Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

Meshark Mwankemwa, Ramadhan Shauri kuzichapa Februari 5 Uwanja wa ndani wa Taifa, jijini Dar

$
0
0
Promota wa mchezo wa ngumi "Masumbwi" wa muda mrefu na Mkurugeni wa Kampuni ya SADICK  & CO. LTD, Sadick Kinyogoli (kati) akiwatambulisha Mabondia Ramadhan Shauri (kulia) na Meshark Mwankemwa (kushoto) watakaozichapa Februari 5, 2017 katika uwanja wa ndani wa Taifa, Jijini Dar es salaam ikiwa ni mpambano wa kuwania mkanda wa Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (66.7kg  Welterweight). Mambondia hao wametambiana kwa kila mmoja kuonyesha nia ya kumshinda mwenzake katika mpambano huo. Kabla ya pambano la Mabondia Ramadhan Shauri na Meshark Mwankemwa, kutakuwa na mapambano ya utangulizi yapatayo saba, likiwepo la Mabondia Mohamed Matumla  na Mfaume Mfaume (62 KG  LIGHT weight).
 Promota wa mchezo wa ngumi "Masumbwi" wa muda mrefu na Mkurugeni wa Kampuni ya SADICK  & CO. LTD, Sadick Kinyogoli (wa pili kulia) akimkabidhi fedha Bondia Meshark Mwankemwa kwa maandalizi ya mpambano wake dhidi ya Bondia Ramadhan Shauri (kulia).
 Promota wa mchezo wa ngumi "Masumbwi" wa muda mrefu na Mkurugeni wa Kampuni ya SADICK  & CO. LTD, Sadick Kinyogoli (katikati) akimkabidhi fedha Bondia Ramadhan Shauri kwa maandalizi ya mpambano wake dhidi ya Bondia Meshark Mwankemwa.
 Bondia Ramadhan Shauri akimwaga wino kukubali kuzichapa na Bondia Meshark Mwankemwa
 Naye Bondia Meshark Mwankemwa akimwaga wino kukubali kukipiga na Bondia Ramadhan Shauri.
Promota wa mchezo wa ngumi "Masumbwi" wa muda mrefu na Mkurugeni wa Kampuni ya SADICK  & CO. LTD, Sadick Kinyogoli akiwatambulisha Mabondia Mohamed Matumla (kulia) na Mfaume Mfaume.

MATUMIZI YA BIOTEKNOLOJIA YA KISASA KATIKA KILIMO NI UKOMBOZI KWA WAKULIMA NA TAIFA KWA UJUMLA

$
0
0
MATUMIZI ya Bioteknolojia ya Kisasa katika Sekta ya Kilimo nchini yataleta mafanikio makubwa kwa wakulima na taifa kwa ujumla.

Hayo yalielezwa na Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAM), Dk. Nicholaus Nyange wakati akitoa taarifa kwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba alipotembelea shamba la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma.

"Matumizi ya Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo Tanzania ni muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho maeneo mengi ya nchi yanakabiliwa na ukame kutokana na tabia nchi" alisema Dk.Nyange.

Alisema taaluma ya uhandisi jeni inawezesha kuhamisha jeni kutoka kwa kiumbe hai kimoja na kuingiza katika kiumbe hai kingine ili kupata sifa lengwa na kutengeneza bidhaa kwa matumizi mbalimbali.

Akizungumzia kuhusu usalama wa matumizi ya Bioteknolojia hapa nchini alisema ni vema kuanza mchakato wa kuendeleza mazao yaliyofanyiwa mabadiliko ya kijenetiki (GMO) ambayo yameleta mafanikio makubwa katika nchi nyingine kwa mfano mahindi yanayostahimili ukame na bungua muhogo unaostahimili ugonjwa wa batobato na michirizi kahawia, migomba yenye ukinzani dhidi ya ugonjwa wa mnyauko na pamba yenye ukinzani kwa wadudu waharibifu.

