Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1540 | 1541 | (Page 1542) | 1543 | 1544 | .... | 3283 | newer

  0 0

  East African Court of Justice, Arusha, 31st January 2017The First Instance Division on Friday 3rdFebruary 2017, will deliver a judgement in the case filed by Hon. Margaret Nantongo Zziwa versus the Secretary General of the East African Community. Hon. Zziwa’s case alleges that the process of her removal from the Office of EALA Speaker was illegal and an infringement of Articles 53 and 56 of the Treaty for the Establishment of the East African Community. 
  Hon. Zziwa (pictured) was the then elected Speaker of the EALA, after her impeachment, the Assembly elected Hon. Daniel Kidega as the Speaker for  EALA up to date.

  The Court heard the court oral evidence from witnesses for both parties’ witnesses (the Applicant and Respondent) from 26th to 29th July 2016. Also court heard oral highlights of written submissions by counsels for the parties on 21st November 2016 that concluded the hearing of the case. The judgement will be delivered by the Honourable Judges of the First Instance Division; these are; Lady Justice Monica Mugenyi (Principal Judge), Justice Isaac Lenaola (Deputy Principal Judge), Dr. Justice Faustin Ntezilyayo, Justice Fakihi A. Jundu and Justice Audace Ngiye. 
  On 15th February, the Appellate Division will also resume sessions which will go up to 28th February 2017. Only four appeals will come up before the Court for scheduling conferences and hearing. All appeals will be brought before the Honourable Judges of the Appellate Division; Dr. Justice Emmanuel Ugirashebuja (President), Justice Liboire Nkurunziza (Vice President), Justice Edward Rutakangwa, Justice Aaron Ringera, and Geoffrey Kiryabwire. 
  On 28th February the First Instance Division, will again continue with the sessions up to 30th March 2017. A number of cases will come up for hearing, scheduling conferences and delivery of rulings and Judgments. These include; 5 hearings, 4 scheduling conferences, 2 rulings, 1 Judgement and other 2 matters. 
  The Court seats for a month every quarter due to the ad-hoc nature service of the Judges. Currently the President and the Principal Judge of the court are the only resident Judges in Arusha, other Judges come only when there are sessions or other court business. 
  All matters will be in open Court 2nd Floor EACJ wing

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe amekabidhi Tuzo na Hati za Pongezi kwa Viongozi wa Mikoa ya Iringa na Njombe kwa kufaikisha na kutekeleza kikamilifu Mpango wa Usajili na kutoa Vyeti vya Kuzaliwa kwa Watoto walio na Umri chini ya Miaka Mitano uliozinduliwa katika Mikoa hiyo tarehe 22 Septemba 2016. 

  Tuzo hizo zimetolewa kwa Halmashauri 11 za Wilaya na Miji, Ofisi za Wakuu wa Wilaya 7 na Ofisi za Wakuu wa Mikoa 2 kwa kuweza kusajili na kuwapa vyeti vya kuzaliwa kwa asilimia 100 hivyo kuvuka lengo lililokuwa limewekwa. Usajili kupitia mfumo huu ulifanyika kwa kutumia Ofisi za Watendaji Kata na Vituo vya Tiba vinavyotoa Huduma ya afya ya mama na mtoto. Hafla ya kukabidhi tuzo ilifanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Njombe.
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mikoa ya Iringa na Njombe mara baada ya kukabidhi tuzo za pongezi kwa kufanikisha Mpango wa Usajili na Kutoa Vyeti vya kuzaliwa kwa watoto. Viongozi wengine (waliokaa) kuanzia kulia ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Iringa Mhe. Mary Shangali, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bi. Emmy Hudson. Waliosimama ni Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Iringa na Njombe.
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe amekabidhi Tuzo na Hati za Pongezi kwa Viongozi wa Mikoa ya Iringa na Njombe kwa kufaikisha na kutekeleza kikamilifu Mpango wa Usajili na kutoa Vyeti vya Kuzaliwa kwa Watoto walio na Umri chini ya Miaka Mitano uliozinduliwa katika Mikoa hiyo tarehe 22 Septemba 2016. Tuzo hizo zimetolewa kwa Halmashauri 11 za Wilaya na Miji, Ofisi za Wakuu wa Wilaya 7 na Ofisi za Wakuu wa Mikoa 2 kwa kuweza kusajili na kuwapa vyeti vya kuzaliwa kwa asilimia 100 hivyo kuvuka lengo lililokuwa limewekwa. Usajili kupitia mfumo huu ulifanyika kwa kutumia Ofisi za Watendaji Kata na Vituo vya Tiba vinavyotoa Huduma ya afya ya mama na mtoto. Hafla ya kukabidhi tuzo ilifanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Njombe.
  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka akionesha tuzo aliyokabidhiwa kutokana na Mkoa wake kufanikisha kusajili watoto kwa asilimia mia moja. Wengine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza.

