Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

BENKI YA KILIMO YAJIDHATITI KUWAINUA WAKULIMA

0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TABD) Bw. Francis Assenga akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es saalam kuhusu mikakati ya Benki hiyo kuwainua wakulima wadogo ili waweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. Kushoto ni Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa Benki hiyo, Bw. Albert Ngusaru.
  Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji  wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TABD) Bw. Francis Assenga akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam ambapo alibainisha kuwa Benki hiyo imekuwa ikitoa mikopo kwa wakulima ili kuziba pengo la upatikanaji wa fedha kwenye minyororo ya thamani katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na mazao ya misitu. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara Bw. Geofrey Mtawa na kushoto Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha Bw. Albert Ngusaru.
 Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara Bw. Geofrey Mtawa akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu mpango wa Benki hiyo kuhakikisha kuwa wakulima wote wanawezeshwa ili kuinua kilimo hapa nchini. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji  wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TABD) Bw. Francis Assenga.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania leo Jijini Dar es salaam.

(Picha na Frank Mvungi- Maelezo)


DKT. KIGWANGALLA ATOA SIKU 7 KWA KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA KUMALIZA CHANGAMOTO ZINAZOIKUMBA HOSPITALI YA RUFAA YA KITETE

0
0

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa siku siku 7  kwa Katibu Mkuu kumaliza changamoto zinazoikumba hospitali ya Rufaa ya Kitete iliyopo mkoani Tabora.

Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo alipofanya  ziara ya kushtukiza  katika hospitali ya Rufaa ya Kitete Mkoani Tabora na kukagua miradi ya  chumba cha upasuaji  pamoja na Chuo cha AMOS kilichopo mkoani humo .


“Chumba hiki cha upasuaji na  Chuo vimekamilika mpaka thamani za ndani tangu miaka miwili iliyopita Sababu ni kwamba Serikali yetu haikutoa counter-part funding huku Benki ya Maendeleo ya Afrika  ikiwa imetimiza ahadi yake kwa asilimia mia moja”alisema Dkt. Kigwangalla.


Hata hivyo Dkt. Kigwangalla amesema kuwa amefurahishwa kutekelezwa kwa baadhi ya maagizo aliyoyatoa  kama vile  kuondoa msongamano wa wagonjwa kwenye wodi za wanawake wajawazito na watoto.


Kwa mujibu wa Dkt. Kigwangalla amesema kuwa uongozi wa Hospitali hiyo umefanikiwa  kuboresha huduma ya upatikanaji wa dawa zote muhimu na huduma kwa wateja ikiwemo  lugha nzuri kutoka kwa wahudumu imeboreshwa..


Aidha Dkt. Kigwangalla amesema anashukuru uongozi wa Hospitali hiyo kwa kufanya ukarabati mkubwa wa majengo ya wodi za wagonjwa na sasa hakuna tena msongamano na huduma zinatoka kwa wakati sahihi.

MUHIMBILI YATOA MSAADA WA VITANDA KWA HOSPITALI YA WILAYA YA KIBITI LEOA

0
0
Katika kuendelea kuboresha mazingira ya utoaji huduma ya afya ya uzazi kwa kina mama, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imetoa msaada wa vitanda viwili vya kujifungulia kwa Hospitali ya Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani. 

Akikabidhi vitanda hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili , Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Agnes Mtawa amesema lengo ni kuboresha huduma za afya na kumuwezesha mama kujifungua katika mazingira salama. 

"Wenzetu wanahuitaji mkubwa wa vitanda vya kujifungulia hivyo tumeona tuwasaidie, natoa wito kwa Watanzania watambue kwamba hospitali hizi ni za kwetu na zinawahudumia Watanzania hivyo wale wenye nafasi ya kusaidia ni vema wakafanya hivyo ili kuendelea kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto" amesema Sister Mtawa. 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo wa Huduma za Uuguzi na Ukunga tatizo la ukosefu wa vitanda husababisha Mkunga kupata shida wakati mama anapojifungua. 

Naye Mhandisi Ujenzi wa Halmashauri ya Kibiti, Ayub Ngereza akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa wilaya ya Kibiti, ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa msaada huo kwani utasaidia kuboresha huduma za afya. 