Dk. Nyange alisema Changamoto kubwa iliyopo katika matumizi ya teknolojia hiyo ni kuongezeka kwa upotoshaji kutoka kwa wanaharakati na wapinzani kutokana na

ufahamu na uelewa wa watafiti, viongozi, wanasiasa na umma kwa jumla kuhusu masuala ya taaluma hiyo kuwa bado ni mdogo ukiwemo uwekezaji mdogo katika utafiti na maendeleo.
Watafiti wakiwa lango kuu la kuingia katika shamba la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO), chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma. Watafiti hao walikuwa wameongoza na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba kutembelea shamba hilo.
Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAM), Dk. Nicholaus Nyange (kulia), akitoa mada ya matumizi ya Bioteknolojia ya kisasa katika sekta ya kilimo mbele ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Hassan Mshinda (kulia), akitoa maelezo mbele ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba (wa pili kushoto), alipotembelea shamba la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) lililo chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma juzi.

GOLF JWTZ WAAANZA MAANDALIZI MAADHIMISHO MIAKA 10 YA KLABU

$
0
0
NA LUTENI  SELEMANI SEMUNYU JWTZ
Klabu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo iko katika maandalizi ya viwanja kwa ajili ya mashindano ya kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo mwaka 2006.

Akizungumza na waandishi wa Habari msimamizi wa viwanja ambaye pia ni mchezaji wa kulipwa wa klabu ya Lugalo David Helela alisema kila kitu kinaenda sawa na wanaangalia sehemu ngumu kuchezeka kuondoa vikwazo visivyo na sababu.

“kuna vikwazo vinavyopaswa kuwepo katika Uwanja wa golf  lakini kuna vikwazo vingine vinakuwepo lakini havina sababu wala havina mchango katika kuonyesha umahiri wa mchezaji hivyo tunaviondoa”, Alisema Helela.


Aliongeza kuwa mbali na kuviondoa bado viwanja kama namba 12 vitaendel;ea kuwa moja ya kiwanja kigumu kwa mchezaji atakayecheza katika uwanja huo kutoka na jinsi ulivyowekwa kwa lengo tu la kukamilisha sifa za uwanja wa Golf.

Helela Alisema katika kuelekea kuadhimiasha Miaka 10 klabu ya lugalo itabaki kuwa ndio klabu pekee inayothamini kwa kiwango kikubwa mchango wa wachezaji wa kulipwa ambao mbali na kuwatumia katika kufundisha vijana na kusimamia sheria za mchezo  lakini wamekuwa wakishirikishwa katika mashindano ya wachezaji wa kulipwa .

Kwa Upande wake Afisa Tawala wa Klabu hiyo Kapteni Amanzi Mandengule alisema amefanya ukaguzi wa Awali kazi zinaenda vizuri na kutoa wito kwa wadhamini kuongeza nguvu ili kuwa na mashindano Bora.

“ Kuna wadhamini tuliofanikia na wako tayari na wameanza maandalizi lakini Milango iko wazi kwa wadhamini wengine kujitokeza kwani Mashindano ya Miaka 10 ya Klabu yanatarajiwa kuwa ya Aina yake ukilinganisha na mashindano yaliyowahi kuandaliwa”Alisema kapteni Mandengule.

Aliongeza kuwa taarifa rasmi ya mashindano na Mgeni rasmi inatarajiwa kutolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Klabu Brigedia Jenerali Michael Luwongo ili kuelezea kwa kina mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika katikati ya Mwezi wa Pili.

Katika mashindano hayo yanayotarajiwa kuwa ya siku tatu Vilabu vyote vimealikwa na makundi yote ya mashindano yatashirikishwa katika mashindano hayo ambayo yatakuwa ni mashindano ya Kwanza makubwa nchini kwa mwaka 2017 .
Mwenyekti wa Klabu ya Golf ya Jeshi ya Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo akizungumza na Wachezaji wa Klabu hiyo Jijini Dar es Salaam,wachezaji hao wanataraji Kuwakilisha katika mashindano ya Miaka 10 ya Klabu yanayotarajiwa kufanyika Mwezi February mwaka huu.
Baadhi ya Wachezaji wa kulipwa na wale wa Ridhaa wa Klabu ya Golf ya Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo wakiwa katika mazoezi kwa Ajili ya Maandalizi ya mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu hiyo yanayotarajiwa kufanyika Mwezi February Mwaka huu 2017 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wachezaji wa kulipwa na wale wa Ridhaa wa Klabu ya Golf ya Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo wakijadiliana wakati wa mazoezi kwa ajili ya mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu hiyo yanayotarajiwa kufanyika Mwezi February Mwaka huu 2017 Jijini Dar es Salaam. (Picha na Luteni Selemani Semunyu)

SIMIYU YAPANIA KUONGOZA MAPINDUZI YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI NCHINI

$
0
0
BENKI ya NMB imekubali kutoa fedha kwa ajili ya kujenga 'skimu' kubwa ya mfano ya umwagiliaji katika Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.

