ni entertainers na stress relieves wakubwa sana

  Mdau. J Chingwile-
  mamtoni , olimpia ugiriki

  0 0


  John Sitta alonga na Vijimambo aeleza historia yake kwa ufupi na ni kitugani kilimshawishi kuja Marekani na Abdallah Kitwara amemjulia wapi kabla ya kufanya kazi Vizion One, Inc alishawahi kufanya kazi nyingine hapa Marekani? kama ndio ni wapi?. MSIKILIZE

  0 0

  Rais wa Chama cha Wakala wa Forodha na Uondoshaji wa Shehena Tanzania (TAFFA) Bw. Stephen Ngatunga akisisitiza kuhusu serikali kulifanyia kazi suala uundaji wa mkakati wa kutangaza bandari zetu nje ya nchi kwa kufungua ofisi katika nchi zinazotuzunguka kwa lengo la kuongeza watumiaji wa bandari . Kushoto ni Mkurugenzi mshauri wa TAFFA na Bw. Jimmy Mwalugerwa (Mkurugenzi TAFFA).
  Viongozi wa Chama cha Wakala wa Forodha na Uondoshaji wa Shehena Tanzania (TAFFA). Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

  0 0

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meet and hold talks with President of Japan international Cooperation Agency (JICA) Dr. Akihiko Tanaka in Yokohama this morning. President Kikwete is in Yokohama City Japan to attend the 5th Tokyo International Conference on African Development TICAD.(photo by Freddy Maro).


  0 0

  Mhe. Spika, Anne Makinda akiwa na Mama Maria Nyerere, Waziri Mkuu Mstaafu, Ndg. John Samweli Malecela na Balozi wa Tz nchini Ug, Ndg. Komba Wakisubiria kuanza kwa ibada hiyo maalumu iliyofanyika Juni 1, Namgongo, nchini Uganda.
  Mhe. Spika katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na Viongozi wa kanisa hilo
  Mhe. Spika akiwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Margaret Nantongo Zziwa, baada ya kupanda miti ya kumbukumbu.
  Mhe. Spika akishiriki ibada hiyo maalumu iliyofanyika Namgongo nchini Uganda, pembeni yake ni Waziri wa Nchi ya Uganda, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi maalumu, Bi. Tarsis Kabwegyele na Mama Maria Nyerere.

  0 0

  Mwenyekiti wa Baraza la michezo Tanzania Dionis Malinzi(kushoto) akimkabidhi Kikombe nahodha wa timu ya chuo cha CBE,Abukakar Amri  mara baada ya chuo hicho kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Lager Pool Competitio 2013yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Leadres jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Baraza la michezo Tanzania Dionis Malinzi(kushoto) akimkabidhi zawadi ya Bingwa wa Pool wanawake 2013,Liliana Meory kutoka chuo cha mara baada ya kuibuka Bingwa.
  Mwenyekiti wa Baraza la michezo Tanzania Dionis Malinzi(kushoto) akimkabidhi zawadi ya mshindi wa Pool wanaume,Said Mohamed (kulia) wa Chuo Kikuu Ruaha (RUCO) mara baada ya kuibuka bingwa katika fainali hizo. Katikati ni meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
  Mabingwa wa Pool 2013 timu ya Chuo cha Biashara jijini Dar es Salaam(CBE) wakishangilia na Kombe mara baada ya kukabidhiwa na Mwyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania,Dionis Malinzi yaliyofanyika katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  0 0
 • 06/03/13--02:27: hapa vipi??


 • 0 0

   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea fimbo ya Kitemi kutoka kwa  Antonia Mipamo maarufu kwa jina la Tonisiza ambaye pia ni Mtemi Chigoku Masa wa Simiu baada ya  kutawazwa muwa Mtemi wa Wasukuma wakati alipozindua sherehe za Utamaduni wa Wasukuma katika uwanja wa Bujora, Kisese jijini Mwanza Juni 2, 2013.
   Baadhi ya watemi wa Kisukuma wakiingia kwenye Kituo cha Utamaduni wa kabila la Wasukuma cha Bujora kilichopo Kisesa Mwanza ambako sherehe za  Utamaduni  wa wasukuma maarufu kwa jina la Bulabo zilifanyika Juni 2, 2013.
    Baadhi ya washiriki wa sherehe za  umtamaduni wa Wasukuma maarufu kwa jina la Bulabo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia alipozindua sherehe hizo kwene uwanja wa Bujora Kisesa jijini , Mwanza  juni 2, 2013.