  0 0

  Mahojiano maalumu ya TBC na Spika wa Bunge Job Ndugai kuhusiana na vikao vya bunge la sita vinavyoanza hii leo mjini Dodoma.Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Presidents H.E. Dr John Pombe Magufuli (Tanzania) and H.E. Uhuru Kenyatta(Kenya) chat with President of African Court  of Justice Sylvain Ore (2nd left) and Justice Ben Kioko (Vice President, third left) on the side-lines of the AU Summit in Addis Ababa, Ethiopia,  yesterday. State House Photo.

  0 0

  Promosheni ya ‘Nogesha Upendo’ iliyozinduliwa mwezi uliopita imemalizika leo ambapo imewawezesha  watumiaji  wengi wa mtandao huo kujishindia fedha taslimu na vifurushi vya muda wa maongezi na intanenti.

  Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu,amesema kuwa promosheni hiyo imekuwa na mafanikio makubwa na kufanikisha lengo lililokusudiwa na kuwapa watumiaji wa mtandao huo zawadi ya kipekee.

  “Hadi kufikia sasa  wateja wapatao 400  wameweza kujishindia fedha taslimu shilingi milioni 1/-kila mmoja na wateja zaidi ya 1,200 wamejishindia fedha taslimu shilingi laki 1/-kila mmoja na wapo maelfu ya wateja ambao wamezawadiwa dakika za muda wa maongezi na MB za intanenti bure”.Alisema Nkurlu.

  Alisema Vodacom inayo furaha kuona promosheni hii imewezesha maisha ya wateja wake kuwa murua na itaendelea kubuni promosheni nyingine zenye lengo la kubadiilisha maisha ya wateja nahuduma mbalimbali za kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa kidigitali.

  ”Tunawashukuru sana wateja wetu wote walioshiriki katika promosheni hii kwa kuendelea kuwa katika familia ya Vodacom na tunawaahidi kuendelea kuwapatia huduma bora wakati wowote na mahali popote.
  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuchezesha droo ya mwisho ya Promosheni ya”Nogesha Upendo”jana jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya washindi 400 wamejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 1/-kila mmoja na zaidi ya wateja 1200 wamejishindia shilingi laki 1 kila mmoja kupitia promosheni hiyo iliyofikia tamati jana ambayo iliwawesha wateja wa kampuni hiyo kuzawadiwa dakika za muda wa maongezi, MB za intanenti bure na fedha taslimu pindi wakijiunga na kifurushi chochote cha mtandao huo,Kushoto ni Afisa Masoko wa kampuni hiyo,Mosi Nassoro.

  0 0

  Matokeo ya Kidato cha nne kwa wananfunzi waliohitimu mwaka 2016, yametangazwa wakeza kuyaona kwa KUBOFYA HAPA


  0 0

  BAADA ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, kuanza rasmi mazoezi jana jioni kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Ndanda, daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa, amezungumzia hali za kiafya za baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi.

  Wachezaji wa Azam FC waliokuwa majeruhi ni nahodha John Bocco ‘Adebayor’, Stephan Kingue waliopata majeraha ya misuli ya paja kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Simba, ambao matajiri hao walishinda bao 1-0 lililofungwa na Bocco.

  Wengine wanaouguza majeraha, ambao waliukosa mchezo huo ni kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, kipa Mwadini Ally (nyama za paja) na beki Shomari Kapombe, ambaye ni mgonjwa lakini hivi sasa akiendelea vema.

  Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz mara baada ya mazoezi ya jana, Mwankemwa alisema kuwa Bocco na Kingue watakaa nje ya dimba kwa muda wa wiki mbili tokea jana, huku Sure Boy akitarajiwa kuanza rasmi mazoezi leo na Mwadini akipumzishwa kwa siku tatu kuanzia jana.

  “Bocco hali yake inaonekana kuimarika vizuri tokea alipopata majeraha hayo ya kuchana msuli wa nyuma ya paja, Stephan (Kingue) kwa upande wake naye amechana msuli wa mbele ya paja, hivyo wote watakaa nje ya dimba kwa muda wa wiki mbili kutoka sasa (jana) na wataanza mazoezi mepesi baada ya wiki moja,” alisema.

  Daktari huyo bingwa mzoefu, alisema hali za wachezaji wengine ziko vizuri kabisa kuendelea na mikikimikiki ya maandalizi kuelekea mechi zijazo za ligi pamoja na michuano mingine.

  0 0

  KASULU – Baadhi ya wakimbizi wanaoishi katika Kambi ya Nyarugusu, Magharibi mwa Tanzania wameanza kupokea fedha taslimu kutoka Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) katika hatua za awali za kubadilisha mfumo wa sasa wa kuwapatia chakula kila mwezi. 

  Wakimbizi wapatao 10,000 sasa wanapokea fedha taslimu kama sehemu ya mradi wa majaribio wa miezi mitatu. Mradi huu unafadhiliwa na nchi ya Canada kupitia mchango wake wa Dola za Canada 500,000 (Dola za Marekani 385,000) kwa WFP.

  WFP itatoa Shilingi za Tanzania 10,000 (Dola za Marekani 4.50) mara mbili kwa mwezi kwa kila mwanakaya wa kaya iliyo katika mradi wa majaribio. Fedha itatumwa kwa mlengwa kupitia mtandao wa simu. Katika kipindi chote cha mradi, wakimbizi wataendelea kupata mgao wa mafuta ya kupikia yalioongezewa virutubisho na mchanganyiko maalumu wa uji wakati ambapo badala ya mahindi, kunde na chumvi wanufaika watapewa fedha taslimu.
  Utoaji wa fedha taslimu unawapa wakimbizi uhuru wa kuchagua chakula gani cha kununua na wakati huohuo kuingiza fedha katika uchumi wa ndani. Soko la Pamoja la Nyarugusu, lililofunguliwa mwaka huu, ni eneo huru kati ya kambi na jamii ya wenyeji, ambako wafanyabiashara wanapata nafasi ya kuwauzia wakimbizi bidhaa zao.

  “Canada inafurahi kusaidia shughuli za WFP za kuhudumia wakimbizi nchini Tanzania,” alisema Mheshimiwa Ian Myles, Balozi wa Canada nchini Tanzania. “Kuunganisha msaada wa chakula na fedha taslimu kunawapa wanawake na wanaume uhuru zaidi katika kukidhi mahitaji yao na kunaweza kuwa na matokeo mazuri kwa jamii ya wenyeji.”

  Zaidi ya wakimbizi robo milioni wamepata hifadhi nchini Tanzania katika kambi tatu magharibi mwa nchi. Wakimbizi nchini Tanzania, hususan kutoka katika nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, wanategemea sana msaada wa WFP kama chanzo chao kikuu cha chakula.
  Kabla ya kuanza kwa mradi wa majaribio wa fedha taslimu, wakimbizi walikuwa wakipokea msaada wa chakula tu kutoka WFP. Kwa ushirikiano wa karibu na Serikali ya Tanzania, Shirika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na washirika wengine, mradi wa majaribio wa fedha taslimu unasaidia baadhi ya kaya zilizo hatarini zaidi za wakimbizi katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu.

  “Kutoa fedha taslimu kwa wakimbizi kunawajengea uwezo wa kufanya uaumzi wao kuhusu chakula kipi wanunue na kupika nyumbani,” alisema Michael Dunford, Mwakilishi wa Nchi wa WFP Tanzania. “Fedha taslimu huwapa wakimbizi fursa ya kula vyakula tofautitofauti, na hivyo kuwasaidia kubadili mlo wao.” 