Hivi karibuni Hospitali ya Taifa Muhimbili ilikabidhi msaada wa vitanda vitano vya kujifungulia kwa Hospitali ya wilaya ya Mafya ambapo kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Abdalah Bhai walihitaji vitanda vitano ambao ulikidhi mahitaji.
 Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agenes Mtawa akimkabidhi vitanda Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Kibiti, Ayub Ngereza kutokana na hospitali ya halmashauri hiyo kuwa na upungufu wa vitanda vinavyotumiwa na kinamama wakati wa kujifungua. Mhandisi Ngereza amepokea msaada wa vitanda hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Kibiti. 
 Mhandisi Ngereza akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kukabidhiwa vitanda hivyo na uongozi wa hospitali hiyo.
 Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga, Mtawa katika hospitali hiyo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada huo kwa Halmashauri ya Kibiti. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Halmashauri hiyo wakipakia vitanda hivyo kwenye gari leo

RUVU SHOOTING MIKONONI MWA MBAO LEO, WAPANIA KULIPA KISASI

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Timu ya Ruvu Shooting leo inashuka dimbani katika uwanja wa CCM Kirumba kupambana na Wauza Mbao wa Mwanza, Mbao Fc katika mchezo wa ligi kuu utakaokuwa wa ushindani huku Ruvu wakitaka kulipa kisasi cha goli 4-1 waliyofungwa kwenye mzunguko wa kwanza kwenye Uwanja wa Mabatini Pwani.

Ruvu watawakosa Shaban Kisiga ambaye ni mgonjwa pamoja na Jabir Aziz anayetumikia kadi tatu za njano.

Kikosi cha Ruvu Shooting leo
Jan 27, 2017
CCM Kirumba
Mbao FC vs Ruvu Shooting

Ruvu Shooting Line Up
1. Abdallah Rashid 1
2. Abdul Mpambika 12
3. Yusuph Nguya 2
4. Renatus Kisase 5
5. Damas Makwaya 20
6. Zuberi Dabi 24
7. Ayoub Kitala 7
8. Baraka Mtuwi 15
9. Ismail Mgunda 27
10. Fully Zulu Maganga 28
11. Abdurahman Mussa 17

Sub
GP Bidii Hussein 18
2. Said Madega 19
3. Shaibu Nayopa 26
4. Said Dilunga 3
5. Shabani Msala 4
6. Chande Magoja 21
7. Alex Seth 22

WAZIRI KAIRUKI AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA WAKALA ZA SERIKALI AZITAKA ZIFANYE KAZI NA KUJITEGEMEA

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akifungua mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro akiongea na Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali nchini, leo jijini Dar es salaam, kushoto kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb)
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA), Dkt. Jabiri Bakari akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali leo, jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Henry Mambo (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali nchini leo, jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akisikiliza mada pamoja na washiriki wengine wakati wa mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali nchini, uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Washiriki wa mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali nchini wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala hizo nchini leo, jijini Dar es salaam.

MADEREVA WAKANUSHA TAARIFA ZA KUWEPO KWA MGOMO

0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWA) Bw. Shabani Mdemu (kulia) akikanusha taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya mitandao ya kijamii hapa nchini kuwa madereva wamepanga kufanya mgomo mapema mwezi Februari, amesema chama hicho hakijapanga mgomo wowote kama ilivyotangazwa hivyo wananchi wapuuze taarifa hizo kwa kuwa si za kweli. Kushoti ni Msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Ridhiwani Wema.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi Wasafirishaji kwa Njia ya Barabara Bw. Salum Abdallah akitoa wito kwa wananchi kupuuza taarifa za kuwepo kwa mgomo wa madereva kama ilivyoripotiwa na baadhi ya mitandao ya kijamii na kuliomba Jeshi la Polisi kuchukua hatua kwa wote waliohusika kusambaza taarifa hizo za upotoshaji. Kulia ni Mwenyekiti wa chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWA) Bw. Shabani Mdemu.
Msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Ridhiwani Wema akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu taarifa za upotoshaji kuhusu kuwepo kwa mgomo wa madereva zilizosambazwa kupitia mitandao ya kijamii.


