Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1524 | 1525 | (Page 1526) | 1527 | 1528 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ) ya Jijini Mwanza, Deborah Mallaba, akikagua shamba la hekari mbili la taasisi hiyo ambalo lina mkusanyiko wa matunda na mbogamboga za aina mbalimbali, lililopo Igombe Ziwani, Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.

  Na Binagi Media Group

  Taasisi ya AMI-TZ inajihusika na kilimo cha matunda na mbogamboga kama vile matikiti maji, nyanya, bamia, nyanya, pilipili mbuzi na aina nyinginezo nyingi.

  Baada ya mavuno, taasisi hiyo hufanya usindikaji wa mazao kwa ajili ya kuwafikishia wateja wake majumbani, maofisini na mengine huuzwa moja kwa moja shambani.

  "Baadhi ya vijana ukiwaeleza suala la kilimo wanakuona kama vile umepitwa na wakati lakini wale wanaojitambua wameingia kwenye kilimo na kinawalipa. Hivyo niwahamasishe watumie muda wao vizuri kwa kujishughulisha kwenye kilimo hivyo wasisubiri tu kazi za maofisini". Anasisitiza Deborah Mallaba, Mwanahabari na Mkurugenzi wa Taasisi ya AMI-TZ.

  Mallaba anawasisitiza viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya Kata hadi Wilaya, kuongeza jitihasa za kuwakusanya vijana pamoja na kuwapatia mitaji ikiwemo pembejeo ili wajikite kwenye kilimo maana kilimo ni biashara na kinalipa ambapo pia hatua hio itasaidia kupunguza vijana mitaani.

  "Napenda kuwaambia akina dada waamuke maana si vyema kuzurura tu wakisema hakuna ajira. Mfano mimi nimeanza kujiwekea kipato changu kupitia kilimo na nataka kuwa mafano bora kwa vijana wengine". Anasisitiza Aneth Shosha ambaye ni Afisa Masoko wa taasisi ya AMI-TZ huku akiwakaribisha vijana wengine kwenye taasisi hiyo ili wajifunze zaidi kuhusu kilimo.
  Aneth Shosha ambaye ni Mratibu/ Afisa Masoko wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ), akimwagilia maji kwenye shamba la bamia.
  Wachapa kazi wakichakarika.
  Mfumo wa umwagiliaji kwa kutumia mashine kutoka Ziwa Victoria ndio hutumika kwenye shamba hili.

  0 0

  Mshauri maalumu wa Rais wa Gambia, Adama Barrow amesema zaidi ya dola za Kimarekani milioni 11 zinaaminika kutoweka katika hazina ya serikali, kufuatia kuondoka madarakani kwa mtawala wa muda mrefu Yahya Jammeh.

  Mia Ahmad Fatty amewaambia Waandishi wa habari katika mji mkuu wa Senegal Dakar kwamba wataalamu wa masuala ya fedha wanatathmini kujua ni kiasi gani kwa sasa kimepotea. Amesema Gambia kwa sasa ina tatizo kubwa kifedha kwa hazina yake kutokuwa na kitu.

  Kwa sasa Rais Barrow amekuwa akifanya kazi na timu ya wataalamu wa masuala ya fedha na wengine kutoka Benki kuu ya nchi hiyo kupata kiasi halisi kilichopo.

  Habari zinasema magari ya kifahari na mali nyingine zilionekana zikipakiwa katika ndege ya mizigo ya Chad kwa niaba ya Rais Jammeh siku alipoondoka nchini humo.

  Maelfu ya watu walikusanyika katika Ikulu ya nchi hiyo jana jioni wakiyaangalia majeshi ya Senegal yakiingia kwa ajili ya kuweka usalama kabla ya kurejea nchini kwa Adama Barrow.

  Rais Barrow yupo nchini Senegal na bado haijulikani ni lini hasa atarudi Gambia na kuingia ofisini.
  Alisema atarejea tu baada ya kuhakikishiwa usalama wake.chanzo: BBCSwahili

  0 0

   Basi la abiria mali ya Kampuni ya Kimbilinyiko lenye namba za usajili T 440 DCW likiwa limegongana na Gari ndogo aina ya Nissan Hardbody pickup yenye namba za usajili SU 37965, katika ajali iloyotokea jana jioni eneo la Miseyu, Barabara kuu ya Morogoro - Dar es salaam. inadaiwa mtu mmoja alipoteza maisha na wengine kujeruhiwa. chanzo cha ajali hakikuweza patikana kwa haraka.Picha na Josephat Mmbando.
   
  Gari hizo zinavyoonekana kufuatia ajali hiyo.
  Sehemu ya Mashuhuda pamoja na abiria waliokuwemo kwenye basi hilo.

