Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1538 | 1539 | (Page 1540) | 1541 | 1542 | .... | 3272 | newer

  0 0

  BAADA ya  mradi  wa maji Ipalamwa  kujengwa chini ya  kiwango kwa bomba kupasuka ovyo kabla ya mradi  kukabidhiwa, baraza   la madiwani  la Halmashauri ya  wilaya ya  Kilolo  mkoani  Iringa  limempa muda  wa  wiki  mbili mkandarasi  wa kampuni ya Norcom Ltd kukamilisha mradi  wa maji wa Ipalamwa  kwa  ubora unaotakiwa zinginevyo mkataba  wake  utavunjwa.
  Na Wakatihuo huo mkuu  wa  wilaya  ya  Kilolo  Mhe. Asia  Abdallah ameiagiza Halmashauri hiyo  kutomlipa fedha  yeyote  mkandarasi   huyo hadi  hapo atakapokamilisha mradi  kwa  kiwango  kinachotakiwa,    vinginevyo kama  kuna pesa  alilipwa awali basi  pindi  mkataba  wake utakapovunjwa atapaswa  kuzirudisha  fedha  hizo.

  Mkuu wa Wilaya ya Kilolo  Mhe. Asia Abdallah  akifafanua  jambo
  Mwenyekiti  wa Halmashauari ya  Kilolo  akifugua  kikao  kushoto  ni mkurugenzi  mtendaji wa Halmashauri ya  Kilolo

  Baraza la madiwani  Kilolo.
  Kwa habari kamili BOFYA HAPA

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya jamii

  KIPA wa Kagera Sugar, David Burhan amefariki dunia asubuhi ya leo katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza, baada ya kuugua ghafla.

  Kocha wa timu ya Kagera Sugar, Mecky Mexime, amethibitisha kutokea kwa kifo cha mchezaji wake huyo na kusema kuwa, Burhan alikuwa anasumbuliwa na Malaria.

  Aidha Mexime amesema kuwa  matatizo hayo yalianza wakati wamekwenda Singida kucheza na wenyeji wao, Singida United mechi ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania, maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) katikati ya wiki.

  Amesema alipanga kumuanzisha David Burhan katika mchezo huo, lakini hali yake ikabadilika ghafla hivyo akampanga kipa mwingine, Juma Kaseja badala yake.

  “Tumecheza mechi, baada ya mechi wakati tunarudi, tunafika Biharamulo, macho yake yakaanza kubadilika yakawa ya njano, ikabidi alazwe pale, kesho yake akahamishiwa hospitali ya mkoa wa Kagera, ambako baada ya kupimwa wakasema apelekwe Bugando,”amesema Mexime.

  “ uongozi wa Kagera Sugar ukafanya jitihada za haraka kumchukulia ndege kwenda Bugando Mwanza ambako alifika jana na kuanza matibabu kabla ya kufariki dunia leo asubuhi” amesema Mexime.

  Amesema Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kurejeshwa kwao Iringa na kuhusu mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Mexime amesema kwamba hawajajua kama utachezwa au la.

  “Sasa hivi ndiyo tunakwenda kwenye kikao cha kabla ya mechi, Pree Match Meeting tukifika huko ndiyo tutajua, ila kwa kweli upande wetu wachezaji wote wameshitushwa mno na taarifa hizi na sidhani kama wapo tayari kwa mechi ya leo,”alisema.

  Burham alijiunga na Kagera Sugar msimu huu akitokea Maji Maji ya Songea, ambayo nayo ilimtoa Mbeya City. Huyo ndiye aliyekuwa kipa wa kwanza Mbeya City wakati inapanda Ligi Kuu misimu mitatu iliyopita chini ya kocha Juma Mwambusi na akawa kipa bora wa msimu wa 2013/2014.

  0 0


  0 0

   Ulishawahi kukosa dili la hela kwasababu umepata dharura na ukashindwa kukamilisha kazi kwa wakati? Microsoft wanakwambia tumia kifaa chako mahali popote ulipo kupitia program ya Office365 kukamilisha mipango yako ya kibiashara au kiofisi, usikubali kupitwa na chochote.  Uwe mtandaoni au la, uwe ofisini au nje ya ofisi, ukitumia kompyuta au simu yako ya mkononi yenye program endeshi ya Android, iOS au windows unapata unachohitaji muda wowote na mahali popote.

  Kupitia vifurushi vingi ya Office365, utaweza kuweka program zilizotoka hivi karibuni za Microsoft Office kwenye vifaa vyako vya kazi hivyo kukuwezesha kufanya kazi ukiwa mtandaoni au usipokuwa mtandaoni. 
  Programu za Office365 huboreshwa mara kwa mara na ni rahisi kuzitumia na zinakuwezesha kufikia malengo yako ya kazi.

