Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110026 articles
Browse latest View live

SERIKALI KUANGALIA UPYA KANUNI ZA TAFITI ILI ZIWEZE KUFANYA KAZI KWA WAKATI

$
0
0

Dotto Mwaibale, Dodoma

SERIKALI imesema itaangalia upya taratibu na kanuni zilizopo ili kuharakisha tafiti za kilimo zinazofanyika nchini zianzekufanya kazi kwa wakati.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,  Charles Tizeba wakati alipotembelea jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo asubuhi.

"Binafsi nisema katika teknolojia hii ya uhandisi jeni kwa hapa nchini tumechelewa kutokana na taratibu na kanuni zetu kutuchelewesha kwani maarifa ya watafiti wetu hayawafii walengwa kutokana na kanunu hizo" alisema Tizeba.Alisema ni lazima serikali kuangalia jambo hilo ili kufupisha matokeo ya utafiti wa wataalamu wetu kuendelea kufanya hivyo ni kucheleweshana.

Alisema mbegu hii ambayo inafanyiwa utafiti kwa wenzetu wa Afrika Kusini wameanza kuitumia wakulima wao lakini kwa sisi kwa utaratibu wetu mbegu hiyo tutaanza kuitumia mwaka 2021 ni miaka minne zaidi.

"Tusisubiri taratibu hizi tutazungumza na wenzetu wa Ofisi ya Mkamu wa Rais  Mazingira na Tume ya Taifa Sayansi na Teknlojia (Costech) ili kuona namna ya kupunguza taratibu na kanuni hizo ambazo hazina tija kwa mkulima.

Alisema kama utafiti umefanyika na ukatoa matokeo mazuri hakuna sababu ya kusubiri na kupoteza muda wa matumizi ya teknolojia hiyo.Alisema leo tabia nchi imeendelea kukua na ukame lakini sisi tunajifunga katika jambo ili ni lazima tujipange na kutumia teknolojia hii muhimu.
 Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,  Charles Tizeba (kushoto), akizungumza na watafiti wa kilimo na wanahabari (hawapo pichani), wakati alipotembelea shamba la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk.Hassan Mshinda.
 Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,  Charles Tizeba (kulia), akizungumza na watafiti wa kilimo wakati alipotembelea jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya na Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kati Makutupora, Leon Mroso.
 Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kushoto), akimuelekeza jambo Waziri Tizeba.
 Taswira ya shamba hilo la jaribio la mbegu za mahindi lililopo Makutupora mkoani Dodoma.
Waziri Tizeba  (wa sita kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na watafiti wa kilimo baada ya kutembelea shamba hilo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA



MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 21, 2017

TAASISI ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) kufanya kazi na Mkoa wa Simiyu

$
0
0
TAASISI ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) imeahidi kufanya kazi na Mkoa wa Simiyu katokana na utayari wake wa kutafsiri kivitendo dhamira ya Rais Dk Magufuli ya Tanzania ya Viwanda.
"Tumekubali kuja Simiyu kufanya 'feasibility study' ya kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa za sekta ya afya zitokanazo na pamba, " alisema 
Prof Mkumbukwa, Mkurugenzi Mkuu wa TIRDO, ambaye pia alimwambia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,  Mh Anthony Mtaka kuwa wako tayari kuanza kazi hiyo mara moja.
"Tuna PhD 12 hapa na wengine wote ni Masters, tuko tayari kuja kufanya ukaguzi wa mwanzo wa kimazingira (preliminary environmental impact assessment) kwasababu tunaunga mkono juhudi zenu," alisema Prof Mkumbukwa.
Akiongea na wafanyakazi wa TIRDO,  Mh. Mtaka aliwapongeza kwa kuwa 'reference laboratory' ya Tanzania, dhamira iliyojengwa na credibility iliyowafanya wachague kufanya nao kazi.
"Nyie ndiyo mmetusaidia kufanya chaki zetu kuwa salama kabisa tofauti na chaki zingine," alisema na kuongeza kuwa TIRDO walihakikisha kuwa vumbi la chaki halina madini yanayoweza kumwathili mwalimu au mtumiaji wake.