  0 0

  Mmoja wa wageni kutoka nchini Uturuki akiulizia bei ya vifaa vya mapambo ya bahari kwa mchuuzi wa samaki katika soko la Kimataifa la Samaki, feri jijini Dar leo.
  Kundi la Wafanyabishara na wanahabri wakiwasili katika soko la Samaki Feri .
  wauza Samaki wakiwa katika mnda wa Samaki katika eno la mauzo sokoni hapo.
  Boti ya uvuvi ikiwasili katika soko la Samaki Feri kwa ajili ya kupakua Samaki 
  Mchuuzi wa Samaki wa soko la Samaki feri akimkata kata samaki aina ya Songoro kwa ajili ya kupeleka mtaani kuuzwa.
  Wafanyabiashara wa Samaki wa soko la Samaki Feri wakipara Samaki 
  Baadhi ya wageni kutoka nchini Uturuki wakila Samaki aina ya Pweza katika Soko la Samaki feri walipozuru katika soko hilo kabla ya kwenda kwenye hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu-Magogoni,jijini Dar leo.
  Baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchini Utruki wakipiga picha sehemu ya maandhari ya soko la Samaki Feri kabla ya kuingia katika mkutano na Rais Dkt John Pombe Magufuli,Ikulu jijini Dar.
  Mmoja ya Mwandishi wa habari kutoka nchini Uturuki akiuliza maswali kwa muuzaji wa Samaki wa soko la Samaki feri jijini Dar es Salaam

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


  KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, leo saa 10.00 jioni itakuwa kibaruani kupambana na Cosmopolitan katika mchezo wa raundi ya tano ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup), utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.


  Azam FC inaingia kwenye mchezo huo  leo ikiwa imejidhatiti vilivyo kuweza kuanza vema kwa kupata ushindi na kuitupa nje timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Pili (SDL) na kutinga raundi ya 16 bora. Kwa muda wa siku tatu, Azam FC imefanya mazoezi makali kujiandaa na mchezo huo, na itakumbukwa kwenye mtanange wa mwisho iliyotoka kucheza ukiwa ni wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), matajiri hao walilazimishwa suluhu ya bila kufungana na Mbeya City.

  Kuelekea mchezo huo Nahodha wa timu hiyo, John Bocco ‘Adebayor’, atakuwa akirejea kucheza dhidi ya timu yake hiyo ya zamani ambayo ndiyo imemtoa hadi kupata nafasi ya kusajiliwa na Azam FC miaka tisa iliyopita wakati ikishiriki ligi ya madaraja ya chini na kuipandisha rasmi Ligi Kuu mwaka 2008 baada ya kufunga mabao mawili yaliyoipandisha daraja Azam FC walipoichapa Majimaji ya Songea 2-0.

  Nahodha huyo Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, amepanga kuipa heshima maalumu Cosmopolitan leo kwa kutoshangilia bao atakalofunga kutokana na kutambua mchango wao wa kumtoa hadi kusajiliwa na Azam FC.

  “Ni jambo zuri sana kucheza dhidi ya timu yako ya zamani, najisikia furaha sana ni moja ya mchezo mzuri kwangu na nitacheza kwa nguvu ili niweze kuisaidia timu yangu iweze kupata matokeo mazuri, siwezi kushangilia nikifunga bao, ile ni timu yangu ambayo imenitoa,” alisema.

  Bocco alisema kuwa wao kama wachezaji wanamorali kubwa kwa ajili ya kucheza mchezo huo, huku akidai kuwa wamejipanga kupambana uwanjani kuhakikisha wanashinda mtanange huo. “Maandalizi mazuri, tumemaliza mazoezi ya mwisho, kwanza mchezo utakuwa mgumu timu tunayocheza nayo ni timu ya madaraja ya chini, lakini naamini itakuwa imejiandaa vema, sisi tutaenda kupambana ili kuibuka na ushindi, ukizingatia lazima tushinde mchezo huo ili tuweze kusonga kwa raundi inayofuatia,”..

  Hii ni michuano ya pili ya FA Cup kwa Azam FC kuweza kushiriki tokea ianze kucheza Ligi Kuu msimu wa 2008/2009, ya kwanza ilikuwa msimu uliopita ambapo ilifanikiwa kufika hadi fainali, lakini haikuwa na bahati ya kubeba taji hilo baada ya kufungwa na Yanga mabao 3-1.

  0 0

  Benki ya Exim Tanzania hivi karibuni ilitunukiwa tuzo mbili katika hafla iliyoandaliwa na Shirikisho la Waajiri Tanzania (ATE). Benki ya Exim ilishinda tuzo ya Uongozi na Utawala- Rasilimali Watu (HR- Leadership & Governance) na tuzo ya Ushirikisho wa Wafanyakazi (Employee engagement). Tuzo hizo mbili muhimu zilitolewa kwa benki katika hafla ya mfanyakazi bora wa mwaka 2016 na zilikabidhiwa na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi.


  Utawala bora katika kitengo cha rasilimali watu na ushirikishwaji wa wafanyakazi ni nguzo muhimu katika uendeshaji wa kitengo hicho cha Exim ambacho hufanya kazi ya kuhakikisha wafanyakazi wanatekeleza majukumu yao katika namna ambayo inayohakikisha benki inafanikisha mipango na malengo yake huku ikiendelea kupata faida kila mwaka. Mwaka 2016 Exim ilitimiza miaka 19 ya operesheni huku ikifanya bidii katika kuongeza viwango vya kushirikisha wafanyakazi wake katika shirika hilo.


