Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1542 | 1543 | (Page 1544) | 1545 | 1546 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) David Kanyatta akiwasilisha mada kwa Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi kunavyoathiri sekta ya utalii katika semina iliyofanyika jana mjini Dodoma .
  Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Yussuf Hussein, akichangia hoja mara baada ya mada kuweza kuwasilishwa na wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu utalii wa baharini ambao umekuwa haupewi kipaumbele katika kutangazwa pamoja na kuendelezwa katika semina hiyo.
  Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Marwa Chacha, (katikati) akichangia hoja mara baada ya mada kuweza kuwasilishwa na wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu wanyamapori waharibifu wa mazao kama vile tembo wanavyoathiri maisha ya wapiga kura wake kwenye vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti katika semina iliyofanyika jana mjini Dodoma. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo .
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Atashasta Nditiye, (katikati) Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ( kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani ( wa kwanza kulia) wakifuatilia kwa makini michango ya wajumbe wa kamati hiyo wakati walipokuwa wkichangia hoja kuhusu mada mbalimbali zilizotolewa na wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi, tatizo la ujangili wa tembo na faru pamoja madhara yanayosababishwa na wanyama waharibifu wa mazao kama vile tembo katika vijiji vinavyozunguka hifadhi nchini, iliyofanyika jana mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Devota Minja, MB ( wa kwanza kulia) pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu wa Wizara hiyo kuhusu madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi, tatizo la ujangili wa tembo na faru pamoja madhara yanayosababishwa na wanyama waharibifu wa mazao kama vile tembo katika vijiji vinavyozunguka hifadhi nchini katika semina iliyofanyika jana mjini Dodoma. Kwa upande wa kushoto ni viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii .
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj.Gen. Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia) pamoja na na viongozi wa taasisi katika semina ya kamati ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii iliyofanyika jana mjini Dodoma .

  0 0


  Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo, Mjini Dodoma limepisha Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa Mwaka 2016 (The Legal Aid Bill, 2016).

  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa akitoa taarifa wakati wa kuwasilisha muswada huo amesema kuwa muswada huo wa sheria umepitia hatua nyingi na umechukua muda mrefu hadi kufikia hatua ya kujadiliwa na Bunge tukufu.

  Aliendelea kwa kusema kuwa muswada huo unapendekeza kutungwa kwa sheria ya msaada wa kisheria kwa lengo la kuanzisha (kwa mara ya kwanza katika histori ya nchi) mfumo wa kisheria wa kusimamia, kuratibu, kurasimisha na kutambua utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria katika mashauri yote ya Jinai na Madai kwa mahitaji.

  Aidha utaratibu uliokuwepo kwa miaka mingi kwa upande wa Serikali unahusu baadhi tu ya makosa ya Jina, makosa yenye adhabu kubwa kama vile ya kunyongwa hadi kufa na vifungo virefu. Ambapo huduma hiyo imekuwa ikitolewa katika ngazi ya Mahakama Kuu pekee na kwa wigo mdogo tu pale inapohitajika kwa maslahi ya haki na kwa maelekezo ya Jaji Mkuu au yeyote aliyekasimiwa mamlaka ya kutoa maelekezo hayo.

  “Kumekuwepo na ongezeko kubwa la mahitaji ya huduma ya msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria. Kutokana na hali hiyo, Serikali imeona ulazima wa kuanzisha mfumo wa kusimamia na kuratibu utoaji wa huduma hiyo ili kuhakikisha inatolewa na watu wenye sifa, kwa wahitaji halisi na kwa taratibu zinazofahamika ili iendane na matakwa ya kikatiba,” alifafanua Dkt. Mwakyembe.

  Vile vile ameeleza kuwa muswada huo unalenga kuwatambua wasaidizi wa kisheria, kufuta sheria ya msaada wa kisheria (katika mashauri ya Jinai).

  Kwa upande wake Mbunge Selemani Zedi amesema kuwa, muswada huo utawasaidia wananchi ambao hawana uwezo wa kuwalipa Mawakili wanapohitaji msaada wa Kisheria.

  Aidha, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson ameipongeza Serikali kwa muswada huo muhimu ambao Bunge umeipitisha unasuobiria kutiwa saini na Mhe. Rais ili kuwa Sheria.

