Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

TANZANIA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KUHARAKISHA MAENDELEO YA NCHI

0
0
Benny Mwaipaja,WFM-Dar es salaam

SERIKALI imesema kuwa inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi wa nchi na kuahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano na sekta hiyo ili kuharakisha maendeleo ya wananchi kupitia sekta ya viwanda na biashara.

Hayo yamesema na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha -IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa uchumi wa nchi unategemea sana sekta binafsi yenye nguvu na yenye utulivu ambayo itachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi kwa njia ya uwekezaji na ulipaji kodi.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, amesema kuwa Shirika lake limeridhika na kiwango kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa Tanzania miongoni mwa nchi za Afrika na kwamba wanatarajia kuona uchumi huo ukiendelea kukua zaidi kwa ushirikiano na sekta binafsi.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto), akiwa katika mazungumzo na mgeni wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, walipokutana Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (katikati) pamoja na maafisa waandamizi wa Wizara hiyo wakiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Ujumbe wa Tanzania na Shirika la Kimataifa la Fedha-IMF wakiwa katika mazungumzo Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam, ambapo Shirika hilo limeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania ili kufikia maendeleo inayoyatarajia kwa manufaa ya Taifa na wananchi wake kiuchumi na kijamii.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto), akiagana na mgeni wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam, ambapo IMF, imesifu jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano, katika kusimamia na kukuza uchumi wa Taifa.


KINANA AMNADI MGOMBEA UDIWANI NGARENANYIUKI LEO

0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimnadi mgombea Udiwani katika kata ya Ngarenanyuki, Arumeru mkoani Arusha, Mwalimu Zakaria Nnko, wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hiyo, uliofanyika katika uwanja wa shule ya Ngarenanyuki, leo Januari 21, 2017. (Picha na Bashir Nkoromo)

Inroducing "Zaba" by Mtafya & Nolesy

Bamiza Music Chart 21st January 2017

BODI YA FILAMU TANZANIA YAWAKUTANISHA WADAU WAKE KWENYE KIKAO KAZI CHA KUANDAA SERA YA TAIFA YA FILAMU NCHINI

0
0
Kilio cha muda mrefu cha wadau wa sekta ya filamu nchini sasa kinaelekea kupata ufumbuzi wa kudumu baada ya Bodi ya Filamu Tanzania kuwakutanisha wadau wake kwa ajili ya maandalizi ya sera mahususi itakayotoa mwongozo na kuendeleza sekta hiyo nchini.
Sekta ya filamu nchini imekuwa ikisimamiwa na Sera ya Utamaduni na Sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza Na. 4 ya mwaka 1976 pamoja na kanuni zake. 
Kukosekana kwa sera mahususi ya filamu nchini kuliibua changamoto mbalimbali. Changamoto hizo ni pamoja na kuwepo kwa filamu na michezo mingi ya kuigiza inayotayarishwa chini ya viwango, kutokuwepo kwa mitaji na uwekezaji wa kutosha, sekta ya filamu kutoendeshwa kibiashara, kukosekana kwa mifumo bora ya usambazaji, kutokuwepo kwa weledi na ubunifu wa kutosha, uharamia wa kazi za filamu n.k. 
Changamoto zilizoainishwa hapo juu zilibainika baada ya Bodi ya Filamu Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kufanya tafiti kuhusu hali halisi ya tasnia (situational analysis) na kuuwasilisha mbele ya kikao kazi cha wadau kilichofanyika tarehe 3 Oktoba, 2016 ukumbi wa uwanja wa Taifa. Kwenye kikao hicho, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye, aliagiza uongozi wa Bodi ya Filamu Tanzania na wizara yake kushirikiana pamoja kuhakikisha sera mahususi ya filamu inapataikana mapema iwezekanavyo. 
Sera hiyo mahsusi ya filamu nchini inategemewa kuwa mwarobaini wa changamoto zinzoikabili sekta hiyo kwa muda mrefu sasa.
 Ikumbukwe wadau wa tasnia ya filamu nchini wamekuwa wakilalamika kukosa mapato stahili yanayotokana na kazi zao, kushindwa kupata mitaji ya kuwawezesha kuwekeza miundo mbinu ya kisasa kwenye uzalishaji na mfumo hafifu wa kupambana na uharamia wa kazi zao.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo akitoa mchango wake mbele ya wajumbe wanaoshiriki kikao kazi cha maandalizi ya rasimu ya sera ya filamu nchini. Katikati ni rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifamba.