"Maji ni raslimali muhimu sana inayotoa uhakika wa kuvuna pamoja mbali ya pembejeo na uhifadhi', alisema Seif Ahmed, afisa mkuu upande wa biashara ya kilimo (Agribusiness) mwishoni mwa wiki.

"Mkuu wa Mkoa ninakupongeza wewe na timu yako kwa nia ya kuwaletea wananchi wa Simiyu maendeleo, " alisema na kuongeza, "Ninawahakikishia kuwa tutawapatia mkopo huo."

Ahmed aliahidi kufanya kazi pamoja na Mkoa wa Simiyu kuhakikisha mradi unaleta mabadiliko ndani ya jamii.

Afisa Mwakilishi wa Serikali katika NMB,  Domina Feruz, alisema kilimo cha umwagiliaji kitatoa uhakika wa mavuno na kuwapo uhakika wa marejesho ya mkopo na chakula muda wote wa mwaka", alisema Afisa huyo.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mataka na ujumbe wake katika mazungumzo na Bw.  Seif Ahmed, afisa mkuu wa NMB upande wa biashara ya kilimo (Agribusiness) na timu yake makao makuu ya Benki hiyo  mwishoni mwa wiki jijini Dar es salam
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mataka na ujumbe wake katika mazungumzo na Bw.  Seif Ahmed, afisa mkuu wa NMB upande wa biashara ya kilimo (Agribusiness) na timu yake makao makuu ya Benki hiyo  mwishoni mwa wiki jijini Dar es salam.

KINANA AKUTANA NA PROF. KABUDI, NUNDU , KIA

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (Kushoto), akiwa na Mbunge Mteule, Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa zamani, Omari Nundu, walipokutana jana, Januari 21, 2017, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). (Picha na Bashir Nkoromo).

NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA GEREZA LA RUANDA JIJINI MBEYA

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kushoto) akipata maelezo juu ya utengenezwaji wa kiti kinachotengenezwa na wafungwa wa gereza la Ruanda wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la Magereza.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wakwanza kulia waliokaa), akiangalia picha za thamani za ndani zinazotengenezwa na wafungwa wa Gereza la Ruanda wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la Magereza.Wengine waliokaa baada ya Naibu Waziri ni Mkuu wa Kiwanda hicho,ASP Michael Kuga ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Jesuald Ikonko na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza alipotembelea Kiwanda cha sabuni zinazotengenezwa na wafungwa wa gereza la Ruanda wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la Magereza.Wanaomsikiliza ni Mkuu wa Kiwanda() na Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Paul Kajida. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akiangalia moja ya sabuni zinazozalishwa na wafungwa wa Gereza la Luanda wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la Magereza.Kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

WATANZANIA WAHIMIZWA KUZINGATIA USAWA WA KIJINSIA KATIKA SEKTA YA KILIMO

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) kitabu kinachotumika kutoa elimu juu ya usawa wa kijinsia katika sekta ya kilimo, sheria za kimila leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mhadhiri wa Shule Kuunya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) Bw. Dotto Kuhenga, Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda na Mtaalamu Mwelekezi wa masuala ya Jinsia,Utawala Bora na Maendeleo kutoka LAND O’ LAKES Bibi. Margreth Henjewele.
Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano wao na waandishi hao(hawapo pichani) kuhusu mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono na Mtaalamu Mwelekezi wa masuala ya Jinsia,Utawala Bora na Maendeleo kutoka LAND O’ LAKES Bibi. Margreth Henjewele.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Sehemu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya umma –SJMC) Bw, Dotto Kuhenga akionyesha waandishi wa habari kitabu cha mwongozo wa waandishi wa habari katika utekelezaji wa mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono na Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda (kulia).

