Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110095 articles
Browse latest View live

Mrisho Mpoto alia na umoja kwa wasanii ‘tusiwe wasanii wa bila hit song maisha hayaendi’

$
0
0
Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amewataka wasanii kuondoa makundi yaliyopo kwenye muziki na kuanza kushirikiana kwa pamoja ili kuleta mafanikio kwa wengi.

Akiongea na mwandishi wetu Jumatatu hii muimbaji huyo amedai kila msanii nchini anafanya kazi kivyake hali ambayo inawanyima zaidi wasanii fursa za kibiashara.

“Kwa muda mrefu sasa wasanii wa Tanzania wamekua wakifanya kazi nzuri ndani na nje ya nchi, lakini kila mtu anacheza karata yake kivyake kutokana na network na nguvu yake,” alisema Mpoto. “Nadhani sasa wakati umefika kuondoa tofauti zetu, makundi, tukawa team moja tukae tuone tunawezaje kusaidiana kwenye nyanja za kibiashara,”

Aliongeza, “Kuwa kama wasanii wa Taifa la Tanzania wenye muelekeo mmoja bila kuingilia fani ya mtu wala maisha binafsi, Wazo langu tusitawanyike ikawa kila mtu anaenda kivyake, ukiotea hit basi ndiyo unapata hela, najaribu tu kuwaza kwa sauti kama wazo lina mashiko, #teamtanzania,”

Muimbaji huyo ni mmoja kati ya wasanii ambao wanapiga deal nyingi nje ya muziki ukiachia mbali deal za ubalozi za makumpuni mbalimbali alizopewa

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA PALESTINA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hazem M.Shabat, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kitabu alichokabidhiwa na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hazem M.Shabat, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hazem M.Shabat (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo, Ikulu jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU UMOJA WA MATAIFA (UN) PIA AHUDHURIA MKUTANO WA AU MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Marais wa wa mataifa mbalimbali  katika mkutano wa AU unaoendelea mjini Addis Abba nchini Ethiopia.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres mara baada ya mazungumzo yao.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Malawi Peter Mutharika kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na Rais wa Malawi Peter Mutharika pamoja na viongozi wengine mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Kidemokrasia ya Sahrawi(SADR) Brahim Ghali katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia. 

PICHA NA IKULU

HIZI HAPA HABARI TANO ZA LEO ZA MICHEZO ZA NDANI YA TANZANIA NA NJE YA TANZANIA

$
0
0

Leo tumeangazia habari za michezo zikiwemo za hapa Tanzania na nje ya Tanzania ,Ni habari tano za juu kwa undani wa habari hizo hii hapa video yake.

Attachments area Preview YouTube video HABARI TANO ZA MICHEZO NA RUVUMA TV

NSSF YAFIKA NUSU FAINALI YA MASHINDANO YA SOKA YA MASHIRIKA YA UMMA

$
0
0
Golikipa wa timu ya NSSF, Mfaume Mzee akijaribu kuokoa  moja ya hatari langoni mwake.
Nahodha wa NSSF, Baome Kiwamba akimiliki mpira.
Mshambuliaji wa timu ya NSSF, Shaban Enzi akichuana na beki wa Tanesco, Nicholous Peter katika mchezo wa nusu fainali ya mashindano ya timu zaMashirika ya Umma.

Golikipa wa timu ya NSSF, Mfaume Mzee  akisalimiana na wachezaji wa timu ya Tanesco wakati wa mchezo wa Nusu Fainali ya michuano ya Ligi ya Mashirika ya Umma uliofanyika kwenye uwanja wa TPDC Mikocheni jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Tanesco ilishinda 4-1. (Picha na Francis Dande)

masaa 24 baada ya ajali ya treni, njia ya reli kati ya Dar es salaam na Ruvu imefunguliwa rasmi

$
0
0
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetoa taarifa kuwa kuanzia saa 9 alasiri leo Januari 30, 2017 njia ya reli kati ya Kituo Kikuu cha Dar es salaam na Ruvu imefunguliwa rasmi kwa shughuli za uendeshaji wa reli. 