RC Mtaka aliwaomba TIRDO, katika wakati wote wa mradi, wawapatie ushauri wa kitaalamu katika miradi yao, ombi ambalo lilipokelewa na kukubaliwa palepale.
"Unawezaje kumpa kazi ya kukupa ushauri wa kitaalamu mzungu  au mchina, kutengeneza vifaa vya sekta ya afya wakati yeye mwenyewe anavitengeneza hivyo na anataka uendelee kuwa soko lake na kama mshindani wake anaweza asikupe ushauri wa kukujenga ili ushindane nae, " alisema Mh Mtaka.

"Nitakuwa Balozi wenu popote nitakakokwenda kutokana na kazi nzuri ambayo nimeishuhudia hapa pamoja na raslimali watu walioko hapa" alisema.
Aliwashukuru kwa kukubali kupunguza gharama za utaalam wa kazi ya feasibility study na uandaaji wa mpango wa biashara kutoka milioni 700 ambayo ndiyo gharama halisi hadi milioni 150.
"Tumeamua kujenga mkoa mpya wa kiuchumi Simiyu, tunawaomba TIRDO, TFDA,  TBS,  TEMDO,  TIB, SIDO pamoja na Simiyu, tuungane kujenga viwanda kuifanya Tanzania ya viwanda iwe halisi.
Mh Mtaka na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu, walimaliza ziara yao iliyokuwa na mafanikio makubwa katika jitihada zao za ujenzi wa viwanda na kuanzisha kilimo cha umwagiliaji.

 Mkurugenzi Mkuu wa TIRDO Prof Mkumbukwa akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,  Mh Anthony Mtaka
Mkurugenzi Mkuu wa TIRDO Prof Mkumbukwa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,  Mh Anthony Mtaka kuhusu fursa zilizopo mkoani humo.

Madaktari Nchini Watakiwa Kufanya Upasuaji Bila Kufungua Tumbo kwa Kinamama

$
0
0
Madaktari nchini wametakiwa kufanya upasuaji bila kufungua tumbo kwa kinamama mara kinamama wanapolazimika kupatiwa huduma hiyo kwa kuwa ni njia salama zaidi na gharama nafuu. 
Ushauri huo umetolewa lLeo na Profesa Rafique Parker kutoka nchini Kenya katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es salaam. 
Profesa Parker ametoa mafunzo ya kufanya upasuaji bila kufungua tumbo kwa madaktari wa kinamama kutoka hospitali mbalimbali jijini Dar es Salaam. 
 “Madaktari mnapaswa kubadilika na kufanya upasuaji bila kufungua tumbo. Kama hamtaki kufanya hivyo dunia itawacha nyuma kwani upasuaji huu ni wa kisasa, rahisi kuliko wa kufungua tumbo na wa gharama nafuu,”amesema Profesa Parker. 
Amesema kabla ya daktari kufanya upasuaji huo anapaswa kuhudhuria kozi mbalimbali zinazohusiana na upasuaji wa bila kufungua tumbo na kwamba ili wafanikiwe wanapaswa kusoma na kuweka nia ya dhati ya kutoa huduma hiyo kwa kinamama. 
 Profesa Parker amewaeleza madaktari hao kwamba mafanikio ya kufikia kwenye upasuaji huo, hayaji siku moja bali wanapaswa kuweka juhudi na kupenda kujifunza mara kwa mara ili kufikia hatua hiyo ambayo ni msaada mkubwa kwa kina mama wenye matatizo ya uzazi pamoja na magonjwa mengine ya tumbo. 
 “Huwezi kujifunza upasuaji bila kufungua tumbo kwa siku moja, daktari anapaswa kuudhuria semina nyingi na kutumia zaidi ya saa nyingi kufikia mafanikio. Kuna madaktari wengi baada ya kumaliza masomo yao hawasomi vitabu, wanaamini kwamba wanajua kila kitu, lakini si kweli. Mnapaswa kubadilika,” amesisitiza Profesa Parker. 
 Mafunzo hayo yamehudhuriwa na madaktari bingwa wa Muhimbili, hospitali ya Temeke, Tumaini, Aga Khan, Dar Group, Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS) na hospitali ya Regency pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru.
 Profesa Rafique Parker akiwaeleza madaktari kutoka hospitali ya Temeke, Muhimbili, Aga Khan, Regency, Tumaini, Dar Group na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili umuhimu wa kufanya upasuaji bila kufungua tumbo (laparoscopy) kwa kinamama wanaopaswa kupatiwa huduma hiyo. Semina hiyo imefanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
 Mkurungezi wa Hopsitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (kulia) akiwa  namadaktari wengine wakimsikiliza Profesa Parker wakati akitoa mada kwa madaktari jinsi ya kufanya upasuaji bila kufungua tumbo kwa kinamama.
 Profesa  Rafique Parker akiwaleza madaktari hatua za kufuata kabla ya kufanya upasuaji bila kufungua tumbo.