  Benki ilifanya vizuri sana katika kuhamasisha utawala bora na ushirikishwaji wafanyakazi kupitia njia nyingi za asili. Benki ilipitia upya sera ya rasilimali watu na kuongeza vifungu vinavyohamasisha wafanyakazi kuwa na maisha yenye afya bora. Benki iliingia katika mchakato wa kuimarisha mfumo wa kufanya tathmini ya utendaji ambao ni wa kisasa na umeunganishwa katika mfumo ulioko mtandaoni unaoitwa Adrenalin ambao ni wa uwazi sana.


  Katika uajiri mkakati mkuu ulikuwa ni kuhakikisha usawa wa  jinsia katika wafanyakazi wa kike na kume ambao jumla yao wanafikia 1000. Benki inahakikisha kuwa wafanyakazi watendaji bora wanatambuliwa kupitia tuzo za wafanyakazi, tuzo za wafanyakazi wa muda mrefu, kupandishwa vyeo kutoka nafasi za chini kwenda kwenye nafasi za kati hadi nafasi za juu za umeneja katika shirika kupitia matangazo ya nafasi za kazi ya ndani na programu ya uwezo inayoitwa HIPO. Benki pia iliboresha miundo ya vitengo vyake vyote, kuboresha vyeo na kufanya tathmini za ajira ambazo ziliboresha mifumo ya kazi na hivyo kusababisha usimamizi mzuri na uzalishaji katika vitengo. Vilevile benki iliboresha mifumo ya mawasiliano kupitia majukwaa ya majadiliaano kati ya menejimenti na wafanyakazi ili kujadili utendaji wa benki na kupeana mrejesho uliolenga kuimarisha utendaji wa benki.  


  Kwa upange mwingine benki ya Exim imekuwa ikitumia teknolojia ili kuwapatia wafanyakazi zana bora za kuongeza uzalishaji, kuboresha huduma kwa wateja na mafunzo na maendeleo. Benki ilijikita katika miradi kadhaa iliyolenga kutekeleza teknolojia mbalimbali katika utendaji kwa kuweka namba maalum “whistleblower” inayoweza kutumika na wafanyakazi na wateja pia kutoa taarifa za kiutendaji za benki ikiweka benki katika jukwaa la kidijitali zaidi.


  Katika mafunzo na maendeleo, benki ilianzisha mfumo wa kujifunza kupitia mtandao unaoitwa Elimika. Kusudi la Elimika ni kutoa maarifa kwa wafanyakazi kwa kuwapatia ujuzi unaohitajika katika utendaji wa kazi zao. Matokeo ya Elimika ni wafanyakazi walioelimika zaidi, wenye uelewa na ushirika zaidi. Kasi ya mageuzi haya imekuwa kubwa na kuleta ukuaji katika biashara nchini Tanzania na kuwezesha wafanyakazi walio makao makuu kuweza kutoa msaada na ushirikiano kwa wengine mikoani na katika kampuni tanzu.


  “Exim inajivunia kuwa benki ambayo inajikita katika uvumbuzi na teknolojia. Tunatumia suluhisho za teknolojia ili kutengeneza mazingira yanayoboresha kwa kiwango kikubwa uwezo wa wafanyakazi. Kozi hizi zinasaidia wafanyakazi kuwa na uelewa mkubwa wa majukumu yao na pia kuwa na zana za vitendo kuendeleza ujuzi na vipaji vyao,” alisema Fredrick Kanga ambaye ni mkuu wa kitengo cha rasilimali watu cha Exim.


  “Ni matumaini yetu kuwa wafanyakazi wetu wataendelea kujenga ujuzi wao kupitia Elimika. Na menejimenti ya Exim itaendelea kuboresha mifumo yake ili tuendelee kuwa mwaajiri bora kabisa nchini. Nina imani kubwa kuwa tuna uwezo huo na tumeamua kuileta Exim katika kiwango hicho mwaka huu,” alimalizia Fredrick Kanga. 

  0 0


  Kiungo wa Hull City Ryan Mason amefanyiwa upasuaji baada ya kuumia fuvu la kichwa kwenye mchezo dhidi ya chelsea hapo jana.

  Mason aligongana na Gary Cahill wakati wakiwania mpira mnamo dakika ya 13 na kutolewa nje huku akisaidiwa na mashine ya kupumulia na kupatiwa huduma ya kwanza kwa muda wa dakika 8 kisha kukimbizwa hospitalini.

  Taarifa toka ndani ya klabu yake ya Hull City zimedai kuwa Mason yupo katika hali nzuri na anategemewa kusalia hospitalini kwa siku kadhaa pamoja na kuwashukuru watoa huduma ya kwanza pamoja na wauguzi wote waliomsaidia mchezaji wao.

