Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Bodi ya Mahusiano ya Kigeni kwenye masuala ya Kiuchumi nchini Uturuki (DEIK) wameingia makubaliano kuanzisha Baraza la Kibiashara baina ya nchi mbili,makubaliano hayo yalifikiwa tarehe 23 Januari 2017 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF),Godfrey Simbeye amesema Baraza hilo litakuwa na majukumu na shughuli mbalimbali kama kusaidia kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili,kutoa mchango katika kuanzisha kukuza Viwanda kupitia ushirikiano wa Teknolojia wa mashirika na Taasisi za Kiuchumi za nchini Uturuki.
Pia amesema kuratibu juhudi za pamoja kukusanya,kuunganisha,

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF),Reginald Mengi amesema kuwa Baraza hilo la Kibiashara baina ya Uturuki na Tanzania litagawa katika kamati za Kitaifa mbili.Kila kundi litakuwa na Wanachama wake na Taasisi za Kiuchumi au za Kibiashara.
Amesema kuwa Kamati hizo ndogo za Baraza zinatarajiwa kukutana angalau Mara moja kwa Mwaka,kutazama na kujadili mafanikio ya Baraza kwenye masuala ya Kibiashara,Uwekezaji,
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini,Reginald Mengi akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Uundwaji wa Baraza la Kibiashara baina na Tanzania na Uturuki.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF,Godfrey Simbeye akizungumzia majukumu ya Baraza lilioundwa kati ya nchi mbili za Tanzania na Uturuki.Kushoto ni Mwenyekiti wa TPSF,Reginald Mengi.