  0 0


   TAARIFA KWA UMMA

  MAADHIMISHO YA SIKU YA ARDHIOEVU DUNIANI TAREHE 2 FEBRUARI 2017

  Kesho tarehe 2 Februari, 2017 ni maadhimisho ya siku ya Ardhioevu Duniani. Siku hii inaadhimishwa duniani kote kwa kutoa elimu na kuwakumbusha watu wote kuhusu uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za ardhioevu.
  Ardhioevu ni maeneo ya ardhi yaliyopo kandokando na ndani ya Chemchem, Mito, Maziwa na mwambao wa bahari wenye kina cha maji yasiyozidi mita sita wakati wa kupwa. Ardhioevu pia hujumuisha Madimbwi, Mabwawa, Tingatinga na sehemu zote yanapokusanyika maji kipindi kirefu cha mwaka.
  Tanzania hujumuika na nchi nyingine wanachama wa Mkataba wa “Ramsar” kuadhimisha siku ya ardhioevu duniani Februari 2 kila mwaka. Ujumbe wa mwaka huu wa Siku ya Ardioevu ni: "Ardhioevu Hupunguza Athari za Majanga” (Wetlands for Disaster Risk Reduction)". 
  Tafsiri ya kauli mbiu hii ni kwamba, Ardhioevu huzuia majanga ya mafuriko yanayoweza kutokea katika pwani za bahari, hupunguza athari za kiafya zinazoweza kujitokeza kutokana na madini hatarishi kama Zebaki, hupunguza uwezekano wa kutokea kwa baa la njaa kwa kuwa maeneo okozi wakati wa kiangazi kama vyanzo vya maji na chakula kwa binadamu na wanyama. 
  Ardhioevu pia ni maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa chakula kama vile mpunga na mbogamboga na chanzo cha maji yanayotumika kwenye kilimo cha umwagiliaji nchini. Arhioevu pia ni sekta endeshi ya uchumi wa nchi kwa kuwa ni chanzo cha maji yanayotumika kwenye kilimo, viwandani pamoja na uzalishaji wa umeme wa maji kwa gharama ndogo.
   Inakadiriwa kuwa asilimia 10 ya ardhi ya Tanzania ni ardhioevu ambayo ni muhimu kwa bioanwai, uchumi, shughuli za kijamii na kiikolojia. Maeneo haya ni makazi muhimu ya aina mbalimbali za viumbe hai wakiwemo samaki, viboko, mamba, ndege na viumbe wengine wasio na uti wa mgongo. Katika ikolojia ya ardhioevu tunapata bioanwai kubwa kuliko eneo lingine lolote duniani. 

  0 0

  Thanks

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Wakala wa Serikali wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) leo 31 Januari 2017, wamekutana na wadau wa mafuta katika kuangalia fursa za uagizaji na usambazaji wa mafuta nchini ambapo kwa sasa pia wanaangalia fursa za kutumia bandari ya Tanga ili kusaidia wananchi wa Mikoa ya Kaskazini.

  Hayo yameelezwa leo na Kaimu Wakala Mkuu wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja wa (PBPA) Modestus Lumato wakati akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Lumato amesema kuwa, kwa sasa PBPA inaangalia kushusha mafuta katika bandari ya Tanga ili kupunguza msongamano kwa bandari ya Dar es Salaam pamoja na kuondoa foleni..

  Amesema mwezi uliopita wameanza kushusha mafuta bandari ya Tanga kwa kiwango kidogo kutokana na ukubwa wa eneo la awali, ambapo kwa sasa tenda inayofuata wanatarajia kushushia tena Mkoani Tanga kwani itasaidia wateja wao wa ukanda wa Kaskazini ikiwemo mikoa ya Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na mikoa mingine ya jirani.

  “Tani za mafuta ya Dizeli na Petroli zinatarajiwa kwa awamu ijayo tukashuka bandari ya Tanga kwa kuanzia na tani 45,000. Mikoa ya Mwanza na jirani na mikoa hiyo itanufaika kwa kuja kuchukua bidhaa hiyo Tanga na kuliko kuja Dar es Salaam.” Alieleza Modestus Lumato.

