Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1543 | 1544 | (Page 1545) | 1546 | 1547 | .... | 3286 | newer

  0 0


  geni rasmi wa ufunguzi wa Mkutano wa uhamasishaji wa Afya na lishe kwa vijana (hasa kwa wasichana),Mkurugenzi wa Kinga,Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na watoto Dkt.Neema Rusibamayila akisoma hotuba wakati wa mkuitano huo ambao wa siku tatu unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere
  Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Dkt.Joyce Kaganda akizungumza kwenye mkutano huo
  Baadhi wa washiriki wa mkutano huo wakifuatilia uwasilishaji wa mada.Mkutano huo wa Kimataifa unawashirikisha viongozi wa juu wa serikali, mashirika na taasisi binafsi pamoja na wadau wa maendeleo nchini na nje ya nchi
  Picha ya pamoja ya washiriki wa Mkutano huo ambao unalengo la kutunza afya ya vijana hususani wasichana kwani ni wazazi wa baadae kutoka wanapozaliwa hadi makuzi yao .Nchi zinazoshiriki mkutano huo ni pamoja na Tanzania,Ethiopia,Senegal na Kenya(Picha zote na Rayson Mwaisemba-Wizara ya Afya)

  0 0


   

   Na: Lilian Lundo – MAELEZO - Dodoma

  Vyuo Vikuu hapa Nchini vimeagizwa kuacha mara moja kutoza ada kwa fedha za kigeni kwa wanafunzi ambao ni watanzania.

  Agizo hilo limetolewa leo Bungeni, Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge Jaku Hashimu Ayoub kwamba kumekuwa na malalamiko ya wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania ambao ni wazawa kulipishwa ada ya masomo yao kwa fedha za kigeni badala ya fedha za Kitanzania.

  “Sarafu inayotakiwa kutumika Tanzania ni shilingi ya Kitanzania kwa mujibu wa kifungu cha 25 na 26 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ya mwaka 2006. Aidha, kwa Tanzania malipo ya kitu au huduma yoyote inapaswa kulipwa kwa shilingi ya Kitanzania kama ilivyoainishwa kwenye kifungu cha 28 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania, 2006,” alifafanua Mhandisi Manyanya.

  Aliendelea kwa kusema kuwa japo Wizara haijapokea malalamiko yoyote ya kutozwa fedha za kigeni kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu tangu itoe agizo kama hilo kwa wamiliki wa vyuo Septemba 07, 2016.

  Hivyo basi kwa mara nyingine Mhandisi Manyanya ameviagiza vyuo ambavyo bado vinatoza wanafunzi Watanzania fedha za kigeni kuacha mara moja kwani vyuo hivyo vimeelekezwa kutoza wananchi wa Kitanzania kwa pesa ya Kitanzania.

  Aidha Mhandisi Manyanya amewataka watanzania kutoa taarifa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiwa kuna Chuo chochote kinachotoza ada kwa Watanzania kwa fedha za Kigeni ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.

  0 0

  Na. Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

  Serikali itaendelea kutoruhusu uvuvi kufanyika ndani ya Pori la Akiba la Selous kutokana na ukiukwaji wa taratibu zilizokuwa zimewekwa wa kuingia ndani ya hifadhi hiyo.

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Rufiji Mohamed Mchengerwa juu ya hatua ambazo Serikali inazichukua kutoa ridhaa kwa wananchi waishio maeneo ya hifadhi kupata ruhusa kisheria kuweza kuvua samaki.

  “Mwaka 1994, wananchi wa Kata ya Mwaseni, Mloka, Ngoroka na Kipungila Wilaya ya Rufiji waliruhusiwa kuingia ndani ya Pori la Akiba Selous na kuvua Samaki. Hata hivyo, baadhi ya wanavijiji walikiuka taratibu zilizokuwa zimewekwa kwa kuingia ndani ya hifadhi bila kujiandikisha na kuvua samaki kinyume cha sheria,” alifafanua Mhandisi Makani.

  Aliendelea kwa kusema kuwa baadhi ya wavuvi walibainika kujihusisha na vitendo vya ujangili wa wanyamapori, uvuvi haramu wa kutumia sumu, ukataji miti ovyo kwa ajili ya kukausha samaki na kutengeneza mitumbwi pamoja na uharibifu wa mazingira uliotokana na uchomaji wa moto ovyo kinyume cha sheria.

  Mhandisi Makani amesema kuwa kwa kuzingatia hali ya usalama katika maeneo ya uhifadhi wa wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kutoruhusu uvuvi kufanyika ndani ya Pori la Akiba Selous.