MWANJALE MCHEZAJI BORA WA DESEMBA 2016

$
0
0
Sentahafu wa Simba, Method Mwanjale amechaguliwa kuwa mchezaji bora Desemba wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2016/2017. 

Beki huyo wa kati, aliwashinda kiungo mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima na beki Yakubu Mohamed wa Azam FC. Mwezi Desemba ulichezwa raundi tatu za Ligi hiyo, huku Simba ikicheza mechi mbili ugenini na moja nyumbani. Raundi hizo ni ya 16, 17 na 18.

Mwanjali aliiongoza Simba kushinda mechi zote tatu, hivyo timu yake kupata ushindi wa asilimia 100 kwa kunyakua pointi zote tisa, na kubaki katika nafasi yao ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi, nafasi ambayo walikuwa nayo wakati wanaingia raundi ya 16.

Pia katika raundi hizo tatu ambapo Simba haikufungwa bao hata moja, Mwanjali alicheza dakika zote 270, na bila kuonyeshwa kadi yoyote. Alichangia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio ya timu yake huku akiongoza safu ya ulinzi.

Kwa kushinda tuzo hiyo ya mchezaji bora, Mwanjali atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) na wadhamini wakuu wa Ligi hiyo Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.

Wachezaji wengine walioshinda tuzo za mchezaji bora kwa msimu wa 2016/2017 hadi sasa ni John Raphael Bocco wa Azam (Agosti), Shiza Ramadhan Kichuya wa Simba (Septemba), Simon Happygod Msuva wa Yanga (Oktoba), na Rifati Hamisi wa Ndanda (Novemba).

WANANCHI JIMBO LA DIMANI, ZANZIBAR WAPIGA KURA KWA AMANI NA UTULIVU.

$
0
0

Na. Aron Msigwa – NEC, Zanzibar.

Hatimaye wananchi wa Jimbo la Dimani visiwani Zanzibar waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga leo wamejitokeza kwa wingi katika vituo mbalimbali kupiga kura kumchagua Mbunge atakayewawakilisha kwa kipindi cha miaka miaka 4.

Zoezi la upigaji wa Kura katika vituo mbalimbali lilianza majira ya saa 1 asubuhi  likifanyika kwa hali ya Amani na Utulivu huku baadhi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura wakipongeza maandalizi mazuri yaliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzine (NEC)  kufanikisha Uchaguzi huo.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage akizungumza kuhusu mwenendo wa Uchaguzi huo mara baada ya kutembelea vituo  vya kupigia kura katika jimbo hilo na  kuzungumza  na Mawakala wa Vyama vya Siasa waliokuwepo vituoni, Waangalizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wa Uchaguzi  huo amesema Tume imeridhishwa na kazi nzuri  iliyokuwa ikiendelea katika vituo mbalimbali vya kupigia Kura.

Viongozi wa Tume tumetembelea vituo mbalimbali vya kupigia Kura katika jimbo la Dimani; tumeona wenyewe upigaji wa Kura unaendelea vizuri, tumewauliza Mawakala, Watazamaji na Wasimamizi wa Vituo vya Uchaguzi  kila mmoja amesema Uchaguzi unakwenda vizuri, nachoweza kuwaambia watanzania Uchaguzi Dimani unakwenda Vizuri” Amesema Jaji Kaijage.

Amesema Wasimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo hilo wanaendelea kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili pia kushughulikia kwa haraka changamoto zilizokuwa zikijitokeza katika  baadhi ya vituo vya kupigia Kura.

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) akizungumza na Msimamizi kituo cha Dimani Bi. Abdu Simai Haji leo wakati zoezi la upigaji kura likiendelea katika jimbo la Dimani.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) akizungumza na waandishi wa Habari wa Zanzibar kutoa tathmini ya hali ya Uchaguzi mara baada ya kuetembelea vituo mbalimbali vya kupigia kura katika jimbo la Dimani leo. 
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (wa pili ) akiwa ameambatana na Baadhi ya Watendaji wa NEC na  Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Bi. Idaya Selemani Hamza (wa Kwanza) akiwasili katika kituo cha Kupigia Kura cha Kombeni katika jimbo la Dimani kuangalia maendeleo ya  Upigaji wa Kura leo.
 Mmoja wa Wananchi katika jimbo la Dimani akipiga Kura yake kumchagua Mbunge katika jimbo la Dimani leo.
 Baadhi ya Wangalizi wa Uchaguzi katika jimbo la Dimani wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Dimani leo.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji akutana na mamlaka za udhibiti na utoaji leseni.