  Amesema kuwa wameshatangaza zabuni ambapo wamejitokeza wazabuni watatu katika zabuni hiyo iliyotangazwa .
   Kaimu Mkurugenzi wa wakala waagizaji wa mafuta kwa pamoja (PBPA) Modestus Lumato  wakati akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, 
   
  Sehemu ya wadau wakifuatilia mjadala huo wakati wa mkutano na waandishi wa habari,

  0 0

   Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi leo umezindua kampeni ya upandaji miti katika Wilaya ya Kahama ikiwa na lengo la kupanda mti kwa kila wakia ya dhahabu ambayo imechimbwa kwenye mgodi wa Buzwagi, ambapo miti zaidi ya milioni moja na laki sita inatarajiwa kupandwa katika kipindi cha miaka miwili.

  Akizindua kampeni hiyo Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa hatua hiyo na kusema ni ya kizalendo kwa kuwa itasaidia katika kuboresha hali ya mazingira ya wilaya ya Kahama.

  “Jukumu la upandaji miti na kuhakikisha mazingira yetu yanatunzwa ni letu sote, Wenzetu wa Buzwagi wameanza kuonyesha jitihada kwa kupanda miti milioni moja na laki sita, hivyo sote kama Jamii hatuna budi kuwaunga mkono kwa kuhakikisha kila mmoja wetu katika eneo lake anapanda miti na kuifanya wilaya yetu ya Kahama izidi kupendeza”Alisema Nkurlu.

  Akizungumzia Malengo ya Kampeni hiyo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo amesema kama wadau muhimu wa mazingira wanalojukumu la moja kwa moja kuhakikisha shughuli za utunzaji wa mazingira zinakuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku.
  Mkuu wa wilaya Kahama Fadhili Nkurlu akipanda mti kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti milioni moja na laki sita itakayopandwa katika maeneneo mbalimbali wilayani kahama kwa lengo la kutunza mazingira pamoja na kuufanya mji wa Kahama upendeze.
  Mkuu wa wilaya kahama Fadhili Nkurlu akimwagia maji mti alioupanda wakati alipozindua kampeni ya upandaji miti
  Mkuu wa polisi wilaya ya Kahama Mussa Mchenya akishiriki pia upandaji miti.
  Afisa Usalama wa Wilaya ya Kahama Aretus Lyimo akishiriki upandaji miti wakati wa zoezi la uzindunzi wa upandaji miti milioni moja na laki sita.


  0 0

  Baadhi ya wakazi wa meneo ya Isanga na Ilolo jijini Mbeya wakiangalia jinsi ambavyo mvua kubwa iliyonyesha siku ya jana ilivyoharibu Mashamba yao ya mboga za majani kutokana na maji kujaa mpaka katika maeneo yao ya makazi .Picha Na Fadhiri Atick Mmg Mbeya.
  Kikosi cha Zimamoto na uokoji pamoja na baadhi ya wakazi wakiwa katika maeneo hayo kushuhudia na kujaribu kutoa msaanda kwa baadhi ya wakazi walio kwama kuvuka ng'ambo kutokana na maji mengi kujaa katika maeneo hayo.
  Mmoja kati ya wakazi wa jiji la Mbeya akistaajabu jinsi ambavyo maji yakisonga kwa kasi kutokana na Mvua kubwa iliyo nyesha kwenye baadhi ya maeneo Jijini humo na hakuna mtu alielipotiwa  kuathirika wala kupoteza maisha.
  Wakazi pamoja na wanafunzi wakitazama jinsi ambavyo maji yalivyo furika katika maeneo hayo.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini Mh.William Ntinika wapili kushoto akiwa katika chumba alicho lazwa Mwenyekiti wa Ccm wilaya ya mbeya mjini Ndugu Ephraim Mwaitenda ambe kalazwa katika hospitali ya rufaa jijini Mbeya kuajili ya matibabu ya kutolewa Goroli za lisasi zilizo baki mwilini mara baada ya kupigwa risasi na mtu asie julikana mnamo tarehe- 29 januari Mwaka huu nyumbani kwake usiku akiwa amelala.

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Waziri wa Nishati wa Zambia, Mabumba David wakiwa ndani ya Boti wakati wa ziara ya kutembelea Boya la Kupokea Mafuta la Single Point Mooring (SPM) jijini Dar es Salaam.

  Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imejipanga kuupokea Mradi wa Bomba Jipya la Kusafirisha Mafuta Safi kutoka Tanzania hadi Zambia unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

  Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Deusdedit Kakoko alisema hayo hivi karibuni alipokutana na Mawaziri wa Nishati wa Tanzania na Zambia walipofanya ziara ya kutembelea Boya la Kupokea Mafuta la Single Point Mooring (SPM) ikiwa ni hatua ya kukamilisha ziara yao ya kutembelea njia ya Bomba la TAZAMA na Vituo vya Kusukuma Mafuta waliyoianza jijini Ndola, Zambia na kumalizikia jijini Dar es Salaam, Tanzania.

  Aliyasema hayo kufuatia wito wa Waziri wa Nishati wa Zambia, Mulumba David alipoikumbusha Mamlaka hiyo kuhusiana na kauli iliyotolewa na Rais wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu wakati alipofanya ziara nchini mwezi Novemba Mwaka jana na kuitaka kuhakikisha inaongeza ufanisi wa utoaji huduma zake ikiwemo kuboresha Teknolojia ya kupokelea mafuta.

  Mhandisi Kakoko alisema anakumbuka vyema kauli hiyo ya Rais Lungu na aliongeza kwamba Mamlaka ya Bandari imejipanga vizuri kuhakikisha inatoa huduma zenye kiwango na kwamba hawapo tayari kupoteza ushirikiano wa kibiashara na Zambia.

  “Mlimsikia Rais Lungu alisema wazi Wazambia na Watanzania ni ndugu wa damu lakini alionya kwamba biashara inaweza isiwe ndugu kama tunaichezea; na akasema ni vizuri tuwe na ufanisi na tuwe na gharama ndogo ili Wazambia waweze kufaidi vinginevyo atakwenda kwingine; jambo hili hatuwezi kuruhusu litokee,” alisema Mhandisi Kakoko.

  Alibainisha kuwa, Mamlaka hiyo inapitia upya gharama zake kwa Zambia hususan ikizingatiwa kuwa hivi sasa kuna ushindani mkubwa hasa baada ya Msumbiji kuwa eneo salama.

  Aliongeza kuwa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 wamejipanga vyema kufanya maandalizi yote ya kuimarisha na kuboresha utendaji kazi wa Mamlaka hiyo kwenye suala la ushushaji wa mafuta ikiwemo kuweka Gati litakalohudumia Meli nyingi zaidi na kwa haraka zaidi. “Tunajipanga ili Bomba hili jipya likikamilika liweze kuunga moja kwa moja,” alisema.

  Katika ziara hiyo, ilielezwa kwamba Serikali za Tanzania na Zambia zimefanya tathmni ya kuanza utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Bomba jipya la Mafuta Safi na kwamba taratibu mbalimbali zimeanza kutekelezwa.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akiwaongoza Mawaziri wa Nishati wa Tanzania na Zambia pamoja na Ujumbe walioambatana nao kushuka katika Boti waliotumia kufanya ziara ya kutembelea Boya la Kupokea Mafuta la Single Point Mooring (SPM) jijini Dar es Salaam. Nyuma yake ni Waziri wa Nishati wa Zambia, Mabumba David, Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa.
  Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia). Katikati ni Waziri wa Nishati wa Zambia, Mabumba David walipokuwa ndani ya Boti kwenye ziara ya kutembelea Boya la Kupokea Mafuta la Single Point Mooring (SPM) jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini (Tanzania), Profesa Justin Ntalikwa (katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Zambia, Brigedia Jenerali, Emelda Chola (kushoto) wakati wa ziara ya kutembelea Boya la Kupokea Mafuta la Single Point Mooring (SPM) jijini Dar es Salaam.
  Ujumbe wa Tanzania na Zambia ulioongozwa na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo (wa sita kutoka kulia) na Waziri wa Nishati wa Zambia, Mabumba David (wa saba kutoka kulia) ulitembelea Boya la Kupokea Mafuta la Single Point Mooring (SPM) lililopo kwenye Bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Meneja wa DAWASCO Mkoa wa Ilala, Christian Kaoneka pamoja na fundi kutoka DAWASCO wakibadilisha mita ya Maji chakavu ya mteja kutoka maneneo ya Mtaa wa Jamhuri jijini Dar es Salaam ikiwa ni katika mwendelezo wa Zoezi la ubadilishaji wa mita za Maji chakavu zote kwa jiji la Dar es Salaam na Miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani wa Pwani.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi ameshauri juu ya kuwepo kwa sheria ya manunuzi kwa njia ya mtandao ili kuokoa muda unaotokana na kuzunguka kwa makaratasi katika ofisi.