  Kuna vifurushi tofauti kulingana na mahitaji yako. Tuangalie kimoja baada ya kingine.
  1.ESSENTIAL – Barua pepe, program za Office mtandaoni na usalama wa kutunza taarifa 
  zako mtandaoni
  Kifurushi hiki kinakupatia;-
  -Barua pepe yenye domain yako mfano blogger@jinalakampuni.co.tz 
  -GB50 kwa ajili ya kuhifadhi barua pepe 
  -Unapata kuwekewa programu za Microsoft Office kwenye Kompyuta mpakato au simu yako
  -1TB kuhifadhi mafaili mtandaoni
  2.PRODUCTIVITY – Kuwekewa full package ya programu za Office kwa ajili ya biashara yako na kuhifadhi taarifa zako mtandaoni
  Kifurushi hiki kinakupatia;-
  -Programu za Office 2016 kuingizwa hadi kwenye Kompyuta 5
  -Kupata program za Office mtandaoni
  -Kupata program za Office kwenye simu za mkononi
  -1TB kuhifadhi mafaili mtandaoni

  3.PREMIUM – Unapata barua pepe, program za Office mtandaoni na usalama wa kuhifadhi mafaili
  Kifurushi hiki kinakupatia vyote ambavyo unakipata katika vifurushi viwili vilivyoangalia hapo awali isipokuwa ukiwa na kifurushi kipi unapata vingine vingi vya ziada. 
  -Kukufanyia masuala yote ya kiufundi, vile vile wataisaidia timu yako ya kazi kuunganisha Kompyuta zao. Yote haya yanafanyika ndani ya muda mfupi sana. 
  -Una data nyingi kuzidi kipimo? Zungumza na Microsoft BURE na watakupatia gharama zote za kuhamisha data na kuzihifahdi kwa usalama mtandaoni – hivyo kukuwezesha kufanya kazi popote na kifaa chochote
  -Msaada wa Bure: Wanapatikana kwa njia ya simu muda wa kazi ambao ni Jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 11 jioni kila siku kupitia mfumo maalum wa tiketi ili kukusaidia.

  Kwa Maelezo na taarifa zaidi tafadhali tembelea http://bit.ly/barua_pepeyabiashara au piga simu namba 0784 987363 / 0715 247365 / 022-2127641 au tuma barua pepe kwenda sales@extremewebtechnologies.com

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkura (Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu, Bi. Jennista Mhagama akizungumza kwenye semina Semina Elekezi kwa Kamati za Bunge juu ya ushiriki wa wananchi katika uwekezaji(Local Content) iliyoandaliwa na Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC) na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge (Sheria na Bunge), Bw. Mohamed Omary Mchengerwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza, Dkt. John Jingu mjini Dodoma Juzi.
  KATIBU Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng'i Issa (kushoto) akiwasilisha mada kwenye semina Semina Elekezi kwa Kamati za Bunge juu ya ushiriki wa wananchi katika uwekezaji(Local Content) iliyoandaliwa na Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC) na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), waliokaa kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkura (Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu, Bi. Jennista Mhagama, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge (Sheria na Bunge), Bw. Mohamed Omary Mchengerwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza, Dkt. John Jingu mjini Dodoma Juzi.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), DKt. John Jingu akifafanua jambokwenye semina Semina Elekezi kwa Kamati za Bunge juu ya ushiriki wa wananchi katika uwekezaji(Local Content) iliyoandaliwa na Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC) na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), mjini Dodoma juzi.

  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), akiongozwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando wakati akiwasili ofisi ya mkoa huo kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kuona changamoto za masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi.Wengine ni viongozi wa serikali mkoani hapo.
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando (kushoto), akitoa taarifa ya Mkoa kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mkoani hapo ikiwa na lengo la kuona changamoto za masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi.
  Katibu Tawala Mkoa wa Katavi, Paul Chagonja akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mkoani hapo yenye lengo la kuona changamoto za masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wakwanza kulia), akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mkoani hapo kwa lengo la kuona changamoto za masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi.Wengine ni viongozi wa mkoa huo kutoka kada mbalimbali.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kulia),akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando,(wapili kulia). Naibu Waziri alifika mkoani hapo kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kuona changamoto za masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi. Wengine ni viongozi wa mkoa huo kutoka kada mbalimbali (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

  0 0

  Airtel Africa, a leading telecommunications company with operations in 15 countries across Africa, has refuted speculative media reports erroneously stating its possible exit from Africa. The organization has reaffirmed that it remains committed to Africa and will continue to invest in its operations to grow sustainably in Africa.

  Airtel Africa’s recent 3rd quarter results were strong. The underlying Africa revenues for the quarter accelerated by 6.0 per cent Y-o-Y, the highest over the last 9 quarters. The organizations efforts to improve the quality of customer acquisitions have resulted in a reduction in customer churn to 4.9 per cent from 6.0 per cent. Data consumption and revenues have grown by 91.0 per cent & 24.0 per cent Y-o-Y respectively, led by stronger data networks. The strong focus on cost management has led to a significant underlying EBITDA margin expansion of 4.5 per cent Y-o-Y, which now stands at 24.5 per cent. Africa is now generating positive free cash and is PBT positive in constant currency.

  Raghunath Mandava, Managing Director and Chief Executive Officer, Airtel Africa, said’ “All the steps taken recently with regard to human resources and infrastructure have been geared towards readying the organization to grow efficiently and sustainably in the medium to long term. The company remains committed to competing in various markets and providing more choice to customers through further investments to ensure consistent delivery of quality and value for money services to our customers. We are also accelerating our investments in new data networks and to modernize our existing networks. We are committed to launch 4 G in multiple countries.”

