Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1517 | 1518 | (Page 1519) | 1520 | 1521 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi Morogoro

  Jeshi la Polisi nchini, limeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD) ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wanachama wao kote nchini huku ikiweka dhamira ya kutoza riba ya mkopo kwa  asilimia 10.5 kwa mwaka.

  Akifungua mafunzo ya siku mbili yanayofanyika mkoani Morogoro, Kaimu kamanda wa Polisi hapa (ACP) Leonce Rwegasila, alisema kuwa, kwa kuzingatia umuhimu na uzito wa mkutano huu ni vyema kila mshiriki akazingatia mahudhui ya kile kitakachotolewa ili kuwa mjumbe mzuri kwa kupeleka elimu mahala alikotoka, alisema.

  Hata hivyo, alisema, katika mafunzo haya zipo mada pamoja na mijadala mbalimbali itakayojadiliwa ili kuja na majibu mujarabu yatakayowezesha kuwa na Saccos imara na yenye kukidhi mahitaji kwa  wanachama wao ambao ni askari Polisi pamoja na familia zao.

  Kwa upande wake Meneja Mkuu wa URA SACCOS LTD (SSP) Kim O. Mwemfula, alisema zipo huduma zilizoanzishwa za uhakika za ushirika wa kuweka akiba na kukopa kupitia Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), ambapo askari aliye mwanachama wa ushirika huo uweza kuweka na kukopa kwa riba nafuu ili kuweza kuboresha maisha yake na familia yake katika Nyanja za Kielimu, Biashara na hata Ujenzi wa nyumba.

  Ameongeza kuwa, masuala ya ustawi kwa askari yamesaidia kujenga utulivu wa akili kwa askari Polisi pamoja na kuboresha suala la ustawi wa usalama wa raia na mali zao na kulifanya taifa kuwa la amani na utulivu na kukabiliana na aina zote za matishio ya kiuhalifu na wahalifu.

   Watendaji wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), wakiwasili mkoani Morogoro, kuhudhuria mkutano mkuu wa nane wa chama hicho utakaofanyia kwa muda wa siku mbili na kuwashirikisha watendaji na wawakilishi kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

   Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Mororgoro (ACP) Leonce Rwegasila (katikati), akipokea taarifa ya washiriki wa mkutano mkuu wa nane wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), kutoka kwa (ASP) Emmanuel Katabi, kulia ni Meneja Mkuu wa URA SACCOS (SSP) Kim O. Mwemfula, na wa mwisho ni (ASP) Bakari H. Mzungu.

   Mwezeshaji Mkaguzi wa Polisi (Insp.) Edwin B. Mkole , akiwasilisha mada kuhusiana na taratibu za utoaji wa mikopo kwa wanachama wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), wakati wa mkutano mkuu wa nane wa chama hicho unaofanyika mkoani Morogoro.

  Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Mororgoro (ACP) Leonce Rwegasila (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), mara baada ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa nane unaofanyika mkoani Morogoro
  (Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi)


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  Januari 18, 2017, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba Ikulu jijini Dar es Salaam. Pichani, Makamu wa Rais, akipiga picha na Bw. Mshomba mara baada ya mazungumzo yao. (PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS).
  Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba Ikulu jijini Dar es Salaam, Januari 18, 2017
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan, (kulia), akimsikiliza Mkurugenzio Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, Ikulu jijini Dar es Salaam, Januari 18, 2017.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan, akimkaribisha ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mmkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba Januari 18, 2017.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde  amekabidhi vitanda vya hospital na vyandarua vyenye thamani ya Tsh 3,500,000 kwa Zahanat na vituo vya Afya 20 katika Jimbo la Dodoma Mjini.
  Akiongea wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi vitanda hivyo,Mh Mavunde alisema amefanya hivyo ili kutatua changamoto ya ukosefu wa vitanda vya kutosha hali ambayo imekuwa ikisababisha usumbufu kwa wagonjwa wengi pindi inapotakiwa kupatiwa huduma kwa kupumzishwa katika zahanati hizo,Akaendelea kueleza kwamba Vitanda hivi vitasaidia sana kuboresha huduma ya Afya haswa katika maeneo ya pembezoni mwa Manispaa ya Dodoma na hivyo kuondoa usumbufu kwa wagonjwa pindi wanapohitajika kulazwa.
  Wakati huo huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Ndg Kunambi amemshukuru Mbunge Mavunde kwa jitihada zake kubwa katika kuwahudumia wananchi wa Dodoma,na pia akaeleza kwamba tayari Manispaa ya Dodoma imeshaagiza magodoro kutoka MSD kwa ajili ya vitanda hivyo ili wananchi waanze kuvitumiq mara moja.