(Picha na Frank Mvungi-Maelez

SITAKI TENA KUSIKIA MSAMIATI “MRADI UKO CHINI YA KIWANGO”, RC NCHIMBI AAGIZA.

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi au “mama Nchimbi” kama anavyojulikana jana amefanya ziara ya kikazi Wilaya ya Mkalama na kuagiza watendaji kusimamia miradi kwa umakini kwakuwa hataki kusikia mradi wowote uko chini ya kiwango.

Dkt. Nchimbi amesema msamiati chini ya kiwango hataki kuusikia kwakuwa umekua ukifanya watendaji kuwa wazembe na kuongeza kuwa hatua kali zitachukulkiwa kwa viongozi wote ambao hawatasimamia ipasavyo utekelezaji wa maelekezo hayo.

Ameongeza kuwa watendaji wamekuwa wakiilalamikia serikali na kuirudisha nyuma kwa kutotekeleza majukumu yao ipasavyo na hivyo kupelekea wananchi kuona serikali haifanyi chochote wakati inaleta pesa nyingi za miradi mbalimbali ambapo jukumu la watumishi ni kusimamia miradi ili ifanye kazi ipasavyo.

Dkt. Nchimbi amesema viongozi wote kabla ya kusaini mikataba yoyote ya halmashauri wanapaswa kukiri thamani ya mali zao zinazohamishika na zisizohamishika ili kama mradi utatekelezwa chini ya kiwango, mali zao zitumike kufidia pesa ya serikali iliyopotea.

“Mradi wakati unajengwa Mkurugenzi, Mwenyekiti wa halmashauri na wataalam wanauangalia bila kusema chochote, ukikamilika ndio wanakuambia umejengwa chini ya kiwango, kuanzia sasa sitaki kusikia msamiati wa ‘chini ya kiwango’ na endapo ikitokea chini ya kiwango tutahakikisha fedha ya serikali inarudi”, amesema Dkt. Nchimbi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi akipanda viazi lishe katika shamba la Mkulima wa viazi katika kijiji cha Nkungi Wilayani Mkalama katika ziara yake wilayani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akipanda viazi lishe katika shamba la Mkulima wa viazi katika kijiji cha Nkungi Wilayani Mkalama.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Jakson Masaka akishiri kupanda viazi lishe katika shamba la Mkulima katika kijiji cha Nkungi Wilayani humo.

MTU MMOJA AUWAWA KWA TUHUMA ZA WIZI WA MKOANI MWANZA

0
0

MTU mmoja Mkazi wa Kijiji cha Kanyelele , Safari Bungate (51) ameuawa na kundi la watu waliojichukulia sheria mkononi kwa kumpiga mtu huyo mawe na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya kuiba kuku katika  nyumba ya mmiliki wa kuku, Tetema mathias (40), mkulima na mkazi wa kijiji cha Kanyelele, kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu, Kamishina, Ahmed Msangi amesema tukio hilo limetokea  Januari 26  mwaka huu majira ya saa nne usiku katika kijiji cha Kanyelele tarafa ya Usagara Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Taarifa  hiyo inadaiwa kuwa mwenye nyumba, Tetema Mathias akiwa amelala  na familia yake, alikuja mtu/marehemu akaingia ndani kupitia dirishani na kuiba kuku mmoja, ndipo wakati alipokuwa anataka kuondoka Mathias alimuona na kuanza kupiga yowe ya mwizi akiomba majirani waje wamsaidie kumkamata huku akimkimbiza barabarani.

Hata hivyo taarifa ilidai kuwa  watu/ majirani waliamka na kufanikiwa kumkamata  marehemu akiwa na kuku amemshikilia kisha wakaanza kumpiga  kwa mawe na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake  kitendo kilichosababisha  mtu/ marehemu huyo  kupoteza fahamu na baada ya muda mchache  alifariki dunia.  