 Taarifa hiyo imesema kuwa kazi ya ufunguaji njia imewezekana baada ya Wahandisi na Mafundi wa reli kuyaondoa Mabehewa yaliopata ajali l kutoka relini na pia kuikarabati sehemu iliyo haribika . Kazi hiyo imefanyika kuanzia usiku wa Januari 29, 2017 hadi mchana wa Januari 30, 2017. 
Aidha treni ya abiria iliyoahirisha safari ya kuondoka kwenda bara jana imeondoka leo saa 9:05 alasiri kutoka kituo kikuu cha Dar es Salaam kwenda bara.. 
 Wakati huo huo imefahamika kuwa msafiri mmoja aliyetambulikana kama Nd Basekena O. Bango kutoka Bujumbura Burundi akiwa anasafiri kutoka Kigoma amelazwa katika Hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani wa Pwani kwa ajili ya matibabu zaidi. 
Aligunduliwa kuwa amechanika mguu wake wa kulia hivyo basi kuhitaji kushonwa mguu wake huo. Taarifa kutoka Muhimbili zinaeleza kulazwa kwa majeruhi wawili waliopokelewa hospitalini hapo usiku wa Januari 29, 2017. 
Majeruhi wamefamika kuwa ni Nd. Stephania Mbona (46) kutoka Kigoma alikuwa amekuja Muhimbili kuendelea na matibabu ya ugonjwa wa tumbo, hata hivyo alitibiwa majeraha ya kawaida na anaendelea kulazwa kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wake wa tumbo. 
 Mgonjwa wa pili Nd Alice Jovin (37) mkazi wa Salasala Dar es Salaam alikuwa anatoka Kigoma kuja Dar es Salaam amepata majeraha ya kawadia ametibiwa na alitarajiwa kuruhusiwa leo asubuhi. Kuhusu idadi ya wasafiri treni ya Deluxe yenye uwezo wa kusafirisha abiria zaidi ya 1000 wakati inapata ajali ilikuwa na abiria 480. 
 Aidha imefahamika kuwa ili kufahamika hasara na sababu za ajali hiyo taarifa rasmi itatolewa baada ya uchunguzi wa Kamati maalum inayoundwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za uendeshaji reli za kimataifa. Taarifa hiyo itatolewa baada ya wiki mbili. 
 Imetolewa na Afisi ya Uhusiano: 
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji 
wa TRL Ndugu Masanja Kungu Kadogosa 
Januari 30, 2017 DAR ES SALAAM

SIMU TV: Habari kutoka televisheni

RAIS DKT MAGUFULI ALIPOKUTANA NA RAIS WA MALAWI PROFESA MUTHARIKA NCHINI ETHIOPIA


EXIM BANK na OMAN AIR WAUNGANA.

$
0
0
Makampuni nguli Exim Bank ya nchini Tanzania na shirika la ndege la Oman yaungana kutoka punguzo la aina yake kwa wateja wa benki hiyo. Kwa mwaka mzima, wateja wa huduma ya Preferred Banking ya Exim watapata punguzo la asilimia 15% kwa safari zote za kutoka nchini zinazofanywa na shirika la Oman Air.

Akizungumza ofisini kwake, Meneja masoko wa Exim Bank Bi Mariam Mwapinga alisema ‘Punguzo hilo litadumu kwa miezi 12 kwa wateja watakaokata tiketi za ndege kati ya mwezi Septemba 2016 na Septemba 2017, na kusafiri kabla ya mwezi Desemba 2017.
Kuhusu kiwango hasa cha punguzo hilo, Bi Mwapinga alisema ‘Punguzo ni asilimia kumi na tano, kwa mfano kama gharama ya tiketi ni shilingi milioni moja, basi utapunguziwa laki moja na nusu’.

Alipoulizwa juu ya wateja wapya, kama nao wanaweza kupata punguzo hili, Bi Mwapinga alisema ‘Ndio wanaweza, wanachotakiwa ni kufuata hatua chache tu kuweza kujiunga na familia yetu. Kwanza watatakiwa kutembelea tawi lolote la Exim Bank na kufungua akaunti chini ya huduma ya Preferred Banking.’

