Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110149 articles
Browse latest View live

Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi


INTRODUCING NEW CLUB BANGER - KAJIPU - FROM MJ RECORDS

$
0
0
Tanzalaizer ni msanii mpya Mmasai anayefanya staili ya Muziki wa kisasa. Huu ni wimbo wake wa kwanza unaoitwa KAJIPU aliorekodi katika studio za MJ RECORDS, ukiwa umetengenezwa na Daxo Chali na Video ikifanywa na DEO ABEL. KAJIPU ni wimbo ulio katika mahadhi ya "Afro-pop, house music na kwaito" wenye ujumbe wa utumbuaji majipu.(utatuzi wa matatizo)

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 27/01/2017

KC GLOBAL LINKS: KONTENA LIMEISHAONDOKA NA LITAFIKA DAR MWISHONI MWA FEBRUARY

$
0
0


KONTENA JINGINE LINAONDOKA ALHAMIS IJAYO TAREHE 02/02/2017: BEI ZETU NI NAFUU KULIKO WENGINE WOTE NA HAKUNA CHARGES NYINGINE!

Only £1.75 per kg
Fridge £70
Coocker £60
W/machine £60
Fridge dogo £60
Sanduku dogo £30
Sanduku kuubwaa £50
Box la kawaida £50
Ice cream £2
SALOON CAR ONLY £650
4 x 4 CARS ONLY £850
Ukiwa na mzigo mkubwa tunaelewana tu. Hata matofali leteni tu...Hatuachagi kitu sisi. Bei zetu ni pamoja na 
ushuru na haulipi kingine tena (sio kwa magari)

Tupigie:
+44 1375 85 85 25
+44 790 38 28 119
KC GLOBAL LINKS
SUITE 2 CLIPPER HOUSE
TILBURY DOCKS
RM18 7SG



THE DIFFERENCE IS CLEAR
KC TEAM..!

VOA SWAHILI: Zulia Jekundu S1 Ep 108: Sundance Film Festival, A$AP Rocky, Kendall Jenner, Madonna na SuperBowl 51

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 28,2017

Mrisho Mpoto awatembelea watoto wawili wanaoishi na ablinism ambao alijitolea kuwalea

$
0
0
Msanii wa muziki wa asili nchini Mrisho Mpoto, Ijumaa hii amesafiri mpaka Mkoani Shinyanga kwenda kuwajulia hali watoto wake wawili ambao alijitolea kuwalea. Watoto hao ni Pendo pamoja na Simon ambao wanaishi na albinism katika Kituo cha Buhangija Shinyanga ambacho kinalea watoto wenye mahitaji maalumu.
Muimbaji huyo ambaye bado anafanya vizuri na wimbo Sizonje, aliambatana na wadau mbalimbali kutembelea kituoni hapo na kutoa kidogo alichonacho. 
"Kile kidogo kikubwa, nilichopewa na Mh Rais Magufuli, sikusita kusafiri na mpaka Shinyanga kugawana na wanangu Pendo na Simon wanaoishi na albinism hapa shinyanga," alisema Mpoto.
Muimbaji huyo hivi karibuni alifanya show nzuri katika uzinduzi wa Mabasi ya Mwendo Kasi hali ambayo ilipelekea mgeni rasmi ya shughuli hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kuinuka akiwa pamoja na Mkamu wa Rais wa World Bank Africa, Makhtar Diop na kuanza kumtuza mahela.

