Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MARAIS MBALIMBALI WA AFRIKA KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRIKA (AU) MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA

$
0
0
 Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa kwa ajili ya mazungumzo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi kabla ya kuanza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Akinwumi Adesina mara baada ya kumaliza mazungumzo yao mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za AU mjini Addis Ababa Ethiopia.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn wakati akitoka kwenye mkutano wa AU mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. 



TAASISI MPYA YA KILIMO YAZINDULIWA NCHINI, NI AGRO FOR HELP

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandiliwa akikata utepe kuzindua taasisi mpya ya kilimo ya Agro for help, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa PSPF, Jijini Dar es salaam. kushoto ni wakurugenzi wenza wa taasisi hiyo Neema Shukuru na Mwaka Mohamed.

Na Humphrey Shao, Globu ya jamii.

Wito umetolewa kwa wananchi mbalimbali kujikita katika kilimo ili kuendana na mabadiliko ya uchumi hapa nchini kuelekea katika uchumi wa Viwanda.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandiliwa wakati wa ufunguzi wa taasisi isiyo ya kiserikali inayohusu kilimo ya Agro for Help Foundation.

“katika kuelekea uchumi wa viwanda ni lazima tuwe na kilimo cha uhakika kwani watu wengi sana wamekuwa wakilima pasipokuwa na elimu ya kutosha hivyo kufanya kilimo kisichokuwa na tija” amesema Mgandilwa.

Kwa upande wake muwasisi wa taasisi hiyo, Mwaka Mohamed amesema kuwa wameamua kuanzisha taasisi hiyo ili kuweza kuwasaidia wakulima ambao wengi wao hawana elimu sahihi juu ya kilimo chenye tija.

Amesema kuwa Agro for help Foundation ipo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mkulima wa Tanzania anapata msaada wa kutosha wa mtaji, pembejeo na namna gani wanaweza kufanya kilimo cha kisasa kwa kuunganishwa na wadau mbalimbali wa kilimo.

Aidha ametoa wito kwa wadau wote wenye malengo ya kuhakikisha kuwa kilimo cha Tanzania kinakuwa kwa kuweza kushirikiana na Agro for help Foundation kwa maslahi ya wakulima.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandiliwa akizungumza na wadau wa kilimo wakati wa uzinduzi wa taasisi mpya ya kilimo ya Agro for help, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa PSPF, Jijini Dar es salaam. 
Henry Kazula kutoka Jielimishe akizungumza na wadau mbalimbali waliofika katika uzinduzi wa taasisi mpya ya kilimo ya Agro for help, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa PSPF, Jijini Dar es salaam. 
baadhi ya wadau waliofika katika mkutano huo wakifatilia kinachoendelea
waasisi wa taasisi mpya ya kilimo ya Agro for help, Neema Shukuru na Mwaka Mohamed wakimkabidhi ripoti mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa.

DAWASCO KUZIONDOA MITA CHAKAVU ZA MAJI JIJINI DAR

$
0
0
Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) limeanza zoezi maalum la kuondoa mita za Maji zote chakavu na za muda mrefu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam pamoja na miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani ili kuweza kuongeza ufanisi katika usomaji wa Mita, kupunguza kiasi cha Maji kinachopotea na kutoa matumizi halisi ya Maji yanayotumiwa na mteja.

Akizungumzia wakati wa zoezi hilo hilo, Kaimu Meneja Uhusiano wa Dawasco, Bi. Everlasting Lyaro ameeleza kuwa shirika linaendelea na zoezi la kubadilisha mita za Maji zote ambazo ni mbovu na zenye umri mkubwa kwenye maeneo yote ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na maeneo ya mkoa wa pwani ambapo mita takribani 25,000 zimekwisha badilishwa hadi kufikia sasa.

“Shirika linaendelea na zoezi la kuondoa mita za Maji ambazo ni chakavu na za muda mrefu, tayari tumefanikiwa kubadilisha Mita mpya za Maji zipatazo 25,000 katika makazi ya watu, taasisi pamoja na viwanda na lengo letu mi kuweza kubadilisha Mita za Maji zipatazo 85,000 hadi kufikia mwisho wa mwaka huu ili kusaidia kutoa matumizi halisi ya Maji yanayotumiwa na mteja wetu” alisema.

Alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa wafanyakazi wanaofanya zoezi hilo na endapo watapata wasiwasi basi waulize vitambulisho vya kazi ili kuepuka utapeli.

“Wananchi watupe ushirikiano ili zoezi hili lifanikiwe na kukamilika kwa wakati kwani lina faida kwetu sisi kama shirika na kwa mteja. Pia tukumbuke kuwa zoezi hili ni bure hivyo wananchi wasidanganywe kuchangia hela yoyote” alimalizia Bi Lyaro

Wakizungumzia juu ya zoezi hili wananchi wanaohudumiwa na shirika hilo akiwemo Bi. Hadija Omary mkazi wa Mwananyamala A, amepongeza hatua hiyo iliyochukuliwa na Dawasco kwani itasaidia kuondoa kero iliyokuwepo ya mita hizo kuvuja na kupelekea bili Maji ya mteja kuwa kubwa.

“Tumefarijika sana kuona Dawasco wameanza kubadilisha mita zao kwani ni za muda mrefu na zimekuwa zikivujisha Maji na kupelekea bili zetu za maji kupanda kila wakati” alisema.

Naye, Bw. Boniface Mwakipesile, mkazi wa Mikocheni B, amezilalamikia mita hizo mpya na kudai kuwa tangu zilipofungwa bili yake ya Maji imepanda ikilinganishwa na siku za nyuma, hivyo ameshauri elimu zaidi itolewe kuhusiana na mita hizo.

“Mita hizi mpya za Maji mimi binafsi sizielewi kabisa, tangu zilipofungwa nashangaa bili yangu ya Maji inakuja tofauti, imekuwa kubwa sana ikilinganishwa na zamani hivyo Dawasco wazidi kutuelimisha zaidi maana wengi wanaziona kama mita za mwendo kasi” alisema.

MANISPAA YA ILALA YAWATAKA WANANCHI KULIPA KODI YA MABANGO

$
0
0
Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bi Tabu Shaibu akizungumza wakati wa mkutano wa waandaishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa wananchi kulipa kodi ya mabango ili kuchochea maendeleo katika manispaa hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Sehemu ya Usalama barabarani na mabango Manispaa ya Ilala Bw. James Batinagwa.
Afisa Uhusiano wa Manisapaa ya Ilala Bi Tabu Shaibu akifafanua kwa waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu mikakati ya manispaa hiyo katika kuwaletea wananchi maendeleo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO bi Zamaradi Kawawa.
Mkuu wa Sehemu ya Usalama barabarani na mabango Manispaa ya Ilala Bw. James Batinagwa (kushoto)akisisitiza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) umuhimu wa kutii sheria bia shuruti kwa kulipa kodi ya mabango kwa mujibu wa sheria na kanuni.katikati ni Afisa Uhusiano wa Manispaa hiyo Bi Tabu Shaibu na kulia ni Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO bi Zamaradi Kawawa.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa manispaa ya Ilala na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam ulioenga kueleza mikakati ya Manispaa hiyo katika kuwaletea wananchi maendeleo. (Picha na Frank Mvungi-Maelezo)

MKURUGENZI WA MALINYI AWAPONGEZA WAKUU WA IDARA

$
0
0
Na Humphrey Shao ,Globu ya Jamii

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, Marcelin Ndimbwa amewapongeza wakuu wa idara wote wateule waliopitishwa na baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo.

Ndimbwa alichukua fursa hiyo mara baada ya wakuu hao kupata baraka ya baraza la madiwani wilayani humo.

“ Nina imani kubwa na ninyi, pia wananchi wa Malinyi wana imani kubwa Sana na ninyi. Tekelezeni wajibu wenu kwa kufuata (STK) zaidi Sana tunzeni nidhamu ya Hali ya juu, sio kwa mkurugenzi na m/kiti Bali kwa wananchi tena wale wa hadhi ya chini kabisa, Maana ndo waliotoa dhamana hiyo kwenuNami kwa niaba yao nimekupeni kamisheni”.

Amesema anawategemea Sana kufikia na kutimiza kile alichokikusudia kuwapa wananchi kupitia Ilani ya CCM chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli.

MKWASA AREJEA RASMI YANGA, APEWA UKATIBU MKUU

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


UONGOZI wa klabu ya Yanga umemtangaza aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo na mchezaji wa zamani wa mabingwa hao wa Ligi Kuu Vodacom Charles Boniface Mkwasa kuwa katibu mkuu akichukua nafasi ya Baraka Deusdedit anayerejea kwenye Idara yake ya Fedha.

