Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1544 | 1545 | (Page 1546) | 1547 | 1548 | .... | 3283 | newer

  0 0
  0 0


  Imeelezwa kuwa kusuasua kwa utendaji wa Kituo cha Kusafisha Mafuta cha Indeni Petroleum Refinery Limited cha Ndola, nchini Zambia ni sababu mojawapo iliyochangia kuzorota kwa ufanisi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta la TAZAMA.

  Hayo yemeelezwa hivi karibuni Jijini Dar es Salaam na Mawaziri wa Nishati wa Tanzania na Zambia mara baada ya kukamilisha ziara ya siku nne ya kutembelea mkuza wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la TAZAMA na Vituo vya Kusukuma Mafuta na kuzungumza na wafanyakazi wa vituo hivyo.

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alibainisha kwamba kiwango cha Bomba kimeshuka ikilinganishwa na hapo hapo awali kwani lilikuwa na  uwezo wa kusafirisha lita za ujazo tani milioni 1.1 za mafuta kwa mwaka lakini kwa sasa linasafirisha lita za ujazo tani 600,000 tu.
  Waziri wa Nishati wa Zambia, Mabumba David akizungumza na Wafanyakazi wa TAZAMA, Kituo cha Kigamboni. Katikati ni Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa.

  Alisema usafishaji wa Mafuta unaofanywa na Kituo hicho cha Indeni hauendani na Usafirishaji wa Bomba la TAZAMA na hivyo kuwa ni miongoni mwa sababu zinazochangia Bomba hilo kutofikia malengo.

  Aliongeza kuwa, wakati mwingine inalazimu Pampu za kusukuma mafuta kuzimwa kwani mitambo ya kusafisha inakuwa haifanyi kazi na wakati huo huo matenki ya TAZAMA huko Ndola yanakuwa yamejaa na hivyo hakuna mahala pa kuhifadhi mafuta hayo.

  Aidha, Waziri Muhongo alitaja sababu nyingine inayosababisha Bomba hilo kufanya kazi chini ya kiwango kuwa ni matumizi ya teknolojia ya kizamani ya tangu kujengwa kwake Mwaka 1968 ambayo haijabadilishwa katika maeneo mengi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TAZAMA, Davison Thawethe (kushoto) akizungumza wakati wa ziara ya Mawaziri wa Nishati wa Uganda na Tanzania ya kutembelea Bomba na Vituo vya Kusukuma Mafuta Ghafi vya kampuni hiyo. Kulia ni Waziri wa Nishati wa Zambia, Mabumba David na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo (katikati).

  Alisema mradi huo wa TAZAMA una jumla ya Vituo Saba vya Kusukuma Mafuta (pumping stations), Vitano vikiwa upande wa Tanzania na Viwili vikiwa nchini Zambia lakini ni vituo viwili tu ndivyo ambavyo vimefungwa mitambo ya kisasa huku vingine vikiendelea kutumia teknolojia hiyo ya tangu Mwaka 1968.

  “Katika vituo vyote vya TAZAMA, ni vituo viwili tu ndivyo vimebadilishwa pampu ambavyo ni Elphons Pass-Mikumi na Kigamboni huku vingine vyote bado vikiendelea kutumia teknolojia iliyopitwa na wakati,” alisema Waziri Muhongo.

  Hata hivyo, alibainisha mipango na hatua mbalimbali zinazopaswa kuchukuliwa ili kuhakikisha Bomba hilo linaboreshwa ambapo alisema kuwa, hivi sasa kwa upande wa Serikali ya Zambia ni kuboresha Bomba la Mafuta sambamba na Kituo hicho cha Indeni ili kuwe na uwiano na hivyo kufikia malengo kwa pande zote mbili.
   
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa akizungumza na Wafanyakazi wa Kituo cha TAZAMA- Kigamboni. Katikati ni Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati wa Zambia, Mabumba David.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Kiungo wa zamani wa timu ya Yanga, Tanzania Prisons na Taifa Stars, Godfrey Bony, amelazwa katika Hospitali ya Rungwe mkoani Mbeya huku akiwa hana fahamu.

  Akizungumza na Mwandishi wetu Dada wa mchezaji huyo aliyejulikna kwa jina la Neema Boniface, alisema kuwa Bony alianza kuumwa ugonjwa usiojulikana miezi mitatu iliyopita na mpaka sasa bado haijajulikana anaumwa ugonjwa gani.

  "Alikua anaumwa lakini alikua na nguvu zake, alikua anatoka anaenda kwenye shughuli zake, wakati mwingine anaenda kuangalia mpira" Alisema dada huyo.