 Mwigizaji na mtayarishaji wa filamu za kitanzania Chiki Mchoma akiwasilisha hoja kama mdau wa tasnia ya filamu mbele ya wajumbe wa kikao kazi cha kuandaa rasimu ya sera ya filamu nchini. Wengine kwenye picha kuanzia kulia ni Mwnyekiti wa Bodi kuu Sylvester Sengerema, Mwenyekiti wa kikao Vonavyalo Luvanda, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisso na rais wa shirikisho la filamu nchini Simon Mwakifwamba.

 Wajumbe mbalimbali wanaoshiriki kikao kazi cha kuandaa rasimu ya sera ya filamu nchini wakifuatailia kwa makini hoja inayowasilishwa na mmoja wa wajumbe wa kikao hicho(hayupo pichani). Kikao hicho kinafanyika mjini Bagamoyo kwenye Taasisi ya Sanaa Bagamoyo (TaSUBA).

Wasanii na wadau wa tasnia ya filamu wanaoshiriki kikao kazi cha kuandaa rasimu ya sera ya filamu wakifurahia jambo na mwandishi mkongwe wa riwaya na miswada ya filamu Amri Bawji (mwenye baraghashia). Kikao kazi hicho kinafanyika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Sanaa Bagamoyo (TaSUBA).

ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MKOANI NJOMBE

0
0

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa  Njombe wakati alipokagua ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Njombe katika eneo la Wikichi katika  Wilaya  ya Njombe Januari 21, 2017.
 Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Iwawa wilayani  Makete wakimwimbia Waziri mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipokwenda shuleni hapo kufungua madarasa   yao Januari 21, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  akifungua madarasa  ya shule ya Sekondari ya Iwawa  iliyopo Makete Januari 21, 2017
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka wakiwa wameketi kwenye madawati ya moja kati ya madarasa mawili mapya yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu katika shule ya sekondari ya Iwawa iliyopo Makete Januari 21, 2017.  Katikati ni Mbunge wa Makete, Dkt. Norman Sigala
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole  Sendeka (kulia kwake ) na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Njombe, Deo Sanga kukagua maeneo ya shule ya sekondari ya Iwawa wilayani Makete  baada ya kufungua madarasa ya shule hiyo Januari 21, 2017. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na walimu wa shule ya sekondari ya Iwawa iliyopo Makete baada ya kufungua madarasa  ya shule hiyo Januari 21, 2017. Kwa habari kamili BOFYA HAPA

INTRODUCING "AMEFIA KILABUNI" BY MTOZA MC FT JEBBY

NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI JIJINI MBEYA

0
0
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Polisi alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kubaini mafanikio na changamoto za jeshi hilo.
 
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisikiliza maelezo juu ya gari lililokamatwa likisafirisha wahamiaji haramu   kutoka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benjamini Kaizaga(aliyenyoosha mkono).Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.(
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benjamini Kaizaga, juu ya gari  lililokamatwa likisafirisha madawa ya kulevya.Wengine mstari wa mbele  ni   Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula(wapili kulia)  na  Naibu Kamishna wa Uhamiaji,Asumsio Achachaa .Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
 
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia), akifurahia jambo wakati alipotembelea makazi ya mbwa wanaotumika na Jeshi la Polisi katika masuala ya ulinzi na usalama.Baada ya Naibu Waziri ni Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya,Emmanuel Lukula. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipanda mti katika makazi ya mbwa wanaotumika katika masuala ya ulinzi na usalama na Jeshi la Polisi.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)


WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI NA UBUNGE.

0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) akitoa Risala kuhusu upigaji wa Kura katika uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Dimani Zanzibar na Kata 19 za Tanzania Bara  leo mjini Zanzibar. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Hamid M. Hamid na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (Kulia).
 Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (Kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya Kisheria ya kuzingatiwa na wapiga Kura, Mawakala wa Vyama vya Siasa wakati wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika kesho, Januari 22, 2017. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa NEC, Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage.
Waandishi wa Habari wakiuliza maswali mbalimbali wakati wa Mkutano huo.Picha/ Aron Msigwa - NEC. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Ufungaji wa Kampeni za CCM za Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo Fuoni Mjini Magharibi