   Vitanda na vyandalua vikiwasili 
   Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akikabidhi vyandarua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Ndg Godwin Kunambi
   Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akikabidhi vitanda kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Ndg Godwin Kunambi


  0 0

  Na Fatma Salum-MAELEZO

  Serikali imepanga kutumia bilioni 15 kuwapatia vijana stadi za kazi zitakazowawezesha kujiajiri na kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa Viwanda.

  Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam wakati wa kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano kati ya Taasisi ya Teknolojia Dar es saalam (DIT) na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

  Akizungumzia makubaliano hayo Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Ally Msaki amesema kuwa yatasaidia kuiwezesha Taasisi hiyo kutoa mafunzo kwa vijana hasa ya kuzalisha bidhaa zitokanazo na ngozi ili waweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

  “Vijana 1000 wataanza kupata mafunzo mwezi Februari mwaka huu na yatakayohusu utengenezaji wa bidhaa za ngozi na program hii ipo ndani ya mpango wa miaka mitano.” Alisema Msaki.

  Mafunzo hayo ya stadi za kazi kwa vijana yatagharimiwa na Serikali na yatahusisha vijana walio katika mfumo rasmi na wale wasio katika mfumo rasmi wa elimu lengo likiwa ni kuwakwamua vijana ili washiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.

  Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) Prof.Preksedis Ndomba (kushoto) na Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Ally Msaki wakisaini makubaliano ya ushirikiano kati ya Serikali na Taasisi hiyo utakaowezesha vijana kupata mafunzo ya uzalishaji wa mazao ya ngozi katika Taasisi hiyo Kampasi ya Mwanza ili kuchochea uchumi wa viwanda nchini.
  Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) Prof.Preksedis Ndomba (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano ya ushirikiano na Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.Ally Msaki (kulia), makubaliano hayo ni kati ya Taasisi hiyo na Serikali ili kuwawezesha vijana kupata mafunzo ya uzalishaji wa mazao ya ngozi.


  0 0

  Mkurugenzi wa sekta ya uzalishaji kutoka Jumuia ya Afrika Mashariki Jean Baptiste Havugimana akimkabidhi Mfamasia Mkuu wa Zanzibar Habib A. Shariff Mashine 6 za uchunguzi wa Dawa kutoka Ujerumani kwa kupitia mradi wa EAC, MRH Projat.
  Professa. Richard Jahnke kutoka Ujerumani akitoa maelezo ya matumizi ya vifaa vipya vya uchunguzi wa dawa (Minilab Kid) kwa washiriki wa mafunzo ya siku 5 ya uchunguzi wa dawa kutoka nchi za Afrika Mashariki yaliyofanyika Mbweni.
  Washiriki wa mafunzo ya uchunguzi wa dawa kujua kuwa ziko salama kwa matumizi ya binadamu wakiwa katika mafunzo ya vitendo yaliyofanyika katika Kitivo cha Madaktari cha Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar kilichopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
  kurugenzi wa sekta ya uzalishaji kutoka Jumuia ya Afrika Mashariki Jean Baptiste Havugimana akimkabidhi cheti mshiriki wa mafunzo hayo, Hidaya Juma ambae ni Mratibu wa Mradi wa uwiano wa udhibiti wa dawa wa nchi za Afrika Mashariki ambae pia ni Mfamasia kutoka Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar.
  Washiriki wa mafunzo ya uchunguzi wa Dawa kujua kama ipo salama kawa matumizi ya binadam kutoka nchi wanachama wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi wao na walikwa.Picha na Makame Mshenga.


  0 0
  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


  OFISI YA WAZIRI MKUU


   

  KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU  MAOMBI YA NAFASI 1000 ZA MAFUNZO YA STADI ZA KUTENGENEZA VIATU


  1.         Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu (OWM-KVAU) inatekeleza Programu ya Kukuza Stadi za Kazi Nchini ya miaka mitano (2016 -2021) ambayo imelenga kuwezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la ajira. Hivyo, OWM-KVAU imeingia makubaliano na


  Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam Kampasi ya Mwanza iliyo eneo la IlemelaMwanza, kutoa mafunzo ya stadi za kutengeneza viatu na bidhaa za ngozi. Lengo ni kuhakikisha nchi inakua na nguvu kazi ya kutosha yenye ujuzi unaohitajika katika soko la ajira katika kutengeneza bidhaa za ngozi nchini.