  He added “Mergers and acquisitions continue to be the norm for any multinational organization and they affect all global organizations in equal measures as and when they happen. As a strategy, we look for opportunities to acquire or merge in opcos that are operating in a fragmented market structure with too many players in a small market. Last year, Airtel and Orange reached a mutually beneficial agreement on the assets in Sierra Leone and Burkina Faso. Similarly, Airtel also acquired assets in Uganda, CongoB and Kenya in recent times. The agreements brought together the strengths of Airtel, Warid and Essar. This has offered benefits to customers in the form of a superior and wider network, affordable voice / data services and better customer care. Away from Africa, recently, we merged with Robi in Bangladesh to create a solid and profitable No.2 player in the market.” 

  The recent results demonstrate the effectiveness of Airtel’s business strategy in Africa.  The organization sees an opportunity ahead to emerge with a broader reach and sharper execution. 

  0 0

  Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewataka Vijana kuwa na tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara kwani kufanya hivyo kunapelekea Afya zao kuwa imara na kuepuka magonjwa yanayoweza sababisha vifo vya mapema.
  Akizungumza Jijini Dar es Salaam wakati akizindua Bonanza la Michezo maeneo ya Tabata lililoandaliwa na Windhoek beer DAS Mpogolo amesema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) vijana wengi wanapoteza maisha kwa kutotunza Afya zao na kueleza kuwa vifo takribani 3000 vimeripotiwa vinavyotokana na shinikizo la damu huku Tanzania ikiwa nchi ya 85, huku kwa ugonjwa wa kisukari watu takribani 9257 wamepoteza maisha na Tanzania ikishika nafasi ya 35 kidunia na Kiharusi zaidi ya 5000 wamepoteza maisha na Tanzania ikishika nafasi ya 102 kidunia.
  Kutokana na Takwimu hizo DAS Mpogolo amesisitiza mazoezi kwa vijana kwa kufanya michezo ambayo inawakutanisha na kuanzisha mahusiano na kuleta undugu, huku akiwasisitiza waandaaji waandae mabonanza kama hayo yakishirikisha michezo ya aina tofauti siyo mpira wa miguu pekee.
  Bonanza hilo lilikuwa kivutio baada ya Timu mbili za Kwetu Pazuri wakiwa wenyeji na Bongo Fleva, huku timu ya Kwetu Pazuri ikiwa na wachezaji ambao ni wasanii wa familia moja Ali Kiba na Abdul Kiba na mchekeshaji maarufu kama Kupe ambaye aliipatia ushindi Kwetu Pazuri kwa kushinda goli mbili kwa nunge, na kwa upande wa Bongo Fleva timu yao ilipambwa na mastaa wakongwe akiwemo KR, Mchizi Mox, Soggy Doggy, Suma G, M2THE P, na Juma Nature.

  0 0

  Kampuni ya Kusafirisha Mafuta Ghafi ya TAZAMA imetakiwa kutumia uchumi kushusha gharama za matumizi ili kumudu ushindani wa soko Nchini Zambia.

  Wito huo umetolewa hivi karibuni kwa nyakati tofauti na Mawaziri wa Nishati wa Tanzania na Zambia, Profesa Sospeter Muhongo (Tanzania) na Mabumba David (Zambia) walipokuwa wakizungumza na wafanyakazi wa Vituo vya Kusukuma Mafuta (Pumping Stations) vilivyopo Mkoani Mbeya na Iringa wakati wa ziara ya kutembelea vituo hivyo.

  Profesa Muhongo alisema dhamira ya Serikali za Tanzania na Zambia ni kuhakikisha Bomba pamoja na Mfumo mzima wa uendeshaji wa kampuni hiyo vinaboreka na kuweza kushusha bei ya mafuta ili kumudu ushindani.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) na Waziri wa Nishati wa Zambia, Mabumba David (nyuma yake) wakikagua Kituo cha Kusukuma Mafuta Ghafi (Pumping station) cha TAZAMA kilichopo Mkoani Mbeya.

   Alisema kampuni ya TAZAMA haiwezi kuendelea na utendaji wa kizamani huku ikitumia gharama kubwa kwenye uendeshaji na hivyo kusababisha kuuza mafuta yake kwa bei ya juu ikilinganishwa na wauzaji wengine kwenye soko.

  Aliongeza kwamba zinahitajika jitihada za makusudi kuhakikisha uzalishaji unaongezeka kwa lengo la kuweza kuingia kwenye ushindani wa soko.

  Alisema teknolojia inayotumiwa na kampuni hiyo kwa ujumla wake imepitwa na wakati na ili kuongeza uzalishaji ni muhimu kuhakikisha teknolojia hiyo inaboreshwa sambamba na uboreshwaji wa utendaji wa wafanyakazi wake. “Hampaswi kuridhika na kiwango mnachosafirisha kwani ni kidogo sana ikilinganishwa na hapo awali; mkiendelea hivi mnaweza kujikuta mnasafirisha hata lita laki moja,” alisema.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akikagua moja ya mtambo wa Kusukuma Mafuta Ghafi wa TAZAMA Mkoani Iringa.