  Neema aliendelea kueleza kwamba wiki mbili zilizopita hali ya Bony, ilibadilika ghafla na kuwa mbaya zaidi ambapo alikua akilalamika kuishiwa nguvu na wakati mwingine kupoteza fahamu hali iliyolazimu kupelekwa hospitali.

  "Tulimleta hospitali ya Makandana, Hospitali ya wilaya ya Rungwe lakini vipimo havikuonesha ugonjwa wowote ndiyo juzi ikabidi apigwe X Ray ya kifua na vipimo tumeambiwa vimetoka jana lakini jioni wakati madaktari wameishaondoka kwa hiyo wamesema watatupatia leo".

  Kwa mujibu wa maelezo ya dada huyo ni kwamba hali ya kaka yake si nzuri kwa sababu hana fahamu.

  Wadau wa Soka popote nchini, TFF na wapendasoka wote kwa ujumla mnaombwa kujitokeza kumsaidia Godfrey Bony ili aweze kupata matibabu husika na kujua ugonjwa unaomsumbua ili nyota huyu wa taifa aliyetoa jasho lake kuipeperusha bendera ya taifa letu aweze kupata msaada wa matibabu na hatimaye kurejea katika hali yake ya kawaida. 

  Kwa yeyote mwenye nia njema ya kumsaidia Godfrey anaweza kuwasiliana na dada yake kwa simu namba 0765 359 290. Chanzo: mtandao wa wapenda soka

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akikata utepe kuzindua rasmi ofisi yake iliyopo Makao Makuu ya Nchi Dodoma. Wanaoshuhudia ni watumishi wa ofisi hiyo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Vyombo vya Habari kabla ya kuzindua rasmi utoaji wa huduma wa ofisi yake iliyopo Makao Makuu ya Nchi Dodoma. Wengine ni baadhi ya Watumishi wa ofisi hiyo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akijionea moja ya shubaka linalotumika kutunzia majalada katika masijala ya ofisi yake, mara baada ya kuzindua utoaji wa huduma wa ofisi hiyo iliyopo Makao Makuu ya Nchi Dodoma. Wanaoshuhudia ni baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Idris Kikula.


  0 0

  Na  Bashir  Yakub.

  1.NI  WAKATI  GANI  WANATAKIWA  KULINDWA.
  Ni  ule  wakati  ambao  marehemu  ameacha  mali  lakini  bado  hajapatikana  msimamizi  wa  mirathi  kwa  ajili  ya   kusimamia  mali  hizo huku  kukiwa  kuna  watoto  wanaohitaji  mahitaji  muhimu  kutoka  katika  mali  hizo.  Pengine hajapatikana  msimamizi  wa  mirathi  kwakuwa  kuna  mgogoro  mahakamani,   au  ndugu  hawaelewani, au  msimamizi  wa  mirathi  aliyeteuliwa  hajulikani  alipo,   au  kuna  utata  katika  wosia n.k.  
  Chochote  kile  ambacho  kitasababisha  msimamizi  wa mirathi  achelewe  kupatikana  basi  ujue  ni  wakati  huo  ambapo  mahitaji  na  maslahi  ya  mtoto  yanatakiwa  kulindwa.

  2.  YAPI  MAHITAJI  YA  WATOTO  WADOGO.
  Mahitaji  ya  watoto  wadogo  ni  kama  ada  za  shule,  mavazi, matibabu,  na  kila  ambacho  ni  muhimu   kwa  ustawi  wa  mtoto. Na  kwa  suala  la  ada mtoto  si  lazima  awe  mdogo  sana  bali  hata  wale  wa  kidato  cha  tano,  sita,  chuo  nao  waweza  kuwa  watoto  ambao  maslahi  yao  ni  muhimu  kulindwa .

  3.  WATOTO  WANAOSTAHILI  KULINDWA.
  Watoto  wanaostahili  kulindwa  ni  wale  ambao  watakuwa  ni  warithi  halali  wa  marehemu.  Ni  wale  ambao  hakuna mgogoro  kuwa  ni  warithi  au  si  warithi. Aidha  ikiwa  kuna  mgogoro  kama  watoto  au  mtoto  fulani  ni  mrithi  halali  au  si  mrithi  basi  pia  unaweza  kuomba   kulinda maslahi  yake    ambapo  mahakama  itaamua  ikiwa  anastahili  au  hastahili.

  4.  NINI  UFANYE  KULINDA  MAHITAJI  YA WATOTO.
  ( a )  Mtu  yeyote  mwanafamilia,  ndugu,  mzazi  aliyebaki,mlezi  anatakiwa  kupeleka  maombi  mahakamani   akiiomba  mahakama   kusimamia  baadhi  ya  mali  kwa  muda  ili  kupata  mahitaji  ya  watoto  wakati  wakisubiri  utatuzi  wa  mgogoro  katika  familia.