VIJANA WA CCM WILAYA YA MBEYA MJINI WAADHIMISHA MIAKA 40 YA CHAMA CHA MAPINDUZI JIJINI MBEYA

$
0
0
Vijana wa chama cha mapinduzi (Uvccm) Wilaya ya Mbeya mjini waadhimisha mika 40 ya chama cha mapinduzi Ccm kwa kufanya maandamano ya amani kutoka ofisi za Ccm Mkoa wa Mbeya mpaka eneo la Kabwe na kupanda Miti wakiongozwa na mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini Mh.William Ntinika ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Mbeya mjini.Picha zote na Mr.Pengo Mmg Mbeya.
 Mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini Mh.William Ntinika ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Mbeya mjini akizungumza na baadhi ya vijana wa chama Cha mapinduzi ccm eneo la kabwe mara baada ya kumaliza zoezi la kupanda miti katika eneo hilo la Kabwe.
Mwenyekiti wa Vijana (Uvccm) Ndugu Malanyingi Matukuta nae akizungumza jambo katika maadhimisho ya kilele cha chama cha mapinduzi kutimiza miaka 40 yanayo tarajia kufanyika kitaifa tarehe 5, ya mwezi wa pili Mjini Dodoma.
Katibu wa (Uvccm) wilaya ya Mbeya Mjini.Jeradi Kinawile nae akizungumza machache kwa wanachama wa ccm wilaya ya Mbeya mjini.
 Mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini Mh.William Ntinika ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya mbeya mjini akipanda mti eneo la kabwe jijini Mbeya. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

KIPUTE CHA AZAM NA SIMBA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR HIVI SASA

$
0
0
 Kikosi cha Azam Fc.
 Kikosi cha Simba kilichoanza leo.
 Mshambuliaji wa Timu ya Simba, Pastory Athanas akikabiliana na Mabeki wa timu ya Azam Fc, katika kipute cha Ligi Kuu Tanzania Bara duru la pili, unaoendelea kuchezwa hivi sasa katika uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Azam FC yaongoza kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Mshambuliaji John Bocco.
 Beki wa Azam Fc, Aggrey Moris akiondosha hatari iliyokuwa imeelekezwa langoni kwake.
 Kipa wa Simba, Daniel Agyei akinyaka mpira kwa umaridadi kabisa huku Beki wake, Method Mwanjale akimzuia Mshambuliaji wa Azam, John Bocco asiweze kuufikia mpiara huo.
 Beki wa Simba, Mohammed Hussein akisepa na kijiji cha Azam, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara duru la pili, unaoendelea kuchezwa hivi sasa katika uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Azam FC yaongoza kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na Mshambuliaji John Bocco.


AZAM YAIADHIBU SIMBA KWA MARA NYINGINE, YAICHAPA BAO 1-0 UWANJA WA TAIFA LEO

$
0
0
TIMU ya soka ya Azam imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Mchezo huo ulioanza kwa kila upande kucheza kwa umakini na kutafuta goli la ushindi uliweza kudumu kwa takriban dakika 45 bila timu hizo kufungana.

Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kufanya mabadiliko ya kumtoa Mchezaji wake Mzamiru Yassin na kuingia Shiza Kichuya ili kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji, baadae akaingia  Ibrahim Ajib akichukua nafasi ya Janvier Bukungu aliyeumia.

Mnamo dakika ya 70 ya mchezo, John Bocco akitumia udhaifu wa beki Method Mwanjali aliweza kuifungia timu yake goli la kwanza na la ushindi ambalo lilidumu mpaka dakika 90 za mchezo.

Azam waliendelea kulisakama goli la Simba kutaka kutafuta goli la pili lakini kwa upande wa Simba nao waliendelea kusaka goli la kusawazisha na kufanya mchezo huo, kumalizika kwa ushindi wa goli 1-0 kwa upande wa Azam.

Baada ya matokeo haya, Simba inaendelea kusalia kileleni kwa alama 45, wakifuatiwa na Yanga wenye alama 43 wakiwa na mchezo mmoja mkononi na Azam wakipanda mpaka nafasi ya tatu kwa alama 34.
 Mshambuliaji wa Azam, John Bocco "Adebayor" akiachia shuti kali lililomshinda Kipa wa Simba, Daniel Agyei na kwenda moja kwa moja wavuni na kuipatia timu hiyo bao la ushindi lililodumu mpaka mwisho wa mchezo.
 Mshambuliaji wa Azam, John Bocco "Adebayor" akishangulia baada ya kuifungia timu yake bao la kuongoza na la ushindi.
 Wachezaji wa Azam wakifurahia ushindi wao.
 Beki wa Azam, Yakubu Mohammed akiwania mpira na Mshabuliaji wa Simba, Laudit Mavugo katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo. Azam imeshinda bao 1-0.

AMSHA KIPAJI CHAKO NA MICHUZI TV NA AMMICHIBA WA MBEYA...