  0 0

  Kiongozi wa Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe (MU) akipokea cheti cha Shukrani kutoka kwa Mgeni Rasmi Katibu Tawala Msaidizi Menejementi ya Serikali za Mitaa, Noeli Kazimoto wakati wa kilele cha shindano la Wanafunzi la Excel with Grandmalt 2013 mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Katikati ni Meneja wa Kinywaji cha Grandmalt, Consolatha Adam.
  Kaimu Mshauri wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilomo Sokoine (SUA), Lydia Bupilipili (kushoto) akipokea cheti cha Shukrani kutoka kwa Mgeni Rasmi Katibu Tawala Msaidizi Menejementi ya Serikali za Mitaa, Noeli Kazimoto wakati wa kilele cha shindano la Wanafunzi la Excel with Grandmalt 2013 mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Katikati ni Meneja wa Kinywaji cha Grandmalt, Consolatha Adam.
  Washindi mbalimbali wa Shindano la Excel With Grandmalt 2013 kutoka Chuo Kikuu Mzumbe wakipiga picha ya pamoja huku wakiwa wameshikilia zawadi zao za fedha wakati wa kilele cha mashindano hayo kwa vyuo vya viwili vya Mzumbe na Sokoine mkoani humo mwishoni mwa wiki.
  Washindi mbalimbali wa Shindano la Excel With Grandmalt 2013 kutoka Chuo Kikuu Cha Kilimo Sokoine (SUA) Morogoro, wakipiga picha ya pamoja huku wakiwa wameshikilia zawadi zao za fedha wakati wa kilele cha mashindano hayo kwa vyuo vya viwili vya Mzumbe na Sokoine mkoani humo mwishoni mwa wiki.

  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishuka kutoka kwenye kivuko cha MV Sengerema tayari kufungua kampeni za udiwani kata ya Nyampulukano.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimia na wakazi wa Sengerema waliokuja kumpokea Busisi leo.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimiana na Hashimu Lundenga,mara baada ya kuwasili Busisi ,Sengerema leo.

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimiana na wakazi wa Sengerema katika viwanja vya shule ya Msingi Sengerema.
   Mzee  Bukilo akiongoza kundi lake wakati wa mkutano wa hadhara wa ufunguzi wa kampeni kata ya Nyampulukano, wilaya ya Sengerema ,Mwanza.
   Mbunge wa Sengerema ,William Ngeleja akihutubia wakazi wa kata yaNyampulukano na kuelezea jinsi ilani ya uchaguzi ilivyotekelezwa pamoja na ufafanuzi juu ya mradi mkubwa wa maji kwa wakazi wa Sengerema.
   Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita, Ndugu Joseph  Kasheku  'Musukuma' akihutubia wakazi wa Sengerema wakati wa ufunguzi wa kampeni za udiwani kata Nyampulukano,Sengerema, Mwanza.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa, Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Nyampulukano, Sengerema wakati wa ufunguzi wa kampeni za udiwani. Juni, 3, 2013.
  Mgombea kiti cha udiwani kata ya Nyampulukano  kupitia CCM,Ndugu Charles Gabriel Rugabandana akisalimia wananchi mara tu baada ya kutambulishwa rasmi.Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe 16,Juni,2013. Picha na Adam H. Mzee

  0 0

  Na Shaffie Dauda

  Mabingwa wastaafu wa soka  Tanzania bara, Smba SC imetangaza kuwa haitashiriki katika michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa kanda ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA, ikiwa itaandaliwa katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

  Uamuzi huo umechukuliwa kufuatia mjadala ulioibuka katika bunge la Tanzania baada ya waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Benard Membe kuhoji hali ya Usalama katika eneo hilo.

  Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amesema uongozi wa CECAFA ni sharti ubadilishe mahala 
  pa fainali hizo la sivyo wao hawatashiriki: ''Hatuwezi kwenda Darfur kuvalia (bullet proof) mavazi yasiyopenya risasi,'' alisema Rage na kuongeza: ''Ni wazi kuwa hali ya usalama katika eneo hilo sio nzuri kama ilivyothibitishwa na serikali.''