 Daktari bingwa wa kinamama, Dk Tarimo (kushoto) wa Muhimbili akiwa na madaktari wengine kutoka katika hospitali mbalimbali jijini Dar es Salaam.
 Madaktari kutoka katika hospitali mbalimbali jijini Dar es Salaam wakifuatilia somo.

PAC yatoa miezi 6 kwa Taasisi na Mashirika kuilipa ankara Tanesco laasivyo kukatiwa umeme.

$
0
0
Na Zuena Msuya, Mbeya

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) imetoa miezi sita kwa Taasisi  na Mashirika yote kulipa madeni ya ankara wanayodaiwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na endapo watashindwa kufanya hivyo watakatiwa huduma hiyo.

Agizo hilo limetolewa mkoani Mbeya na Mwenyekiti wa Kamati ya PAC , Livingtone Lusinde wakati wa ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo wakati wa kukagua matumizi halisi ya fedha za Serikali katika kutekeleza Miradi ya Umeme Vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati wa Vijijini( REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini Tanesco.

Lusinde alisema Tanesco imekuwa ikishindwa kutimiza majukumu yake kutokana na kukosa fedha za kutosha kujiendesha na hivyo kuwakosesha wananchi hudumu muhimu ya umeme katika maeneo mbalimbali .

" Tanesco imetapakaa nchi nzima, lakini haiwezi kutoa huduma bora za uhakika kwa wateja wake katika maeneo yote hayo kutokana na miundominu mibovu na kutomfikia mteja kwa wakati kwa vile tu hawana fedha", alisema Lusinde.

 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali( PAC), wakielezwa  na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani( katikati) namna ambavyo kifaa maalum kinachofahamika kama umeme tayari( UMETA) umeme tayari kinavyofanya kazi,

 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC), wakiwa katika ziara ya kukagua matumizi halisi ya fedha za Serikali katika utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini.

 Wafanyakazi wa Kampuni ya JV State Grid wanaotekeleza Miradi ya Umeme Vijijini katika wakiendelea na kazi ya kujenga miundombinu ya Umeme Vijijini katika kijiji cha Masukulu wilayani Rungwe.

 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC), wakiwa katika ziara ya kukagua matumizi halisi ya fedha za Serikali katika utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani(kulia), Mwenyeketi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali( PAC) Livingstone Lusinde (katikati) wakisaini vitabu vya wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, wakati wa ziara ya kukagua miradi ya umeme vijijni wilayani humo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MAZIWA YA ASAS DAIRIES LTD NI MAZIWA BORA - MAJALIWA

WAZIRI NAPE NNAUYE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ITALIA NCHINI

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akisalimiana na Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Roberto Mengoni wakati alipotembelewa ofisini kwake leo 21 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) akieleza masuala mbalimbali yanayohusiana na habari na utamaduni wa Italia wakati alipomtembelea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye leo 21 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Picha zaidi BOFYA HAPA