RAIS DKT MAGUFULI AELEKEA ADDIS ABABA, ETHIOPIA, KWENYE MKUTANO WA 28 WA WAKUU WA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa  Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa  katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama  katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama  katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wafanyakazi katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati

akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Mungano wa Visiwa vya Comoro Mhe. Azali Assoumani walipokutana kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 tayari kwa safari ya Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU). Rais Assoumani alikuwa akitokea Comoro kupitia Dar es salaam. Picha na IKULU

TANZANIA NA ZAMBIA ZASAINI MAKUBALIANO YA KUANZISHA KITUO CHA PAMOJA CHA FORODHA

$
0
0

Benny Mwaipaja-WFM, Mbeya

TANZANIA na Zambia, zimetiliana saini Mikataba Minne kwa ajili ya uanzishwaji rasmi wa kituo cha pamoja katika mpaka wa Tunduma na Nakonde, kitakachoanza kufanyakazi rasmi Februari mosi mwaka huu, ili kurahisisha ufanyaji biashara kati ya nchi hizo mbili

Uamuzi wa kuanzishwa kwa huduma hiyo ijulikanayo kama One Stop Border Post, ni utekelezaji wa maagizo ya Marais wa nchi hizo Mbili, Waheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, na Edger Lungu, waliyoyatoa wakati Rais huyo wa Jamhuri ya Zambia, Edger Lungu alipofanya ziara ya kikazi hapa nchini hivi karibuni.

Mikataba iliyotiwa saini ni makubaliano ya Mwongozo wa Utendaji wa Kituo cha Pamoja cha Tunduma/Nakonde pamoja na Mfumo wa Urahisishaji Biashara kwa lengo la kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili.

Waliosaini Mikataba hiyo kwaniaba ya Serikali ya Tanzania, Mjini Vwawa, wilaya ya Momba, mkoani Songwe, ni Naibu Katibu Mkuu wa Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda, huku Zambia ikiwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa nchi hiyo, Bi. Kayula Siame.

Wakizungumza baada ya kutiwa saini kwa mikataba hiyo Makatibu wakuu hao wamesema kuwa Uanzishwaji wa Kituo cha Pamoja Mpakani Tunduma/Nakonde, utarahisisha ufanyaji wa biashara kati ya Tanzania na Zambia kwa kupunguza ukaguzi kwani ukaguzi utafanyika mara moja katika kituo cha kuingia badala ya kufanyika mara mbili katika nchi zote mbili pamoja na kuongeza makusanyo ya kodi

“Lengo la kituo hicho pia ni kuifanya biashara kati ya Tanzania na Zambia kuwa huru lakini ikifuata misingi na taratibu za kufanya biashara mpakani. Pia kitarahisisha biashara katika eneo la mpakani na kuvutia wananchi na wafanyabiashara kutoka nchi zote mbili kutumia kituo hiki na kuepuka kutumia njia zisizo rasmi kupitisha mizigo na hivyo kupunguza ufanyaji wa biashara za magendo kama si kukomeshwa kabisa” Alisisitiza Bi. Amina Khamis Shaaban

Alisema kuwa utaratibu huo unatarajia kuona kuongezeka kwa ushirikiano kati ya taasisi za serikali za nchi hizi kwani shughuli katika kituo zitakuwa zinafanyika kwa uwazi katika eneo moja.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakitia saini mmoja wa Mikataba ya kuanzishwa kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Tunduma/Nakonde, ifikapo Februari Mosi, 2017.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakionesha Mikataba ya kuanzishwa kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani baada ya kusainiwa ili kuruhusu kuanzishwa rasmi kwa kituo cha mpakani cha Tunduma/Nakonde, ifikapo Februari Mosi, 2017.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakibadilishana Mikataba ya kuanzishwa kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani Tunduma/Nakonde baada ya kusainiwa ili kuruhusu kuanzishwa rasmi kwa kituo hicho ifikapo Februari Mosi, 2017.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakitia saini moja ya mikataba ya kuanzishwa kwa Kituo Cha Pamoja na Mpakani katika Mpaka wa Tunduma na Nakonde unaotarajiwa kuanza kufanyakazi rasmi Februari mosi, 2017.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakionesha mikataba waliyosaini ili kuruhusu kuanzishwa rasmi kwa Kituo Cha Pamoja cha Mpakani katika Mpaka wa Tunduma na Nakonde unaotarajiwa kuanza rasmi Februari mosi, 2017.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakibadilishana Mikataba waliyosaini ili kuruhusu kuanzishwa rasmi kwa Kituo Cha Pamoja na Mpakani katika Mpaka wa Tunduma na Nakonde unaotarajiwa kuanza rasmi Februari mosi, 2017.