0
0
 Baadhi ya Wanachama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Dimani wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alipokuwa akizungumza katika ufungaji wa Kampeni za CCM za Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo Dimani  leo katika uwanja wa Mpira Fuoni  Mkoa wa Mjini Magharibi 
 Maelfu ya  Wanachama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Dimani wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alipokuwa akizungumza nao leo katika ufungaji wa Kampeni za CCM za Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo Dimani katika uwanja wa Mpira Fuoni  Mkoa wa Mjini Magharibi
 Wanachama wa Chama cha  Mapinduzi CCM Jimbo la Dimani wakinyanyua mikono juu kuunga mkono Hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alipokuwa akizungumza katika ufungaji wa Kampeni za CCM za Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo Dimani  leo katika uwanja wa Mpira Fuoni  Mkoa wa Mjini Magharibi
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alipokuwa akizungumza na Wanachama wa Chama cha  Mapinduzi CCM  katika ufungaji wa Kampeni za CCM uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo Dimani  leo katika uwanja wa Mpira Fuoni  Mkoa wa Mjini Magharibi 
 Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohameed Shein, akimtambulisha Mgombea wa Ubunge Jimbo la Dimani CCM Zanzibar,Juma Ali Juma wakati wa ufungaji wa kampeni za Uchaguzi mdogo wa Ubunge wa jimbo hilo uliofanyika leo katika viwanja vya mpira Fuoni. Picha na IKULU

Mdau CHRIS LUKOSI AKABIDHIWA UBANI WAKE, AWASHUKURU DIASPORA UK

0
0
Na Chris Lukosi
Napenda kuwashukuru sana Watanzania wote waishio UK kwa kujitolea kwa hali na mali wakati wa msiba wa Baba yangu 

Pamoja na makubwa waliyonifanyia ni pale waliponichangia kwa kila mtu alichokua na nacho ambapo ilisaidia kwa kiasi kikubwa kukamilisha mazishi ya mzee wangu.
Lakini wana diaspora hawakuishia hapo.  Leo hii Uongozi wa Tanzuk Diaspora (Watanzania Uingereza)   wamenikabidhi hundi ya pesa tasilimu pounds £2,400 kama rambi rambi  kutoka kwa uongozi wa Diaspora UK . Hizi ni tofauti na zile ambazo wana diaspora walinichangia kwa moyo mmoja moja kwa moja kwenye account yangu

Kwa kweli sina la kuwalipa zaidi ya asante, mliyonifanyia namuomba Mungu atuwezeshe tuwe na umoja huu wakati wote
UMOJA NI NGUVU...!
Mungu Awabariki Sana - AMINA

 Cheki aliyokabidhiwa Chris leo
Chris akikabidhiwa ubani wake kutoka kwa mmoja wa viongozi wa TZUK DIASPORA BW. Abraham Sangiwa nyumbani kwake Uingereza

LIVE! HARUSI YA MDAU KAINAMULA BWENGE UKUMBI WA MRINA JIJINI DAR

JUST IN: RAIS DKT MAGUFULI AMTEUA ANNA KILANGO-MALECELA KUWA MBUNGE

WAZIRI MWIJAGE AKAGUA MANDELEO YA AWALI UJENZI WA KIWANDA KIPYA CHA VIGAE, CHALINZE MKOANI PWANI

0
0
Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage (wa pili kushoto) akiwa ameongozana na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics, Jack Feng (kushoto) wakati walipokuwa wakitembea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani. Waziri Mwijage ameridhishwa na maandalizi ya ujenzi wa kiwanda hicho na kumpongeza muwekezaji wake hasa kwa kasi wanayoenda nayo. Kwa mujimu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics ambao ndio wamiliki wa kiwanda hicho, amesema kuwa ifikapo mwanzoni mwa mwezi septemba mwaka huu, kiwanda hicho kitakuwa kimekamilika na kitaanza kufanya kazi. Uwepo wa kiwanda hicho, utaweza kufungua fursa za ajira kwa vijana mbalimbali nchini.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage (katikati) akizungumza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics, Jack Feng (kulia) wakati alipotembea eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kulia) akimuonyesha kitu, Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage wakati walipokuwa wakitembea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage akimsikiliza Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Pendo Gondwe wakati akimueleza jambo, wakati alipotembea eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.
 