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais, Dkt. John Magufuli hajawahi kutangaza ama kutoa kauli ya kufutwa kwa vyama vya siasa nchini.

  Ametoa kauli hiyo leo (Februari, 2, 2017) Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Mbowe  katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu.

  Katika swali lake Mheshimiwa Mbowe alisema Rais Dkt.  Magufuli alinukuliwa akisema atahakikisha anafuta vyama vyama vya upinzani na ifikapo mwaka 2020 hakuna upinzani nchini.

  Pia Mheshimiwa Mbowe alitaka kujua nini kauli ya Serikali kuhusu kunyimwa dhamana kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema ambaye anashikiliwa kwa muda miezi mitatu.

  Mbali na Mheshimiwa Lema, pia kiongozi huyo alitaka kujua kuhusiana na kufungwa kwa Mbunge wa Kilombelo, Mheshimiwa Peter Lijualikali pamoja na madiwani sita wa chama hicho ambao wamefungwa na viongozi wengine 215 wanakabiliwa na kesi mbalimbali.

  “Kwanza nataka nikanushe kwamba Mheshimiwa Rais hajawahi kutangaza kuvifuta vyama vya upinzani. Pia Watanzania wote wanajua nchi hii inaongozwa kwa sheria, kanuni na taratibu i,” amesema Waziri Mkuu.

  Waziri Mkuu ameongeza kuwa “tunajua katika kuendesha nchi tunaendesha kwa mihimili mitatu ipo Serikali, Mahakama na Bunge na hakuna mhimili unaoweza kuuingilia mhimili mwingine,”.

  “Pia Watanzania wote wanajua kwamba jambo lolote ambalo lipo Mahakamani haliwezi kuzungumzwa mahali pengine popote, hivyo siwezi kutumia nafasi hii kuzungumzia mambo yote yanayoendelea chini ya sheria na yaliyo mahakamani,” amesema.
  Wakati huo huo; Waziri Mkuu amewahakikishia Watanzania kwamba suala la upungufu wa sukari halitatokea nchini kwa sababu viwanda vya ndani vinaendelea kuzalisha na hadi mwishoni mwa Januari vilifikia asilimia 86 ya uzalishaji.

  “Hadi kufikia mwishoni mwa msimu wa uzalishaji ambao ni mwezi Machi, tunaweza kuwa tumefikia malengo na kama itajitokeza upungufu Serikali itatafuta namna nzuri ya kupata sukari kwa kushirikiana na wenye viwanda nchini,” amesema.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mvomero, Mheshimiwa Suleiman Sadiq aliyetaka kujua hali ya sukari ilivyo nchini kwa sasa na hatua gani zinazochukuliwa na Serikali ili kunusuru hali ya uhaba wa sukari isijitokeze.

  0 0

  The First Instance Division on Friday 3rd February 2017, will deliver a judgement in the case filed by Hon. Margaret Nantongo Zziwa versus the Secretary General of the East African Community. Hon. Zziwa’s case alleges that the process of her removal from the Office of EALA Speaker was illegal and an infringement of Articles 53 and 56 of the Treaty for the Establishment of the East African Community.

  Hon. Zziwa was the then elected Speaker of the EALA, after her impeachment, the Assembly elected Hon. Daniel Kidega as the Speaker for  EALA up to date.

  The Court heard the court oral evidence from witnesses for both parties’ witnesses (the Applicant and Respondent) from 26th to 29th July 2016. Also court heard oral highlights of written submissions by counsels for the parties on 21st November 2016 that concluded the hearing of the case. The judgement will be delivered by the Honourable Judges of the First Instance Division; these are; Lady Justice Monica Mugenyi (Principal Judge), Justice Isaac Lenaola (Deputy Principal Judge), Dr. Justice Faustin Ntezilyayo, Justice Fakihi A. Jundu and Justice Audace Ngiye,

  On 15th February, the Appellate Division will also resume sessions which will go up to 28th February 2017. Only four appeals will come up before the Court for scheduling conferences and hearing. All appeals will be brought before the Honourable Judges of the Appellate Division; Dr. Justice Emmanuel Ugirashebuja (President), Justice Liboire Nkurunziza (Vice President), Justice Edward Rutakangwa, Justice Aaron Ringera, and Geoffrey Kiryabwire.

  On 28th February the First Instance Division, will again continue with the sessions up to 30th March 2017. A number of cases will come up for hearing, scheduling conferences and delivery of rulings and Judgments. These include; 5 hearings, 4 scheduling conferences, 2 rulings, 1 Judgement and other 2 matters.