Kocha huyo ambaye pia amewahi kuifundisha Yanga ameingia kandarasi ya miaka miwili ya kuitumikia Yanga. 

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema kwamba Mkwasa anaanza majukumu yake rasmi Februari 1, mwaka huu na sababu kubwa ya kumchagua Mkwasa ni kuimarisha safu ya uongozi wa klabu hiyo ambapo aliyekuwa kaimu katibu mkuu, Baraka Deusdedit anarejea katika nafasi yake ya zamani ya Ukurugenzi wa Fedha.

Sanga alisema kuwa wanajua kuwa Mkwasa ana uwezo mkubwa wa kuitumukia vema nafasi hiyo na kuleta maendeleo na mabadiliko ndani ya Yanga na nafahamu watu watashangaa na kujiuliza sababu ya kupatiwa nyadhifa hiyo ila kiukweli ana uzoefu mkubwa katika kazi hiyo tofauti na watu wanavyomuelewa.

“Na hii si mara ya kwanza, hata Zambia, Kalusha Bwalya amewahi kuwa katibu mkuu wa chama cha soka nchini humu huku wakijua kuwa ni mchezaji mstaafu au kocha, Yanga tumemuona Mkwasa ni bora ya zaidi katika nafasi hiyo,” alisema Sanga.

Kwa upande wake Mkwasa alisema kuwa nafasi hiyo aliyopewa ni kubwa na nyeti sana katika masuala la soka sehemu yoyote. Alisema kuwa kwa sasa yupo tayari kujitolea kadri ya uwezo wake kuhakikisha Yanga inakuwa na kufikia malengo yake kwa wakati uliopongwa.

Mkwasa alisema kuwa mbali na kuitumikia nafasi hiyo mpya atakuwa tayari kushirikiana na benchi la ufundi la timu hiyo kwa maslahi mapana zaidi ya timu. "Kwa sasa napenda kuwaahidi wanayanga wote kuwa nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha tunailetea klabu yetu maendeleo na nitahakikisha tunafanya vizuri ndani na nje ya nchi", alisema Mkwasa

MAKALLA ATOA SIKU 14 KWA HALMASHAURI ZOTE MKOANI MBEYA KUWAONDOA WALIOVAMIA MAENEO YA HIFADHI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na waanchi wa kijiji Cha Hanzya Kata ya Itagano jijini Mbeya katika kilele cha Kampeni ya Upandaji MitiKimkoa .

Na Emanuel Madafa,Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ametoa siku 14 kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya kuhakikisha inawaondoa watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi za misitu pamoja na hifadhi ya misitu ya mlima Mbeya.

Aidha amesema agizo hilo pia liendane na suala la kudhibiti shughuli zote za kibinadamu kando kando ya mita 60 kwa kufuata sheria ya mita 60.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa agizo hilo katika kilele cha upandaji miti kimkoa katika eneo la chanzo cha maji cha mto Hanzya kata ya Itagano jijini Mbeya. Amesema lazima agizo hilo litekelezwe mapema sanjali na kufanya tathimini ya hali yauhalibifu wa mazingira katika maeneo yot.

"Nikazi bure kuendelea kupanda miti wakati ile iliyopandwa mwaka uliopitwa imehalibiwa kwa kukosa matunzo au kuhalibiwa kwa shughuli za kibInadam"Alisema Makala.

Aidha Makalla ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kupanda miti ya vivuli na matunda kwenye maeneo yao hususani katika maeneo ya vyanzo vya maji kwani ni muhimu kwa maisha ya kila siku.

"Serikali imeweka lengo la kupanda miti isiyopungua milioni 1 kwa mwaka katika kila halmashauri mkoani humo ambapo mwezi juni mwaka huu kufanyika tathimini ya pamoja kuona zoezi hilo lilipo fikiwa"Alisema .

Naye Afisa Misitu Mkoa wa Mbeya Ndugu Joseph Butuyuyu mpango wa kuhifadhi safu ya Mlima Mbeya umeanza kwa mafanikio makubwa hasa kutokana kuungwa mkono na waziri mwenye dhamana ya Mazingira Ndugu January Makamba mara baada ya kutembelea safu ya Mlima huo.
Wananchi wa kijiji cha Hanzya kata ya Itagano wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla katika kilele cha Upandaji Miti Kimkoa katika SAFU ya Mlima Mbeya January 31 ,2017.