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 22, 2017


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKABIDHI MSAADA WA LAPTOP

0
0
 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Laptop Mwandishi Chipukizi wa Vitabu vya Taaluma, Ali Salum Alujai ukiwa ni msaada aliompatia ili aweze kufanya vizuri zaidi katika uandishi wake. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ikulu ndogo ya Njombe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


MAJALIWA:SERIKALI IMEANZA KULIPA MADENI YA WATUMISHI
*Jumla ya sh. bilioni 29 zililipwa mwaka jana

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imelipa jumla ya sh. bilioni 29 kwa watumishi mbalimbali wa umma wakiwemo walimu ikiwa ni sehemu ya madeni yao.

Alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Januari 21, 2017) wakati akizindua vyumba vitatu vya kisasa vya madarasa katika shule ya sekondari Iwawa iliyoko wilayani Makete.

Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kumaliza madeni ya watumishi hao, ambapo hadi kufikia Novemba mwaka jana jumla sh. bilioni 29 zililipwa kwa watumishi 31,000.Alisema kwa sasa Serikali imejipanga kuhakikisha hakuna madeni mapya yanayozalishwa hivyo amewataka watumishi wa umma na wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali.

Hata hivyo alisema Serikali inaendelea na mikakati ya kuboresha sekta ya elimu kwa kujenga mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia.“Tumeanza mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu katika halmashauri nchini. Hapa Makete tumeleta sh. milioni 557 kwa ajili ya ujenzi huo,” alisema.

Alisema nyumba hizo za walimu zinazojengwa katika maeneo mbalimbali hususan ya vijijini ni za kisasa ambazo zinalenga kuwaondolea changamoto ya makazi.Waziri Mkuu alisema Serikali inafanya jitihada za dhati za kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu kwa kuwa elimu ni kichocheo cha maendeleo ya jamii.

“Tumedhamiria kumpatia elimu kila Mtanzania, hivyo halmashauri zihakikishe kila kijiji kinakuwa na shule ya msingi na lazima ziwe na darasa la awali,” alisema.Naye Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Novatus Msivala aliishukuru Serikali kwa kugharamia ujenzi wa vyumba hivyo vitatu vya madarasa na matundu 10 ya vyoo pamoja na uingizaji wa maji kwenye vyoo na utengenezaji wa madawati 46.

Alisema ujenzi huo umegharimu sh. milioni 95 ambao utasaidia kupunguza msongamano kwa wanafunzi. Kwa sasa Serikali na wananchi wanaendelea kukamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya walimu.
                        
Katika hatua nyingine jana Waziri Mkuu alitimiza ahadi yake ya kumpatia laptop mwanafunzi Ally Alijai wa Chuo kikuu cha SAUT tawi la Songea mkoani Ruvuma.Ahadi hiyo aliitoa mwanzoni mwa mwezi huu alipokuwa katika ziara yake kikazi mkoani Ruvuma, lengo likiwa ni kuendeleza kipaji cha utunzi wa vitabu kwa mwanafunzi huyo.

Alisema mwanafunzi huyo alionyesha umahiri mkubwa katika utungaji wa kitabu ambacho kinaweza kutumika kufundishia katika shule za sekondari.

Hata hivyo Waziri Mkuu alisema tayari kitabu hicho kimeshawasilishwa Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) kuona kama kinaweza kuanza kutumika kwa kufundishia. Mwanafunzi huyo alishukuru kwa zawadi hiyo na kuahidi kutunga vitabu vizuri zaidi.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JANUARI 22, 2017.

VIJIJI 53 NJOMBE KUPATIWA HUDUMA YA MAJI -MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema jumla ya vijiji 53 vya mkoa wa Njombe vitapatiwa huduma ya maji safi na salama katika mwaka huu wa fedha.

Alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Januari 21, 2017) wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Wanging’ombe katika mkutano wa hadhara katika kata ya Ilembula.

Waziri Mkuu alisema zaidi ya sh. bilioni 2.4 zimetengwa kwa ajili ya kugharamia mradi huo wa maji katika miji ya Makambako, Njombe na wilaya ya Wanging’ombe.Alisema kati ya vijiji hivyo vitakavyopatiwa maji, vijiji 22 ni vya wilaya ya Wanging’ombe, hivyo aliwaomba wananchi hao kuwa na subira.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu tayari zabuni ya mradi huo imeshatangazwa, hivyo amewaagiza viongozi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji watafute mkandarasi mzuri.Alisema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya maji katika umbali usiozidi mita 400 kutoka mahali anapoishi.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo baada ya Mbunge wa Wanging’ombe, Mheshimiwa Mhandisi Gerson Lwenge kumuomba awasaidie katika kutatua kero ya maji.Mbunge huyo ambaye pia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji alisema “Mheshimiwa Waziri Mkuu sisi tunakabiliwa na changamoto ya maji, leo tunaomba ututatulie kero hii”.