HOJA YA HAJA: UTEUZI WA DR POSSI KUWA BALOZI, HAUJASABABISHWA NA UTATA WA KIKATIBA

$
0
0

Na Augustino Chiwinga
Hamna Ibara yoyote ile  katika katiba ya  Tanzania inayomlazimisha Rais we Tanzani kuteua wabunge kwa uwiano wa  kijinsia.
Naona kuna baadhi ya watu wanapiga chapuo huenda kuteuliwa kw Daktari wa sheria Abdallah Possi  (pichani) kuwa Balozi huenda kumesababishwa na hatua ya Rais Magufuli kuteua wabunge sita wa kiume na wawili wa kike na kwamba anavunja ibara ya 66(e). 
Kwanza ieleweke kwa mujibu wa sharia katiba inayotumika na  kutambulika ni ile iliyochapishwa katika lugha ya kiswahili ambayo haijaweka masharti kwa Rais kuteua wabunge kwa uwiano wa kijinsia.
Kwa mujibu wa kifungu cha  84 ya Interpretation of Laws Act 
(1)Lugha za sheria za Tanzania zitakuwa ni Kiswahili au Kiingereza au lugha zote mbili.
(2) Pale ambapo Sheria yoyote imetafsiriwa kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine na kuchapishwa kwa lugha zote mbili, na iwapo itatokea mgongano au kutakuwa na mashaka ya maana ya maneno, maelezo, lugha ambayo imetumika wakati wa kupitisha Sheria hiyo na Bunge ndiyo itakayokuwa ya kipaumbele.
Kifungu kilichonakiliwa hapo juu kinaelekeza kwamba iwapo sheria imechapishwa kwa lugha zote mbili na ikatokea mgongano au mashaka katika maneno/ maelezo yaani  toleo la lugha moja linakuwa na maana inayokinzana/tofautiana na toleo la lugha nyingine, kinachotakiwa kutumika hapa ni toleo la lugha ambayo ilitumika na Bunge kuipitisha sheria husika. 
Swali muhimu sana je lugha ipi basi amabayo ilitumika kuipitisha Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania??? Katika kesi Daudi Pete v. Republic [1993] TLR 22 at p. 33  mahakama iliweka bayana kwamba; "that the controlling version of the Constitution is the Kiswahili one and not the English version because the Constitution was enacted in Kiswahili." (Maana yake ni kwamba toleo la kiswahili la Katiba ndiyo lenye nguvu na sio toleo la Kiingereza kwa sababu Katiba ilipitishwa katika lugha ya Kiswahili.) 
Kwa hiyo basi kutokana na uamuzi wa Mahakama katika kesi ya Daudi Pete pale inapotokea kuna tofauti ya maana au maelezo baina ya toleo la Kiswahili la Katiba na toleo la Kiingereza la Katiba, maana iliyopo kwenye toleo la Kiswahili ndiyo itakayotumika. 
Kwa maelezo hayo niliyotoa ni dhahiri kuwa uamuzi wa Rais Mheshimiwa John Pombe Magufuli kuteua  wabunge wengi wa kiume uko sahihi kisheria wala hajavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.
Dr Possi ameteuliwa kua Balozi ni kutokana na sifa  kielimu  ,weledi wake uzoefu, uadilifu wake na uchapakazi wake na sio kwa lengo la "kubalance" uwiano wa kijinsia kama baadhi ya watu wanavyopotosha.

MO DEWJI ATANGAZWA KUWA MSHINDI WA TUZO YA AFRICAN LEADERSHIP MAGAZINE PERSON OF THE YEAR 2016

$
0
0
Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji ametangazwa na Jarida la African Leadership kuwa mshindi wa tuzo ya African Leadership Magazine Person of the year 2016 baada ya kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro kilishohusisha watu nane. 

MO Dewji ambaye ni Mtanzania anayejihusisha na biashara kupitia kampuni yake ya MeTL Group na kusaidia jamii kupitia Taasisi ya MO Dewji ameibuka mshindi kwa kupata asilimia 60.8 ya kura zote zilizopigwa akifuatiwa na Rais mstaafu wa Ghana, Dramani Mahama ambaye alipata asilimia 30.2. 
Wengine waliowania tuzo hiyo ni Strive Masiyiwa, Chris Kirubi, Akinwumi Adesina, Cyril Ramaphosa, Atiku Abubakar na Aisha Mohammed. 
Akizungumza kuhusu MO Dewji, Mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Jarida la African Leadership, Joe Beasley amemtaja MO Dewji kama mtu ambaye anaumuhimu mkubwa kutokana na dhamira yake ya kusaidia bara la Afrika kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa kutoa nafasi nyingi za kazi. 
“Dhamira ya Dewji ni kutengeneza ajira jambo ambalo ni kiini cha tatizo kubwa linalokabili Afrika la ukosefu wa ajira … kupitia biashara zake amesaidia kupunguza ukosefu wa ajira, kupata utajiri na kutoa ajira kwa vijana ambao hawana ajira barani (Afrika),” alisema Beasley.

Mohammed Dewji anakuwa mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka 2016 ambapo kwa mwaka 2015 ilichukuliwa na Rais Mstaafu wa Nigeria, Goodluck Jonathan.