  WFP inalenga kuongeza idadi ya wakimbizi wanaopokea fedha taslimu badala ya masaada wa chakula katika mwaka wa 2017.
  Tangu kuanza kwa machafuko ya kisiasa nchini Burundi mwezi Aprili, 2015, takribani Warundi 190,000 wametafuta hifadhi nchini Tanzania. Kwa kuunganisha na idadi ya wakimbizi waliokuwepo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Tanzania hivi sasa inahifadhi zaidi ya wakimbizi robo milioni. Mamia ya wakimbizi wanaendalea kuwasili kila siku kutoka Burundi. 

  WFP inahitaji takribani Dola za Marekani milioni 6 kwa mwezi ili kuendelea kuwasaidia wakimbizi katika mwaka 2017 ambao idadi yao inaendelea kuongezeka. 

  0 0


  Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa, MB. anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye harambee iliyoitishwa na Shirika lisilo la kiserikali la Land O’Lakes ikilenga kukusanya fedha kwa ajili ya uwezeshaji wa wanawake katika kilimo hasa kilimo biashara nchini kupitia taasisi iliyojikita kwenye kuendeleza wanawake katika kilimo Tanzania (CAWAT).

  Akizungumza na waandiishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Mradi wa Ubunifu  Katika Maswala ya Kijinsia na Kuimarisha Uhakika wa Chakula Katika Ngazi ya Kaya, unaoendeshwa na Land O Lakes, na kufadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Watu wa Merekani (USAID),  Dk Rose Kingamkono, alisema katika harambee hiyo Waziri Mkuu Majaliwa,ataungana na wageni waalikwa wengine zaidi ya 200 na kwamba zaidi ya sh milioni 150 zinatarajiwa kukusanywa.

  Alisema lengo la harambee hiyo inayotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Februari 17 mwaka huu ikiwa na kauli mbiu “WEZESHA KILIMO BIASHARA ILI KUKUZA  AJIRA, JAMII NA VIWANDA ENDELEVU” ni kukusanya kiasi hicho cha pesa kitakachosaidia kuijengea uwezo wa kiutendaji taasisi hiyo mpya ya CAWAT iliyoanzishwa mahususi kusimamia programu endelevu katika kumnyanyua mwanamke kupitia kilimo chenye tija na ufanisi.

  “Mwanamke akijengewa uwezo  wa kufanya shughuli za uzalishaji mali kwa ufanisi atakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha  ustawi wa familia na jamii kwa ujumla, huku pia akiondoa kabisa tatizo la upungufu wa chakula na lishe duni katika kaya zetu na hayo ndio malengo ya kuanzishwa kwa CAWAT tunayoipigania sasa.

  “Tafiti zimeonyesha kwamba uchumi ulioshikiliwa mikononi mwa mwanamke huelekeza matumizi yake kwa ajili ya ustawi wa familia zaidi kuliko ilivyo kwa uchumi ulioshikiwa mikononi mwa mwanaume’’ alisema.

  Alisema taasisi hiyo ya CAWAT kwa sasa ipo kwenye mchakato wa awali wa kuanza kujitegemea yenyewe kiuendashaji bila kutegemea msaada iliyokuwa ikiupata kutoka kwenye mradi  unaohusu ‘Ubunifu katika masuala ya kijinsia na kuimarisha uhakikaka wa chakula katika ngazi ya kaya (Innovations in Gender Equality (IGE), to Promote Household Food Security  unaotarajiwa kuisha Machi  mwaka huu.

  “Kuelekea katika kujiendesha yenyewe bila kutegemea msaada inayoupata kutoka mradi wa IGE, taasisi hii ya CAWAT bado ina safari ndefu inayohitaji msaada kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo ili iweze kutimiza wajibu wake wa kuwasaidia wakina mama walio kwenye sekta hii muhimu ya uzalishaji. Tunawaomba sana  watanzania mmoja mmoja, taasisi, mashirika, balozi mbalimbali waguswe katika kusaidia hili.’’ Alisema.