$
0
0
Waziri wa viwanda, Biashara na uwekezaji akutana na kamati ya kuboresha ya mazingira ya biashara ambayo inahusisha wataalamu kutoka sekta mbalimbali katika wizara zote, TBS, EWURA, SUMATRA, TRA, OSHA, WMA, NCC, n.k na kujadili changamoto mbalimbali ambazo ni vikwazo katika wepesi wa kufanya shughuli.

Waziri amehimiza wataalamu hawa kujadili changamoto na kutoa mapendekezo ya namna ya kuondoa kero hizo ili kuboresha urahisi wa kufanya shughuli nchini Tanzania na kuvutia wawekezaji.

Waziri amehimiza ulipaji wa kodi ili kuleta maendeleo ya watu, kwani kwa takwimu Tanzania ni ya 154 kati ya nchi 190 hivyo kuhimiza wafanyabiashara wote kuwa na Tin namba na pia kulipa kodi.

Mkutano huu umefanyika jumamosi tarehe 21/1/2017 ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na muhogo mjini Kibaha.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza katika kikao cha wadau kutoka taasisi mbalimbali waliokutana na kamati ya  marekebisho ya wepesi wa kufanya shughuli nchini, kushoto kwa waziri ni Katibu Mkuu biashara na uwekezaji Mhe. Prof. Adolf Mkenda, Mwenyekiti wa kamati ya kuboresha mazingira ya biashara Dkt. John Mduma, kulia kwa  waziri ni Katibu tawala Kibaha Ndg. Anatory Mhango.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza katika kikao cha wadau kutoka taasisi mbalimbali waliokutana na kamati ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini katika ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na muhogo mjini Kibaha.
Katibu Mkuu Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Adolf Mkenda akizungumza katika kikao cha wadau kutoka taasisi mbalimbali waliokutana na kamati ya  kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini katika ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na muhogo mjini Kibaha.
Wadau kutoka taasisi mbalimbali za serikali waliokutana na kamati ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini katika ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na muhogo mjini Kibaha.
Wadau kutoka taasisi mbalimbali waliokutana na kamati ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini katika ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na muhogo mjini Kibaha.
Wadau kutoka taasisi mbalimbali waliokutana na kamati ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini katika ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na muhogo mjini Kibaha.

WAZIRI MWIJAGE APONGEZA KWA UJENZI WA KIWANDA CHA VIGAE

$
0
0

Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwa na  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete wakati walipokuwa wakitembea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani. 
Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiwa na  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete wakati walipokuwa wakitembea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani. 

Na.Mwandishi Wetu

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amepongeza jitihada zinazofanywa na muwekezaji wa kampuni TwyFord Tanzania Cereramics,kwa ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza vigae "Tiles" katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.


Waziri Mwijage, amesema hayo alipotembelea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo, litakalojengwa kiwanda hicho cha kutengeneza vigae "Tiles" kitakachotoa ajira kwa watanzania zaidi ya elfu mbili katika mfumo rasmi,na ajira elfu nne zisizo rasmi.



NEEMA YA MAJI SAFI NA SALAMA YANUKIA MAKAMBAKO

RAIS WA UTURUKI AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Uturuki, Mhe. Recep Tayyip Erdogan akiwa ameambana na mkewe Mama Emine Erdogan, wakiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Erdogan atakuwa nchini kwa ziara ya siku mbili kuanzia leo tarehe 22 Januari, 2017. 
 RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini leo jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na mgeni wake
 RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan mara baada ya kuwasili nchini leo jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,kulia ni mke wa Rais wa Uturuki,Mama Emine Erdogan

RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini leo jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.
Rais huyo ameambatana na mkewe Mama Emine Erdogan pamoja na Mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Mevlüt Çavuşoğlu,Waziri wa Uchumi Mheshimiwa Nihat  Zeybekekci na Waziri wa Nishati na Maliasili Mheshimiwa Berat Albayrak. Pia Rais huyo ameambatana na wafanyabiashara wapatao 85 wa nchi hiyo.