KAULI YA SERIKALI BUNGENI DODOMA KUHUSU MWENENDO WA HALI YA UCHUMI WA TAIFA

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwasilisha kauli ya Serikali kuhusu Mwenendo wa Hali ya Uchumi wa Taifa, Bungeni Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (Katikati) akitoka nje ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kuwasilisha kauli ya Serikali kuhusu Mwenendo wa Hali ya Uchumi wa Taifa, Bungeni Mjini Dodoma.
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakibadilishana mambo mawili matatu, baada ya kumalizika kwa shughuli za Bunge Mchana Mjini Dodoma (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

BALOZI KAIRUKI ATEMBELEA TIC LEO

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Clifford Tandari akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini China, Balozi Mbelwa Kairuki wakati alipokwenda kumtembelea ofisini kwake, leo Januari 31, 2017 ambapo walifanya Mkutano wao wa kuhakikisha Uwekezaji zaidi wa makampuni kutoka China haswa katika ujenzi wa Viwanda unakuzwa ili kuendana na Agenda kuu ya awamu ya Tano ya Uwekezaji katika viwanda ili kuongeza ajira na kupanua wigo wa kodi. Kituo cha Uwekezaji kiliahidi kutoa ushirikiano kwa balozi huyo ili kuhakikisha kuwa juhudi zetu za kuitangaza Tanzania kwa Wawekezaji wa nchini China zinafikiwa kwa haraka.

Serikali Yachukua Hatua Kuhakikisha Hali ya Chakula na Lishe ni Imara Nchini

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.

Katika kukabiliana na athari za ukame, Serikali imechukua hatua za makusudi kuhakikisha kuwa hali ya chakula na lishe ni imara nchini.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba ameyasema hayo leo Mjini, Dodoma katika Kikao cha Bunge alipokuwa akitoa kauli ya Serikali kuhusu hali ya chakula na lishe kwa mwaka 2016/2017.

“Tathimini imebainisha kuwa Halmashauri za wilaya 55 zinahitaji jumla ya tani 1,969 za mbegu bora za mahindi, mtama na mizizi inayokomaa kwa muda mfupi na kustahimili ukame,” alifafanua Dkt. Tizeba.

Aliendelea kwa kusema kuwa mbegu hizo zinahitajika ziwafikie mwezi Februari 2017 iliziweze kupandwa katika msimu wa 2016/2017 katika maeneo yanayoendelea kupata mvua wakati huu wa mwaka.

Dkt. Tizeba alizitaja hatua ambazo Serikali inazichukua kuhakikisha kuwa hali ya chakula na lishe ni imara kuwa ni pamoja na;

Kusimamia usambazaji wa mbegu za mazao ya kilimo zinazostahimili ukame na zinazozaa kwa muda mfupi ambazo ni pamoja na mtama, uwele na mbegu za mazao aina ya mizizi za mihogo na viazi vitamu ili kuzitumia vizuri mvua zinazonyesha sasa.

Kuhamasisha wakulima kupanda mazao aina ya mizizi, mtama na uwele kwa maeneo yanayopata mvua za masika ambazo zinaendelea kunyesha na mawakala wa pembejeo pamoja na vivutio vya utafiti vilivyopo katika kanda mbalimbali hapa nchini.

Vile vile Serikali kupitia Wakala (NFRA) inaendelea kuhifadhi kwa uangalifu chakula kilichopo ili kitumike pale kitakapohitajika.

Hatua nyingine ni Kuhamasisha sekta binafsi kununua mazao ya chakula katika maeneo yaliyo na ziada na kuyauza katika maeneo yenye uhaba wa chakula. Aidha wafanyabiashara waliohifadhi mahindi wanaombwa kusambaza chakula hicho katika masoko ya ndani ya nchi ili kupunguza mfumuko wa bei.

Aidha Serikali inaendelea kuhimiza usindikaji wa mazao ya chakula kwa kuyaongezea thamani na kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhiimu wa kula vyakula vya aina zote.