  Aidha Wizara inawashauri wananchi wa Kata za Mwaseni, Mloka na nyinginezo zilizo jirani kutumia mabwawa mengine yaliyoko nje ya Pori hilo yenye fursa kubwa kwa kufanya shughuli za uvuvi.

  Mabwawa ambayo wananchi wameshauriwa kuyatumia ni Bwawa la Zumbi lililoko vijiji vya Nyaminywili, Kipugira na Kipo, Bwawa la Ruwe lililopo Mkongo, Lugongo lililopo kijiji cha Mtanza na Bwawa la Zimbwini lililopo Mji wa Kibiti.

  Mabwawa hayo ya Mto Rufiji yatatoa fursa ya shughuli za uvuvi hivyo kusaidia kuinua kipato cha wananchi.

  Vile vile Mhandisi Makani amesema kuwa, Wizara hiyo kwa kutambua mahitaji ya wananchi katika maeneo hayo ya kufanyia kazi na kujiletea maendeleo kiuchumi na kijamii. Wizara hiyo inaendelea kushauriana na Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kuhusu namna ya kutekeleza mpango wa kuwajengea mabwawa ya samaki ili pamoja na mabwawa ya asili yaliyopo yawawezeshe kufanya shughuli za uvuvi endelevu.

  0 0
 • 02/01/17--07:31: Article 7 • 0 0

  NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo amewataka wanafunzi na walimu wa shule ya msingi ya Chang’ombe kutunza na kuitumia miundombinu iliyojengwa ili kuongeza ufaulu katika shule hiyo.

  Jafo ametoa kauli hiyo leo alipotembelea shule hiyo ili kukagua utekelezaji wa agizo alilolitoa juu ya kukamilisha ukarabati wa miundombinu katika shule hiyo ifikapo 10 januari, mwaka huu.

  Novemba 3, mwaka jana Jafo alitoa agizo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa matundu 20 ya vyoo na vyumba vya madarasa 8 pamoja na ukarabati wa vyumba vya madarasa 2 katika shule ya Chan’gombe A ifikapo januari, 10 mwaka huu kabla ya msimu wa masomo kuanza.

  Katika ziara hiyo, Jafo amesema ameridhishwa kwa hatua nzuri ya ukarabati huo na kupongeza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa , kamati ya shule ya Chang’ombe ,walimu na Diwani wa Kata ya Chang’ombe kwa utekelezaji huo.

  Amesema shule hiyo inapaswa kuongeza ufaulu wake ili iwe mfano mzuri wa kuigwa kwa shule nyingine .Amesema awali alitoa agizo hilo baada ya kubaini changamoto mbalimbali katika shule ya msingi ya Chang’ombe A .

  ‘’Maagizo niliyoyatoa yalikuwa magumu sana lakini nia yangu ilikuwa kuwatengenezea mazingira rafiki wanafunzi na walimu , nimefarijika na utekelezaji wake, hali haikua nzuri hapo mwanzo lakini nimefarijika kwa kazi nzuri, muonekano wa madarasa unaridhisha nawapongeza sana’’ amesema Naibu Waziri huyo

  Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Nelly Kinyaga ameishukuru serikali kwa kuboresha miundombinu ya shule hiyo ambapo awali mazingira ya shule hiyo yalikuwa sio rafiki kwa wanafunzi na walimu kutokana na upungufu wa matundu 20 ya vyoo na vyumba vya madarasa 8.

  ‘’Kwakweli kulikuwa na changamoto sana wanafunzi walikua wengi na madarasa machache lakini kwasasa hatuna watoto wanaokaa chini na msongamano wa wanafunzi darasani umepungua kwa kiasi kikubwa ,naishukuru serikali na Jafo kwa kutilia mkazo ukarabati wa miundombinu ya shule yetu’’ amesema

  Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, Ally Mohamed Swalehe ameishukuru serikali kwa kuboresha miundombinu ya shule hiyo rafiki kwa kuwa itaongeza ufaulu katika mitihani na kuepusha magonjwa ya milipuko shuleni hapo.


  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Seleman S.Jafo akizungumza na walimu, wanafunzi na Kamati ya shule ya msingi Chang’ombe A Manispaa ya Dodoma alipofanya ziara kujionea maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ambao umekamilka kwa asilimia mia moja. Kulia kwake ni Kaimu Afisa Elimu Mkoa Dodoma Bw. Tumsifu Mwasamale na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi. Nelly kinyaga kushoto kwake ni Diwani Kata ya Chang’ombe Mhe.Bakari Samweli Fundikira 
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Seleman S.Jafo akifungua mlango ili kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa ambao umekamilika kwa asilimia mia moja.Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Seleman S. Jafo akitoa agizo kwa halmashauri, kamati za shule na mikoa nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kutumia juhudi na maarifa ili kuwaletea wananchi maendeleo kwa haraka. Ameridhishwa na ubora na kasi waliyoitumia kujenga majengo hayo.