Aliendelea kutoa maelezo, ‘Huduma ya Preferred Banking ni huduma ya kipekee, yaani unaweza kupata huduma zote za kibenki kwa kujinafasi. Ukiwa na akaunti hii utapata meneja uhusiano, maalumu kwa ajili yako pekee, viwango vyenye upendeleo wakati ukibadili fedha za kigeni, punguzo maalumu kwa makampuni washirika kama vile kama Ramada Hotels na maduka ya Shoppers. Pia utapata punguzo la asilimia 15 unaposafiri na ndege za Oman Air kuelekea safari zaidi ya 50 duniani.’
Kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kujiunga na Exim Preferred Banking na kupata punguzo hii, fika katika tawi lililo karibu nawe au piga simu namba +255 784 107 600. Pia unaweza kutuma barua pepe kwenda customerservice@eximbank-tz.com au tembelea kurasa zao za Facebook na Twitter @eximbanktz na @Exim_BankTz. Safari njema, wasalimie uendako.

The year 2500

AZAM MARINE YASHUSHA MELI KUBWA YA KISASA ITAKAYOKWENDA PEMBA NA UNGUJA KUTOKA MKOANI TANGA

$
0
0
Meli Kubwa inayoweza kuingia abiria 1600, magari 50 na mizigo kwa pamoja ambayo itafanya safari zake kati ya Tanga-Unguja na Pemba ikiwa inaingia bandari ya Tanga leo wakati wa uzinduzi wake ambapo uwekezaji huo mkubwa umefanywa na kampuni ya Azam Marine ili kuwanusuru wananchi wa mkoa wa Tanga na changamoto za usafiri huo.
Meli Kubwa inayoweza kuingia abiria 1600, magari 50 na  mizigo kwa pamoja ambayo itafanya safari zake kati ya Tanga-Unguja na Pemba ikiwa inaingia bandari ya Tanga leo wakati wa uzinduzi wake ambapo uwekezaji huo mkubwa umefanywa na kampuni ya Azam Marine
 Meneja Mkuu wa Azam Marine Husein Mohammed wa pili kulia akitazama namna wananchi wanavyoshuka kwenye meli hiyo itakayopunguza adha na usumbufu kwa wananchi wanaosafiri kutoka mkoani Tanga kwenda Unguja na Pemba.
 Baadhi ya Sehemu ya VIP ndani ya Meli hiyo kama inavyo onekana 

                                 
                                                    Kwa picha zaidi BOFYA HAPA




JUMA PONDAMALI "MENSAH" AFUNGUKA

$
0
0
Mcheza soka mkongwe  Juma Pondamali “Mensah” ambeye kwa sasa ni kocha wa makipa wa  Yanga  amefunguka mbelea ya Super News Tv Online na kumtaja kocha ambaye alimkuza kisoka toka akiwa mdogo yaani umri wa miaka 13-14.
Juma Pondamali alikuwa ni golikipa hodari aliye fanikiwa kuiwakilisha Tanzania miaka ya 1980 katika michuano ya “African Cup of Nation”.

Tumia dakika zako kadhaa kuitaza hii video ili ujue mengi kuhusu Nyota huyo.  Endelea kutufuatilia hapa soon tutakuletea Taarifa yake mpya ya kuachia wimbo wake wa singeli…..

RC SHIGELLA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA VIWANDA MKOANI TANGA, AVITAKA KUONGEZA UZALISHAJI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella  katikati akionyeshwa namna chuma zinavyozalishwa kwenye kiwanda cha Unique  Steel Mill) wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akiangalia ubora wa nondo zinazozalishwa kwenye kiwanda cha kuzalishia chuma cha Unique Steel Mill wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akiangalia ubora wa nondo zinazozalishwa kwenye kiwanda cha kuzalishia chuma cha Unique Steel Mill  wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.



SSRA NA TRA ZAKOMBA TUZO ZA UMOJA WA AFRIKA (AU)

$
0
0

Msemaji wa Serikali kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mindi Kasiga, akifurahia jambo pamoja na Ofisa Habari wa wizara hiyo, Freddy Maro, wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo kwa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na TRA jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Baadhi ya Maofisa wa SSRA na TRA, wakiwa katika hafla ya kikabidhi tuzo hizo za Umoja wa Afrika (AU) kwa taasisi hizo.
Meneja Mifumo ya Forodha toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  Bw. Tinkasimile Felix (kushoto) akipokea tuzo ya ubunifu wa mradi TANCIS, ambao umeunganisha mifumo midogomidogo ya Forodha toka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde, akilifurahia kombe hilo la ushindi wa jumla.