Dkt. Tizeba amesema kuwa kutokana na hali ya mwenendo wa unyeshaji wa mvua za vuli na msimu kutoridhisha katika maeneo mengi ya nchi, Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanashauriwa kuendelea kuhamasisha na kusimamia wakulima kutuma mbegu zinazokomaa mapema na kupanda mazao yanayostahimili ukame.

Aidha Serikali imewataka wakulima kuendelea kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha kwa kupanda mazao yanayostahimili ukame na kukomaa kwa muda mfupi na pia waendelee kutunza na kutumia chakula walichonacho kwa uangalifu.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba

AZAM FC KUKIPIGA NA MAMELOD SUNDOWN KESHO UWANJA WA TAIFA

$
0
0
 Afisa habari wa Azam Jafar Iddy Maganga.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KLABU ya Azam imeridhia kucheza na mabingwa wa Afrika Mamelod Sundown baada ya timu za Yanga na Simba kujiondoa na kila mmoja akitoa sababu zake.

Akiyasema hayo, Afisa habari wa Azam Jafar Iddy Maganga amesema kuwa mechi yao na mabingwa hao wa Klabu Bingwa Afrika utafanyika majira ya saa moja usiku kwenye Uwanja wa Taifa ambapo wanategemea kutumia kikosi chao cha kwanza kujipima nao.

Maganga amesema kuwa, mwaka jana walivyoenda kuweka kambi nchini Afrika Kusini na wakafanikiwa kucheza nao mechi ya kirafiki kwahiyo hawana budi nao kufanya hivyo ingawa wamepata taarifa ya  mchezo huo ikiwa imechelewa.

"tumechelewa kupata taarifa ya mchezo huo, ni jana usiku ila uongozi wa klabu ya Azam umeamua kukubali mechi hiyo ichezwe kesho saa 1 usiku kwani hata sisi mwaka jana tulivyoenda kuweka kambi nchini Afrika Kusini tuliwaomba mechi na tukacheza nao,"amesema Maganga.

Kwenye mchezo huo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Mamelodi, Azam walifanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0.

Klabu za Yanga na Simba zimegomea kucheza mechi hiyo ya kirafiki huku Simba wakisema kuwa hawawezi kucheza mechi siku ya Jumatano halafu Jumamosi wakacheze mchezo wa ligi dhidi ya Majimaji na kwa upande wa Yanga nao wamesema kucheza Ijumaa dhidi ya Mamelod na jumapili wakutane na Stand haiwezekani.

TRA YATANGAZA MWISHO WA UHAKIKI KWA TIN NAMBA KWA MKOA WA DAR ES SALAAM

HAKUNA MUDA WA KUONGEZA UHAKIKI WA TIN NAMBA KWA MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) imesema uhakiki wa namba ya utambulisho ya mlipa kodi ‘TIN Number’ kwa Mkoa wa Dar es Salaam  umekwisha na uhakiki mwingine utahamia Mikoa mingine.

Akizungumza na Blogu ya Jamii ya Michuzi ,jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo amesema uhakiki TIN Number muda wake ulikuwa ukiongezeka kutokana na mahitaji.

Kayombo amesema kuwa kwa sasa muda hautaongezwa ,na wenye Tin number hawatakiwi kutumia mpaka pele watakapopata maelezo katika ofisi za TRA ili waweze kuendelea kutumia namba hizo.

Amesema uhakiki huo ulianza Agasti hadi Oktoba na kuongeza tena muda wa miezi mitatu ambao umeishia leo.

Kayombo amesema kuwa wale ambao wana Tin number na zinadaiwa TRA wanazo na wanatakiwa kulipa kodi zao ambazo wanadaiwa.

Amesema uhakiki wa Number unasaidia kupata taarifa za mfanyabiashara kwa namba ya simu, makazi, sehemu anayofanyia kazi pamoja na anuani za mlipa kodi.

‘’Watu wote wenye Tin Number wasizitumie mpaka pele watapokuwa wamepata maelezo juu ya kuzitumia namba hizo za utambulisho wa wafanyabiashara’’ amesema Kayombo.


Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo akizungumza na Blogu ya Jamii ya Michuzi juu ya uhakiki wa Tin Namba leo jijini Dar es Salaam. 


 
Sehemu baadhi ya wananchi wakiwa katika uhakiki wa TIN namba leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii).