  2.         Ofisi inapenda kutangaza nafasi 1,000 za mafunzo yatakayoanza ifikapo tarehe 20 Februari, 2017 katika Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam Kampasi ya Mwanza. Vijana wa Kitanzania, wenye elimu ya msingi na kuendelea na umri kati ya miaka 18 hadi 35 wanaopenda kujiunga na mafunzo wawasilishe maombi yao kuanzia tarehe 22/ 01/2017 hadi 04/02/2017 yakiambatana na nyaraka zifuatazo:


  (i)      Barua ya maombi yenye anuani kamili ikiwa na namba za simu pamoja na barua pepe;


  (ii)      Nakala ya Cheti cha Elimu uliyohitimu

  (iii)       Nakala ya cheti cha kuzaliwa au kadi ya mpiga kura;

  (iv)      Barua  ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa anaoishi mwombaji; na

  (v)      Picha nne za paspoti.


  3.         Maombi yawasilishwe kwa Mkuu wa Kampasi, TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ESSALAAM – KAMPASI YA MWANZA, S.L.P. 2525, Mwanza au kwa barua pepe:info@mwanzacampus.dit.ac.tz


  4.         Watakao kuwa na sifa na vigezo wataitwa kwenye usaili kuanzia tarehe 8 hadi 11 Februari, 2017.  IMETOLEWA NA:

  KATIBU MKUU


  18 Januari, 2017


  0 0

  Na Woinde Shizza, Arusha 

  WAFANYABIASHARA wa maduka jijini Arusha, wameilalamikia halmashauri hiyo, wakipinga notisi ya miezi mitatu waliyopewa, inayowataka kuondoka katika maduka hayo ifikapo Machi 30, mwaka huu kufuatia maduka yao kudaiwa kumilikiwa na madalali na hivyo kuikosesha mapato halmashauri hiyo.

   Aidha walidai kuwa hawapo tayari kuhama na hawatambui notisi hiyo na wataendelea kufanyabiashara zao kama kawaida kwa kuwa wamekuwa wakilipa mapato ya halmashauri kama inavyopaswa. 

  Wakizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, uliolenga kujadili notisi hiyo, mwenyekiti wa wafanyabiashara hao jijini Arusha, Loken Masawe alisema halmashauri hiyo imetoa notisi kwa lengo la kutangaza tenda kwenye maduka hayo, hatua hiyo walisema haiwatendei haki kwani wengi wao walijenga maduka hayo na hatua hiyo itawasababisha washindwe kulipa fedha walizokopa kwenye mabenki mbalimbali. 

  "Sisi hatujakataa tenda wanayotaka kutangaza kwenye maduka hayo ila kwanini wanataka kuweka watu wao ili sisi tufe njaa, familia zetu tutazilisha nini, tunachosema tenda hii sio halali na hatutakubali" alisema Masawe 

  Wafanyabiashara hao ambao ni zaidi ya 1200 wanaomiliki maduka katika maeneo mbalimbali katika jiji hilo, walienda mbali zaidi kwa kumtaka Rais John Magufuli kuingilia kati ili kuwanusuru na kadhia hiyo inayolenga kuwadhalilisha wao na familia zao.

   Naye mfanyabiashara Meja Willson Lukumamu alisema kuwa walijenga maduka katika eneo la stand ndogo kwa gharama zao, wakati huo eneo hilo lilikuwa pori na kwamba hadi sasa hawakuwahi kurejeshewe gharama zao . 

  "Huu mpango unaofanywa na manispaa ni batili kwani sisi kama wafanyabiashara hatujawahi kushirikishwa, tunachotaka usitishwe na biashara zetu ziendelee kama kwaida’’ alisema.
  Akizungumzia malalamiko ya wafanyabiashara hao, Meya wa jiji la Arusha, Kalisti Lazaro alisema kimsingi madai yao hayana msingi, kwani mpango huo ni utekelezaji wa maoni ya tume iliyoundwa na mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo iliyolenga kuchunguza uhalali wa umiliki wa maduka hayo. 

  Kalisti alisema kuwa halmashauri hiyo haitarudi nyuma katika mpango huo kwani imekuwa ikipoteza zaidi ya shilingi bilioni 2.1 kutokana na maduka hayo kumilikiwa na madalali ambao huwapangishia wafanyabiashara kwa gharama kubwa huku halmashauri hiyo ikipata mapato kiduchu. 