Balozi Seif aongoza Maulid ya Uzawa wa Mtume Muhammad (SAW) ya Jumuiya ya Ismailia Jijini Dar es salaam.

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akipokewa na Rais wa Jumuiya ya Ismailia Tanzania Bwana Amin Lakhani kwenye Maulidi ya Uzawa wa Mtume Mhammad (SAW) yaliyoandaliwa na Jumuiya hiyo hapo Upanga Mjini Dar es salaam. Kati kati yao ni Mwakilishi wa Agakhan upande wa Zanzibar Bwana Mohame Bhaloo.
 Mkurugenzi wa masuala ya Taaluma na Dini ya Kiislamu na Historia wa Jumuiya ya Isimailia Tanzania Dr. Amin Rehmani akichambua masuala mbali mbali ya Dini ya Kiislamu kwenye muhadhara huo wa Maulidi. 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akihutubia kwenye hafla ya Maulid ya Uzawa wa Mtume Muhammad (SAW) ya Jumuiya ya Ismailia Jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu waliohudhuria Maulidi ya Uzawa Mtume Muhammad (SAW)  yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Ismailia Upanga Mjini Da es salaam.
 Sheikh wa Jumuiya ya Darkhana Jamat Alfaran Dewji akisoma fatha ya kufunga hafla ya Maulidi ya Uzawa wa Mtume Muhammad (SAW) ya Jumuiya hiyo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


MHE. WAMBURA AONGOZA MAZOEZI UWANJA WA SAMORA IRINGA ASUBUHI YA LEO

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akipongeza  wananchi  kwa  kuitikia mazoezi ,katikati ni mkuu wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza na mkuu wa  wilaya  Iringa Richard Kasesela
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura mwenye kikoi shingoni akiongoza mazoezi  Iringa  leo
Mazoezi  ya  viungo  kwa afya  yakiendelea

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura wa tatu kushoto na  viongozi mbali mbali wakiongozwa  kufanya mazoezi na Dc Iringa  Richard Kasesela,wa  kwanza  kushoto  ni mkuu  wa mkoa Iringa Amina Masenza, mbunge wa viti wa  maalum mkoa  wa Iringa  Ritta Kabati ,mbunge  wa Kilolo Venance  Mwamoto na katibu tawala  mkoa  wa Iringa  Wamoja  Ayub.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

NEWS ALERT: BALOZI MTEULE DKT. ABDALLAH POSSI AJIUZULU UBUNGE

MAHAFALI YA 12 CHUO KIKUU CHA TAIFA SUZA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) akimtunuku Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Kemia "MASTER OF SCIENCE IN CHEMISTRY"Nd.Issa Juma Salim katika sherehe ya mahfali ya kumi na mbili ya chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) akimtunuku Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Mazingira  "MASTER OF SCIENCE IN ENVIROMENTAL SCIENCE" Saklim Masoud Msabaha  katika sherehe ya mahfali ya kumi na mbili ya chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) akimtunuku Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Mazingira  "MASTER OF SCIENCE IN ENVIROMENTAL SCIENCE" Saklim Masoud Msabaha  katika sherehe ya mahfali ya kumi na mbili ya chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kutoa hutuba yake kwa wananchi  katika sherehe ya mahfali ya kumi na mbili ya chuo hicho yaliyofanyika leo katika kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja. Picha na Ikulu.
Habari kamili BOFYA HAPA

Mkutano wa East African Power Pool wafanyika Jijini Arusha

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini Pofesa Sospeter Muhongo akiongea na Waandishi wa Habari Baada ya Mkutano wa East African Power Pool Uliofanyika Jijini Arusha. Mkutano huo ulihudhuriwa na nchi wanachama 11  (Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia, Misri, Sudan, Rwanda, Burundi, DRC, Somalia na Elitrea),  Lengo la mkutano huo likiwa  kuandaa mpango kazi na Bajeti ya Kuendeleza miradi ya umeme katika nchi wanachama

AFCON 2017


JK Ashiriki Uzinduzi wa Baraza la Kutokomeza Malaria Duniani (End Malaria Council) Davos, Uswisi