   Mkurugenzi wa Mradi wa Ubunifu  Katika Maswala ya Kijinsia na Kuimarisha Uhakika wa Chakula Katika Ngazi ya Kaya, unaoendeshwa na taaisisi ya Land O Lakes, na kufadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Watu wa Merekani (USAID),  Dk Rose Kingamkono (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na harambee iliyoitishwa na taasisi hiyo ikilenga kukusanya fedha kwa ajili ya uwezeshaji wa wanawake katika kilimo biashara  kupitia taasisi iliyojikita kwenye kuendeleza wanawake katika kilimo Tanzania (CAWAT). Wengine ni maofisa wa taasisi hiyo.  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

  BOTI ya mizigo iliyokuwa ikitokea Kigoma kuelekea Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ya Kalemi, imepotea katika ziwa Tanganyika ikiwa na Watu sita pamoja na Shehena ya vitungu gunia 110, ngano mifuko180 ,Mafuta ya taa dumu 20 na kreti za soda 70  ambayo mpaka sasa haijulikani ilipo.

  Akizungumza na Wanahabari Mkoani humo kamanda wa polisi  Mkoa wa Kigoma Fredinandi Mtui alisema Mnamo tarehe 23 januari majira ya saa 16:30 jioni boti iliyotengenezwa  kwa mbao MV.Ngendo ya Buchuma, boti ya mizigo inayo milikiwa na  Mussa Hamisi Mkazi wa ujiji Kigoma Manispaa ,iliondoka  Katika Bandari ya Kibirizi ikiwa na shehena ya vitunguu, Ngano na watu sita kuelekea Congo ambayo mpaka sasa haijafika Congo na haijulikani ilipo.

  Mtui alisema mpaka sasa boti hiyo haijulikani ilipo na hakuna chochote kilicho onekana kati ya mizigo wala abiria Waliokuwa wamepanda katika boti hilo, Askali wanamaji wakishirikiana na Chama cha Wamiliki wa maboti Wanaendelea na taratibu za kuitafuta boti hiyo inasemekana imepotelea maji ya Kongo.

  Alisema kumekuwa na taarifa zilizo kuwa zikizungumzwa mitaani kwamba  kunamiili imeonekana, taarifa hizo sio za kweli hadi sasa hawajajua kama watu hao watakuwa hai au wamekufa maji, tumewasiliana na Watu waliopembezoni mwa ziwa Tanganyika hawajaona kitu chochote hadi sasa , aliwataka Wananchi kuwa na subira kuweza kutambua kama watakuwa salama au wamekufa.

  "Baada ya kupata taarifa kuhusu  Boti hiyo iliyokuwa ikielekea Congo kwamba haijafika kwa Muda ulio takiwa,Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wamiliki wa Maboti walianza jitihada za kuitafuta boti hiyo maeneo ya mwambao mwa ziwa Tanganyika, na hatujapata taarifa yoyote ambapo ingekuwa imezama mizigo iliyo kuwemo katika boti hiyo ingekuwa imeanza kuelea, tumewasiliana na  Mikoa baadhi ambayo ziwa Tanganyika limepita pamoja na Nchi za Burundi na Congo kupitia ubalozi mdogo waweze kutujulisha endapo wataiona boti hiyo",alisema Mtui.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba alipomtembelea ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.


  0 0

  Serikali ya Ufaransa kupitia Benki ya Maendeleo ya Nchi hiyo (AFD) imeahidi kuwa inampango wa kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu kutoka wastani wa euro milioni 50 hadi euro milioni 100 kwa mwaka katika miaka ijayo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

  Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Malika Berak ametoa kauli hiyo Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokutana na Kufanya mazunguzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhusu hatua zilizofikiwa katika uandaaji wa kongamano la uwekezaji litakalofanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.

  Balozi huyo amesema mkopo huo itaiweza na kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi hasa katika sekta za maji na usafi wa mazingira na miradi ya umeme. Kuhusu uandaaji wa kongamano la uwekezaji nchini, Balozi Malika Berak amemweleza Makamu wa Rais kuwa maandalizi ya kongamano hilo kubwa la Kibiashara linalolenga kujenga na Kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Ufaransa yanakwenda vizuri.