  ‘’Baada ya tume kuundwa na mkuu wa mkoa, Mrisho Gambo ilifanyakazi ya kuchunguza uhalali wa umiliki wa maduka hayo na kubaini kuwa wamiliki wa maduka hayo wengi wao ni madalali na wamekuwa wakipangisha maduka hayo kwa gharama kubwa na kuilipa halmashauri kiwango kidogo’’alisema Meya 

  Alitolea mfano mfanyabiashara Morice Makoi kuwa anamiliki maduka 27, eneo la kituo cha daladala na amepangisha kwa shilingi laki tano hadi laki nane kwa duka moja huku yeye akiilipa halmashauri hiyo shilingi 50,000 kwa mwezi, jambo ambalo alisema halikubaliki. 

  Alisisitiza kuwa halmashauri hiyo haina mpango wa kuwafukuza wafanyabiashara hao ila inachofanya ni kutangaza tenda upya ili kila mmoja aweze kuomba umiliki na atakayeshinda atakabidhiwa duka lake kwa mkataba maalum.

  Aliwataka wafanyabiashara hao kuacha kulalamika badala yake wafuate taratibu ikiwemo kuleta maombi mapya ya barua yatakayoambatana na TIN namba, Lesen na kwamba watakao kidhi vigezo hivyo watakabidhiwa duka mara moja.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto) akizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii  katika ukumbi wa Ngorongoro wizarani hapo jana. Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Ramo Makani, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kemilembe Lwota, Mwenyekiti wa Kamati, Mhandisi Atashasta Nditiye, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Aloyce Nzuki.

   Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Nditiye baada ya kuwasili makao makuu ya Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam jana huku akiongozana na wajumbe wa kamati hiyo.

  Kikao kikiwa kinaendelea katika ukumbi wa Ngorongoro, Makao Makuu ya Wizara hiyo, Mpingo House, Jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na  Bashir  Yakub.

  Hivi karibuni kumeibuka  miradi  mingi  binafsi  na  ya  serikali   hasa kupitia  NHC ya  ujenzi  wa  nyumba   za  pamoja. Miradi ipo  kwa  majina  tofauti  ipo  inayoitwa APARTMENT, CITY,  VILLAGE,  TOWN, n.k. Baadhi  ipo  kigamboni,  Arusha  na  maeneo  mengine .

   Pia  ipo  katika  mitindo  tofauti  ipo  ile  ya  maghorofa   ya  kwenda  juu, maghorofa  ya mshazali,  na  ile  ya  nyumba  moja  moja   lakini  katika  eneo  moja (common ground).  

  Kutokana  na  hilo  makala yalenga kukufahamisha  usinunue  tu  kwa kupenda  muonekano,mazingira  na  rangi , bali  pia uwe  na  uhakika  wa  faraja(comfortability)  inayotokana  na mambo mengine  nje ya muonekano,  rangi  na  mazingira.

  1.TOFAUTI  KATI  YA  NYUMBA  ZA  MIRADI  NA  NYUMBA  ZA  KAWAIDA.

  Ipo  tofauti  kati  ya  nyumba  za  kawaida  tulizozoea  na  hizi  za  miradi  zilizotajwa  humu.  Tofauti  ipo  katika ngeli hizi :
  ( a )   Taratibu  zake  za  ununuzi.
  ( b )  Vitu  unavotakiwa kujua  kabla   ya  ununuzi.  
  ( c )   Sheria  zinazozilinda   na,  
  ( d )  Maisha   yako  baada  ya  kuwa  umenununua.

  Makala  yataeleza   vitu  unavyotakiwa  kujua    vinavyotofautisha   nyumba  hizi  na  nyingine za  kawaida.

   2.     VITU  UNAVYOTAKIWA  KUJUA.

  ( a )   Uwepo  wa  malipo  na  michango  mbalimbali.  Pamoja na  kuwa ni mali  yako umenunua , kanuni  ya  15( 2 )  ya  The  Unit  Title  Regulations, G.N 357/2009  imeeleza   baadhi  ya  michango. Ipo  michango  kwa  ajili  ya  chama  na  uongozi,  michango  kwa  ajili  ya  maeneo  ya  matumizi  ya  pamoja, michango  kwa  ajili  ya  huduma  mbalimbali  mnazotumia  pamoja.  