Usajili Kili Marathon kufanyika Mlimani City jijini Dar

$
0
0
Usajili wa mbio maarufu za Kilimanjaro Marathon sasa utaanznia jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mlimani City, imefahamika.

Muandaaji mkuu na muanzilishi wa mbio hizo, John Addison alisema usajili huo utaania Mlimani City na hii itakuwa mara ya kwanza kwa zoezi hilo kufanyika jIjini Dar es Salaamtangu kuanzishwa kwa mbio hizo miaka 15 iliyopita.  

Alisema usajili huo utafayika Februari 18 na 19 eneo la kuegesha magari mbele ya mgahawa wa Grano pembeni ya KFC kuanzia saa nane mchana hado saa mbili usiku. “Tunaamini watu wengi watajitokeza kwa sababu itakuwa mwishoni mwa wiki,” alisema na kuongeza kuwa hii itapunguza msongamano wa usajili Mjini Moshi.
Meneja Mkuu wa Mlimani City, Pastors Mrosso alisema wanajivunia kuwa wabia wa Kilimanjaro Marathon ambazo kwao ni mbio kubwa na wanaamini watu wengi watajitokeza kujisajili na pia kutembelea maduka mbalimbali na kupata huduma kutoka Mlimani City.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli ambaye ni mdhamini mkuu aliwapongeza waandaaji kwa kuanzisha usajili wa Dar es Salaam na kusema itarahisisha zoezi zima na kuhakikisha kila mtu anasajiliwa kwa wakati na kuepusha msongamano wa watu siku za mwisho.

Umie Naye Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini, George Lugata aliwataka washiriki wote watumie fursa hii vizuri ili waweze kushiriki katika mbio hizi.
Kwa mujibu wa Bw. Addison, Usajili Arusha utafanyika Kibo Palace Hotel Februari 21 na 22 kuanzia saa nane mchana hadi saa mbili usikuna Moshi usajili utafanyika Keys Hotel  Februari 23 (saa sita mchana hadi saa kumi na moja jioni), Februari 24 (saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni) na Februari 25 (saa tatu asubuhi hadi saa sita mchana).

“Tumeongeza siku za usajili kwa vituo vyote ili watu wengi zaidi watumie fursa hii na kuepusha msongamano wa watu Mjini Moshi tunawaomba washiriki wote watambue kuwa safari hii usajili utafungwa mapema kabisa kwani hakuna usajili utaendelea baada ya saa sita mchana Februari 25,” alisema Bw. Addison.
Wadhamini wa mbio za mwaka huu ni Kilimanjaro Premium Lager-42km, Tigo 21km, GAPCO 10 km-walemavu, Grand Malt-5km. Wengine ni KK Security, TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile, Rwandair, Keys Hotel and new sponsors Anglo Gold Ashanti na KNAUF Gypsum.

Mbio za mwaka huu zitafanyika Februari 26 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kuanzia saa kumi na mbili asubuhi 

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UFARANSA NCHINI NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA CUF PROFESA LIPUMBA KWA NYAKATI TOFAUTI JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak (kushoto), ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza kwa makini Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak wakati wa mazungumzo yao yaliofanyika ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba alipomtembelea ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.


SHIRIKISHO VYUO VYA ELIMU YA JUU-CCM, LAWATAKA VIJANA KUZIDISHA UADILIFU NA UZALENGO KUKIDHI LENGO LA RAIS DK. MAGUFULI

$
0
0
Shirikisho la vyuo vya Elimu ya Juu nchini, limewahimiza Vijana kuzidisha uadilifu na uzalendo ili kufikia malengo yatakayoakisi CCM mpya na Tanzania mpya, kama anavyotaka Mwenyekiti wa Chama, Rais John Magufuli.

"Ili matakwa haya ya Rais wetu na Mwenyekiti wa Chama, yaweze kufikika, ni lazima  Watanzania  hasa sisi vijana, tubadilike, kifikra na kimtazamo na kuacha kufanya kazi kwa mazoea", alisema Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho hilo, Daniel Zenda, wakati wa kufungwa kambi maalum ya siku tatu ya Vijana kutoka  vyuo mbalimbali, nchini, jana, Hombolo, mkoani Dodoma.