ALHAJ ALI HASSAN MWINYI AWATAKA WATANZANIA KUWA NA TABIA YA KUENDELEZA YALIYO MEMA.

$
0
0
Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi amewataka watanzania kuwa na tabia ya kuyafanyia muendelezo yale mema wanayoyafanya, kama walivyofanya kampuni ya NIDA TEXTILES kusherekea kumbukumbu ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W).

Akizungumza  katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam Alhaji Mwinyi amesema  kuwa Mtume Muhammad (S.A.W) alikuwa akifunga kila siku ya Jumatatu ikiwa ni ishara ya kusherekea siku aliyozaliwa.

 Hivyo ni vyema kuiga mfano huo wa kufanya matendo mema kwa kuyarudia mara kwa mara na kuyadumisha, huku akipongeza uongozi wa NIDA kwa kuwaalika na kusherekea pamoja kwani amejifunza mengi kupitia mawaidha yaliyotolewa na viongozi wa dini waliohutubia akiwemo Sheikh Ally Basaleh.

Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali akiwemo Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Gharib Bilal, Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo, Naibu Waziri Wizara ya Afya Hamis Kigwangala, Waziri wa zamani wa Ulinzi Profesa Juma Kapuya, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba, Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega. Viongozi wa dini waliokuwepo ni pamoja na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum na Kadhi Mkuu wa Tanzania Abdallah Mnyaa.

 Rais mstaafu wa awamu ya pili  Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza na  viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali juu ya watanzania  kuyafanyia muendelezo wa yale mema kama walivyofanya kampuni ya NIDA TEXTILES kusherekea kumbukumbu ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W). leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib  Bilal, akizungumza na  viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali katika kusherekea kumbukumbu ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W). leo jijini Dar es Salaam.
 Shehe Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Sheikh Alhadi Mussa Salim akizungumza machache katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0


SIMU.TV: Ujenzi wa kiwanda kikubwa cha vigae mkoani Pwani umeelezwa kuwa unaendela vizuri na kinatarajiwa kuanza uzalishaji ifikapo julai mwaka huu. https://youtu.be/2-aT3PPQl6g

SIMU.TV: Mamia ya wananchi katika jimbo la Dimani leo wamejitokeza kupiga kura ya kumchagua mbunge huku ulinzi ukiwa umeimarishwa katika vituo vyote. https://youtu.be/ZuMPbwiH_24

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo ameuagiza uongozi wa wilaya ya Rufiji kufanya uchunguzi  ili kubaini kama kuna watu wanao jihusisha na uvunaji wa mazao ya misitu kinyume na sheria. https://youtu.be/ef1rnm5Q3co

SIMU.TV: Mchakato wa utatuzi wa mgogoro wa Ardhi katika pori tengefu la Loliondo umeonekana kuwa mgumu baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha kuunda timu nyingine kuainisha maeneo muhimu ya hifadhi. https://youtu.be/0Zyn7dNtoUA

SIMU.TV: Serikali wilayani Hai mkoani Kilimanjaro imemtaka mwekezaji katika shamba la mboga mboga la Kilimanjaro Vegetables kusitisha shughuli zake kutoka na kukiuka sheria. https://youtu.be/-ktXIMxifcY

SIMU.TV: Wafugaji wa kabila la Baribaig wamegoma kuondoaka katika hifadhi ya jamii ya ziwa Mburuge licha ya serikali ya kijiji kuwataka kuondoka. https://youtu.be/IGP2ePptkec

SIMU.TV: Wananchi wa mtaa wa Polisi katika manispaa ya Songea wameiomba serikali kubomoa nyumba ya mwenyekiti wa CCM Ally Mandamba ambayo imejengwa katikati ya barabara. https://youtu.be/QYuls3Op-Fg

SIMU.TV: Beki mahiri wa klabu ya Simba Method Mwanjali amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi desemba wa ligi kuu Tanzania bara. https://youtu.be/bKFBAgR_8ek