Taarifa  ya Kamanda Msangi amesema raia wema walitoa taarifa polisi ndipo askari walifika eneo la tukio na kukuta mtuhumiwa wa wizi akiwa tayari amefariki dunia na mwili wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi na daktari na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.

Jeshi la Polisi linamshikilia Tetema Mathias kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo. Naibu, Kamishina Msangi ametoa  wito kwa wakazi wa Jiji na Mkoa wa Mwanza, akiwataka kuacha tabia ya kujichulia sheria mkononi kwani ni kosa la jinai, aidha anawataka wananchi pindi wanapomkamata mhalifu wamfikishe katika vyombo vya sheria ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.


RAIS DKT MAGUFULI AKUBALI OMBI LA KUJIUZULU WADHIFA WAKE DC WA UYUI MKOANI TABORA

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MJINI NJOMBE PIA ATEMBELEA MAJENGO YA POLISI YANAYOJENGWA LUDEWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka kesho awapeleke wakaguzi wa heshabu kwenda kukagua mapato na matumizi ya  Mamlaka ya Maji ya Mji wa Njombe (NJUWASA).

Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Januari 27, 2017) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Mpechi, Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Waziri Mkuu amesema wakaguzi hao mbali na kukagua mapato na matumizi ya mamlaka hiyo pia waangalie kama wananchi walihusishwa katika ukokotoaji wa gharama za malipo ya bili za maji.

Ametoa agizo hilo baada ya wananchi kuilalamikia mamlaka hiyo kupitia mabango kwamba wanatozwa bili kubwa ya maji licha ya huduma hiyo kupatikana kwa kusuasua katika mji huo.

Kufuatia malalamiko hayo Waziri Mkuu alimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa NJUWASA, Bw. Daudi Majani kutoa ufafanuzi juu ya jambo hilo ambapo alisema kwa mwezi wanakusanya sh. milioni 75 zinazotumika kuendeshea na uboreshaji wa huduma.

“Maji hakuna unasema unaboresha unaboresha huduma gani? Wananchi wanalalamika maji hakuna na mnawatoza gharama kubwa, Mkuu wa Mkoa kesho peleka wakaguzi wakakague kwa mwezi anakusanya kiasi gani na anafanyia nini,”

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma kujiwekea utaratibu wa kwenda kwa wananchi na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuzitafutia ufumbuzi badala ya kujifungia maofisini.

“Uwepo wa mabango mengi kwenye mikutano ya hadhara ya viongozi ni ishara tosha kwamba watendaji hamuendi kwa wananchi kuwasikiliza kero zao. Mabango mengi hapa si ya Waziri Mkuu ni hapahapa,” amesema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, JANUARI 27, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa mpira wa shule ya sekondari ya Mpechi mjini Njombe Januari 27, 2017.
 Mmoja wa wananchi waliofika kwenye uwanja wa  mpira wa Shule ya Sekondari ya Mpechi mjini Njombe akitoa dukuduku lake kwa njia ya karatasi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa mpira wa Shule ya Sekondari ya Mpechi, Januari 27, 2017. 
   Wananchi wa Mji wa Njombe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara  kwenye uwanja wa mpira wa Shule ya Sekondari ya Mpechi Januari 27, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa mji wa Njombe wakati alipowasili kwenye uwanja wa  mpira wa Shule ya Sekondari ya Mpechi kuhutubia mkutano wa hadhara Januari 27, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua nyumba za Askari Polisi ambazo kwa muda mrefu hazijakamilika katika mji wa Ludewa Januari 27, 2017.

SERIKALI KUTUMBUA WAHUJUMU WA TAZARA

0
0
Na Chalila Chibuda

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, 
Profesa  Makame  Mbarawa  amesema Serikali haitamvumilia mtumishi yoyote ambaye ataendelea kuisababishia hasara Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kwa kuendelea kuihujumu na kusababisha mamlaka kujiendesha kwa hasara.



Profesa Mbarawa ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Tazara, kuangalia utendaji ambapo amebaini matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa na Serikali na kuahidi kuchukua hatua stahiki.