  Upande wa Gary Cahill amemtakia Masona afya njema mapema sawa na wachezaji wengine wengi pamoja na kocha wa Chelsea Antonio Conte

   Kocha mkuu wa Chelsea Antonio Conte alisema: "Kila mtu katika klabu ya Chelsea wanampa pole Ryan Masom kwa matatizo aliyoyapata kwani ilikuwa ni ajali mbaya katui yake na Gary Cahill.        Kila mtu katika timu yetu ya  Chelsea, tunatarajia kumuona Mason akirejea  uwanjani na kupona haraka sana.  Matukiuo ya uwanjani baada ya kuumia kwa Ray Mason jana katika mchezo wa Hully City na Chelsea.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla leo Januari 23, 2017 amefanya ziara ya kutembelea vituo viwili vya Redio vilivyopo mkoani humo, na kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na wananchi wa Mkoa Mbeya.

  Makalla alisema ameamua kutembelea vituo hivyo ambavyo vimemuwezesha kuzungumza na wananchi moja kwa moja ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero zao, Makala alivichaguwa vituo hivyo kwa kuwa ndivyo kituo pekee kufanya mahojiano ya moja kwa moja na wananchi wa mkoa wa Mbeya tangu aingie rasmi mkoani humo.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza moja kwa moja na wananchi wa Mkoa wa Mbeya, kupitia kituo cha Redio 91.3 Dream FM cha mkoani humo, ikiwa ni sehemu yake ya ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari vilivyomo kwenye Mkoa huo.Picha na Fadhiri Atick Mmg Mbeya.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akipokea kitabu cha usimamizi wa biashara na fedha kilicho andaliwa na Fred Matola Msemwa, kutoka kwa Meneja masoko wa Redio 91.3 Dream Fm ya jijini Mbeya, Sam Mhina.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akifanyiwa mahojiano ya moja kwa moja na Mtangazaji wa Kituo cha Redio 106.5 Big Star Fm cha jijini Mbeya.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza jambo na Mkurugenzi wa kituo cha redio Big Star Fm 106.5 Mbeya, Kura Mayuma.

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Viongozi walioapishwa na Rais Dk. Shein katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar ni Dk. Sira Ubwa Mamboya ambaye anakuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiekuwa na Wizara Maalum.


  Wengine ni Bi Zainab Omar Mohammed ambaye anakuwa Mshauri wa Rais wa Masuala ya Jamii, Wazee, Wanawake na Watoto, Dk. Maua Abeid Daftari anakuwa Mshauri wa Rais- Pemba na Bi Rahma Ali Khamis ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.


  Hafla hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd,  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar  Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Gavu.


  Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Mawaziri wasio na Wizara Maalum ambao pia, ni Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Shadya Mohamed Suleiman, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.  Na wengine ni Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dk.Sira Ubwa Mamboya kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi (BLM) na Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum,katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja.(Picha na Ikulu)
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bi,Zainab Omar Mohamed kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Jamii Wazee Wanawake na Watoto,katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja. 

  0 0

  MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku (pichani )amewataka  madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda jijini Tanga kuacha kuendesha mwendokasi kwani maisha ya watu yanapotea kwa sababu yao.

  Sambamba na hilo amewataka kuondokana na tabia ya kupakia abiria zaidi ya mmoja wanapokuwa barabarani maarufu kama mshikaki kwani jambo hilo ni hatari kwa mustakabali wa maisha yao wanapokuwa njiani.

  Mbunge huyo alitoa wito huo  wakati akizungumza na madereva wa pikipiki Kata ya Kirare Jijini Tanga ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuwatembelea wananchi na kuangalia changamoto zinazowakabilia kasha kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi.

  Aliwataka pia kutii sheria za usalama kwa kuvaa kofia ngumu na kuacha kuwa na mbwembwe wanapokuwa barabarani jambo ambalo linaweza kusababisha ajali zinazoweza kugharimu maisha ya watu.“Lakini pia madereva wa bodaboda hakisheni mnakuwa nadhifu kwa wateja wenu pendeni kazi ikiwemo kuacha kuvaa malapa badala yake wavae viatu vya ngazi “Alisema mbunge huyo.

  Hatua ya mbunge hiyo inatokana na kuwepo kwa malalamiko kwa baadhi ya waendesha bodaboda hao kuwa wamekuwa wakikamatwa na askari wa usalama barabarani wanapokuwa kwenye shughuli zao jambo ambalo linasababisha kushindwa kufikia malengo yao.

  Bakari Juma ambaye ni mwendesha bodaboda eneo hilo alisema kuwa wamekuwa wakikumbana na wakati mgumu katika kufanya shughuli hizo kutokana na kukamatwa mara kwa mara na kutakiwa kutoa faini.

  Naye Zuberi Omari alimuomba mbunge huyo kuangalia namna ya kuwasaidia waendesha bodaboda hao ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha chama cha kukopa na kuweka akiba (Saccos) yao ambayo inaweza kuwa mkombozi.