  Michango  hapa haihusishi bili  zako  za  umeme,maji n.k. Michango  hii  inaweza  kuwa  inalipwa  kila  mwezi   au  vinginevyo   kadri  ya  utaratibu  wa  eneo  husika.

  Hii  ni  tofauti  na  nyumba  za  kawaida  ambazo  haziko  katika  mfumo  huu  ambapo  ukinunua  umenunua  hakuna  mchango  wa  chama  au  vinginevyo.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Mwalimu wa shule ya sekondari Ndugu,Wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe,Christian Kiyeyeu mwenye umri wa miaka 31 ameibuka mshindi baada ya kubashiri vyema matokeo ya mechi kupitia Kampuni ya M-Bet na kujishindia kitita cha Shilingi Milioni 30/-.

  Kiyeyeu amekabidhiwa fedha zake leo katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam kwenye ofisi za M-Bet

  Kwa upande wake, Msemaji wa M-Bet, Godluck Wambura alisema kuwa Kiyeyeu alifanikiwa kuzoa kitita hicho baada ya kufanikiwa kutabiri matokeo ya mechi…. za ligi ya Ulaya kwa mtindo wa kucheza kawaida.

  “Tumefurahi kumkabidhi mshindi wetu kitita hichi cha Sh milioni 30/- akiwa ndiye mshindi wa M-Bet ambapo amesema ataiwekeza katika biashara zake na kuweza kumalizia nyumba yake ambayo tayari alikwishaanza kuijenga,” alisema Wambura.

  Aliwataka watanzania kuchangamkia kutumia mtandao wa intaneti kuonyesha ushabiki halisi wa soka akisema kuwa Perfect 12 na michezo mingine ni michezo mizuri inayoweza kubadilisha maisha yako mara moja ukiwa umelala masikini na kuamka tajiri kwa kutabiri kwa kiasi cha Tsh 1,000 tu unaoruhusu kutabiri mechi 12 kwa mchezo wa perfect 12 ambapo ukipatia zote unaondoka na kitita chako mchana kweupe.

  Naye Mshindi huyo, Christian Kiyeyeu amewashauri watanzania wote hususani walimu wenzake wenye umri unaoruhusiwa kisheria kujitokeza kubashiri matokeo ya mechi mbalimbali kupitia Kampuni ya M-Bet .

  "Nashukuru sana M-Bet kwa kuniwezesha kujikwamua kimaisha, nitatumia fedha hizi kutimiza ndoto yangu ya kumalizia nyumba yangu kwa ujenzi", alisema Kiyeyeu.

  Kuhusu m-Bet, ni Kampuni iliyosajiliwa chini ya Sheria za Tanzania na kupewa leseni na Bodi ya Michezo ya kubahatisha tanzania kwa lengo la kufanya upatikanaji rahisi na mwingiliano wa huduma ya mchezo wa kubahatisha (Sim Betting) nchi nzima.
  Meneja wa huduma kwa wateja wa M-bet, Jaykishan Kaba (kushoto)akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 30/- mshindi wa M-bet, Mkazi wa mkoa wa Songwe,Christian Kiyeyeu(kulia)katika hafla fupi ya makabidhiano hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,Katikati ni Msemaji wa M-bet Gudluck Wambura. 
  Meneja wa huduma kwa wateja wa M-bet,Jaykishan Kaba(kushoto) na mshindi wa M-bet, Mkazi wa mkoa wa Songwe,Christian Kiyeyeu(kulia)wakimsikiliza Msemaji wa M-bet Gudluck Wambura,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 30/- mshindi huyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

  0 0

   Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mkazi hapa nchini wa Taasisi ya Fredrich Ebert Stiftung (EFS) ya Ujerumani, Michael  Schultheiss, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Januari 19, 2017. (Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa mikoa ya Singida, Mbeya, Iringa na Dodoma wawasimamie wananchi wao na kuhakikisha hakuna shughuli za kibinadamu zinazofanyika ndani ya vyanzo vya maji.

  Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Januari 19, 2017) alipozungumza na watumishi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Mtera alipotembelea bwawa la Mtera akiwa njiani kwenda mkoani Njombe kwa ziara yake ya kikazi.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo baada ya Kaimu Meneja wa Kituo cha kuzalishia umeme cha Mtera, Mhandisi Edmund Seif kutaja baadhi ya changamoto zinazokikabili kituo hicho kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu ndani ya vyanzo vya maji.

  Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu ameagiza vifanyike kwa vikao vya ujirani mwema ili wananchi waelimishwe umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na ni marufuku kuendesha shughuli za kibinadamu ndani ya kilomita 60 kutoka kwenye chanzo.