  Mojawapo ya madarasa yaliyokamilika katika shule ya msingi Chang’ombe A Manispaa ya Dodoma. Jumla ya vyumba vya madarasa sita vimejengwa ili kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa katika shule hiyo inayotokana na wingi wa wanafunzi, shule hiyo ina zaidi ya wanafunzi 2000

  0 0

  Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa mikopo kwa vijana na malipo ya ada kwa fedha za kigeni. Ufafanuzi huo umetolewa mjini hapa leo wakati wa kikao cha pili katika Mkutano wa Sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Kuwainua Vijana Kiuchumi

  Akijibu hoja kuhusu namna vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini wanavyoweza kufaidika kiuchumi, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Anthony Mavunde, amesema Serikali imetenga fedha za kutosha kupitia mifuko mbalimbali kuwawezesha vijana kwa mitaji na mafunzo ya ujasiriamali ili kuwainua kiuchumi.

  Ameongeza kuwa vijana wenyewe ndio wanaopaswa kuchangamkia fursa hizo na pale wanapojiunga katika vikundi mbalimbali wamekuwa wakipewa mikopo kwa ajili ya mitaji. Alitoa mfano wa jinsi Serikali ilivyowawezesha vijana waliojiunga na kuwekeza katika viwanda vidogo vya maziwa na chaki mkoani Simiyu.

  Amewataka pia Wabunge na Halmashauri zote nchini kuendelea kupigania kutengwa maeneo maalum katika sekta mbalimbali kwa ajili ya kuwapatia vijana na kutengwa kwa asilimia 5 ya mapato ya Halmashauri kwa maendeleo ya vijana

  Ada kwa Fedha za Kigeni

  Serikali imesema, ingawa haijapokea malalamiko yoyote kuhusu wananchi wasioridhihwa na mtindo wa kutakiwa kulipa malipo ya ada kwa fedha za kigeni katika baadhi ya shule na vyuo, lakini imesisitiza kuwa wale wanaotoza ada kwa fedha za kigeni wanakiuka Sheria.

  Akitoa ufafanuzi huo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya amesema kwa mujibu wa kifungu cha 28 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT), 2006, fedha inayopaswa kutumika kwa malipo ya huduma nchini ni Shilingi ya Tanzania. Ameviagiza vyuo na shule nchini kuacha kutoza ada kwa fedha za kigeni na kuhimiza wananchi watakaobainika kufanya hivyo kutoa taarifa Serikalini.

  Si Tatizo Kutumia Majengo UDOM

  Serikali imesisitiza kuwa baadhi ya Wizara zilizoanza kutekeleza agizo la kuhamia Dodoma kutumia baadhi ya majengo kwa muda kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) hakutaathiri shughuli za chuo.

  Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama. Waziri Jenista amesisitiza kuwa baadhi ya Wizara zitatumia majengo ya UDOM kwa sababu mengi ya majengo hayo yalikuwa hayatumiki kwa sasa kwa shughuli za chuo hicho na hakutakuwa na muingiliano na shughuli za chuo.

  Mradi wa Mabilioni Maji Dar

  Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Dar es Salaam imeanza kutekeleza mradi wa usambazaji wa maji utakaogharimu Dola za Marekani milioni 32.772 ambazo ni mkopo kutoka Benki ya Exim ya China. Mradi huo utahusisha sehemu yote ya jimbo la Kawe, Dar es Salaam. Mradi huo utachukua miezi 15.

  Imetolewa na:

  Idara ya Habari-MAELEZO.

  0 0  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee John Malecela wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Kilimani mjini Dodoma leo Februari 1, 2017.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee John Malecela wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Kilimani mjini Dodoma Februari 1, 2017. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee John Malecela wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Kilimani mjini Dodoma leo Februari 1, 2017. Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu.

  0 0

  Na Mwandishi wetu

  Taasisi ya Global Peace Foundation (GPF) Tanzania, imemteua mshindi wa Big Brother Africa Hotshots 2014) Idris Sultan, kuwa balozi wa amani kwa vijana duniani.