“Ninafahamu kuna watu 10 hapa ambao wao ni chanzo kikubwa cha matumizi mabaya ya fedha na miongoni mwao wapo Watanzania na Wazambia, nawahakikishia kuwa kila atakayetumia vibaya fedha zinazotolewa na Serikali hatutamvumilia kwenye Serikali hii’, amesema Prof. Mbarawa.



Profesa Mbarawa amesema kumekuwa na idadi kubwa ya watumishi ambao hawana tija na kuagiza menejimenti ifanye uhakiki na kubaini mahitaji halisi ya Watumishi na watakaobainika kuzidi wahamishiwe ofisi ya tazara Mkoa waDar es Salaam.



Aidha Prof. Mbarawa ameuagiza uongozi wa Tazara Makao Makuu kuacha mara moja kutumia mtandao ya kampuni binafsi kutuma taarifa za Ofisi na kuagiza kuanza kutumia mtandao wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) mara moja.



‘Nikirudi tena hapa sitaki kuona mnatumia mitandao wa Kampuni binafsi kutuma taarifa za kiofisi ninawaomba muhakikishe mnatumia  mtandao wa TTCL’ amesisitiza Prof. Mbarawa.



Kwa upande Meneja wa TAZARA Mkoa wa Tanzania, Bw. Fuad Abdalla amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa mkoa umejipanga vizuri kuhakikisha changamoto zote zinatatuliwa na Mamlaka inajiendesha kibiashara.



‘Kama mkoa tumekuja na mikakati mizuri ya kutumia mifumo ya Tehama kama njia ya  udhibiti wa mapato, kama ulivyona hivi sasa tunakamilisha mfumo wa Tehama tunaoutumia kufatilia treni kila inapoondoka kwenye Stesheni ya Makao Makuu Dar es Salaam na mfumo huu ukikamilika tutawaashawishi na wenzetu wa Zambia kutumia mfumo huu ili tuweze kudhibiti upotevu wa mapato’ Amesisitiza Bw. Fuad Abdalla.



Bw. Fuad ameongeza kuwa pamoja na mifumo mipya ya Tehama Tazara inaendeleza kwa kasi ukarabati wa mabehewa ya abiria na mizigo ili kuongeza tija na kuiwezesha Mamlaka kupata faida.


 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akimsikiliza mmoja wa wataalam wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), akimweleza namna  wanavyosimamia mafuta yanayotumika kwenye treni za Mamlaka hiyo, alipowatembelea jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Karakana ya Dar es Salaaam ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), Eng. Timothy Kayani, akimwonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa vipuri vya treni vilivyotengenezwa katika karakana hiyo jijini Dar es Salaam, alipotembelea karakana ya Mamlaka hiyo kuona utendaji wake.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akiangalia behewa la treni lililofanyiwa ukarabati na kukamilika katika karakana ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), alipotembelea karakana hiyo jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Karakana ya Reli Dar es Salaaam ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), Eng. Timothy Kayani, akifafanua namna behewa la treni linavyoanza kufanyiwa ukarabati kwa   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto) katika karakana hiyo, wakati Waziri huyo  alipotembelea kuona utendaji wake. Wa pili kushoto ni Meneja wa TAZARA Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Fuad Abdalla.
 Mtaalam wa mifumo ya Tehama wa Kampuni ya Qmax Bi. Jenirose Jabakila akimweleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, namnamfumo walioutengeneza wa kufatilia treni inapokuwa njiani unavyofanya kazi, wakati alipotembea Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akifafanua jambokwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), alipotembelea mamlaka hiyo kuona utendaji kazi.


Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Article 2

LIVE: President Trump Holds a Joint Press Conference with Prime Minister Theresa May of the United Kingdom

0
0

Kwa hisani ya White House

Bidhaa za Mexico kutozwa kodi Marekani, kufidia ujenzi wa ukuta

0
0
Ikulu ya Marekani imesema Rais wa nchi hiyo Donald Trump anaweza kutoza asilimia 20 ya kodi kwa bidhaa zinazoingizwa nchini humo kutoka Mexico ili kuweza kusaidia mpango wa kujenga ukuta kati ya nchi hizo mbili kuzuia kuingia kwa Wahamiaji haramu na madawa ya kulevya.