  Alisema hivi sasa baadhi ya watu mbalimbali wamekuwa wakianzishya vikundi mbalimbali vikiwemo vya kukopa na kuweka fedha hivyo nasi tungeweza kupata fursa hiyo ingeweza kutusaidia kukabiliana na ugumu wa maisha.

  Akizungumzia suala hilo, Mbunge Mussa alisema lazima wahakikisha wanaheshimu sheria za usalama barabara kwa kuacha kuendesha mwendokasi ikiwemo kuwa na leseni za kufanya shughuli hizo ili kuweza kuzifanya kwa usalama zaidi bila kuwepo kwa usumbufu.

  Mussa aliwataka pia kuacha kutumia mtindi wa kupakia abiria zaidi ya uwezo wanaakiwa kuwapakia wanaopokuwa kwenye shughuli hizo maarufa kama mshikaki kwani madhara yake ni makubwa sana kwa usalama wao na abiria hao kwani wanaweza kukumbana na ajali ikiwemo kugharimu maisha yao.

   “Leo hii ukiangalia wapo watu ambao wanaendesha vyombo vya moto kama vile bodaboda hawavai elementi lakini wanapakia abiria mishikaki sasa hawa wanakuwa na hatari kubwa kwa usalama barabarani hivyo niwatake muache suala hilo “Alisema.Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki amezindua rasmi safari ya awamu ya kwanza kwa kuaga msafara wa magari yaliyobeba vifaa vya Ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo kuelekea Dodoma.

  Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Kairuki alisema umefika wakati wafanyakazi wa Serikali kuanza safari ya kuamia makao makuu Dodoma ili kutimiza ahadi iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli wakati wa Maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa.

  “Kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri Mkuu kama kiongozi na mratibu wa shughuli za Serikali alihamia Dodoma Mwezi Septemba 2016,Wizara nyingine zimeendelea na maandalizi ya kutekeleza azma hii ya serikali, nami leo napenda kutumia fursa hii kuuarifu umma wa watanzania kuwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekamilisha maandalizi ya kuhamia Dodoma na hivi punde vifaa vya kundi la kwanza vitaondoka kwenda Dodoma”,Aliongeza Mhe. Kairuki.

  Amesema katika kundi la kwanza jumla ya watumishi 87 watahamia Dodoma na litahusisha uongozi wa Juu wa Wizara ukiwajumuisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu na Baadhi ya Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Maafisa Waandamizi na Watumishi wengine.

  Katika hatua nyingine Mh. Kairuki alisema wale wote wanaohitaji kukutana na Waziri,Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wake wafike katika Ofisi zilizopo Dodoma na kwa masuala yote yanayohusuu Sera na Sheria za Utumishi wa Umma na Utawala wa Utumishi wa Umma kwa Ujumla yatatekelezwa Mjini Dodoma lakini.

  Aidha masuala ya Mishahara,Uendelezaji rasilimali watu,Ukuzaji maadili,Anuai za jamii,Uchambuzi ushauri na Utendaji kazi na Huduma ya teknolojia ya habari na mawasiliano yataendelea kushughulikiwa na ofisi ya Dar es Salaam.

  Alisema Ofisi yake itafunguliwa Rasmi Mjini Dodoma Tarehe 30 Januari 2017 na itakuwa katika Jengo la College of Humanities and Social Sciences katika eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma kama makao yake ya muda mpaka hapo itakavyoelezwa vinginevyo.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki akizungumza na waandishi wa habari juu ya safari ya kuhamia Dodoma iliyoanza rasmi leo kwa kuhamisha vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo.Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro na Naibu Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi. 
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki akizungumza na watumishi wa ofisi yake juu ya safari ya kuhamia Dodoma iliyoanza rasmi leo kwa kuhamisha vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro wakiuaga msafara wa magari yaliyobeba vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakielekea Dodoma kwenye makao makuu ya nchi.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro na Naibu Katibu wa Ofisi hiyo Bi. Susan Mlawi wakifuatilia kwa makini uamishwaji wa vifaa vya Ofisi yao kabala ya kuondoka kwenda Dodoma leo hii. Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.

  0 0

  Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa tahadhari kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano nchini kuwa makini na utapeli unaofanywa kupitia simu za mkononi.Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Meneja Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Semu Mwakyanjala wakati akizungumza na waandishi wa habari.

  Semu alisema kuwa kuna ongezeko la matapeli wanaoghushi utaratibu wa mawasiliano na kuwalaghai watu kutuma pesa kwa simu za mkononi hivyo Mamlaka na vyombo vya usalama vinashughulikia suala hilo.“Usitekeleze maagizo yoyote yanayohusu fedha kwa mawasiliano ya simu hata kama yanatoka kwa mtu unayemfahamu, mpigie aliyekutumia ujumbe kwa namba nyingine ili kuthibitisha’’ alifafanua Semu.