MWANDISHI WA HABARI LEO AULA KAMATI YA UTENDAJI CHAMA CHA WAAMUZI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MWANDISHI wa Gazeti  la HabariLeo na SpotiLeo, Rahel Pallangyo (pichani) amechaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya Utendaji  wa Chama cha Waamuzi wa Soka Mkoa wa Dar es Salaam kuwakilisha wanawake.
Rahel ambaye pia ni kocha mwenye leseni B inayotambuliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) alimwangusha mpinzani wake Isabela Kapera ambaye ni mwamuzi mstaafu wa FIFA aliyepata kura moja dhidi ya tano za Rahel.
Nafasi ya Mwenyekiti ilikwenda kwa Omar Abdulqudir aliyepata kura tano na Makamu Mwenyekiti ni Sijali Mzeru aliyepata kura sita na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa alichaguliwa Jovin Ndimbo kwa kura sita.
Katibu Mkuu alichaguliwa Said Mbwana kwa kura tano, msaidizi ni Waziri Hunda aliyepata kura sita na Mhazini ni Job Wandiba aliyepata kura sita.

Awali akizungumza kwa niaba ya wenzake wa uongozi uliopita muda, Hemed Nteza alishukuru kwa ushirikiano wa wajumbe na wachama kipindi chote walichokaa madarakani na kuwaasa watakaochaguliwa kuendeleza umoja.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Victor Mwandike alishukuru kwa kufanikisha uchaguzi kufanyika na kushukuru wajumbe wa mkutano kamati yake kwa kushirikiana vema.
"Nashukuru wajumbe na mwanasheria wa kamati kwa kutusaidia kutafsiri vifungu vya katiba na hatimaye tumemaliza kazi, nawatakia kila la heri katika kutekeleza majukumu yenu," alisema Mwandike.
Katika hatua nyingine  Mwenyekiti mpya, Abdulqudir  aliwateua Hemed Nteza na Mzee Malipula kuwa wajumbe wa heshima wa kamati ya utendaji.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 31, 2017

wakuu wa nchi za umoja wa Afrika katika mkutano wao wa 28 jijini Addis Ababa, Ethiopia

$
0
0
Picha ya pamoja ya wakuu wa nchi za umoja wa Afrika katika mkutano wao wa 28 jijini Addis Ababa, Ethiopia. Rais Dkt John Pombe Magufuli ni wa pili mstari wa pili kulia.

ROTARY CLUB OF DAR ES SALAAM DONATES BOOKS TO 12 SCHOOLS IN DAR

$
0
0
Rotary club of Dar es salaam President, Nirmal Sheth hands over a book to Tambaza Secondary school Head teacher Hussein Mavumba. The books were donated by Rotary club in partnership with the volunteers who are mainly spouses of World Bank employees and retired staff from the World Bank Group. Others are Rotary club of Dar es salaam secretary Azzan Shahid (right) the school official Simon Lupogo (left).
Oysterbay Primary school students displaying books which were provided by the Rotary club of Dar es salaam during the handover ceremony took place recently in 12 schools in Dar es salaam under the book project. With the aim of improving the quality of basic education, the Book Project is managed by volunteers who are mainly spouses of World Bank employees and retired staff from the World Bank Group and Rotarians from Rotary Club of Dsm. Others are Rotarian Kumail Manji (right), Rotarian Ramanan Ramamurthy (second left) and the school official Lucy Mwamunyange(left).
Some members of the Rotary club of Dar es salaam with pupils from Bongoyo and Oysterbay primary schools during the handover of books to schools. The club donated books to 12 schools in Dar es salaam recently.