  Kwa upande wake Waziri David alisema TAZAMA inapaswa kuelewa dhamira ya Serikali hizo mbili ili ifanye jitihada ya kufikia malengo hususan ikizingatiwa kwamba mahitaji ya mafuta nchini Zambia yameongezeka tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

  Alisisitiza kuwa ni lazima kukafanyika mabadiliko ya kiteknolojia na kiutendaji ili kufikia lengo na alitaja sababu mojawapo inayosababisha mafuta ya TAZAMA kuuzwa kwa bei ya juu kuliko wengine ni kwamba mafuta yanayosafirishwa ni machache wakati gharama ya usukumaji wa mafuta hayo inabaki kuwa kubwa.

  “Mkisafirisha mafuta mengi ni lazima gharama zitapungua na hivyo mtaweza kuuza mafuta yenu kwa bei ndogo ikilinganishwa na wengine,” alisema.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa Kituo cha Kusukuma Mafuta Ghafi cha TAZAMA kilichopo Mkoani Iringa. Kulia kwake ni Waziri wa Nishati wa Zambia, Mabumba David. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Zambia, Brigedia Jenerali Emelda Chola.

  Aliwaasa wafanyakazi wa TAZAMA kuwa waelewa na kukubali kubadilika kwa faida yao binafsi na kwa faida ya nchi za Tanzania na Zambia kwa ujumla.


  0 0

  Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akihutubia leo wakati wa kufungua baraza la ushauri (RCC) Mkoa wa Dodoma ambapo lilishirikisha Wizara,Idara na Wadau mbalimbali wanaoratibu ujio wa Serikali kuhamia Makao makuu Dodoma Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Chuo cha mipango ya Maendeleo Vijijini Dodoma ( Picha na PMO)
  WAZIRI MKUU Kassm Majaliwa amesema wakati umefika wa kuwa na watumishi wenye weledi wa kutosha kwenye Halmashauri zote nchini na pia hazitakiwi kuwa pango la wezi, wazembe au jalala la kutupa wabadhilifu walioshindikana kwingineko.

  Aidha, Waziri Mkuu amesemma Serikali za Mitaa na Halmashauri zote nchini zinatakiwa zianze kujitathmini na kujipanga vizuri zaidi kuona ni kwa namna gani zitakuwa chachu ya maendeleo ya viwanda vinavyotarajiwa.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Januari 30, 2017) wakati akifungua Kikao cha Baraza la Mashauriano (RCC) mkoani Dodoma. Amesema kikao ni chombo muhimu na endapo kitatumika vizuri kitaweza kusaidia kusukuma maendeleo ya Mkoa na kupunguza migogoro kwenye Halmashauri.

  Amesema Serikali itaendelea kuongeza kiwango cha ruzuku kwa Halmashauri zote nchini kwa kadiri uwezo utakavyoruhusu na kusisitiza kwamba fedha hizo lazima zisimamiwe vizuri na zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo inayowagusa wananchi.

  “Endapo itabainika kwamba kuna baadhi ya Sheria zinazokwamisha utendaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, hatutasita kuzifanyia mapitio na hatimaye kuzibadili ili ziendane na azma yetu ya kutoa huduma bora kwa wananchi,” amesema.

  Amesema Serikali ina maslahi makubwa kwa Serikali za Mitaa, sio tu kwa kuwa ni Serikali kamili katika ngazi hiyo, bali pia kutokana na ukweli kwamba kero nyingi za wananchi ziko katika ngazi hiyo.

  Waziri Mkuu amesema vyanzo vingi vya mapato ya Serikali vinapatikana kwenye Halmashauri huku changamoto kubwa ikiwa ni kulegalega kwa  Halmashauri nyingi katika ukusanyaji wa mapato ya kodi na yasiyo ya kodi jambo linalozorotesha utoaji wa huduma kwa wananchi.

  Hivyo Waziri Mkuu ametoa rai kwa Halmashauri hizo kuendelea kuboresha huduma kwa wananchi na kutatua kero zao kikamilifu na kwa wakati pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato.

  Pia zihakikishe malipo yote yanafanyika kwa njia za kielektoniki na zihamasishe vijana na akina mama wajiunge kwenye vikundi vya uzalishaji mali na kuwapatia stadi za kazi na mikopo yenye masharti nafuu ili waweze kuwa chanzo cha mapato hapo baadaye.

  Amesema watendaji wa Halmashauri wanatakiwa  kujiepusha na vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa mali za umma na uzembe kazini na watakaobainika kufanya vitendo hivyo  wachukuliwe hatua kali za kisheria na kinidhamu.

  “Someni taarifa ya CAG (Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali) na kutoa majibu ya kina ya namna mtakavyodhibiti mianya ya rushwa na ubadhilifu kama ilivyoainishwa kwenye ripoti hizo,” amesema.