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, Davos, Uswisi
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameshiriki katika uzinduzi wa Baraza la Kutokomeza Malaria Duniani (End Malaria Council) uliofanyika tarehe 19 Januari, 2016 huko Davos Uswisi.
Baraza la Kutokomeza Malaria linaundwa na Wajumbe 9 ambao ni watu mashuhuri katika sekta ya umma na sekta binafsi duniani. Wajumbe hao ni wafuatao:
1. Bill Gates- Mwanzilishi na Mmiliki wa Bill Gates Foundation
2. Ray Chambers- Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malaria
3. Peter Chermin-Mwanzilishi wa Chermin  Entertainment na Chermin Group
4. Aliko Dangote- Rais na Mtendaji Mkuu wa Dangote Group
5. Mhe. Idrisa Deby-Rais wa Chad kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa Taasisi ya ALMA
6. Mhe. Jakaya Kikwete-Rais Mstaafu wa Tanzania
7. Mhe.Graca Machel- Mwanzilishi wa Foundation for Community Development,Msumbiji
8. Luis Alberto Moreno-Rais wa Inter-American Development Bank
9.Mhe. Ellen Johnson Sirleaf- Rais wa Liberia.

Lengo la Baraza hilo ni kuunganisha nguvu za wadau na mataifa duniani kukabiliana na hatimaye kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2030. Kuanzishwa kwa Baraza hilo kumetokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika vita dhidi ya malaria katika miaka 15 iliyopita katika kupunguza vifo na maambukizi ya Malaria duniani kama ilivyoripotiwa na Ripoti ya MalariaDuniani ya mwaka 2016 ya Shirika la Afya Duniani. Msingi wa mafanikio hayo ndio chachu ya jitihada mpya za kutokomeza Malaria duniani ifikapo 2030.

Katika kikao chake cha kwanza kilichofanyika Davos, Baraza hilo limejadili kuhusu upatikanaji wa rasilimali za kutosha za kuwezesha kutoa msukumo katika upatikanaji wa vifaa tiba, dawa, tafiti na uvumbuzi wa mbinu na nyenzo za kisasa za kuzuia, kupambana na hatimaye kutokomeza ugonjwa wa Malaria katika nchi za Afrika, Asia na Amerika ya Kusini.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa Baraza hilo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, ambaye utotoni kwake alipoteza kaka yake kwa ugonjwa wa  Malaria pamoja na ndugu wengine wengi kaika maisha yake amesema, " Kutokomeza Malaria iliwahi kuwa ndoto isiyotekeleza, lakini sasa kuifikia ndoto hiyo ni dhahiri.....tunawea kuifanya Malaria kuwa historia na kuutokomeza ugonjwa huu katili katika uso wa dunia".

Tanzania ni moja ya nchi zinazosifika barani Afrika na duniani kwa kuweza kupiga hatua kubwa katika kutokomeza ugonjwa wa Malaria. Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, takwimu zinaonyesha kuwa maambukizi ya malaria yamepungua kwa asilimia 70 na vifo vimepungua kwa asilimia 50.
Kwa habari zaidi fuatilia kwenye www.endmalariacouncil.org

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Bw. Ray Chambers ambaye ni  Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malaria  katika uzinduzi wa Baraza la Kutokomeza Malaria Duniani (End Malaria Council) uliofanyika tarehe 19 Januari, 2016 huko Davos Uswisi.
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Aliko Dangote na Bill Gates katika uzinduzi wa Baraza la Kutokomeza Malaria Duniani (End Malaria Council) uliofanyika tarehe 19 Januari, 2016 huko Davos Uswisi.
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akiongea na Bw. Bill Gates akisalimiana na Mwanzilishi na Mmiliki wa Bill Gates Foundation katika uzinduzi wa Baraza la Kutokomeza Malaria Duniani (End Malaria Council) uliofanyika tarehe 19 Januari, 2016 huko Davos Uswisi.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akiongea na Bw. Bill Gates,  Mwanzilishi na Mmiliki wa Bill Gates Foundation, katika uzinduzi wa Baraza la Kutokomeza Malaria Duniani (End Malaria Council) uliofanyika tarehe 19 Januari, 2016 huko Davos Uswisi.

WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI NA UBUNGE

$
0
0
Na. Aron Msigwa –NEC, Zanzibar.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wananchi wanaoishi katika kata 19 zitakazofanya Uchaguzi mdogo wa Madiwani kwa upande Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani Zanzibar, Januari 22, 2017 wajitokeze kwa wingi kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka 3.