  The Court seats for a month every quarter due to the ad-hoc nature service of the Judges. Currently the President and the Principal Judge of the court are the only resident Judges in Arusha, other Judges come only when there are sessions or other court business.

  All matters will be in open Court 2nd Floor EACJ wing

  The East African Court of Justice (EACJ or ‘the Court’), is one of the organs of the East African Community established under Article 9 of the Treaty for the Establishment of the East African Community. Established in November 2001, the Court’s major responsibility is to ensure the adherence to law in the interpretation and application of and compliance with the EAC Treaty. Arusha is the temporary seat of the Court until the Summit determines its permanent seat. The Court’s sub-registries are located in the respective National Courts in the Partner States.

  0 0

  Na Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

  Nchi za Afrika Mashariki zimekubaliana kuwa Makao Makuu ya Lugha ya Kiswahili kuwa Tanzania ambayo yatakuwepo Zanzibar.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya jitihada mbalimbali ambazo Tanzania inazichukua katika kukuza Lugha ya Kiswahili katika ngazi ya Kimataifa.

  Nape amesema kuwa maamuzi hayo ya kuifanya Tanzania kuwa Makao Makuu ya Lugha ya Kiswahili yametokana na Tanzania kuzalisha walimu wengi wa Kiswahili ambao wanatumika katika ngazi mbalimbali za elimu ndani na nje ya nchi.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Anastazia Wambura amesema kuwa Wizara hiyo kwa sasa inachukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinakuwa mawakala wa kulinda Lugha ya Kiswahili ambapo Baraza la Kiswahili la Taifa  (BAKITA) kwa kushirikiana na wadau wa Kiswahili limeendelea kuendesha semina, warsha, makongamano na kutoa elimu inayohusu matumizi fasaha ya Lugha ya Kiswahili.

  Aidha, aliendelea kwa kusema kuwa Waandishi wa Habari wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha Lugha  hiyo inaendelezwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuzingatia matumizi sahihi ya Lugha hiyo katika majukumu yao ya kila siku.

  “Kutumia zana kama vile Kamusi na vitabu vya miongozo ya uandishi pamoja na kuhudhuria makongamano ya Kitaifa na ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili inasaidia kuongeza ujuzi na uweledi wa  Lugha ya Kiswahili, kujua istilahi za kisayansi na kiteknolojia na hivyo kuandika na kutangaza kazi bora na zenye maudhui lengwa kwa jamii na kuepuka upotoshaji wa maneno ya Kiswahili usio wa lazima,” alifafanua Anastazia Wambura.

  Hata hivyo Wizara hiyo iko katika maandalizi ya Sera ya Lugha ambayo itabainisha majukumu ya Vyombo vya Habari katika matumizi na uendelezaji wa Lugha ya Kiswahili.

  0 0


  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017.
  Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017 wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017.


  0 0

  NA Beatrice Lyimo-MAELEZO.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Mahakama kukusanya Shilingi Trillioni 7.3 ambazo ni matokeo ya serikali kushinda kesi mbalimbali za ukwepaji kodi.

  Rais Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Sheria na Mwaka mpya wa Mahakama iliyobeba kauli Mbiu isemayo Utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.

  Alisema  kuwa Takwimu zinaonesha kuwa kumekuwa na baadhi ya kesi za pingamizi za kodi ambapo  Serikali imeshinda kesi hizo japo  fedha hizo hazijakusanywa mpaka sasa.“Kukwepa au kutolipa kodi ni kosa kubwa sana, kila mtu anawajibu wa kulipa kodi nchini kwa maendeleo ya nchi” nalifafanua Dkt Magufuli.

  Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa katika kuelekea ukuaji wa uchumi, Mahakama iwe sehemu ya chanzo cha pato la taifa kwa kwa kuhakikisha wale wanaotakiwa kulipa fidia baada ya kushindwa kesi wanafanya hivyo pamoja na kuwabana wakwepa kodi kwani kutimiza hilo kutaleta mabadiliko katika uchumi wa nchi.

  Katika hatua nyingine Rais Magufuli alisema kuwa Maendeleo ya nchi hayaangalii chama chochote, hivyo amevitaka vyombo vya utoaji haki kutoa haki kwa usawa.Kwa upande wake Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma alisema kuwa Mahakama imeandaa Mpango mkakati uliolenga kufanya maboresho ndani ya Mahakama.

  Alisema kuwa mpango mkakati huo umelenga masuala makuu matatu ikiwemo Utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali, upatikanaji wa haki na kwa wakati, uimarishaji wa amani kwa wananchi na ushirikishwaji wa wadau katika shughuli za mahakama.