Mexico imesisitiza kuwa haitolipia gharama za ujenzi wa ukuta huo na kwamba pendekezo hilo jipya lililotolewa litasababisha kuzidisha ufa wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili na kusababisha Rais Enrique Pena Nieto kufuta ziara yake ya kukutana na Rais Trump wiki ijayo mjini Washington.

Uamuzi wa Rais Pena Nieto umeungwa mkono nchini mwake, akiwemo pia mtangulizi wake Vicente Fox.

Bwana Fox amesema ana uhakika Mexico italipiza kisasi kwa kutoza kodi bidhaa zitokazo Marekani, iwapo mipango hiyo ya Rais Trump itatimizwa.

Katika Hatua nyingine Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May atakuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kukutana na Rais Trump.

Katika ziara yake nchini Marekani tayari amekutana na wanachama wa Republican mjini Philadelphia ambapo amesema Uingereza na Marekani hazipaswi kurudi katika kile alichokiita sera za uvamizi zilizoshindwa, walizokuwa wakizitumia awali.

Hata hivyo amesema nchi hizo mbili bado zina jukumu la kuongoza dunia.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

0
0

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameagiza kuwachukulia hatua watumishi wa wilaya ya Ludewa kutokana na upotevu wa fedha za ujenzi wa ofisi ya halmashauri. https://youtu.be/x8ecaTOIXuk

SIMU.TV: Mkoa wa Mtwara unakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa zaidi ya elfu mbili jambo linalo sababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu mkoani humo. https://youtu.be/3eBUgjh765M

SIMU.TV: Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi vijana na ajira Anton Mavunde amekitoza faini kiwanda cha kuzalisha nywele za wanawake aina ya Stella kwa kosa la kutokuwa na vifaa vya usalama mahali pa kazi kwa wafanyakazi wake. https://youtu.be/J69LAxOC_xo

SIMU.TV: Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan ameishukuru serikali ya India kwa ufadhili wake wa miradi ya maji katika miji kumi na saba hapa nchini. https://youtu.be/ZH2Os6rnW88

SIMU.TV: Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha inatoa huduma bora za afya kwa mama na mtoto na kukabiliana na vifo vya mama na mtoto vinavyosababishwa na uzembe. https://youtu.be/xohyKwd2QnQ

SIMU.TV: Serikali mkoani Dodoma imewataka wafanyabishara wa mkoa huo kutumia fursa ya kuanzishwa kwa kituo cha biashara cha benki ya NMB ili kukuza mitaji yao. https://youtu.be/SIUZSDWIsAM

SIMU.TV: Serikali imesema itendelea kuhimiza wafanyabiashara na wakulima hapa nchini kuongeza thamani kwa bidhaa wanazozalisha ili kupanua wigo wa biashara na mataifa ya nje. https://youtu.be/81UPJPnS9pc

SIMU.TV: Soko kuu la wilaya ya Liwale mkoani Lindi limeelezwa kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa vyoo vya uhakika. https://youtu.be/KA5WWh1RRSs

SIMU.TV: Serikali imeufungulia uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam na kuruhusu kutumika kwa mchezo kati ya Simba na Azam hapo kesho. https://youtu.be/aPoodwGb8Ck

SIMU.TV: Vinara wa ligi kuu Tanzania bara hapo kesho wanatarajia kuwa wenyeji katika mchezo wao dhidi ya Azam fc utakao chezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. https://youtu.be/Zxoh3ir9SDU

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt. Binilith Mahenge amelazimika kuitisha kikao cha dharura kwa viongozi wa soka mkoani humo kujadili namna ya kuinusuru timu ya Maji Maji kushuka daraja. https://youtu.be/gPCjM5-EjZ4

Invitation for Application for Admission of Postgraduate Programmes for 2017-2018 Academic Year