  Hata hivyo amesema kila Halmashauri iandae mpango wa utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye maeneo makubwa ya kipaumbele kama vile ujenzi wa miundombinu ya shule,  maboresho kwenye sekta ya afya (ujenzi wa hospitali, zahanati na vituo vya afya).

  “Endeleeni kuwa na mahusiano mazuri miongoni mwenu, mfanye kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.  Kila mmoja kwa nafasi aliyonayo atimize wajibu wake na kuzingatia mipaka ya nafasi yake. Punguzeni migogoro, matusi, dharau, bezo na vitisho. Mshirikiane na jamii ione mpo wamoja,” amesema.

  0 0

  Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetoa taarifa kuwa kuanzia saa 9 alasiri leo Januari 30, 2017 njia ya reli kati ya Kituo Kikuu cha Dar es salaam na Ruvu imefunguliwa rasmi kwa shughuli za uendeshaji wa reli.

  Taarifa hiyo imesema kuwa kazi ya ufunguaji njia imewezekana baada ya Wahandisi na Mafundi wa reli kuyaondoa Mabehewa yaliopata ajali l kutoka relini na pia kuikarabati sehemu iliyo haribika . Kazi hiyo imefanyika kuanzia usiku wa Januari 29, 2017 hadi mchana wa Januari 30, 2017.

  Aidha treni ya abiria iliyoahirisha safari ya kuondoka kwenda bara jana imeondoka leo saa 9:05 alasiri kutoka kituo kikuu cha Dar es Salaam kwenda bara..

  Wakati huo huo imefahamika kuwa msafiri mmoja aliyetambulikana kama Nd Basekena O. Bango kutoka Bujumbura Burundi akiwa anasafiri kutoka Kigoma amelazwa katika Hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani wa Pwani kwa ajili ya matibabu zaidi. Aligunduliwa kuwa amechanika mguu wake wa kulia hivyo basi kuhitaji kushonwa mguu wake huo.

  Taarifa kutoka Muhimbili zinaeleza kulazwa kwa majeruhi wawili waliopokelewa hospitalini hapo usiku wa Januari 29, 2017. Majeruhi wamefamika kuwa ni Nd. Stephania Mbona (46) kutoka Kigoma alikuwa amekuja Muhimbili kuendelea na matibabu ya ugonjwa wa tumbo, hata hivyo alitibiwa majeraha ya kawaida na anaendelea kulazwa kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wake wa tumbo.

  Mgonjwa wa pili Nd Alice Jovin (37) mkazi wa Salasala Dar es Salaam alikuwa anatoka Kigoma kuja Dar es Salaam amepata majeraha ya kawadia ametibiwa na alitarajiwa kuruhusiwa leo asubuhi.

  Kuhusu idadi ya wasafiri treni ya Deluxe yenye uwezo wa kusafirisha abiria zaidi ya 1000 wakati inapata ajali ilikuwa na abiria 480.

  Aidha imefahamika kuwa ili kufahamika hasara na sababu za ajali hiyo taarifa rasmi itatolewa baada ya uchunguzi wa Kamati maalum inayoundwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za uendeshaji reli za kimataifa. Taarifa hiyo itatolewa baada ya wiki mbili.

  Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:
  Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
  Ndugu Masanja Kungu Kadogosa
  Januari 30, 2017
  DAR ES SALAAM

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


  MWANDISHI wa Gazeti  la HabariLeo na SpotiLeo, Rahel Pallangyo amechaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya Utendaji  wa Chama cha Waamuzi wa Soka Mkoa wa Dar es Salaam kuwakilisha wanawake.

  Rahel ambaye pia ni kocha mwenye leseni B inayotambuliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) alimwangusha mpinzani wake Isabela Kapera ambaye ni mwamuzi mstaafu wa FIFA aliyepata kura moja dhidi ya tano za Rahel.

  Nafasi ya Mwenyekiti ilikwenda kwa Omar Abdulqudir aliyepata kura tano na Makamu Mwenyekiti ni Sijali Mzeru aliyepata kura sita na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa alichaguliwa Jovin Ndimbo kwa kura sita.

  Katibu Mkuu alichaguliwa Said Mbwana kwa kura tano, msaidizi ni Waziri Hunda aliyepata kura sita na Mhazini ni Job Wandiba aliyepata kura sita.

  Awali akizungumza kwa niaba ya wenzake wa uongozi uliopita muda, Hemed Nteza alishukuru kwa ushirikiano wa wajumbe na wachama kipindi chote walichokaa madarakani na kuwaasa watakaochaguliwa kuendeleza umoja.

  Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Victor Mwandike alishukuru kwa kufanikisha uchaguzi kufanyika na kushukuru wajumbe wa mkutano kamati yake kwa kushirikiana vema.

  "Nashukuru wajumbe na mwanasheria wa kamati kwa kutusaidia kutafsiri vifungu vya katiba na hatimaye tumemaliza kazi, nawatakia kila la heri katika kutekeleza majukumu yenu," alisema Mwandike.

  Katika hatua nyingine  Mwenyekiti mpya, Abdulqudir  aliwateua Hemed Nteza na Mzee Malipula kuwa wajumbe wa heshima wa kamati ya utendaji.