  Alitahadharisha kuwa mtu akipokea taarifa kwa njia ya simu au ujumbe mfupi wa maandishi kuwa ametumiwa fedha kimakosa na kutakiwa kuzirudisha asifanye hivyo mpaka atakapojiridhisha na uhalali wa taarifa hiyo.  Akizungumzia matumizi ya huduma za kifedha kwa njia ya mitandao, Semu alibainisha kuwa kwa miezi miwili ya Novemba na Desemba 2016 jumla ya fedha iliyopita kwenye mitandao ya simu za mkononi ni shilingi trilioni 13.07 hali inayothibitisha ongezeko kubwa la matumizi ya huduma za kifedha kwa njia ya mitandao hapa nchini.  Alitaja makampuni yaliyohusika na takwimu za miamala hiyo kuwa ni Zantel (EASY PESA), Tigo (TigoPesa), Vodacom (M PESA), Airtel (Airtel Money) na Halotel (HALOPESA).


  Aidha aliwataka wananchi kutoa taarifa polisi kuhusu matapeli na kuwasilisha malalamiko yao ya huduma za mawasiliano kwa TCRA kupitia sanduku la posta 474 Dar es salaam au wafike kwenye ofisi za TCRA zilizo karibu au wapige simu namba 0784 558270, 0784 558271 na barua pepe (malalamiko@tcra.go.tz)
   Kaimu Meneja  Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Semu Mwakyanjala akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu ulaghai kupitia simu za mkononi unaofanywa na matapeli katika kipindi hiki. Kulia ni Afisa Uhusiano wa TCRA Bi. Mabel Masasi

  Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo Jijini Dar es salaam. (Picha na Frank Mvungi-Maelezo).

  0 0

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii .

  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vinguti , Omary Kumbilamoto, ameahidi kuendelea kushirikiana na wakazi wa kata hiyo hili kuakikisha wanapata maendeleo. 

  Kumbilamoto amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa mtaa wa Kaza buti kata ya Vingunguti wakati akikabidhi vifaa vya michezo na mabati kwa tasisi ya Makazi kazi na vikundi vya michezo. 

  “nitoe shukrani kwa wakazi wa eneo la kazabuti kwa jinsi mlivyoweza kuniamini katika uchaguzi mkuu mwaka jana na kunipa fursa ya kuwa Diwani wenu na leo nimekuja kuwatembelea kwa ajili ya kutimiza moja ya ahadi zangu hivyo naomba niwaambie kuwa nitakuwa nanyi bega kwa bega katika kuakikisha kuwa tunaleta maendeleo katika kata yetu” amesema Kumbilamoto. 

  Kumbilamoto amesema kuwa amemaliza mwaka mmoja ndani ya utawala wake kwa kuweza kutimiza ahadi kadhaa ambazo aliahidi ikiwemo ununuzi gari ya kubebea wagonjwa , Mashine yakufulia katika Zahanati ya vingunguti na ujenzi wa choo kwa ajili ya wodi ya kinamama wajawazito. Aidha ametaja kuwa pia katika mwaka huu mmoja maeweza kuwasaidia wanawake wajasilimali ambao aliwapa vyerehani viwili hiki kuendeleza vikundi vyao. 

  Kumbilamoto alimaliza kwa kuwataka wakazi wa Vingunguti kuwa wachapakazi kwa kila jambo kama Rais wanchi Dkt John Pombe Magufuli. 
  Mwenyekiti wa Haki za Binadamu wa Chama cha Wananchi (CUF) Mohamed Mluya, akikabidhi jezi kwa vikundi vya Joging.
  Naibu Meya wa Manispa aya Ilala, Omary Kumbilamoto, akikabidhi jezi kwa kikundi cha Makazi Kazi kilichopo katika mtaa wa Kaza Buti
  Naibu Meya na wenzie wakicheza muziki mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo
  Wananchi wakifatilia mkutano huo kwa makini


  0 0


   Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Uvccm Bw Peter Thadeo Akimkabidhi Hati ya Umiliki jengo na eneo Katibu wa Tawi la Ccm Kipala Bi Sharifa Mnenje
   Mjumbe wa Mkutano mkuu Taifa UVCCM  Bw Peter Thadeo ambaye amemuwakilisha katibu wa Ccm Uchumi na Fedha wilaya ya Mkuranga Dkt Thadeo Mutembei akiongea na Wanachama na viongozi mbalimbali wa Kata ya Mwandege.
   Mwenyekiti wa CCM Kata Bw Kazibure Mtorokudu akifafanua jambo kwa wanachama wa CCM katika mkutano huo.
  Mjumbe wa Mkutano mkuu Taifa Uvccm Bw Peter Thadeo katikati akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kipitia chama cha Mapinduzi CCM.Picha na Yassir Adam -GLobu ya Jamii