Zenda alisema, mabadiliko ya kifikra, mtazamo na kiutendaji, ndivyo vitakavyoonyesha udhati wa vijana na Watanzania kwa jumla katika kuendelea kumuunga mkono, Rais Dk. Magufuli, katika jitihada zake za kuiletea Tanzania mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutendaji kwa kushika misingi ya kuinua uchumi huku akipambana na uzembe na ubadhirifu.

Zenda, aliwapongeza vijana 219, walioshiriki katika kambi hiyo, akisema, mafunzo ya ukakamavu na yale ya kujenga utaifa, waiyopata kwa muda wa siku tatu hadi kufikia jana, yatawasaidia sana, katika kutambua nafasi yao katika kulitumikia taifa kwa uadilifu na uzalendo mkubwa.

Aliwataka Wanashirikisho la vyuo vya Elimu ya Juu katika mikoa mbalimbali kuendelea kufanya shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwa ni kutekeleza maagizo  yanayotaka kila mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhakikisha anashiriki shughuli kama hizo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa kwa CCM.

Zenda aliipongeza Viongozi wa Shirikisho katika baadhi ya mikoa ikiwemo Dar es Salaam, Mbeya, Arusha na Dodoma ambao tayari wamekuwa wakishirikiachama na wanachama na wananchi kwa jumla katika kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kufanya usafi na kujitolea damu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo ya miaka 40 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 5, 2017.

Kambi hiyo ya Hombolo ilifungwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainabu Abdalla Issa, ambaye akifunga kambi hiyo alisema, kwa kuwa CCM imekuwa ikionyesha kuwajali vijana kwa kuweka mipango mbalimbali ya kuwaendeleza sambamba na watanzania wengine, basi hawana budi nao kuhakikisha CCM inazidi kuimarika na kuwa CCM mpya.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu, Daniel Zenda akizungumza wakati wa kufungwa Kambi ya Vijana 219,  waliokuwa katika kambi ya kukuza Uzalendo, iliyowekwa Hombolo mkoani Dodoma.
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu, Mkuu wa Wilaya ya Pangani mkoani Tanga, Zainabu Abdallah Issa, akizungumza wakati wa kufunga Kambi ya Vijana 219 wa Shirikisho hilo, jana, Hombolo mkoani Dodoma.
 Vijana walioshiriki Kambi wakiwa ukumbini
 Baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu, wakiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula alipotembelea kambi ya Vijana 219 wa Shirikisho hilo, Hombolo mkoani Dodoma. Kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho hilo Daniel Zenda

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MARAIS MBALIMBALI WA AFRIKA KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRIKA (AU) MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA

$
0
0
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kwenye mazungumzo yake pamoja na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Akinwumi Adesina mara baada ya kumaliza mazungumzo yao mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao rasmi katika moja ya Ofisi za AU mjini Addis Ababa Ethiopia.

NBC yawapongeza wafanyakazi wake bora

$
0
0
 Mkuu wa Idara ya Mauzo wa NBC, Mongateko Makongoro (mwenye suti nyeusi) akipiga picha ya pamoja na washindi wa tuzo ya utoaji wa mikopo binafsi walioingia kwenye Kundi la Watu Mashuhuri wa NBC lijulikanalo kama ‘ ‘Kundi la Shilingi Billioni Moja’. Tuzo hizo zilitolewa kwenye sherehe maalum ya kuwatunuku watumishi bora kwa mwaka 2016.Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Huduma Reja Reja za Kibenki wa NBC, Filbert Mponzi (wa tatu kushoto), akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi bora waliofanya vizuri katika mwaka 2016 walio chini ya kurugenzi yake, katika sherehe maalum ya kuwatunuku watumishi bora kwa mwaka 2016. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
 Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Corporate, Mariam Kombo (kushoto), akionyesha cheti alichotunukiwa mara baada ya kutangazwa meneja bora wa mwaka 2016 kutokana na utendaji wake mahiri katika sherehe maalum ya kuwatunuku watumishi bora. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma Rejareja za Kibenki wa NBC, Filbert Mponzi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.  
 Meneja wa amana za wateja NBC, Dorothea Mabonye (kushoto), akikabidhi kombe la ushindi kwa Meneja wa Tawi la NBC Sea Cliff baada ya tawi hilo kuibuka kidedea katika kutoa huduma za kibenki kwa wateja wa akaunti ya malengo kwa mwaka 2016 . Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
  

MAGAZETI YA LEO JUMATANO FEBRUARY 1, 2017

MGODI WA BUZWAGI WALIPA KODI ZAIDI YA MIL 700 KWA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA

$
0
0
HALMASHAURI ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga imepokea kiasi cha Sh Mil 700,040,000 kutoka kwa kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ikiwa ni sehemu ya kodi ya huduma (service levy) ya kipindi cha mwezi Julai na Desemba 2016.