Makatibu Wakuu kutoka Tanzania na Zambia wanaohusika na masuala ya fedha, biashara na viwanda wakiwa katika kikao cha kupitia nyaraka mbalimbali za mikataba ya namna ya kuendesha Kituo cha Pamoja cha Mpakani, Tunduma/Nakonde, uliofanyika Jijini Mbeya. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Miundombinu wa Zambia, Mhandisi Charles Mushota, na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais wa Zambia, Bright Nundwe.


PROF. MBARAWA AITAKA NIT KUENDANA NA MAGEUZI SEKTA YA UCHUKUZ

$
0
0
Serikali imekitaka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), kuboresha mitaala yake ili kuendana na mageuzi makubwa yanayofanywa katika sekta ya uchukuzi hapa nchini.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hayo leo katika mahafali ya 32 ya Chuo hicho na kusisitiza kuwa Serikali itatoa nyenzo zote stahiki kwa chuo hicho ili kukiwezesha kutoa wanafunzi watakaokuwa na soko ndani na nje ya nchi.

“Tumeanza kufanya mageuzi makubwa katika Sekta ya Uchukuzi ambapo tayari tumenunua ndege katika mkakati wa kuboresha usafiri wa anga na hivi karibuni tutaanza ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge), itakayowezesha treni ya kisasa naya mwendo kasi kutoa huduma kwa kuanzia Dar es salaam hadi Morogoro”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Amesema reli ya kisasa itakuwa inatumia umeme ili kuwa na mwendo kasi wa kilomita 160 kwa saa na hivyo kuwezesha usafiri wa Dar es Salaam-Morogoro kuwa wa chini ya muda wa saa mbili.Amesisitiza awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli hiyo utaanza hivi karibuni mara baada ya taratibu za kumpata mzabuni wa ujenzi huo kukamilika.

Amebainisha kuwa katika mwaka wa fedha ujao, Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kukarabati ujenzi wa miundombinu ya chuo hicho ili kukiwezesha kuwa cha kisasa na kitakachotoa elimu bora katika ukanda wa Kusini mwa Afrika na kuhakikisha wahitimu wa fani ya ‘Logistics na Transport Management’ wanapata bodi ya kitaaluma ili kuratibu fani hiyo .


“Hakikisheni mnaimarisha utawala bora, utafiti, ushauri wa kitaalamu, machapisho na huduma yenu iwe ya viwango vya ubora ili kuwezesha wahitimu wenu kupata soko pindi wanapohitimu”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) katika mahafali ya 32 ya Chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho na pembeni yake ni Mkuu wa Chuo hicho Prof. Zacharia Mganilwa
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Prof. Blasius Nyichomba (kulia), akizungumza na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika mahafali ya 32 ya Chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihutubia kongamano la mahafali ya 32 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa fani za Shahada ya Uzamili, Stashahada ya Uzamili, Shahada na Diploma katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alipokuwa akihutubia kongamano la mahafali ya 32 ya Chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

SERIKALI IMESEMAINAFANYA JUHUDI ZA KUOKOA WATU 14 WALIOFUKIWA GEITA

$
0
0
NAIBU waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani ametembelea Mgodi wa RZ uliofukia Watanzania 13 na raia mmoja wa Nchini China anayetambulika kwa jina la Meng Juping na kusema kuwa serikali itaendelea kuweka nguvu ili kusaidia uokoaji.

Katika ziara yake hiyo ya dharura Naibu Waziri huyo ametoa pole kwa niaba ya serikali kwa uongozi wa Mkoa, Wananchi pamoja na Mgodi huo kukumbwa na tukio hilo.