Tume ya Mipango kuanza Safari ya kuhamia Dodoma Mwezi Machi mwaka huu

0
0
Na Adili Mhina
Katika kuitikia na kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la Serikali kuhamia Dodoma, Tume ya Mipango inatarajia kuanza kuhamisha watumishi wake kuelekea Makau Makuu ya Nchi ifikapo mwezi Machi Mwaka huu. 
Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri alipokutana na watumishi wa taasisi hiyo Ijumaa Januari 26, 2017 kwa lengo la kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu taasisi hiyo.
Pamoja na agenda zingine kujadiliwa katika kikao hicho, suala la kuhamia Dodoma lilionekana kuchukua nafasi kubwa miongoni mwa wafanyakazi mara baada ya ratiba ya zoezi hilo kutolewa rasmi ambapo wengi walionesha kufurahishwa na kutendo cha kutimiza ahadi ya Rais kwa wananchi ya kuhamia Dodoma.
Mwanri alieleza kuwa Tume ya mipango itahamisha watumishi wake katika awamu tatu ambapo makundi mawili yanatarajiwa kuhamia Dodoma ndani ya mwaka huu.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri Akiongea na watumisi wa Tume ya Mipango (hawapo pichani) wakati wa mkutano wake na watumishi hao. Kulia ni Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia Klasta ya Sekta za Uzalishaji Bw. Maduka Kessy na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bw. Abdulrahman Mdimu akifuatiwa Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe. 

MAMA ALIYE MWAGIWA TINDIKALI NA MUAJIRI WAKE MKOANI MBEYA.

Mamelodi Sundowns FC ya Afrika Kusini kutua mwisho wa mwezi, kucheza na simba na Yanga Dar es salaam

0
0
 Mabingwa wa soka barani Afrika Mamelodi Sundowns FC ya Afrika Kusini wanatarajiwa kuwasili nchini mwisho wa mwezi huu kwa mwaliko wa klabu ya African Lyon. 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa  African Lyon, Rahim Kangezi, Mamelodi wanatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam Januari 30, 2017 na kucheza michezo miwili ya kirafiki na Simba SC na Yanga.

 “Mamelodi wanakuja Tanzania kuiunga mkono Tanzania katika kampeni yake ya “LINDA TEMBO WETU” ambayo ni mahususi kupiga vita ujangili na biashara haramu ya pembe za tembo. 
Kangezi amesema mchezo wa kwanza Mamelodi watacheza na February 1, 2017 na Simba na February 3, 2017 watachuana na Yanga.





TRA yatwaa Tuzo ya Ubunifu wa Miradi kwa Sekta za Afrika

0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imepata tuzo kutoka Umoja wa Afrika (AU) kutokana na mfumo wa Uondoaji Mizigo Bandarini (TANCIS) ambao unafanya kazi kwa ufanisi na uharaka zaidi pamoja na kudhibiti mianya ya rushwa.

Tuzo hiyo imetolewa na Umoja wa Nchi za Afrika jijini Addis Ababa Ethiopia,   baada ya kufanyika shindano la Taasisi za Serikali za Umoja wa Nchi hizo kutokana na kuboresha mifumo ya utendaji kazi katika taasisi zao.

Akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kisiga amesema kuwa TRA na Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) ndiyo taasisi pekee za Serikali zilizoweza kufanya vizuri katika ubunifu katika utendaji wa taasisi hizo.

“Tuzo hizi zinatolewa na nchi za Umoja wa Afrika kwa taasisi za Serikali ambapo hushindanishwa katika masuala ya ubunifu katika utendaji kazi wa taasisi husika,” alisema Bi. Mindi.

Akizungumza kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata,  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Richard Kayombo alisema TRA imeshinda tuzo hiyo kutokana na ubunifu wa mfumo wa TANCIS ambao umeundwa kwa kuzingatia kanuni za hali ya juu za kiteknolojia kwa lengo la kuongeza ufanisi, uharaka, uwazi na uhakika katika usimamizi wa masuala ya forodha. 

Meneja Mifumo ya Kielektroniki ya  Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  Bw. Tinkasimile Felix (kushoto) akipokea tuzo ya ubunifu wa mfumo wa TANCIS kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasilianokutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga. Mfumo huu wa TANCIA umeundwa kwa kuzingatia kanuni za hali ya juu za kiteknolojia kwa lengo la kuongeza ufanisi, uharaka, uwazi na uhakika katika usimamizi wa masuala ya forodha.
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images