  0 0

   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea salamu za heshima baada ya kuwasili kituo cha Uhamiaji Kasumulu, kinachosimamia masuala ya uingiaji na utokaji nchini kwa wananchi wa Nchi za Tanzania na Malawi. Kulia ni Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa kituo hicho, Kamishna Msaidizi Taniel Magwaza. Naibu Waziri yupo wilayani Kyela kwa ziara ya kikazi. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto),  akikagua hati ya kusafiria ya mwananchi kutoka nchi ya Malawi, Miston Chikankheni aliyekuwa anaingia  nchini katika Kituo cha Uhamiaji Kasumulu, wilayani Kyela mkoa wa Mbeya. Naibu Waziri yupo wilayani Kyela kwa ziara ya kikazi. 
   Mrakibu Mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji, Gragiza John  akijibu maswali aliyoulizwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto) ,baada ya kutembelea moja ya vipenyo vinavyopitisha wahamiaji haramu kutoka Malawi katika mpaka wa Kasumulu. Naibu Waziri ameiagiza  idara hiyo wakishirikiana na Jeshi la Polisi kudhibiti njia hizo ili kuzuia uingiaji wa wahamiaji hao, wakati wa ziara ya kikazi wilayani Kyela.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Wasanii wachoraji 14 kutoka Tanzania wamewasili Nairobi kufanya maonyesho ya kazi zao katika tamasha la majuma mawili kwenye ukumbi wa Village Market litakaloanza rasmi Jumatano tarehe 25 Januari. Kundi hilo lilitembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya leo na kukutana na Kaimu Balozi, Bi. Talha Mohamed Waziri.

  Msemaji wa Kundi hilo, Bw. Amani Abeid, alisema lengo lao ni kutambulisha kazi zao katika soko la Kenya na kuwa baada ya hapo wataelekea Rwanda. Washiriki kwenye maonyesho hayo ya Nairobi ni Cathbert Semgoja, Masoud Kibwana, Haji Chilonga, Amani Abeid, Localfanatics, Nadir Tharan, Thobias Minzi, Lutengano Mwakisopile, Moses Luhanga, Raza Mohammed, Ludovic Kaija, Cloud Chatanda na Salum Kambi.
  Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Bi. Talha Mohamed Waziri (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wasanii kutoka Tanzania ambao wako jijini Nairobi kufanya Maonyesho ya Sanaa Oni.

  0 0

  KAMATI ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC) imeridhishwa na matumizi ya Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) yenye lengo la kuwakwamua wakulima nchini.

  Wajumbe wa kamati hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari wakati walipotembelea shamba la majaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo walisema hatua iliyofikiwa na watafiti hao ni kubwa hivyo haipaswi kuachwa ikapotea bure. 

  Elisa Moses kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe ambaye ni mjumbe wa NBC alisema teknolojia hii ya bioteknolojia ni nzuri na inaonesha uhalisia halisi na inaweza kusaidia changamoto za ukosefu wa chakula iliyopo nchi.

  "Binafsi nimefurahi kujionea hali halisi ya teknolojia hii hasa ninapoyaona mahindi haya ya GMO yalivyomakubwa kwani ni muhimu sana katika kukabiliana na ukame uliopo sehemu kubwa nchini" alisema Moses.

  Mjumbe mwingine wa kamati hiyo kutoka Chemba ya Wanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo, Magdalene Mkocha alisema wamefurahi kuona jambo walilolipitisha linafanyiwa kazi vizuri na linaleta matumaini makubwa kutokana na matokeo ya jaribio hilo.

  Alisema wadau wa sekta binafsi wanasubiri kwa hamu kuhusu matokeo hayo baada ya kuthibitishwa na takwimu za kisayansi kwani kwa kuangalia kwa macho mahindi yanaonekana ni bora zaidi.

  Ofisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Kanda ya Kati Dodoma, Sebastian Kandira alisema hapo awali tafiti hizo zilikuwa hazifikishwi kwa wakulima ndio maana zilikuwa hazieleweki vizuri lakini hivi sasa wameanza kuzielewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

  Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso alisema wakati wanaanza majaribio hayo kulikuwa na changamoto nyingi kutokana na wadau kutokuwa na uelewa hasa kwa mahindi yaliyobadilishwa vinasaba kikubwa ni mshukuru Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba kwa kufika katika shamba hili la majaribio ambalo tulipanda mahindi Oktoba 5, mwaka jana na kutupa faraja kuwa kuna kila sababu ya kuharakisha matumizi ya teknolojia hiyo ili iweze kutumika kama zinazofanya nchi zingine zinazofanya tafiti za namna hiyo.
  Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kulia), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC), kuhusu matumizi ya Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) walipotembelea shamba la majaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo.
  Meneja wa shamba hilo, Bakar Mohamed akielezea kuhusu shamba hilo.
  Safari ya kuelekea kuangalia shimo la kuchomea uchafu mbalimbali baada ya kufanya utafiti ikiendelea. 

  Wajumbe wa kamati hiyo na watafiti wa kilimo wakiangalia shimo la kuchomea uchafu mbalimbali baada ya kufanya utafiti huo.