  Mkurugenzi Mkazi wa GPF Tanzania, Martha Nghambi alisema kuwa wameamua kumtumia Idris kutokana na mvuto wake kwa vijana na kutokana na hilo atafikisha ujumbe kirahisi kwa vijana ambao ni zaidi ya asilimia 60 ya idadi ya watu Tanzania.

  Alisema kuwa bado kuna changanoto nyingi za kudumisha amani duniani kwani mpaka sasa kuna baadhi ya nchi zipo katika matatizo makubwa yaliyosababishwa na uvunjifu wa amani.

  Martha alisema kuwa Idris ni mtu sahihi katika kampeni yao na wanaamini kuwa kupitia yeye vijana na watu wengine watapata ujumbe wa kuhamaisha kudumisha amani duniani.

   “Kuna baadhi ya nchi zina matatizo ya amani, waswahili wanasema, ukiona kwa mwenzako kunawaka moto… kwako andaa maji, sisi tumeamua kuchukua tahadhari mapema ili kulinda amani yetu,”

  Kwa upande wake, Idris alifurahi sana kupewa nafasi hiyo ambayo ni kubwa sana katika maisha yake.

  “Wamenithamini na kuniona ninafaa katika kampeni hii, ni kweli, amani inatakiwa kuanzia kwenye familia mpaka juu ambako wengi wanadhani vita tu ndiyo inatakiwa kupigiwa kelele,  vijana ndiyo nguvu kazi ya ya taifa na hivyo tunatakiwa kuwa na mawazo yaliyopanuka ili kujipatia vipato na kuachana na lawama kutokana na kukosa soko la ajira,” alisema Idris.

  Alifafanua kuwa kuwa balozi ni jukumu zito na atalitumikia ipasayo ili kufikia malengo yaliyowekwa. “Amani ni  kazi ya kila siku na ni muhimu, leo hii wasanii wanaigiza na wanamuziki wanafanya kazi zao bila kuwa na woga, hii yote inatokana na amani,” alisema.

  Global Peace Foundation ni shirika lisilo la kiserikali na lisilo tengeneza faida lenye makao yake makuu, mjini Washington DC, Marekani. Shughuli kubwa la shirika hili ni kuhamasisha amani duniani kupitia matawi yake mbalimbali duniani.

  Mbali ya Tanzania, matawi mengine katika bara la Afrika ni Kenya, Uganda na Nigeria. Kauli mbiu ya shirika hilo ni “We are all  “One family under God”(sisi wote ni familia moja kwa Mungu).

  Kwa sasa Global Peace Tanzania inaendesha kampeni ya kuhamsisha amani kuanzia ngazi ya familia ijulikanyo kama “Vijana na Amani”. Kupitia kampeni hii, GPF Tanzania inahamasisha amani kwa kutoa elimu katika shule, vyuo na jamii kwa ujumla.


   Mshindi wa Big Brother Africa Hotshots 2014) Idris Sultan (kulia), akipokea cheti cha utambulisho  wa kuwa balozi wa Amani kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi Taasisi ya Global Peace Foundation (GPF) Martha Nghambi.
  Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Global Peace Foundation (GPF) Tanzania, Martha Nghambi (wa pili kushoto) na mshindi wa Big Brother Africa Hotshots 2014) Idris Sultan (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa kuwa balozi wa amani kwa vijana Tanzania

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan va viongozi wengine mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akishuka kwenye ndege katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017. Mbele yake ni Mkuu wa Itifaki Balozi Grace Martin.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilsalimiana na baadhi ya wafayanyazi katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam alipowasili akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wananchi mikono alipowasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Inspecta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017.

  0 0
  0 0


  0 0

   Timu ya Taifa ya Misri imetinga hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya kufanikiwa kuitoa timu ya Burkina Faso kwa mikwaju ya penati 4-3 kufuatia kumalizika kwa dakika 120 za mchezo huo kumalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana goli 1-1. 

  Mchezo huo uliomalizika hivi punde, ulikuwa ni wenye mvuto wa aina yake huku timu zote zikioneshana uwezo wa kushambuliana kwa zamu. Misri ndio walioanza kuliona lango la wapinzani wao mnamo dakika ya 66 kupitia kwa Mshambuliaji wake, Mohamed Salah na dakika saba baadae Burkina Faso walisawazisha goli kupitia kwa Aristide Bance.
  Misri sasa itamsubiria mshindi wa mechi ya nusu fainali ya pili itakayopigwa hapo kesho kwa kuwakutanisha miamba wawili ambao ni Cameroon na Ghana.