  Balozi huyo amesema kuwa kongamano hilo ambalo litakuwa la Kikanda litajadili kwa kina fursa za uwekezaji hapa nchini hasa kwenye maeneo ya nishati, usafirishaji, teknolojia ya habari na Mawasiliano na miradi ya maendeleo.

  Balozi Malika Berak amemhakikishia Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kuwa kongamano hilo la kibiashara litawakutanisha pamoja wafanyabiashara Watanzania na wenzao wa Ufaransa katika kujadili na kubadilisha uzoefu katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kibiashara kama hatua ya kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.

  Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameipongeza Serikali ya Ufaransa kupitia kwa balozi wake hapa nchi kwa ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika sekta ya maji na usafi wa mazingira, nishati na mapambano dhidi ya umaskini nchini.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Balozi wa Ufaransa hapa nchini Malika Berat kuwa Tanzania itaendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano yaliyopo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande Mbili yaani Tanzania na Ufaransa.

  Makamu wa Rais pia amepongeza jitihada za Serikali kupitia Ubalozi wake hapa nchini za kuona umuhimu wa kuandaa Kongamano la kibiashara hapa nchini ambalo litatoa fursa kubwa kwa watalaamu wa sekta mbalimbali nchini kukutana na kujadiliana mambo kadhaa ikiwemo fursa za uwekezaji nchini.

  Amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakt John Magufuli inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini kwa kupambana na vitendo vya rushwa kama hatua ya kuhamasisha wawekezaji wengi kuja kuwekeza hapa nchini.

  Makamu wa Rais amemweleza Balozi wa Ufarana hapa nchini kuwa milango ya ofisi yake ipo wazi muda wote hivyo kama watakwama sehemu yeyote katika kuandaa kongamano hilo amfahamishe haraka ili aweze kuchukua hatua haraka kusaidia mchakato huo kutokana na muhimu wa kongamano hilo hasa wakati huu ambapo Tanzania inataka kujenga uchumi wa viwanda nchini.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak (kushoto), ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akimsikiliza kwa makini Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak wakati wa mazungumzo yao yaliofanyika ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake,  Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa(MB) akimsikiliza Mbunge wa Iramba Mashariki Mheshimiwa Allan Kiula wakati walipo kutana katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma Waziri Mkuu yupo Mkoani Dodoma katika kushiriki Mkutano wa Sita wa Bunge la Kumi na moja amabao umeanza leo Tarehe 31 January 2017

  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0  Na.Vero Ignatus, Arusha.


  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mashaka Mrisho Gambo amefungua Kongamana kutoa taarifa ya maendeleo katika mkoa wa Arusha ambapo kongamano hilo limewashirikisha wadau wa habari katika kuangalia na kutafakari na kupitia pamoja na kuangalia mpango mkakati wa maendeleo katika mkoa.

  Gambo amesema kuwa kongamano hilo lina lengo la kutoa mrejesho kwa Watanzania kupitia waandishi kwa kipindi cha miezi sita ,na kuangalia mambo gani serikali ikiyapa kipaumbele itaondoa changamoto mbalimbali katika jamii kwa ujumla.

  Aidha amesema kuwa utekelezaji wa shughuli za kiserikali katika mkoa wa Arusha kwa kipindi cha miezi sita hadi kufikia desemba 2016 umekuwa na mafanikio makubwa ,ambapo amesema kuwa hii ni kutokana na utamaduni wa kufanya na kutekeleza majukumu ya kazi kwa vitendo.

  Amesema utekelezaji huo umechangia katika kuboreka kwa maeneo mbalimbali ya sekta muhimu katika kukuza uchumi katika mkoa hasa pato la mkoa na wananchi moja kwa moja.

  “Katika kipindi hiki,miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa na kupewa kipaumbele cha kutosha hivyo kwa namna moja kutekeleza mkakati wa Taifa wa kukuza uchumi na kuondoa umaskini (MKUKUTA II)katika mkoa na taifa kwa ujumla”alisema Gambo.