  Aidha Kaimu Jaji Mkuu alisema kuwa Mahakama imefanikiwa kusikiliza mashauri ya kesi za uchaguzi kwa asilimia 100.“kati ya mashauri ya kesi 249 ikiwemo 53 za ubunge na 196 za madiwani ya waliopinga uchaguzi kati ya kesi hizo, kesi 52 za ubunge zilikamilishwa na kesi zote za madiwani zilikamilishwa” alifafanua Kaimu Jaji Mkuu.

  Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa Katiba imeanisha bayana Kanuni ambazo zinapaswa kuzingatiwa na Mahakama wakati ikitekeleza mamlaka yake ya utoaji haki.“utoaji haki mapema ipasavyo ni moja ya Kanuni ambazo Mahakama inapaswa kuzingatia katika utekelezaji wa majukumu yake kama inavyoelekezwa katika Katiba” alifafanua Mwanasheria Mkuu.


  Alisema kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kufanya biashara katika nchi ya Tanzania hivyo kuchochea maendeleo ya kiuchumi.Siku ya Sheria nchini ilioanzishwa mwaka 1996 ikiwa ni siku muhimu ya kuombea Majaji na Mahakimu ili kuweza kusikiliza kesi.

  0 0

  Wahe,Waandishi wa Habari,nimewaiteni hapa leo kwa ajili ya kuwapa Taarifa za hujuma zinazopangwa kufanywa dhidi ya chama chetu.

  Kama mnavyofahamu kwamba,Chama chetu kiko katika sintofahamu ya Mgogoro wa Kiuongozi.Hata hivyo pampja na hali hiyo kuwepo,tunaimani kwamba,sintofahamu hii ya Kiuongozi tutaumaliza wana CUF wenyewe.

  Mara nyingi huwa siyo kawaida yangu kusimama hadharani kuzungumzia hali ya chama kupitia Vyombo vyenu vya habari,lakini kwa hali ilivyo nimewajibika kutokeza hadharani kuzungumza nanyi.

  Kwa mujibu wa Katiba ya CUF Ibara ya 88 (2) Nanukuu.Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama atakuwa na wajibu Ufuatao,Mwisho wa kunukuu.Ibara ya 88 (2) (a) Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Chama Ibara ya 87 (1)Wajibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Taifa ni kuhakikisha Usalama wa Chama Nchini kote

  Nimeona ninukuu vifungu hivi vya Katiba ya CUF ili kuweka sawa uhalali wangu katika kutoa Taarifa hii kwenu ninyi Waandishi wa Habari.Tunazo Taarifa kwamba,Katibu Mkuu wetu anafanya Vikao mbalimbali na Viongozi wa Chadema vyenye muelekeo wa kuhujumu harakati za chama chetu pamoja na baadhi ya Viongozi wa CUF upande wa Tanzania Bara.

  Napenda kuchukua fursa hii kumsihi Katibu Mkuu wa Chama changu,Mhe,Maalim Seif,kwamba aache kufanya hivyo kwani vikao hivyo havina tija kwake ziadi ya kujenga Uhasama dhidi ya Wanachama na Viongozi wa CUF wa Bara na Zanzibar.

  Nimshauri Katibu Mkuu wangu kwamba,Viongozi wa Chadema anaowatumainia kama ndiyo wataweza kumsaidia katika dhamira zake,atakuwa anapoteza muda wake bure.Tunazo Taarifa kwamba kuna Vijana wanaandaliwa kuja kuvamia Ofisi Kuu za CUF Buguruni kwa ajili ya kufanya Uharibifu wa Mali za Chama.

  Nichukue fursa hii pia kutoa ONYO KALI kwamba Vijana hao wasithubutu wala kujaribu kufanya kitu kama hicho kwani Ulinzi wa Chama umejipanga vyema kukabiliana vikali na Kikundi chochote ambacho kina dhamira ya kufanya hujuma yeyote dhidi ya chama chetu cha CUF.

  Kuhusu kuwafanyia hujuma baadhi ya Viongozi wa Chama chetu,tunawaambia kwamba,wote wanaotaka kufanya Vitendo hivyo tunawajua mmoja mmoja na anapoishi,ila kwa sababu maalum,sitoweza kuwataja kwa sasa,lakini kwa kuwa,chama chetu kinafanya kazi kwa mujibu wa sheria za Nchi,Tayari tumevitaarifu Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Serikali juu ya Vitisho ya vitendo dhalimu vinavyokusudiwa kufanywa na Wasaliti wa Chama chetu dhidi ya Viongozi wetu wa Chama upande wa Tanzania Bara.