  0 0


  0 0


  0 0

  Tshisekedi alikuwa kiongozi maarufu wa upinzani kwa miongo kadhaa
  Image captionTshisekedi alikuwa kiongozi maarufu wa upinzani kwa miongo kadhaa
  Kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Etienne Tshisekedi, amefariki dunia mjini Brussels nchini Ubelgiji akiwa na umri wa miaka 84.
  Tshisekedi alikwenda mjini Brussels mwishoni mwa mwezi jana kwa ajili ya matibabu.Bwana Tshisekedi alikuwa mmoja wa wanasiasa wakongwe waliokuwa mstari wa mbele kupigania demokrasia ya nchi yake.
  Tshisekedi alikuwa na mvuto mkubwa kwa wananchi wa DRC
  Image captionTshisekedi alikuwa na mvuto mkubwa kwa wananchi wa DRC
  Alisimama kidete katika utawala wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Rais Mobutu Sese Seko, ambae utawala wake ulidumu kwa miongo kadhaa kabla ya kupinduliwa. 
  Etienne Tshisekedi pia alikuwa mpinzani wa Rais Laurent Kabila, ambae aliingia madarakani mnamo mwaka 1997, na mwanae, Rais Joseph Kabila, ambae hivi sasa ndio anatawala nchi hiyo.
  Chanzo: BBC

  0 0

  Mahakama kuu ya Tanzania imesema itafanya mpango wa kuongeza kasi ya utoaji wa haki kwa watu wote ikiwemo kupunguza  kesi za zamani katika ngazi zote za mahakama nchini.
  Hayo yamesemwa  jijini Dar es salaam na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma katika kilele cha maonyesho ya wiki ya sheria, akisisitiza watongeza vitendea kazi na watumishi wa mahakama ili kuwepo na urahisi katika mfumo wa kusikiliza kesi na kuzitolea hukumu.
  Akizungumzia baadhi ya malalamiko yaliyotolewa na mmoja wa wananchi Profesa Juma amesema kuwa wamepokea malalamiko juu ya mahakama moja ambayo hakuitaja jina lake ambayo watumishi wake wamekuwa wakitoa lugha chafu,uzembe,kuchelewesha haki,kutumika kama vishoka sambamba na kuongea lugha za jazba hali ambayo ilimkwaza mwananchi huyo.
  ‘’Natoa rai kwa mahakama kuhakikisha wanatoa takwimu nawakumbusha kwamba kuna waraka wa Jaji Mkuu wa mwaka 2013  ambao aliwataka Majaji wafawidhi,Majaji wafawidhi na watendaji kuona kila baada ya miezi mitatu kuanzia Julai 2013 kuwasilisha mashauri ya  muda mrefu’’.amesema Profesa Juma.
   Pia ametoa rai kwa wadau wote kuendeleza yale mazuri yaliyojitokeza katika wiki ya huduma za kisheria katika viwanja vya mnazi mmoja ikiwemo kusikiliza kero za kisheria zinazowakabili wananchi hata watakapofika katika ofisi zao.
   Kaimu Jaji  Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma akizungumza katika ufungaji wa maonesho ya wiki ya sheria katika viwanja vya Mnazi  mmoja jana jijini  Dar es Salaam.
   Kaimu Jaji  Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma akimkabidhi laptop Hakimu  Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Kimara, Mhe. Asia Mjemah kwa ajili ya uchapishaji nakala za hukumu jana  jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya viongozi mbalimbali na wananchi wakimsikiliza Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma katika ufungaji wa maonesho ya wiki ya sheria katika viwanja vya Mnazi  mmoja jana jiji Dar es Salaam

  Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa,Ibrahimu Juma akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mblimblia katika viwanja vya Mnazi  mmoja leo jiji Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  0 0
  0 0


  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango, mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akifafanua baadhi ya vipengele vya Muswada wa marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, kuhusu marekebisho ya Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana. Muswada huo ulipitishwa kuwa Sheria na Bunge Februari Mosi, 2017.
   Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. George Masaju, akihitimisha mjadala wa Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, uliopitishwa na wabunge kuwa Sheria Februari Mosi, 2017, Mjini Dodoma
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Naibu Waziri wake, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakipitia nyaraka za Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, Bungeni Mjini Dodoma, Muswada ambao tayari Bunge limeupitisha kwa kishindo kuwa Sheria Februari Mosi, Mjini Dodoma.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimweleza jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Dkt. Medard Kalemani (Mb), nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma, baada ya Bunge kupitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, Februari Mosi, 2017.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM).


older | 1 | .... | 1543 | 1544 | (Page 1545) | 1546 | 1547 | .... | 3286 | newer