  Profesa Janabi ameyasema hayo leo wakati akifungua mafunzo ya watumishi wa taasisi hiyo wanaohusika na manunuzi ambayo yameratibiwa na Bodi ya Manunuzi na Ugavi (PSPTB), amesema uwepo wa mafunzo hayo, utasaidia kutatua changamoto hizo.

  "kuendesha manunuzi katika mtandao kutapunguza gharama ambazo zinaweza kuokoa fedha nyingi zitakazotumika katika masuala mengine" alisema Profesa Janabi.

  Nae Mratibu Mkuu wa utafiti na ushauri wa PSPTB bwana Amos Kazinza, amesama kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 budget ya serikali imetenga asilimia 76 kwa ajiliya Ununuzi. Hivyo manunuzi huchukua kiasi kikubwa cha fedha. Amesema mabadiliko ya sheria yamelenga kuongeza ufanisi na kuhakikisha kwamba thamani ya fedha inapatikana.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi akizungumza na wataalamu wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya manunuzi ya Umma kwa watumishi wa tasisi hiyo.
  Washiriki wa mafunzo hayo wakisikiliza na kufatilia hotuba ya ufunguzi .
  Wataalamu kutoka bodi ya manunuzi na ugavi (PSPTB) wakiongozwa na afisa habari, Shamim Mdee katika mkutano huo .
  Mratibu mkuu wa Utafiti na ushauri wa PSPTB, Amos Kazinza akitoa elimu juu ya masuala ya manunuzi kwa watumishi wa tasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete.

  0 0

  Baada ya ukimya wa muda Jarida namba moja kwa stori za burudani Tanzania "Baabkubwa Magazine" linakuarifu wewe mdau wetu, tumeanza kazi kwa msimu mpya na soon as possible toleo jipya linatuwa mtaani kwako likiwa na muonekano tofauti na wakuvutia kwa kusoma kila pages utakayotupia macho. NikoHub and Baabkubwa ipo chini ya Candy and Candy Co LTD.

  NikoHub ni application ambayo imeziunganisha Migahawa, Movie stores, Maduka ya wines and spirit, Bars na Clubs zote za Tanzania, inafanya kazi kwa kupatanisha muuzaji na mnunuzi moja kwa moja na unaweza kupokea orders au kufanya delivery au vyote kwa pamoja mahali popote na karibu mtu anapokuwa. mnunuzi anapata nafasi ya kuona kitu anachohitaji kwa urahisi, unaweza ku-compare prices na mnunuzi anapata nafasi ya kuona kile competitors wake wanafanya hivyo kuweza kujirekebisha, na pia inampa nafasi ya kujulikina zaidi worldwide na kupata wateja wengi.

  Nikohub and Baabkubwa inaachiwa kwenye soko la Tanzania na imekuandalia special offer (Cake and Moet) ya Valentines ambayo itahusika na kila mtu, na couples 500 watakua featured kwenye Baabkubwa Magazine and TV show, ujumbe huu umepokelewa vyema na so far more than 17,000 people wamesha download nikohub app wakingojea kwa hamu hii special offer. Ofisi za Baabkubwa Magazine and NikoHub zipo Masaki opposite na Cape Town Fish Market, unaweza kutembelea page zetu za mitandao ya kijamii kama vile;
  Instagram- @Baabkubwamagazine/ @nikohubtz
  Facebook- Baabkubwa Magazine/ Nikohub Tanzania
  Twitter- Baabkubwa Magazine
  Website- Baabkubwa.com

  0 0

  Dodoma, Jumatano, 1 Februari, 2017:  Serikali imetoa ufafanzi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa mikopo kwa vijana na malipo ya ada kwa fedha za kigeni. Ufafanuzi huo umetolewa mjini hapa leo wakati wa kikao cha pili katika Mkutano wa Sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  

  Kuwainua Vijana Kiuchumi 

  Akijibu hoja kuhusu namna vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini wanavyoweza kufaidika kiuchumi, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Anthony Mavunde, amesema Serikali imetenga fedha za kutosha kupitia mifuko mbalimbali kuwawezesha vijana kwa mitaji na mafunzo ya ujasiriamali ili kuwainua kiuchumi.