Kiasi hiki ni zaidi ya kilichotolewa kipindi cha Julai na Desemba mwaka 2015 ambapo mgodi huo uliikabidhi halmashauri ya mji wa Kahama hundi yenye thamani ya kiasi cha sh Mil 500,088,000 kama kodi ya huduma ikiwa ni utekelezaji wa sheria kwa kulipa kodi zilizopo kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Hundi ,Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo alisema Buzwagi inamatumaini makubwa kuwa katika siku za karibuni halmashauri itaanza kutekeleza mradi huo na hivyo kutoa matumaini kwa wananchi wa Kahama kupata huduma nzuri za afya ndani ya wilaya.

“Mpaka sasa kama Kampuni tumekwisha kabidhi kwenu takribani kiasi cha bilioni 1.4 hii ikiwa na maana ya kodi yote ya ushuru wa huduma katika kipindi cha mwaka 2016, wananchi wangetamani kuona mradi huu unaanza maana kiasi hicho kilichopo kama kitatumika kinaweza kutekeleza sehemu kubwa ya mradi huu kwa kuanzia wakati tukisubiri awamu zingine” alisema Mwaipopo.

Katika hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika katika viwanja vya makazi ya viongozi katika wilaya hiyo,Mwaipopo alisema licha ya Kampuni yake kulipa kodi mbalimbali bado imekuwa ikijishughulisha katika kuhakikisha inakuwa mdau muhimu wa maendeleo kwa kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yanayozunguka Mgodi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Fadhili Nkurlu aliyepokea hundi hiyo kutoka kwa uongozi wa Buzwagi na baadae kuikabidhi kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama ameupongeza uongozi
wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanalipa kodi mbalimbali pamoja na jushirikiana na Jamii katika kutekeleza miradi mbalimbali.

Alisema Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi umeekua mstari wa mbele katika kulipa kodi mbalimbali ambako mpaka kufikia sasa zimefikia zaidi ya shilingi bilioni 197 ambazo zimetolewa katika vipindi tofauti.

Akizungumzia matumizi ya pesa hizo katika kutekeleza mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kahama Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kahama Anderson Msumba alisema halmashauri iko katika hatua za mwisho za utekelezwaji wa ujenzi huo.

Miloni 700,040,000 zilizotolewa zinafanya juma ya pesa zote zilizotolewa katika vipindi vya miaka miwili kufikia Bil 1.2 fedha ambazo zitasaidia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ukiwemo wa Afya.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo(wa pili kutoka kulia) na Meneja Uendelevu wa Mgodi wa Buzwagi ,George Mkanza wakikabidhi hundi ya kodi ya huduma ya zaidi ya Sh Mil 740 kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama ,Fadhili Nkurlu(wa pili toka kushoto) tukio lililofanyika juzi mjini Kahama ,Wa kwanza kushoto ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kahama Bi Marry Manyambo.
Mkuu wa Wilaya Kahama,Fadhili Nkurlu na akimkabidhi hundi iliyotolewa na Mgodi wa Buzwagi kama Kodi ya Huduma yenye thamani ya zaidi ya Sh Mil 740 , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa hospitali kubwa ya wilaya ya Kahama, mradi ambao ujenzi wake utategemea fedha zinazotokana na kodi za ushuru wa huduma unaolipwa na Mgodi huo.
Baadhi ya waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama wakifuatilia hafla ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya mji wa Kahama.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo akiwahutubia waheshimiwa madiwani wa halmashauri ya Kahama pamoja na wadau mbalimbali waliohudhuria hafla ya kukabidhi hundi kwa halmashauri ya Mji wa Kahama
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (aliyesimama) akihutubia wageni waalikwa wakati wa hafla ya kupokea hundi ya ushuru wa huduma kutoka Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi. Kutokea kushoto waliokaa ni Katibu
tawala wa wilaya Kahama Timothy Ndanya na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo.
Mkuu wa wilaya Kahama na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi wakiteta jambo.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images