  0 0

   Makamu Mwenyekiti wa bodi ya DCB Lucian Msambichakana akimkabidhi aliyekuwa meneja mwandamizi wa tawi la Magomeni Gray Ndandika tuzo ya Chairman's awards baada ya kuibuka kidedea.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  BENKI ya DCB wamewazawadia tuzo tawi la Magomeni inayojulikana kama Chairman's awards baada ya kufanya vyema kiutendaji na kuwapiku matawi mengine ya benki hiyo na kutakiwa kuendelea kudumisha  ufanisi wa kazi.

  Akizungumza kabla ya kutangaza kwa mshindi, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa alisema kuwa matawi ya benki hupimwa kwa kutekeleza viashiria mbalimbali ikiwemo ukuaji wa amana zitokanazo na akaunti za hundi na akiba kwa asilimia 15, utoaji wa mikopo kwa asilimia 15, faida kabla ya kodi, ufuatiliaji wa mikopo chechefu na asilimia ya mikopo chechefu.

  Mkwawa alisema kuwa, ili mshindi aweze kutangazwa ni lazima tawi husika kufikisha alama 60 ambzo zitagawiwa katika kutekeleza viashiria 10 na shindano hili lilianza toka Oktoba 2011 na tawi la Tabata ndilo lilikuwa la kwanza kuanza kuchukua tuzo hiyo.

  Mbali na hilo, benki hiyo iliweza kutoa zawadi kwa meneja wa mikopo kwa vikundi kiasi cha shillingi laki tano (500,000), wasimamizi 9 wa mikopo kutoka matawi yoye kila mmoja akizawadiwa shilingi laki tatu (300,000) na maafisa watano kila mmoja shilingi laki mbili (200,000) ikiwa na lengo la kuwapatia motisha ya kufanya kazi kwa bidii zaidi na kusimamia vizuri uendeshaji wa mikopo hiyo.

  Makamau Mwenyekiti wa bodi hiyo, Lucian Msambichaka amewapongeza tawi la Magomeni kwa jitihada kubwa walizozionyesha na kuwataka kuendelea kufanya vizuri zaidi na kuwasisitiza kuongeza ufanisi wa kibiashara kwa kuleta changamoto ya kushindanisha matawi hayo katika kila nyanja za huduma za kibenki.
    Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akizungumza wakati wa utoaji wa tuzo kwa tawi la Magomeni baada ya kufanya vyema kiutendaji na kuwapiku matawi mengine ya benki hiyo na kutakiwa kuendelea kudumisha  ufanisi wa kazi.
  Makamu Mwenyekiti wa bodi ya DCB Lucian Msambichaka akizungumza wakati wa utoaji wa tuzo kwa tawi  la Magomeni baada ya kufanya vyema kiutendaji na kuwapiku matawi mengine ya benki hiyo na kutakiwa kuendelea kudumisha  ufanisi wa kazi.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0


  Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla  akizungumza na wafanyabiashara pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoani Mbeya, juu ya kukuza na kupanuka kwa wigo wa biashara mkoani humo, katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa. Picha na Mr.Pengo Mmg

  Mmoja wa wafanya biashara akichangia mada wakati wa mkutano na Mkuu wa mkoa wa Mbeya
  Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini Mh.William Ntinika katika kikao na wafanyabiashara
  Baadhi ya wafanyabiashara, wadau mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa jiji la Mbeya wakifuatilia mkutano wa mkuu wa mkoa wa Mbeya
  Mkutano ukiendelea katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya leo                 

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi,Saleh Mhando akiwa sambamba na kamati ya Ulinzi na Usalama,kwa pamoja wakiwa kwenye ziara ya  siku tatu ya kukagua hali ya Kilimo cha mazao ya Mahindi, Mpunga, Alizeti na Tumbaku.Dc Mhando amesema kuwa kwa ujumla hali ni nzuri sana na Wananchi wanatarajia kupata mavuno ya kutosha pamoja na ziada.
   
   Moja ya shamba la Mahindi yakiwa yamestawi vyema
    Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi,Saleh Mhando akiwa sambamba na kamati ya Ulinzi na Usalama wakikagua mashamba ya mpunga na kujionea hali halisi ya kilimo cha mpunga.
  Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi,Saleh Mhando akiwa sambamba na mmoja wa Wanakamati ya Ulinzi na Usalama wakikagua moja ya mashamba ya mahindi na kujionea hali halisi ya kilimo   Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi,Saleh Mhando akiwa sambamba na kamati ya Ulinzi na Usalama wakikagua mashamba ya mpunga na kujionea hali halisi ya kilimo cha mpunga.
   Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi,Saleh Mhando akiwa sambamba na kamati ya Ulinzi na Usalama wakijadiliana jambo mara baada ya kumaliza kukagua baadhi ya mashamba ya Mahindi na Mpunga wilayani humo mkoani Katavi