  Amesema kuwa Mkoa umesimamia utekelezwaji wa shughuli za serikali na kushuhudia mafanikio katika sekta zakilimo,afya,maji,barabara,mofugo,maliasili na nyinginezo kama takwimu zilivyowasilishwa .Amesema kuwa serikali imejipanga kuhangaika na wale wote ambao wanachochea migogoro kwa wananchi na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi hatutawafumbia macho.

  Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akiingia ukumbini tayari kwa kuanza rasmi kwa kongamano na waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa maendeleo katika mkoa wa Arusha.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika kongamano hilo lililoitishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha ili kuangalia na kujadili maendeleo ya mkoa kwa ujumla.
  Wa kwanza kushoto ni mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi Mussa Juma ,akifuatiwa na Omary Moyo wakiwa katika kongamano hilo.
  Mgeni rasmi mkuu wa mkoa pamoja na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari waliohudhuria kongamano hilo.Picha na Vero Ignatus Blog.


  0 0

  Katika swala zima la kumkomboa mwanamke mjasajiriamali, Benki ya KCB Tanzania inaendelea na programu ya mafunzo kwa ajili ya wanawake wajasiriamali yanayoitwa 2JIAJIRI. Programu hii inalenga kumkomboa mwanamke mjasiriamali kutoka katika changamoto zinazosababisha biashara yake ishindwe kuendelea.

  Benki ya KCB imepanga kufundisha wanawake wajasiriamali 315 kutoka mikoa ya Dar Es salaam, Mwanza, Morogoro, Arusha, Moshi na Zanzibar ambapo matawi ya benki hiyo yapo.

  Mafunzo haya ni bure kabisa, benki ya KCB inagharimia gharama zote. na yanahusisha Elimu ya Fedha (Financial Literacy), Kufikiwa huduma za kifedha (Financial Inclusion), Masuala ya Kisheria (Legal Framework), Ushindani wa Kibiashara (Business Competitiveness) na kuwa na sifa za kukopesheka (How to be bankable).

  Zaidi ya mafunzo hayo, benki ya KCB itawapatia wanawake wajasiriamali hao maafisa watakao wafundisha kwa vitendo kwenye maeneo ya biashara zao. Maafisa hao watakua ni afisa fedha, afisa sharia na afisa masoko.

  Kwako mwanamke mjasiliamali “JIULIZE KWANINI uhangaike wakati benki ya KCB tupo!”
  Meneja wa kanda ya kaskazini wa Benki ya KCB Tanzania Judith Lubuva, akiongea na wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hyo mkoani Arusha.
  Afisa Mawasiliano ya Umma wa benki ya KCB Margaret Makere akiongea na wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hiyo mkoani Arusha.

  Mwalimu wa Ujasiriamali wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Nina Nchimbi akitoa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Benki ya KCB Tanzania kwa wanawake wajasiriamali wa mkoa wa Arusha.
  Meneja wa kanda ya kaskazini wa Benki ya KCB Tanzania Judith Lubuva (aliyekaa wapili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali waliohudhuria na kumaliza mafunzo ya ujasiriamali yalitolewa na benki hiyo katika mkoa wa Arusha.

  0 0
  Dodoma, Jumanne, Januari 31, 2017:  

  Serikali leo imeainisha utekelezaji na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi katika sekta mbalimbali katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa Sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Majibu ya Serikali kwa baadhi ya hoja ni kama ifuatavyo:

                            Ujenzi Nyumba za Walimu.

  Akijibu hoja kuhusu ujenzi wa nyumba za walimu, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo, ameliambia Bunge kuwa Serikali ilitenga kiasi cha Sh. Bilioni 13.9 katika Bajeti ya mwaka huu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu wa Sekondari, na Shilingi bilioni 11.4 kwa nyumba za walimu wa Shule za Msingi.

  Aidha, Waziri Jafo ameeleza kuwa tayari nyumba 146 za walimu zimeshajengwa nchini kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari. Pia amezungumzia Serikali kuanza kulipa madeni ya walimu.