Mara baada ya kupokea taarifa ya maafa hayo, iliyosomwa na kamishina msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria, Dk. Kalemani aliutaka uongozi wa Mkoa pamoja kamati ya uokoaji kujikita zaidi kwenye shughuli ya uokojai na waachane na mambo mengine ambayo yanaweza yakasababisha zoezi hilo liwe gumu.

‘’Ndugu zangu mimi kwa niaba ya serikali kuu napenda nitoe pole kwa hiki kilichowakumba Mkoa pamoja na Mgodi lakini napenda kuwaambia kuwa Kamati ya ulinzi na Usalama pamoja natimu ya uokoaji mhakikishe mnasimamia vyema zoezi hili ili tuwaokoe ndugu zetu ambao wamo humo ndani ya shimo,’’alisema Naibu waziri Kaleman.

‘’Kingine niagize hapa hakikisheni mnatoboa shimo kwa kutumia drilling ili tupate mwanya wa kuwapatia chakula ndugu zetu ambao wamefukiwa na udongo wakati juhudi za kufukua zikiendelea ,’’aliongeza.

Akizungumza na Maduka online mapema asubuhi ya leo kamishina msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria Yahaya Samamba alisema kuwa kamati ya uokozi kwa kushirikiana kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Geita, ilibadilisha mfumo wa uokoaji kwa kutumia wachimbaji wadogowadogo baada ya mashine za kisasa kufikia usawa mita 20 ambazo haziwezi kuhimili uzito.

‘’Mitambo hii imekomea mita 20 tumeona tutumie wachimbaji wadogo ili twende sambaba na uokoaji uliosalama..kwahiyo usiku wa jana (juzi) saa 5:00 kamili usiku tulisitisha kutumia mashie yaani Magreda kutokana na usawa tuliofikia kuwa laini,’’alisema Samamba.
Naibu waziri wa Nishati na madini Dr,Merdadi Kalemani akiwasilia katika mgodiwa wa RZ ambako kumetokea tukio la watu 14 kufukiwa na udongo wakati wakiendelea na kazi za uchimbaji.
Mbunge wa Jimbo la Busanda ,Lorencia Bukwimba akiwapa pole ndugu na jamaa ambao walikuja kujua kile ambacho kitaendelea kwa undugu zao.
Wananchi wakiwa nje ya Ngome ya mgodi wakifatilia kile ambacho kinaendelea
Sehemu ambayo inatumiwa kutolea udongo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Ezekiel Kyunga akiwa katika eneo la tukio akifatilia kile kinachoendelea.


Serikali ya TANZANIA Kujenga Reli Inayotumia Umeme Kutoka Dar es Salaam Kwenda Morogoro

$
0
0
Na Benedict Liwenga

Serikali iko mbioni kujenga Reli ya Kati kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro yenye kutumia umeme ambayo itakuwa ikisafiri kwa kasi ya Kilomita 160 kwa saa.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 32 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Mhe. Mbarawa amesema kwamba kwa sasa Serikali iko katika hatua za mwisho za kumpata mzabuni atakayejenga reli hiyo kwa kiwango cha Kisasa (Standard Gauge).

“Reli hiyo sio Garimoshi, ni reli itayotumia umeme, kwahiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro tutaweza kwenda kwa saa moja na nusu ambapo ndani ya reli hiyo kutakuwa na huduma nzuri na za kisasa ikiwemo huduma ya intaneti na mambo mengine mengi”, alisema Profesa Mbarawa.

Katika hatua nyingine Mhe. Mbarawa amewapongeza Wahitimu wa kozi mbalimbali kwa bidii zao walizozifanya wakati wa masomo yao kuwataka kutumia hazina kubwa ya elimu waliyoipata chuoni hapo kwa manufaa yao binafsi, ya familia na Taifa kwa ujumla.