  "Marufuku wafugaji kuingiza ng'ombe ndani ya vyanzo vya maji na badala yake utafutwe utaratibu wa kuwachimbia mabwawa pembeni. Pia wakulima nao wazuiwe kulima ndani ya vyanzo vya maji. Lazima tushirikiane kulinda vyanzo vyetu," amesema.

  Awali, Mhandisi Seif alisema kituo hicho cha Mtera kinazalisha megawati 80 kwa siku ambazo zinaingizwa kwenye gridi ya Taifa. Alisema bwawa hili kwa sasa lina maji ya kutosha kuzalisha umeme hadi msimu ujao wa mvua.
   Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ia SAS, Bw. Salim Abri  wakati alipokwenda kwenye shamba la ng'ombe la ASAS lililoko nje kidogo ya mji wa Iringa Januari 19, 2017. (Picha na Ofisi ua Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ukamuaji ng'ombe wa maziwa katika shamba la Ng'ombe la ASAS nje kidogo ya mji wa  Iringa Januari 19, 2017.  Wapili kushoto  ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wakurugenzi wa kampuni ya ASAS  baada ya kutembelea shamba la ng'ombe la ASAS nje kidogo ya mji wa Iringa Januari  19, 2017.   Kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimlaki Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa baada ya maongezi yao ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzi na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya kumbukumbu na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman na ujumbe wake pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu Wizara hiyo Mhe. Dotto James Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman wakiwa pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu Wizara hiyo Mhe. Dotto James Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017

  0 0

  Rais mpya wa FIFA Gianni Infantino anaonekana kutaka kubadili soka kabisa kwa kutaka kuondoa kila kitu cha Sepp Blatter na kuleta vyake hasa baada ya kupelekea mapendekezo ya kuongeza timu zitakazoshiriki kombe la dunia 2026 kufikia timu 48 na sasa amekuja na mpya ya kutaka kubadili namba ya kupiga penati.

  Kwa kumtumia mkurugenzi wa mambo ya ufundi wa FIFA Marco Van Basten wamependekeza baadhi ya sheria mpya katika soka.
  Kuondoa offside.

  Akihojiwa na gazeti la Ujerumani liitwalo Bild,Van Basten amesema wanawaza kuondoa mchezo wa kuzidi katika soka.Alisema “sipati picha soka isipokuwa na ofside,washambuliaji watapata nafasi nyingi sana za kufunga”.Van Basten alisema mpira wa miguu utakuwa wakuvutia sana kama offside itaondolewa na anaamini jambo hilo litawafurahisha mashabiki na washambuliaji.

  Kingine ni kubadili upigaji wa penati, Van Basten pia anaona kuna haja kubwa kwa FIFA kubadili aina ya upigaji wa penati na adhabu ya penati mchezaji ambapo upigaji wa penati ni mita kadhaa karibu na goli na kuupiga lakini sheria mpya anataka mpiga penati auweke mpira mita 25 kabla ya goli na kama anaweza atembee nao kuelekea golini kwa muda usiozidi sekunde nane.Aina hii ya upigaji penati sio ngeni kwani mwaka 1999 ilishafanyiwa majaribio nchini Marekani.

  Kupunguza adhabu mipira ya kushika, Van Basten anaona kama adhabu ya kadi nyekundu ni kali mno kwa tukio hilo na  wanaliona kama tukio dogo lisilohitaji adhabu hiyo na wanazani inapaswa ipunguzwe kusitolewe kadi nyekundu mpira ukishikwa. Adhabu kam ile ya tukio la Luis Suarez mwaka 2010 wakicheza dhidi ya Ghana aliposhika mpira wakati ukiingia golini na kutaka ibadilishwe na kuwa ya njano.

  Kapteni awe mtu pekee kuongea na mwamuzi, kama katika Rugby ni kapteni tu anayeongea na mwamuzi,asiruhusiwe mtu yeyote,mchezaji yeyote kuongea na mwamuzi.Aina  ya faulo ya mchezo wa kikapu pale mchezaji anapocheza madhambi matano anatakiwa atoke uwanjani na  sasa Van Basten anaamini staili hiyo inapaswa kuletwa katika soka.

  Kupunguza idadi ya mechi, hii itafurahiwa sana na makocha wageni Uingereza. Alianza Van Gaal akaja Jurgen Klopp walilalamikia idadi ya mechi kuwa nyingi Epl.Van Basten anataka idadi ya mechi zipunguzwe kutoka mechi 80 kwa msimu hadi 50 kwa msimu.