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasikiliza Mawaziri wa Nishati kutoka Tanzania na Zambia wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi kutoka Tanzania mpaka Zambia, Mawaziri hao ni Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Mhe.Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Waziri wa Nishati wa Zambia Bw. David Mabumba (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Mhe.Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Waziri wa Nishati wa Zambia Bw. David Mabumba (kushoto) mara baada ya kumaliza mkutano wa kumpa taarifa Makamu wa Rais ya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Nishati wa Zambia Bw. David Mabumba (kushoto) mara baada ya kupokea taarifa ya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi litakalotoka Dar es Salaam, Tanzania mpaka Ndola, Zambia, Ikulu jijini Dar es Salaam.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Tanzania na Zambia ambao ulifanya ziara ya kukagua pampu na bomba la mafuta la TAZAMA kutoka Ndola, Zambia mpaka Dar es Salaam Tanzania wakiongozwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati wa Zambia Bw. David Mabumba ambapo walifanya tathmini ya ujenzi wa bomba jipya la mafuta safi litakalotoka Dar es Salaam, Tanzania mpaka Ndola, Zambia.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


  0 0  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

  MKUU wa Wilaya Ya Buhigwe Kanali Marco Gaguti amewataka Viongozi wa Serikali ngazi zote kusimamia ipasavyo zoezi la ulinzi na usalama la kuanzisha Nyumba kumi za kiusalama litakalo saidia kukomesha wahamiaji halamu wanao ingia nchini kinyume na sheria na vitendo vya kiuhalifu vinavyo fanywa na watu wasio na mapenzi mema na Nchi yao.

  Rai hiyo aliitoa mapema juzi usiku wakati wa doria ya kukagua zoezi la ulinzi wa Nyumba kumi za kiusalama linaloendelea wilayani humo,ambapo Dc Gaguti alibaini baadhi ya Mabalozi wa Nyumba kumi za kiusalama hawana uelewa juu ya uendeshaji wa zoezi hili,hivyo aliwataka maafisa watendaji pamoja na wenyeviti wa vitongoji kutoa elimu hiyo kama walivyo pewa mafunzo kabla ya zoezi hilo kuanza.

  Gaguti alisema lengo la kuanzisha Nyumba kumi za kiusalama ni kuhakikisha Kila balozi wa Nyumba hizo, anafahamu kila nyumba ina wakaazi wangapi Pamoja na kuweka daftari la kumbukumbu na kufahamu wageni wanao ingia na kutoka katika kaya hizo, ilikuhakikisha Wahamiaji halamu wanaiingia nchini kinyume na utaratibu wanakamatwa na na kuchukuliwa hatua za kisheria.

  Alisema kumekuwa na Matukio ya kiuhalifu yaliyo kuwa yakifanywa na Wahamiaji halamu wanaoingia Nchini wakiwa na silaha na kushirikiana na baadhi ya Wananchi wa Wilaya hizi zilizopo Mpakani kufanya unyang'anyi kwa kutumia silaha. Zoezi hili la ulinzi wa Nyumba kumi likifanyika kwa ufanisi litasaidia sana kupunguza vitendo hivyo na kubaini wahamiaji wanaoingia.
  MKUU wa Wilaya Ya Buhigwe Kanali Marco Gaguti akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Buhigwe,hivi karibuni alipofanya doria ya kukagua zoezi la ulinzi wa Nyumba kumi za kiusalama linaloendelea wilayani humo mkoani Kigoma
  MKUU wa Wilaya Ya Buhigwe Kanali Marco Gaguti akikagua moja ya daftari lililowekwa kwa na balozi wa nyumba kumi kwa ajili ya kuorodhsha majina ya wakazi wa balozi husika,Kanali Gagugti alifanya doria ya kukagua zoezi la ulinzi wa Nyumba kumi za kiusalama linaloendelea wilayani humo mkoani Kigoma.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imesema kwamba inaunga mkono juhudi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika programu za maendeleo ya vijana, hususani nia yake ya dhati kushiriki michuano ijayo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan mwaka 2020.

  Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Omari aliyasema hayo mara baada ya kusikia program za TFF kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Makamu Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau katika hafla ya uzinduzi wa kampeni maalumu za kuifanikisha Tanzania kushiriki michuano ijayo ya Olimpiki.

  “Nimesikia program mbalimbali za TFF, naona zinakuja wakati mwafaka. Nimewapongeze kwa mipango yenu mizuri kwa sababu inaleta matumaini. Jambo kubwa ambalo linanisukuma na kuwapongeza ni kuwa na program ya vijana, hatuwezi kufanikiwa kama hatutakuwa na program ya vijana," amesema Omary. Serikali inatambua haya yote mnayofanya. Na ili kuboresha, Serikali imetenga shule 55 ambazo zitakuwa ni maalumu kwa ajili ya vijana, lengo ni kupata vipaji bora ambavyo vitakuwa vikiendelezwa, huku wakiwa wanapata elimu.

  Aliendelea, kusema kuwa anasikia  TFF wameunda Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu hususani vijana ni jambo zuri, lakini rai yangu ni kwamba watakapounda kamati ya mfuko huo wawe watu wenye heshima ili wananchi waipende na ikiwa hivyo itafanikiwa wao kama Serikali watafanya kazi bega kwa bega na kamati hiyo na jambo kubwa ni kwamba lazima wakutane mara kwa mara.