“Tunasherehekea mahafali haya ya 32 huku chuo kikiwa kimebadilika na kupiga hatua za haraka katika miaka 42 ya kuwepo kwake tangu kianzishwe mwaka 1975, maendeleo makubwa yameonekana na sisi sote ni mashahidi, na maendeleo haya yasingeonekana bila juhudi za pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi pamoja na juhudi za Baraza la Uongozi, Uongozi wa Chuo, nyie Wanafunzi, wadau wengine na Watanzania wote kwa ujumla, nachukua fursa hii kuwapongeza sana kwa kazi kubwa mlioifanya”, alisema Profesa Mbarawa.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Mhandisi Profesa Zacharia M.D Mganilwa amesema kuwa, anaishukuru Serikali kwa ushirikiano mkubwa inaoutoa katika chuo hicho tangu kuanzishwa kwake takribani miaka 42 iliyopita ambapo ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana ikiwemo ongezeko la Wahitimu toka 688 katika Mahafali ya 31 hadi kufikia wahitimu 1,118 katika mahafali hayo ya 32 ya chuo hicho.

Ameongeza kuwa, mafaniko mengine yanaonekana katika upande wa elimu ya mafunzo yatolewayo chuoni hapo, kuwa ni chuo pekee kinachotoa mafunzo katika sekta ya usafirishaji na uchukuzi, hivyo kimekuwa kikitoa mafunzo kuanzia ngazi ya watendaji yaani Astashahada na shahada na pia kwa Mameneja.

Amezitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili chuo hicho kuwa ni upatikanaji wa vifaa vya kufundishia ambavyo huendana na mabadiliko ya kiteknolojia na baadhi ya vifaa hivyo ni aghali, vile vile suala la mahitaji ya Wataalam katika nyanja mbalimbali ambapo miundombinu iliyopo imekuwa haitoshelezi idadi ya wanafunzi wanaosoma chuoni hapo.

Awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo hicho, Mhandisi. Profesa Blasius Bavo Nyichomba amesema kuwa, chuo hicho kwa sasa kipo katika mkakati wa kuendelea kutafuta fedha za kununua vitendea kazi kupitia mapato ya ndani pamoja na fedha toka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

Katika mafahali hayo yaliyofanyika leo 28 Januari, 2017, jumla ya Wahitimu 1,118 wamehitimu katika kozi mbalimbali za Stashahada ya Uzamili, Shahada, Stashahada na Astashahada zitolewazo na Chuo hicho.

PIKIPIKI ZALETA MAFANIKIO KATIKA SEKTA YA ELIMU.

$
0
0
Na. Lilian Lundo – MAELEZO

Mratibu Elimu Kata (MEK) ni mmoja kati ya kiungo kikubwa kati ya ofisi ya elimu ya wilaya na shule za Serikali katika ngazi ya kata ambaye ndiye mfuatiliaji mkubwa wa maendeleo ya elimu ndani ya kata.

Shughuli nyingine zinazofanywa na MEK ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya taalamu ya wanafunzi katika kata yake, kukagua ufundishaji wa walimu, kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi pamoja na kusimamia vikao mbalimbali vya shule zilizoko katika kata yake.

Asilimia kubwa ya Waratibu Elimu Kata walikuwa wanashindwa kufikia malengo ya kazi zao kutokana na changamoto ya usafiri, ambapo wengi wao walikuwa wakitumia usafiri wa baiskeli ambao ha ukuwa usafiri rafiki kutokana na kazi yao ya kukagua shule zote katika kata wanazozisimamia.

Serikali kwa kuliona hilo, kupitia Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-T) ilitoa pikipiki kwa kila MEK katika mikoa ya Dodoma, Kigoma, Lindi, Shinyanga, Simiyu na Mara ili kurahisha ufuatiliaji wa mendeleo ya shule zao kwa urahisi.

Pikipiki hizo zimeleta mafanikio kwa kupunguza idadi ya wanafunzi watoro, kiwango cha ufaulu kupanda kutokana na ukaguzi wa mara kwa mara wa walimu pamoja na matatizo kutatuliwa kwa haraka kufuatia taarifa za shule kufika ofisi za wilaya kwa wakati.

Sweetbert Malimi ni Mratibu Elimu Kata wa Sanzawa Wilaya ya Chemba, Mkoani Dodoma anasema kwamba Pikipiki imemuwezesha kushughulikia kwa wakati matatizo yanayotokea katika shule anazozisimamia tofauti na kipindi ambacho hakuwa na pikipiki.