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongoza msafara wa ujumbe wa Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) Bwana Erik Solheim walipotembelea dampo la taka la Pugu Kinyamwezi jijini Dar Es Salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akifanunua jambo kwa Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) Bwana Erik Solheim mbele ya Waandishi wa Habari wakati wa ziara ya kutembelea dampo la Pugu Kinyamwezi wakati wa ziara ya Mkurugenzi huyo hapa Nchini.
  Meneja wa Dampo la Pugu Kinyamwezi Bwana Richard Kishera akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) Bwana Erik Solheim, jinsi ya uendeshaji wa dampo hilo najinsi ya utunzaji wa taka unavyofanyika katika eneo hilo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akimuelezea juu ya uzalishaji wa mkaa Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) Bwana Erik Solheim na Ujumbe wake walipotembelea kituo cha uuzaji wa mkaa eneo la Ubungo jijini Dar Es Salaam.
  Sehemu ya taka zinazotupwa katika eneo la utupaji taka la Pugu Kinyamwezi zikiwa zimerundikwa na Wananchi wakiendelea na shuhuli zao za kila siku za ukusaji wa chupa pamoja na ghafi taka nyingine zilizobaki kwenye takataka.

  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  Serikali ya Tanzania na Serikali ya Uturuki zimesaini mikataba tisa ya makubaliano ya kiuchumi inayolenga katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa maendeleo baina ya nchi hizo.

  Mikataba hiyo inahusisha sekta za uchukuzi, mawasiliano, habari, elimu, utalii, utafiti, viwanda, afya na ulinzi.

  Akizungumza mara baada ya kusaini kwa mikataba hiyo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alisema ujio wa Rais wa Uturuki na ujumbe wake ni kielelezo cha ukuaji wa mahusiano baina ya Tanzania na Uturuki katika nyanja ya biashara na kimaendeleo baina nchini hizo.

  Rais Magufuli alisema katika mazungumzo yake aliyofanya na Rais Recep Erdogan kuhusu ujenzi wa Reli ya Standard Gauge nchini, alimjulisha kiongozi huyo kuwa miongoni mwa wakandarasi walioomba zabuni ya ujenzi wa reli hiyo kuwa ni kampuni kutoka Uturuki, hivyo endapo itashinda zabuni hiyo itasaidia kukuza uhusiano uliopo baina ya nchi hizi mbili.

  Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa, Serikali ya Tanzania inatarajia kuomba mkopo kupitia Benki ya Exim ya Uturuki katika kujenga sehemu ya kipande cha ujenzi wa reli hiyo.

  Rais magufuli alisema Tanzania inaendelea kunufaika na uwepo wa Shirika la Ndege la Uturuki kwa kufanya safari zake za moja wka moja kutoka nchini Uturuki, kwa kuwa utasaidia kuongezeka kwa idadi ya watalii nchini na hivyo kukuza uchumi wa nchi hizo.

  Kwa upande wake Rais wa Uturuki, Recep Erdogan alisema kuwa uwepo wa mikataba hiyo baina ya Tanzania na Uturuki itasaidia kupata matokeo mazuri ya uhusiano pamoja na fursa mbalimbali za ushirikiano katika nyanja ya Kilimo, Utalii, Ulinzi, Reli ambazo zitawezesha kukuza uchumi wa mataifa hayo.

  Rais Erdogan alisema kuwa Uturuki imelenga kukuza ushirikiano uliopo baina yake na Tanzania kupitia makongamano ya wafanyabiashara yenye malengo ya kukuza uchumi, kuongeza ajira pamoja na kukuza ujasiriamali baina ya Tanzania na Uturuki.

  “Kiwango cha Biashara ya uwekezaji katika nchi ya Uturuki ni Dola za kimarekani 150 ambapo lengo letu ni kufika Dola za kimarekani 500” alisema Rais huyo.Aidha Rais Erdogan alisisitiza kuwa kufanya kazi kwa pamoja kutasaidia nchi hizi kusonga mbele na kufanikiwa katika nyanja mbalimbali.

  Nae Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe alisema kuwa makubaliano ya mkataba baina ya Tanzania na Uturuki katika Sekta ya Utalii yatasaidia katika kutangaza vivutio vilivyopo nchini, kubadilishana wataalamu, kubadilishana taarifa na kuongeza idadi ya watalii nchini.

  Prof. Magembe aliongeza kuwa makubaliano hayo yatakuza sekta ya utalii katika kuvutia uwekezaji wa katika maeneo ya hoteli, fukwe na mbuga za wanyama zilizopo nchini.

  0 0

  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akimshukuru Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan kwa kufanya ziara nchini pamoja na makubaliano ya kushirikiana katika kuiendeleza jamii leo Jijini Dar es Salaam.
   Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akimkabidhi zawadi Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan leo Jijini Dar es Salaam.
   Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan akimkabidhi zawadi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli leo Jijini Dar es Salaam.
   Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan wakikata utepe kuzindua jingo la zamani la King George’s V lililopo katika Jengo la makumbusho ya taifa jijini Dar es Salaam lililokarabatiwa na Shirika la Maendeleo la Uturuki (TIKA).
  Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan akitoka katika moja ya nyumba ya kabila la kigogo alipotembelea katika kijiji cha Makumbusho Kijitonyama Jijini Dar es salaam.


older | 1 | .... | 1524 | 1525 | (Page 1526) | 1527 | 1528 | .... | 3348 | newer