  Ameongeza kuwa vijana wenyewe ndio wanaopaswa kuchangamkia fursa hizo na pale wanapojiunga katika vikundi mbalimbali wamekuwa wakipewa mikopo kwa ajili ya mitaji. Alitoa mfano wa jinsi Serikali ilivyowawezesha vijana waliojiunga na kuwekeza katika viwanda vidogo vya maziwa na chaki mkoani Simiyu. 

  Amewataka pia Wabunge na Halmashauri zote nchini kuendelea kupigania kutengwa maeneo maalum katika sekta mbalimbali kwa ajili ya kuwapatia vijana na kutengwa kwa asilimia 5 ya mapato ya Halmashauri kwa maendeleo ya vijana

  Ada kwa Fedha za Kigeni

  Serikali imesema, ingawa haijapokea malalamiko yoyote kuhusu wananchi wasioridhihwa na mtindo wa kutakiwa kulipa malipo ya ada kwa fedha za kigeni katika baadhi ya shule na vyuo, lakini imesisitiza kuwa wale wanaotoza ada kwa fedha za kigeni wanakiuka Sheria.

  Akitoa ufafanuzi huo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya amesema kwa mujibu wa kifungu cha 28 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT), 2006, fedha inayopaswa kutumika kwa malipo ya huduma nchini ni Shilingi ya Tanzania. Ameviagiza vyuo na shule nchini kuacha kutoza ada kwa fedha za kigeni na kuhimiza wananchi watakaobainika kufanya hivyo kutoa taarifa Serikalini.

  Si Tatizo Kutumia Majengo UDOM 

  Serikali imesisitiza kuwa baadhi ya Wizara zilizoanza kutekeleza agizo la kuhamia Dodoma kutumia baadhi ya majengo kwa muda kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) hakutaathiri shughuli za chuo. 

  Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama.  Waziri Jenista amesisitiza kuwa baadhi ya Wizara zitatumia majengo ya UDOM kwa sababu mengi ya majengo hayo yalikuwa hayatumiki kwa sasa kwa shughuli za chuo hicho na hakutakuwa na muingiliano na shughuli za chuo.

  Mradi wa Mabilioni Maji Dar

  Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Dar es Salaam imeanza kutekeleza mradi wa usambazaji wa maji utakaogharimu Dola za Marekani milioni 32.772 ambazo ni mkopo kutoka Benki ya Exim ya China. Mradi huo utahusisha sehemu yote ya jimbo la Kawe, Dar es Salaam. Mradi huo utachukua miezi 15. 

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wakati alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa zamani wa baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja leo katika semina ya Siku moja kuhusu Umuhimu wa Takwimu na matumizi yake.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akifungua semina ya siku moja kuhusu Umuhimu wa Takwimu na Utekelezaji wake kwa Viongozi mbali mbali katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja leo,(kushoto) Makamo wa Rais Balozi Seif Ali Iddi na katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Kiongozi Dkt.Abduhamid yahya Mzee (kulia).
  Mtakwimu Mkuu wa Serikali Bibi Mayasa Mahfoudh Mwinyi alipokuwa akitoa Muhtasari wa Majukumu ya Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali katika Upatikanaji wa Takwimu na Utekelezaji wake katika semina ya viongozi iliyofanyika leo katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mjini Unguja.


  0 0
  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  KOCHA mkuu wa Mamelod Sundown Pitso Mosimane aahidi kuondoka na ushindi katika ardhi ya Tanzania dhidi ya Azam mechi itakayopigwa saa 1 usiku  kwenye dimba la Uwnaja wa Taifa.

  Mamelod ambao ni mabingwa wa Klabu Bingwa Barani Afrika wanajiandaa na mchezo wa Super Cup dhidi ya mabingwa wa kombe la Shirikisho TP Mazembe na wakaamua kutafuta mechi za kirafiki ili kujipima nguvu.

  Akizungumza walipomaliza mazoezi hayo jana, Mosimane ameweka wazi kuwa timu yake imejiandaa kufanya vizuri kwenye mechi hizi za kirafiki atakazocheza hapa nchini na kikubwa ni kuwa wanajiandaa na mechi dhidi ya Mazembe ambapo inatarajiwa kuw aya ushindani mkubwa sana.