  Lakini pia napenda kuchukua fursa hii kutoa Onyo pia kwa wale wanaojiita ni Viongozi wa CUF halafu wanazungumzia Uchochoroni na kuwatukana Viongozi halali wa Chama cha CUF,kwamba waache mara moja,tumewavumilia sana kiasi cha kutosha sasa dawa yao iko jikoni mmoja mmoja baada ya mwingine tutawajibika nao.

  Waheshimiwa Wanahabari nawashukuru,asanteni sana kwa kunisikiliza.

  HAKI SAWA KWA WOTE

  Masoud Omar Mhina

  MKURUGENZI WA ULINZI NA USALAMA CUF TAIFA.
  Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Wananchi (CUF), Masoud Mhina, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu madai ya hujuma zinazopangwa kufanywa dhidi ya chama hicho. Kushoto ni Ofisa Dawati wa CUF, Awadhi Mdoe.
  Ofisa Dawati wa CUF, Awadhi Mdoe, akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Naibu Kamanda wa Blue Gurd, Wilaya ya Kinondoni, Mohamed Kiotola, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Zainabu Mdolwa, Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Wananchi (CUF), Masoud Mhina na Mkurugenzi wa Blue Gurd wa Wilaya ya Temeke, Saidi Mtumbwe.
  Wafuasi wa chama hicho wakiwa kwenye mkutano huo.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza mwananchi, Bi. Sobha Mohamed, aliyejitokeza kueleza kero ya masuala ya mirathi anazozipata katika mahakama mbele yake wakati wa sherehe za Kuzinduz Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama Mtaa wa Chimala Ocean road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017.

  Jaji Kiongozi Mhe Ferdinand Wambali akichukua melezo ya mwananchi, Bi. Sobha Mohamed, aliyejitokeza kueleza kero ya masuala ya mirathi anazozipata katika mahakama mbele yake wakati wa sherehe za Kuzinduz Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama Mtaa wa Chimala Ocean road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017. PICHA NA IKULU

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamiii

  Katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati wa maadhimisho ya mwaka mpya wa kimahakama, Bi Sobha Mohamedi ameibua taflani  na kugeuka shujaa mara baada ya kufanikiwa kuelezea tuhuma zake kwa namna alivyodhurumiwa haki zake katika mahakama ya mwanzo mkoani Tanga.

  Sobha ambaye alifanikiwa kupenya katikati ya watu na kusogea mbele akiwa na bango ambalo lilikuwa likieleza jinsi alivyodhulumiwa kisha kuzuiwa na walinzi wa Rais lakini Rais Dk John Pombe Magufuli akaamuru asogee mbele asikilizwe.

  Mama huyo mara baada ya kufika mbele ya Rais aliweza kueleza kila kitu na mwenendo wa jinsi kesi yake ilivyokwenda na hatimae kupewa hukumu ambayo ilikuwa ya pande mbili ambayo haitoi haki ya moja kwa moja ya  kuendelea kuwa mmiliki wa mirathi aliyofungua.

  Mara baada ya kujieleza hivyo Rais Magufuli aliagiza mamlaka zote kuhakikisha kuwa mahakama na mamlaka zinazo husika kushughulikia kesi hiyo kuhakikisha kuwa haki inatendeka .


  Dk Magufuli ameagiza jeshi la Polisi kumpatia mama huyo ulinzi ili aweze kuishi kwa amani bila kubugudhiwa na mtu yeyote,huku akiendelea kutunza ushahidi wa kesi hiyo. 

  0 0


   Waya wa umeme uliokatika ukiwa unaanza kufuka moshi baada ya kukatika mtaa wa Mchikichi na Msimbazi, jijini Dar es salaam.
   Gari la Zimamoto likiwa eneo la tukio mtaa wa Mchikichi na Msimbazi baada ya waya wa umeme kukatika na kuanza kutoa moshi na hatimaye moto.    Kikosi cha Zimamoto kikiwa eneo la tukio mtaa wa Mchikichi na Msimbazi baada ya waya wa umeme kukatika na kuanza kutoa moshi na hatimaye moto.

   Askari wa zimamoto wakiwa wanajaribu kuuzima moto huo kabla ya shirika la umeme la Tanesco hawajafika.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akizungumza na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji nchini kabla ya Balozi huyo kuzindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja ulioandaliwa na Idara hiyo ambao unalenga kuboresha zaidi huduma zitolewazo na Uhamiaji ambapo kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana kwa siku tano za kazi mara baada ya mteja kuiomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi. Uzinduzi huo umefanyika Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto (upande wa pili) ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli.