Anaendelea kusema kuwa, matatizo yalipokuwa yakitokea katika shule anazosimamia yalikuwa yakimsubiri MEK hata kwa mwezi mzima. Lakini sasa hivi hali imekuwa tofauti kutokana na urahisi wa kufikika kuzitembelea kutembelea shule zake hata mara mbili kwa wiki.

MAJALIWA AHITIMISHA ZIARA YA MKOA WA NJOMBE

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na baadhi ya wanawake wa Njombe kabla ya kuondoka kwenye Ikulu ndogo baada ya kuhitimisha ziara yake ya mkoa huo Januari 28, 2017. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Njombe, Luth Msafiri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa wilaya ya Njombe, Luth Msafiri kwenye Ikulu ndogo ya Njombe baada ya kuhitimisha ziara yake ya mkoa huo, Januari 28, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

TAMASHA LA "MAJIMAJI FLAVA" LAFANA I

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi. Leah Kihimbi ambaye alimwakilisha Mhe. Waziri Nape Nnauye akitoa maoni yake kuhusiana na igizo la Tamasha la "MajiMaji Flava" ambalo lilionyesha baadhi ya matukio ya ukatili yaliyofanywa na Wajerumani enzi za ukoloni dhidi ya watu weusi. Tamasha hilo lilifanyika jana 27/01/2017 Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam. 
Waigizaji wa Tamasha la "MajiMaji Flava" wakielimisha jamii kwa vitendo juu ya baadhi ya matukio yaliyowahi kutokea wakati wa kipindi cha ukoloni wa Wajerumani nchini Tanzania 27/01/2017 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wageni waalikwa toka mataifa mbalimbali wakishuhudia maigizo mbalimbali wakati wa Tamasha la "MajiMaji Flava" ambalo lilionyesha baadhi ya matukio ya ukatili yaliyofanywa na Wajerumani enzi za ukoloni dhidi ya watu weusi. Tamasha hilo lilifanyika jana 27/01/2017 Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam. 
Waigizaji kutoka Ujerumani na Tanzania wakitoa burudani ya muziki wakati wa "Tamasha la MajiMaji Flava" lililofanyika jana 27/01/2017 Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Benedict Liwenga-WHUSM).

SHINDANO LA KUMSAKA MLIMBWENDE WA MISS KIBOSHO 2017 JIJINI MWANZA LAFANA.

$
0
0
Shindano la kumsaka mlimbwende wa MISS KIBOSHO 2017 Jijini Mwanza limeanza jana katika viunga vya Kibosho Luxury Bar iliyopo Kiseke Ilemela Jijini Mwanza ambapo wanyange 10 wanawania nafasi hiyo.

Wanyange hao kama wanavyoonekana pichani ni Caren Nestory, Dorice Ezra, Jullieth Michael, Elizabeth Faustine, Christina Lucas, Nasra Ramadhan, Jacline Moses, Denzry Michael, Kephlin Jacob na Aida Gazar.

Shindano hilo limeandaliwa na Raj Entertainment kwa udhamini wa Kibosho Luxury Bar, Wema Salon na Ngenda Salon huku likiwa limelenga kukuza sanaa ya ulimbwende kuanzia za mitaa hadi kitaifa.

Baada ya usiku ya kuamkia leo wanyange hao kuchuana vikali, fainali itafanyika leo kuanzia majira ya saa moja jioni katika viunga hivyo vya Kibosho Luxury Bar Kiseke Jijini Mwanza kwa kiingilio cha shilingi 5,000 tu.
Binagi Media Group
Wanyange wa shindano la Miss Kibosho 2017 wakionesha makeke yao jukwaani
Washereheshaji wakimtambulisha Matron wa Miss Kibosho 2017, Fania Hassan (katikati) ambaye alikuwa Miss Utalii nchini mwaka 2006.
Kila mlimbwende alionesha makeke ya hali ya juu hadi kuwapa wakati mgumu majaji. Kumbuka majaji ni Leonald Kaduguda (kushoto), Mama Ngenda Lutalo (katikati) na Mwl.Tatu Ngelengela (kulia).

Viewing all 110149 articles
Browse latest View live




Latest Images