  Miaka minne iliyoiputa timu ya Mamelod iliweza kucheza mechi ya kirafiki na Azam nchini Afrika Kusini walipokuwa wameenda kuweka kambi na mshambuliaji wa Azam kwa kipindi hiuko Gaudency Mwaikimba aliweza kuifungia timu yake bao pekee la ushindi dhidi ya Mamelod Sundown.

  Baada ya mechi yao dhidi ya Azam , Mamelod watacheza na timu ya African Lyon Februari 3 kwenye Uwanja wa Taifa.
   Kocha mkuu wa Mamelod Sundown Pitso Mosimane akiwa anafuatilia mazoezi ya wachezaji jana katika Uwanja wa Taifa.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Nusu fainali ya kwanza ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) inayifanyika nchini Gabon inaendelea tena leo kwa mchezo mmoja kuchezwa kati ya Burkina Faso dhidi ya Misri utakaochezwa kwneye dimba la Stade de l'Amitié, Libreville. Timu hizo zinakutana zikiwa zimetinga hatua hiyo baada ya kuziondoa timu za Moroco na Tunisia kwneye mchezo wa hatua ya robo fainali.
  TAKWIMU 

  Februari 25 1998, kwenye kombe la mataifa Afrika kwenye kombe ka Mataifa  Afrika timu zilikutana na Burkina Faso kufungwa kwa goli 2-0 dhid ya Misri.
  Januari 01 2000, kwenye kombe la Mataifa Afrika zilikutana tena lakini Burkina Faso akiendelea kunyanywasa na Misri na kuambulia kipigo cha 4-2.
  Februari 27 2016, zilikutana tena katika mchezo wa kirafiki na Misri kufanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-0.


  BURKINA FASO  Hii ni mara ya kumi (10) kwa timu ya taifa ya Burkina Faso kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika, mara ya kwanza iliweza kushiriki michuano mwaka 1970.

  Mwaka 1998 Burkina Faso ikiwa mwenyeji waliweza kushika nafasi ya nne na mafanikio makubwa iliyowahi kupata timu hii ni mwaka 2013 ambapo ilifika kwenye hatua ya fainali.

  Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Burkina Faso ni Paulo Duarte, raia wa Ureno anayejulikana kwa jina la utani la  “Les Étalons” Ikiwa na maana ya Farasi.

  Kikosi kamili cha Burkina Faso: 

  Makipa: Herve Koffi (ASEC/CIV), Moussa Germain Sanou (Beauvais/FRA), Aboubacar Sawadogo (Kadiogo)

  Mabeki: Ernest Congo (Khemisset/MAR), Yacouba Coulibaly (Bobo), Issoufou Dayo (Berkane/MAR), Bakary Kone (Malaga/ESP), Souleymane Kouanda (ASEC/CIV), Issoumaila Lengani (Happoel Ashkelon/ISR), Patrick Malo (Smouha/EGY), Issouf Paro (Santos/RSA), Steeve Yago (Toulouse/FRA)

  Viungo: Cyrille Bayala (Sheriff Tiraspol/MDA), Adama Guira (Lens/FRA), Charles Kabore (Krasnodar/RUS, capt), Prejuce Nacoulma (Kayserispor/TUR), Bakary Sare (Moreirense/POR), Blati Toure (Omonia Nicosia/CYP), Abdoul Razack Traore (Karabuspor/TUR), Alain Traore (Kayserispor/TUR), Bertrand Traore (Ajax Amsterdam/NED), Jonathan Zongo (Almeiria/ESP)

  Washambuliaji: Aristide Bance (ASEC/CIV), Banou Diawara (Smouha/EGY), Jonathan Pitroipa (Al Nasr/UAE.

  MISRI

  Haya yatakuwa mashindano ya 23 kwa timu ya taifa ya Misri inayifahamika kama Pharaohs, wanarejea katika michuano hii kwa mara ya kwanza baada ya kushiriki mara ya mwisho mwaka 2010.

  Misri wanasalia  kuwa taifa bora, kuweka historia ya kushinda mataji mengi ya taji hili, mara 7 mwaka 1957,1959,1986,1998,2006,2008 na 2010.

  Safari ya kwenda Gabon  Misri ilipangwa katika kundi moja na Nigeria na Tanzania katika michuano ya kufuzu kwa fainali ya mwaka huu. Kati ya mechi nne ilizocheza nyumbani na ugenini baada ya Chad kuondolewa katika michuano hiyo, ilishinda mechi tatu na kutoka sarena  hivyo kuongoza kundi la G kwa alama 10.