                               Ujenzi wa Viwanda Nchini

  Akijibu swali kuhusu uwekezaji wa viwanda nchini hususani mkoani Tabora ambako kuna kilimo cha Tumbaku na maeneo mengine yenye malighafi, Mhandisi Edwin Ngonyani kwa niaba ya Waziri wa Viwanda ameliambia Bunge kuwa tayari Serikali imeshafanya mazungumzo na wawekezaji kutoka Vietnam na kuzitaka Halmashauri zote nchini kuendelea kuitikia wito wa kutenga maeneo ya uwekezaji.

  “Kituo cha uwekezaji Nchini (TIC) kimepewa maelekezo maalum kunadi fursa hii kwa wawekezaji katika sekta ya tumbaku na sigara hapa nchini,” alisema Mhandisi Ngonyani ambaye pia ni Naibu Waziri, Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

                     Tupende Bidhaa Zetu.

  Akijibu hoja kuhusu bidhaa nyingi za Kenya kuingia nchini, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Suzan Kolimba amesema moja ya changamoto inazozikumba bidhaa za Tanzania ni wananchi wake kupenda vya nje.

  “Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali iliunda Kamati ya Kitaifa ya Kudhibiti na Kusimamia Uondoaji wa wa Vikwazo visivyo vya Kiforodha na kuhamasisha wafanyabiashara nchini kuzalisha bidhaa zenye ubora,” alisema.


  0 0

  Katika bajeti ya mwaka 2016/17, Serikali imetenga shilingi bilioni 13.9 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu 1,157 wa shule za msingi nchini.

  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ameyasema hayo leo, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge Viti Maalum, Mhe. Juliana Daniel Shonza juu ya mpango wa kuboresha miundombinu ya elimu vijijini kama vile nyumba za walimu pamoja na kulipa malimbikizo ya madeni ya walimu.

  “ Katika bajeti ya mwaka 2016/17, Serikali imetenga shilingi Bil. 13.9 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu 1,157 kwa shule za msingi na shilingi bilioni 11.14 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 661 kwa shule za sekondari,” alifafanua Jafo.

  Aliendelea kwa kusema kuwa, Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMESII) imekamilisha ujenzi wa nyumba 146 kati ya nyumba 183 ambazo kila nyumba wataishi walimu Sita (6 multi-unit houses).

  Aidha ameeleza kuwa ujenzi wa nyumba hizo umegharimu shilingi bilioni 21.9 ambapo nyumba 37 zinaendelea kujengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 5.5 na zinategemea kukamilika tarehe 30 Aprili, 2017.

  Kuhusu ulipaji wa madeni ya walimu, Jafo amesema kuwa Serikali imeendelea kulipa madeni kadri yanavyojitokeza na kuhakikiwa ambapo katika mwezi Oktoba, 2015 Serikali ililipa madeni ya shilingi bilioni 20.12 kwa walimu 44,700 na shilingi bilioni 1.107 zililipwa mwezi February, 2016 kwa walimu 3221.

  0 0  0 0

  Afisa Uhusiano wa Manisapaa ya Ilala Bi Tabu Shaibu akifafanua kwa waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu mikakati ya manispaa hiyo katika kuwaletea wananchi maendeleo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO bi Zamaradi Kawawa.
  Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bi Tabu Shaibu akizungumza wakati wa mkutano wa waandaishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa wananchi kulipa kodi ya mabango ili kuchochea maendeleo katika manispaa hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Sehemu ya Usalama barabarani na mabango Manispaa ya Ilala Bw. James Batinagwa.
  Mkuu wa Sehemu ya Usalama barabarani na mabango Manispaa ya Ilala Bw. James Batinagwa (kushoto)akisisitiza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) umuhimu wa kutii sheria bia shuruti kwa kulipa kodi ya mabango kwa mujibu wa sheria na kanuni.katikati ni Afisa Uhusiano wa Manispaa hiyo Bi Tabu Shaibu na kulia ni Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO bi Zamaradi Kawawa.
  Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa manispaa ya Ilala na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam ulioenga kueleza mikakati ya Manispaa hiyo katika kuwaletea wananchi maendeleo.

  (Picha na Frank Mvungi-Maelezo)

  0 0older | 1 | .... | 1540 | 1541 | (Page 1542) | 1543 | 1544 | .... | 3283 | newer