  Na Humphrey Shao, Globu ya jamii.

  Idara ya uhamiaji imezindua mkataba wa huduma kwa wateja ambao utawawezesha kutoa hati ya kusafiria ndani ya siku tano bila kuchelewa.

  Akizungumza na wahabari katika makao makuu ya idara ya uhamiaji jijini Dar es Salaam,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya amesema kuwa kama watumishi wa idara hiyo watashindwa kukidhi vigezo hivyo walivyojiwekea wananchi wana haki ya kulalamika na kutoa taarifa katika ngazi za juu.

  “Tumejiwekea viwango kuwa wakati wote mtu kama ataomba pasipoti apewe ndani ya sikutano mkataba huo umeonyesha wajibu wa mtoaji huduma  kumuhudumia mteja vile inavyotakikana” amesema Balozi Yahya.

  Ameongeza kuwa kuanzia sasa mteja ni mfalme pindi anapofika katika idara hiyo kuhitaji hati ya kusafiria na sasa ana fursa ya kulalamika pindi huduma atakayopata kuwa aitakuwa na radha.Amemaliza kusema kuwa kuwa kuanzia sasa watu wote watapewa huduma kwa heshima na taadhima kutoka idara ya uhamiaji.
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa Idara ya Uhamiaji. Mkataba huo ambao unalenga kuimarisha huduma mbalimbali za Idara hiyo pia umeelekeza kuanzia sasa Hati za Kusafiria (Pasipoti) zitatolewa kwa siku tano za kazi kwa watakaoomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli. Uzinduzi huo umefanyika Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akionesha machapisho ya mkataba wa huduma kwa wateja kati ya Idara ya Uhamiaji na wananchi.
  Baadhi ya wananchi waliofika katika halfa ya uzinduzi wa mkataba huo.
  . Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya katikati akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa idara ya uhamiaji.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akisalimiana na watendaji wa uhamiaji.

  0 0

  Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rogers Kibula akimuelezea maendeleo ya wagonjwa wa Moyo waliolazwa katika wodi namba tatu Mohammed Barhoumi ambaye ni Makamu Rais wa Kampuni ya Medtronic kutoka nchini Lebanon ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo alipotembea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea jambo na Mohammed Barhoumi ambaye ni Makamu Rais wa Kampuni ya Medtronic kutoka nchini Lebanon ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo alipotembea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimuonyesha jengo la Maabara Kuu ya Taifa (halipo pichani) Mohammed Barhoumi ambaye ni Makamu Rais wa Kampuni ya Medtronic kutoka nchini Lebanon ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya moyo. Kushoto ni Divin Akaba na kulia ni Stranix William wote kutoka Medtronic.
  Daktari Bingwa ya upasuaji wa magonjwa ya Moyo kwa watoto Godwin Sharau akimueleza jinsi wanavyofanya upasuaji wa moyo kwa watoto Mohammed Barhoumi ambaye ni Makamu Rais wa Kampuni ya Medtronic kutoka nchini Lebanon ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya moyo. Kulia ni Daktari wa Upasuaji wa Mgonjwa ya Moyo Hussein Hassanali.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiagana na Mohammed Barhoumi ambaye ni Makamu Rais wa Kampuni ya Medtronic kutoka nchini Lebanon ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya moyo mara baada ya kumaliza kutembelea Taasisi hiyo leo na kujionea kazi mbalimbali wanazozifanya. 


  Picha na Anna Nkinda – JKCI

  0 0

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

  Nchi za Afrika Mashariki zimekubaliana kuwa Makao Makuu ya Lugha ya Kiswahili kuwa Tanzania ambayo yatakuwepo Zanzibar.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya jitihada mbalimbali ambazo Tanzania inazichukua katika kukuza Lugha ya Kiswahili katika ngazi ya Kimataifa.

  Nape amesema kuwa maamuzi hayo ya kuifanya Tanzania kuwa Makao Makuu ya Lugha ya Kiswahili yametokana na Tanzania kuzalisha walimu wengi wa Kiswahili ambao wanatumika katika ngazi mbalimbali za elimu ndani na nje ya nchi.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Anastazia Wambura amesema kuwa Wizara hiyo kwa sasa inachukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinakuwa mawakala wa kulinda Lugha ya Kiswahili ambapo Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa kushirikiana na wadau wa Kiswahili limeendelea kuendesha semina, warsha, makongamano na kutoa elimu inayohusu matumizi fasaha ya Lugha ya Kiswahili.

  Aidha, aliendelea kwa kusema kuwa Waandishi wa Habari wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha Lugha hiyo inaendelezwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuzingatia matumizi sahihi ya Lugha hiyo katika majukumu yao ya kila siku.