  Kuongeza idadi ya Substitution.Van Basten anatamani kuongeza idadi ya wachezaji wa sub kuanzia 5-7,kwa muda mrefu wadau wa soka wamekuwa wakizungumzia kuhusu suala la kuongeza wachezaji wa akiba na sasa FIFA inatarajia kuliangalia suala hili.

  Kuzifanya dakika 10 za mwisho kutumika ipasavyo.”Tunajua kutokana na kuongeza idadi ya wachezaji wa akiba pamoja na aina ya upigaji penati vitachukua mda mrefu uwanjani na itatubidi kuhakikisha dakika 10 za mwisho zinatumika kiuhakika” Van Basten alisema watahakikisha hakuna upotezaji muda katika dakika zamwisho za mchezo.

  Hayo ni mapendekezo tu kutoka kwa mkurugenzi wa ufundi wa FIFA na  sasa atawasilisha mapendekezo hayo katika kamati ya FIFA yaweze kujadiliwa.

  0 0

  Gari lililombeba  Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa likipita kwenye daraja la bwawa la kuzalisha umeme  Kituocha Kuzalisha Umeme cha  Mtera kwenye mpaka wa mkowa Dodoma na Iringa  Januari 19, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alifanya ziara fupi  ya kukagua kina cha maji kwenye bwawa hilo . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)  katika bwawa la Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Mtera lililoko kwenye mpaka wa  mkoa wa Dodoma na Iringa wakati alipofanya ziara fupi ya kukagua kina cha maji kwenye bwawa hilo  Januari 19, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipata maelezo kuhusu kina cha maji kwenye bwawa la  Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Mtera lililoko kwenye mpaka wa mkoa wa Dodoma na Iringa  wakati alipofanya ziara fupi ya kukagua kina cha maji kwenye bwawa hilo Januari  19, 2017.  Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua kina cha maji kwenye bwawa la  Kituo cha kuzalisha Umeme cha Mtera lililoko kwenye mpaka wa mkoa wa Dodoma na Iringa Januari 19, 2017.   Kushoto ni Kaiu Meneja wa Kituo hicho,  Mhandisi Edmund Seif. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kina cha maji kwenye bwawa la  Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Mtera  lililoko  kwenye  mpaka wa mkoa wa Iringa na Dodoma  wakati alipokwenda kukagua kina cha maji kwenye bwawa hilo Januari  19, 2017. 

  0 0
 • 01/19/17--04:41: TAARIFA KUTOKA TFF LEO
 • OMBI LA ZANZIBAR KUJADILIWA CAF 
  Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limepitisha ombi la Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) la Zanzibar kuwa mwanachama kamili wa CAF. Katika kikao chake cha Kamati ya Utendaji kilichoketi Januari 12, mwaka huu kiliamua kupitisha ombi hilo kuwa moja ya ajenda za Mkutano Mkuu wa CAF utakaofanyika Machi 16, 2017 huko Addis Ababa, Ethiopia.
  Hivyo sasa Mkutano Mkuu huo utapiga kura na kama Zanzibar itapata idadi ya kura theluthi mbili yaani 2/3 ya wanachama wote, itatangazwa kuwa mwanachama mpya kamili wa CAF ambako atakuwa na haki mbalimbali za kama mwanachama.
  Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini 
  NYOTA AIRTEL WATAWALA LIGI YA WANAWAKE, MECHI MBILI KUCHEZWA KESHO 
  Wakati Ligi Kuu soka ya Wanawake ikitarajiwa kuendelea kesho Ijumaa Januari 20, 2017 kwa michezo mitano, wachezaji 19 kati 25 bora walioteuliwa katika mradi wa kuibuka na kukuza vipaji vya soka wa Airtel (Airtel Rising Stars), wametawala katika klabu zinazoshiriki michuano hiyo, inayoendelea.
  Wachezaji hao wanaocheza kwa mafanikio makubwa ni Agatha Joel, Fabiola Fabian, Eva Jackson, Zainabu Mrisho, Fumu Mohamed, Stella Wilbert, Christina Samwel, Shamimu Hamisi, Oppa Msolidi na Yustina Mboje ambao wamesajiliwa na Klabu ya Evergreen ya Temeke, Dar es Salaam.
  Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini 