Akizungumza na vyombo vya Habari leo mjini Zanzibar, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles kaijage amesema kuwa maadalizi ya Uchaguzi huo yamekamilika na wananchi wote wenye sifa za kupiga kura katika uchaguzi wajitokeze wingi kutimiza wajibu wao wa Kikatiba.

Mhe. Kaijage amewapongeza wananchi wanaoishi katika Jimbo la Dimani, Zanzibar na wale wa Kata 19 za Tanzania Bara watakaofanya uchaguzi mdogo hapo kesho (Januari 22, 2017) kwa utulivu waliouonyesha katika kipindi chote cha Kampeni za wagombea wa vyama mbalimbali vya Siasa.

Amesema licha ya kuwepo kwa dosari za hapa na pale zilizojitokeza zikiwemo za ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi kwa baadhi ya Vyama na wagombea wao, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilichukua hatua za kukemea vitendo hivyo ili kuwezesha Kampeni za Uchaguzi kufanyika kwa Usalama na Amani.

“Licha ya kwamba kutakuwa na ulinzi wa kutosha katika vituo vya kupigia kura, Ni matumaini ya Tume kuwa hali ya Amani na Utulivu ambayo imekuwepo hadi sasa na kama ilivyokuwa katika Chaguzi zilizopita itaendelea kudumishwa ili kuhakikisha uchaguzi huu unafanyika kwa Utulivu, Amani na Ustawi wa Taifa letu” Amesema Jaji Kaijage.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) akitoa Risala kuhusu upigaji wa Kura katika uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Dimani Zanzibar na Kata 19 za Tanzania Bara leo mjini Zanzibar. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Hamid M. Hamid na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (Kulia).
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (Kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya Kisheria ya kuzingatiwa na wapiga Kura, Mawakala wa Vyama vya Siasa wakati wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika kesho, Januari 22, 2017. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa NEC, Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage.
Waandishi wa Habari wakiuliza maswali mbalimbali wakati wa Mkutano huo. 

ZIARA YA MAJALIWA MKOANI NJOMBE

$
0
0
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Iwawa wilayani Makete wakimwimbia Waziri mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipokwenda shuleni hapo kufungua madarasa yao Januari 21, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka wakiwa wameketi kwenye madawati ya moja kati ya madarasa mawili mapya yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu katika shule ya sekondari ya Iwawa iliyopo Makete Januari 21, 2017. Katikati ni Mbunge wa Makete, Norman Sigala., (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NAIBU MEYA ILALA AWATAKA WENYE VIWANDA KULINDA MASLAHI YA WAFANYAKAZI

$
0
0
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary  Kumbilamoto akizungumza na wadau wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha dawa cha ZENUFA.
Mkurugenzi wa kiwanda cha Zenufa Laboratories Ltd,Hitesh Upret akizungumza na wadau wa wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho na muonekano wa alama mpya.
Afisa Tarafa Ilala , Edita Samson akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Wilaya ya Ilala wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya dawa ya Zenufa.
Mkurugenzi mtendaji wa bohari ya Dawa nchini(MSD), Laurean Rugambwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya dawa ya Zenufa.
Wadau wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha dawa cha ZENUFA.


UHUSIANO WA TANZANIA NA CHINA UNACHOCHEA UCHUMI – MAMA SAMIA.

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 70 na laki nne kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Chato kutoka kwa Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam leo wakati hafla ya kufungua sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Jamhuri ya watu wa China.China inasherehekea Mwaka Mpya ambapo mwaka huu umepewa jina la Jogoo (Rooster).
Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Dkt. Lu Youqing akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika hafla ya kuadhimisha mwaka mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo wakitembelea baadhi ya mabanda yaliyopo katika viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni sehemu ya maadhimisho yam waka mpya wa China leo jijini Dar es Salaam. China wanasherehekea mwaka mpya leo na kesho katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 11 jioni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.Maadhimisho hayo yanafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 4;00 asubuhi hadi saa 11 jioni na yanatarajiwa kumalizika kesho tarehe 22 Januari 2017.

Picha zote na: Frank shija & Shamimu Nyaki


Viewing all 110026 articles
Browse latest View live




Latest Images