  Membe aliliambia bunge la Tanzania kuwa alishangazwa sana na uamuzi wa kuandaa fainali hizo katika eneo la Darfur ambalo limekubwa na mapigano ya mara kwa mara. Membe amesema serikali ya Tanzania, inachunguza hali ilivyo na kuwa watachukua uamuzi muafaka kuhusiana na suala hilo.

  ''Hatuwezi kuwatuma vijana wetu katika eneo ambalo hatuna hakikisho la Usalama,'' alisema Membe.

  Mabingwa watetezi Yanga, vile vile kutoka Tanzania ambao walikuwa wameonyesha nia ya kushiriki katika fainali hizo za Darfur, pia nao wanasema watafuata ushauri kutoka Serikalini.

  Katibu Mkuu wa Shirikisho la mchezo wa soka nchini Tanzania, TFF, Angetile Osiah, amesema wao wamehakikishiwa usalama na eneo watakalopiga kambi wakati wa mashindano hayo.

  Endapo timu hizo mbili kutoka Tanzania zitajiondoa kutoka kwa fainali hizo, itakuwa pigo kubwa kwa waandalizi wa mashindano hayo.

  Timu mbili kubwa nchini Sudan Al Hilal na Al Merreikh tayari zimethibitisha kuwa hazitashiriki kutokana na hofu za kiusalama.

  Katibu mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye amekariri kuwa eneo hilo la Darfur ni salama kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

  0 0

  Picture
  JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepata ujumbe  kupitia simu za mkononi ambao umesambazwa kwa wananchi mbalimbali ukisadikishwa kuwa unatolewa na JWTZ.

  Ujumbe huo wa simu ya mkononi unasema ‘Habari zilizotufikia hivi punde. Mtanzania yeyote, kaa makini usiokote kitu chochote ambacho una shaka nacho, kuna bomu zimerushwa toka nchi jirani Malawi zaidi ya 30 zenye uzito usiopungua tani 100. Hivyo basi uonapo kitu kipo kama chupa la chai chenye rangi ya fedha. Usiguse’
   Piga namba 0756 000042. SMS hii tuma kwa watu uwezavyo. Imetolewa na JWTZ’.

  JWTZ linapenda kuwaondoa wananchi hofu kutokana na taarifa hiyo. Kwanza, Ujumbe huo haujatolewa na
   JWTZ. JWTZ  haliwezi likatumia mfumo huo wa SMS kuwapa wananchi wake taarifa za hatari kama hizo. Aidha, JWTZ hutangaza kupitia vyombo rasmi kama vile Magazeti, Radio na Television.

  Pili, bomu la tani 100 ni zito mno,  halijawahi kutengenezwa duniani. Na kama lipo, haifahamiki bomu hilo litarushwa vipi , kwa kutumia ndege au Mzinga?.  Lakini pia, mzinga wa aina hiyo haupo duniani kote na wala hakuna ndege yenye uwezo huo, hasa kwa bomu lenye umbile dogo kama hilo(Chupa ya Chai).

  Tatu, habari hizi hazina ukweli kisayansi wala kiuhalisia au fikra za kawaida. Tunawaomba wananchi wazipuuzie taarifa hizi kwani sio za kweli ni uongo mtupu. JWTZ lipo kwa ajili ya Wanachi hivyo, kwa taarifa hizi za hatari,lazima lingewajulisha wananchi kwa njia zilizoelezwa hapo juu na si kwa simu za mkononi.

  Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
  Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
  SLP 9203, Simu: 0764-742161
  Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk

  0 0

  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI JUMATATU ALIKUWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA MIRADI YA BARABARA YA DODOMA BABATI SEHEMU YA MAYAMAYA- BONGA (188.15 KM) NA BARABARA YA TUNDURU-MANGAKA-MTAMBASWALA (202.5 KM) INAYOFADHILIWA NA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (ADB) PAMOJA NA SHIRIKA LA MAENDELEO LA JAPAN (JICA).
  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKISOMA HOTUBA YAKE KABLA YA KUZINDUA MIRADI HIYO MIKUBWA