  0 0

  Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya soka ya FIFA kwa miaka minne ijayo. Uteuzi huo unaanza mwaka huu 2017 hadi 2021.
  Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Januari 18, 2017 iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa FIFA, Fatma Samoura inasema: “Tuna faraja kukufahamisha kuwa umeteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya FIFA. Tunachukua nafasi hii kukupongeza kwa uteuzi huu,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
  Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Kamati hiyo inayoongozwa na Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Bara la Asia, ina majukumu ya kusimamia mipango ya maendeleo ya mpira wa miguu duniani kote.Wajumbe wengine wote watatangazwa kwenye tovuti ya FIFA ambayo ni www.FIFA.com.
  Huu ni mfululizo wa Tanzania kupata nafasi katika vyombo vikubwa vinavyoendesha soka FIFA na CAF. Mwishoni mwa mwaka jana, CAF – Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika lilimteua Rais Malinzi kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati maalumu inayoongozwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou ya kuboresha mfumo wa uongozi wa CAF.
  TFF inamshukuru Rais Gianni Infantino na kamati yake ya ushauri kwa kumteua Malinzi katika nafasi ya ujumbe katika kamati hiyo muhimu ya maendeleo ya soka ulimwenguni. 

  0 0

  NA VICTOR  MASANGU, KIBITI

  KATIKA kuunga mkono juhudi za  serikali ya awamu ya tano  katika kupambana na wimbi la umasikini hususan kwa vijana na wakinamama, halmashauri ya Wilaya mpya ya Kibiti mkoani Pwani imejiwekea mipango madhubuti kwa ajili ya kuweza  kuwasaidia katika vikundi vya ujasiriamali kwa lengo la kuweza kuondokana na dhana ya kuwa tegemezi na badala yake wafanye kazi ili kuweza kuleta maendeleo.

  Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa  halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Alvera Ndabagoyo wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika mahojiano maalumu  kuhusiana na changamoto ya siku nyingi ya wimbi la umasikini kwa vijana wa wakinamama pamoja na mikakati yao waliyojiwekea ili kuondokana kabisa na hali hiyo.

  Mkurugenzi huyo alisema kwamba kwa sasa anatambua kuna baadhi ya vijana na wakinamama katika Wilaya hiyo ya Kibiti wanakabiliwa na tatizo la kutokuwa na ajira hivyo uongozi wa halmashauri hiyo umeshaanza kufanya jitihada za hali na mali katika kuhakikisha fedha ambazo zitakuwa zikitengwa kwa ajili yao zinawafikiwa walengwa  ili waweze kuzifanyia shughuli halali za kimaendeleo  na kujipatia kipato.

  Pia Alvera alibainisha kuwa katika mwongozo wa serikali inatakiwa kila halmashauri katika kila bajeti yake  ya  mwaka  itenge  kiwango cha asilimia 10 cha fedha  kwa ajili ya kuweza  kuvisaidia vikundi mbali mbali vya wakinamama pamoja na vijana ili waweze kuendelea kufanya shughuli zao mbali mbali za kijasiriamali lengo ikiwa ni kuweza kupamabana na umasikini.

  Aidha aliongeza kuwa ana imani kubwa endapo  vikundi vya vijana na wakinamama katika Wilaya ya Kibiti vikijiunga kwa pamoja na kuwezeshwa kwa kupatiwa fedha kwa ajili ya kufanyia biashara  vitaweza kufika mbali na kuweza kuleta mabadiliko  chanya ya kimaendeleo kuanzia ngazi za familia zao hadi kuwasaidia na wananchi wengine .

  Katika hatua ngingine Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa wananchi wote wa Wilaya ya Kibiti kuachana na kuwa na tabia ya kuwa tegemezi kila kukicha na badala yake sasa wabadilike na kujiunga katika vikundi mbai mbali vya ujasiliamari ili pindi fedha inapotolewa na halmahsuari iwe rahisi kuwafikia walengwa kuliko kuwa  mtu mmoja mmoja.

  Hata hivyo Mkurugenzi huyo aliahidi kushirikiana bega kwa began a baraza la madiwani, watendaji, pamoja na wadau wa maendeleo katika kuhakikishwa wanapambana vilivyo katika kuzitatua kero na changamoto mbali mbali ambazo zimekuwa zikiwakabili  kwa kipindi kirefu wananchi wa Wilaya mpya ya Kibiti mkoani Pwani.

  0 0older | 1 | .... | 1517 | 1518 | (Page 1519) | 1520 | 1521 | .... | 3272 | newer