SIMU.TV: Watumishi wa idara za serikali wamehimizwa kushiriki katika mazoezi na michezo mbalimbali ili kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza. https://youtu.be/5WcMmJGRee4

SIMU.TV: Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta ameendelea kung’ara katika ligi ya Ubelgiji baada ya hapo jana kuifungia bao la ushindi timu yake ya Genk. https://youtu.be/zjVxxdcB1IQ


MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 23,2017

MKUU WA WILAYA YA MKURANGA FILBERTO SANGA AFUNGUA RASMI LIGI YA MBUNGE (ULEGA CUP)

$
0
0
Na Emanuel Masaka, Globu ya Jamii

LIGI ya Mbunge wa Jimbo la Mkuranga  (Ulega Cup) imefunguliwa  rasmi jana kwa kuzikutanisha timu za Kipalang'anda  kombaini Fc na Mkuranga kombaini uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga.

Mashindano  hayo yamefunguliwa  na mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga  ukishuhudiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Juma Abed pamoja na baadhi ya madiwani wanaounda halmashauri hiyo.

Michuano hiyo ambayo ilianzia ngazi ya Vijiji ilishirikisha timu  125 na  baadae kuchujwa na kubakia timu 25 ambazo zimeingia ngazi ya wilaya na mshindi wa ligi hiyo ndio atakuwa bingwa wa wilaya. 

Akizungumza  na wachezaji wa timu hizo katika ufunguzi wa michuano hiyo Mkuu wa Wilaya hiyo Firbato Sanga  alisema michezo ni udugu na ujirani mwema hivyo aliwatakia michezo mwema.

Akizungumzia michuano hiyo Mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega amesema kuwa ni matarajio yake michuano hiyo itakwenda vyema  na lengo lake kubwa nikuona wanapata vijana wenye vipaji na watakaoweza kuipaisha Mkuranga.

"Nimatarajio yangu mambo yatakwenda kama nilivyopanga na kama mnavyoona wenyewe waandishi wa habari  vijana wa kutoka Mkuranga ndio wanaocheza "alisema Ulega

Amesema  tangu awali alisha kataa timu hizo kukodi watu Kutoka nje ya Mkuranga na anashukuru Mungu hayo yamezingatiwa na katika michuano hiyo mshindi ndio atakuwa bingwa wa Wilaya.

Amesema kuwa ana matumaini makubwa kwamba kupitia ligi hiyo watapatikanika vijana wenye uwezo ambao wataweza kuchukuliwa  na timu kubwa.

Aidha amesema kuwa michezo ni Afya ,ajira,na upendo kwani kupitia mashindano hayo watakuwa wametengeneza ujirani mwema hivyo watumie fursa hiyo kudumisha Umoja na mshikamono miongoni mwao.

Mchezo huo ulimalizika kwa goli moja lililofungwa na mchezaji wa timu ya Mkuranga Kombaini,Abdallah Mohamed  katika dakika ya kumi kipindi cha kwanza.

 Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ufunguzi wa Ligi ya Mbunge wa Jimbo la Mkuranga  (Ulega Cup)  uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga akizungumza  na wachezaji wa timu  za Kipalang'anda  kombaini Fc na Mkuranga kombaini katika ufunguzi wa Ligi ya Mbunge wa Jimbo la Mkuranga  (Ulega Cup)  uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Juma Abed  katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani.


.Mchezo ukiendelea ambapo mchezo huo ulimalizika kwa goli moja lililofungwa na mchezaji wa timu ya   Mkuranga Kombaini,Abdallah Mohamed katika dakika ya kumi kipindi cha kwanza.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii Pwani.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Mkuranga Kombaini pamoja viongozi mblimbali katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Kipalang'anda  kombaini Fc katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga mkoani Pwani. 