  MTENDAJI MKUU WA TANROADS ENG.PATRICK MFUGALE AKIZUNGUMZA KABLA YA KUZINDULIWA KWA MIRADI HIYO MIKUBWA

  BAADHI YA WAHESHIMIWA WABUNGE WALIOHUDHURIA KATIKA HAFLA HIYO YA UZINDUZI WA MIRADI HIYO YA BARABARA INAYOPITA KATIKA MAJIMBO YAO WAKIMSIKILIZA WAZIRI WA UJENZI.
  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKIWA PAMOJA NA MKUU WA MKOA WA DODOMA DKT REHEMA NCHIMBI KABLA YA KUZINDUA MIRADI HIYO MIKUBWA

  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKISALIMIANA NA MBUNGE WA CHILONWA MHESHIMIWA HEZEKIAH CHIBULUNJE WAKATI WA UZINDUZI HUO MJINI DODOMA

  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIZUNGUMZA NA ALIYEWAHI KUWA WAZIRI WA UJENZI KATIKA SERIKALI YA AWAMU YA TATU MHESHIMIWA MAMA ANNA ABDALAH MARA BAADA YA KUZINDUA MIRADI HIYO MIKUBWA YA BARABARA.
  WAZIRI WA UJENZI AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WASHIRIKI MBALIMBALI MARA BAADA YA KUZINDUA MIRADI HIYO YA BARABARA


  0 0

  Taifa Stars imetua Marrakech, Morocco,  salama salimini tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Morocco itakayochezwa Jumamosi- Juni 8 mwaka huu.
   
  Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia hoteli ya Pullman ambayo pia ilikaa timu ya Ivory Coast ilipokuja kucheza na Morocco. Kikosi hicho kina wachezaji 21 wakati Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu watawasili leo Juni 4, 2013  mwaka huu saa 8 mchana wakitokea Maputo, Msumbiji ambapo timu yao ya TP Mazembe ilikuwa na mechi ya Kombe la Shirikisho.
   
  Mechi kati ya Stars na Morocco itachezwa kuanzia saa 3 usiku kwa saa za Morocco ambapo nyumbani Tanzania itakuwa ni saa 5 usiku.