Rais Donald Trump wa Marekani amtumbua kaimu mwanasheria mkuu kwa "usalit"

$
0
0
Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi kaimu mwanasheria mkuu Sally Yates saa chache tu baada ya kuwaagiza mawakili wa idara ya haki nchini humo kutotetea uamuzi wa kuwawekea vikwazo raia wanaotoka katika baadhi ya mataifa ya kiislamu. 
Taarifa ya Ikulu ya Whitehouse imemshtumu kwa usaliti. Sally Yates ambaye aliteuliwa na Obama alisema kuwa hafikirii kwamba marufuku hiyo ya muda kwa raia wa mataifa saba ya Kiislamu ni halali.
Wadhfa wake umechukuliwa na kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kijimbo huko Virginia Dana Boente. 
Agizo hilo la rais lililotiwa saini Ijumaa iliopita limesababisha maandamano nchini Marekani na ughaibuni. 
Awali kundi moja la wanadiplomasia liliandika barua likikosoa agizo hilo wakisema litazidi kuhatarisha usalama wa taifa hilo. 
Chanzo: BBC

ANNA ABDALAH AWATAKA VIONGOZI WANAWAKE WAWAFUNDE WASICHANA ILI WAWE VIONGOZI BORA WA BAADAYE

$
0
0
 Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Girl Guide Association (TGGA), Profesa Martha Qorro (kushoto), akimvisha beji Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA,  Zakhia Meghji wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar es Salaam juzi. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Kamishna Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi, akimpongeza Anna Abdalah 


Na Richard Mwaikenda

MJUMBE wa Bodi mpya ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Anna Abdalah, amewataka viongozi Wanawake kukutana na Wasichana kuwapiga msasa wa kuwaaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.

Anna Abdalah ambaye amekuwa kiongozi wa muda mrefu nchini, aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya TGGA, Mikocheni Dar es Salaam juzi.

Alisema ana mpango wa kuwaalika viongozi mbalimbali Wanawake akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akutane na Wasichana wanachama wa TGGA wawafundishe maadili ya uongozi kwa lengo la kuwaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.

Anna Abdalla alisema kuwa  hata yeye na Zakia Meghji pamoja na baadhi ya viongozi wengine wanawake walioshika nyadhifa mbalimbali nchini, enzi za usichana wao walipitia kwenye chama hicho na kulelewa vizuri. 

Pia katika kikao kijacho cha Bunge, anatarajia kukutana na Wabunge Wanawake na kuwaeleza umuhimu wamara kwa mara  kukutana na wasichana  kuwafundisha kwa kuwapa hamasa uongozi ili nao wawe kuwa wabunge na hata miongoni mwao kuwa Spika na mawaziri.

"Nataka siku za usoni,tuwaalike viongozi mbalimbali akiwemo, Samia Suluhu Hassan, Naibu Spika wa Bunge, Wabunge na Mawaziri Wanawake ili mje mjumuike nao pamoja, mjifunze mambo mbalimbali ya uongozi na mhamasike, ili siku moja nanyi mje kuwa kama, Samia, Kamishna, Spika wa Bunge, Wabunge na hata uwaziri pia" alisema Anna Abdalah, huku akipigia makofi na waalikwa katika hafla hiyo.

Katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Engera Kileo, ilihudhuriwa na wanachama wa chama hicho, wakiwemo pia wasichana watatu waliotoka Rwanda, Uganda na Madagasca waliokuwepo 

nchini katika mafunzo ya uongozi, maadili na utamaduni. Wasichana hao ni; Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), Recheal Baganyire (Uganda) na Andriambolamanana Vahatrimama. 

Kamishna Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi, aliwataja Wajumbe wa Bodi hiyo kuwa ni; Zakia Meghji, Anna Abdalah, Grace Makenya, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia  Mjema na Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Tunu Pinda. Mwenyekiti wa Bodi hiyo  atateuliwa miongoni mwao.
  Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Profesa Martha Qorro (kushoto), akimpongeza Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA,  Anna Abdalah wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar es Salaam juzi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya TGGA, Sophia Mjema (aliyekaa kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa TGGA wakati wa hafla hiyo. Aliyekaa kushoto ni Mariamu Kimbisa  ambaye ni Kamishna wa Kimataifa wa TGGA. Wa tatu kulia waliosimama ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi.

Viewing all 110095 articles
Browse latest View live




Latest Images