  Kabla ya Mkurugenzi Singo kuzungumza, Makamu Rais wa TOC, Ndugu Tandau, alipongeza pia harakati za kuanza mapema akisema: “Shukrani TFF kwa kuthamini TOC. Ni vizuri tumeanza mapema. Michuano ya Olimipiki ni mikubwa na inahitaji timu zenye viwango vya juu kufanikiwa kufuzu.”

  Alieleza hadhara iliyohudhuria hafla hiyo, kuwa TOC inakuwa na Mawasiliano ya maandalizi Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki inayoitwa ‘Olympic Solidarity Program’ ambayo hutoa sehemu ya fungu ya maandalizi na kwamba TFF haina budi kuwasilisha program yake kwa ajili ya kuingia kwenye bajeti ambayo inaitwa ‘Team Support Grant’.

  Awali kabla ya viongozi hao kuzungumza, Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema kinachofanywa sasa na Shirikisho si kutafuta miujiza kwenye matokeo badala yake ni kujenga timu (Maandalizi) kwa dhana kwamba Timu za Taifa haziokotwi kama embe dodo.“Mhe. Mkurugenzi, kujenga timu hizi ni gharama kubwa. Hata matunda ambayo tunasubiri moshi mweupe ya timu ya vijana, hayakutokea hivi hivi ni maandalizi. Si ajabu kabla ya mwisho wa wiki hii tukaona moshi mweupe,” alisema Malinzi.


  Alisema ili vijana wa Tanzania waweze kufanya vema, hakuna budi wadau wakiwamo Serikali, Kampuni, Mashirika ya umma na watu binafasi kusapoti mbio hizo za kwenda Tokyo, Japan pamoja na timu nyingine za taifa. “Program nzima ni gharama kubwa,” Kadhalika, ili kutekeleza program hiyo, Rais Malinzi alizungumzia utulivu katika kufanya kazi kwa sasa kwa kuwa historia inaonesha kuwa kumekuwa na nia ovu ya baadhi ya wadau kutaka kutibua mambo mazuri yanayofanywa na uongozi wa mpira wa miguu.

   Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Omari akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu za kuifanikisha Tanzania kushiriki michuano ijayo ya Olimpiki 2020 na kuipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzaniana nchini  kwa  juhudi za kuandaa programu za maendeleo ya vijana.
   Rais wa    Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Jamal Malinzi akizungumza wakati wa  uzinduzi wa kampeni maalumu za kuifanikisha Tanzania kushiriki michuano ijayo ya Olimpiki 2020 na kuwataka wadau wa michezo kuunga mkono jitihada zake na wasimuache peke yake katika kulisongesha gurudumu la michezo.
    Picha ya pamoja ya viongozi wa mpira wachezaji wa timu ya vijana  sambamba na Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Omari.

  Wachezaji watimu ya vijana wakiwa katika mazoezi leo wakati wa  uzinduzi wa kampeni maalumu za kuifanikisha Tanzania kushiriki michuano ijayo ya Olimpiki 2020.Picha na Zainab Nyamka.

  0 0

  Mhandisi Mtigumwe ametoa kauli hiyo wakati wa kikao maalumu cha kuhusiana na uamuzi wa serikali kuhamia Makao Makuu ya Nchi mkoani Dodoma kilichokuwa na lengo la kujadili kwa pamoja namna ya utendaji kazi katika wizara hiyo sambamba na kutoa utaratibu utakavyokuwa kuelekea mjini Dodoma.

  Mtigumwe amebainisha kuwa Awamu ya Kwanza ya uhamisho utawahusisha watumishi 88 kutoka Idara Kuu ya Mazao, ambapo katika mchakato huo watumishi 41 watahamia Dodoma kuanzia tarehe 14 – 15/2/2017 na wengine 47 waliobaki watahamia muda wowote katika kipindi cha kuanzia mwezi Februari hadi kufikia mwezi Juni.

  Mtigumwe amewaeleza watumishi hao kuwa maandalizi ya ofisi za Wizara ya kilimo zilizopo mjini Dodoma zinaendelea vizuri na tayari baadhi ya maeneo yamekamilika huku mengine yakiendelea kukamilishwa ili kukidhi matakwa kwa ajili ya watumishi wote watakapohamia mjini Dodoma.

  Uamuzi wa Watumishi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kuhamia mjini Dodoma ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kuitaka Serikali yote kuhamia Dodoma ili kutekeleza uamuzi uliofikiwa tangia miaka ya 70 na Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutambua na kutangaza kuwa Dodoma ndio Makao Makuu ya Nchi.

  Mhandisi Mtigumwe amebainisha hayo hii leo katika kikao cha pamoja na watumishi wa wizara ya kilimo katika Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja na wafanyakazi wa wizara hiyo.

  Watumishi wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakimsikiliza kwa makini Katibu mkuu wa wizara hiyo Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Mathew John Mtigumwe hii leo amewaondoa hofu watumishi wa wizara yake kuhusu zoezi la serikali kuhamia Dodoma kuwa litafuata misingi na stahili za watumishi kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa Umma.

older | 1 | .... | 1538 | 1539 | (Page 1540) | 1541 | 1542 | .... | 3272 | newer