  0 0

  Jamhuri ya Singapore (mji mkuu wake pia ni Singapore) ni nchi ya kisiwan Kusini Mashariki ya bara la Asia, ikiwa kusini mwa ncha ya Peninsula ya Malai na kilometer 137 kutoka mstari wa Equator. Ukubwa wa kisiwa kikuu cha Singapore ni km42 kwa urefu, wakati upana ni km23, na kina ukubwa wa kilomita za mraba 586.5. Ukubwa wake kwa jumla ukichanganya na visiwa vyake vyote ni kilomita za mrada 646.1(Zanzibar ina ukubwa wa kilomita za mraba 1464, ikiwa ni urefu wa km 86 na upana wa km36).
   Singapore ni nchi inayofanywa na visiwa 63, ikiwa imetenganishwa na nchi ya Malaysia na ghuba ya Johor kwa upande wa kaskazini na visiwa vya Riau vya Indonesia katika ghuba ya Singapore upande wa kusini. Ni nchi ya vikwangua anga ambayo imeanza mambo ya biashara miaka ya 1819, ambapo mwaka 1824 Waingereza waliitawala. Baada ya kukaliwa na Japan katika vita vya pili vya dunia nchi hii ndogo ilijipatia uhuru wake mwaka 1963, ambapo miaka miwili baadaye ikaja kujitenga na Malaysia waliyokuwa wakitawaliwa nayo kwa pamoja na Uingereza. 
  Toka wakati huo imeendelea na kuwa moja ya nchi tajiri duniani, na ni mojawapo ya nchi nne zijulikanazo kama Chui wa Asia. Singapore ni nchi ya nne duniani kama kituo kikuu cha biashara, ambapo bandari yake ni moja kati ya tano ambazo zinafanya kazi sana duniani. Uchumi wake zaidi unategemea biashara ya kusafirisha bidhaa nje ya nchi na bandari. 
  Hivi sasa Singapore  ni ya tatu duniani kwa kuwa na watu wenye kipato kikubwa. Sifa zingine za nchi hii ni kuwa ya pili duniani kwa wingi wa ma Casino na kumbi za kuchezea kamari, ni mojawapo ya vituo vitatu vikubwa vya kuchujia mafuta na pia wanaongoza katika kufanya mategenezo ya meli. Benki ya dunia tayari imeitaja Singapore kama nchi iliyo nyepesi kufanya ama kufanyia biashara, na inaongoza kwa mambo ya biashara ya fedha za kigeni, ikiwa nyuma ya London, New York na Tokyo. 
  Asilimia kubwa ya wakaazi wake ni Wachina, wkifuatiwa na watu wa mataifa ya Asia kama Wahindi, Malay na wengineo. Katika sense ya mwaka 2011, idadi ya watu wa Singapore ilikuwa milioni 5.18, ambapo milioni 3.25 ama asilimia 63 ni raia, na waliosalia (37%) ni wakaazi wa kudumu ama wafanyakazi wa mataifa mengine. Asilimia 23 ya raia wa Singapore walizaliwa nje ya nchi hiyo. Na hiyo huchanganyi na watu milioni 11 wanaotembelea kisiwa hicho kila mwaka. Lugha rasmi za Singapore ni nne. Kichina (49.9%) Kiingereza(32.3%) Ki-Malay (12.2%) na Tamil.
  Kwa kuwa Singapore ni Kisiwa kidogo kinachokaliwa na watu wengi, idadi ya magari binfasi iko chini sana kwani uthibiti wake si mchezo ili kupambana na uchafuzi wa hali ya hewa na foleni. Yaani mtu akitaka kununia gari binfasi inabidi alipe ushuru ambao ni mara moja na nusu ya bei ya hilo gari. Pia inabidi apate hati ya kukaa nalo hilo gari ya miaka 10, na bei ya kununulia hiyo hati ni sawa na bei ya gari aina ya Porsche huko Marekani! Yaani bei ya gari binfasi Singapore ni ya juu kuliko nchi yoyote inayoongea Kiingereza duniani. Hivyo ni mtu mmoja tu katika 10 mwenye gari binafsi. 
  Cha kufurahisha ni kwamba kuna sheria kadhaa zinazodumisha nidhamu na usafi wa mazingira nchini Singapore. Ya kwanza ni kosa la jinai kutumia choo na kukiacha bila ku-flush. Ukikamatwa unapigwa faini hadi upate kizunguzungu. Ni kazi ya Askari polisi kuhakikisha vyoo vya umma viko safi kila mara. 
  Sheria ingine kali ambayo ilitungwa toka mwaka 1968 ili kuhakikisha nchi inabaki safi ni hii ya usafi. Ni kosa la jinai kutupa taka ovyo barabarani. Faini yake ni dola 1,000 na pia unaweza ukaadhibiwa kutumikia adhabu ya kufanya kazi za kijamii. Ukitenda kosa hilo mara tatu unavalishwa alama inayosema “Mimi ni mchafuzi wa mazingira” 
  Kula pipi ubani (Big G ama bazooka) nako kuna sheria zake, kwanza zimepigwa marufuku kuuzwa hovyo hovyo. Ukitaka unakwenda duka la madawa na unapoitafuna hakikisha masalia unayatupa kwenye pipa la taka. Ukikutwa umetema barabarani unapigwa bonge la faini. 
  Mambo ya kukumbatiana na mpenzi wako hadharani pia ni marufuku. Hayo mambo kafanyieni ndani kwenu. Ukikutwa ni faini na hata kifungo jela. Haya ni baadhi tu ya maajabu ya Singapore ambako Ankal anakula vekesheni yake huku akiwa makini asibambwe kafanya kosa la aina hizo hapo juu.
   Sehemu ya jiji la Singapore linavyoonekana usiku
  Ankal akiwa katikati ya jiji la Singapore usiku wa kuamkia leo
  Ni saa moja na nusu asubuhi  ya leo Jumanne (Bongo ni saa 10 za Alfajiri) na Ankal analishangaa jiji la Singapore kabla ya kuweka ze fulanazzz pembeni na kuanza kula tizi la nguvu.

  0 0
 • 06/03/13--19:59: KIJIWE CHA UGHAIBUNI

 • 0 0
 • 06/03/13--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Kalala Mbwebwe na Orchestra Super Sound walitesa na "Fantaar"

older | 1 | .... | 153 | 154 | (Page 155) | 156 | 157 | .... | 3278 | newer