  Hali ya kisiasa imekuwa ikielezwa kuwa moja ya sababu ya Misri kukosa kufika katika michuano hii tangu mwaka 2010, na kuwepo kwao huenda kukaleta ladha tofauti.

  Kocha.
  Kocha wa timu hii ni raia wa Argetina Héctor Cúper mwenye umri wa miaka 61, alianza kuifunisha Misri mwaka 2015 na ndio timu ya kwanza ya taifa kunolewa na Muargentina huyona  ambaye ana uzoefu mkubwa kufuza soka katika klabu mbalimbali.

  Alianza kufundisha soka mwaka 1993, wakati huo akiifunza klabu ya Huracan na baadae  Internationale ya Italia kati ya mwaka 2001-2003, Mallorca 2004-2006 na Parma mwaka 2008. Kabla ya kupewa kibarua nchini Misri, alikuwa anaifunza Al Wasl FC kutoka Falme za Kiarabu kati ya mwaka 2013-2014.

  Kikosi
  Makipa: Ahmed El-Shennawy (Zamalek), Essam El-Hadary (Wadi Degla), Sherif Ekramy (Al Ahly) 

  Mabeki: Ahmed Fathi (Al Ahly), Ahmed Elmohamady (Hull City – Uingereza), Mohamed Abdel-Shafy (Al-Ahli – Ksa), Karim Hafez (Lens – Ufaransa), Ahmed Hegazy (Al Ahly), Saad Samir (Al Ahly), Ahmed Dweidar (Zamalek), Ali Gabr (Zamalek), Omar Gaber (Basel – Uswizi).

  Viungo wa Kati: Mohamed Elneny (Arsenal – Uingereza), Tarek Hamed (Zamalek), Ibrahim Salah (Zamalek), Abdallah El-Said (Al Ahly), Amr Warda (Panetolikos – Ugiriki), Ramadan Sobhi (Stoke City – Uingereza), Mahmoud Hassan ‘Trezeguet’ (Royal Mouscron – Ubelgiji). 

  Washambuliaji: Ahmed Hassan ‘Koka’ (Braga – Ureno), Marwan Mohsen (Al Ahly), Mahmoud Abdel-Moneim ‘Kahraba’ (Al-Ittihad – Ksa), Mohamed Salah (As Roma – Italia).

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Klabu ya Yanga imeendelea na mazoezi yake leo kwenye viwanja vya Chuo cha Polisi Kilwa Road huku Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Zimbabwe Donald Ngoma akirejea kujiunga na wenzake.

  Mshambuliaji huyo ameanza mazoezi rasmi leo na kujiunga na wenzake baada ya kuwa nje kwa takribani mwezi m moja pamoja na kupata matatizo ya kifamilia ya kufiwa na kaka yake aliyekuwa anaugua ugonjwa wa kansa.

  Ngoma aliyeumia goti kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi aliweza kukosa michuano hiyo kuanzia mchezo waio dhidi ya Zimamoto na pindi alivyorejea alitakiwa kukaa nje kwa wiki zisizopungua sita.

  Akizungumza na Globu ya Jamii, Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema kuwa Ngoma ameungana na wenzake leo na tayari ameanza nao mazoezi ya pamoja na hivi karibuni atarejea uwanjani.

  Saleh amesema kuwa, Kocha Mkuu George Lwandamina aanaweza kumtumia katika mchezo unaofuata dhidi ya Stand siku ya Ijumaa kwani yuko fiti kwa sasa.  Andrew Vicent 'Dante' ameanza pia mazoezi na wenzake na mwalimu anaweza kumtumia kwenye mchezo ujao wa ligi kuu.

  "Malimi Busungu ndiye hajaweza kuungana na wenzake kwakuwa alikuw ana malaria kali na alikuwa amelazwa sema kwa sasa ametoka anaendelea vizuri,"amesema Saleh. 

  Yanga wanakutana na Stand United huku wakitaka kuhakikisha wanatoka na ushindi ili kuendelea kuongoza ligi na kutetea ubingwa wao. Kikosi hicho kinaingia kambini baada ya mazoezi ya kesho asubuhi.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma jFebruari 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0  0 0older | 1 | .... | 1542 | 1543 | (Page 1544) | 1545 | 1546 | .... | 3285 | newer