Changamoto nyingine aliyoitaja Mheshimiwa Lwenge ni pamoja na ukosefu wa hospitali ya wilaya, ambapo Waziri Mkuu aliigiza halmashauri hiyo kuanza ujenzi.Alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 inaelekeza kuwa na hospitali katika kila wilaya, kituo cha afya kwa kila kata na zahanati kwa kila kijiji.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Ally Kasinge kukutana na viongozi wa kata na vijiji vinavyozunguka hifadhi ya Mapanga Kipengele ili kutatua kero ya mpaka.
                   

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JANUARI 22, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua jengo la Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe katika eneo la Igwachanya Januari 17, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo hilo katika eneo la Igwachanya , Januari 17, 2017.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha chai cha Kibena wilayani Njombe Januari 21, 2017.

                                       

MH ANASTAZIA WAMBURA AONGOZA MAZOEZI IRINGA

0
0
Naibu waziri wa habari, utamaduni, sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wikiendi hii  aliongoza wananchi wa mkoa wa Iringa katika mazoezi ya pamoja yaliyofanyika Uwanja wa michezo wa Samora Machel kupambana na magonjwa kama kisukari na shinikizo la damu. 
Mazoezi hayo ambayo yalianzia ofisi ya mkuu wa mkoa yalishirikisha viongozi, watumishi wa taasisi mbalimbali pamoja na wanachi. Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza alimshukuru Naibu Waziri kwa kutenga muda wake na kujumuika na wana Iringa. Akihitimisha mazoezi hayo Mhe wambura alisisitiza suala la lishe bora na kuwaasa watanzania kugeuza mazoezi kuwa utamaduni. “ Kila mtanzania popote alipo aanze sasa kuona mazoezi ni moja ya mila na desturi yake au utamaduni” 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela alisisitiza kuwa mazoezi hayo yataendelea kila Jumamosi kasoro Jumamosi ya usafi, na kwamba arehe 4/2/2017 mazoezi haya yatafanyika tena ambapo anatarajiwa kualikwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe Ummy Mwalimu kuja kushiriki mazoezi. 
Wananchi wa rika mbali mbali walitembea pamoja na viongozi wa mkoa na wilaya. Akihojiwa kamanda wa Polisi wa Mkoa Kamishna Msaidizi wa Polisi Mjengi alisema amaefarijika kuona mwamko wa mazoezi “ Sisi (polisi) tunafanya mazoezi karibu kila siku mwamko huu ukiendelea Iringa hakutakuwa na magonjwa kabisa pia itawajenga wananchi kujilinda na uhalifu.”
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongoza jinsi ya kufanya mazoezi ya viungo katika Uwanja wa Samora Machel
  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongoza jinsi ya kufanya mazoezi ya viungo katika Uwanja wa Samora Machel
  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongoza jinsi ya kufanya mazoezi ya viungo katika Uwanja wa Samora Machel
 Naibu waziri wa habari, utamaduni, sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiongoza mazoezi
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa na  kamanda wa Polisi wa Mkoa Kamishna Msaidizi wa Polisi Mjengi kwenye mazoezi hayo.

VOA Swahili: Maandamano ya Wanawake Washington

TANZIA: Kamanda wa polisi wa zamani mkoa wa kilimanjaro Dkt. Mohamed Chico afariki dunia

0
0
Kamanda wa polisi wa zamani mkoa wa kilimanjaro Dkt. Mohamed  Chico amefariki Dunia  usiku wa kuamkia leo jijini Dar es salam. 
Kwa mujibu wa msemaji wa familia Bw. Awadhi Chico, mazishi yake yamepangwa kufanyika leo Jumapili 22/01/2017 jioni katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. 
Msiba upo nyumbani kwa marehemu Kijitonyama. Habari ziwafikie ndugu, jamaa, marafiki na majirani popote pale walipo.
Mwenyezi Mungu amjaalie kauli thabit na ailaze roho yake mahali pema peponi - AMIN

Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un


Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images