  “Kutumia zana kama vile Kamusi na vitabu vya miongozo ya uandishi pamoja na kuhudhuria makongamano ya Kitaifa na ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili inasaidia kuongeza ujuzi na uweledi wa Lugha ya Kiswahili, kujua istilahi za kisayansi na kiteknolojia na hivyo kuandika na kutangaza kazi bora na zenye maudhui lengwa kwa jamii na kuepuka upotoshaji wa maneno ya Kiswahili usio wa lazima,” alifafanua Anastazia Wambura.

  Hata hivyo Wizara hiyo iko katika maandalizi ya Sera ya Lugha ambayo itabainisha majukumu ya Vyombo vya Habari katika matumizi na uendelezaji wa Lugha ya Kiswahili.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea katika uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa dhamana ya Hifadhi ya Mazingira. Bodi hiyo iko chini ya Uenyekiti wa Bw Ali A. Mafuruki. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwakaribisha wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa dhamana ya Hifadhi ya Mazingira (hawapo pichani), kulia ni Bw. Ali Mufuruki Mwenyekiti wa Bodi.
  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava (kushoto) akiwa na Bw. Ali Mufuruki Mwenyekiti wa Bodi, wakati wa halfa ya uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa dhamana ya Hifadhi ya Maizngira jiini Dar es Salaam.
  Sehemu ya Wajumbe wa Bodi (mstari wa mbele) wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika hafla ya uzinduzi wa Bodi na Mfuko wa Dhamana ya Mazingira.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa dhamana ya Hifadhi ya Mazingira, mara baada ya kuizindua hii leo, Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais, Dkt. John Magufuli hajawahi kutangaza ama kutoa kauli ya kufutwa kwa vyama vya siasa nchini.

  Ametoa kauli hiyo leo (Februari, 2, 2017) Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Mbowe  katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu.

  Katika swali lake Mheshimiwa Mbowe alisema Rais Dkt.  Magufuli alinukuliwa akisema atahakikisha anafuta vyama vyama vya upinzani na ifikapo mwaka 2020 hakuna upinzani nchini.

  Pia Mheshimiwa Mbowe alitaka kujua nini kauli ya Serikali kuhusu kunyimwa dhamana kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema ambaye anashikiliwa kwa muda miezi mitatu.

  Mbali na Mheshimiwa Lema, pia kiongozi huyo alitaka kujua kuhusiana na kufungwa kwa Mbunge wa Kilombelo, Mheshimiwa Peter Lijualikali pamoja na madiwani sita wa chama hicho ambao wamefungwa na viongozi wengine 215 wanakabiliwa na kesi mbalimbali.

  “Kwanza nataka nikanushe kwamba Mheshimiwa Rais hajawahi kutangaza kuvifuta vyama vya upinzani. Pia Watanzania wote wanajua nchi hii inaongozwa kwa sheria, kanuni na taratibu i,” amesema Waziri Mkuu.

  Waziri Mkuu ameongeza kuwa “tunajua katika kuendesha nchi tunaendesha kwa mihimili mitatu ipo Serikali, Mahakama na Bunge na hakuna mhimili unaoweza kuuingilia mhimili mwingine,”.

  “Pia Watanzania wote wanajua kwamba jambo lolote ambalo lipo Mahakamani haliwezi kuzungumzwa mahali pengine popote, hivyo siwezi kutumia nafasi hii kuzungumzia mambo yote yanayoendelea chini ya sheria na yaliyo mahakamani,” amesema.
  Wakati huo huo; Waziri Mkuu amewahakikishia Watanzania kwamba suala la upungufu wa sukari halitatokea nchini kwa sababu viwanda vya ndani vinaendelea kuzalisha na hadi mwishoni mwa Januari vilifikia asilimia 86 ya uzalishaji.

  “Hadi kufikia mwishoni mwa msimu wa uzalishaji ambao ni mwezi Machi, tunaweza kuwa tumefikia malengo na kama itajitokeza upungufu Serikali itatafuta namna nzuri ya kupata sukari kwa kushirikiana na wenye viwanda nchini,” amesema.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mvomero, Mheshimiwa Suleiman Sadiq aliyetaka kujua hali ya sukari ilivyo nchini kwa sasa na hatua gani zinazochukuliwa na Serikali ili kunusuru hali ya uhaba wa sukari isijitokeze.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  S. L. P. 980,
  DODOMA.

  ALHAMIS, FEBRUARI 02, 2017

older | 1 | .... | 1544 | 1545 | (Page 1546) | 1547 | 1548 | .... | 3283 | newer