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

SIMU TV:YALIYOJIRI KATIKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI LEO January 21, 2017

$
0
0


Makamo wa rais wa Tanzania amesema Tanzania itaendeelea kudumisha na kuimarisha mahusiano mazuri na jamuhuri ya watu wa china: https://youtu.be/iUDEmN4fxA4

Waziri mkuu amesema serikali imetoa shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Njombe: https://youtu.be/ZMNf9HgyKBE

Uhaba wa chakula unaowakumba baadhi ya wananchi hapa nchini   umechukua sura mpya baada ya wakazi wa mkoa wa Rukwa kudai kuwa hawana njaa ya chakula: https://youtu.be/finpdqBqHng

Watanzania wapewa changamoto ya kuchangamkia  fursa ya masomo   zinazopatikana nchini Uturuki  ili waweze kupata taaluma bora: https://youtu.be/kh1Q1bk_5Jg

Spika wa bunge Mh.Jobu Ndugai amepokea barua ya kujiuzulu ubunge kutoka kwa Abdallah Posi  baada ya kuteuliwa kuwa balozi: https://youtu.be/FXLXvjmR_Xs

Klabu la gofu ya jeshi la ulinzi wa  wananchi wa Tanzania wapo kwenye maandalizi ya maadhimisho ya miaka 10 ya klabu ya Lugalo: https://youtu.be/U4_RmCEtPp8

TAHMEF YAWEZESHA MAMIA YA VIJANA KUCHANGIA DAMU WAGONJWA WENYE SELEMUNDU (SICKLE CELL) HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR

$
0
0
Shirika la Afya na elimu ya tiba Tanzania limefanikiwa kuendesha zoezi la uchangiaji damu kwa wagonjwa wenye selimundu (Sickle Cell) Siku ya Jumamosi Januari 21, 2017 katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.
Kijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA)  akichangia damu.
Zoezi hili limepewa ushirikiano mkubwa kutoka kwa vijana wakitanzania kutokana na idadi ya wachangiaji damu siku hiyo ambapo asilimia 95% ya wachangiaji damu ni vijana walio chini ya umri wa miaka 30 na asilimia 5% tu wakiwa juu ya miaka 30.

Mbali na uchangiaji damu vijana wengi walioshiriki wametumia vyema mitandao ya kijamii katika kuhamasisha watanzania kushiriki katika zoezi hili la uchangiaji damu.

Zoezi hili limelenga kuhusisha uchangiaji Damu kwa wagonjwa wa Selimundu na hivyo kuelimisha na kuchochea uelewa juu ya ugonjwa wa Selimundu (Sickle Cell) pia kuhimiza uboreshaji wa huduma za Afya Nchini kama inavyotajwa katika lengo la tatu katika malengo ya maendeleo endelevu duniani (Sustainable development Goals)

Zoezi zima liliandaliwa na kuendeshwa na Shirika la Afya na Elimu ya Tiba Tanzania (TAHMEF) kwa kushirikiana na Taasisi ya umoja wa wagonjwa wa Selimundu Tanzania, Vijana wa umoja wa mataifa (YUNA) na Lions Club ya Msasani Dar es salaam.

Shukrani Ziwafikie watanzania wote walioshiriki katika zoezi hili kwa njia mbalimbali ili kuokoa maisha ya watanzania wenzetu wenye uhitaji wa damu salama.

Zoezi hili linatarajiwa kuendelezwa tena kila baada ya miezi mitatu.
Muanzilishi wa shirika la Afya na Elimu ya Tiba (TAHMEF), Juliana Busasi (kushoto) akiwa na Muanzilishi wa Taasisi ya umoja wa wagonjwa wa selimindu Tanzania, Arafa Said (kati) na mmoja wa vijana waliochangia damu (kulia)
Lions Club Msasani wakikabidhi mahitaji ya zoezi la uchangiaji damu kwa wanachama wa TAHMEF.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

INTRODUCING: Mchezo Mbona Simple - Stamina,Beka Tittle,Darassa,King Kapita,James Cuca

$
0
0
Baada ya kimya cha muda kutoka studio Za Grandmaster Records, sasa wamekuja na kuendeleza mtiririko wa ile mixtape ya kihistoria ambayo safari yake iliianza na Life Goes On (Video iko chini pale. wanaomba mpokee zawadi hii kama mwanzo wa kuendeleza pale walipoishia. Isikilize hiyo ngoma hapo chini. Video ya ngoma ya Life Goes On hii hapa chini.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live


Latest Images